Thursday, April 12, 2012

Adabu za kufanya mapenzi!



1.Mtume s.a.w.w. amesema:
"Msisuhubiane na wake zenu kama kuku.Fanyeni mapenzi ya kutosha,mubusu na hatimaye munapojawa na raha ndipo musuhubiane”.

2.Watu wengi wanachukulia mambo ya kishetani katika kusuhubiana huku wakipuuza njia aliyoihalalisha Allah swt. Wao wanaingilia njia ya nyuma i.e. panapopitia choo kwa kisingizio cha kupata raha zaidi kumbe kunakujitumbukiza katika hatari ya kuweza kuambukizwa magonjwa hatari kabisa kwa sababu hiyo ni nafasi ya kupitia uchafu mtupu uliojaa magonjwa ya kila aina. Kwa msomaji ni ushauri wangu kuwa aonane na mganga (daktari)ili aweze kupata ukweli na uhakika wa swala hili ili aweze kuelewa vyema falsafa ya Islam katika swala hili.

3.Manukato ya maua na mafuta mazuri yanaweza kuwafanya kustarehe zaidi katika kusuhubiana.

4.Kwa kubaki mbali na mke kwa kipindi kirefu bila ya kusuhubiana naye au kwa udhuru mwingine wa kisheria haifai kumtukana au kumuudhi kwani kunaweza kwa urahisi kumfanya mke aende nje kwa waume wengine na hapa bwana ndiye atakaye wajibika.

5.Wataalamu wanasema kuwa bibi na bwana wanaposuhubiana,inawabidi wasiingiliane tena illa baada ya siku tatu au hata zaidi.Ingawaje hakuna ushahidi wa kuleta madhara.

6.Haifai kusuhubiana wakati tumbo likiwa limejaa (ameshiba) au likiwa tupu (njaa) bali baada ya kula iwapo utakuwa umepita muda wakutosha,basi hakuna madhara.

7.Baada ya kusuhubiana kwa bibi na bwana,wasioshe sehemu zao za siri kwa maji baridi wala wasioge kwa maji baridi kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuwaingiza katika magonjwa mengi mno na kuna uwezekano mkubwa wa mishipa kulegea.Lakini kusafisha kwa kitambaa chenye maji si vibaya.Bibi na bwana hawatakiwi kusafisha sehemu zao za siri kwa kutumia kitambaa kimoja tu kwani kunapunguza mapenzi baina yao.

8.Baada ya kusuhubiana wote wawili wanashauriwa kujisaidia haja ndogo (kukojoa mkojo) na kwa kufanya hivyo mishipa haitalegea.

9.Kusuhubiana kwa kijana mwenye umri mdogo na mwanamke mwenye umri mkubwa ni hatari sana kwa siha ya mwanamme kwani ni sawa na sumu kali sana.

10.Umri wa mwanamke: kuanzia miaka kumi na miwili hadi ishirini ni kama bibi harusi,na katika umri huu anaweza kutoa uridhisho mzuri kabisa katika kusuhubiana.Vile vile kuanzia umri wa miaka ishirini hadi thelathini anaweza kutoa uridhiano mzuri na bwana pia anaweza kuridhika. Na mwanamke kuanzia thelathini hadi arobaini si mbaya. Kuanzia arobaini hadi hamsini huwa hisia zimekuwa sugu,hata hivyo hana madhara.

11.Mtume s.a.w.w. alimwambia Imam Ali a.s. "Ewe Ali! Unapomleta mke wako nyumbani mwako,ondoa viatu vyake ili aweze kuketi vyema na uoshe vikanyagio vya miguu yake na kumwagilia maji hayo mlangoni na kona zote na kuta za nje ya ya nyumba;kwa kwa kufanya hivyo kutaondoa mawazo na shida sabini elfu na kutakuletea baraka na rehema sabini elfu za Allah swt.Na vile vile kila kona ya nyumba itakuwa imebarikiwa na bibi harusi atakuwa amehifadhika na ugonjwa wa kichaa,kubabuka ngozi kichwani na ukoma.Usimpatie kwa siku saba za kwanza maziwa,siki,giligilani na tufahachachu.Alipouliza Imam Ali a.s. sababu yake,alijibiwa:"kwa kula vitu hivyo,mwanamke anapoteza nguvu za kushika mimba na hawezi kuzaa mtoto.Kipande cha mkeka kilichotupwa nyumbani ni bora kuliko mwanamke asiyezaa."

(1). Wakati unaokatazwa:



1.Ni haramu kusuhubiana na mwanamke anapokuwa katika haidh (mwanamke anapotokwa na damu ya kila mwezi) au nifas (damu inayotoka baada ya kuzaa),na vile vile si vyema kumgusa kuanzia sehemu zake za siri hadi magoti yake.
2.Hairuhusiwi kusuhubiana na mwanamke baada ya kufunga damu ya haidh na nifas na kabla ya mwanamke hajaoga (hajafanya ghusl) Maulamaa wengi wanasema kuwa ni haramu kusuhubiana na kwa hakika ndivyo inavyotakiwa lakini iwapo mtu atataka kusuhubiana,basi itawabidi wasafishe vyema sehemu hizo ndipo waweze kusuhubiana.
3.Iwapo mtu atapenda kusuhubiana na mwanamke aliye katika Istehadha (zisizozidi siku zaidi ya haidh) basi itambidi huyo mwanamke aoge istehadha na kukamilisha masharti yote ya istehadha ndipo hapo atakapoweza kusuhubiana naye.
4.Kila wakati mwanamme anaposuhubina na mke wake haruhusiwi kumwaga nje manii (shahawa au mbegu za kiume) nje ya uuke wa mke bila ya ruhusa ya mke wake na baadhi ya Maulamaa wanasema kuwa ni haramu kufanya hivyo.Lakini hata hivyo anaposuhubiana na kijakazi wake anayo ikhtiyari ya kufanya hivyo.Lakini wataalamu wanapinga kumwaga nje manii.
5.Haitakiwi kusuhubiana usiku wa kuamkia jumatano kwani iwapo atachukua mimba,basi kuna uwezekano wa kuanguka kwa mimba kabla ya kufikia muda wake na iwapo itakamilika basi kunaweza kuzaliwa kwa mtoto mwendawazimu au mwenye ugonjwa wa yabisi.
6.Haitakiwi kusuhubiana siku za mwanzoni,katikati na mwishoni mwa kila mwezi kwani vile vile kuna hatari ya kuanguka kwa mimba changa na iwapo atazaliwa mtoto basi kunauwezekano wa kuwa mwendawazimu au mwenye yabisi.
7.Wakati wa kusuhubiana haitakiwi kuzungumza kwani kunauwezekano wa kuzaliwa kwa mtoto kiziwi.
8.Wakati wa kusuhubiana hairuhusiwi kuangalia sehemu za siri kwani kunahatari ya kuzaliwa kwa mtoto kipofu,lakini katika riwaya nyingine inaelezea kuwa hakuna ubaya wowote ule.Mbali na wakati wa kusuhubiana,hapana makatazo ya aina yoyote ile katika kutazamana.
9.Iwapo kutakuwa kumepakwa khizaab,basi haitakiwi kusuhubiana.
10.Vile vile hairuhusiwi kusuhubiana wanapokuwa katika maji.
11.Hairuhusiwi kusuhubiana mbele ya watoto kwani kuna hatari ya kuzaliwa mtoto mzinifu.
12.Iwapo kutakuwa na aliye macho au asikiaye sauti za wakati wa kusuhubiana,basi haitakiwi kusuhubiana wakati huo.
13.Iwapo mtu atasuhubiana na kijakazi wake mmoja na kuwa na hamu ya kusuhubiana na kijakazi wa pili basi itambidi afanye wudhuu (kutawadha) kwanza.
14.Hairuhusiwi kuwalaza wanawake wawili (iwapo mtu atakuwa na wake wawili) kwa pamoja kitanda kimoja lakini anaruhusiwa kwa ajili ya vijakazi wawili.
15.Hairuhusiwi kusuhubiana huku uso au mgongo ukielekea Qibla.
16.Vile vile hairuhusiwi kusuhubiana wakati wanapokuwa wakisafiri katika meli au jahazi.
17.Iwapo mtu alitokwa na manii bila ya kusuhubiana, (akiwa usingizini au kwa sababu zinginezo) basi itambidi kwanza afanye ghusl-i-janaba, ndipo aweze kusuhubiana kwani bila ya kufaya hivyo kuna uwezekano wa kuzaliwa mtoto mwendawazimu.
18.Ni haramu kusuhubiana wakati wa kupatwa kwa jua na mwezi au kunapotokea mtetemeko au jua lionekanapo kuwa rangi njano.
19.Kusuhubiana wakati wa adhuhuri kunaweza kuzaliwa mtoto mwenye macho makengeza.
20.Imam Ali a.s. amesema:"Iwapo utamwona mwanamke wa nje na iwapo utaghalibiwa na Sheitani hata ukatamani kusuhubiana na mke wako,basi usithubutu kufanya hivyo kwani ujiambie kuwa kile alichonacho huyo hata mke wako pia anacho.Na iwapo atakuwa hana mke,basi inambidi asali rakaa mbili na kumwomba Allah swt amjaalie mke,naye atapata kuoa."
21.Iwapo watasuhubiana wakiwa wamesimama,basi kunauwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na tabia ya kujikojolea kitandani hata akiwa na umri mkubwa.
22.Iwapo kutasuhubiwa katika usiku wa Idd ul-Fitr, mtoto atakayezaliwa atakuwa na maovu mengi mno.
23.Vile vile inabidi kujiepusha na kusuhubiana usiku wa Idd ul-Adh-ha kwa sababu kunauwezekano wa kuzaliwa mtoto mwenye vidole vinne au sita.
24. Kwa sababu ya kusuhubiana chini ya miti ya matunda, mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa kiongozi wa dhalimu.
25. Haitakiwi kusuhubiana wakati miale ya jua ikiwaelekea kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye wasiwasi hadi kufa kwake.
26. Hairuhusiwi kusuhubiana baina ya Adhaan na Iqamah mtoto atakayezaliwa atakuwa daima mwenye kutaka kumwaga damu yaani muaji.
27. Kutaka kusuhubiana na mwanamke mwenye mimba, inabidi mwanamme awe katika hali ya wudhuu kwani bila hivyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye roho ngumu na mchoyo.
28. Haitakiwi kusuhubiana usiku wa tarehe kumi na tano ya Shaaban, kwani mtoto atakayezaliwa hatakuwa
mwenye bahati na atakuwa na madoti meusi usoni mwake.
29. Hairuhusiwi kusuhubiana katika siku za mwisho za mwezi wa Shaaban kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa jambazi na mwenye ukatili na kuna hofu ya kuwaua watu wengi mno.
30. Hairuhusiwi kusuhubiana juu ya paa za nyumba kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mlaghai na asiye na imani.
31.Haitakiwi kusuhubiana usiku wa kuamkia safari kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye kutumia vibaya mali ya watu na watu kama hao ni ndugu wa masheitani.
32.Atazaliwa mtoto asiye na raha kwa sababu ya kusuhubiana wakati wanapokuwa wazazi katika safari isiyozidi siku tatu.
33.Iwapo kutasuhubiana wakati wa mwanzoni mwa usiku basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mchawi na ambaye ataithamini dunia kuliko Aakhera.
34. Hairuhusiwi kusuhubiana mahala ambapo ni wazi kama chini ya mbingu.
35.Allah swt,Mitume na Aimma a.s.,Malaika pamoja na wanaadamu pia hulaani vikali mno kule kusuhubiana barabarani au njiani ambapo hupitwa na watu.
36.Iwapo mtu atakuwa anatakiwa kuoga ghusl-i-Mayyit basi hatakiwi kusuhubiana na iwapo atataka kufanya hivyo,basi itambidi afanye wudhuu
37.Iwapo mtu atapenda kusuhubiana kwa mara ya pili baada ya kwanza,basi itambidi afanye wudhuu.
38.Iwapo mtu atataka Shaitan asiwe mshiriki katika kusuhubiana kwao,basi aiseme kikamilifu "Bismillah".
39.Baada ya ndoa,haifai kusuhubiana kwa mara ya kwanza katika 'tahtush-shoaa' (usiku mbili au tatu za mwisho za mwezi ambapo mwezi hauonekani).
40.Ni haraam kusuhubiana wakati mwanamke anapokuwa katika haidh na nifas, na kwa kukiuka kunatakiwa kulipa kaffarah yake.
41.Mtume s.a.w.w. amesema iwapo atazaliwa mtoto mwenye ugonjwa wa ukoma,basi wazazi ndio watakaojilaumu.
42.Ipo riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Imam Jaafer as-Sadiq a.s."Adui wetu sisi Ahlul-Bait a.s. ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. ama atakuwa ni waladuz-zinaa au waladul-Haidh. Hivyo mtu akiona kuwa moyoni mwake anayo mapenzi ya Ahlul-Bayt a.s. basi amwombee kheri mama yake mzazi kwa kutomzaa mwana haramu." Ipo riwaya moja isemayo "alikuwa baba mmoja akisema kuwa mtu mwenye mapenzi ya Ahli Bayti a.s. ni mwana halali na mwenye uadui nao ni waladuz-Zinaa. Basi mtoto wake alimwambia baba yake kuwa yeye alikuwa adui mkubwa wa Ahli-Bayti a.s. Sasa jee yeye alikuwa ni waladuz-zinaa ?
Baba yake alimwambia akamwulize mama yake kwani yeye anavyoelewa, alikuwa kweli mwana haramu kwa sababu baba yake alifanya mapenzi na mama yake na walisuhubiana kabla ya ndoa, na mama yake akashika mimba. Baadaye walifanya tawba na kufunga ndoa.Hivyo,kwa kifupi alizaliwa kabla ya wao kufunga ndoa.
43.Haifai kusuhubiana na mke mmoja mbele ya mke wa pili lakini haina shida iwapo kutasuhubiana na kijakazi mbele ya kijakazi mwingine.
44.Haifai kusuhubiana katika hali ya kuwa uchi kabisa bila kujifunika kwani kunawafukuza Malaika.Lakini walimwuliza Imam Musa al-Kadhim a.s. iwapo nguo ikisogea,naye alijibu kuwa hapakuwa na matatizo.
45.Iwapo mtu atasuhubiana na mwanamke aliyepakaa rangi kichwani,basi mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa khanisi.
46.Inambidi mtu aondoe pete alizovaa ambazo zimechongewa majina matukufu au naqshi kabla ya kusuhubiana.
47.Haifai kusuhubiana iwapo kuna shida ya kupata maji kwa ajili ya kufanya ghusli
48.Ni makrooh (karaha) kusuhubiana wakati wa alfajiri kabla hapajapambazuka au kuchwa kwa jua kamili.
49.Ni vyema kufunga macho wakati wa kusuhubiana.
50. Hairuhusiwi kusoma Quran Tukufu katika kitanda ambapo wamesuhubiana bibi na bwana na bado hawajaoga ghusl-i-janabakwani kutaweza kusababisha adhabu ya Allah swt kuwaadhibu wote wawili.

(2). Wakati unaopendekezwa:

1.Ni Sunnah kusuhubiana usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani.
2.Mtoto atakayezaliwa kwa kusuhubiana usiku wa jumatatu basi atakuwa (hafidhi Quran) mwenye kuihifdhi
Quran kwa moyo na Allah swt atakuwa amemwia radhi na kwa bahati yake njema.
3.Mtoto atakayezaliwa kwa sababu ya kusuhubiana usiku wa jumanne,iwapo ni mvulana atapata ufalme wa Din ya Islam yaani atakuwa mwema mno na roho yake itakuwa yenye huruma,mikono yake madhubuti na ulimi wake utakuwa umehifadhika na ghibah na buhtan (kusengenya na kusingizia) watu.
4.Kwa kusuhubiana usiku wa alhamisi (kuamkia ijumaa),na mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa Hakimu wa Shariah au atakuwa Aalim.
5.Kwa kusuhubiana wakati wa mchana wa siku ya Ijumaa mtoto atakayezaliwa atakuwa amekaa mbali na Shaitan na Allah swt atamjaalia usalama wa Din na dunia.
6.Ukimwona mtoto ni mzungumzaji wa lugha tamu na msomaji wa khutbah basi ujue kuwa huyo ni matokeo ya kusuhubiana usiku wa Ijumaa.
7.Mtoto atakayezaliwa kwa kutokana kusuhubiana baada ya adhuhuri ya Ijumaa ,basi atakuwa akijulikana kwa ukarimu wake.
8.Kwa kusuhubiana baada ya salat al-'Ishaa ya siku ya Ijumaa,mtoto atakayezaliwa atakuwa ni mwenye wadhifa katika Din

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget