Friday, April 6, 2012

Wanawake katika Uislamu,Ukristo & Uyahudi
Wanawake katika Uislamu
Ukilinganisha na Wanawake katika
Mafundisho ya Kiyahudi-Kikristo:
Hadithi za kubuni na uhakika
Dr. Sherif Abdel Azeem

Wanawake katika Uislamu
Ukilinganisha na Wanawake katika
Mafundisho ya Kiyahudi-Kikristo
Hadithi za kubuni na uhakika
DR. SHERIF ABDEL AZIM
Ph.D. - QUEENS UNIVERSITY,
KINGSTON, ONTARIO, CANADA
1

Yaliyomo
U
UTANGULIZI .................................................................................................. 3
SEHEMU 1- KOSA LA HAWA (EVA) ............................................................... 6
SEHEMU 2- URITHI WA HAWA ..................................................................... 7
SEHEMU 3 - MABINTI WANAOTIA AIBU ................................................... 11
SEHEMU 4 – ELIMU KWA WANAWAKE ...................................................... 13
SEHEMU 5 – MWANAMKE MWENYE HEDHI SI MSAFI .............................. 15
SEHEMU 6 – HAKI YA KUTOA USHAHIDI ................................................. 16
SEHEMU 7 - UASHERATI ............................................................................ 18
SEHEMU 8 - KULA KIAPO NA KUWEKA NADHIRI..................................... 20
SEHEMU 9 – MALI ZA MKE ........................................................................ 22
SEHEMU 10 – TALAKA ................................................................................ 25
SEHEMU 11 – AKINA MAMA ..................................................................... 31
SEHEMU 12 – MIRATHI KWA WANAWAKE. ............................................. 34
SEHEMU 13 – HALI MBAYA YA WAJANE .................................................... 36
SEHEMU 14 – UKEWENZA .......................................................................... 38
SEHEMU 15 – HIJABU ................................................................................. 45
SEHEMU 16 – HITIMISHO .......................................................................... 50
2

UTANGULIZI
Miaka mitano iliyopita, nilisoma makala katika gazeti la Toronto Star toleo la Julai 3,
1990, yenye kichwa ‘‘Uislamu sio pekee wenye itikadi ya kuwatukuza wanaume’’,
iliyoandikwa na Gwynne Dyer. Makala hiyo ilichambua majibu makali mno kutoka
kwa washiriki wa mkutano juu ya wanawake na kushika Madaraka uliofanyika
Montreal ili kujibu maelezo ya mtetezi maarufu wa haki za wanawake kutoka Misri,
Dr. Nawal Saadawi. Taarifa yake ambayo kisiasa si sahihi inajumuisha: ‘‘viini vyenye
vikwazo vingi kwa wanawake vinapatikana, kwanza kabisa katika Uyahudi katika
Agano la Kale, kisha katika Ukristo na katika Quran’’ ‘‘dini zote zinatukuza
wanaume kwa sababu zote zimeanzishwa kutokana na misingi ya jamii zenye
kutukuza wanume’’ na ‘‘hijabu za wanawake si matendo ya Kiislamu peke yake
lakini ni utamaduni wa kale uliorithiwa wenye kufanana na dini ya kisista (utawa).’’
Washiriki walishindwa kuvumilia na kukaa chini, huku imani zao zikilinganishwa na
Uislamu. Kwa hiyo, Dr. Saadawi alipokea mlolongo wa kukosolewa. ‘‘Maelezo ya
Dr. Saadawi hayakubaliki. Majibu yake yanaonyesha ukosefu wake wa kutofahamu
imani za watu wengine,’’ alitamka Bernice Dubois wa Maendeleo ya Kinamama
Duniani. ‘‘Lazima nizuie’’ alisema mwanajopo Alice Shalvi wa mtandao wa
wanawake wa Kiisraeli, ‘‘Hakuna itikadi ya hijabu katika Uyahudi.’’ Makala hiyo
imetoa upinzani huo mkali kwa mtazamo mkali wa Kimagharibi, kwani kuusingizia
Uislamu kuwa ndio unaotekeleza hayo ni sehemu ya urithi wa utamaduni wa
Kimagharibi. ‘‘Watetezi wa haki za Wanawake wa Kikristo na Kiyahudi
hawakuridhia kuendelea kukaa na kujadili kwa namna ile ya kuwapo kundi moja na
Waislamu, ambao ni Waovu.’’ Imeandikwa na Gwynne Dyer.
Sikushangazwa kuona washiriki wa mkutano huo wameshikilia msimamo mbaya
dhidi ya Uislamu, na hasa hasa inapohusika kadhia ya wanawake. Katika nchi za
Magharibi, inaaminika kuwa Uislamu ndio alama ya kuwadhalilisha na kuwadunisha
wanawake kupita kiasi. Ili kufahamu kwa kiasi gani imani hiyo ilivyo, inatosha
kuonyesha kuwa Waziri wa Elimu wa Ufaransa, nchi ya mabadiliko (Voltaire), hivi
karibuni ameagiza wafukuzwe wasichana wote wa Kiislamu wanaovaa hijabu
                              1
watolewe shule za Ufaransa! Mwanafunzi msichana wa Kiislamu avaae kitambaa
cha kufunika kichwa ananyimwa haki yake ya kupata elimu nchini Ufaransa huku
wanafunzi wa Kikatoliki wavaao misalaba au wanafunzi wa Kiyahudi wavaao kikofia
cha Kiyahudi hawazuiwi. Mandhari ya Polisi wa Kifaransa wakiwazuia wasichana
wa Kiislamu wanaovaa vitambaa vya kufunika vichwa wasiingie shule zao za
sekondari ni jambo lisilosahaulika. Jambo hilo linaibua kumbukumbu ya tukio lingine
la fedheha linalomuhusu Gavana George Wallace wa Alabama mwaka 1962 akiwa
amesimama mbele ya geti la shule huku akijaribu kuzuia kuingia wanafunzi weusi ili
kuulinda Ubaguzi wa Rangi wa shule za Alabama. Tofauti ya matukio mawili hayo ni
kuwa wanafunzi weusi walionewa huruma na watu wengi wa Marekani na dunia
nzima.
1
The Globe and Mail, Oct. 4, 1994.
3

Rais Kennedy alitumia jeshi la ulinzi wa taifa la Marekani ili kulazimisha kuingia
kwa wanafunzi hao weusi. Kwa upande mwingine, wasichana wa Kiislamu,
hawakupokea msaada wowote kutoka kwa yoyote yule. Sababu yao ilikuwa inatia
huruma kidogo sana ndani ya Ufaransa au nje. Sababu yenyewe ni yenye kuenea sana
nayo ni kutofahamika vizuri na woga juu ya kila kitu cha Kiislamu ulimwenguni leo
hii.
Kile kilichonivutia sana katika mkutano wa Montreal kilikuwa ni swali mojawapo:
Je, maelezo yaliotolewa na Saadawi, au yoyote katika wakosoaji wake ni ya uhakika?
Kwa maneno mengine, Je, dini ya Uyahudi, Ukristo na Uislamu zina itikadi
inayofanana juu ya wanawake? Je, dini hizi zinatofautiana kiitikadi? Je, ni kweli
kuwa, Uyahudi na Ukristo unawatendea vyema wanawake kuliko Uislamu? Ukweli
ni upi?
Si rahisi kutafuta na kupata majibu ya maswali haya magumu. Ugumu wa kwanza
kabisa ni kuwa mtu anatakiwa awe mwadilifu na asiegemee upande wowote au, kwa
uchache, afanye kila liwezekanalo ili awe hivyo. Na hivyo ndivyo unavyofundisha
Uislamu. Quran imewafundisha Waislamu waseme ukweli hata ikiwa dhidi ya watu
wa karibu yao. ‘‘…Na sema (katika shahada na penginepo) Semeni kwa insafu
ingawa ni jamaa; Quran (6: 152) ‘‘Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha
uadilifu, mtowapo ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; ijapokuwa ni juu ya nafsi
zenu, au (juu ya) wazazi (wenu) na jamaa (zenu). Akiwa tajiri au masikini (wewe
usitazame). (Quran 4: 135).
Jambo jengine lilogumu sana ni kuushinda upeo wa mapokezi na kuvumilia kadhia
hiyo. Kwa hiyo katika kipindi cha miaka michache ya hivi karibuni, nimetumia
masaa mengi kuisoma Biblia, ensaiklopidia ya dini na ensaiklopidia ya Uyahudi
nikitafuta majibu. Pia nimesoma vitabu vingi vinavyojadili nafasi ya mwanamke
katika dini mbalimbali vilivyoandikwa na wanazuoni (wataalamu), watetezi, na
wakosoaji. Taarifa zilizowasilishwa katika sura zifuatazo zinaleta matokeo muhimu
yaliyopatikana kutokana na uchunguzi huu wa kinyenyekevu. Sidai kuwa sikuegemea
upande wowote ule kikamilifu. Kwani jambo hilo lipo nje ya uwezo wangu. Kile
ninachoweza kusema ni kuwa nimejaribu, kwa kupitia utafiti huu, nikaribie ukamilifu
wa Quran wa kuongea kiadilifu.
Ningependa kusisitiza katika utangulizi huu kuwa lengo langu katika utafiti huu si
kuupaka matope Uyahudi wala Ukristo.
Tukiwa kama Waislamu, tunaamini kuwa kuna asili ya utakatifu kwa mitume wote
wawili. Hakuna mtu atakaye kuwa Mwislamu wa kweli bila ya kuwaamini Musa na
Yesu kwamba wao ni mitume mikuu ya Mwenyezi Mungu. Lengo langu ni
kuuthibitisha na kuutukuza Uislamu, na kuupa ujumbe wa mwisho wenye kuaminika,
utokao kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa jamii ya wanadamu kile inachokistahiki
kwa muda mrefu katika nchi za Magharibi. Vile vile napendelea kutilia mkazo kuwa
mimi nazingatia na najihusisha sana na mafundisho ya dini husika. Na hilo, ndilo
nitakalojihusisha nalo, kwa kiasi kikubwa, nafasi ya mwanamke katika dini tatu kama
4

ilivyo katika vyanzo asilia vya dini hizo na sio mambo yanayotendwa na mamilioni
ya wafuasi wa dini hizo ulimwenguni leo hii.
Kwa hiyo, ushahidi mwingi utakaokuwepo katika kitabu hiki umetokana na Quran,
hadithi za mtume Muhammad (S.A.W.), Biblia, Talmudi (kitabu cha Wayahudi), na
maneno ya baadhi ya Mapadri wa makanisa wenye mvuto mkubwa na ambao
mitazamo yao imetoa mchango usiokadirika katika kuufahamisha na kuutengeneza
Ukristo. Hamu hii ya kupata vyanzo asilia inafungamana na ukweli kwamba
kuifahamu dini fulani kutokana na mitazamo na mienendo ya baadhi ya wafuasi wake
kwa majina ni upotoshaji. Watu wengi wanachanganya utamaduni na dini, na
wengine wengi hawajui vitabu vyao vya kidini vinasema nini, na wengine wengi
hawajali kabisa.
5

SEHEMU 1- KOSA LA HAWA (EVA)
Dini tatu hizi zinakubaliana juu ya hakika moja ya msingi: wanawake na wanaume
wote wameumbwa na Mungu, ambaye ni Muumba wa ulimwengu wote. Hata hivyo,
tofauti zinaanzia punde tu baada ya kuumbwa mwanamume wa kwanza - Adam na
mwanamke wa kwanza – Hawa. Itikadi ya uumbwaji wa Adam na Hawa kwa
Wayahudi na Wakristo imesimuliwa, kwa ukamilifu, katika kitabu cha mwanzo 2:4-
3:24. Mungu aliwakataza wote wawili wasile matunda ya mti uliokatazwa. Nyoka
alimshawishi Hawa ale matunda ya mti huo na Hawa, naye, akamshawishi Adam ale
pamoja naye.
Wakati Mungu alipomkaripia Adam kwa alichokifanya, Adam naye akamtupia Hawa
lawama zote, Mwanzo 3:12 ‘‘Adam akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe
pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.’’ Kwa matokeo hayo,
Mungu alimwambia Hawa: Mwanzo 3:16 “Akamwambia mwanamke, Hakika
nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa
yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.’’ Na kwa Adam Mungu alimwambia:
‘‘Kwa kuwa umesikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti…ardhi
imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha
yako…’’ Itikadi ya Kiislamu juu ya uumbwaji wa mwanzo inapatikana sehemu
nyingi ndani ya Quran, kwa mfano:
 ‘‘(Kisha Mwenyezi Mungu akasema kumwambia Nabii Adam) ‘‘Na wewe Adam!
Kaa Peponi pamoja na mkeo, na kuleni mnapopenda, lakini msiukaribie mti huu
msije kuwa miongoni mwa waliodhulumu (nafsi zao.) Basi Shetani (naye ni yule
Iblisi), aliwatia wasiwasi ili kuwadhihirihishia aibu zao walizofichiwa, na akasema:
‘‘Mola wenu hakukukatazeni mti huu ila (kwa sababu hii:) msije kuwa Malaika au
kuwa miongoni mwa wakaao milele (wasife).’’ Naye akawaapia (kuwaambia): ‘‘Kwa
yakini mimi ni mmoja wa watowaoshauri njema kwenu’’ Basi akawateka (wote
wawili) kwa khadaa (yake). Na walipouonja mti ule aibu zao ziliwadhihirikia na
wakaingia kujibandika majani ya (miti ya huko) Peponi. Na Mola wao akawaita
(Akawaambia): ‘‘Je, sikukukatazeni mti huu na kukwambieni ya kwamba Shetani ni
adui yenu aliyedhahiri?’’ Wakasema: “Mola wetu! Tumedhulumu nafsi zetu; na
kama hutatusamehe na kuturehemu, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wenye
khasara (kubwa kabisa)’’ (Quran 7:19-23).
Mtazamo yakinifu juu ya fikra mbili hizi kuhusu kisa cha Uumbwaji, unafunua
baadhi ya tofauti za kimsingi. Qurani, kinyume na Biblia, inatoa lawama zilizo sawa
sawa kwa wote wawili Adam na Hawa kwa makosa yao. Hakuna sehemu hata moja
katika Quran ambapo mtu atakuta hata kidokezo kidogo sana ambacho kinaashiria
kuwa Hawa alimshawishi Adam ale katika mti huo au hata kuwa Hawa ndiye
aliyekula kwanza kabla ya Adam. Hawa katika Quran si mshawishi wala si mlaghai
na si mdanganyifu. Zaidi ya hayo, Hawa si wa kulaumiwa kwa machungu ya uzazi.
Mungu, kulingana na Quran, hamuadhibu yeyote kwa kosa la mwingine. Wote
wawili, Adam na Hawa, wametenda dhambi kisha wakamuomba Mungu msamaha
Naye akawasamehe wote wawili.
6

SEHEMU 2- URITHI WA HAWA
Taswira ya kuwa Hawa ni mshawishi iliyo ndani ya Biblia imeleta matokeo ya athari
mbaya kwa kiasi kikubwa kwa wanawake katika mafundisho ya Uyahudi-Ukristo.
Wanawake wote waliaminiwa kuwa wamerithi kutoka kwa mama yao, Hawa wa
Kibiblia, mambo mawili: zambi zake na hila zake. Kwa hiyo, wanawake wote
wakawa hawaaminiwi, madhaifu wa uadilifu, na waovu. Kupatwa na hedhi, mimba,
na kuzaa; vitu hivi vilizingatiwa kuwa ni adhabu ya uadilifu kwa dhambi ya milele ya
kulaaniwa kwa jinsi ya kike. Ili tufahamu vizuri ni naman gani mkanganyiko mbaya
juu ya Hawa wa Kibiblia ulivyokuwa kwa vijukuu vyake vya kike vyote tunalazimika
kutazama maandiko ya baadhi ya Wayahudi na Wakristo muhimu sana wa kila zama.
Hebu acha tuanzie na Agano la Kale na tuone dondoo kutoka katika kile kiitwacho
Maandiko ya Busara ambayo kwayo tunakuta: “Naona uchungu sana kuliko uchungu
wa kifo mwanamke ambaye ni ghiliba, ambaye moyo wake ni mtego na mikono yake
ni minyororo. Mwanamume anayempendeza Mungu atamuepuka mwanamke huyo,
lakini muovu atatekwa na mwanamke huyo… Wakati nilipokuwa naendelea kutafuta
bila kupata, nilipata mwanamume mmoja wa kuaminika miongoni mwa maelfu, lakini
sijapata hata mwanamke mmoja wa kuaminika miongoni mwa wanawake wote’’.
(Ecclesiastes 7:26-28).
Katika sehemu nyingine ya maandiko ya Kiyahudi ambayo yanapatikana katika
Biblia ya Kikatoliki tunasoma: “Hakuna uovu unaotokea sehemu yeyote
unaokaribiana na uovu wa mwanamke…. Dhambi huanza kwa mwanamke na
tunamshukuru mwanamke kwa kuwa sote lazima tufe’’; (Ecclesiasticus 25:19-24).
Wataalamu wa dini ya Kiyahudi wameorodhesha laana tisa zinazowatesa wanawake
ikiwa ni matokeo ya Kuporomoka: “Yeye ametoa laana tisa na kifo kwa mwanamke:
Mzigo wa damu ya hedhi na damu ya bikra; mzigo wa kubeba mimba; mzigo wa
kuzaa; mzigo wa kulea watoto; kichwa chake kinafunikwa kama vile mtu yupo katika
maombolezo; mwanamke anatoboa masikio yake kama vile mtumwa wa kudumu au
mjakazi ambaye anamtumikia bwana wake; mwanamke asiaminiwe kuwa ni shahidi;
                                2
na baada ya yote hayo… kifo.”
Kwa hivi sasa, Wayahudi wakiume wa Kiorthodoksi katika sala zao za kila siku
asubuhi wanakariri “Baraka ni za Mungu mfalme wa ulimwengu wote kwa kuwa
hajaniumba mwanamke”; Wanawake, kwa upande mwingine, wanakariri “shukraniii
                                                                  3
ni za Mungu kila asubuhi kwa kuniumba kulingana na Matakwa yake.”
Dua nyingine inayopatikana katika vitabu vingi vya dua za Kiyahudi: “Shukrani ni za
Mungu kwa kuwa hajaniumba nikiwa mtu wa mataifa (mtu ambaye si Myahudi).
2
 Leonard J. Swidler, Women in Judaism: the Status of Women in Formative Judaism (Metuchen, N,J: Scarecrow Press,
1976) p. 115.
3
 Thena Kendath, “Memories of an Orthodox youth” in Susannah Haschel ed. On being a Jewish Feminist (New
         York:Schocken Books, 1983), pp. 96-97.
7

Shukrani ni za Mungu kwa kuwa hajaniumba mwanamke. Shukrani ni za Mungu kwa
                          4
kuwa hajaniumba mjinga.’’
Hawa wa Kibiblia amechukua sehemu kubwa katika Ukristo kuliko katika Uyahudi.
Dhambi yake imekuwa nitegemeo kwa imani yote ya Kikristo kwa sababu itikadi ya
Kikristo juu ya sababu za kazi ya Yesu Kristo Duniani imejengwa kutokana na maasi
ya Hawa wa Biblia kwa Mungu. Hawa alifanya dhambi kisha alimshawishi Adam
afuate mkumbo wake. Kwa hiyo, Mungu aliwafukuza wote wawili watoke Peponi
waende ardhini, ardhi ambayo imelaaniwa kwa ajili yao. Walirithisha dhambi yao,
ambayo haikusamehewa na Mungu, kuwarithisha kizazi chao chote na kwa hiyo,
binadamu wote wanazaliwa wakiwa na dhambi. Ili kuwatakasa wanadamu kutoka
katika “dhambi zao za asili,” Mungu alilazimika kumtoa muhanga msalabani, Yesu,
ambaye anazingatiwa kuwa ni mwana wa Mungu. Kwa hiyo, Hawa anabeba kosa
lake, dhambi ya mumewe, dhambi ya asili ya binadamu wote, na kifo cha Mwana wa
Mungu. Kwa maneno mengine, matendo ya mwanamke mmoja kwa nafsi yake
                                         5
yamesababisha kuangamia kwa binadamu. Je, kuna nini kwa mabinti zake? Hao nao
ni wakosaji kama yeye na wanalazimika kutendewa kama alivyotendewa yeye.
Sikiliza muono wa kuhuzunisha wa mtakatifu Paulo katika Agano Jipya: “Mwanamke
na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya
kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana
Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa,
ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” (1 Timotheo
2:11-14).
Mt. Tertullian pia alikuwa butu mno kuliko Mt. Paulo, alipokuwa akiongea na
                                              6
‘watawa wake awapendao sana kiimani, alisema: “Je, hivi hamjui kuwa nyinyi nyote
ni akina Hawa? Hukumu, (Maelezo) ya Mungu juu ya jinsia yenu yanaishi katika
zama hizi: uovu nao lazima uwe unaishi. Nyinyi ni mlango wa Shetani: Nyinyi ndio
waondoaji kizuizi cha mti ulioharamishwa: Nyinyi ndio wa mwanzo kuacha sheria
takatifu: Nyinyi ndio yule mwanamke aliyemshawishi mwanamume ambaye shetani
alishindwa kupata ujasiri wa kutosha kumvamia. Nyinyi ndio mlioharibu kirahisi
picha ya Mungu, mwanamume. Kwa sababu ya dhambi zenu hata Mwana wa Mungu
amelazimika afe.”
Mt. Augustine alikuwa ni mwaminifu kwa waliomtangulia, alimuandikia rafiki yake:
“Hakuna tofauti kwa mwanamke awe mke au mama, ataendelea kuwa ni Hawa tu
ambaye ni mshawishi kwa hiyo, lazima tujihadhari na mwanamke yeyote yule…
Nimeshindwa kupata faida ya mwanamke kwa mwanamume, ukitoa tendo la kuzaa
watoto.”
  Swidler, op. cit., pp 80-81.
                   Christianity”, in Arvind Sharma, ed., Women in World Religions (Albany State University of New
York Prees, 1987) p. 209
6
 For all the sayings of the Prominent Saints, see Karen Armstrong, The Gospel According to Woman (London: Elm
Tree Books, 1986) pp. 52-62. See also Nancy van Vuuren, The Subversion of Women as Practiced by Churches,
Witch-Hunters, and Other Sexists (Philadelphia: Westminister Press) pp. 28-30.
5 Rosemary R. Ruether, “
4
8

Baada ya karne kadhaa, Mt. Thomas Aquinas aliendelea kuamini kuwa wanawake ni
wasaliti: “Kwa mintarafu ya tabia ya kimaumbile ya kila mmoja, mwanamke ni
masaliti na ni mwanaharamu, kwa nguvu iliyo hai, kwa mbegu ya mwanamume
inaelekea kutoa tunda lenye kufanana kikamilifu na jinsia ya kiume; huku tunda la
mwanamke linakuja kutoka katika dosari ndani ya nguvu iliyohai au kutoka katika
baadhi ya malighafi mbovu, au hata kutoka baadhi ya athari za nje.”
Mwisho, mwanamageuzi mashuhuri Martin Luther hajaona faida yoyote kwa
mwanamke ispokuwa kuleta watoto wengi duniani kwa kiasi kinachowezekana bila
kujali athari mbaya zozote: “Kama watachoka au kufa, hakuna tatizo. Waache wafe
kwa kuzaa, kwani hiyo ndio sababu ya kuwepo kwao.”
Tena na tena wanawake wote ni wa kuadhiriwa kwa sababu ya taswira ya Hawa
ambaye ni mlaghai, shukrani zende kwa fikra iliyopo katika kitabu cha Mwanzo.
Kwa muhtasari, itikadi ya Kiyahudi-Kikristo juu ya Mwanamke imetiwa sumu kwa
imani ya kuamini dhambi ya asili ya Hawa na watoto wake wa kike. Na kama, kwa
sasa tutaangalia Quran inasema nini juu ya wanawake, punde tu, tutatambua kuwa
itikadi ya Kiislamu juu ya mwanamke ina tofauti za kimsingi na itakadi za Kiyahudi-
Kikristo. Acha Quran iongee yenyewe:
 “Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake
wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu; na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za
Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani; na wanaume wanaotii, na
wanawake wanaotii; na wanaume wasemao kweli, na wanawake wasemao kweli; na
wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri; na wanaume wanaonyenyekea na
wanawake wanaonyenyekea; na wanaume wanaotoa (Zaka na) sadaka na wanawake
wanaotoa (Zaka na) sadaka, na wanaume wanaofunga; na wanawake wanaofunga;
na wanaume wanaojihifadhi tupu zao; na wanawake wanaojihifadhi; na wanaume
wanaomtaja Mungu kwa wingi; na wanawake wanaomtaja Mwenyezi Mungu (kwa
wingi) Mwenyezi Mungu; amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.” (Quran 33:35)
 “Na wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake, ni marafiki wao kwa wao.
Huyaamrisha yaliyo mema na huyakataza yaliyo mabaya na husimamisha Sala na
hutoa Zaka na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio ambao Mwenyezi
Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye
hikima. (Quran 9:71)
 “Mola wao Akawakubalia (maombi yao kwa kusema): “Hakika Mimi sitapoteza
juhudi (amali) ya mfanya juhudi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au
mwanamke, (kwani nyinyi) ni nyinyi kwa nyinyi….” (Quran 3:195).
“Afanyaye ubaya hatalipwa ila sawa na huo uwovu wake na afanyaye mema, akiwa
mwanamume au mwanamke, naye ni Mwislamu, basi hao wataingia Peponi,
waruzukiwe humo bila hisabu.” (Quran 40:40)
9

 “Wafanyaji mema, wanaume au wanawake, hali ya kuwa ni, Waislamu
Tutawahuisha maisha mema, na Tutawapa ujira wao (Akhera) mkubwa kabisa kwa
sababu ya yale mema waliyokuwa wakiyatenda. (Quran 16:97).
Ni wazi kuwa mtazamo wa Quran juu ya wanawake hauna tofauti na mtazamo wake
juu ya wanaume. Wao wote, (wanawake na wanaume) ni viumbe wa Mungu ambao
lengo kuu la kuletwa kwao duniani ni kumuabudu Mungu wao, kutenda matendo
mema, na kujiepusha na maovu na wote wawili watalipwa kwa matendo yao. Quran
haijaonyesha kuwa mwanamke ni mlango wa Shetani wala kuwa amezaliwa akiwa ni
mlaghai. Quran pia, haijataja kuwa mwanamume ni sura ya Mungu; lakini wanaume
wote na wanawake wote ni viumbe vya Mungu, bila ziada. Kwa mujibu wa Quran,
kazi za mwanamke duniani si kuzaa watoto tu, lakini pia anatakiwa atende mema
mengi kama mwanamume anavyotakiwa afanye. Kamwe Quran haijasema kuwa
hakuna mwanamke mwema aliyewahi kuishi. Kinyume chake tunaona Quran
imeshawafundisha waumini wote, wake kwa waume, kufuata mfano wa wanawake
wakamilifu kama vile Bikira Maria na Mke wa Firauni:
 “Na Mwenyezi Mungu amepiga (anapiga) mfano wa wale walioamini kweli, ni
mkewe Firauni. (Mumewe kafiri kubwa namna hilo na yeye Mwislamu mzuri namna
hivyo). (Wakumbusheni watu) aliposema: “Ee Mola wangu! Nijengee nyumba
Peponi karibu yako, na Uniokoe na Firauni na amali zake (mbovu), na Niokoe na
watu madhalimu.” Na mariamu mtoto wa ‘Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na
Tukampulizia humo roho Yetu, (inayotokana na Sisi) na akayasadikisha maneno ya
Mola wake, na Vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa).
(Quran 66:11-12)
10

SEHEMU 3 - MABINTI WANAOTIA AIBU
Kwa hakika, tofauti iliyopo kati ya mtazamo wa Quran na Biblia juu ya jinsia ya kike
inaanza punde tu anapozaliwa mwanamke. Kwa mfano, Biblia inaeleza kuwa kipindi
cha mama aliyezaa cha kuwa si msafi kwa mujibu wa sheria za kidini ni mara mbili
ya urefu wa kawaida ikiwa mtoto atakuwa mwanamke kinyume na mwanamume.
(Mambo ya Walawi 12:2-5). Biblia ya Kikatoliki inaeleza kikamilifu kuwa:
“Kuzaliwa kwa binti ni hasara” (Ecclesiasticus 22:3). Kinyume cha maelezo haya
yanayotia mshtuko na kupaza roho, watoto wa kiume wanapokea sifa za kipee:
“Mwenamume anayemuelimisha mwanawe wa kiume atahusudiwa na maadui zake.”
(Ecclesiasticus 30:3).
Wanazuoni wa Kiyahudi wameamrisha Wayahudi wa kiume wazaliane watoto wengi
ili waendeleze kabila la Kiyahudi. Wakati huo huo, hawafichi upendeleo wao wa
wazi kwa watoto wa kiume: “Ni uzuri kwa wale wote ambao watoto wao ni wa kiume
lakini ni ubaya kwa wale wote ambao watoto wao ni wanawake”, “Anapozaliwa
mtoto wa kiume, watu wote wanashangilia…. na anapozaliwa mtoto wa kike watu
wote wanahuzunika” na “wakati mtoto wa kiume anapokuja duniani, amani inakuja
                                                                             7
duniani… Wakati mtoto wa kike anapokuja duniani, hakuna kitu kinachokuja.”
Binti anazingatiwa kuwa ni mzigo mzito, chanzo cha uwezekano wa aibu kwa baba
yake: “Binti yako ni mkaidi? Jihadhari ya kwamba asije akawachekesha maadui
zako, Na uwe gumzo la watu mji mzima, mada ya udaku wa kawaida, na atakutia
aibu mbele za watu.” (Ecclesiasticus 42:11). “Lazima uwe mkali na binti mkaidi, au
vinginevyo atatumia vibaya kumdekeza kwako. Mchunge vikali Sana katika macho
yake yasiyo na aibu, usishangae kama atakuletea aibu.” (Ecclesiasticus 26:10-11).
Ilikuwa ni fikra ile ile ya kuwatendea mabinti kwa mtazamo wa kuwa wao ndio
chanzo cha aibu ambayo iliwapelekea wapagani wa Kiarabu, kabla ya kuja kwa
Uislamu, kuwafanyia wanawake mauaji wangali wachanga.
Quran imelaani vikali mno tendo hilo la kuchukiza: “(Akawa) anajificha na watu
kwa sababu ya khabari mbaya ile aliyoambiwa! (Anafanya shauri!) Je, akae naye juu
ya fedheha hiyo au amfukie udongoni (kaburini, na hali ya kuwa mzima ili afe?)
Sikilizeni! Ni mbaya mno hukumu yao hiyo.” (Quran 16:59).
Ni lazima ionyeshwe kuwa uovu huu usingekoma katika bara Arabu kama
kusingekuwa na nguvu za matamamko makali ya Quran ambayo yalilaani matendo
hayo. (Quran 16:59, 43:17, 81:8-9). Quran, juu ya hayo, haifanyi ubaguzi kati ya
wavulana na wasichana. Kinyume na Biblia, Quran inazingatia kuwa kuzaa mtoto wa
kike ni zawadi na baraka kutoka kwa Mungu, na hivyo hivyo katika kuzaa mtoto wa
kiume. Pia Quran imetanguliza kutaja zawadi ya kuanza kuzaa mtoto wa kike:
“Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; Anaumba Apendavyo,
7
Swidler, op. cit., p. 140
11

Anampa Amtakaye watoto wa kike na Anampa Amtakaye watoto wa kiume”. (Quran
42:49).
Ili kukomesha kabisa kabisa matendo yote ya kuwaangamiza wanawake mwanzoni
mwa jamii ya Kiislamu, Mtume Muhammad (S.A.W) aliwaahidi wale wote
waliobarikiwa kuzaa watoto wa kike kuwa watapata thawabu kubwa kama watawalea
vizuri: “Yoyote atakayemlea mtoto wa kike, na kwa mujibu wa kuwatendea wema
watoto hao, watoto hao watamkinga baba yao dhidi ya Moto wa Jahannamu”
(Bukhari na Muslim), “Yoyote atakayewalea watoto wawili wa kike hadi wakakua,
mimi na yeye tutakuwa kama hivi siku ya Kiyama; na aliashiria kwa kuvibana
pamoja vidole (akimaanisha kuwa watakuwa pamoja). (Imepokelewa na Muslim).
12

SEHEMU 4 – ELIMU KWA WANAWAKE
Tofauti iliyopo kati ya itikadi ya Biblia na ya Quran juu ya wanawake haijafungika
katika kuzaa tu mtoto wa kike, lakini inaendelea na kupanuka kwa upeo mkubwa
sana kuliko hivyo. Hebu acha tulinganishe mitazamo ya vitabu hivyo juu ya
majaribio ya mtoto wa kike kujifunza dini yake. Moyo wa Uyahudi ni Torati,
ambayao ni sheria. Hata hivyo, kulingana na kitabu Talmudi, (kitabu muhimu sana
kwa Wayahudi), inasema: “wanawake hawaruhusiwi kujifunza Torati.” Baadhi ya
wanazuoni wa Kiyahudi kwa ukali wametangaza kuwa “ni bora kuyaacha maneno
ya Torati yaunguzwe moto kuliko kusomwa na mwanamke” na “Yeyote
                                                           8
atakayemfundisha Torati binti yake amemfundisha uchafu.”
Mtazamo wa Mt. Paulo katika Agano Jipya haupo wazi: “Wanawake na wanyamaze
katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo Torati
nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe
nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.” (Wakorintho wa
Kwanza 14:34-35)
Vipi mwanamke ataweza kujifunza ikiwa haruhusiwi kuongea? Vipi mwanamke
atakua kiakili ikiwa amelazimishwa kuwa katika hali ya utiifu kikamilifu? Vipi
mwanamke ataweza kujipanua upeo wake wa kielimu ikiwa chanzo chake cha pekee
cha kupata elimu ni mumewe tu akiwa nyumbani?
Sasa, ili tuwe waadilifu, tunapaswa tuulize: Je, nafasi ya Quran ina tofauti yeyote?
Moja ya habari fupi iliyosimuliwa ndani ya Quran inataja nafasi yake kwa ufahamu
wa kina zaidi. Bibi Khawlah alikuwa ni mwanamke wa Kiislamu ambae mumewe
bwana Awsi alipokuwa na hasira alimtamkia maneno haya: “Wewe kwangu mimi ni
sawa na mgongo wa mama yangu.” Jambo hilo lilikuwa likichukuliwa na wapagani
wa Kiarabu kuwa ni maneno ya talaka ambayo inamuacha huru mume, asitende
mambo yote ya unyumba yanayomlazimu lakini hayamuachi huyo mwanamke huru
aiache nyumba ya mume au aolewe na mtu mwingine. Aliposikia maneno hayo
kutoka kwa mumewe, Khawlah akawa na wakati mgumu sana. Bibi huyo akaenda
moja kwa moja hadi kwa Mtume wa Uislamu ili kutetea kesi yake. Mtume (S.A.W)
alikuwa na rai ya kumtaka bibi huyo awe mtulivu kwa kuwa hakuna njia ya kutatua
tatizo hilo kwa wakati huo. Khawlah akaendelea kujadiliana na Mtume (S.A.W)
akijaribu kuokoa ndoa yake iliyotundikwa. Punde tu, Quran ikaingilia kati; na
maombi ya Khawlah yakakubaliwa. Hukumu takatifu ikakomesha tabia hiyo mbaya
sana. Sura moja kamilifu (sura ya 58) ya Quran inaitwa “Almujadilah” au
“mwanamke ambaye amefanya mjadala” iliitwa hivyo kwa ajili ya tukio hilo:
 “Mwenyezi Mungu amekwishasikia usemi wa mwanamke yule anayejadiliana nawe
sababu ya mumewe, na anashtaki mbele ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu
anayasikia majibizano yenu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia (na)
Mwenye kuona.” (Quran 58:1)
8
Denise L. Carmody, “Judaism”, in Arvind Sharma, ed., op. cit., p. 197.
13

Mwanamke katika itikadi ya Quran anayo haki ya kupinga rai, hata kama ni rai ya
Mtume wa Uislam (S.A.W). Hakuna mwenye haki ya kumnyamazisha Mwanamke.
Mwanamke hayupo chini ya amri ya kumtaka mumemewe awe ndiye marejeo yake
ya pekee katika masuala ya kisheria na kidini.
14

SEHEMU 5 – MWANAMKE MWENYE HEDHI SI MSAFI
Sheria na hukumu za Kiyahudi juu ya hedhi ya wanawake ni kali mno. Agano la kale
linamchukulia mwanamke yeyote mwenye hedhi kuwa si msafi na ni najisi. Zaidi ya
hayo unajisi wake “unaambukiza” wenginewe vile vile. Mtu yeyote au kitu chochote
atakachokigusa kitanajisika kwa siku nzima: “Mwanamke ye yote, kama anatokwa na
kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika
kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi
hata jioni. Na kitu cho chote akilaliacho katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na
kila kitu ambacho akiketia kitakuwa najisi. Mtu ye yote atakayekigusa kitanda chake
huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
Mtu yeyote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua
nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni. Kwamba ni katika
kitanda, au cho chote alichokilalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho,
atakuwa najisi hata jioni”. (Law. 15:19-23).
Kwa sababu ya maumbile yake ya “kutia najisi”; mwanamke mwenye hedhi mara
nyingine alipelekwa uhamishoni ili kuepusha uwezekano wowote wa kukutana naye.
Hupelekwa nyumba maalumu ziitwazo “nyumba ya wasio wasafi” kwa kipindi chote
                9
cha hedhi yake. Talmudi inamchukulia mwanake mwenye hedhi ni “mauti” hata
kama hakuna mafungamano ya kimwili: “Walimu zetu wa dini ya Kiyahudi
wametufunza… kama mwanamke mwenye hedhi atapita kati ya (wanaume) wawili,
ikiwa ni mwanzoni mwa hedhi yake, mwanamke huyo atamnyonga mmoja wao, na
kama akiwa mwishoni mwa hedhi yake, atasababisha ugomvi kati ya wanaume hao.”
(Bpes.111a.)
Zaidi ya hayo, mume wa mwanamke mwenye hedhi alizuiwa kuingia sinagogini
kama atachafuliwa na mkewe tena hata kwa mavumbi yaliyo chini ya miguu yake.
Kasisi yeyote ambaye mkewe, bintiye, au mamaye ni mwenye hedhi hakuruhusiwa
                            10
                               Si ajabu kuwa wanawake wengi wa Kiyahudikuhubiri baraka sinagogini.
                                         11
wanaendelea kuona kuwa hedhi ni “laana.”
Uislamu hauoni kuwa mwanamke mwenye hedhi ana aina yoyote ya “najisi ya
kuambukiza kwa kugusana”. Mwanamke mwenye hedhi si mtu wa “kutoguswa” wala
“laana.” Mwanamke huyo anafanya shughuli zake za kawaida huku kukiwa na
jambo moja tu linalotolewa: Kwa wale walioolewa hawaruhusiwi kutenda tendo la
ndoa wakiwa katika kipindi cha hedhi. Lakini matendo mengine yote ya kugusana
kimwili baina yao yanaruhusiwa. Mwanamke mwenye hedhi amekatazwa asitende
baadhi ya ibada kama vile sala za kila siku, na kufunga akiwa katika kipindi cha
hedhi.
9
  Swidler, op. cit., p. 137.
   Ibid., p 138.
11
   Sally Priesand, Judaism and the New Woman (New York: Behraman House, Inc., 1975) p.24.
10
15

SEHEMU 6 – HAKI YA KUTOA USHAHIDI
Kadhia nyingine ambayo Quran na Biblia hazikubaliani ni kadhia ya mwanamke
kutoa ushahidi. Ni kweli kuwa Quran imewafunza waumini ambao wanashughulika
na mikataba ya kibiashara wawe na mashahidi wawili wa kiume au mwanamume
mmoja na wanawake wawili (Quran 2:282). Hata hivyo, ni kweli kwamba Quran
katika matukio mengine inakubali ushahidi wa mwanamke ukiwa ni sawa sawa na wa
mwanamume. Na kwa hakika ushahidi wa mwanamke unaweza ukawa ni bora zaidi
kuliko wa mwanamume. Na kama mwanamume atamtuhumu mkewe kuwa anafanya
uzinzi, mwanamume huyo anatakiwa na Quran aape kiapo cha dhati mara tano hii
ikiwa ni kama ushahidi wa kuwa mke ni muovu. Na kama mke atapinga na kuapa
kama hivyo mara tano, mwanamke huyo hazingatiwi kuwa ni muovu na kwa hali
yoyote likitokea jambo hilo ndoa itavunjwa. (Quran 24:6-11)
Kwa upande mwingine, katika jamii za kale za Kiyahudi wanawake hawakuruhusiwa
               12
kutoa ushahidi. Wanazuoni wa Kiyahudi waliwahesabu wanawake kuwa hawawezi
kutoa ushahidi. Jambo hilo ni miongoni mwa laana tisa zinazowatesa wanawake wote
kwa sababu ya “kuporomoka” (tazama sehemu ya Urithi wa Hawa). Katika Israeli ya
                                                                              13
leo, wanawake hawaruhusiwi kutoa ushahidi katika mahakama za kidini.
Wanazuoni wanahalalisha sababu za kutoruhusiwa kwa wanawake kutoa ushahidi
kwa kukariri (Mwanzo 18:9-16), pale ilipoeleza kuwa Sara mke wa Ibrahimu
ameongopa. Wanazuoni wa Kiyahudi wanatumia tukio hili kama ni ushahidi wa
kuwa wanawake hawana vigezo vya kuwa mashahidi. Hapa inapaswa izingatiwe
kuwa, kisa hiki kilichosimuliwa na Mwanzo 18:9-16 kimetajwa zaidi ya mara moja
katika Quran bila ya kudokeza kama Sara aliongopa. (Quran 11:69-74, 51:24-30).
Katika Ukristo wa Kimagharibi, vyanzo viwili Ecclesiastical na sheria ya uraia
                                                                          14
viliwakataza wanawake wasitoe ushahidi hadi mwishoni mwa karne iliyopita.
Kama mwanmume atamtuhumu mkewe kwa uzinzi, ushahidi wa mwanamke huyo
hautokubaliwa kabisa kabisa kwa mujibu wa Biblia. Mke anayetuhumiwa lazima
akabiliwe na hukumu ya kuchunguzwa kwa kuteswa. Katika majaribio hayo, mke
atakabiliwa na kanuni za kidini zikichanganyika na kufedheheshwa ambazo
zitapendekezwa ili kuthibitisha uovu wake au utakatifu wake. (Hesabu 5:11-31). Na
kama atapatikana na hatia baada ya kuchunguzwa kimateso, mwanamke huyo
atahukumiwa kifo. Na kama itagundulika si muovu, mumewe atakuwa hana hatia
yoyote ya kumtendea vibaya.
Licha ya hayo, kama mwanamume atamuoa mwanamke kisha akamtuhumu kuwa si
bikira, ushahidi wa mwanamke huyo hautokubaliwa. Wazazi wake watalazimika
kuleta ushahidi wa ubikira wake mbele ya wazee wa mji. Na kama wazazi
watashindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha utakatifu wa binti yao, binti huyo
atapigwa mawe hadi afe mlangoni katika ngazi za nyumba ya babaye. Na kama
12
13
   Swidler, op. cit., p. 115
   Lesley Hazleton, Israel Women The Reality Behind the Myths (New York: Simon and Schuster, 1977) p. 41.
14
   Gage, op. cit. p. 142
16

wazazi wataweza kuthibitisha utakatifu wake, yule mume atapigwa faini tu; ya
shekeli za fedha mia moja na mume huyo haruhusiwi kumuacha mke huyo maisha:
 “Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, kisha akimshitaki mambo ya aibu
kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia
sikuona kwake alama za ubikira; ndipo babaye yule kijana na mamaye
watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni; na
baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe
mkewe, naye amchukia; angalieni amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa
binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na
wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji. Basi wazee wa mji ule na wamtwae
yule mtu mume na kumrudi, wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule
kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe;
hana ruhusa ya kumuacha siku zake zote. Lakini likiwa ni kweli neno hili, la
kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira, na wamtoe nje yule kijana
mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata
afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israel, kwa kufanya ukahaba katika
nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondo uovu katikati yako. (Kum. 22:13-21).
17

SEHEMU 7 - UASHERATI
Uzinzi unazingatiwa kuwa ni dhambi katika dini zote. Biblia inatangaza adhabu ya
kifo kwa wote wawili mzinifu mwanamume na mzinifu mwanamke (Law. 20:10).
Uislam pia unatoa adhabu iliyo sawa kwa wote wawili mzinifu mwanamume na
mzinifu mwanamke (Quran 24:2). Hata hivyo, ufafanuzi wa Quran juu ya uzinzi una
tofauti sana na ufafanuzi wa Biblia. Uzinzi, kwa mujibu wa Quran, ni kushiriki tendo
la ngono nje ya ndoa kwa aliyeoa au aliyeolewa. Lakini Biblia inazingatia tendo la
ngono nje ya ndoa kuwa ni uzinzi kwa mwanamke aliyeolewa. (Law. 20:10, Kum
22:22, Methali 6:20-7:27).
 “Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na
mume, na wafe wote wawili, mtu mume alielala na mwanamke, na
yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli.
(Kum 22:22)
 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani
yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa. (Law. 20:10).
Kwa mujibu wa ufafanuzi wa Biblia, kama mwanamume aliyeoa atalala na
mwanamke asiyeolewa, jambo hilo halichukuliwi kuwa ni uovu kabisa kabisa.
Mwanamume aliyeoa anayefanya ngono nje ya ndoa na mwanamke asiyeolewa si
mzinzi na mwanamke asiyeolewa aliezini naye, pia, si mzinzi. Uovu wa zinaa
unatendeka pale tu, mwanamume aliyeoa au asiyeoa, anapolala na mwanamke
aliyeolewa. Kwa hali hii mwanamume anachukuliwa kuwa ni mzinifu, hata kama
hajaoa, na mwanamke anachukuliwa kuwa ni mzinifu. Kwa ufupi, uzinzi ni uovu wa
kingono unaomuhusisha mwanake aliyeolewa. Matendo ya ngono nje ya ndoa
yanayomuhusu mwanamume aliyeoa si uzinzi kwa mujibu wa Biblia. Kwa nini huu
undumilakuwili? Kwa mujibu Insaiklopidia ya Kiyahudi, mke anazingatiwa kuwa ni
miliki ya mume na uzinzi unatoa madaraka ya uvunjaji wa sheria kumvunjia mume
kwa haki ya kipekee aliyonayo kwa mwanamke; mke kama miliki ya mume hana
                              15
haki kama hiyo kwa mumewe. Hiyo ndio maana, kama mwanamume atafanya
ngono na mwanamke aliyeolewa, mwanamume huyo atakuwa amevunja mali ya
mwanamume mwingine na, kwa hiyo lazima aadhibiwe.
Hadi hivi leo katika nchi ya Israeli, kama mwanamume aliyeoa atajitumbukiza katika
ngono nje ya ndoa na mwanamke asiyeolewa, watoto wake kwa mwanamke huyo
wanazingatiwa kuwa ni watoto wa halali wa ndoa. Lakini, kama mwanamke
aliyeolewa atafanya ngono nje ya ndoa na mwanamume mwingine (si mumewe)
aliyeoa au asiyeoa, watoto wake kwa mwanamume huyo si wa halali tu lakini pia
wanazingatiwa kuwa ni watoto wa haramu na ni haramu kwa watoto huo kuoa au
kuolewa na Myahudi yeyote ispokuwa aliyeitoka dini ya Kiyahudi na watoto wa nje
  Jeffrey H. Togay, “Adultery,” Encyclopaedia Judaica, Vol. 2, col. 313. Also, see Judith Plaskow, Standing Again at
Sinai: Judaism from a Feminist Perspective (New York: Harper & Row Publishers, 1990) pp. 170-177.
15
18

ya ndoa wengine. Katazo hili linaendelea kwa vizazi vya mtoto huyo kwa madaraja
                                                          16
ya vizazi 10 mpaka uvundo wa uzinzi uthibitishwe kufifia.
Quran, kwa upande mwingine, kamwe haijamzingatia mwanamke yeyote kuwa ni
mmilikiwa na mwanamume yeyote. Quran kiuadilifu anaelezea uhusiano kati ya
mume na mke kwa kusema:
 “Na katika Ishara zake (za kuonyesha ihsani Zake juu yenu) ni kuwa Amekuumbieni
wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na
huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiria.”
(Quran 30:21).
Hii ndiyo itikadi ya Quran juu ya ndoa; mapenzi, huruma, na utulivu, raha, na sio
miliki na undumilakuwili.
16
Hazleton, op. cit., pp. 41-42.
19

SEHEMU 8 - KULA KIAPO NA KUWEKA NADHIRI
Kwa mujibu wa Biblia, mwanamume lazima atimize kila nadhiri na kiapo alichoapa
kwa Mungu. Haramu kugeuza neno lake. Kwa upande mwingine, nadhiri au kiapo
cha mwanamke hakilazimiki kwake. Nadhiri au kiapo cha mwanamke lazima
kitimizwe na baba yake, kama atakuwa anaishi kwenye nyumba ya baba yake, au
atimiziwe na mumewe, akiwa ameolewa. Kama baba/mume hajaidhinisha nadhiri
ama kiapo cha binti yake au mkewe, viapo, ahadi, nadhiri na dhamana zote
zilizofanywa na mwanamke huyo zinakuwa ni batili na ni kazi bure:
 “Lakini kama huyo baba yake akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo
zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika….” Na mumewe
alisikia akamnyamazia, wala hakumkataza; ndipo nadhiri Zake zote zitathibitika na
kila kifungo alichofunga kitathibitika. (Hesabu 30:5-15).
Kwa nini iwe maneno ya mwanamke hayashurutishwi kwake? Jibu ni lepesi: Ni kwa
sababu mwanamke anamilikiwa na baba yake, kabla ya kuolewa, au na mumewe
baada ya kuolewa. Utawala wa baba kwa binti yake ulikuwa ni dhahiri kwa upeo
ambao, kama atataka, anaweza kumuuza! Na jambo hilo limeonyeshwa katika
maandiko ya wanazuoni wa Kiyahudi kuwa: “Mwanamume anaweza kumuuza binti
yake, lakini mwanamke hawezi kumuuza binti yake, Mwanamume anaweza
                                                                             17
kumchumbia binti yake, lakini mwanamke hawezi kumchumbia binti yake.”
Mafundisho ya wanazuoni wa Kiyahudi, vile vile yanaonyesha kuwa ndoa
inawakilisha ahamishaji wa utawala toka kwa baba kwenda kwa mume: “Uchumba,
unamfanya mwanamke awe miliki tukufu sana … mali isiyokiukwa kwa mume….” Ni
wazi, kama mwanamke anahesabiwa kuwa ni mali ya mtu mwingine, mwanamke
huyo hatoweza kula kiapo chochote ambacho hakitathibitishwa na mmiliki wake.
Ni muhimu kuona kuwa Jambo hili la mafundisho ya Biblia kuhusu viapo vya
mwanamke limeendelea kuathiri vibaya nafasi ya wanawake katika itikadi ya
Kiyahudi-Kikristo hadi mwanzoni mwa karne hii. Mwanamke aliyeolewa katika
ulimwengu wa Kimagharibi hana hali ya uhalali wa nafsi yake. Hakuna tendo la
mwanamke lenye thamani yoyote kisheria. Mumewe anaweza kukana mkataba
wowote; mapatano ya kibiashara, au mpango wowote alioufanya. Wanawake katika
nchi za Kimagharibi (eneo kuu lilorithi mtazamo wa Kiyahudi-Kikristo) hawawezi
kuweka masharti yoyote ya kimikataba kwa sababu wanawake hao wanamilikiwa na
watu wengine. Wanawake wa Kimagharibi walitaabika kwa takriban miaka elfu
mbili, kwa sababu ya mtazamo wa Biblia juu ya nafasi ya wanawake kwa baba zao
                   18
na kwa waume zao. Katika Uislamu, kiapo cha kila Mwislamu, mwanamume au
mwanamke, anashurutishwa kwa nafsi yake mwenyewe. Hakuna mtu mwenye
madaraka ya kukana kiapo cha mtu mwingine yeyote.
17
18
Swidler, op. cit., p. 141.
Matilda J. Gage, Woman, Church, and State (New York: Truth Seeker Company, 1893) p. 141.
20

Kushindwa kutekeleza kiapo ipasavyo, kilichoapwa na mwanamume au mwanamke,
ni lazima alipe fidia kama ilivyotajwa katika Quran:
 “Mwenyezi Mungu hatakuteseni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakukamateni
kwa viapo mlivyoapa kwa nia mliyoifunga barabara. Basi kafara yake ni kuwalisha
masikini kumi kwa chakula cha katikati mnachowalisha watu wa majumbani mwenu,
au kuwavisha, au kumpa uungwana mtumwa, Lakini asiyeweza kupata hayo, basi
afunge siku tatu. Hii ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na vilindeni viapo
vyenu, (msiape kisha msitimize). Namna hii Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya
Zake ili mpate kushukuru.” (Quran 5:89)
Wafuasi wa Mtume Muhammad (S.A.W) waume kwa wake, walikuwa wakiwasilisha
viapo vyao vya kumtii, wao wenyewe. Wanawake, sawa na wanaume, walikuwa
wanamuendea Mtume kila mtu mwenyewe na kula viapo vyao.
 “Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake walioamini wanakuahidi ya kwamba
hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini,
wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzusha tu wenyewe
baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana
ahadi nao na uwatakie maghufira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu
ni Mwingi wa maghufira, Mwingi wa rehema.” (Quran 60:12)
Mwanamume haruhusiwi kula kiapo kwa niaba ya binti yake au mkewe. Wala hawezi
kukana kiapo cha yeyote miongoni mwa jamaa zake wa kike.
21

SEHEMU 9 – MALI ZA MKE
Hizi dini tatu zinashirikiana katika imani isiyo na mashaka kuhusu umuhimu wa ndoa
na maisha ya kifamilia. Pia zinakubaliana katika suala la kumpa mwanamume
uongozi wa familia. Bila ya kujali, tofauti za wazi zilizopo kati ya dini hizo tatu,
pamoja na kuheshimu mipaka ya uongozi. Mafundisho ya Kiyahudi-Kikristo
hayafanani na ya Uislamu, katika ukweli wa upeo wa uongozi wa mume hadi kufikia
umiliki wa mume kummiliki mkewe.
Mafundisho ya Kiyahudi yanalichukulia jukumu la mume kwa mkewe kuwa
linaanzia kutoka katika itikadi ya kuamini kuwa mume anammiliki mke kama
                             19
anavyomiliki mtumwa wake. Itikadi hii imekuwa hoja nyuma ya undumilakuwili
katika sheria ya uzinzi na nyuma ya uwezo wa mwanamume wa kubatilisha viapo
vya mkewe. Itikadi hii pia inahusika katika kumzuia mke asisimamie mali yake au
mapato yake. Mwanamke wa Kiyahudi mara tu anapoolewa, mwanamke huyo
anapoteza kabisa kabisa usimamizi wa mali zake na mapato yake, na kuchukuliwa na
mumewe. Wanazuoni wa Kiyahudi wanatetea haki ya mwanamume kwa mali ya
mkewe kama ni matokeo ya kummiliki kwake mke huyo: “Mtu anapokuwa mmiliki
wa mwanamke je, jambo hilo halipelekei kuwa mtu huyo atakuwa mmiliki wa mali za
mwanamke huyo vile vile?” na “Na mwanamume ajitwalie mwanamke je,
                                                20
hatajitwalia mali za mwanamke huyo vile vile? Kwa hiyo, ndoa imesababisha
mwanamke tajiri sana awe hana kitu! Talmudi inachambua hali ya kiuchumi ya
mwanamke kama ifuatavyo:
 “Vipi mwanamke awe na chochote; chochote ambacho ni chake kinamilikiwa na
mumewe? Kwa mume kile ambacho ni chake basi hicho ni chake na kwa mwanamke
kile ambacho ni chake basi hicho ni cha mwanamume vile vile… Pato la mwanamke
na chochote atakachokipata mitaani ni cha mumewe vile vile. Vitu vya nyumbani
hata kipande cha mkate juu ya meza ni vya mume. Kama atamualika mgeni
nyumbani kwake na kumlisha, atakuwa anamuibia mumewe …” (san. 71a, Git.Ra).
Ukweli wa mambo ni kwamba mali za mwanamke wa Kiyahudi zina maana ya
kuwavutia wachumba. Familia ya Kiyahudi inatoa fungu la binti yao katika
kiwanja/shamba la baba yake litumiwe kama mahari atoayo mke ili aolewe. Mahari
hiyo ndiyo sababu iliyowafanya mabinti wa Kiyahudi wewe ni balaa lisilotakiwa kwa
baba zao. Baba analazimika kumlea binti yake kwa miaka mingi kisha aandae ndoa
yake kwa kutoa mahari kubwa. Kwa hiyo, msichana katika familia ya Kiyahudi
                                                   21
amekuwa ni dhima isiyo na kikomo na sio rasilimali. Dhima hii isiyo na kikomo
inafafanua kwa nini kuzaa binti ilikuwa si furaha na shangwe katika jamii za
Kiyahudi za zamani (tazama sehemu; “Mabinti wanaotia aibu”). Mahari ilikuwa ni
zawadi apewayo bwana harusi ili iwe milki yake chini ya sheria ya mpango wa
maisha. Mume anakuwa ni mmiliki halisi wa mahari lakini haruhusiwi kuiuza. Bibi
19
20
   Louis M. Epstein, The Jewish Marriage Contract (New York: Arno Press, 1973) p. 149.
   Swidler, op. cit., p. 142.
21
   Epstein, op. cit., pp. 164-165.
22

harusi anapoteza madaraka yote juu ya mahari katika kipindi cha ndoa. Zaidi ya
hayo, mwanamke anatarajiwa afanye kazi baada ya kuolewa na pato lake lote lazima
liende kwa mumewe ikiwa ni malipo ya huduma za lazima ambazo bibi huyo
anazipata kutoka kwa mumewe. Mwanamke huyo anaweza kurudisha mali zake
katika hali mbili tu: Talaka au kifo cha mumewe. Na kama mke akifa kwanza, mume
anarithi mali zake. Na katika hali ya kufa kwa mume mke anarudishiwa mali zake za
kabla ya ndoa lakini hajatajwa kama anarithi fungu lolote katika mali za mumewe
aliyefariki. Ni lazima iongezwe kuwa mume vile vile analazimika atoe mahari kwa
bibi harusi, lakini kwa mara nyingine tena mume huyo huyo ndio mmiliki halali wa
                                           22
zawadi hiyo kwa muda wote wa ndoa yao.
Ukristo, hadi hivi karibuni, umekuwa unafuata mafundisho yale yale ya Kiyahudi.
Zote mbili dini na mamlaka za sheria za raia katika himaya ya Ukristo wa Kiroma
(baada ya Constantine) zinaomba maafikiano ya mali kama ni sharti la kutambuliwa
kwa ndoa. Familia zinawapa mabinti zao mahari za ziada kama matokeo ya sheria
hiyo. Wanaume wananuia kuoa mapema huku familia za mabinti zikichelewesha
                                       23
ndoa za mabinti zao kuliko kawaida. Chini ya sheria ya urai, mke ametajwa kuwa
anarudishiwa mahari yake kama ndoa imebatilishwa, ila kama mwanamke huyo ni
mzinzi, katika hali hii, mwanamke huyo ananyang`anywa haki yake ya mahari
                                                       24
ambayo imesalia kuwa mikononi mwa mumewe. Chini ya sheria ya kanuni na
sheria ya uraia mwanamke aliyeolewa katika dini ya Ukristo wa Ulaya na Marekani
ameshapoteza haki za mali zake, hali hii ilikuwa inaendelea hadi mwishoni mwa
karne ya kumi na tisa na mwanzoni mwa karne ya ishirini. Kwa mfano, haki za
wanawake chini ya sheria ya Uingereza zilizotungwa na kuchapishwa 1632.
                                                                                 25
Miongoni mwa haki hizo ni: “Cha mume ni chake. Na cha mke ni cha mumewe.”
Mke sio tu anapoteza mali zake katika ndoa, pia anapoteza utu wake. Tendo lolote la
mwanamke lilikuwa halina thamani yeyote kisheria. Mumewe anaweza kubatilisha
uuzaji au zawadi iliyotolewa na mke kwa kuwa haina sharti lenye thamani kisheria.
Mtu yeyote atakayeingia mkataba na mke wa mtu anachukuliwa kuwa ni haramia
kwa kushiriki katika ulaghai. Zaidi ya hayo, mwanamke hawezi kushtaki au
                                                                                 26
kushtakiwa kwa jina lake mwenyewe, wala hawezi kumshitaki mumewe.
Mwanamke aliyeolewa alikuwa anatendewa kama vile ni mtoto mchanga katika jicho
la sheria. Kirahisi kabisa, mke alimilikiwa na mumewe na kwa hiyo anapoteza mali
                                                    27
zake, utu wake kisheria, na jina lake la kifamilia.
Tangu karne ya saba C.E., (baada ya kuzaliwa Yesu) Uislamu umewapa wanawake
waliolewa uhuru binafsi ambao Uyahudi-Ukristo wa Kimagharibi umewanyima hadi
hivi karibuni tu! Katika Uislamu, bibi harusi na familia yake hawalazimishwi kutoa
   Ibid., pp. 112-113. See also Priesand, op. cit., p. 15.
   James A. Brundage, Law, Sex, and Christian Society in Medieval Europe (Chicago: University of Chicago Press,
1987) p.88.
24
   Ibid., p. 480.
25
   R. Thompson, Women in Stuart England and America (London: Routledge & Kegan Paul, 1974) p. 161.
26
   Mary Murray, The Law of the Father (London: Routlendge, 1995) p.67.
27
   Gage, op. cit., p.143.
23
22
23

kitu chochote kiwe kama mahari ya kumpa bwana harusi. Msichana katika familia ya
Kiislamu si dhima isiyo na kikomo. Mwanamke ana heshima kubwa sana katika
Uislamu kiasi cha kutotakiwa atoe zawadi yoyote ya kumvutia mumewe mtarajiwa.
Ispokuwa bwana harusi ni lazima atoe mahari ya ndoa kumpa bibi harusi. Na mahari
hiyo inahesabiwa kuwa ni mali ya mke na si ya mume wala familia ya bibi harusi
haina fungu au haimiliki mahari hiyo. Katika baadhi ya jamii za Kiislamu hivi sasa ni
                                                                   28
kawaida mahari kufikia lukiki za Dola za Kimarekani, na almasi. Mke anamiliki
mahari yake hata kama ataachwa hapo baadaye. Mume haruhusiwi kutumia mali ya
                                                                           29
mkewe ispokuwa ile apewayo na mkewe kwa ridhaa yake mwenyewe. Quran
imeelezea msimamo wake juu ya mada hii kwa uwazi kabisa:
 “Na wapeni wanawake mahari yao, hali ya kuwa ni hadiya (aliyowapa Mungu).
(Lakini hao wake zenu) wakikupeni kwa radhi ya nafsi zao kitu katika hayo (mahari)
basi kuleni kwa furaha na kunufaika. (Quran 4:4)
Mali na pato la mke vipo chini ya utawala wake kikamilifu na ni kwa ajili ya
                                                                            30
matumizi yake peke yake, na mutumizi ya watoto, ni jukumu la mumewe. Bila
kujali huyo mke ni tajiri kiasi gani, mwanamke halazimishwi kuwa mchumiaji
mwenza wa mwanamume kuihudumia familia ispokuwa kama atajitolea mwenyewe
na kuamua kufanya hivyo. Wanandoa wanarithiana. Zaidi ya hayo, mke katika
                                                                      31
Uislamu anamiliki uhuru wa utu wake kisheria pia na jina lake la ukoo. Jaji mmoja
wa Kimarekani, mara moja alitoa maelezo juu ya haki za wanawake wa Kiislamu
kwa kusema: “Msichana wa Kiislamu anaweza kuolewa mara kumi, lakini uhuru
wake haunyonywi kwa kufanya hivyo yaani na waume zake mbalimbali. Mwanamke
wa Kiislamu ni sayari katika mfumo wa jua akiwa na jina na utu wake mwenyewe wa
          32
kisheria.
   For example, see Jeffrey Lang, Struggling to Surrender, (Beltsville, MD: Amana Publications, 1994), p. 167.
   Elsayyed Sabiq, Figh al Sunnah (Cairo: Darul Fatah Lile`lam Al-Arabi, 11th edition, 1994), vol. 2, pp. 218-229.
30
   Abdel-Haleem Abu Shuqqa, Tahreer al Mar`aa fi Asr al Rasala (Kuwait: Dar al Qalam, 1990) pp. 109-112.
31
   Leila Badawi, “Islam”, in Jean Holm and John Bowker, ed., Women in Religion (London: Pinter Publishers, 1994)
p.102.
32Amir H. Siddiqi, Studies in Islamic History (Karachi: Jamiyatul Falah Publications, 3rd edition, 1967) p. 102.
29
28
24

SEHEMU 10 – TALAKA
Hizi dini tatu zina tofauti zilizo wazi kimtazamo juu ya talaka. Ukristo unapinga
talaka moja kwa moja. Agano Jipya kwa kauli moja linapigania ndoa isiyotanguka.
Inasemekana kuwa Yesu amesema: “Lakini mimi nawaambia, kila mtu amwachaye
mkewe, ispokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa
yule aliyeachwa, azini. (Matayo 5:32). Ukamilifu huo ulio mgumu kutekelezeka na
usiobadilika bila ya shaka si jambo la hakika. Jambo hilo linaibua dhana ya ukamilifu
wa kimaadili ambao haufikiwi na jamii ya kibinadamu. Wakati wanandoa
wanapogundua kuwa ndoa yao haiwezi kuendelea, tendo la kuharamisha talaka
haliwatendei wema wowote wanandoa hao. Kuwalazimisha wanandoa
wanaochukiana waishio kwa ubaya wakae pamoja kinyume na matakwa yao ni
jambo lisilo na maana yeyote wala si la haki. Si ajabu ulimwengu wa Wakristo wote
unalazimisha kuruhusiwa kwa talaka.
Wayahudi, kwa upande mwingine, wanaruhusu talaka hata ikiwa bila sababu. Agano
la kale linampa mume haki ya kumtaliki mkewe hata kama hana kosa au kwa kuwa
hampendi tu.
 “Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa
ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi
mwake na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake,
ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa
akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na
kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa
mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa
unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo asiitie dhambini
nchi, akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi.” (Kum 24:1-4)
Aya iliyo hapo juu imesababisha mjadala mkali kwa Wanazuoni wa Kiyahudi kwa
sababu ya kutokubaliana kwao juu ya tafsiri ya maneno. “Uovu, chuki, kutia aibu,
tabia mbaya” na “kutopenda” yaliyotajwa katika hizo aya. Kitabu cha Talmudi
kinasajili rai zao zilizotofauti tofauti:
 “Madhehebu ya Shamai inakamata kuwa mwanamume haruhusiwi kumwacha
mkewe ila kama atampata na hatia ya uzinifu, huku madhehebu ya Hillel yanasema
kuwa mwanamume anaweza kumwacha mkewe hata kama huyo mwanamke
amevunja kibakuli cha mumewe. Na mwanazuoni Akiba anasema mwanamume
anaweza kumwacha mke hata kama kwa sababu nyepesi ya kwamba amempata
mwanamke mwingine aliyemzuri sana kuliko wa kwanza.” (Gittin 90a-b).
Agano Jipya linafuata rai ya Shamaites huku sheria ya Kiyahudi imefuata rai ya
                      33
Hillelites na R. Akiba Tangu kuenea kwa rai ya Hillelites, imekuwa ni mafundisho
yasiyokeukwa kwa sheria ya Wayahudi ya kuwapa uhuru wanaume wa kumuacha
mkewe bila ya sababu yoyote. Agano la Kale sio tu linampa mume haki ya kumtaliki
33
Epstein, op. cit., p. 196.
25

mkewe “aliyemuhuzunisha” lakini pia linazingatia kumwacha “mke muovu” ni
lazima:
 “Mke mbaya analeta fedheha, muono wa kuhuzunisha, na maumivu ya moyo.
Mgoigoi wa mkono na mdhaifu wa goti ni mwanamume ambaye mkewe ameshindwa
kumfurahisha. Mwanamke ni dhambi ya asili, na kupitia kwake sote tutakufa.
Usiache tangi lenye ufa kuchimba au kumruhusu mke mbaya asema atakacho. Na
kama mwanamke huyo hakubali utawala wake, mwache na mfukuze.” (Ecclesiasticus
25:25).
Talmudi imesajili matendo maalumu kadhaa ya wake wanaolazimika kuachwa na
waume zao: “Kama mwanamke atakula mitaani, kama atakunywa kwa pupa mitaani,
kama atanyonyesha mtaani, kwa matendo hayo yote mwanazuoni Meir amesema
kuwa mwanamke huyo lazima aachane na mumewe.” (Git. 89a).
Vile vile Talmudi imefanya jambo hilo kuwa ni mamlaka ya kumuacha mwanamke
mgumba (ambaye hazai kwa kipindi cha miaka kumi): “Mwanazuoni wetu
ametufundisha: Kama mwanamume amejitwalia mke na kuishi nae kwa miaka kumi
na mwanamke huyo hajazaa mtoto, mwanamume huyo amuache mke huyo.” (Yeb.
64a).
Wake, kwa upande mwingine, hawawezi kutoa talaka chini ya ya sheria ya Kiyahudi.
Mke wa Kiyahudi, hata hivyo, anaweza kuomba talaka mbele ya mahakama ya
Kiyahudi huku akithibitisha sababu nzito ya kufanya hivyo. Ni nafasi ndogo sana
apewayo mke ili aweze kuomba talaka. Miongoni mwa nafasi hizo ni: ikiwa mumewe
ana ugonjwa mbaya au ugonjwa wa ngozi, mumewe akishindwa kutekeleza wajibu
wa ndoa n.k. Hiyo mahakama inaweza kuunga mkono madai ya mke ya kutaka talaka
lakini haina uwezo wa kuvunja ndoa. Ni mume tu awezaye kuvunja ndoa kwa
kumtoza mkewe faini ya talaka. Na mahakama inao uwezo wa kutoa adhabu ya
viboko, faini, kifungo na kumtenga na sinagogi huyo mume ili kumlazimisha apokee
malipo ya lazima ya kumtaliki mkewe. Hata hivyo, kama mume atakuwa mbishi vya
kutosha, anao uwezo wa kutotoa talaka na kuendelea kubaki na mkewe bila ya
mipaka. Na baya zaidi, ni kuwa, mume anao uwezo wa kumtelekeza mkewe bila ya
kumpa talaka na kumuacha akiwa si mwolewa wala si mtalikiwa. Na huyo mume
anaweza kuoa mke mwingine au hata kuishi na kimada bila ya ndoa na kupata watoto
kwa huyo kimada, (watoto hao wanahesabiwa kuwa ni wa halali katika sheria za
Kiyahudi).
Mke aliyetelekezwa, kwa upande mwingine, haruhusiwi kuolewa na Myahudi
mwingine, kwa kuwa yeye ni mke wa mtu kisheria na hawezi kuishi na mwanamume
mwingine kwa sababu atahesabiwa kuwa ni mzinifu na watoto wake kwa huyo
mwanamume mwingine pia si wa halali kwa vizazi kumi. Mwanamke atakayekuwa
                                                               34
katika hali hiyo anaitwa agunah (yaani mwanamke aliyetundikwa). Leo hii nchini
Marekani kuna, takriban maagunot 1000 hadi 1500 miongo mwa wanawake wa
Kiyahudi ambao ni maagunoti (agunot ni wingi wa agunah), wakati nchini Israeli
34
Swidler, op. cit., pp. 162-163.
26

idadi yao ni kubwa kufikia kiasi cha 16,000. Waume wanaweza kunyang`anya
maelfu ya dola kutoka kwa wake zao waliowatia mtegoni na hiyo ikiwa ni malipo ya
                    35
talaka ya Kiyahudi.
Uislamu unashikilia nafasi ya katikati baina ya Ukristo na Uyahudi, pamoja na
kuiheshimu talaka. Ndoa katika Uislamu ni kufunga mkataba mtakatifu ambao
hauruhusiwi kuvunjwa ila kwa sababu nzito. Wanandoa wanafundishwa watafute kila
njia ya kutatua matatizo yao ili waokoe ndoa yao, iliyo hatarini.
Talaka isiwe ndio kimbilio ila kama kutakuwa hukana njia nyingine ispokuwa talaka.
Kwa ufupi, Uislamu unaikubali talaka, hata hivyo hauipendi hata kidogo. Hebu
kwanza tuangalie upande wa kuitambua. Uislamu unatambua haki ya wanandoa ya
kumaliza uhusiano wao wa kindoa.
Uislamu unampa mume haki ya kutoa (talaka). Zaidi ya hayo, Uislamu ni kinyume na
Uyahudi, unampa mke haki ya kuvunja ndoa kupitia kile kijulikanacho kama
       36
khulah. Kama mume atavunja ndoa kwa kumtaliki mkewe, hatorudishiwa chochote
miongoni mwa mahari aliyotoa kumpa mkewe. Quran imeeleza kuharamisha kwa
mume aliyeacha mke asirudishiwe mahari bila kujali ughali au thamani ya mahari
yenyewe:
 “Na kama mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, (yaani kumwoa mke mwingine
na kumwacha huyo wa zamani), na hali mmoja wao (nae ndiye huyo anayemwacha)
mumempa mrundi wa mali, basi msichukue chochote. Je, mnachukua kwa dhulma na
kwa khatia iliyo wazi?” (Quran 4:20)
Katika hali ya mke kuamua kumaliza ndoa, huyo mke anatakiwa arejeshe mahari kwa
mumewe. Kurejesha mahari katika hali hii ni fidia ya uadilifu kwa mume ambaye
anapendelea kuendelea na mkewe huku huyo mke anataka waachane.
Quran imewafundisha waume wa Kiislamu wasichukue kitu chochote katika mahari
walizowapa wake zao ispokuwa katika hali ya mke kuamua kuvunja ndoa:
 “…Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlichowapa (wake zenu), ispokuwa
(wote wawili) wakiogopa ya kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi
Mungu. Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi
Mungu, hapo itakuwa hapana dhambi kwao (mwanaume wala mwanamke katika)
kupokea (au kutoa) ajikomboleacho mwanamke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi
Mungu; basi msiiruke. Na watakaoiruka mipaka Mwenyezi Mungu, hao ndio
madhalimu (wa nafsi zao). (Quran 2:229)
Pia, mwanamke mmoja alimuendea Mtume Muhammad (S.A.W) akitaka kuvunjwa
kwa ndoa yake, akamwambia Mtume kwamba yeye hana lalamiko lolote dhidi ya
tabia au hali ya mumewe. Tatizo lake la pekee lilikuwa ni kuwa hampendi huyo
35
36
  The Toronto Star, Apr. 8, 1995.
  Sabiq, op. cit., pp. 318-329. See also Muhammad al Ghazali, Qadaya al Mar`aa bin al Taqaleed al Rakida wal Wafida
(Cairo: Dar al Shrooq, 4th edition, 1992) pp. 178-180.
27

mume, na hawezi kuendelea kuishi naye. Mtume (S.A.W) akamuuliza: “Je,
utamrudishia bustani yake? (mahari aliyokupa) Akasema: “Ndio” Kisha Mtume
(S.A.W) akamfundisha yule mwanamume apokee bustani yake na akubali kuvunjika
kwa ndoa. (Bukhari)
Katika baadhi ya hali, mke wa Kiislamu huenda akawa anataka kuendelea na ndoa
lakini anajikuta analazimika adai talaka kwa sababu kuna sababu zinazolazimisha
kufanya hivyo kwa mfano: ukatili wa mume, kutelekezwa bila sababu, mume
kushindwa kutimiza majukumu yake ya ndoa n.k. Katika hali hizi mahakama ya
                        37
Kiislamu inavunja ndoa.
Kwa muhtasari, Uislamu umempa mwanamke wa Kiislamu baadhi ya haki zisizo na
kifani; mwanamke anaweza kumaliza ndoa kupitia khulah na kufungua mashitaka ya
kudai talaka. Mke wa Kiislamu kamwe hatokuwa mtundikwa na mume mkaidi. Na
zilikuwa ni haki hizi zilizowashawishi wanawake wa Kiyahudi waliokuwa wakiishi
katika jamii za Kiislamu za mwanzo za karne ya saba C.E. watafute kupata malipo ya
talaka kutoka kwa waume zao wa Kiyahudi kupitia mahakama za Kiislamu.
Wanazuoni wa Kiyahudi walitangaza kuwa malipo hayo ni batili na hayafai. Ili
kukomesha mwenendo huo, wanazuoni wa Kiyahudi walitoa haki mpya na
marupurupu kwa wanawake wa Kiyahudi ili kujaribu kudhoofisha mvuto wa
mahakama za Kiislamu. Wanawake wa Kiyahudi waishio katika nchi za Kikristo
hawakupewa chochote katika marupurupu kama yale ya wenzao. Kwa kuwa sheria ya
talaka ya Kirumi inayofanyakazi ilikuwa haina mvuto wa ziada kuliko sheria za
          38
Kiyahudi.
Sasa, hebu acha tutazame namna Uislamu usivyopendelea talaka. Mtume wa Uislamu
amewaambia waumini kuwa: “Jambo la halali linalomchukiza sana Mwenyezi
Mungu ni talaka.” (Abu Dawood).
Mwanamume wa Kiislamu hatakiwi kumtaliki mkewe eti kwa kuwa hampendi.
Quran inawafundisha wanaume wa Kiislamu wawe wema kwa wake zao hata katika
hali ya hisia za kuvuvuwaa au hisia za kutompenda:
 “….Na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani
huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.
(Quran 4:19)
Mtume Muhammad (S.A.W) ametoa mafundisho kama hayo:
 “Muumini wa kiume asimchukie muumini wa kike, kama hapendi moja ya tabia zake
atapendezwa na nyinginezo.” (Muslim).
Vile vile, Mtume, amesisitiza kuwa Waislamu wabora sana ni wale walio wabora
kwa wake zao:
  Ibid., pp. 313-318.
  David W. Amram, The Jewish Law of Divorce According to Bible and Talmud (Philadelphia: Edward Stern & Con.,
Inc., 1896) pp. 125-126.
38
37
28

“Mkamilifu wa imani miongoni mwa waumini ni yule mbora wao kitabia, na aliye
mbora wenu kitabia ni yule mwenye tabia njema kwa mkewe.” (Tirmidhi)
Hata hivyo, Uislamu ni dini ya vitendo na inatambua kuwa kuna wakati ndoa
inakuwa ipo ukingoni karibu kuvunjika. Katika hali kama hizo, ushauri mtupu wa
kuwa mwema au kujizuia nafsi, unakuwa hauna utatuzi wa kutosheleza. Kwa hiyo,
nini cha kufanya ili kuokoa ndoa katika hali ngumu kama hizo? Quran inatoa baadhi
ya ushauri wa kutendwa kwa wanandoa (mume au mke) ambaye mwenziwe (mke au
mume) ni muovu. Kwa mume ambaye mkewe ana tabia mbaya inayotishia ndoa,
Quran inatoa aina nne za ushauri kama zilivyoelezwa kikamilifu katika aya zifuatazo:
 “…Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu; (1) waonyeni (2) na waacheni
peke yao katika vitanda (3) na wapigeni. Na kama wanakutiini msiwatafutie njia (ya
kuwaudhi bure). Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu (na) Mkuu. (4) Na kama
mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basi pelekeni mwamuzi mmoja
katika jamaa za mwanamume na mmoja katika jamaa za mwanamke. Kama wakitaka
mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa
habari za siri na habari za dhahiri. (Quran 4:34-35)
Mambo matatu ya kwanza kutajwa yajaribiwe kwanza. Na kama yameshindwa, ndipo
inapotakiwa kutafutwa msaada wa familia. Ni lazima izingatiwe, kuwa aya za hapo
juu zinaangaza, kuwa kumpiga mke mkaidi, ni kipimo cha muda mfupi ambacho
kinakimbiliwa kikiwa ni hatua ya tatu tena katika hali ya kulazimika kufanya hivyo
huku kukiwa na matarajio ya kuwa hiyo itakuwa dawa ya matendo maovu ya mke.
Kama hilo litafaa, basi mume haruhusiwi kwa hali yoyote ile kuendelea kumsumbua
mke kama ilivyotajwa kwa ufafanuzi katika aya hizo. Na kama njia hiyo imeshindwa,
mume bado haruhusiwi kutumia tena njia hiyo na hapo ndipo njia ya mwisho ya
suluhisho kwa msaada wa familia lazima iangaliwe.
Mtume Muhammad (S.A.W) amewafundisha waumini wa Kiislamu ya kuwa
wasitumie njia hiyo ila katika hali ya mwisho kabisa kama vile uasherati wa wazi
uliotendwa na mke. Hata katika hali kama hiyo adhabu inatakiwa iwe nyepesi na
kama mke ataacha, mume haruhusiwi kumsumbua tena:
 “Kama watafanya uasherati wa wazi wahameni vitandani, na wapigeni mapigo
hafifu. Na kama watakutiini, msiwatafutie sababu ya kuwasumbua.” (Tirmidhi).
Kwa kuongezea, Mtume wa Uislamu amelaani mapigo yoyote yasiyo ya kiuadilifu.
Baadhi ya wake wa Kiislamu walimshitakia Mtume (S.A.W) kuwa waume zao
wamewapiga. Kwa kusikia hivyo, Mtume kwa dhahiri alisema kuwa:
“Wale wafanyao hayo (kuwapiga wake zao) si wabora wenu.” (Abu Dawood).
Lazima ikumbukwe kuwa katika nukta hii Mtume pia amesema:
 “Mbora wenu ni yule mbora kwa familia yake, nami ni mbora wenu kwa familia
yangu.” (Tirmidhi).
29

Mtume (S.A.W) alimshauri mwanamke mmoja wa Kiislamu, jina lake lilikuwa ni
Fatuma binti Qaisi, asiolewe na jamaa mmoja kwa sababu jamaa huyo alikuwa
anajulikana kwa kuwapiga wanawake.
 “Nilimwendea Mtume na kumwambia: Abul Jahm na Mu’awiah wanataka kunioa.
Mtume Muhammad (S.A.W) (kwa njia ya ushauri) alisema: Mu’awiah ni masikini
sana na Abul Jahm amezoea kuwapiga wanawake.” (Muslim).
Lazima ifahamike kuwa ruhusa ya Talmudi ya kumpiga mke kwa kumuadabisha kwa
                    39
lengo la kumnyoosha. Mume hajawekewa mipaka kwa kesi kubwa kubwa kama za
uasherati wa wazi. Ameruhusiwa kumpiga mkewe hata kwa kukataa kufanya kazi za
nyumbani. Zaidi ya hayo, mume hajawekewa mipaka ya kutumia haki ya kuadhibu.
Ameruhusiwa kuvunja ushupavu wa mkewe kwa mjeledi au kwa kumshindisha na
      40
njaa.
Kwa mke ambaye mumewe ana tabia mbaya inayosababisha ndoa ikaribie kuvunjika,
Quran inatoa ushauri ufutao:
 “Na kama mke akiona kwa mume wake kugombanagombana na kutenganatengana,
basi si vibaya kwao wakitengeneza baina yao sulhu (njema wakastahmiliana vivyo
hivyo bila kuachana); maana sulhu ni kitu bora. Na nafsi zimewekewa ubakhili
mbele (ya macho yake). Na kama mkifanya mema (kuwafanyia wake zenu hao
msiowapenda) na mkimcha Mwenyezi Mungu (msiwapunguzie haki zao, basi bila ya
shaka Mwenyezi Mungu atakulipeni), kwani Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote
mnayoyatenda. (Quran 4:128).
Katika hali hii, mke ameshauriwa atafute suluhu na mumewe (akiwa na msaada wa
familia au bila familia). Ni jambo linalofahamika kuwa Quran si yenye kumshauri
mke akimbilie njia mbili za kugomea ngono na kupiga. Na sababu ya tofauti hii ni
kumkinga mke na majibu makali mno ya kuumiza mwili kutoka kwa mumewe
ambaye tayari ashakuwa na tabia mbaya. Majibu hayo yanaweza kusababisha
kuathirika kwa wote wawili mke na mume pamoja na ndoa na kuleta hali mbaya
kuliko kuleta hali nzuri. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wamependekeza kuwa
mahakama inaweza ikatekeleza njia hizo dhidi ya mume kwa niaba ya mke. Hiyo ni
kuwa, kwanza mahakama imuonye mume aliyekengeuka, kisha imkataze kitanda cha
                                                 41
mkewe, na mwisho itekeleze kipigo cha aina yake.
Kwa kumalizia, Uislamu unawapa waliooana ushauri mwingi unaowezekana ili
kuokoa ndoa zao wakati wa matatizo na migogoro. Na kama mmoja wa wanandoa
anahatarisha mafungamano ya mambo ya ndoa, mwanandoa mwenza ameshauriwa
na Quran afanye kila kiwezekanacho na chenye kuleta manufaa ili aokoe huo
muungano mtakatifu. Na kama njia zote zimeshindwa, Uislamu unaruhusu wanandoa
waachane kwa amani na kwa wema.
39
40
   Epstein, op. cit., p. 219.
   Ibid, pp 156-157.
41
   Muhammad Abu Zahra, Usbu al Fiqh al Islami (Cairo: al Majlis al A`la li Ri`ayat al Funun, 1963) p.66.
30

SEHEMU 11 – AKINA MAMA
Agano la Kale katika sehemu nyingi linaamrisha wema na kutenda matendo ya pekee
kwa wazazi na kuwalaani wale ambao hawawatendei wema. Kwa mfano, “Kwa
maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa; amemlaani
baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.” (Mambo ya walawi 20:9) na
“Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; bali mpumbavu humdharau
mamaye.” (Mithali 15:20).
Ingawa kumfanyia wema baba peke yake ndiko kulikotajwa katika baadhi ya
sehemu; kwa mfano, “Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye; Bali
mwenye dharau hasikilizi maonyo.” (Mithali 13:1) Mama peke yake ndiye
asiyetajwa. Zaidi ya hayo, hakuna msisitizo wa kipekee juu ya kumtendea wema
mama kama alama ya kufahamu vizuri tabu nyingi alizozipata wakati wa kujifungua
na matatizo ya mtoto mchanga. Kando ya hayo, akina mama hawarithi kabisa kabisa
                                                        42
chochote toka kwa watoto wao huku akina baba wanarithi.
Ni vigumu kusema kuwa Agano Jipya ni maandiko yanayowataka watu wawafanyie
wema akinamama. Kwa kulinganisha, mtu anaona kuwa Agano Jipya linahesabu
kuwatendea wema akinamama kuwa ni kikwazo katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Kwa mujibu wa Agano Jipya, mtu hawezi kuwa Mkristo mzuri wa kutumainiwa
kuwa yeye ni mfuasi wa Kristo ila amchukie mama yake. Inasemekana kuwa Yesu
alisema:
 “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake,
na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam na hata nafsi yake mwenyewe,
hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” (Luka 14:26)
Kwa kuongezea, Agano Jipya linatoa picha ya Yesu kama ni mtu mwenye tofauti au
asiyemuheshimu mama yake mzazi. Kwa mfano, wakati mama yake alipokwenda
kumtafuta na huku Yesu akiwa anawahubiria makutano, Yesu hakujali wala hakutoka
kwenda kumuona mama yake:
 “Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita. Na
makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka; wakamwambia, Tazama, mama yako
na ndugu zako wako nje, wanakutafuta. Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu
zangu ni akina nani? Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote,
akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana mtu ye yote
atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na
mama yangu.” (Marko 3:31-35).
Mtu anaweza akadai kuwa Yesu alikuwa akijaribu kuwafundisha makutano yake
somo muhimu sana ambalo ni kuwa uhusiano wa kidini si wenye umuhimu mdogo
kuliko uhusiano wa kifamilia. Hata hivyo, Yesu alikuwa na uwezo wa kuwafundisha
wasikilizaji wake somo hilo hilo bila ya kuonyesha huko kutomjali mama yake
42
Epstein, op. cit., p. 122.
31

kulikokuwa kwa wazi wazi. Mwelekeo kama huo usio na heshima unatoa picha ya
wakati alipokataa kuthibitisha maelezo yaliyotolewa na makutano yake ya kuibariki
kazi ya mama yake ya kumzaa na kumlea:
 “Ikawa alipokisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti
yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye
alisem, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.” (Luka 11:27-28)
Ikiwa mama mwenye daraja ya bikira Maria ametendewa matendo yasio na heshima
kiasi hicho, kama ilivyofafanuliwa na Agano Jipya, tena katendewa na mtoto
mwenye daraja ya Yesu Kristo, sasa itakuwaje kwa mama wa kawaida wa Kikristo
vipi atatendewa na wanawe wa Kikristo wa kawaida?
Katika Uislamu, heshima, utiifu, na kutukuza kunaambatana na mfano ambao hauna
kifani. Quran inaweka umuhimu wa kuwatendea wema wazazi kuwa ni jambo la pili
baada ya kumuabudu Mwenyezi Mungu Muweza:
 “Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (ameagiza)
kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, (naye yuko)
pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee. Na
useme nao kwa msemo wa hishima (kabisa). Na uwainamishie bawa la unyenyekevu
kwa (njia ya kuwaonea) huruma (kwa kuwaona wamekuwa wazee). Na useme;
“Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto.” (Quran
17:23-24)
Quran katika sehemu kadhaa imeweka mkazo maalumu kwa kazi ya mama ya kuzaa
na kulea:
 “Na tumemuusia mwanadamu (kuwafanyia ihsani) wazazi wake – mama yake
ameichukuwa mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na (kumnyonyesha na kuja)
kumwachisha kunyonya katika miaka miwili – ya kwamba unishukuru mimi na
wazazi wako; marejeo yenu ni kwangu,” (Quran 31:14)
Nafasi ya pekee ya akina mama katika Uislamu imeelezwa kwa umbuji (ufundi wa
kupanga na kutumia maneno kwa ujuzi wa hali ya juu sana) na Mtume Muhammad
(S.A.W):
 “Mtu mmoja alimuuliza Mtume: “Ni nani nimfanyie wema zaidi? Mtume (S.A.W)
akamjibu: “Mama yako”. “Na nani anafuata?” Aliuliza yule jamaa. Mtume (S.A.W)
akamjibu: “Mama yako”. “Na nani anafuata?” Aliuliza yule jamaa Mtume (S.A.W)
akamjibu: “Mama yako”. “Na nani anafuata?” Aliuliza yule jamaa. Mtume (S.A.W)
akamjibu: “Baba yako”. (Bukhari na Muslim).
Miongoni mwa mafundisho machache ya Uislamu ambayo kwa imani kabisa
Waislamu wanayachunga hadi leo hii ni kuwatendea wema akina mama. Heshima
wanayoipata akina mama wa Kiiaslamu kutoka kwa watoto wao wa kiume na wa
kike inaonyeshwa kwa mifano. Nguvu kali na mafungamano motomoto baina ya
akinamama wa Kiislamu na watoto wao na heshima ya kina ambayo wanaume wa
32

Kiislamu wanawafanyia mama zao kwa kuwasaidia inawashangaza watu wa
           43
Magharibi.
43
Armstrong, op. cit., p, 8.
33

SEHEMU 12 – MIRATHI KWA WANAWAKE.
Moja ya tofauti kubwa kati ya Quran na Biblia ni mitazamo yao juu ya mirathi ya
wanawake kurithi mali za ndugu zao waliofariki. Mtazamo wa Kibiblia una maneno
mafupi yaliyowazi na yalioelezwa na mwanazuoni Epstein: “Mafundisho
yanayoendelea na yasiyovunjika tangu enzi za kuanza Biblia hayampi mwanamke,
mke na mabinti haki ya kurithi mali ya familia. Katika mfumo mkongwe sana wa
urithi, wanafamilia wa kike wanazingatiwa kuwa ni sehemu ya mali ya urithi na
kuwa ni watu wa mbali kabisa na utu, kisheria wanarithiwa na kuwa wao ni kama
watumwa. Wakati ambapo kanuni za Musa zinatoa mirathi kwa mabinti ikiwa hakuna
                                                                     44
mwanaumume. Lakini hata hivyo mke harithi hata katika hali kama hiyo. Kwa nini
wanafamilia wa kike wanachukuliwa kuwa ni sehemu ya urathi? Mwanazuoni
Esptein ana jibu: “Wanawake ni miliki ya baba zao kabla ya kuolewa na ni miliki ya
                             45
waume zao baada ya kuolewa.”
Sheria za mirathi za Biblia zimeelezwa katika Hesabu 27:1-11. Mke hapewi fungu
lolote katika mirathi ya mumewe, huku huyo mume ndio mrithi wa kwanza wa
kumrithi mkewe, tena hata kabla ya watoto wake. Binti anaweza kurithi kama tu
hakuna mwanamume wa kurithi. Mama harithi kabisa kabisa huku baba akirithi.
Wajane na mabinti, katika hali ya kuwepo watoto wa kiume, wamo katika huruma ya
warithi wa kiume kwa kusaidiwa. Na hiyo ndiyo sababu wajane na mayatima wa kike
wamekuwa ni miongoni mwa mafukara sana katika jamii ya Kiyahudi.
Ukristo umekuwa ukifuata sheria hizo hizo kwa muda mrefu. Sheria zote mbili za
kikanisa na za kiraia kwa Wakristo zinazuia mabinti wasishirikiane na kaka zao
katika urithi kutoka kwa baba yao. Kando ya hayo, wake walikuwa wananyimwa
haki zote za kurithi. Sheria hiyo ya udhalimu sana ilidumu hadi mwishoni mwa karne
           46
iliyopita.
Miongoni mwa wapagani wa Kiarabu kabla ya Uislamu, haki za kurithi zilikuwa kwa
ndugu wa kiume tu. Quran imekomesha dhuluma zote hizo za kiutamaduni na
ukawapa ndugu wote wa kike mafungu ya kurithi:
“Wanaume wana sehemu katika mali wanayoyaacha wazazi na jamaa waliokaribia.
Na wanawake (pia) wanayo sehemu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa
waliokaribia. Yakiwa kidogo au mengi. (Hizi) ni sehemu zilizofaridhiwa (na
Mwenyezi Mungu). (Quran 4:7)
Akina mama, wake, wasichana na madada wa Kiislamu wamepokea haki za kurithi
miaka elfu moja na mia tatu kabla ya Ulaya kutambua kuwepo kwa haki hiyo.
Mgawo wa urithi ni somo kubwa sana lenye maelezo kamili katika (Quran 4:7, 11,
12, 176). Sheria mama ni kuwa fungu la mwanamke ni sawa sawa na nusu ya
44
45
   Epstein, op. cit., p. 175.
   Ibid., p. 121.
46
   Gage, op. cit., p. 142.
34

mwanamume ispokuwa katika hali ambazo mama anapata sawa sawa na baba. Hii
sheria mama kama itachukuliwa kwa kutengwa kutoka katika sheria nyinginezo
zinazowahusu wanaume na wanawake inawezekana kuonekana kuwa haina uadilifu.
Ili kufahamu uwiano uliopo katika sheria hii, mtu lazima azingatie ukweli kwamba
mujukumu ya kipesa kwa wanaume katika Uislamu yanazidi sana yale ya wanawake
(Tazama kitengo cha mali za wanawake). Mume lazima ampe mkewe mahari. Mahari
hiyo ni mali ya huyo mke na inaendelea kuwa hivyo hivyo hata kama ataachwa hapo
baadaye.
Bi harusi hana wajibu wa kutoa kitu cha kumpa bwana harusi. Zaidi ya hayo, mume
wa Kiislamu anachajiwa huduma za mkewe na wanawe. Mke, kwa upande
mwingine, halazimishwi kumsaidia mumewe katika majukumu haya. Mali na pato la
mke ni kwa ajili yake binafsi ila kile atakachojitolea kumpa mumewe. Kando ya
hayo, mtu lazima atambue kuwa Uislamu kwa juhudi kubwa unahimiza maisha ya
kifamilia. Uislamu kwa nguvu sana unawahimiza vijana waoane, na unahimiza
kutoachana na haupendi useja (utawa, hali ya kutooa au kutoolewa) eti jambo hilo ni
maadili mema. Kwa hiyo, katika jamii sahihi ya Kiislamu, maisha ya kifamilia (ndoa)
ndio kitu cha kawaida na maisha ya kutooa au kutoolewa ni mara chache sana
kuwepo. Hiyo ni kwa kuwa, takriban wanawake wote walio katika umri wa kuolewa
na wanaume waliofikia umri wa kuoa wameoana katika jamii za Kiislamu. Katika
mwanga wa uhakika huu, mtu anaweza kufahamu vizuri kuwa wanaume wa
Kiislamu, kiujumla, wana mzigo mkubwa sana wa kiuchumi kuliko wanawake kwa
hiyo sheria za mirathi zinamaanisha kufidia kutowiana huko kiasi ambacho jamii
nzima itaishi bila ya kuwa na vita vyovyote vya kijinsia au kitabaka. Baada ya
mlinganisho mdogo kati ya haki za kiuchumi na wajibu wa wanawake wa Kiislamu,
mwanamke mmoja wa Kiislamu ambaye ni Mwingereza, amehitimisha kuwa
Uislamu unawatendea wanawake sio tu kiuadilifu lakini pia unawatendea vizuri
       47
zaidi.
47
B.Aisha Lemu and Fatima Heeren, Woman in Islam (London: Islamic Foundation, 1978) p.23.
35

SEHEMU 13 – HALI MBAYA YA WAJANE
Kwa sababu ya ukweli kwamba Agano la Kale halitambui haki yoyote kwa
wanawake, wajane wamekuwa ni miongoni mwa watu masikini sana katika jamii ya
Kiyahudi. Ndugu wa kiume ambao wamerithi mali yote ya mume aliyefariki ambayo
ilikuwa apewe huyo mke kutoka katika mali hiyo. Hata hivyo, wajane hawana jinsi
ya kujihakikishia matumizi hayo ambayo yameshasombwa, na wanaishi kwa
kungojea huruma za watu wengine. Kwa hiyo wajane wamekuwa ni watu wa daraja
la chini mno katika Israeli ya zamani na ujane ulizingatiwa kuwa ni alama ya
kushuka hadhi sana (Isaya 54:4). Lakini hali mbaya ya mjane katika mafundisho ya
Kibiblia inaenea hadi nga`mbo ya kutengwa kutoka katika mali ya mumewe. Kwa
mujibu wa Mwanzo 38, mjane asiye na mtoto lazima aolewe na ndugu wa mumewe,
hata kama atakuwa ameshaoa, kwa hiyo huyo ndugu azae mtoto kwa ajili ya kaka
yake aliyefariki, jambo ambalo litaimarisha jina la ndugu yake na halitokufa.
 “Yuda akamwambia Onani, uingie kwa mke wa nduguyo ukamwoe, ukamwinulie
nduguyo uzao.” (Mwanzo 38:8).
Radhi za mjane kuridhia ndoa hiyo hazihitajiki. Mjane anatendewa kama ni sehemu
ya mali ya mumewe aliyefariki, mke ambaye faida yake kuu ni kuhakikisha kizazi
                                                                            48
cha mumewe. Hii sheria ya Kibiblia bado inatumiwa katika Israeli ya leo. Mjane
asiye na mtoto katika Israeli ni ridhisho la ndugu wa mumewe. Na kama huyo ndugu
ni mdogo sana hata hawezi kuoa, mjane huyo lazima amsubiri hadi afikie umri wa
kuoa. Kama huyo ndugu akikataa kumuoa, atakuwa huru na anaweza kuolewa na mtu
yeyote aliye chaguo lake. Hilo ni tukio lisilo la kawaida nchini Israeli kwani wajane
ni watu wa kukandamizwa na shemeji zao ili wapate uhuru wao.
Wapagani wa Kiarabu kabla ya Uislamu walikuwa na matendo hayo hayo. Mjane
alikuwa akichukuliwa kuwa ni sehemu ya mali ya mume na anarithiwa na warithi
wake wa kiume na huyo mke alikuwa, mara nyingi, akitolewa aolewe na mtoto
mkubwa wa mumewe aliezaliwa na mke mwingine. Quran kwa ukali imeshambulia
na kutokomeza mila hii ya kudhalilisha:
 “Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu; ispokuwa yale yaliokwisha pita.
(Yaliyopita yamepita yasirejeshwe tena). Bila ya shaka jambo hili ni uovu na
uchukizo na ni njia mbaya.” (Quran 4:22)
Wajane na wanwake walioachwa wanadhalilishwa sana katika itikadi ya Kiyahudi
kiasi ambacho Kuhani Mkuu hakuruhusiwa kumuoa mjane, mtalikiwa, au malaya:
 “Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. Asitwae mjane, wala mwanamke
aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini
atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe. Naye asiwatie unajisi kizazi
chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye.” (Walawi 21:
13-15)
48
Hazleton, op.cit., pp. 45-46.
36

Leo hii katika Israeli, mjukuu mwenye hadhi ya Cohen (Kuhani Mkuu wa siku za
                                                            49
hekaluni) haruhusiwi kumuoa mtalikiwa, mjane au kahaba. Katika sheria za
Kiyahudi, mwanamke aliyewahi kuwa mjane kwa mara tatu ikiwa wanaume wote
watatu wamekufa kwa sababu za kikawaida mwanamke huyo anahesabiwa kuwa ni
                                50
janga na ni haramu kuolewa tena. Quran kwa upande mwingine, haimchukulii mtu
yeyote kuwa ni wa bahati wala ni wa mikosi. Wajane na watalikiwa wana uhuru wa
kuolewa na mwanamume yeyote wamtakaye.
Hakuna aibu inayomkumba mtalikiwa au mjane katika Quran:
 “Na mtakapowapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi
warejeeni kwa wema au tokaneni nao kwa wema. Wala msiwaweke kwa kuwapa
dhara mkaruka mipaka. Na atakayefanya hivyo, amejidhulumu mwenyewe. Wala
msizifanyie mzaha Aya za Mwenyezi Mungu. Na mkumbuke neema za Mungu zilizo
juu yenu, na (khasa ile neema ya) kuteremshiwa Quran; na (kujuvywa) ilimu nyingine
anazokuonyeeni. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni
mjuzi wa kila kitu.” (Quran 2:231)
 “Na wale wanaofishwa (wanaokufa) miongoni mwenu na kuacha wake; hawa
(wake) wangoje (wasiolewe) miezi minne na siku kumi. Na wanapofikia muda wao
(wa kumaliza eda yao hiyo), basi si dhambi juu yenu kwa yale wanayoyafanyia nafsi
zao (hao wanawake) kwa yanayowafiki (kufuata) Sharia. Na Mwenyezi Mungu anazo
habari za yote mnayoyatenda. (Quran 2:234)
 “Na wale wanaofishwa (wanaokufa) miongoni mwenu na wakawaacha wake,
wawausie (mawarithi wao) kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka
mmoja bila ya kutolewa (katika majumba waliyokuwamo, ya waume zao). Na kama
wanawake (wenyewe) wakiondoka, basi si kosa juu yenu kwa yale waliyoyafanya kwa
nafsi zao wenyewe yanayofuata Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na)
Mwenye hikima. (Quran 2:240)
49
50
Ibid., p.47.
Ibid., p. 49.
37

SEHEMU 14 – UKEWENZA
Kwa sasa acha tushughulikie suala muhimu la mitala. Mitala ni jambo la zamani sana
linalopatikana katika jamii za kibinadamu nyingi. Biblia haijakemea mitala. Kwa
kulinganisha, Agano la Kale na maandiko ya wanazuoni wa Kiyahudi mara kwa mara
yanathibitisha haki ya mitala. Inasemekana kuwa mfalme Suleimani alikuwa na wake
700 na masuria 300. (1 Wafalme 11:3) Vile vile, mfalme Daudi, inasemekana
alikuwa na wake wengi na masuria pia (2 Samweli 5:13). Agano la Kale lina sheria
za kugawa mali za mume na kuwapa watoto wake kutoka kwa wake mbali mbali.
(Kumb. 22:7). Kizuizi cha pekee dhidi ya mitala ni kuharamishwa kumtwaa dada wa
mkeo awe mke mwenza. (Walawi 18:18). Talmudi inashauri idadi ya mwisho kuwa
                 51
ni wake wanne. Wayahudi wa Ulaya waliendelea kufanya mitala hadi karne ya
kumi na sita. Mayahudi wa kimashariki kikawaida wanatekeleza mitala hadi
walipofika Israeli, ambako kuliharamishwa mitala chini ya sheria ya uraia. Hata
hivyo, katika sheria za kidini ambazo zinapuuza sheria za kiraia katika shauri hilo,
                     52
mitala imeruhusiwa.
Je, Agano Jipya lina nini? Kwa mujibu wa Baba Eugene Hilman katika kitabu chake
cha utambuzi, mitala inachukuliwa hivi: “Hakuna sehemu yeyote katika Agano Jipya
yenye amri iliyo wazi kuwa ndoa yatakiwa iwe ya mke mmoja au mume mmoja au
                                     53
amri yeyote inayoharamisha mitala.” Zaidi ya hayo, Yesu hajasema kitu dhidi ya
mitala ingawa ilikuwa ikifanywa na Wayahudi wa jamii yake. Baba Hilman ametilia
mkazo uhakika wa kuwa Kanisa huko Roma liliharamisha mitala ili kufuata mila ya
Kigiriki-Kirumi (ambayo imeamuru kuwa na mke mmoja tu wa kisheria huku
ikiruhusu vimada na umalaya). Naye alimtaja Mt. Augustine, “Sasa kwa hakika muda
                                                                                 54
wetu huu, na kwa kuishi na mila za Kirumi, hairuhusiwi kujitwalia mke mwingine.”
Makanisa ya Kiafrika na Wakristo wa Kiafrika mara nyingi wanawakumbusha
wenziwao wa Ulaya kuwa Kanisa kuharamisha mitala ni mila za utamaduni na sio
amri ya sheria thabiti ya Kikristo.
Quran, vile vile imeruhusu ukewenza, lakini sio bila ya mipaka:
 “Na kama mkiogopa kutowafanyia uadilifu mayatima (basi ogopeni vile vile
kutowafanyia uadilifu wanawake). Basi oeni mnaowapenda katika wanawake,
(maadamu mtawafanyia insafu) wawili au watatu au wanne (tu). Na mkiogopa kuwa
hamuwezi kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja tu, au (wawekeni masuria) wale
ambao mikono yenu ya kiume imewamiliki. Kafanya hivi ndiko kutapelekea kutofanya
jeuri.” (Quran 4:3)
   Swidler, op. cit., pp. 144-148.
   Hazleton, op. cit., pp 44-45.
53
   Eugene Hillman, Polygamy Reconsidered: African Plural Marriage and the Christian Churches (New York: Orbis
Books, 1975) p. 140.
54
   Ibid., p. 17.
52
51
38

Quran, kinyume na Biblia, imeweka mipaka ya idadi ya wake hadi wanne tena chini
ya masharti makali ya kuwatendea hao wake kwa usawa na uadilifu. Isifahamike
kuwa Quran inawahimiza waumini wafanye mitala, au kuwa na mitala ndio
ukamilifu. Kwa maneno mengine, Qurani “imesamehe” au “imeruhusu” mitala, na si
zaidi, lakini kwa nini? Kwa nini mitala imeruhusiwa? Jibu ni lepesi: kuna maeneo na
nyakati ambazo zinalazimisha jamii kufanya hivyo, pia malengo ya kimaadili ya
kuwepo kwa mitala. Kama aya ya Quran iliyopo hapo juu ilivyoonyesha, mada hii ya
mitala katika Uislamu haitofahamika peke yake nje ya shuruti za jamii na kuhusu
mayatima na wajane. Uislamu ukiwa kama dini ya dunia nzima unafaa kwa maeneo
yote na nyakati zote kwa hiyo, haungepuuza shuruti na mambo ya lazima.
Katika jamii nyingi za wanadamu, wanawake ni wengi kuliko wanaume. Nchini
Marekani kwa uchache, kuna wanawake milioni nane zaidi ya wanaume. Katika nchi
kama vile Guinea kuna wanawake 122 kwa kila wanaume 100. nchini Tanzania,
                                            55
Kuna wanaume 95.1 kwa kila wanawake 100. Jamii ifanye nini kuhusu huu uwiano
wa kijinsia usio na ulingano? Kuna utatuzi wa aina mbali mbali, baadhi wanaweza
kupendekeza useja, wengine wangependelea kuwauwa watoto wachanga wakike
(Jambo litokealo katika baadhi ya jamii ulimwenguni leo hii!) Wengine wangedhani
kuwa tundu pekee ya kutokea kutoka katika tatizo hilo ni kuwa jamii isamehe aina
zote za ngono: umalaya, ngono nje ya ndoa, kusagana, ushoga n.k. Kwa jamii
nyingine, kwa mfano jamii nyingi za Kiafrika leo hii, dhana kuu inayoheshimika ni
kuruhusu ndoa za mitala kama mila iliyokubaliwa na ni kitu kinachoheshimiwa na
jamii. Nukta ambayo mara nyingi haifahamiki katika nchi za Kimagharibi ni kuwa
wanawake katika jamii nyingine hawalitazami jambo la mitala kwa mtazamo wa
dhulma ya kudhalilishwa. Kwa mfano mabibi harusi wadogo wadogo wengi,
Wakristo, Waislamu au watu wengine, wanapendelea kuolewa na mwanamume
aliyeoa na ambaye tayari huyo mwanamume mwenyewe amejitolea awe mume
mwenye kubeba majukumu.
Wake wengi wa Kiafrika wanawataka waume zao waoe mke wa pili ili wasijihisi
         56
wapweke. Uchunguzi uliowahusisha zaidi ya wanawake elfu 6, wenye umri wa kati
ya miaka 15 hadi 59, walio katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria
wameonyesha kuwa asilimia sitini 60% ya wanawake hao watafurahi kama waume
zao wataoa wake wengine. Ni asilimia 23% tu walioonyesha kukerwa na wazo la
ukewenza. Asilimia 76% ya wanawake waliofanyiwa uchunguzi nchini Kenya
walionyesha kukubali mitala.
Uchunguzi uliofanywa vijijini Kenya, wanawake 25 katika kila 27 wanapendelea
ukewenza kuliko kuwa mke mmoja tu. Wanawake hao wanahisi kuwa ukewenza ni
                                                                    57
furaha na unafaida kama wake wenza watashirikiana na kusaidiana. Ukewenza
katika jamii nyingi za Kiafrika ni msingi unaoheshimika kwa kiasi ambacho baadhi
ya Makanisa ya Kiporestanti yamekuwa yakiruhusu mitala. Askofu wa Kanisa la
55
56
    Ibid., pp. 92. 88-93.
   Ibid., pp. 92-97.
57
    Philip L. Kilbride, Plural Marriage For Our Times (Westport, Conn.: Bergin & Garvey, 1994) pp. 108-109.
39

Kianglikana nchini Kenya ametangaza kuwa, “Ingawa kutokuwa na mitala huenda
likawa ni jambo bora kwa kuelezea mapenzi kati ya mume na mke, Kanisa lazima
lizingatie kuwa katika baadhi ya tamaduni mitala ni jambo linalokubaliwa na jamii
                                                                        58
na kuwa imani ya kuwa mitala ni kinyume na Ukristo si ya kufuatwa tena.
Baada ya uchunguzi yakinifu juu ya mitala ya Waafrika, Reverend David Gitari wa
Kanisa la Kianglikana amehitimisha kuwa mitala ni bora kufanywa, na ndio Ukristo
zaidi kuliko talaka na kuoa tena, ili kuwaonea huruma wake walioachwa na watoto
     59
wao. Mimi binafsi nafahamu baadhi ya wake wa Kiafrika waliosoma sana na
ambao, ingawa wamewahi kuishi Ulaya Magharibi kwa miaka mingi, hawana
pingamizi juu ya mitala. Mmoja wao, anayeishi Marekani, kwa dhati kabisa anamsihi
mumewe aoe mke wa pili ili amsaidie kulea watoto.
Tatizo la ujinsia usio na uwiano limekuwa ni tatizo sugu nyakati za vita. Makabila ya
Wahindi Wekundu, watu asilia wa Marekani walikuwa wanasumbuliwa kwa kiasi
kikubwa na tatizo la ujinsia usio na uwiano baada ya kumalizika vita wakiwa
wameshindwa. Wanawake katika makabila hayo, ambao kwa hakika walifurahia hali
ya kijamii ya hali ya juu, walikubali mitala kuwa ndio kinga bora zaidi dhidi ya
matendo ya mahusiano yasiyo na heshima. Walowezi wa Ulaya, bila ya kutoa tiba
                                                                                   60
mbadala, walilaani mitala ya Wahindi na kudai kuwa ni watu wasiostaarabika.
Baada ya vita vya pili vya Dunia, kulikuwa na wanawake 7,300,000 zaidi ya
wanaume nchini Ujerumani (milioni 3.3 miongoni mwao walikuwa wajane).
Kulikuwa na wanaume 100 wenye umri wa miaka 20 hadi 30 kwa kila wanawake
                                      61
                                           Wengi wa wanawake hao wanahitaji167 walio katika umri wa kuolewa.
mwanamume si wa kukaa naye tu lakini pia awe wa kuleta matumizi ya nyumbani
katika nyakati za umasikini usio na kifani na hali ngumu. Majeshi ya muungano
yaliyoshinda yaliwanyonya wanawake hao kwa sababu ya shida zao. Wasichana na
wajane wengi walijihusisha katika mahusiano ya kiasherati na wanajeshi wa majeshi
ya uvamizi. Wanajeshi wengi wa Kimarekani na Kiingereza walikuwa wakitoa
sigara, chokoleti, na mikate kama malipo ya kustarehe na wanawake hao. Watoto
walikuwa wanafurahia sana zawadi hizo zilizotolewa na wageni hao.
Mtoto wa kiume wa umri wa miaka 10 aliposikia zawadi hizo kwa watoto wengine,
                                                                             62
kwa moyo wake wote alitamani aje “Muingereza” kwa mama yake ili wasife njaa.
Lazima tuulize dhamira zetu kuhusu nukta hii: Nini kinamtukuza zaidi mwanamke?
Kukubali na kuheshimu mke wa pili kama ilivyo kwa mtazamo wa Wahindi wekundu
au umalaya wa hakika usio bayana kama ulivyo kwa mtazamo wa watu wenye
   The Weekly Review, Aug. 1, 1987.
   Kilbride, op. cit., p. 126.
60
   John D`Emilio and Estelle B. Freedman, Intimate Matters: A history of Sexuality in America (New York: Harper &
Row Publishers, 1988) p. 87.
61
   Ute Frevert, Women in German History: from Bourgeois Emancipation to Sexual Liberation (New York: Berg
Pulishers, 1988) pp. 263-264.
62
   Ibid., pp. 257-258.
59
58
40

kustaarabika? Kwa maneno mengine, kipi ni chema zaidi kwa mwanamke, maagizo
ya Quran au itikadi inayotegemea utamaduni wa Himaya ya Kirumi?
Ni jambo la kuvutia kujua kwamba katika mkutano wa kimataifa wa vijana
uliofanyika Munich mwaka 1948 tatizo la ujinsia usio na uwiano nchini Ujerumani
lilijadiliwa. Na ilipodhihirika kwa uwazi kuwa hakuna dawa iliyoafikiwa, baadhi ya
washiriki walipendekeza mitala. Jibu la kwanza la washiriki wa mkutano huo
lilikuwa ni mchanganyiko wa mshtuko na kero. Hata hivyo, baada ya uchunguzi wa
kina juu ya pendekezo hilo, washiriki walikubaliana kuwa jambo hilo lilikuwa ndio
utatuzi wa pekee. Kwa hiyo, mitala ilihitimishwa kuwa ni miongoni mwa
                                          63
mapendekezo ya mwisho ya mkutano huo.
Ulimwengu leo hii unamiliki silaha nyingi za maangamizi kuliko ilivyokuwa hapo
kabla na makanisa ya Ulaya hivi karibuni au baadaye, yatalazimika kukubali mitala
kuwa ndio njia pekee. Baba Hillman ameufahamu kiakili sana hakika hiyo, “Ni
ukweli kwamba silaha za kuangamiza (nyukilia, vijidudu na kemikali…) zitaleta
kutokuwa na uwiano wa kijinsia kwa hiyo, mitala itakuwa ni jambo la lazima ili
kunusurika…. Kisha kinyume na utamaduni na sheria zilizotangulia, tabia ya
kuchosha na heshima za kiutu zitaibua tukio la kuthaminiwa kwa mitala. Katika hali
kama hiyo, wananchi na viongozi wa kanisa haraka haraka wataunda sababu nzito
                                                                  64
nzito na maandiko ya Biblia ili kuhalalisha itikadi mpya ya ndoa.
Leo hii, mitala inaendelea kuwa ni utatuzi wa kijitosheleza kwa baadhi ya matatizo
ya kijamii katika jamii za kisasa. Masharti ya kijamii ambayo yanaonyeshwa na
Quran yakishirikiana na ruhusa ya mitala ni jambo linaloonekana sana leo hii katika
baadhi ya jamii za Kimagharibi, kuliko Afrika. Kwa mfano, nchini Marekani leo hii,
kuna matatizo makali sana ya ujinsia katika jamii za watu weusi. Kijana mmoja
katika kila vijana weusi wa kiume kumi anakufa kabla ya kufikia umri wa miaka 21.
Kwa wale walio na umri wa miaka kati ya 20 na 35, mauaji ndiyo sabau kuu ya vifo
      65
vyao.
Aidha, vijana weusi wengi hawajaajiriwa, wapo jela, au wanatumia dawa za
        66
kulevya. Matokeo yake, mmoja kati ya wanawake weusi wanne, wenye umri wa
miaka 40, hajaolewa, ukilinganisha na mwanamke mmoja katika kila wanawake
                 67
kumi wa kizungu.
Zaidi ya hayo, wanawake weusi wengi wanakuwa ni wazazi wasio na mume kabla ya
umri wa miaka 20 na wanajikuta wanashida ya kutokuwa na mtu wa kuwatafutia
63
64
   Sabiq., op. cit., p. 12.
   Hillman, op. cit., p. 12.
65
   Nathan Hare and Julie Hare, ed., Crisis in Black Sexual Politics (San Francisco: Black Think Tank, 1989) p. 25.
66
   Ibid., p. 26.
67
   Kilbride, op. cit., p. 94.
41

ridhiki. Matokeo ya mwisho ya hali hiyo ya kuhuzunisha ni kuongezeka idadi ya
                                                                        68
wanawake weusi wenye uhusiano ujulikanao kwa jina la “kuchangia-bwana.”
Hiyo ni kwa kuwa, wengi wa wanawake hao weusi wasio na waume, wana bahati
mbaya na wana uhusiano wa kiuasherati na wanaume waliooa. Wake nao mara nyingi
wanakuwa hawatambui ukweli kwamba wanawake wengine wanashirikiana nao kwa
waume zao. Baadhi ya waangalizi wa migogoro ya kuchangia bwana katika jamii ya
Wamarekani Waafrika kwa uzito mkubwa wamependekeza mitala yenye mwafaka
kuwa ndilo jibu la muda kwa tatizo la wanaume weusi hadi hapo mapinduzi kamilifu
                                             69
yatakapopatikana katika jamii ya Kimarekani.
Kwa kukubali mitala wanakusudia mitala ambayo imeruhusiwa na jamii na ile
ambayo wahusika wote wameikubali kama ni mbadala wa ada ya siri ya kuchangia
bwana ambayo inawadhuru wote wawili mke na jamii yote kiujumla. Tatizo la
kuchangia mwanamume katika jamii ya Wamarekani Waafrika lilikuwa ndio mada
ya kujadiliwa na jopo katika Chuo Kikuu cha Temple Philadelphia mnamo Januari
          70
27, 1993. Baadhi ya wazungumzaji walipendekeza mitala kuwa ni moja ya utatuzi
unaowezekana kwa mgogoro huo. Pia walipendekeza kuwa mitala isiharamishwe na
sheria, hasa katika jamii zinazoruhusu umalaya na vimada. Maelezo ya mwanamke
mmojawapo miongoni mwa waliohudhuria amesema kuwa Wamarekani Waafrika
wanatakiwa wajifunze kutoka Afrika ambako mitala inafanyika kwa kubembeleza,
mapenzi na nderemo.
Philip Kilbride, mwana anthropolojia- (mtaalamu wa elimu ya asili na maendeleo ya
mwili wa mwanadamu)- ya urithi wa Romani Katoliki, katika kitabu chake cha
uchokozi, Ndoa ya Wengi kwa Wakati wetu, anapendekeza mitala kama ni ufumbuzi
wa baadhi ya matatizo ya kijamii za Kimarekani huru. Amedai kuwa ndoa za wengi
huenda zikahudumia mbadala unaowezekana, mbadala wa talaka katika hali nyingi ili
kuondoa mmomonyoko wa talaka kwa watoto wengi. Ameonyesha kuwa talaka
nyingi zinasababishwa na kutapakaa kwa ngono za nje ya ndoa katika jamii za
Kimarekani. Kwa mujibu wa Kilbride, kumaliza ngono za nje ya ndoa kwa kuoa
wake wengi, ni bora kwa watoto kuliko talaka, “Watoto wataokolewa vizuri kama
tutadumisha familia zisitengane na kuporomoka, limeonekana ni chaguo mojawapo.”
Zaidi ya hayo, anapendekeza kuwa makundi mengine vile vile yatafaidika kutokana
na ndoa za wengi kama vile: wanawake wakongwe ambao wanakabiliana na tatizo la
ukosefu wa wanaume na Waamerika Waafrika ambao wanajihusisha na kuchangia
              71
mwanamume.
Mwaka 1987, kura ya maoni iliyoendeshwa na gazeti la wanafunzi wa chuo kikuu
cha California cha Barkeley iliwauliza wanafunzi kama wanakubali kuwa wanaume
waruhusiwe na sheria wawe na mke zaidi ya mmoja ili kutambua na kujibu upungufu
68
69
    Ibid., p. 95.
    Ibid.
70
   Ibid., pp. 95-99.
71
    Ibid., p. 118.
42

wa wanaume waoao mjini California. Takriban wanafunzi wote waliopiga kura
wamekubali wazo hilo. Mmoja wa wanafunzi wa kike alieleza kuwa ndoa za mitala
zitatimiza hisia zake na mahitaji yake ya kimwili huku akijipatia uhuru mkubwa
                                            72
kuliko itakavyokuwa kwa ndoa za mmoja tu. Kwa hakika, madai kama hayo pia
yanatumiwa na baadhi ya wanawake wachache wenye msimamo mkali ambao bado
wanaendelea kutekeleza mitala nchini Marekani wao wanaamini kuwa ukewenza ni
njia bora kwa mwanamke ili apate mambo mawili; matunzo na watoto kwa
                                                          73
kusaidiana hao wake wenyewe kwa wenyewe kuwalea watoto.
Lazima tuongeze kuwa mitala ya Uislamu ni jambo la makubaliano ya pande mbili.
Hakuna mtu wa kumlazimisha mwanamke aolewe na mume aliyeoa. Aidha, mke ana
                                                                             74
haki kushurutisha kuwa mumewe asioe mwanamke mwingine kama mke wa pili.
Biblia, kwa upande mwingine na wakati mwingine inakimbilia ndoa za mitala za
lazima. Mjane asiye na mtoto lazima aolewe na ndugu wa mumewe, hata kama tayari
ameshaoa (tazama sehemu ya “Matatizo ya Wajane”), bila kujali radhi zake.
(Mwanzo 38:8-10).
Ifahamike kuwa katika jamii nyingi za leo hii suala la kutekeleza mitala ni chache
mno kwa kuwa mwanya kati ya idadi ya jinsia mbili ya kike na ya kiume si mkubwa.
Mtu, kwa kujiamini, anaweza kusema kuwa kiwango cha ndoa za mitala katika
ulimwengu wa Kiislamu ni kidogo sana kulinganisha na kiwango cha ngono za nje ya
ndoa katika nchi za Kimagharibi. Kwa maneno mengine, wanaume katika ulimwengu
wa Kiislamu leo hii ni wapenda mke mmoja sana kuliko wanaume katika nchi za
Kimagharibi.
Billy Graham, mwinjilisti maarufu wa Kikristo ameutambua ukweli huo: “Wakristo
hawawezi kuafiki suala la mitala. Kama sasa hivi Wakristo hawawezi kufanya hivyo,
huko ni kujivunja wenyewe. Uislamu umeruhusu mitala kama ni utatuzi wa matatizo
ya kijamii na umeruhusu kiwango maalumu cha uhuru wa kimaumbile ya kibinadamu
lakini hayo yote yakiwa katika mzingo wa sheria kali zilizotambulishwa. Nchi za
Kikristo zinaonyesha maonyesho makubwa ya ndoa za mke mmoja, lakini kwa hakika
zinatekeleza mitala. Hakuna mtu asiye na mwanamke zaidi ya mkewe, kuna vimada
vinavyowekwa katika jamii za Kimagharibi. Kwa hiyo, Uislamu ni dini ya
kuheshimika yenye wema wa kimsingi, na umemruhusu Mwislamu aoe mke wa pili
kama atalazimika, lakini pia umeharamisha vikali mno aina zote za ndoa za siri na
                                                               75
uzinzi unaohusika ili kulinda uaminifu wa kimaadili wa jamii.”
Ni jambo la kuzingatia kuwa, katika nchi zisizo za Kiislamu na za Kiislamu
ulimwenguni, leo hii, kuna mitala ya kinyume cha sheria. Kujitwalia mke wa pili hata
kwa radhi za mke wa kwanza, ni uvunjaji wa sheria. Kwa upande mwingine,
kumdanganya mke, bila kujua au kutoa radhi zake, ni jambo linalokubalika kisheria
72
73
   Lang, op. cit., p. 172.
   Kilbride, op. cit., pp. 72-73.
74
   Sabiq, op. cit., pp. 187-188.
75
   Abdul Rahman Doi, Woman in Shari`ah (London: Ta-Ha publishers, 1994) p. 76.
43

kabisa kabisa! Sasa ni nini hekima ya kisheria nyuma ya mgongano kama huo? Je,
sheria imetungwa ili kuwazawadia wadanganyifu na kuwaadhibu wema? Jambo hilo
ni moja ya fumbo lisilofikiwa utatuzi la ulimwengu wetu wa kisasa ‘uliostaarabika’.
44

SEHEMU 15 – HIJABU
Mwisho, acha tuangazie kile kinachohesabika katika nchi za Kimagharibi kuwa ni
alama kuu ya kukandamizwa wanawake na kufanywa watumwa, kitu chenyewe ni
hijabu au kufunika kichwa. Je, hivi ni kweli kwamba hakuna kitu kama hijabu katika
itikadi ya Kiyahudi-Kikristo? Acha tunukuu moja kwa moja. Kwa mujibu wa Rabbi
Dr. Menachen M. Brayer (Profesa wa Maandiko ya Biblia wa Chuo Kikuu cha
Yeshiva) katika kitabu chake, Mwanamke wa Kiyahudi katika mafundisho ya
Kirabbiniki, ilikuwa ni desturi ya wanawake wa Kiyahudi kutoka nje kwenye watu
wengi wakiwa na vifuniko vya vichwa ambavyo, wakati mwingine, vilikuwa
                                                76
vinafunika uso wote na kuacha jicho moja tu. Alinukuu baadhi ya maneno ya
wanazuoni wa kale wa Kiyahudi ambao ni mashuhuri, “Si katika mabinti wa
Kiyahudi watembeao nje bila ya kufunika kichwa” na “Laana iwe kwa mtu
anayeruhusu nywele za mkewe zionekane…. mwanamke anayefunua nywele zake kwa
kujipamba anasababisha umasikini.” Sheria ya Kirabbiniki inakataza kukariri
maneno matakatifu au sala mbele ya mwanamke aliyeolewa na aliye kichwa wazi
kwa kuwa kutofunikwa kwa nywele za mwanmke kunachukuliwa kuwa ni “kukaa
       77
uchi.”
Dr. Brayer vile vile ametaja kuwa “katika zama za Tunnaitiki,” mwanamke wa
Kiyahudi anayeshindwa kufunika kichwa chake alihesabiwa kuwa anafedhehesha utu
wake. Na pindi kichwa chake kinapofunuka atalipishwa faini ya Zumzim mia nne kwa
sababu ya dhambi hiyo.” Dr. Brayer vile vile amefafanua kuwa hijabu ya mwanamke
wa Kiyahudi sio siku zote ilikuwa inazingatiwa kuwa ni alama ya wema. Wakati
mwingine, hijabu ilikuwa inaonyesha alama ya upambanuzi na anasa kuliko wema.
Hijabu inatoa mfano wa ufahari na ubora zaidi wa mwanamke mwema. Vile vile
                                                                             78
inawakilisha nafasi ya mwanmke isiyofikika ikiwa ni mali takatifu ya mumewe.
Hijabu ni alama ya heshima binafsi ya mwanamke na nafasi ya kijamii. Wanawake
wa daraja la chini mara nyingi walivaa hijabu ili waonekane kuwa ni wa hali ya juu.
Ukweli wa kuwa hijabu ilikuwa ni alama ya uungwana ndiyo iliyokuwa sababu
iliyowafanya malaya kuzuiwa kufunika nywele zao katika jamii ya kale ya Kiyahudi.
Hata hivyo, malaya wakati mwingine walikuwa wanavaa vitambaa maalumu vya
                                                  79
kichwani ili waonekane kuwa ni wenye heshima. Wanawake wa Kiyahudi katika
nchi za Ulaya waliendelea kuvaa hijabu hadi karne ya kumi na tisa wakati maisha yao
yalipochanganyika sana na utamaduni wa usiofuata dini (kisekyula) uliowazunguka.
Starehe za nje za maisha ya Kiulaya katika karne ya kumi na tisa iliwalazimisha
wengi wao watoke nje vichwa wazi. Baadhi ya wanawake wa Kiyahudin walionelea
ni jambo la kufaa zaidi kubadilisha utamaduni wao wa hijabu na nywele bandia
zikiwa ni kama mtindo mwingine wa kufunika kichwa. Leo hii, wanawake wa
   Menachem M. Brayer, The Jewish Woman in Rabbinic Literature: A Psychosocial Perspective (Hoboken, N.J: Ktav
Publishing House, 1986) p. 239.
77
   Ibid., pp. 316-317. Also see Swidler, op., cit., pp. 121 – 123.
78
   Ibid., p. 139.
79
   Susan W. Schneider, Jewish and Female (New York: Simon & Schuster, 1984) p. 237.
76
45

Kiyahudi halisi wengi hawafuniki nywele zao ila sinagogini. Baadhi yao, kama vile
                                                              81
wa madhehebu ya Hasidiki, wanaendelea kutumia nywele bandia.
Je, mafundisho ya Kikristo yana nini? Ni jambo maarufu sana kuwa watawa wa
Kikatoliki wamefunika vichwa vyao kwa mimia ya miaka, lakini hilo si la mwisho.
Mt. Paulo katika Agano Jipya ameweka maelezo ya kuvutia sana kuhusiana na
hijabu:
 “Lakini nataka mjuwe ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa
cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Kila mwanamume,
asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaabisha kichwa chake. Bali
kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaabisha kichwa
chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. Maana mwanamke
asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au
kunyolewa na afunikwe. Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa,
kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa
mwanamume. Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke
katika mwanamume. Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali
mwanamke kwa ajili ya mwanamume. Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili
ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.” (1 Wakorintho 11:3-10)
Mantiki ya Mt. Paulo kuhusu suala la hijabu za wanawake ni kuwa hijabu
inawakilisha alama ya mamalaka ya mwanamume, ambaye ni sura na utukufu wa
Mungu, juu ya mwanamke ambaye aliumbwa kutoka kwa mwanamume na kwa ajili
ya mwanamume. Mt. Tertullian katika makala zake mashuhuri “Juu ya Hijabu Ya
Mabikira’’ aliandika, “Wasichana, vaeni hijabu zenu mkiwa nje mitaani, hivyo hivyo
mzivae makanisani, mzivae mnapokuwa na wageni, kisha zivaeni mkiwa na kaka
zenu….” Miongoni mwa sheria za kikanuni za kanisa Katoliki leo hii, kuna sheria
                                                                   82
ambayo inawaagiza wanawake wafunike vichwa vyao makanisani. Baadhi ya
madhehebu ya Kikristo, kama vile Waamish na Wameminites wanaendelea
kuwavalisha hijabu wanawake zao hadi siku hizi. Lengo la hijabu, kama
lilivyotolewa na viongozi wao wa Kanisani, ni kuwa “Kufunikwa kichwa ni alama ya
kutii kwa mwanamke kumtii mwanamume na Mungu.” Ambayo ni mantiki ile ile
                                             83
iliyotolewa na Mt. Paulo katika Agano Jipya.
Kutokana na ushahidi wote huo uliotangulia, ni wazi kuwa Uislamu haujazua hijabu.
Hata hivyo, Uislamu umeithibitisha hiyo hijabu. Quran inawataka waumini waume
kwa wake wainamishe macho yao na walinde heshima zao na kisha inawataka
waumini wa kike wajitande hijabu na kufunika shingo na kifua:
80
   Ibid., pp. 238-239.
   Alexandra Wright, “Judaism”, in Holm and Bowker, ed., op. cit., pp. 128-129.
82
   Clara M. Henning, “Cannon Law and the Battle of the Sexes” in Rosemary R. Ruether, ed., Religion and Sexism:
Images of Weoman in the Jewish and Christian Traditions (New York: Simon and Schuster, 1974) p. 272.
83
   Donald B Kraybill, The riddle of the Amish Culture (Baltimore: Johns Hopkins University Press, 1989) p. 56.
81
80
46

 “Waambie wanaume wainamishe macho Yao (wasitazame yaliyokatazwa), na
wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao; bila shaka Mwenyezi Mungu anazo habari za
(yote) wanayoyafanya. Na waambie wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde
tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao ispokuwa vinavyodhihirika (nao ni uso na
vitanga vya mikono - na wengine wanasema na nyayo). Na waangushe shungi zao
mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba
zao…” (Quran 24:30-31)
Quran ipo wazi kabisa, kuwa hijabu ni asili ya wema na kujihifadhi, lakini kwa nini
iwe kujihifadhi ni muhimu? Quran bado inaendelea kuwa wazi:
“Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu
(wangine - waambie) wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi
wajulikane (kuwa ni watu wa hishima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni
Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.” (Quran 33:59)
Hii ndiyo hoja kamili, heshima imeelezwa kuwa ni kinga kwa wanawake wasiudhiwe
au kugeuzwa ni kitu rahisi rahisi, heshima ni kinga. Kwa hiyo, lengo pekee la hijabu
katika Uislamu ni kinga. Hijabu ya Kiislamu, ni kinyume na ya mafundisho ya
Kikristo, si alama ya mamlaka ya mwanamume kwa mwanamke wala si alama ya
utiifu wa wanawake kwa wanaume. Hijabu ya Kiislamu ni kinyume na ya
mafundisho ya Kiyahudi, si alama ya anasa na kujitenga kwa baadhi ya wanawake
wa tabaka la juu walioolewa. Hijabu ya Kiislamu, ni alama ya heshima tu ikiwa na
lengo la kuwakinga wanawake, wanawake wote. Hekima ya Kiislamu ni kuwa siku
zote ni bora kusalimika kuliko kupewa pole. Kwa hakika, Quran inazingatia sana
suala la kulinda miili ya wanawake na sifa zao kiasi ambacho mwanamume
anayethubutu kumsingizia mwanake kuwa ni mzinifu ataadhibiwa vikali:
 “Na wale wanaowasingizia wanawake watahirifu (kuwa wamezini), kisha hawaleti
mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi, (bakora) thamanini, na msiwakubalie
ushahidi wao tena, na hao ndio mafasiki.” (Quran 24:4)
Linganisha mtazamo huu mkali wa Quran na adhabu ya kustarehesha kabisa kwa
kosa la kubaka iliyo katika Biblia: “Mtu mume akimwona kijana aliye mwanamwali
ambaye hajaposwa akamshika na kulala naye, wakaonekana; yule mtu mume
aliyelala naye na ampe baba yake yule kijana shekeli hamsini za fedha, kisha na awe
mkewe kwa, kuwa amemtweza; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote.”
(Kumbukumbu 22:28-39)
Hapa mtu lazima aulize swali lepesi, ni nani hasa aliyeadhibiwa? Mtu aliyelipishwa
faini tu kwa kubaka, au yule msichana aliyelazimishwa kuolewa na mtu aliyembaka
na aishi naye hadi afe? Swali lingine ambalo pia, linatakiwa liulizwe ni hili: Ni jambo
lipi linalowalinda sana wanawake, je, ni mtazamo mkali wa Kiquran au mtazamo wa
kustarehesha wa Kibiblia?
47

Baadhi ya watu na hasa hasa wa Ulaya Magharibi, wanakusudia kuyadhihaki madai
yote yanayodai kujiheshimu kuwa ni kinga. Madai yao ni kuwa; kinga bora zaidi ni
kueneza elimu, tabia za kistarabu, na kujizuia. Sisi tunasema:
Ni jambo zuri lakini halitoshi. Kama ‘ustaarabu’ ni kinga ya kutosha, kwa nini
wanawake wa nchi za Amerika ya Kaskazini hawathubutu kutembea peke yao katika
mitaa yenye kiza – au katika eneo kubwa la wazi? Kama Elimu ni jibu, kwa nini chuo
kikuu kinachoheshimika sana cha Queen kina ‘huduma ya kurudisha nyumbani’ na
hasa hasa wanafunzi wa kike katika eneo la chuo?
Kama kujizuia ni jibu, kwa nini mashitaka ya unyanyasaji kijinsia makazini
yanaripotiwa katika vyombo vya habari kila siku? Mfano wa mashitaka ya
unyanyasaji wa kijinsia, katika kipindi cha miaka michache iliyopita, inakusanya:
Maofisa wa jeshi la wanamaji, Mameneja, Maprofesa wa vyuo vikuu, Maseneta,
Wakuu wa mahakama, na Raisi wa Marekani!
Sikuweza kuamini macho yangu, niliposoma maelezo yafuatayo, yaliyoandikwa
katika waraka uliotolewa na Mkuu wa ofisi za wanawake wa chuo kikuu cha Queen:
Nchini Canada, kila dakika 6 mwanamke mmoja anashambuliwa kijinsia,
Mwanamke mmoja katika kila wanawake watatu nchini Canada atashambuliwa
kijinsia muda wowote ule maishani mwake.
Mwanamke mmoja katika kila wanawake wanne yupo hatarini kubakwa au
kujaribiwa kubakwa maishani mwake,
Mwanamke mmoja katika kila wanawake wanane atashambuliwa kijinsia wakati
akiwa anahudhuria chuoni, na
Uchunguzi umegundua kuwa aslimia sitini 60% ya wavulana wa vyuo vikuu vya
Canada wamesema watatenda shambulio la kijinsia ikiwa wataona kuwa
hawatakamatwa.
Kuna makosa makubwa mno katika jamii tunamoishi. Mabadiliko ya kina katika
mtindo wa maisha ya kijamii lazima yafanyike. Utamaduni wa kujiheshimu
unahitajika ile mbaya, kujiheshimu kimavazi, maongezi, na tabia za wanaume na
wanawake. Vinginevyo mikwaruzano mikali itaongezeka na kuwa mibaya zaidi siku
baada ya siku, na kwa bahati mbaya. Wanawake peke yao ndio watakaoathirika sana.
Watalipia thamani ya hayo. Kwa hakika sote tunaumia lakini kama Bw. K. Gibran
                                                                     84
alivyosema, “…mtu anaepata vipigo si sawa na yule anayevihesabu.” Kwa hiyo,
jamii kama ya Ufaransa ambayo inawafukuza shule wasichana kwa sababu ya nguo
zao za kujiheshimu, nchi hiyo ipo mwishoni, na inajibomoa yenyewe kirahisi.
Ni moja ya kejeli kubwa katika ulimwengu wetu wa leo kuwa kifuniko cha kichwa
kinachovaliwa kwa lengo la kuonyesha “utakatifu” na mamlaka ya mwanamume,
84
Khalil Gibran, Thoughts and Meditations (New York: Bantam Books, 1960) p. 28.
48

kinapovaliwa na watawa wa Kikakotoliki, hakina tatizo. Na kifuniko hicho kinakuwa
kinaonyesha alama ya kukandamizwa wanawake pale kinapovaliwa kwa lengo la
kujihifadhi na wanawake wa Kiislamu.
49

SEHEMU 16 – HITIMISHO
Swali la pekee ambalo wasiokuwa Waislamu, ambao wameshasoma maelezo
yaliyotangulia ya uchunguzi huu, ni: Je, wanawake wa Kiislamu ulimwenguni leo hii
wanapata huduma hizo nzuri nzuri zilizotajwa humu? Jibu, kwa bahati mbaya ni:
Hapana, kwa kuwa, swali hili lisiloepukika katika majadiliano yoyote yanayowahusu
wanawake katika Uislamu, lazima tuchanganue jibu hilo ili tumpatie msomaji picha
kamili.
Kwanza, ni lazima iwekwe wazi kuwa, tofauti kubwa kati ya jamii za Waislamu
zinafanya kuwajumuisha kuwa ndilo jambo lilorahisi sana. Kuna vivuli vipana mno
vya kimtazamo juu ya wanawake katika ulimwengu wa Kiislamu leo hii. Mitazamo
hiyo inatofautiana toka jamii moja hadi nyingine na ndani ya jamii moja yenyewe
kwa yenyewe. Bila kujali, mitazamo ya kiujumla iliyo maalumu na unayotambulika.
Takriban jamii zote za Kiislamu kwa daraja moja au nyingine, zimekengeuka na
kuacha ukamilifu wa Kiislamu unaoheshimu nafasi ya wanawake. Kukengeuka huko,
kwa sehemu kubwa, kumekuwa katika mwelekeo mmoja kati ya miwili
inayopingana. Mwelekeo wa kwanza ni wa kung`ang`ania sana kwa imani kali ya
tamaduni za Kimashariki (Kiarabu). Huku mtazmo wa pili ukiwa ni wa Kiliberali
(uhuru) sana na ni wa tamaduni za Kimagharibi (Kizungu).
Jamii iliyokengeuka na kufuata mwelekeo wa kwanza inawatendea wanawake
kulingana na mila na tamaduni zilizorithiwa kutoka kwa mababu zao. Mila hizo mara
nyingi zinawanyima wanawake haki nyingi walizopewa na Uislamu. Aidha,
wanawake wanatendewa kwa vigezo tofauti kabisa na vile wanavyotendewa
wanaume. Ubaguzi huo unasambaa katika maisha ya kila mwanamke: mwanamke
anapata kufurahiwa kidogo tu wakati anapozaliwa kuliko mwanamume; hapelekwi
shule; ananyimwa fungu katika mirathi ya familia yake; yupo chini ya upelelezi
unaoendelea ili asiende kinyume huku ikiwa kwenda kinyume kwa kaka yake
kunavumiliwa; anaweza kuuliwa kwa kutenda kile ambacho ndugu zake wa kiume
siku zote wanajisifu kwa kukitenda; hana kauli ila mara chache tena katika mambo ya
kifamilia au mapendekezo ya kijamii; yeye anaweza kuwa hana madaraka kamili kwa
mali yake na mahari ya ndoa yake; mwisho akiwa ni mama, yeye mwenyewe
anaweza kupendelea kuzaa watoto wa kiume ili apate nafasi bora katika jamii yake.
Kwa upande mwingine, kuna jamii za Kiislamu (au baadhi ya matabaka maalumu
ndani ya baadhi ya jamii) ambao wamesombwa na tamaduni na njia za maisha za
Kimagharibi. Jamii hizi mara nyingi zinaiga bila kufikiria, chochote wakipokeacho
kutoka Magharibi na mara nyingi wanaishia kuathirika na kuambulia matunda
yaliyooza ya Ustaarabu wa Kimagharibi. Katika jamii hizi, Usasa wa aina yake, wa
ufahari wa hali ya juu wa maisha ya mwanamke ni kuzidisha uzuri wa mwili wake.
Kwa hiyo, ameshikwa na umbo la mwili wake, ukubwa, na uzito. Mwanamke
anakusudia kuujali sana mwili wake kuliko akili zake na zaidi ni kuhusu haiba yake
kuliko akili yake. Uwezo wake wa kiuzuri, kuvutia, na wa kuamsha vichocheo ni vitu
vya thamani sana katika jamii hiyo kuliko mafanikio yake kielimu, ushughulikiaji wa
kiakili, na kazi za kijamii. Mtu hawezi kukuta nakala ya Quran katika pochi yake kwa
50

kuwa imejaa vipodozi ambavyo anakuwa navyo popote aendapo. Moyo wake hauna
nafasi ya kushughulikia mambo ya kijamii kwa mvuto wake. Kwa hiyo, mwanamke
huyo atatumia maisha yake akipambana na mambo mengi ili ajithibitishie uwanamke
wake kuliko kutekeleza utu wake.
Kwa nini jamii za Kiislamu zinakengeuka na kuuacha ukamilifu wa Kiislamu?
Hakuna jibu lepesi. Maelezo yanayojipenyeza juu ya sababu kwa nini Waislamu
hawashikamani na muongozo wa Quran wa kuwaheshimu wanawake maelezo
ambayo yatakuwa ni kinyume na uwezo wa uchunguzi huu. Ni lazima iwekwe wazi,
hata hivyo, kuwa jamii za Kiislamu zimekengeuka kutoka katika maadili ya Uislamu
unahusisha mitazamo mingi sana ya maisha, tena kwa upeo mkubwa. Kuna mwanya
mpana kati ya kile wanachotegemewa kukiamini na kile wakifanyacho kwa hakika.
Mwanya huu si tukio la hivi karibuni.
Mwanya huo umekuwepo kwa karne nyingi na unaendelea kupanuka siku baada ya
siku. Mwanya huo unaopanuka sana una matokeo ya kuangamiza wigo wa
ulimwengu wa Kiislamu, tena katika takriban mitazamo yote ya kimaisha: udhalimu
wa kisiasa na maangamizi, uchumi kubaki nyuma, dhulma ya kijamii, kufilisika
kisayansi, kudumaa kiakili, n.k, Nafasi ya mwanamke katika jamii za wasiokuwa
Waislamu ulimwenguni leo hii ni dalili tu ya maradhi makubwa. Mapinduzi yoyote
ya mkondo wa nafasi ya wanawake wa Kiislamu hayatarajiwi kukamilishwa kama
hayajaambatana na mabadiliko kamili ya maisha jumla ya jamii za Waislamu.
Ulimwengu wa Kiislamu unahitaji mwamko ambao utaupeleka karibu na ukamilifu
wa Kiislamu na sio kuupeleka mbali mno. Ili kuhitimisha, wazo la kuwa nafasi
mbaya ya wanawake wa Kiislamu leo hii ni kwa sababu ya kutofahamika
(kupotoshwa) kabisa kabisa kwa Uislamu. Kwa ujumla matatizo yao ni kwa ajili ya
kushambuliwa sana, wamefikia kilele kirefu cha upweke na jambo hilo.
Pia, ni lazima kutiliwe mkazo tena, kuwa lengo la utafiti linganishi huu si, kukashifu
Uyahudi wala Ukristo, kwa namna yeyote ile.
Nafasi ya mwanamke katika itikadi ya Uyahudi-Ukristo inaweza kuonekana ni ya
kushtua katika vigezo vya wakati wetu huu wa mwishoni mwa karne ya ishirini. Bila
kujali, ni lazima iangaliwe kwa maandishi kamilifu ya kuhistoria. Kwa ibara
nyingine, makadirio yoyote ya uadilifu juu ya nafasi ya wanawake katika itikadi ya
Uyahudi-Ukristo ni lazima yatie maanani matokeo ya kihistoria ambayo kwayo
mafundisho hayo ndio yameanzia. Kutakuwa hakuna shaka yoyote kuwa mitazamo
ya Marabbi na Mapadri wa makanisa ya kumtazama mwanamke yaliathiriwa na
mitazamo mingi ya kuwaona wanawake katika jamii zao. Biblia yenyewe iliandikwa
na waandishi tofauti tofauti na nyakati tofauti tofauti. Waandishi hao hawakuwa ni
wenye kutopenyeka na kuheshimu njia za maisha za watu waliowazunguka. Kwa
mfano, sheria ya uzinzi ya Agano la Kale inachuki sana dhidi ya wanawake kiasi
ambacho inakataa maelezo ya kimantiki ya wanafalsafa.
Hata hivyo, kama tutazingatia ukweli kwamba makabila ya kwanza ya Kiyahudi
yamejawa na hali moja ya kijenetiki na juhudi za upeo wa juu za kujitambulisha wao
51

wenyewe binafsi na kujitenga na makabila yaliyowazunguka na kwa hiyo ngono ya
uzinifu kwa mwanamke aliyeolewa kwa mataifa inaweza kutishia tamaa ya kutunza
mila hiyo, tunatakiwa tufahamu, lakini si lazima kuionea huruma hoja ya upendeleo
huu. Pia, makemeo ya Mapadri wa makanisa dhidi ya wanawake hayatokuwa na
uadilifu kutokana na muktadha wa maelezo ya kuwachukia wanawake ya utamaduni
wa Kigiriki-Kirumi ambao walikuwa wakiishi katika tamaduni hizo. Utakuwa si
uadilifu kutothamini urithi wa Uyahudi-Ukristo bila ya kutoa muktadha wa maelezo
husika.
Kwa hakika, ufahamu wa muktadha wa maelezo ya historia ya Uyahudi-Ukristo pia
ni muhimu sana katika kufahamu umuhimu wa mchango wa Uislamu katika historia
ulimwenguni na ustaarabu wa wanadamu. Itikadi ya Kiyahudi-Kikristo zimeathiriwa
na kuundwa na mazingira, hali na tamaduni zilipokuwapo katika tamaduni hizo. Hadi
kufikia karne ya saba C.E., athari hizo zilipotosha sura asilia ya ujumbe mtakatifu
uliofunuliwa kwa Musa na Yesu bila ya kutambua. Hali duni ya wanawake katika
ulimwengu wa Kiyahudi-Kikristo katika karne ya saba ni moja ya hoja tu. Kwa hiyo,
kulikuwa na haja kubwa ya ujumbe mtakatifu mpya ambao utaongoza wanadamu
warejee katika njia iliyonyooka. Quran imefafanua kazi ya mjumbe mpya ni
kuwaweka huru Wayahudi na Wakristo kutokana na mizigo mizito ambayo walikuwa
wanaibeba: “Ambao wanamfuata Mtume, Nabii aliye Ummy (asiyejua kusoma wala
kuandika, na juu ya hivi atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya Uislamu), ambaye
wanamuona ameandikwa kwao katika Taurati na Injili ambaye anawaamrisha mema
na anawakataza yaliyo mabaya, na kuwahalalishia vizuri na kuwaharamishia vibaya,
na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao (yaani sharia ngumu za
zamani na mila za kikafiri). Basi wale waliomuamini yeye na kumuhishimu na
kumsaidia na kuifuata Nuru iliyoteremshwa pamoja naye (yaani Quran) hao ndio
wenye kufaulu.” (Quran 7:157)
Kwa hiyo, Uislamu usitazamwe kuwa ni mpinzani wa itikadi ya Kiyahudi au
Kikristo. Inatakiwa uzingatiwe kuwa ni kilele cha ukamilisho, na utimilifu wa
ujumbe mtukufu ambao ulifunuliwa hapo kabla.
Mwisho wa uchunguzi huu, ningependa nitoe ushauri ufuatao kwa jamii ya Waislamu
ulimwenguni. Wanawake wa Kiislamu wengi wamekuwa wakipinga haki zao za
msingi za Kiislamu kwa muda mrefu. Makosa yaliyopita lazima yasahihishwe.
Kufanya hivyo si kusaidia, huo ni wajibu usio na budi kwa kila Mwislamu. Jamii ya
ulimwengu mzima lazima washughulikie mapatano ya haki za wanawake wa
Kiislamu kwa misingi ya mafundisho ya Quran na Mtume wa Kiislamu. Mapatano
hayo lazima yatawapa wanawake wa Kiislamu haki zote zilizotolewa kwao na
Muumba. Kisha, mambo yote ya lazima, lazima yaendelezwe ili kuhakikisha
utekelezaji mkamilifu wa mkataba huo. Mkataba huu unasubiriwa kwa muda mrefu,
lakini ni bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa. Ikiwa wa ulimwengu mzima
hawatatoa dhamana ya kukamilisha haki zote za Kiislamu za mama zao, wake, dada,
na mabinti zao, ni nani mwingine atakayefanya hivyo?
52

Kwa kuongezea, lazima tuwe na ushujaa wa kukabiliana na mambo yetu yaliyopita,
na kuaacha papo hapo mila na tamaduni za wahenga wetu pale walipovunja sheria ya
maadili ya Kiislamu. Je, Uislamu haukosoi vikali mila za wapagani wa Kiarabu za
kufuata tamaduni za wazee wao kiupofu? Kwa upande mwingine, lazima tuendeleze
mtazamo wa ukosoaji dhidi ya kila tunachopokea kutoka Magharibi au kutoka
tamaduni nyingine zozote zile. Kuathiriana na kujifunza kutoka katika tamaduni za
watu wengine ni jambo la thamani sana. Quran, kwa ufupi na uwazi, inazingatia
kuathiriana huko kuwa ni moja ya malengo ya kuumbwa kwetu. “Enyi watu! Kwa
hakika Tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja; Adamu) na (yule
yule) mwanamke (mmoja; Hawwa). Na Tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali
mbali) ili mjuane (tu basi; siyo mkejeliane).... (Quran 49:13). Kitu hicho kinaendelea
lakini hakisemwi, hata hivyo, kuwaiga kibubusa watu wengine, kwa hakika ni alama
ya kutojithamini.
Na kwa wasomaji wasiokuwa Waislamu, wawe Wayahudi, Wakristo au wowote
wale, haya maneno ya mwisho ni wakfu. Ni jambo la kutatanisha kwa nini dini
ambayo imefanya mapinduzi ya kumkomboa mwanamke imetengwa na kupakwa
matope kuwa ni ya kukandamiza sana wanawake. Ufahamu huu juu ya Uislamu ni
moja ya mauzauza yalioenea sana duniani leo hii. Mauzauza hayo yamekuwa
yanaendelezwa na mlolongo usio na mwisho wa vitabu vya kusisimua, makala,
taswira ya vyombo vya habari, na sinema za Hallwood. Matokeo yasioepukika ya
mlolongo huu wa taswira ya kupotosha umekuwa ni kutofahamika kabisa kabisa na
hofu juu ya kila kitu kinachofungamana na Uislamu. Taswira hii ya kuuona vibaya
Uislamu katika vyombo vya habari ulimwenguni lazima ikome kama tunataka kuishi
katika dunia huru iliyoepukana na mielekeo yote ya kibaguzi, madhara, na kupotosha.
Wasiokuwa Waislamu wanatakiwa watambue kuwa kuna mwanya mpana kati ya
imani ya Kiislamu na matendo ya Waislamu na ukweli mwepesi kuwa matendo ya si
lazima yawe yanawakilisha Uislamu. Ili kutoa jina kwa nafasi ya mwanamke katika
ulimwengu wa Kiislamu leo hii kuwa ni ya “Kiislamu” ni jambo lililombali sana na
ukweli, sawa na kuita nafasi ya mwanamke katika nchi za kimagharibi leo hii kuwa
ni ya “Kiyahudi-Kikristo”. Kwa ufahamu huu, Waislamu na wasio Waislamu lazima
waanze hatua ya kuwasiliana na kuzungumza ili kuondosha upotoshaji, wasiwasi na
hofu. Mustakabali wenye amani kwa familia ya kibinadamu unalazimisha kuwepo
mazungumzo hayo.
Uislamu lazima utazamwe kama dini iliyoithibitisha sana nafasi ya wanawake na
umewapa haki nyingi ambazo dunia ya kisasa umezitambua katika karne hii. Uislamu
bado una mengi ya kuwapa wanawake wa kisasa: utu, heshima, na ulinzi katika kila
nyanja na kila hatua ya maisha yake toka kuzaliwa hadi kifo, kwa kuongezea ili
kutambulisha, kuwa na uwiano, na kima cha mahitajio yake yote ya kiroho, kifikra,
kimwili na kimawazo. Si ajabu wengi wa wale wanaochagua kuwa wawe Waislamu
katika nchi kama vile Uingereza ni wanawake. Nchini Marekani wanawake
wanaobadili dini na kuwa Waislamu ni wengi zaidi kuliko wanaume kwa kiwango
             85
cha 4 kwa 1.
85
The Times, Nov. 18, 1993.
53

Uislamu una mengi ya kuupa ulimwengu wetu ambao unahitaji sana mwongozo wa
kimaadili uongozi. Balozi Herman Eilts, akitoa ushahidi mbele ya tume ya uhusiano
wa mamabo ya nje katika baraza la wawakilishi-Congress la Marekani Juni 24, 1985,
amesema, “Idadi ya jamii ya Kiislamu ulimwenguni leo hii inakaribia bilioni moja.
Na hiyo ni idadi ya kushtusha. Lakini kinachonishangaza zaidi ni kuwa leo hii
Uislamu unakuwa haraka sana kuliko dini nyingine zenye kuamini Mungu mmoja.
Jambo hili lazima tulizingatie. Kuna kitu cha haki katika Uislamu. Uislamu
unawavutia watu wema wengi.” Ndio, kuna haki katika Uislamu na huu ndio wakati
wa kujua hivyo. Natarajia kuwa uchunguzi huu ni hatua mojawapo ya mwelekeo huo.
54

Kimefasiriwa na
Bw. Omari Juma Mangilile, Mwanafunzi katika Kitivo cha malezi na ualimu kiwango cha
                   shahada ya uzamili chuo kikuu cha Cairo,
Na ni Mwanachama wa Tanzania Students Union (TSU)
E_mail:mangilile@yahoo.com
Cairo. (A.R.E).
Kimepitiwa na,
Bw. Mohammed Sultani Ngunde
55

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget