Monday, June 11, 2012

DHANA MBAYA


Miongoni mwa maafa yaliowasibu watu na jamii ni dhana mbaya, jambo ambalo linakata mapenzi kati ya watu, na mwenye dhana mbaya huwaangalia watu kwa jicho ovu, na bila shaka dhana mbaya ni kuhalifi sheria ya kiislamu.
Ilikubaki mafungamano yetu na watu kuwa mazito ni kuwakabili watu hali ya kuwa nyoyo zetu zimesalimika pia kuwa safi na nyuso kuwa na bashasha na kuwadhania watu uzuri pindi tunaposalimiana nao. Tunapozingatia mafungamano ya Waislamu yamesambaratika kutokana na dhana mbaya. Unaposikia maongozi ya Waislamu twasikia wakisema Fulani amekusudia hivi, na Fulani ametaka jamabo hili. Yote yanapelekea kupatikana kwa chuki mwisho na kuvunjika au kusambaratika kwa mafungamano. Dhana mbaya inapeleka kufuatilia aibu za watu na kuchunguzana kwa ajili hiyo utasikia kwa mwenye dhana mbaya akisema “ Nitajaribu kuhakikisha basi atachunguza na kusengenya na kumtaja mwenzake kwa uovu. Kuenea kwa dhana mbaya kunakosekana uaminifu kati ya watu na kukatana jambo ambalo kwamba linapelekea kutofaulu katika mambo yetu. Anasema Mwenyezi Mungu (SW):
قال الله نعالى : { وأطيعوا الله ورسوله ولا تنازعوا فتفشلوا وتذهب ريحكم واصبروا إن الله مع الصابرين }
{{ Na mtiini Mwenyezi Mungu  na Mtume wake wala msizozane, msije mkaharibikiwa na kupotea nguvu}}.  Dhana mbaya haileti kheri na ni njia ya kuenea kwa uadui na kupatikana kwa madhambi hayo ni duniani ama kesho akhera ni majuto. Tazama watu waovu walivyo wakejeli Waislamu na kuwadhania maovu pindi Mwenyezi Mungu (SW) Aliposema:
قال تعالى:{ وقالوا ما لنا لا نرى رجالا كنا نعدهم من الأشرار, أتخذناهم سخريا أم زاغت عنهم الأبصار}
{{ Kisha wale wabaya watasema: Imekuwaje, Mbona hatuwaoni wale watu tulikuwa tukiwahisabu katika waovu kwa kumfuata Muhammad. Je, tuliwafanyia mzaha (huko duniani, na hali yakuwa ni watu wakubwa Akhera au wamo Motoni humu pamoja na sisi) ila macho yetu haya waoni tu ?}}. Anasema Mwenyezi Mungu (SW):
 قال تعالى:{ فاليوم الذين آمنوا من الكفار يضحكون على الأرائك ينظرون, هل ثوب الكفار ما كانوا يفعلون}.
{{ Basi leo walioamini watawacheka waliokufuru. Wata kuwa Juu ya viti vya fahar, wakitazama (neema zao). Je, makafiri wamepewa malipo ya yale walyokuwa wakiyatenda?}}. Anasema Mwenyezi Mungu (SW):
قال تعالى: { ياأيها الذين ءامنوا اجتنبوا  كثيرا من الظن إن بعض الظن إثم }.
{{ Enyi mlioamini, Jiepusheni sana na dhana mbaya. Kwani dhana mbaya ni dhambi}}. Inajulisha Aya katika kuhifadhi heshima ya muislamu kwa kutangulia na katazo la dhana. Ni uzuri ulioje kwa mujtama ulio salimika na dhana mbaya.Mtume (SAW) amesema: [ Jiepusheni na dhana hakika ya dhana ni maongezi ya urongo wala musichunguzane wala musichukiane kuweni ndugu katika waja wa Mwenyezi Mungu]. Wamesema badhi ya wanavyuoni dhana amabyo inafaa kuepukwa ni ile ambayo kwamba haijulikani njia yake kuwa ni ya sawa na sababu iliyokuwa ya wazi, mfano anayedhaniwa akiwa ni mtu mwema na akapewa amana kuwadhania kuwa amekhini ni haramu. Kinyume na amabae anajulikana anayefanya maovu wazi wazi kwa ajili hiyo wamesema wanavyuoni dhana mbaya kwa mtu mwema haifai na hapana tatizo kudhania uovu mtu muovu.
Imepokewa hadith Said ibn Musaib akisema: “ amewaandikia baadhi ya maswahaba wacha uwema kwa jambo la ndugu yako maadamu hujashindwa wala usidhani neno baya limetoka kwa ndugu yako ikiwa inawezekana kuchukulia kwa uzuri na huo ndio mfano wa watu wema pindi kutoelewa baadhi ya maneno, kwa hukumu makosa watu wengine bila ya kuzingatia nia na hali ya yule mtu. Ibn Qayyim amesema: “Neno moja husemwa na watu wawili mmoja wao anakusudia haki mmoja wao anakusudia batil kwa ajili hiyo haku hukumiwa kwa mkafir aliyesema “ Ewe mola wangu wewe ni mja wangu na mimi ni mola wako” hakukusudia kujifanya Mwenyezimungu. Amesema Sheikhul Islam Ibn Taymiyya pindi anaponukuu maneno ya wenye kumkhalifu akisema “ maneno haya yanaupana, na haki huchukuliwa kwa uzuri na batil huwa na mambo mengi”
Mwanadamu hana haki kwa ndugu yake ispokuwa kwa mambo yaliyowazi. Amepokea Abdulrazaq kutoka kwa Omar Ibn Khattab akisema: “ watu walikuwa wakipokea wahyi wakati wa Mtume (SAW) na wahyi ukakatika, lakini tunachukua sasa kwa yale yaliyodhihiri kutokana na vitendo vyenu kwa atakae dhihiri kheri tutamuamini na tutamkaribisha haitujalishi sisi usiri wake na Mwenyezi Mungu ndiye atakaye muhisabu kutokana na usiri wake na atakae dhihiri shari lake kwetu hatutomuamini wala hatutomsadiki hata akisema kuwa usiri wake ni mwema”. Kwa Muislamu ahisabu kuwa kila neno analozungumza au hukumu anayotamka na akumbuke Neno lake Mwenyezi Mungu (SW):
قال تعالى: {  ولا تقف ما ليس لك به علم إن السمع والبصر والفؤاد كل أولائك كان عنه مسؤولا  }.
 {{ Wala usifuate usiyo na ilimu nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa}}.

Waja wa Mwenyezi Mungu sababu za dhana mbaya ni kuenukia mtu katika mazingira maovu na atakaefuata matamanio yake ataingia katika dhana mbaya; kupenda kitu hufanya mtu kuwa kipofu na kiziwi mwanadamu akifuata matamnio yake kwa kumpenda mtu mwengine makosa yake huwa ni mema na akimchukia mtu mwengine mema yake huwa ni maovu. Baadhi ya watu anajienua utu wake na kujiona saa zote kuwa yuko katika na watu wengine katika batil na kujitakasa nafsi yake kudharau watu wengine jambo amabalo kwamba linaleta dhana mbaya kwa watu wengine.Dhana mbaya ni sababu ya kupatikana tuhuma kwa watu na kuwagura bila ya sababu ya kisheria na kuwadhulumu kama alivyosema msemaji: “ Naona uadui wala sioni sababu zake yote kutokana na mshikano uliokatika, dhana ilivyokuwa na madhambi, na kusengenya kuliokuwa kuovu.  Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
قال تعالى: {والذين يؤذون المؤمنين والمؤمنات بغير ما اكتسبوا فقد احتملوا بهتانا وإثما مبينا}
{{ Na wale wanaowaudhi wanaume Waislamu  na wanawake Waislamu pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhahiri}}.

Suluhisho la dhana mbaya
(a) kuwadhania watu dhana nzuri fikiri kwa kina kabla hujatoa hukumu na kutuhumu kwani kukosa kwa kumdhania mtu wema ni bora kuliko kwa kumdhania mtu uovu. Amesema Umar : “ Dhania kheri kwa neno litakalo kwa ndugu yako baada ya kuwa na dhana, ikiwa panapatikana ndani yake kheri.(b) Kutoa udhuru kwa watu na kutofuata aibu za watu na kuwajibika katika adabu za kiislamu katika kutoa hukumu kwa watu na kumuachia Mwenyezi Mungu mambo yaliyofichamana.

Mwisho
Ndugu katika Imani, tumeona hatari mbaya ya Muislamu kumdhania Muislamu mwenzake vibaya, na athari yake katika jamii ya kislamu. Jamii ya kislamu ni jamii ilio hifadhiwa na sheria za Allah (SW). Muislamu akipata khabari yoyote kuhusu Muislamu mwingine ni lazima kwanza apime khabari hiyo kwa mizani ya sheria, ili aweze kujuwa ukweli wa khabari hiyo.Namuomba Mwenyezi Mungu atuondelee dhana mbaya na atuwezeshe kuwadhania watu dhana mzuri, na kuwapa udhuru watu.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget