HISTORIA FUPI YA MAKANISA YA MWANZO YA ZANZIBAR
WARENO 1500 – 1800
Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno. Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya matumaini mema – Cape of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao wa Afrika.
Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499 walianzisha Ujumbe wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa Zanzibar. Wareno kwa miaka 200 iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli za Afrika Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la mwambao. Mabaki ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na Fukuchani Kaskazini Unguja na Kisiwani Pemba. Ngome Kongwe ambayo ipo karibu na bandari ya mji wa Zanzibar ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la kikatoliki la mwanzo baada ya kutekwa na Jeshi la Oman. Jeshi hili la Oman inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwangóa Wareno waliokuwa makatili na madhalimu.
Baada ya miongo ya vita na maangamizo ambayo yaliyoshuhudi kuwaka moto mji wa Mombasa, Wareno walirudi nyuma, na kurejea kuendea kusini, mbali na mafikio ya mashambulizi ya moja kwa moja ambayo yaliyotokana na pepo za miongo za jahazi (waarabu).
OASISI YA UVUMILIVU (OASIS OF TOLERANCE)
Katika mwaka 1841 mpiganaji wa Kioman/Oman Sultan, Seyyid Said alivutiwa sana na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo alihakikisha anahamishia makao makuu yake Zanzibar kama ni mji mkuu. Malezi yake katika maisha ya Jangwani yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote kuviendeleza visiwa hivyi vyenye ustawi. Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni Oasisi katika bahari. Alisimamia mipango mikubwa ya upandaji miti, alichimba visima vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha mamia ya wageni. Sultan alitambua wageni watakaa na kujiliwaza katika Oasisi. Na alijua kwamba biashara itakuwa na kufanyika katika eneo hili ikiwa litaimarishwa kwa vitu na mambo mengine pamoja na usalama. Vile vile alitarajia na kutambua kwamba angelipata asilimia fulani inayotokana na shughuli za kibiashara zitakazo endeshwa Visiwani kama ni malipo ya kuviimarisha visiwa hivyi. Aliwakaribisha na kuwaomba wafanyabiashara kutoka India kufungua matawi ya ofisi zao ndani ya Zanzibar ili kuimarisha biashara. Wafanyabishara hawa wengi kutoka India walikuwa ni raia wa kiingereza hii ilikuwa ni kwa sababu ya kutekwa India na Uingereza. Kwa maana hiyo, alianza kuwakaribisha maofisa wa kiingereza visiwani ili kuwakilisha maslahi ya raia hawa wahindi wa kiingereza. Mara tu tena baadae alianza kuingia katika mikataba rasmi ya kibiashara na Serikali ya kiingereza na Serikali nyengine za Magharibi.
Majengo ya biashara yalijengwa ndani ya Mji Mkongwe na Kampuni za Kimarekani, Kijerumani, Ufaransa na na Kiingereza. Bandari ya Zanzibar ilitoa huduma za fueli na kufanyia
matengenezo Meli za kivita na vyombo vya usafiri vya wafanyabiashara. Meli hizi zilileta mapote ya ziada ya watu wa magharibi ndani ya Zanzibar. Kama ni makaribisho mema ya wageni wengi katika Oasisi yake. Sultani aliruhusu watu wa imani zote kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda.


1800 – 1900
WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA AFRIKA YA KATI ( UMCA)
Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa ndio waliobakia Zanzibar.
Wakiristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza kuifanya hai jumuia yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi. Baadae katika miaka 1800 makundi ya watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari waliokuwa wakipita pita mara chache na wachungaji katika meli bandarini. Katika mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la kiingereza (English Church Missionary Society). Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi.


Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA). Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham na Dublin. Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni “Askofu wa Afrika ya kati” na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea huko Afrika ya Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA) lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi. Kwa ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika katika sehemu iliyojulikana kama Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia kushindwa kwa aina yake kutekeleza malengo yake. Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na kupelekea kufa kwa askofu. Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea na hali ya hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa. Askofu mpya, George Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu liligundulika kuwa halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika kati kati ya Afrika. Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha Johanna, maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano, upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora. Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar tarehe 31/08/1864.

Ruhusa iliyotolewa na Sultan Majid kwa Wafaransa hawa kuanzisha duka ndani ya Zanzibar ilitafsiriwa kama ni juhudi za Sultani za kuweka “ uwiano wa nafasi kubwa waliokuwa nao Waingereza Zanzibar kwa kuwakaribisha wapinzani wao wakuu wa kizungu.” Ikiwa ushindani wa kisiasa ndio uliompelekea Sultan Majid za kukaribisha pamoja matawi tofauti ya wamisionari wakiristo hata hivyo matokeo hayakuwa hayo kwani kwa upande wa wamisionari hawa hakukuwa na msuguano wowote. Mahusiano yao mazuri makundi hayo mawili ya wamisionari ulitokana na ukweli kwamba Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati wa kianglikana (UMCA Anglicans) ulikuwa ni ujumbe wa watu watukufu ambao wenye mafunzo ya kikatoliki ya kiengereza (Anglon Catholic Learnings)

Juu ya ukarimu wa watu wa Zanzibar, Wazanzibar hawa kidogo hawakuwa na azma yoyote kufuata imani ya wageni hawa wapya. Wamisionari wa kikatoliki walilielewa hili lakini waliamini
kwamba kundi kubwa la wafuasi wapya wa dini hii ya kikiristo litaweza kupatikana masafa machache kuvuka mlango bahari wa Zanzibar huko Tanzania Bara.
Walipeleka ujumbe mdogo Bagamoyo katika mwambao wa Tanzania Bara katika mwaka 1868 na kwa sehemu kubwa walitumia nafasi walizonazo Zanzibar kama ni makao makuu ya kuzidisha harakati zao Tanzania Bara. Harakati hizi ikiwemo ujenzi wa “ Hospitali ya Kifaransa” ndani ya Bagamoyo.


“ Hospitali ya Kifaransa” ndani ya Zanzibar ilijengwa mkabala na jengo la watawa. Hospitali ilimalizwa kujengwa na kuanza kazi kufikia mwaka 1890. Kipindi hicho wakatoliki walien delea kutumia uhusiano mzuri na majirani zao wa Zanzibar, wakipata ruhusa ya kujenga kanisa la mtakatifu Joseph katika mwaka 1894. (Cathedral of Saint Joseph in 1894). Jiwe la msingi la
kanisa hili kuu liliekwa tarehe 10 Julai 1896. Misa ya mwanzo katika kanisa hili kuu jipya iliendeshwa na Askofu Allegeyer katika usiku wa krismas 1898.

%20apx.%201900_small.jpg)
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) hawakuzubaa katika kipindi hichi. Akianzia kwanza kuishi katika nyumba Mambo Msiige, katika eneo la Shangani, ambapo haikuwa mbali na ujumbe wa Kifaransa, Muingereza mchapa kazi shupavu alianzisha ustawi wa
majengo ya ukubwa wa kuvutia na ya aina tofauti. Kwanza walinunua sehemu ya ardhi ya kilimo Kiungani pembezoni mwa mji wa Zanzibar Kaskazini. Ujenzi wa “bweni kwa ajili ya vijana watumwa walioachiwa huru” uliendelea katika eneo hilo kufikia mwaka 1866. Karibu ya hapo mava sehemu ya kuzikia ilianzishwa, na hadi leo mava hii inayo baadhi ya mabaki ya wakiristo wa mwanzo wa Zanzibar.

Baadae ilinunuliwa ardhi nyengine katika mwaka 1873, ardhi hii ilikuwa karibu na kitovu cha mji ambalo ni jengo kubwa zima la mjini ambalo liliwahi kuwa uwanja wa soko kongwe, ambapo watumwa walikuwa wakiuzwa, Mara wito ulitolewa wa fedha kusaidia ujenzi wa kanisa katika eneo hilo ambao uovu huo wa biashara ya utumwa ulifanyika. Huu ulikuwa mwanzo kanisa kuu la kristo (Christ Church Cathedral).
Mwaka uliofuata Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) walinunua ardhi ya kilimo Mbweni kusini mwa mji karibu na bahari.


Jiwe la msingi la kanisa kuu la ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA Cathedral)
liliekwa mwaka 1873 katika siku ya siku kuu ya krismas katika eneo la mjini. Uwanja wa soko kongwe ulianza kujazwa majengo ya ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati.

“Jumba la Mkunazini” lilijengwa katika mwaka 1875 na kanisa mara baada ya kujengwa jumba la kunazini lilihamisha makao makuu yake kutoka Mambo Msiige na kuwa Mkunazini. Zahanati
ilijengwa katika mwaka 1877, hatimae iligeuzwa kuwa hospitali yenye kutoa huduma kamili katika mwaka 1893. Skuli ya Mtakatifu Mon`ica, nyumba ya kasisi mkuu na Askofu ilijengwa katika uwanja wa soko kongwe. Jengo hilo la skuli ya Mtakatifu Monica bado mpaka leo linatumika kama ni hostel/dahalia Mtukufu Monica.

Mwenye kustahiki sifa ya mafanikio haya ilikuwa hakika ni kanisa kuu la kristo. Mradi usio wa kibiashara ambao ulisimamiwa binafsi na Askofu wa tatu wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati Edward Steere, utabakia kuwa moja ya mifano ya kuvutia na bora wa usanifu majengo ndani ya Afrika uliofanywa na wakiristo wa mwanzo.














Theodore Buft aliamini kwamba biashara na ukiristo ilikuwa ndio njia ya uongofu na kuweza kuweza kuelimika.
Watumwa na Waliobadili Dini

Lakini juu ya hivyo, wingi wa wakiristo hawa wapya na mahitaji yao maku bwa yalikuwa ni changamoto kwa raslimali na subira ya wafadhili wao. Wakiangalia demografia wamisionari waliona njia pekee ya kuwahudumikia wakiristo wapya ni kuanzisha chimbuko la Padri wa kiafrika.
Kwa hivyo wote wakatoliki na waprotestanti walifanya bidii kuwajumuisha makundi ya kienyeji shughuli na mambo ya kanisa na hii yote ilipelekea kujua na kufunza mtumishi bora kwa ajili ya kuendesha shughuli za kidini.
Kwa Zanzibar harakati zote hizi zilikuwa katika eneo la Kiungani ambapo kwanza ilianzishwa “dahalia kwa watumwa vijana walioachiwa huru”, na baadae “Chuo cha Mafunzo ya ualimu cha Mtakatifu Andrew” na baadae “Chuo cha kidini/theolojia” kila moja kati ya hivyo kilijaribu kuwafunza na kutathmini matokeo ya vijana wa kiafrika. Kiasi cha wanafunzi 50 kwa kipindi kimoja cha wakati waliishi na kusoma Kiungani. Mitaala ilisisitiza heshima, elimu, imani na michezo. Wanafunzi wazuri walifanywa kuwa walimu na wanafunzi bora kuliko wote walifanywa kuwa mapadri.


Serikali ya Zanzibar ilitoa stempu mwaka 1963 kuadhimisha historia ndefu ya uvumilivu wa kidini Zanzibar.

Picha hizi za Stempu, kutoka kushoto kwenda kulia,
Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Kanisa Kuu la Kristo,
Msikiti wa Malindi, Msikiti wa Hujjatul Islam,
Hekalu la Kihindi.
Imekusanywa na kuhaririwa na Barghash mwaka 2006,
No comments:
Post a Comment