Monday, April 9, 2012

Tiba ya Kiislamu na Historia yake


Na; Bakar Alliy
Baada ya kumshukuru Mola muumba,nakumtakia rehema na amani mtukufu Mtume(s.a.w.w) .
Nachukua nafasi hii kuelezea kwa ufupi historia ya tiba kwa sura ya ujumla, na  kisha kuangalia mtazamo wa dini ya kiislamu kunako tiba .
Swali lipaswalo kujiuliza ni kwamba elimu ya tiba ilianza zama gani? Pia mtazamo wa uislamu kuhusu tiba ni upi? Ndugu msomaji tushirikiane ili kupata majibu mema yatakayo tunufaisha sisi na   jamii kwa ujumla.

Kuna khitilafu baina ya wataalamu na wanahistoria kunako uanzishwaji wa elimu hii (ya tiba) Ambapo baadhi yao wakadai kwamba mwanzilishaji wa elimu hii ni Nabii Idrisa(a.s).
Wengine wakasema kuwa mwanzilishi wake ni:Harmas Lul, na wengine wakainasibisha elimu hii ya tiba na tamaduni za Babel, Yemen, Misri, Ajemi, India, Ugiriki  n.k.
Wengine wakasema kuwa elimu ya tiba ilianzishwa  na kutambulikana kama sanaa, na  baada ya karne nyingi kupita ikapata mfumo na sura mpya na kuwa  elimu kamili.
Ndugu msomaji vyovyote  vile iwavyo elimu ya tiba iko sambamba na kuwepo mwandamu katika sayari hii (ya dunia) kwa sababu magonjwa yanaambatana na maisha ya mwanadamu, hivyo kulikuwa kuna aina mbali mbali za matibabu zilizokuwa zikitumika katika kujiponya.
Isipokuwa tiba ya zama hizo ni tofauti na sasa kwa kulinganisha  maendeleo ya zama zile na sasa.

katika zama za Jalinus(201), Biqrati(277) na Plato (428) elimu ya tiba ilipangiliwa kiufanisi na kitaalamu haikuwa kwa maana ya uwanzilishi wa elimuhii,pia baada ya kudhihiri uislamu utabibu uilipanuka zaidi,hii kwasababu uislamu  unasisitiza utafutaji wa elimu katika nyanja tofauti,pia katika kombi maalumu kama vile tiba na kombi nyinginezo.
Mtume  mtukufu [s.a.w.w] anasema ; tumbo nimakazi ya kila magonjwa na kujiepusha{na visababibishavyo matatizo}ndio msingi wa lika ponyo...
Maendeleo ya tiba yaliboreka kama ifuatavyo;
 a)Kutoka zama za Mtume mtukufu mpaka mwaka[133 A.H] sawa na[750 A.D]
Zama hizi ni kuanzia zama za uongozi wa Mtume mpaka mpaka zama za makhalifa wanne.
Katika zama hizi kwa sababu ya upya wa serikali ya kiislamu zama zile waislamu walishindwa kuipa kipaombele kwa sababu hiyo hakukuwa na madaktari wengi waliobobea katika elimu hii.

Isipokuwa kuna watu kadhaa walikifahamika  zama zile kama;
1-Shimrdel
2-Dhamad bin Thaalabah
3-Ibun Abi Ramdhah Tamimi
{mpasuaji}.
b)Kutoka mwaka (133A.H)mpaka mwaka (287A.H) sawa na (900A.D)
katika zama hizi kulifanyika kazi mbili nazo ni kama zifuatazo;
1)Tarjama:Zama hizi waislamu walianza kutarjum vitabu vya Kigiriki, Kirumi na Kihindi kuelekea katika lugha ya kiarabu kiongozi wa kazi hii alikuwa ni; Abu Zaidi Husayni bin Is-haka na mwanawe.
2)Zama za utunzi na uandishi wa vitabu vya tiba ambapo Abu Hasan Ally bin Sahari bin Tabariy ambae aliandika kitabu kwa jina la Firdawsi al Hikmah, akiwa ni mwandishi wa kwanza katika  elimu ya tiba kwa  waislam.
c)kuanzia mwaka (287-700A.H) 
katika zama hizi waislamu walipiga hatua na kuendelea katika taaluma ya tiba kiasi kwamba wasomi wa kimagharibi walisema kuwa muda huu ni: wa thamani na wa dhahabu kwa waislamu kimaendeleo.

Dokta G.I. PARK anasema: katika zama ambazo wamagharibi walipokuwa katika kipindi kibaya, kipindi  ambacho waislamu katika miji tofauti ya kitamaduni ulimwenguni wakisonga mbele kimaendeleo ambapo Bagdad, Damaskas, Kairo na miji mengine ambayo mashule ya katabibu pia mahospitali yalijengwa katika miji hiyo hali ambayo ilionyesha maendeleo ya hali ya juu katika elimu ya tiba na udaktari. Anaendelea kusema kuwa Baghdad zilijengwa hospitali zaidi ya 60 na Kairo 33 hali ya kuwa ndani ya Ulaya hospitali ya kwanza ilijengwa mwaka 1793 (A.D) katika mji  wa Yuraki Uengereza.
Matabibu wa kiislamu mashuhuri wa zama hizi:Katika zama hizi walipatikana madaktari tofauti miongoni mwao :Avicenna, Razi, Ahwazi, Jurjaniy, n.k
baada ya waislamu kufikia kilele cha utabibu katika zama hizi zilitokea sababu tofauti ambazo zilipelekea kushuka kitaaluma{utabibu} miongoni mwazo ni: 

A -Kukithiri kwa vita
B –Kukithiri khitilafu za kimadhehebu baina  ya waislamu
C –Kukimbia kwa wanazuoni na kwenda nchi nyengine
D –Kuchomwa moto maktaba za kiislamu .

hizi ni baadhi ya sababu zilipelekea waislamu kuporomoka kielimu  waislamu.
Hivyo baada ya kuporomoka waislamu ndipo nchi za kimagharibi zikaanza kupambamoto na kuanzisha kitengo cha kuhuisha elimu ya tiba katika  karne ya 16 nchini Uengereza mji wa  Yurak. Hii ni ishara iyoneshayo kuchelewa kimaendeleo katika nchi za kimagharibi ukilinganisha na wasilamu katika kipindi hicho.

*  Misingi  ya tiba na udaktari ulianza pamoja na kuwepo mwanadamu katika sayari na kwa kupitia karne mpaka kwenda nyengine elimu hii ikiimarika zaidi na ulipofika uislamu kwa kuwa uislamu unasisitiza kutafuta elimu na kutafakari pia uashiriaji  wa uislamu  kunako aya na hadithi za tiba na udaktari .Waislamu walijiingiza katika elimu hii hatimae kutoa madaktari mfano wa Avicenna. 

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget