Kwa jina la Allah,
Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
1. kumbuka kwamba Uislamu ni wa Allah,
Sub-hanahu wa Ta'ala. kwa hivyo ni muhimu wewe uingie katika Uislamu kwa sababu
(na makusudio) ya Allah pekee, na wala sio
kwa kutaka manufaa yoyote ya kibinafsi au kwa lengo la yasiyokuwa Twaa (kumtii Muumbaji).
2. Binadamu anapoupata ukweli huwa ni wajibu
kwake kuushikilia na kuutetea kwa vyovyote vile, bila kujali yatakavyokuwa
matokeo. Zaidi ya hayo, sharti awe na subira ili aweze kuwa na uthabiti katika
huo ukweli (ambao amupata).
3. kuwapendelea wenzako mema unayoyapenda
wewe, ni sehemu ya shukurani kwa Allah, Aliye juu, Mtukufu aliye mkuu, kwa
neema hii ya Uislamu aliyokutunuku (aliyokupa).
Kwa hivyo wakaribishe wenzako, ili nao wapate sehemu yao ya Neema hii Tukufu (Uislamu).
4. Uislamu sio mali ya mtu yeyote. Sio Mali ya
Waarabu kwa kuwatenga wasiokuwa Waarabu, wala sio Mali ya Matajiri kwa
kuwatenga masikini. Kwa hakika ni uwanja ulio wazi kwa wote, na zaidi ni kwamba
aliye Mtukufu mbele ya Allah kuwashinda wenzie ni yule anayewazidi wenzake
katika kushikamana na mafundisho, kwa kuwa anatenda kama inavyohitajika na
ndiye anayetarajiwa zaidi kuwa katika daraja ya juu siku ya kiama (siku ya kufufuliwa).
5. Kumbuka kwamba baada ya wewe kuwa Muislamu
utapata marafiki wapya kama watakavyozuka pia maadui - kiongozi wao akiwa
Shetwani - na atajaribu kuweka kizuizi baina yako na Uislamu, au kwa kiwango
cha chini sana, kukuzuilia maendeleo ndani ya dini yako, ili pia usiwanufaishe
wenzako.
6. Allah,
mwenye Uwezo wote na Utukufu na Ufalme ndiye Msaidizi wako, asiyekuwa na shaka.
kwa hivyo, kumbuka kwamba ikiwa Allah Atatambua kwamba wewe ni muaminifu Rohoni
mwako, fahamu naye Atakutendea wema unaofaa Duniani na Akhera.
7. Uislamu ni mfumo wa maisha uliopangwa vizuri,
utokao kwa Mola wa ulimwengu. Na pia ni kama vile katiba. Kuhusu waislamu wote,
wao ni binadamu tu ambao baadhi ya wakati, wanafanya makosa au wanakosea
wakijitahidi kufanya mema. Baadhi yao wanaushikilia Uislamu vyema na hali kunao
walio wapungufu, ki-elimu au ki-tabia au ki-ibada. Kwa hivyo yeyote miongoni
mwao anayetenda yaliyo sawa, ni kutokana na kuwa anafahamu Uislamu vyema. Na
vitendo anavyovitenda vinakuwa ndiyo sawa. Vile vile anayetenda yasiyo sawa, basi
makosa yake yatamletea yeye madhara. Haiwezekani kuulaumu Uislamu kwa makosa
yanayotendwa na mtu au watu ambao hawakutekeleza vyema mafundisho ya Uislamu.
8. Pengine Waislamu walifurahi sana kwa wewe
kujiunga na mila hii (ya Nabii Ibrahim), na
pengine walikukaribisha sana pale mwanzo. Haya ni kutokana na wanavyokupenda.
pamoja na hivyo ni muhimu Allah, Mwenye Nguvu na Utukufu, aone uaminifu wako
katika Roho yako na katika vitendo vyako.
9. Uislamu ni mfumo ulio na mpangilio wa maisha
bora, kama vile Mashule yanavyokuwa na mpangilio wa kuwalea wanafunzi (yaani Manhaj au syllabus). Na ni njia ya maisha
inayofaa kufuatwa na kufuatiliwa katika maisha yote. Kwa hivyo, kama
unavyoamrisha Uislamu Mtu kuswali, kufunga (saum),
kutoa zaka na sadaka, na kwenda kuhiji Makka, pia unaamrisha Mtu kuwa muaminifu
na mkweli katika maongezi (kauli), mwenye
huruma kwa walio wadhaifu na maskini. Aliye na heshima kwa wazee na anaishi na
watu vizuri. Vile vile kama unavyokataza Uislamu Mtu kulewa na kuzini (na mke wa watu au binti yao), hivyo hivyo ndivyo
unavyokataza Dhulma, Wivu, Uhasidi na Tabia mbaya. Kwa ufupi Uislamu unaamrisha
kila wema na maarifa yenye manufaa na unakataza kila ubaya unaodhuru watu (iwe ni Maneno au Vitendo au Itiqadi).
10. Allah Amefanya Maisha ya hii Dunia kuwa
pahala pa kufanyiwa Watu Mtihani ili kupambanua Ukweli na Uwongo, na yaliyo
sawa na yaliyo makosa. Vile vile Allah, Sub-hanahu wa taala, Ametenga mtihani
maalumu kwa Waumini, ili kuchunguza (imani ya)
Roho zao. Kwa njaa au umasikini au
maradhi au kuondokewa na wapenzi, kwa mauti au mitihani aliyoichagua Allah, ili
kuwapandisha ngazi (peponi ikiwa walikuwa na subira
na kudumu katika Imani na haki na vitendo vizuri). kwa hivyo kumbuka
ukweli huu unapokuwa Maishani mapya.
11. Ni
jambo la dharura kuwa Muislamu anahitajika kuwa mwenye nguvu, anayefurahia (kujivunia) Maisha yake mapya. Sio lazima kila
wakati kuwa anachukua nafasi ya kujilinda. Badala yake anafaa pia kuwapa watu
aliyonayo yeye (yaani Uislamu), akiwa na
heshima zake na kujivunia Dini yake. kwa ukweli yeye ndiye aliye na bidhaa
tukufu na takatifu zaidi. Wakati huo huo anafaa kuwa mwenye Hikima na mwenye
Subira wakati anaongea na kutekeleza lolote na binadamu wenzake.
12. Uislamu sio tu kutamka LA ILAHA ILLA ALLAH, MUHAMMAD RASUULU LLAHI. Kwa kweli mfumo wa amri kutoka
mbinguni (SHARIA) ndiyo unaoendesha maisha ya mwanadamu vyema na
kikamilifu. Uislamu unazo hukumu (ahkaam),
Aadabu (adabu au mpangilio wa kutekeleza mambo),
Ibaadat (vitendo vya kuabudia) na Muamalaat,
yaani tartibu za kutendeana baina ya Mtu na Watu (katika
jamii au biashara). Kwa hivyo inahitaji mtu kujifundisha Uislamu hatua
kwa hatua.
13. Mwisho tunakuhimiza ujiunge na chuo cha
kufunza Waislamu wapya. vyuo ambavyo huwa vimeanzishwa pahali tofauti tofauti
katika vituo vya Da'awa (vituo vya makaribisho),
ili upate kuelimika kuhusu mambo yote ya Uislamu.
No comments:
Post a Comment