Tuesday, February 21, 2012

Makasisi (viongozi wa kikristo) wasilimu


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU 
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU


MAKASISI WAINGIA UISLAMU
Yaliyomo
1. KASISI YUSUFU ESTES ALIYEKUWA MFANYABIASHARA WA KIKRISTO &
MUHUBIRI (USA) ............................................................................................................... 3
2 – ABDULLAH M. AL-FARUQUE ALIYEKUWA AKIIITWA KENETH L. JENKINS,
MCHUNGAJI NA MZEE WA KANISA LA PENTECOSTAL. (USA) ........................... 23
3- DR. JERALD F. DIRKS (ABU YAHYA) ALIYEKUWA MCHUNGAJI (SHEMASI)
WA KANISA LA MUUNGANO WA WAMETHODISTI. ANA STASHAHADA YA
UZAMILI YA THEOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA HARVARD NA STASHAHADA
YA UDAKITARI WA FALSAFA KATIKA MAMBO YA KISAIKOLOJIA YA CHUO
KIKUU CHA DENVER. (USA) ......................................................................................... 31
4 - SISTA KHADIJA “SUE” WATSON ALIYEKUWA MCHUNGAJI, MMISHIONARI,
NA PROFESA ANA STASHAHADA YA UZAMILI YA MASWALA YA THEOLOJIA
(NI MMAREKANI MWENYE ASILI YA KIFILIPINO) ................................................. 45
4 - SISTA KHADIJA “SUE” WATSON ALIYEKUWA MCHUNGAJI, MMISHIONARI,
NA PROFESA ANA STASHAHADA YA UZAMILI YA MASWALA YA THEOLOJIA
(NI MMAREKANI MWENYE ASILI YA KIFILIPINO) ................................................. 46
5 IBRAHIM KHALIL AHMED (IBRAHIM KHALIL PHILOBUS) PADRI WA COPTIC
NA NI MMISHIONARI (MISRI)....................................................................................... 50
6- MARTIN JOHN MWAIPOPO ALIYEKUWA KASISI MKUU WA KILUTHERANI
(TANZANIA)...................................................................................................................... 57
7- RAPHAEL NARBAEZ ALIYEKUWA MCHUNGAJI WA MASHAHIDI WA
YEHOVA (USA) ................................................................................................................ 62
8- GEORGE ANTHONY – ALIYEKUWA PADRI WA KIKATOLIKI (SRI LANKA) . 72
9- DR. GARY MILLER (ABDUL-AHAD OMAR) MWANAHISABATI NA
MMISHIONARI WA KIKRISTO (CANADA) ................................................................. 74
10- REV. DAVID BENJAMIN KELDANI (ABDUL’L-AHAD DAWUD) (IRAN). ....... 80
11- MUHAMMAD AMAN HOBHM MWANADIPLOMASIA, MMISHIONARI NA
MFANYAKAZI WA KAZI ZA JAMII (UJERUMANI). .................................................. 83
12- PADRI MKUU VIACHESLAV POLOSIN (URUSI). ................................................ 85

3
1.KASISIYUSUFUESTESALIYEKUWA
MFANYABIASHARA WA KIKRISTO & MUHUBIRI (USA 1)
ﺓﺭﻮﺻ Chaplain
ﺓﺭﻮﺻ Chaplain
Sasa hivi jina langu ni Yusufu Estes, lakini miaka iliyopita rafiki zangu
walikuwa wakiniita Skip. Nimeshahubiri Ukristo na kufanya kazi za burudani
na muziki tangu nilipokuwa mdogo katika miaka ya hamsini. Mimi na baba
yangu tulianzisha duka la muziki, vipindi vya t.v, redio na burudani za nje ya
nyumba kwa ajili ya kujifurahisha na (kujinufaisha). Nilikuwa mchungaji wa
upande wa muziki, pia nilikuwa naendesha farasi na kuwaburudisha watoto
nikiwa ni (Skippy the Clow).
Niliwahi kutoa huduma ya uwakilishi katika mazungumzo ya amani ya
viongozi wa kidini wa Umoja wa Mataifa, kwa sasa mimi ni mstaafu wa
taasisi ya kutunza taarifa za wafungwa nchini Marekani. Vilevile nafanyakazi
pamoja na wanafunzi wa Kiislamu, jumuia za vijana na shule za watoto wa
Kiislamu. Kwa hiyo, natembea ulimwengu mzima, nikitoa mihadhara na
kushiriki katika kutoa ujumbe wa Kristo katika Quran kwenye Uislamu.
Tumeshafanya mazungumzo na mijadala ya pamoja na watu wa imani zote na
tumefurahia kufanya kazi ubavuni mwa marrabi 2 wa Kiyahudi, wachungaji,
wahubiri na mapadri wa kila sehemu. Baadhi ya kazi zetu zinafanyika katika
maeneo ya ustawi wa jamii, jeshi, vyuo vikuu na majela. Kimsingi lengo letu
ni kuelimisha na kufikisha ujumbe sahihi wa Uislamu na kufahamisha ni
nanihasa ndio Waislamu wa kweli. Ingawa kwa sasa Uislamu umeshakua na
kuukaribia Ukristo ambao ni dini kubwa duniani. Tumeona wengi katika wale
wanaodai kuwa ni Waislamu, hawafahamu vizuri hata kutangaza ujumbe wa
“Amani, utiifu, na kusalimu amri kwa Mwenyezi Mungu. [Arabic =
‘Islam’]
Ilitokeaje: Inawezekana kuonekana ni ajabu sana, huku ikiwa huenda
tukashirikiana baadhi ya taswira chache zilizotofauti tofauti pia itikadi juu ya


1-USA ni kifupi cha United States of Amerca yaani Marekani.
2-Marrabi ni Wanazuoni au wakuu wa dini ya Kiyahudi.

4
Mungu, Yesu, Utume, dhambi na uwokovu. Lakini unajua tena, kipindi fulani
nilikuwa katika boti moja na watu wengi walio katika boti hiyo sasa hivi.
Kwa hakika nilikuwemo. Acha nieleze.
Nimezaliwa katika familia ya Kikristo madhubuti sana katika Midwest.
Familia yetu na wazee wake sio tu wamejenga makanisa na shule katika ardhi
hii ya Midwest, pia walikuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kufika
hapo. Nilipokuwa shule ya msingi, tulikuwa tunakaa Huston, Texas mwaka
1949 (nikiwa ni mtu mzima). Kila siku tulikuwa tunaenda kanisani na
nilibatizwa Pasadena, Texas nikiwa na umri wa miaka 12. Nikiwa kijana wa
umri wa miaka kumi na kitu, nilipendelea kutembelea makanisa mengine ili
nijifunze zaidi mafundisho na imani zao. Kanisa la Kibatisti, Methodisti,
Episcopalians, Charismatic movement, Full Gospel, Agepe, Katoliki,
Presbyterians, na mengine mengi. Nilikuwa nimeshapevuka vizuri na kiu ya
(Injili) au kama tuiitavyo; “Habari njema.” Uchunguzi wangu juu ya dini
haukuishia Ukristo, hata kidogo. Ulishirikisha, dini ya Kihindu, Kiyahudi,
Kibudha, Metaphizikia, imani za wamarekani asilia. Na ilikuwa ni dini moja
tu ambayo sijaitazama kwa makini, nayo ilikuwa ni “Uislamu” Kwa nini?
Swali zuri.
Mchungaji wa Muziki
Kwa vyovyote vile, nilikuwa navutiwa sana na aina mbali mbali za muziki, na
hasa hasa muziki wa Injili na Klasikia. Kwa kuwa familia yangu yote ilikuwa
ni ya kidini na muziki ilioufuata ndiyo huo huo nilioufuata na nikaanza
masomo yangu katika maeneo hayo mawili. Mambo yote hayo yamenifanya
niwe katika nafasi mwafaka ya uchungaji wa muziki katika makanisa mengi
ambayo nilikuwa mshiriki wake kwa miaka mingi. Nilianza kufundisha ala ya
Kibodi mnamo mwaka 1960 na hadi kufikia 1963 nilikuwa namiliki studio
yangu mwenyewe eneo la Laurel, Maryland, iitwayo ‘Estes Music Studiy.’
Miradi ya Biashara mjini Texas, Oklahoma na Florida.
Miaka therathini iliyofuata, mimi na baba, tulifanya kazi pamoja katika miradi
mingi ya kibiashara. Tulikuwa na vipindi vya burudani, kuonyesha shoo na
vivutio. Tulifungua maduka ya piano na vinanda katika maeneo yote kuanzia
Texas na Oklahoma hadi Florida. Tulichuma mamilioni ya dola katika miaka
hiyo, lakini hatukupata utulivu wa moyo ambao unaweza kuja kwa kupitia
kuufahamu ukweli na kuupata mpango sahihi wa uwokovu tu. Nina hakika
kuwa umeshajiuliza swali hili “Kwa nini Mungu ameniumba?” au “Mungu
ananitaka nifanye nini?” au “Nani ndiye Mungu wa kweli, kwa vyovyote

5
vile?” “Kwa nini tunaamini dhambi ya asili?” na “Kwa nini wanadamu
wamelazimishwa wakubali ‘dhambi’ za Adamu na kisha matokeo yake
waadhibiwe milele?” Lakini kama utamuuliza mtu yeyote maswali hayo,
watakujibu kuwa unalazimika uamini bila ya kuhoji, au kuwa hiyo ni “siri
isiyoelezwa” na hutakiwi kuuliza “Kaka wewe amini tu.”
Maana ya Utatu
Jambo la kushangaza sana, neno ‘utatu’ halimo katika Biblia. Na limekuwa
likihusishwa na wanazuoni wa kidini mapema mnamo miaka mia mbili baada
ya kunyanyuliwa kwa Yesu kwenda kwa Mungu wake Muweza.
Ningewaomba wahubiri na wachungaji wanipe japo fikra, vipi ‘moja’
itapigwa hesabu ili iwe ‘tatu’ au vipi Mungu mwenyewe awezaye kufanya
kila kitu atakacho, hawezi kuwasamehe watu na dhambi zao, isipokuwa hadi
ajifanye mwanadamu, aje chini duniani, awe mtu, na kisha achukuwe
madhambi ya watu wote; huku tukiweka akilini kuwa pamoja na hayo yote
yeye ni Mungu wa Ulimwengu wote na anafanya atakalo kulifanya, popote
pale, ndani na nje ya ulimwengu kama tunavyojua. Hao wahubiri na
wachungaji kamwe hawaonyeshi kuwa wataweza kuleta kitu kingine zaidi ya
maoni yao au mlinganisho wa kiajabu ajabu.
Baba - Mchungaji Msimikwa Asiye Na Madhehebu
Baba yangu alikuwa mchangamfu sana katika kuunga mkono kazi za kanisa,
na hasa hasa vipindi vya shule ya kanisa. Akasimikwa ukasisi katika miaka ya
sabini. Yeye na mkewe (mama yangu wa kambo) walikuwa wanawajua
wainjilisti na wahubiri wa kwenye tv wengi, vilevile wameshamtembelea Oral
Roberts na wamesaidia kujenga ‘mnara wa sala’ katika Tulsa, pia walikuwa ni
waungaji mkono imara wa Jimmy Swaggart, Jim na Tommy Fae Bakker,
Jerry Fallwell, John Haggi na Pat Robertson.
Kukutana na Mtu Kutokea Misri
Ilikuwa ni mwanzoni mwa 1991 pale baba yangu alipoanza kufanyabiashara
na mtu kutoka Misri na kuniambia kuwa anataka nikutane na mtu huyo. Wazo
hilo lilinivutia kwani niliwaza juu ya wazo la kuwa na ladha ya kimataifa.
Unajua tena, mapiramidi, Sphinx, mto Naili na mengineyo.
Alikuwa ni ‘Mwislamu’: Watekajinyara, Walipuaji mabomu, Magaidi,
na ni nani ajuaye kingine ni nini?

6
Kisha baba yangu alieleza kuwa mtu huyo ni ‘Mwislamu.’ Awali, nilichukia
wazo la kukutana na mtu asiye na imani, mtekajinyara, mlipuaji mabomu,
gaidi, kafiri.’ Mtu yeyote wa kawaida angelikataa wazo hilo. Sikuamini
masikio yangu. Mwislamu?’ Haiwezekani! Nilimkumbusha baba yangu
mambo mbali mbali tuliyoyasikia juu ya watu hao ‘Waislamu.’
Uongo dhidi ya Waislamu na Uislamu – walitwambia, kuwa Waislamu:
  Hata hawaamini Mungu.
  Wanaabudu boksi jeusi liliopo jangwani.
  Na wanabusu ardhi mara tano kwa siku.
Haiwezekani! Sikutaka Kukutana Naye!
Sikutaka kukutana na Mwislamu huyo. Haiwezekani! Baba yangu alisisitiza
nikutane naye na akanihakikishia kuwa mtu huyo ni mwema sana. Hilo
lilikuwa ni kubwa mno kwangu. Na hasa hasa walokole tuliokuwa tunasafiri
nao wote waliwachukia sana Waislamu na Uislamu. Hata walikuwa wakisema
vitu visivyo vya kweli ili kuwatisha watu waougope Uislamu. Kwa hiyo, kwa
nini mimi nihitaji kitu cha kufanya na watu hao?
Wazo: ‘Kumbadilisha Awe Mkristo.’
Kisha wazo fulani lilinijia, ‘Tunaweza kumbadili mtu huyo awe Mkristo.’
Kwa hiyo, nilikubali na kuafiki kukutana naye. Lakini kwa masharti yangu.
Nikutane naye nikiwa na Biblia, Msalaba na kofia ya chopeo (kepu)
iliyoandikwa ‘Yesu ni Bwana.’ Nilikubali nikutane naye siku ya Jumapili
baada ya kutoka kanisani. Kwa hiyo, sote tungesali na kusimama vizuri na
Bwana. Ningechukua Biblia yangu chini ya kwapa kama desturi. Ningekuwa
na msalaba wangu mkubwa ung`aao na kuning`inia pia ningevaa kofia yangu
isemayo: ‘Yesu ni Bwana.’ Maandishi yaliyo kwa mkato upande wa mbele.
Mke wangu na mabinti zangu wawili wadogo wangekuja na sote tungekuwa
tayari kwa kukabiliana kwa mara ya kwanza na ‘Waislamu.’
Yupo wapi? Nilipoingia dukani na kumuuliza baba; “Huyo Mwislamu yupo
wapi”, aliashiria na kusema: “Yule pale.” Nilichanganyikiwa. Huyo hawezi
kuwa Mwislamu. Haiwezekani.
Kiremba na midevu? Nalitafuta jitu kubwa lenye majoho yanayoburura,
mremba mkubwa kichwani mwake, midevu inayofikia nusu ya shati lake na

7
minyusi ya machoni ambayo inakatiza paji la uso wake akiwa na upanga au
bomu chini ya koti lake.
Hakuna Kiremba – Hakuna Midevu – [Hakuna Nywele Kabisa!]
Mtu huyo hakuwa na midevu. Kwa hakika, hakuwa na nywele kabisa
kichwani mwake. Alikuwa nusu kipara. Zuri zaidi, alikuwa anapendeza sana
pamoja na karibisho moto moto na kupeana mikono. Lakini jambo hilo
halikuwa na taathira. Nilifikiria kuwa wao ni magaidi na walipua mabomu. Je,
yote hayo ni kwa nini?
Mtu huyo anahitaji Yesu bila kujali. Nitamshughulikia mtu huyo. Anahitaji
kuokolewa kwa ‘Jina la Yesu’ na mimi na Bwana tutafanya hivyo.
Kutambulishana na mahojiano
Baada ya kutambulishana kwa haraka haraka, nilimuuliza: “Je, unamwamini
Mungu?”
Akasema: “Ndiyo (vizuri!)
Kisha nikasema: “Je, unaamini Adamu na Hawa?”
Akasema: “Ndiyo (vizuri sana!)
Nikasema: “Vipi kuhusu Ibrahimu? Je, unamwamini na namna
alivyojaribu kumtoa muhanga mwanawe kwa ajili ya Mungu?”
Akasema: “Ndiyo (hata inawezekana ni vizuri zaidi!)
Kisha niliuliza: “Vipi kuhusu Musa?” “Amri kumi” “Kuvuka bahari
nyekundu?”
Kwa mara nyingine akasema: “Ndiyo (bado ni vizuri zaidi!)
Kisha: Vipi kuhusu Mitume mingine, kama Daudi, Suleimani na Yahya
(Yohana mbatizaji)?”
Akasema: “Ndiyo (bab kubwa!)
Nilimuuliza: “Je, unaiamini Biblia?”
Kwa mara nyingine, akasema: “Ndiyo (ok!)
Kwa hiyo, kwa hivi sasa ilikuwa ndio muda wa swali kubwa; Je,
unamwamini Yesu? Aliyekuwa ndiye Messiah Kristo wa Mungu?
Kwa mara nyingine akasema: “Ndiyo (Safi sana!)
Sasa ni vizuri – “Huyu atakuwa ni mwepesi sana kuliko nilivyofikiria.”
Alikuwa tayari kubatizwa ila alikuwa hatambui jambo hilo. Nami
nilikuwa ndiye nitakayemfanya hivyo.
Elimu ya Kushtua Waislamu wanaamini Biblia?

8
Siku moja katika majira ya michipuo mwaka 1991, nilijua kuwa Waislamu
wanaamini Biblia. Nilishtushwa. Hilo litakuwaje? Lakini hilo si la mwisho,
wanaamini Yesu kuwa ni:
    Mtume wa kweli wa Mungu.
    Nabii wa Mungu.
    Kazaliwa kimiujiza bila ya tendo la ndoa la wanadamu.
    Alikuwa ni “Kristo” au Messiah kama alivyobashiriwa na Biblia;
    Kwa sasa yupo pamoja na Mungu na la muhimu sana ni:
    Atarejea tena siku za mwishoni kuwaongoza waumini dhidi ya
      mpinga Kristo.
Baada ya “kushinda roho na kuipeleka kwa Bwana, kwa Yesu” siku baada
ya siku, jambo hilo litakuwa ndiyo mafanikio yangu makubwa, kumnasa
mmoja wa “Waislamu” hawa na ‘kumbadili’ awe Mkristo.”
Nilimuuliza kama anataka chai na akanijibu ndiyo. Kwa mbali, tulikiendea
kibanda kidogo kilichopo katika jengo kubwa la biashara, kukaa na
kuzungumzia mada yangu niipendayo ya Imani. Tulipokuwa tumekaa katika
kiduka hicho cha chai kwa masaa huku tukizungumza (nilikuwa ndiye
muongeaji sana) nikagundua kuwa alikuwa ni mtu mzuri sana, mtulivu na ni
mwenye kuona haya kidogo. Alinisikiliza kwa umakini kila neno
nililolazimika kulisema na hakunikatiza hata mara moja. Niliipenda njia ya
mtu huyo na nilifikiria kuwa mtu huyo ana uwezekano wa wazi wa kuwa
Mkristo mzuri. – Ni kidogo nilichokijua juu ya mtiririko wa matukio
yanayojifungua mbele ya macho yangu.
Kwanza kabisa, niliafikiana na baba yangu kuwa tufanye biashara na mtu
huyo na hata kupigia debe wazo la kusafiri naye katika misafara yangu ya
kibiashara kuvuka eneo la Kaskazini mwa Texas. Siku baada siku tutaendesha
na kujadili mambo mbali mbali yanayofungamana na imani za watu mbalil
mbali. Tukiwa njiani, kwa hakika nilikuwa nahanikiza baadhi ya vipindi vya
redio vya mambo ya kiibada nilivyokuwa navipenda sana na kuvitukuza ili
vinisaidie kufikisha ujumbe kwa huyo masikini aliyepeke yake.
Tulizungumza juu ya maana ya Mungu; maisha; lengo la kuumbwa; Mitume
na kazi zao; na jinsi Mungu anvyofunua ufunuo wake kwa binadamu. Pia
tulishiriki kujadili uzoefu na fikra za kila mtu binafsi.
Siku moja nilijua kuwa rafiki yangu, Mohammed alikuwa anataka kuhama
kutoka katika nyumba aliyokuwa akiishi na rafiki yake na alikuwa anataka

9
kukaa msikitini kwa muda fulani. Nilienda kwa baba na kumuomba
tumwalike Mohammed aje kuishi nasi katika nyumba yetu kubwa iliyopo
kijijini. Baada ya yote, anaweza kushirikiana nasi kazi na kulipia baadhi ya
gharama na atakuwepo wakati tutakapokuwa tunaenda safari zetu. Baba
alikubali na Mohammed akahamia.
Bila ya shaka nilikuwa bado ninapata nafasi ya kuwatembelea rafiki zangu
wahubiri na wachungaji waishio Texas. Mmoja wao alikuwa anaishi Texas
karibu na mpaka wa Mexico na mwingine aliishi karibu na mpaka wa
Oklahoma. Muhubiri mmoja alipendelea salaba la mbao kubwa sana ambalo
lilikuwa kubwa kuliko gari ndogo. Alikuwa anaubeba juu ya mabega yake na
kuuburuza. Kitako chake ardhini na kupita nao mtaani au barabarani huku
akihanikiza miale miwili iliyoundwa kwa umbo la msalaba. Watu
walisimamisha magari yao na kumwendea na kumuuliza kulikoni; naye
angewapa vijitabu na vijikaratasi juu ya Ukristo.
Siku moja rafiki yangu mwenye msalaba alipatwa na mshtuko wa moyo na
kulazimika aende hospitali ya Veterans ambako alikaa kwa muda mrefu.
Nilikuwa namtembelea hapo hospitalini kwa mara kadhaa kwa wiki na
nilikuwa namchukuwa Mohammed pamoja nami, nikiwa na matarajio ya
kuwa sote tutashiriki mada ya imani na dini. Rafiki yangu mwenye msalaba
hakupandishwa mori, na ilikuwa ni wazi kuwa hakutaka kujua chochote
kuhusu Uislamu. Kisha siku moja yule mtu ambaye alikuwa anashirikiana na
rafiki yangu alikuja huku akiendesha kiti chake cha magurudumu na kuingia
chumbani. Nilimwendea na kumuuliza jina lake na akasema kuwa hilo si
muhimu na nilipomuuliza ametokea wapi alisema kuwa ametokea sayari ya
Jupita. Nilifikiria kile alichokisema na kisha nilianza kustaajabu je, kama
ningekuwa katika wodi ya mshtuko wa moyo au katika wodi ya wagonjwa wa
akili ingekuwaje.
Nilijua kuwa yule mtu alikuwa ni mpweke na amefadhaika na anahitaji mtu
katika maisha yake. Kwa hiyo, nilianza kumthibitishia kuhusu Bwana.
Nilimsomea kwa sauti kitabu cha Jonah katika Agano la Kale. Na fikra
ilikuwa ni kuwa kwa hakika hatuwezi kukimbia matatizo yetu kwa kuwa siku
zote tunajua tulichokifanya na cha ziada, Mungu pia daima anajua ambacho
tumekifanya.
Padri wa Kikatoliki

10
Baada ya kushiriki mazungumzo hayo na yule mtu aliye katika kiti cha
magurudumu, mtu huyo alinitazama na kuniomba msamaha. Akaniambia
kuwa amehuzunishwa na tabia yake ya ufedhuli na kuwa yeye amepatwa na
matatizo makubwa hivi karibuni. Kisha akasema kuwa anataka kuungama
kitu mbele yangu. Nikamwambia kuwa mimi si padri wa Kikatoliki na kwa
hiyo, sitoi huduma ya kuungama dhambi. Akanijibu kuwa anajua hilo. Kwa
hakika, alisema “Mimi ni padri wa Kikatoliki.”
Nilishtushwa. Hapa nilikuwa najaribu kumuhubiria Ukristo padri. Nini
kilikuwa kinatokea hapa duniani?
Padri Wa Amerika Kusini
Yule padri akaanza kushiriki mazungumzo kwa kueleza kuwa, yeye alikuwa
mmishionari 3 wa kanisa kwa zaidi ya miaka kumi na mbili katika maeneo ya
kusini na kaskazini mwa Amerika na Mexico na hata New York Hell’s
Kitchen.’ Alipotolewa hospitalini alihitaji sehemu ya kusubiria apone nami
sikumwacha akakae na familia ya Kikatoliki, nilimueleza baba yangu kuwa
tumwalike ahamie na kuishi na sisi kijijini pamoja na Mohammed. Jambo hilo
lilikubaliwa na wote waliokuwepo, na kwa hiyo, mara moja akahamia.
Padri Lazima Ausome UISLAMU? – Ndiyo!
Katika msafara nje ya nyumba yetu, nilizungumza na padri kuhusu baadhi ya
itikadi na imani za Kiislamu na kwa mshangao alikubali na kisha
akashirikiana nami mazungumzo juu ya hilo kwa sana. Nilishtushwa
aliponiambia kuwa mapdri wa Kikatoliki kwa hakika wanausoma Uislamu na
baadhi yao wanafikia hata stashahada ya Udakitari katika somo hilo. Jambo
hili lilinipa mwangaza sana. Lakini kulikuwa bado kuna mengi yatakayojiri.
Matoleo Ya Biblia Tofauti Tofauti
Baada ya kujipanga, sote tulianza kujikusanya kuizunguka meza ya jikoni
baada ya chakula cha usiku kila usiku ili kujadili mambo ya kidini. Baba
yangu ataleta toleo lake la Biblia ya King James Version of Bible, mimi
nitaleta toleo langu la Biblia ya Revised Standard Version of the Bible, mke
wangu alikuwa na toleo lingine la Biblia (huenda ni kitu kama vile Jimmy
Swaggart’s “Good News For Modern Man.” Yule padri bila ya shaka,
alikuwa na Biblia ya Kikatoliki ambayo ina vitabu saba vya ziada kuliko
Biblia ya Kiprostanti. Kwa hiyo, tulitumia muda mwingi kuzungumzia
3
Mjumbe maalum wa kutangaza Ukristo katika maeneo yaisiyo ya Kikristo.

11
Biblia ipi ndiyo ya haki, na sahihi zaidi, kuliko tulivyokuwa tukijaribu
kumkinaisha Mohammed awe Mkristo.
Quran Ina Toleo Moja Tu – La Kiarabu – Na Bado Lipo.
Nukta moja ninayoikumbuka ni kumuuliza kuhusiana na Quran ina matoleo
mangapi ambayo yamekuwepo katika kipindi cha miaka 1400. Akaniambia
kuwa kulikuwa na Quran Moja tu. Na kuwa kamwe haijabadilishwa. Pia
akawafahamisha kuwa Quran yote imehifadhiwa na mamia kwa maelfu ya
watu, na imetawanywa duniani katika nchi mbali mbali. Baada ya karne
nyingi tangu kuteremshwa kwa Quran, mamilioni wameshaihifadhi Quran
yote kimoyo moyo na wameshawafundisha wengineo ambao nao
wameshaihifadhi kikamilifu, kuanzia jalada hadi jalada, kila herufi bila ya
kukosea. Leo hii, zaidi ya Waislamu milioni tisa wameshahifadhi Quran
nzima kuanzia jalada hadi jalada.
Jambo lililoonekana kuwa haliwezekani kwa upande wangu. Baada ya yote,
lugha zote za asili za Biblia zimekufa kabisa kabisa kwa karne nyingi na
nyaraka zenyewe zimepotea katika uasili wake kwa mamia na maelfu ya
miaka. Kwa hiyo, vipi itakuwa kitu kama hicho kiweze kulindwa kirahisi na
kusomwa kuanzia jalada hadi jalada.
Hata hivyo, siku moja yule padri alimuomba Mohammed kama ataongozana
naye na kuelekea msikitini ili aone kuna nini huko msikitini. Wakarudia
kuongelea uzoefu wao kuhusu huko msikitini nasi hatukuwa na subira ya
kungoja kumuuliza padri nini kilitokea huko msikitini na aina gani za taratibu
za kidini walizokuwa wakizifanya. Naye akasema kuwa, Waislamu kwa
hakika hawafanyi lolote. Wao huwa wanakwenda na kuswali na kuondoka.
Nikasema: “Wanaondoka?” Bila ya mazungumzo yeyote au kuimba?
Akasema hivyo ndivyo ilivyo.
Padri Aingia Uislamu!
Siku chache nyingine, zilipita na yule padri wa Kikatoliki alimuomba
Mohammed kama atamkubalia ajiunge naye tena ili waende msikitini na
jambo hilo wakalifanya. Lakini mara hii ilikuwa ni tofauti. Hawakurejea kwa
muda mrefu. Hadi ikawa kiza na tukaogopa isije ikawa kuna kitu
kilichowatokea. Mwishowe walifika na walipoingia mlangoni kwa haraka
haraka nilimtambua Mohammed, lakini ni nani huyu aliye ubavuni mwake?
Ni mtu anaevalia joho leupe na kofia nyeupe. Kwa kujiachia muda kidogo!
Alikuwa ni yule padri. Nilimwambia: “Pete? – Je, umekuwa “Mwislamu?”

12
Akasema ameshaingia Uislamu siku hiyo hiyo. PADRI AMEKUWA
MWISLAMU!! Nini kinafuata? (Utaona).
Mke wangu anatangaza Uislamu wake!
Kwa hiyo, nilienda upande wa juu kufikiria vitu vya juu kidogo na nikaanza
kuongea na mke wangu kuhusiana na kadhia nzima. Kisha naye akaniambia
kuwa yeye ataingia Uislamu, kwa kuwa ameshajua kuwa Uislamu ni dini ya
kweli.
Kwa sasa nilikuwa nimeshtushwa barabara. Nilienda upande wa chini na
kumwamsha Mohammed na kumtaka atoke nje pamoja nami ili tujadiliane.
Tulitembea na tulizungumza usiku kucha.
Ukweli Umeshafika!
Wakati alipokuwa yupo tayari kuswali swala ya Alfajiri (swala ya Asubuhi
kwa Waislamu) nilijua kuwa mwishowe ukweli umeshafika na sasa ilikuwa ni
juu yangu kufanya sehemu yangu. Nilienda nje ya nyumba ya baba yangu na
kukuta kipande cha tabaka za mbao cha zamani kikiwa chini ya Overhang na
hapo hapo niliinamisha kichwa changu chini ya ardhi nikielekea upande
wanaouelekea Waislamu katika sala zao tano za kila siku.
Niongoze! O Mungu! Niongoze!
Sasa, katika nafasi hiyo, nikiwa nimenyoosha mwili wangu katika zile tabaka
za mbao na kichwa changu kikiwa juu ya ardhi, niliomba: “O Mola. Kama
upo huko, niongoze, niongoze.”
Na kisha baada ya muda niliinua kichwa changu na nikagundua kitu. Sijaona
ndege wala Malaika wanaotokeza kutoka mbinguni wala kusikia sauti au
muziki, wala sijaona mwangaza na nuru, hapana. Ambacho nilikigundua ni
mabadiliko ndani ya nafsi yangu. Kwa sasa nilikuwa nipo macho zaidi kuliko
nilivyokuwa hapo kabla na huo ndiyo ulikuwa muda wangu wa kukomesha
uongo wowote na kufanya chochote cha kisiri siri. Huu ndiyo muda
madhubuti wa kutenda na kuwa mtu mwaminifu. Kwa sasa nimeshajua kitu
nilicholazimika kukifanya.
Kwa hiyo, nilienda upande wa juu na kuoga kwa itikadi tofauti kabisa ya
kuwa nilikuwa ninaosha madhambi ya mtu wa zamani mwenye dhambi tena

13
aliyekuwa nazo kwa miaka mingi. Na kwa sasa nimeingia katika maisha
mapya. Maisha yanayoegemea juu ya ukweli na uthibitisho.
Majira ya saa 11:00 asubuhi hiyo, nilisimama mbele ya mashahidi wawili,
mmoja wao ni padri wa zamani, ambaye alikuwa akifahamika kama padri
Peter Jacob`s na mwingine ni Mohammed Abdel Rahmani na kutangaza
‘shahada’ yangu (ushuhuda wa wazi juu ya Upweke wa Mungu na Mtume
Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake).
“Nashuhudia kuwa hakuna Mola wa kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah
Muweza, yeye peke yake hana mshirika na ninashuhudia kuwa
Muhammad ni mjumbe wake na ni mtume wake.”
Dakika chache baadaye, mke wangu alifuatia na kutoa shahada hiyo hiyo.
Lakini shahada yake ilikuwa mbele ya mashahidi watatu (mimi nikiwa ndiye
wa tatu).
Baba yangu alichelewa kidogo katika suala hilo na alisubiri miezi michache
kabla naye hajatoa shahada (ushuhuda wa mbele za watu). Lakini yeye naye,
hatimaye aliingia katika Uislamu na akaanza kusali na mimi na Waislamu
wengine katika msikiti wa mtaani.
Watoto walitolewa kutoka katika shule za Kikristo na kuingizwa shule za
Kiislamu. Na kwa sasa ikiwa imepitamiaka kumi, watoto hao
wameshahifadhi sehemu kubwa ya Quran na mafundisho ya Kiislamu.
Mwishowe mke wa baba yangu alikubali, kabla hajafariki, kuwa Yesu
haiwezekani awe mtoto wa Mungu na lazima atakuwa ni Mtume mkuba wa
Mwenyezi Mungu, na siye Mungu. Naye alifariki ndani ya miezi michache
baada ya maneno hayo akiwa na umri wa miaka 86. Allah mkubalie maneno
yake ya kiimani, aamiin.
Sasa hebu simama na ufikiri. Familia zote za watu kutoka makundi, makabila
na historia mbali mbali, wamejumuika pamoja katika ukweli ili wajifunze
namna watakavyomjua na kumwabudu Muumba na Mpaji wa ulimwengu.
Fikiria. Padri wa Kikatoliki; mchungaji wa muziki na muhubiri Injili;
mchungaji msimikwa na mjenzi wa mashule ya Kikristo; na watoto; hata
kibibi kikongwe – wote hao wameingia Uislamu!

14
Ni kwa rehema za Mungu tu ndiyo sisi sote tumeongoka na kuona ukweli
halisi wa Uislamu, kwa kuondoshwa vizibo juu ya masikio yetu na upofu juu
ya macho yetu, na hakuna tena vizibo juu ya mioyo yetu – Mungu
anatuongoza hivi sasa.
Kisa cha kushangaza – famila na marafiki kuingia Uislamu – kutokana
na mtu mmoja. Ingekuwa napaswa kusimama hapa, nina hakika kuwa
ungekubali kuwa, kwa uchache, hiki ni kisa cha kushangaza sawa? Baada ya
yote, viongozi watatu wa kidini wa madhehebu matatu tofauti tofauti wote
wanaingia imani iliyokinyume kabisa na imani zao kwa wakati huo huo
baadaye familia nzima.
Ziada? – Naam! Mwanafunzi wa seminari (shule ya kidini) ya Kibaptisti
anasoma Quran – anaukubali Uislamu. Lakini hayo sio ndiyo ya mwisho.
Kuna ya ziada! Mwaka huo huo nilipokuwa Grand Prairie, Texas (karibu na
Dallas) nilikutana na mwanafunzi wa seminari ya Kibaptisti atokeaye
Tennessee aitwaye Joe, ambaye naye aliingia Uislamu baada ya kusoma
Quran Tukufu wakati alipokuwa katika CHUO CHA SEMINARI CHA
KIBAPTISTI!
Ziada? – Naam! Padri wa Kikatoliki anaupenda Uislamu – lakini
anahitaji kazi yake! – Kuna mengine vilevile. Ninakumbuka kadhia ya padri
wa Kikatoliki katika chuo cha mjini ambaye alizungumzia mambo mazuri ya
Uislamu kwa sana kiasi ambacho nikalazimika nimuulize kwa nini hajaingia
Uislamu? Akajibu; “Nini?” Kisha nipoteze kazi yangu?” – Jina lake ni Baba
John na tunaendelea kumuomba Allah amwongoze.
Padri mwingine wa Kikatoliki anatoa shahada
Mwaka uliofuata nilikutana na padri wa zamani Mkatoliki ambaye
ameshawahi kuwa ni mmishionari kwa miaka minane barani Afrika.
Amejifunza Uislamu wakati alipokuwa huko na akaingia Uislamu. Kisha
akabadili jina lake na kuitwa Omar na akaenda Dallas Texas.
Lolote la ziada? Tena – naam! Askofu wa Kiothodoksi analiacha kanisa
na kuingia Uislamu. Miaka miwili baadaye, nikiwa San Antonio, Texas
nilielekezwa Askofu wa zamani wa kanisa la Kiothodoksi la Kirusi ambaye
amejifunza Uislamu na kutupilia mbali kazi yake na kuingia Uislamu.

15
Binti wa kiongozi Bingwa wa Kihindu (Hindu Pundit) – anaukubali
Uislamu na kusaidia Uislamu kwa maelfu ya mapesa.
Nilikutana na mwanamke mjini New York aliyetaka kutengeneza CDs zetu
kuhusiana na “Uislamu ni nini?” Baada ya kupewa ruhusa yake miaka kadhaa
iliyopita, nimesoma kuwa ameshatengeneza na kusambaza zaidi ya CDs laki
sita kwa wasio Waislamu ndani ya Marekani. Allah amlipe thawabu na ampe
nguvu katika juhudi zake, aamiin.
Mamia – Maelfu – Bado yanakuja
Tangu kuingia kwangu katika Uislamu na kuwa kasisi wa Waislamu ndani ya
nchi na dunia nzima, nimeshakabiliana na watu wengi mmoja mmoja, ambao
walikuwa ni viongozi, walimu na wanazuoni wa dini nyingine waliousoma
Uislamu na wakauingia. Wamekuja kutoka katika dini za Kihindu, Kiyahudi,
Kikatoliki, Kiprotestanti, Mashahidi wa Yehova, na Waothodoksi wa Kigiriki
na Kirusi, wakibti kutokea Misri, makanisa yasiyo na madhehebu na hata
wanasayansi ambao walikuwa wanamkana Mungu.
Mchanganyiko huo daima unaonekana ni ule ule; watu ambao kiuaminifu
wanatafuta ukweli na wanataka kuweka kando tofauti za kihisia na upendeleo
wao na kuanza kumuomba Mungu awaongoze katika maisha yao.
Kwa hiyo, hadi sasa umeshapata utangulizi wa kisa cha kuingia kwangu
Uislamu na kuwa Mwislamu. Kuna mengi katika internet kuhusu kisa hiki na
kuna picha nyingi vilevile. Tafadhali tenga muda na uniandikie email na
uturuhusu tujumuike pamoja katika kweli tupu inayoegemea katika ushahidi
ili tufahamu asili yetu, malengo yetu na makusudiyo katika maisha haya na ya
baadaye.
Je, nitoe pendekezo kwa mtafutaji wa ukweli? Chukua hatua tisa
zifuatazo ili utakase moyo.
   1. – Safisha – fikra zako, moyo wako, na nafsi – ondosha hisia zote za
      upendeleo.
   2. – Mshukuru Mungu – kwa kile ulichokuwa nacho – kila wakati kila
      siku.
   3. – Soma – tafsiri nzuri ya maana za Quran Tukufu katika lugha
      uifahamuyo vizuri.
      (www.islamtomorrow.com/downloads/noblequran.exe)

16
4. – Tafakari juu ya maana yake na uzingatie ukarimu wa Mola wako.
5. – Tafuta – kusamehewa dhambi kwa Mungu na jifunze
   kuwasamehe watu wengine.
6. – Omba – kimoyo moyo uongozwe kutoka juu.
7. – Funga – moyo wako na akili zako.
8. – Endelea – kufanya haya kwa miezi michache. Na jizoeshe kufanya
   hayo kila siku.
9. – Jiepushe – na sumu ya shetani wakati moyo wako utakapofunguliwa
   ili “kuzaliwa upya kwa moyo wako”.
Kumbuka – kujisafisha; kutoa shukrani; kusoma; kutafakari, kisha tafuta,
“na nyinyi hakika mtapata. Omba, na utapewa. Bisha hodi utafunguliwa.”
Kisha endelea na Jiepushe:
Lililobaki ni kati yako na Mungu Muweza wa Ulimwengu. Kama kweli
unampenda Mungu, Yeye tayari anajua hilo na atatushughulikia kila mmoja
wetu kulingana na mioyo yetu.
Majibu ya Maswali:
Kwa sasa kama nilivyowaahidi kuna majibu ya maswali mengi niliyoulizwa
yanayofungamana na chaguo langu la Uislamu:
1. Vipi umebadilika kutoka katika mpango mkamilifu wa uwokovu
   wa Yesu Kristo msalabani kuokoa dhambi zako?
Jibu: Swali lako linaashiria bado hujazingatia mlingano uliopo kati ya
mafundisho ya Biblia na Quran.
“Uislamu” maana yake ni kujisalimisha, kunyenyekea na kumtii Mola wako
kwa uaminifu na amani.” Yeyote anayejaribu kufanya hayo, ni Mwislamu.
“Kama mtu anaamini Mungu Muweza kuwa ni Mungu Mmoja na ni Mola
Mmoja anayetaka kuyafanya maisha yao ili kumtumikia Yeye na kutii amri
zake, mtu huyo atakuwa katika njia sahihi na watu hao watakuwa
“wameokolewa.” Kulingana na Rehema za Mungu. Hakuna wa kuchukua
dhambi za wengine na waovu lazima wasimame na kushitakiwa kwa vile
walilivyovitenda. Itakuwa ni juu ya Mola Muweza kuwasamehe au
kuwaadhibu kwa mujibu wa Hukumu yake katika siku hiyo.

17
Kwa mujibu wa mabaki ya tafsiri ya Biblia juu ya Yesu, Mungu amrehemu,
hajahubiri habari za uwokovu kwa kumwabudu yeye. Jambo hili
limeongezwa baada yake na Saul (ambaye baadaye akawa Paulo). Tunapata
maelezo ya wazi kabisa yanayoashiria uwokovu utakaokuja kupitia kumkiri
Mungu Muweza kuwa ni Mungu mmoja na kumwabudu kwa moyo wote,
akili na nguvu zote tu! Yesu, Amani iwe juu yake, amefundisha wafuasi wake
waabudu hivi “Mungu wangu Ndiye Mungu Wenu, Mola wangu Ndiye Mola
wenu.”
Kwa mara nyingine, kwa mujibu wa tafsiri ya Biblia ya Kingereza iliyobaki,
tunamuona mtu aangukwaye msalabani akilia kwa kusihi sana, “Eloi, Eloi,
lama sabakhthani? (Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?)”
Sentensi hii juu ya msalaba kwa uwazi kabisa inaonyesha kuwa yule mtu
aliye msalabani hajafurahishwa na hali hiyo na wala haichukulii hali hiyo
kuwa ni haki au uadilifu. Kwa hiyo, mtu lazima ahitimishe jambo hilo kuwa
lilikuwa ni kitu ambacho hakikutakiwa na Yesu wala kukubaliwa au
vinginevyo ni mtu mwingine aliyekuwa msalabani katika nafasi yake. Kwa
njia yeyote ile utakavyolitazama jambo hilo, mtu aliyekuwa msalabani
hakukubali jambo hilo kuwa ni mpango wa uwokovu.
Quran kwa ukamilifu inapingana na mafundisho hayo, na Waislamu
wanamwabudu Mungu na Bwana yule yule wa Yesu, Musa, Ibrahimu na
Adamu, amani iwe juu yao. Quran katika sehemu nyingi inaeleza, hakuna mtu
atakayebebeshwa kazi za dhambi za Mwingine, wala hakuna mtu atakaye
beba mzigo wa mwingine. Sote tutakuwa na mambo yetu wenyewe siku hiyo.
Na ninamuomba Allah awerehemu na awasamehe wote waliomwamini,
aamiin.
Ninajiona kuwa sijaacha mafundisho ya Yesu Kristo, (amani iwe juu yake).
Kinyume chake, nahisi kuwa nipo karibu na Yesu, amani iwe juu yake, na
ninatarajia kurejea kwake hapa duniani kuliko nilivyokuwa zamani. Kwa sasa
ninamwabudu Mungu yule yule anayemwabudu na ninamtumikia Bwana yule
yule anayemtumikia, katika njia ile ile aifanyao. Yesu alimuomba Mungu
Muweza, na alifundisha wafuasi wake wafanye hayo hayo. Mimi kwa wepesi
kabisa ninafanya kile alichokiamrisha kwa uwezo wangu na ninamuomba
Mungu Muweza anikubalie matendo yangu.
2. “Je, unadhani kuwa ni kweli “umeokolewa” na kwa hakika
   umezaliwa upya?”

18
Jibu: Wabatisti wanamsemo usemao: “Aliyeokolewa, huokolewa daima”
nilimuuliza mmoja wao kuhusu hilo na akakubali hilo kuwa ni kweli. Kisha
nikataja kuwa kuna mara moja nilibatizwa (nikiwa na umri miaka kama kumi
hivi) lakini kwa sasa nimeshakuwa Mwislamu. Pia niliokolewa na kubatizwa
nikiwa na miaka kumi na mbili. Nilikubali maneno ya Yesu ya kuwa yeye
ndiye njia, nuru na ukweli na hakuna mtu atakayekwenda kwa Baba ispokuwa
kwa njia ya Yesu. Niliyafahamu maneno hayo kuwa yanamaanisha kuwa
lazima nimfuate Yesu na mafundisho yake. Kwa hiyo, niliisoma Biblia mimi
mwenyewe na sikuwaruhusu watu wengine waniambie jambo la kufikiria
kuhusu nilichokuwa nakisoma.
Biblia inaeleza kuwa Yesu aliomba aokolewe nafsi yake katika bustani ya
Gethsemane kwa njia hii. “Baba yangu ikiwezekana kikombe hiki
kiniepuke; walikini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.”
Dua hili lilirudiwa na Yesu, amani iwe juu yake, mara nyingi na
imeonyeshwa katika Injili nyingi. Ndiyo, kwa mujibu wa fikra za Kibiblia,
Hilo Kombe halikumwepuka na dua zake hazikukubaliwa. Uislamu
unafundisha kuwa dua zake zilikubaliwa naye hakukaa katika matendo ya
ukatili na wala hajafa msalabani, lakini alichukuliwa akiwa hai na yupo
pamoja na Mungu Muweza kwa hivi sasa na yupo tayari kurejea katika siku
za Mwishoni ili kuleta ushindi kwa waumini.
Jambo la kuongezea, tunamkuta Yesu, amani iwe juu yake, anawafundisha
wafuasi wake waombe kama hivi; “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako
litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama
huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi
tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na
yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata
milele.] Amin.” Kila Mwislamu niliyewahi kukutana naye anakubali kila
neno la dua hii ila tamko la kumwita “Allah” “Baba yetu.” Waislamu
wanchukulia kuwa ni vizuri kumwita Mungu Muweza kwa majina yake,
ambayo tunayoyachukulia kuwa ni “matukufu.”
3- “Familia yako iliitikia vipi kusilimu kwako?”
Jibu: Jambo hilo daima ni gumu kwa familia kukaa sawa na mara nyingi
linachukuwa muda mrefu. Familia yangu haikuwa na pingamizi. Ingawa mke
wangu na watoto wangu waliingia Uislamu na hatimaye baba yangu

19
akatangaza kuwa Uislamu ndiyo njia ya uwokovu kwake, mama yangu mzazi
na watu wengine katika familia waliendelea kukasirishwa na kuingia kwetu
katika Uislamu hapo mwanzoni. Mwishoni mambo yakawa ya kawaida na
tuliishi kwa ukaribu, ingawa wao bado wanajihusisha na Ukristo.
Allah anaahidi kuwatia majaribuni wale wote wanaotangaza imani yao juu
yake, kwa kuwapa aina nyingi za mambo magumu magumu, na familia ni
moja ya mambo hayo yaliyotajwa kuwa ni jaribio ndani ya Quran.
Nanawaombea Allah awaongoze wafuate kitu kilicho bora kabisa duniani na
Ahera. Lakini juu ya Allah, kama anawataka wawe katika utiifu kwake
(Uislamu maana yake ni, utiifu kwa Allah) au kama hataki kuwa hivyo.
4- “Vipi kuhusu usharika wako? Wamesema nini?
Jibu: Kamwe sijawahi kuwa na kanisa langu mwenyewe. Nilikuwa ni
mchungaji wa muziki kanisa la Mungu (Anderson, Indiana branch) mjini
Texas na nilikuwa natoa mahubiri yangu kwa wafanyabiashara na kwa
makutano yasiyo ya kawaida. Wote wanaonijua kwa sehemu kubwa hawana
kizuizi na baadhi yao wameshaingia katika Uislamu, lakini kuna wachache
ambao walihisi kuchanganyikiwa sana na wakanitukana, kwa “kumkana
Yesu, amani iwe juu yake.” Bila kujali kile nilichojaribu kukisema au
kukitenda, hawa watu maalumu walio wachache hawasikilizi wala hawataki
chochote kinachohusu Uislamu.
5- Je, umeshapata matatizo mengi kwa kubadili dini?
Jibu: Bila ya shaka, kila mtu atakaye kuuzingatia Uislamu siku hizi, kama
ilivyokuwa mida iliyopita, lazima atambue kuwa kutakuwa na matatizo ya
majaribio maalumu katika njia yake hiyo. Wafuasi wa Yesu, amani iwe juu
yake, walikosolewa na kuteswa sana hadi walifikia kuuliwa (soma kile
alichokisema Paulo kwamba alikuwa anakifanya kwa wanafunzi wa Yesu
ndani ya Biblia; kitabu cha Matendo ya Mitume). Wote waliomfuata
Muhammad, amani iwe juu yake, waliteswa mikononi mwa watu wa
makabila yao wenyewe, ndiyo kuwa, walikuwa wameshaazimia kumwabudu
Mungu Muweza peke yake, bila ya mshirika na kutii matakwa yake.
Tatizo kubwa kwa wasiokuwa Waislamu ni, ukosefu wao wa elimu na
ufahamu juu ya nini ndiyo Uislamu wa kweli na akina nani wanaozingatiwa

20
kuwa ndiyo Waislamu. Ninawaombea na kumuomba Allah awasamehe
Waislamu kwa kutuonyesha picha nzuri kwa kila mtu.
6- “Nani ndiye muhusika mkuu katika kukubadilisha dini?”
Jibu: Nikiwa kama Waislamu wote, tunaamini kuwa ni Allah pekee
aongozaye watu na yeyote amwongozaye hatopotoka na yeyote amwachaye
apotee hakuna atakayeweza kumwongoza. Kwa hiyo, inamaanisha kuwa
hatuamini kuwa kuna awezaye kumbadili dini mtu mwingine.
Pia, tunakubali kuwa watoto wote wanazaliwa wakiwa na maumbile ya
kumtii Mungu Muweza na kwa hiyo, hilo linamaanisha kuwa wao ni
Waislamu. Watoto wakifa wataingia Peponi kwa kuwa hawataulizwa kile
wasichokifahamu.
7 – Je, hujawahi kufikiria juu ya kuwa Mkristo tena?
Jibu: “Mkristo” inaashiria mfuasi wa Kikristo. Wakati Yesu, amani iwe juu
yake, atakaporudi duniani siku za Mwisho, Waislamu wote watalazimika
kumfuata. Lakini hatojiita “Mkristo” kama atakavyokuwa. Yeye au wafuasi
wake, kamwe, hawajajiita “Wakristo.” Biblia inatueleza kuwa wao kamwe
hawajapatapo kuitwa “Wakristo” hadi pale Paulo alipohubiri ujumbe wake
mjini Antokia.
8- “Je, jambo hilo halikukuudhi kwa kuacha njia ya amani, uadilifu na
upendo na kuingia dini ya chuki, fujo na ukandamizaji dhidi ya
wanawake na watu wengine?”
Jibu: Mitume wote, amani iwe juu yao, waliwaita watu waje wamwabudu
Mungu Muweza ambaye ni Mungu Mmoja na ni Bwana Mmoja. Kwa hiyo,
wote wasiotaka kumtii Mungu Muweza watawapinga hao Mitume na
kuwatendea uadui, hadi kuwaua, kama alivyofanya Paulo alipokuwa
Mfarisayo. Mitume, rehema na amani ziwe juu yao, waliwatia nguvu wafuasi
wao waishi kwa amani na kuishi na watu kwa wema na mapenzi ya pekee
kwa mtindo wa hali ya juu wa kihisia za kibinadamu zinazoweza kutendwa
kwa watu wengine.
Naam, wakati huo huo waumini wanalazimika kujikinga nafsi zao, familia
zao na dini yao, ili isije kuwa wale wasioamini wakaondosha imani kutoka

21
katika kila eneo la ardhi. Uislamu, kama Ukristo unahubiri ujumbe wa amani
na kuvumiliana – kwa kina. Lakini linapokuwa jambo hilo haliwezekani bila
ya maafikiano ya moja kwa moja na mtu kupoteza njia ya maisha na mfumo
wa imani, hapo ndipo kunapokuwa hakuna hiari ispokuwa kutumbukia katika
mapigano ya kisilaha ya wazi dhidi ya wale wote wanaopigana dhidi ya
waumini.
Yesu aliwaita wafuasi wake wauze makoti yao na wanunue mapanga. Naye
akafafanua kuwa Yeye hakuja kwa amani bali kwa ncha ya upanga. Yeye na
wafuasi wake walitumbukia katika pigano kuu na maadui zao, Wafarisayo
wakati fulani pale mtumishi wa makasisi alipolazimika kukatwa sikio lake
kwa upanga. Kisha Yesu akawaambia waweke chini mapanga yao. Jambo hili
limetajwa katika Biblia.
Neno “upanga” limetajwa zaidi ya mara mia mbili katika Biblia- lakini hata
hivyo, lugha ya Kiarabu ina zaidi ya dazeni moja ya maneno yenye maana ya
upanga, lakini hakuna hata moja miongoni mwa maneno hayo liliopo katika
sehemu yeyote ile ndani ya Quran.
Mapigano yameamrishwa na Quran, chini ya masharti maalumu na yenye
kiwango maalumu tu, na hakuna lolote zaidi ya kile ambacho leo hii
tunachoweza kukiita “vita vya ugaidi.” Kupambana dhidi ya matendo yote
makundi ya uchokozi, ukandamizaji, utesaji na ugaidi ni jambo la lazima juu
ya waumini wote. Lakini bila ya shaka yana mipaka maalumu na wanawake,
watoto, wazee na yeyote asieshiriki hawauliwi au kuumizwa katika matukio
hayo. Matendo ya kuwafanyia wafungwa wa kivita hayatakiwi yawe ya
kuabisha au mateso ya aina yeyote ile. Hata maiti za maadui zinatakiwa
zizikwe kwa heshima na wema.
  Mungu akuongoze katika safari yako ya kuelekea ukweli kamili. Aamiin.
Na akufungue moyo wako na fikra zako katika uhakika wa ulimwengu huu na
                    lengo la maisha haya. Aamiin.
Amani iwe juu yako, pia na uwongofu kutoka kwa Mungu Muweza, ambaye
ni Mmoja Mwenye Nguvu, Muumba na Mpaji wa kila kitu kilichopo.
Rafiki yako,
Yusuf Estes

22
    6317 Edsall Rd.
 Alexandria, VA22312
United States of Amerca
SHEIKYUSUF@AOL.COM Tel: 001-703-354-5224
http://www.islamtomorrow.com/yusf.htm
http://thetruereligion.org/modules/xfsection/

23
2 – ABDULLAH M. AL-FARUQUE ALIYEKUWA AKIIITWA
KENETH L. JENKINS, MCHUNGAJI NA MZEE WA KANISA
LA PENTECOSTAL. (USA)
ﺓﺭﻮﺻ CHRISTIAN
PREACHER
Nikiwa ni mchungaji na ni mzee wa kanisa la Kristo, hapo zamani, ilikuwa ni
wajibu wangu kuwaelimisha wale wote wanaoendelea kutembea kizani.
Baada ya kuingia Uislamu nilihisi haja kubwa mno ya kuwasaidia wale wote
wasiobarikiwa na kupata nuru ya Kiislamu.
Namshukuru Mungu Muweza, Allah, anihurumie, anijaalie niujue uzuri wa
Uislamu kama ulivyofundishwa na Mtume Muhammad na maswahaba 4 zake
waongofu. Ni kwa rehema za Allah tu, ya kwamba sisi tunapokea uongofu wa
kweli kweli na uwezo wa kufuata njia iliyonyooka, inayoongoza katika
mafanikio katika maisha haya na ya kesho ahera.
Mungu asifiwe kwa wema niliofanyiwa na sheikhi “Abdallah bin Abdul-
Azeez bin Baz” wa Falme ya Saudi Arabia juu ya kuingia kwangu Uislamu.
Naishi kwa matumaini na nitapitia juu ya elimu yote iliyopatikana kutokana
na kila kikao nlichokaa naye. Kuna wengine wengi walionisaidia kwa kunipa
nguvu na kunielimisha. Ni jambo la kutosha kusema kuwa namshukuru
Mungu Muweza, Allah, kwa madada na makaka wote walioruhusiwa na
Mungu kushiriki katika ukuaji na maendeleo yangu nikiwa Mwislamu.
Naiombea kazi hii fupi, iwe ni kwa faida ya wote. Natarajia Wakristo
watagundua kuwa bado kuna matarajio licha ya masharti ya ukaidi
yanayoshawishi makundi mengi ya Wakristo. Ufumbuzi wa matatizo ya
Wakristo haupatikani kwa Wakristo wenyewe, kwani wao, kwa namna
4
Swahaba ni mfuasi wa Mtume Muhammad (S.A.W) aliyekuwepo zama za Mtume.

24
nyingi, ndiyo mzizi wa matatizo yao wenyewe. Kiasi ambacho, Uislamu
umekuwa ndiyo suluhisho la matatizo yaliyosababishwa na ulimwengu wa
Kikristo, pia kwa matatizo yanayoukabili ulimwengu wote wa kidini. Allah
atuongoze na atulipe kwa mujibu wa matendo yetu mema na nia zetu.
Nikiwa kijana mdogo, nilimuogopa sana Mungu. Kwa kuwa kwa kiasi fulani
nililelewa na bibi yangu aliyekuwa ni Mpentekoste mwenye msimamo mkali,
na kanisa lilikuwa ni sehemu ya lazima katika maisha yangu tangu nikiwa
mdogo. Nilipofikia miaka sita, nilijua vizuri kabisa faida inayoningojea huko
Peponi kama nitakuwa kijana mwema, na adhabu ya Moto inayowangojea
watoto watukutu. Nilifundishwa na bibi yangu kuwa uongo wa aina yeyote
unaangamiza na unapeleka Motoni, sehemu ambayo waovu wataunguzwa
milele na milele.
Mama yangu alikuwa anafanya kazi mara mbili na huku akiendelea
kunikumbusha juu ya mafundisho aliyonipa kutokea kwa mama yake. Kila
Jumapili tulienda kanisani huku tukivalia nguo nzuri nzuri kabisa. Babu
yangu alikuwa ndiye tegemeo letu katika masuala ya usafiri. Muda wa kukaa
kanisani ulidumu, kama nilivyokuwa nikiuona, kama kwa masaa machache
tu. Tulikuwa tunafika mida ya saa tano asubuhi na wakati mwingine, tulikuwa
hatuondoki hadi saa tisa jioni. Babu yetu hakuwa mwendaji wa kanisani,
lakini alilitazama jambo hilo kuwa “familia yangu imelifanya liwe hivyo”
kwa kila Jumapili. Mwishowe babu alipatwa na ugonjwa wa kupooza na
kumfanya, kwa kiasi fulani, awe amepooza, na matokeo yake, tukawa
hatuwezi kuhudhuria kanisani kama kawaida. Kipindi hicho ilikuwa ni moja
ya hatua za maana sana katika maisha yangu.
Kujitolea kwa dhati.
Nilifarijika kiakili, kwa kule kutoweza tena kwenda kanisani, lakini nilihisi
nasukumwa niende mwenyewe kwa muda huo na baadaye. Katika umri wa
miaka 16 nilianza kuhudhuria kanisani kwa rafiki yangu ambaye baba yake
alikuwa ni mchungaji. Kikanisa chenyewe, kilikuwa ni jengo dogo la stoo ya
mbele ya nyumba, kikiwa na washiriki ambao ni, familia ya rafiki yangu,
mimi, na wanafunzi wengine wachache tu. Jambo hili liliendelea kwa miezi
michache tu kabla ya kufungwa kwa kanisa hilo. Baada ya kumaliza masomo
ya sekondari na kuingia chuo kikuu nilifufua matendo yangu ya kidini na
nikawa ni mwenye kujitumbukiza kikamilifu katika mafundisho ya
Kipentekoste. “Nilibatizwa na kujazwa roho mtakatifu.” Ikiwa ni kama
uzoefu niliouita. Nikiwa mwanafunzi wa chuo, kwa haraka haraka nikawa

25
fahari ya kanisa. Kila mtu alikuwa na matarajio makubwa juu yangu, na
nilikuwa ninafuraha kwa mara nyingine tena kuwa hivyo, “katika njia ya
kuelekea uwokovu.”
Nilihudhuria kanisani kila mara ilipofunguliwa milango yake. Nilijifunza
Biblia kwa masiku na mawiki, katika kipindi hicho. Nilihudhuria mihadhara
iliyotolewa na wanazuoni wa Kikristo wa zama zangu, na nikajulikana na
kualikwa katika uchungaji nikiwa na miaka ishirini. nilianza kuhubiri na
kuwa mashuhuri sana, upesi upesi. Nilikuwa naamini na kung’ang’ania
kikamilifu kuwa hakuna atakayepata uwokovu ila awe katika kundi la kanisa
langu. Nami kwa waziwazi nilimlaumu kila mtu ambaye hakumjua Mungu
kwa njia niliyomjua mimi. Nilifundishwa kuwa Yesu Kristo (amani iwe juu
yake) na Mungu Muweza walikuwa ni kitu kimoja. Nilifundishwa kuwa
kanisa letu haliamini utatu lakini Yesu (amani iwe juu yake) kwa hakika
ndiye aliyekuwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Mimi mwenyewe
nilijaribu kutaka kuelewa jambo hilo, hivyo, nililazimika kukiri kuwa jambo
hilo haliingii akilini mwangu (halifahamiki). Niliheshimu nguo takatifu za
wanawake na tabia njema ya wanaume. Nilifurahia kuitekeleza imani, pale
ambako wanawake walitakiwa wavae maguo yanayowafunika gubi gubi,
wasitie rangi nyuso zao kwa vipodozi, na wawe mabalozi wa kweli wa Kristo.
Nilikinaishwa nyuma ya pazia ya mashaka kuwa hatimaye nimepata njia ya
kweli ya kuingia katika furaha ya kweli. Nilikuwa nabishana na yeyote wa
kutoka kanisa lolote na imani yeyote na nilikuwa nawanyamazisha kabisa
kabisa kwa elimu yangu ya Biblia. Nimehifadhi mamia ya vifungu vya Biblia,
na hilo lilikuwa ndilo nembo ya mahubiri yangu. Naam, hata hivyo, nilihisi
kuwa kwa hakika nipo katika njia iliyosahihi, na sehemu yangu nyingine
ilikuwa bado inatafuta. Nilihisi kuwa kulikuwa na ukweli wa hali ya juu
ambao unatakiwa ufikiwe.
Nilipokuwa peke yangu nilikuwa natafakari na kumuomba Mungu aniongoze
katika dini sahihi na anisamehe ikiwa kile nilichokuwa nakitenda kilikuwa ni
makosa. Kamwe nilikuwa sijawahi kuwa na mawasiliano na Waislamu. Watu
pekee wanaodai kuwa Uislamu ndiyo dini yao walikuwa ni wafuasi wa Elijah
Muhammad, ambao walikuwa wakizingatiwa na watu wengi kuwa ni
“Waislamu Weusi” au “The Lost-Found Nation.” Na ilikuwa katika kipindi
hiki mwishoni mwa miaka ya sabini pale mchungaji Louis Farrakhani kwa
hakika, alikuwa vizuri katika kukijenga upya kile kilichojulikana kama ni
“Taifa la Kiislamu” nilienda kumsikiliza mchungaji Farrakhani alipokuwa
akizungumza katika mwaliko wa wafanyakazi wa ushirika na nikakata shauri

26
kuwa jambo hilo limekuwa ni uzoefu unaoweza kubadili maisha yangu kwa
mtindo wa kisanaa. Kamwe maishani mwangu sijapatapo kumsikia mtu
mweusi akiongea kwa njia aliyoongea. Nami kwa haraka haraka nilitaka
kuandaa nikutane naye ili nijaribu kumbadili na aingie dini yangu. Nilifurahia
kuhubiri Injili, nikitaraji kuzipata nyoyo zilizopotea ili niziokoe ziepukane na
Moto wa Jehannamu- bila kujali watu hao ni akina nani.
Baada ya kumaliza chuo kikuu nilianza kufanya kazi kamili. Nilifikia kilele
cha uchungaji wangu, huku wafuasi wa Elijah Muhammad wakiwa
wanaonekana sana, na niliziheshimu juhudi zao za kujaribu kuiondoa jamii ya
watu weusi waepukane na maovu ambayo yalikuwa yakiwaharibu. Nilianza
kuwaunga mkono, akilini, kwa kununua maandiko yao na hata kukutana nao
kwa mazungumzo. Nilihudhuria mazungumzo na masomo yao ili nijue nini
hasa walichokuwa wanakiamini. Kwa namna niliyokuwa nawajua, wengi wao
walikuwa waaminifu, lakini sikuweza kununua (kukubali) wazo la kuwa
Mungu, ni mtu mweusi. Nilipinga utuimiaji wao wa Biblia kuunga mkono
upande wao katika mambo maalumu. Hiki kilikuwa ndicho kitabu
nilichokijua vizuri sana, na nilisumbuka sana kwa kile nilichokifikiria kuwa
ni kufahamu vibaya kwao, na upotoshaji wao wa kitabu hicho. Nilienda shule
ya Biblia ya mtaani na nikawa na elimu kubwa katika nyanja mbali mbali za
masomo ya Biblia.
Baada ya takriban miaka sita nilienda Texas na nikawa nashiriki katika
makanisa mawili. La kwanza lilikuwa linaongozwa na mchungaji kijana
ambaye alikuwa hana uzoefu wala elimu ya kutosha. Elimu yangu ya
maandiko ya Kikristo kwa muda huo ilikuwa imeendelea kwa kitu kisicho cha
kawaida. Nilijawa na mafundisho ya Kibiblia. Nikaanza kutazama kwa kina
ndani ya maandiko na nikatambua kuwa nilikuwa ninajua zaidi kuliko
kiongozi aliyekuwepo. Kwa kuonyesha heshima, nililiacha na kujiunga na
kanisa lingine katika mji mwingine ambako nilihisi kuwa nitajifunza zaidi.
Mchungaji wa kanisa hili la kipekee alikuwa ni mwanazuoni sana. Alikuwa ni
mwalimu wa daraja la juu lakini alikuwa na baadhi ya ya fikra ambazo
hazikuwa za kawaida kwa umoja wa kanisani kwetu. Yeye alikuwa na
mitazamo ya kiliberali lakini bado nilikuwa nafurahia mafundisho yake.
Punde tu nikajifunza somo la thamani sana juu ya maisha yangu ya Ukristo,
ambalo lilikuwa ni “Kila king’acho si dhahabu” kinyume na umbile lake la
nje, kulikuwa na uovu uliochukua nafasi ambao kamwe sijaufikiria kuwa
unawezekana kuwepo kanisani. Uovu huo ulinisababishia nitafakari kwa kina,
na kuanza kusaili mafundisho ambayo nilijizatiti nayo kwa sana.

27
Karibu Katika Ulimwengu Wa Kweli Wa Kanisa.
Punde tu niligundua kuwa kulikuwa na wivu mkubwa ulioenea katika
makasisi watumishi wa Bwana. Vitu vimebadilika kutoka vile nilivyovizoea.
Wanawake walikuwa wanavaa nguo ambazo nilidhani kuwa ni za kuaibisha.
Watu walivaa ili kuvutia, na mara nyingi watu wa jinsia nyingine.
Nimegundua kuwa pesa na uchoyo vinacheza pati kubwa katika huduma za
kazi za kanisani. Kulikuwa na makanisa madogo madogo mengi yakisuasua,
na wao walituita tuitishe mikutano na kuwasaidia kuwachangia pesa.
Niliambiwa kuwa kama kanisa halina idadi maalumu ya wanachama,
nisipoteze muda wangu kuhubiri katika kanisa hilo kwa sababu sitopata faida
ya mali ya kutosha. Kisha nami nilieleza kuwa mimi sipo katika kanisa hilo
kwa ajili ya pesa na kwa hiyo, ningehubiri hata kama kungekuwa na mtu
mmoja tu… na ningefanya hivyo bure! Jambo hilo lilisababisha
mkanganyiko. Nilianza kuwahoji wale wote niliowadhania kuwa ni wenye
busara, ili nijue kama wameingia katika ulaghai. Nikagundua kuwa pesa,
nguvu na madaraka vilikuwa ni vitu muhimu sana kwao kuliko kufundisha
ukweli juu ya Biblia. Nikiwa mwanafunzi wa Biblia nilijua kwa ukamilifu
kuwa kulikuwa na makosa, kupingana na uzushi. Nilidhani kuwa lazima watu
wawekwe wazi kuelekea ukweli kuhusu Biblia. Wazo hili la kuwawekea watu
wazi mtazamo huo wa Kibiblia lilikuwa ni wazo ninalolidhania kuwa ndilo
linaloungwa mkono na shetani. Lakini kwa uwazi, nilianza kuwauliza walimu
zangu maswali mengi wakati wa darasa za Biblia, maswali ambayo hakuna
hata mmoja wao aliyeweza kuyajibu. Hakuna hata mmoja aliyeweza
kufafanua vipi Yesu anafanywa kuwa ni Mungu, Mwana na Roho Mtakatifu
aliyefinyangwa pamoja na kuwa mmoja na bado si sehemu ya utatu.
Mwishowe, wahubiri kadhaa walilazimika kukiri kuwa wao pia
hawajafahamu jambo hilo lakini tulitakiwa kuamini tu kirahisi rahisi.
Kesi za uzinzi na uasherati zilipita bila ya kutolewa adhabu. Baadhi ya
wahubiri walitawaliwa na madawa ya kulevya na wameshaharibu maisha yao
na ya familia zao. Viongozi wa baadhi ya makanisa waligundulika kuwa ni
mashoga. Kulikuwa na wachungaji waovu watendao uzinzi na mabinti
wadogo wadogo wa makanisa mengine. Yote hayo yalihusishwa na
kushindwa kupata majibu ya kile nilichokifikiria kuwa ni maswali magumu
yaliyotosha kunifanya nitafute mabadiliko. Mabadiliko hayo yalikuja wakati
nilipokubali kufanya kazi nchini Saudi Arabia.

28
Mwanzo Mpya
Haikuchukua muda mrefu baada ya kuwasili Saudi Arabia nikaona
mabadiliko ya haraka katika mfumo wa maisha ya Waislamu. Walikuwa
wanatofautiana na wafuasi wa Elijah Muhammad na mchungaji Louios
Farrakhan kwa upande wa kuwa wote walikuwa ni wazalendo, rangi moja na
lugha moja. Nami, kwa haraka haraka nilieleza shauku yangu ya kusoma zaidi
kuhusu dini hii ya kipekee yenye kushangaza. Nilishangazwa na maisha ya
Mtume Muhammad na nilitaka kuyafahamu zaidi. Niliazima vitabu kutoka
kwa mmoja wa jamaa aliyekuwa mchangamfu katika kuwalingania watu
waingie Uislamu. Nilipewa vitabu vyote nilivyokuwa navitaka. Nilikisoma
kila kitabu. Kisha nikapewa Quran Tukufu na nikaisoma yote yote kwa mara
kadhaa katika kipindi cha miezi minne. Kilichonivutia zaidi ni kuwa, wale
jamaa hawakuwa ni wenye kunigandamiza kwa elimu zao. Kama ndugu
yeyote hakujua jibu la swali aliloulizwa, aliniambia kwa wepesi kabisa, kuwa
hawezi kulijibu na ataliangalia kwa mtu anayeliweza. Na siku inayofuata
daima ataniletea jibu. Nikaona jinsi ya unyenyekevu ulivyofanya kazi kubwa
katika maisha ya watu hao wa ajabu wa mashariki ya kati.
Nilishangazwa kuwaona wanawake wakijifunika kuanzia nyuso zao hadi
miguuni. Sijaona dini yeyote ya makasisi ikiwa hivyo. Hakuna mtu
aliyeshindana kwa ajili ya kupata cheo cha kidini. Yote hayo yalikuwa ni
mazuri ajabu, lakini vipi nitaziendesha fikra za kuacha mafundisho ambayo
nimeshayafuata tangu nikiwa mdogo? Je, kuna nini kuhusiana na Biblia?
Nilijuwa kuwa kuna baadhi ya ukweli ndani yake hata hivyo,
imeshabadilishwa na kurejewa kwa mara nyingi. Kisha nilipewa mkanda wa
video wa mahojiano kati ya sheikh Ahmadi Deedat na Reverend Jimmy
Swaggart. Baada ya kutazama mjadala huo kwa haraka haraka nikawa
Mwislamu.
Unaweza kusikiliza majadiliano hayo katika website
   sitehtt:// www.islam.org/audiyo/ra622_4.ram
ﺓﺭﻮﺻ Ahmad
Deedat

29
Unaweza kuvishusha vitabu vya
  Shaykh Ahmadi Deedat
    Kupitia website hizi:
  www.ahmed-deedat.co.za
   au www.aljame3.com
Nami kirasmi nilitangaza kuukubali Uislamu. Na ilikuwa hapo ndipo
nilipopewa ushauri wa mdomo juu ya namna ya kujiandaa kwa safari ndefu
huko mbele. Ilikuwa ni mazazi ya kweli kutoka kizani na kuingia katika nuru.
Nilistaajabu, kivipi, wenzangu wa kutoka kanisani wangenifikiria
watakaposikia kuwa nimeingia Uislamu. Haikuchukuwa muda mrefu kabla
sijagundua. Nilirudi USA kwa ajili ya likizo na nilikosolewa vikali mno kwa
“ukosefu wangu wa imani.” Nilibandikwa majina mengi – kuanzia muhaini
hadi mpotovu. Watu waliambiwa na viongozi wa kanisa hata wasinikumbuke
wakati wa sala. Hiyo ilikuwa ni kama ugeni, inavyoonekana kwani mwishoni
sikuudhika. Nilikuwa na furaha sana kwa kuwa Mungu Muweza, Allah,
amenichagua na kuniongoza katika haki ambayo hakuna kitu kingine cha
kukijali.
Kitu pekee, ninachohitaji kwa sasa ni kuwa Mwislamu niliyejitolea kwa dhati
kama nilivyokuwa Mkristo. Hili, bila ya shaka, linamaanisha kusoma.
Nilitambua kuwa mtu anaweza kukua kielimu kama atakavyo ndani ya
Uislamu. Hakuna ukiritimba wa elimu – na elimu ni bure kwa kila atakaye
kujinufaisha kwa nafasi ya kusoma. Nilipewa seti ya Saheeh Muslim kama
zawadi kutoka kwa mwalimu wangu wa Quran. Na ilikuwa ni hapo ndipo
nilipogundua kuwa kuna haja ya kujifunza kuhusu maisha, maneno na
matendo ya Mtume Muhammad. Nilisoma na kijifunza hadithi nyingi
zilizokuwepo katika Kingereza kwa kadiri ilivyowezekana. Nilitambua kuwa
elimu yangu ya Biblia ilikuwa ni rasilimali ambayo inafaa zaidi kwa sasa
katika kushughulika na wale wenye historia ya kuwa Wakristo. Kwangu
maisha yalikuwa na maana mpya kabisa. Moja ya mabadiliko ya kimtazamo
ya maana sana ni matokeo ya kujua kuwa maisha haya kwa hakika yatumiwe
kwa kujiandaa na Ahera. Pia, ilikuwa ni uzoefu mpya kujua kuwa tunalipwa
hata kwa nia zetu. Kama umenuia kutenda jema, utalipwa. Hiyo ilikuwa ni
tofauti kabisa na kanisani. Mtazamo ulikuwa ni “njia ya Motoni imepambiwa
nia nzuri nzuri.” Kulikuwa hakuna njia ya kushinda. Kama umefanya dhambi,
ulitakiwa uungame kwa mchungaji, na hasa hasa kama dhambi yenyewe ni
kubwa, kama vile uzinzi. Ulihukumiwa moja kwa moja kwa matendo yako.

30
Wakati Uliopo na Mustakabala
Baada ya kufanya mahojiano na gazeti la Madinah niliulizwa kuhusu kazi
zangu za sasa na mipango yangu ya baadaye. Kwa sasa, lengo langu ni
kusoma Kiarabu, na kuendelea kujifunza ili kupata elimu kubwa kuhusu
Uislamu. Kwa sasa nimejizatiti katika nyanja ya da’wah na ninawaita, kwa
mahubiri wasiokuwa Waislamu ambao wamekuja kutokea Ukristo. Kama
Allah Muweza, ataniacha hai, natarajia kuandika zaidi kuhusu somo la
mlinganisho wa dini.
Ni wajibu wa Mwislamu ulimwenguni kote afanye kazi ya kusambaza elimu
ya Kiislamu. Kama vile nilivyotumia muda mwingi nikiwa kama mwalimu
wa Biblia, nahisi hisia za pekee za wajibu wa kuwaelimisha watu kuhusu
makosa, mikanganyiko na visa vya kughushi vya kitabu kinachoaminiwa na
mamilioni ya watu. Moja ya furaha kuu ni kujua kuwa silazimiki kujidhatiti
katika mabishano na Wakristo, kwa sababu nilikuwa ni mwalimu ambaye
amefundisha mbinu nyingi za mabishano wanazozitumia. Pia nimejifunza
namna ya kubishana kwa kutumia Biblia ili kuulinda Ukristo. Na wakati huo
huo ninajua jibu la mabishano ambayo sisi, kama wachungaji, tulikatazwa na
wakuu wetu tusiyajadili au tusiyaweke wazi.
Namuomba Allah anisamehe uzembe wangu wote na atuongoze njia ya
Peponi. Sifa zote ni za Allah. Rehema na Amani ziwe juu ya Mjumbe wake
wa mwisho, Mtume Muhammad na familia yake, na wafuasi wa kweli wote.
Abdullah Muhammad al-Faruque (Kenneth L. Jenkins)
         At-Ta’if, Kingdon of Saudi Arabia
ﺕﺎﻗﺎﻄﺑ ﺓﺭﻮﺻ
ﺓﺭﻮﺻ ﺕﺎﻗﺎﻄﺑ

31
3- DR. JERALD F. DIRKS (ABU YAHYA) ALIYEKUWA
MCHUNGAJI (SHEMASI) WA KANISA LA MUUNGANO WA
WAMETHODISTI. ANA STASHAHADA YA UZAMILI YA
THEOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA HARVARD NA
STASHAHADA YA UDAKITARI WA FALSAFA KATIKA
MAMBO YA KISAIKOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA
DENVER. (USA)
ﺓﺭﻮﺻ ﻪﺗﺩﺎﻬﺷ
Moja ya kumbukumbu zangu za utotoni kabisa ni kusikia mlio wa kengele ya
kanisani kwa ajili ya ibada ya Jumapili katika kitongoji nilichokulia. Kanisa
hilo la Methodisti, lilikuwa kongwe, la miti, na lina mnara wa kengele, shule
ya kila Jumapili yenye madarasa madogo madogo ya watoto wawili
iliyokuwepo nyuma ya zizi, milango ya mbao inayotenganisha madarasa hayo
na eneo la kanisa, kulikuwa na roshani ya kwaya inayotoa makazi kwa
madarasa ya shule ya Jumapili kwa vijana walio wakubwa. Kanisa hilo
lilikuwepo umbali si zaidi ya magorofa mawili kutokea nyumbani kwangu.
Kengele inapogonga, sote tulikuwa tunaenda kwa pamoja kama familia, na
kufanya hija yetu ya kila wiki kulitembelea kanisa hilo.
Katika kijiji kilichoanza tangu miaka ya 1950, makanisa matatu
yaliyokuwepo katika mji huo yenye takriban watu mia tano ndiyo yaliyokuwa
makao makuu ya maisha ya usharika. kanisa la Methodisti la mtaani, ambalo
lilikuwa linamilikiwa na familia yangu, lilikuwa linatoa askrimu za kijiti,

32
askrimu zilizotengenezwa nyumbani, chakula cha usiku cha (chicken potpie),
na losti ya vikopo. Mimi na familia yangu daima tulikuwa tukishiriki katika
makanisa yote matatu, lakini kila moja tuliliendea mara moja kwa mwaka.
Kwa kuongezea, kulikuwa na shule ya usharika wa Biblia ya wiki mbili kila
mwezi wa Juni, kila siku, nilikuwa nahudhuria shule yangu ya hatua nne kwa
mwaka. Hata hivyo, ibada ya Jumapili asubuhi na shule ya Jumapili yakiwa ni
matukio ya kila wiki, na nilijitahidi kuulinda mjumuisho wangu na
kuhudhuria sehemu hizo kikamilifu, nilijifunga kibwebwe na kupata zawadi
ya kuhifadhi Biblia.
Katika siku za shule za hatua ya kwanza ya sekondari. Lile kanisa la
Methodisti la mtaani lilifungwa, na tulikuwa tunahudhuria kanisa la
Methodisti lilokuwepo katika mji wa karibu, ambalo ni kubwa kidogo kuliko
lile la kitongoji alimokuwa akiishi. Hapo kwanza fikra zangu zilianza
kutazama uchungaji kama unavyoitwa. Nikiwa mchangamfu katika ufuasi wa
umoja wa vijana wa Methodisti, na hatimaye nikahudumia pande mbili, jimbo
na uofisa wa mazungumzo. Pia nikawa muhubiri wa kawaida katika kipindi
cha huduma kwa vijana siku za Jumapili kila mwaka. Mahubiri yangu
yalianza kuongeza idadi ya washirika, na kabla ya muda kurefuka mara kwa
mara nilikuwa najaza nafasi za membari za padri katika makanisa mengine,
katika nyumba za uuguzi, katika usharika wa vijana wa makanisa mbali mbali
na makundi ya akina mama, sehemu ambazo kwa aina yake, niliweka rekodi
za mahudhurio.
Nilipotimiza miaka miaka kumi na saba nilianza masomo ya mwaka wa
kwanza chuo kikuu cha Harvard, uamuzi wangu wa kuingia uchungaji
ulikuwa wa nguvu. Katika kipindi cha mwaka wangu wa kwanza chuoni
hapo, nilijiandikisha katika kozi ya mihula miwili ya mlinganisho wa dini
ambayo ilikuwa inafundishwa na Wilfred Cantwell Smith, aliyekuwa
mtaalamu bingwa wa dini ya Kiislamu. Katika kozi hiyo, nilitoa mazingatio
madogo kiasi kwa Uislamu kuliko dini nyinginezo, kama vile Uhindu na
Ubudha, kwani hizo mbili za mwishoni zilionekana ni za faragha sana na ni
ngeni sana kwangu. Ikiwa ni kinyume na Uislamu, ulionekana kuwa, kwa
kiasi kidogo ni sawa sawa na dini yangu ya Ukristo. Kwa hiyo, sikutoa
umakini mkali juu ya Uislamu kama inavyotakiwa, ingawa ninaweza
kukumbuka kuandika waraka wa istilahi za hiyo kozi juu ya maana ya ufunuo
katika Quran. Hata hivyo, kwa kuwa kozi hiyo ilikuwa ni moja ya kozi
ngumu kabisa, kwa viwango vya kitaalamu, nilihitaji maktaba ndogo ya nusu
dazeni ya vitabu vya Kiislamu, hivyo vyote viliandikwa na wasiokuwa

33
Waislamu, na vyote vilikuwa ni vya kunihudumia kwa umadhubuti, miaka
ishirini na tano baadaye. Pia nilihitaji tafsiri tofauti tofauti za maana ya Quran
kwa Kingereza, ambazo nilizisoma kwa muda huo.
Katika majira ya michipuo chuo cha Harvad kilinitangaza kuwa ni
mwanazuoni mkali, akimaanisha kuwa, nilikuwa ni mmoja wa wanafunzi wa
hali ya juu katika maandalizi ya theolojia chuoni hapo. Katika majira ya
kiangazi ya mwaka wangu wa kwanza chuoni Harvard na mwaka wa pili,
nilifanya kazi ya uchungaji kwa vijana walio katika kanisa kubwa kabisa la
umoja wa Wamethodosti. Kiangazi kilichofuata, nilipata leseni ya kuhubiri
kutoka kanisa la muungano wa Wamethodosti. Baada ya kumaliza chuo cha
Havard mwaka 1971, nilijiandikisha shule ya Utakatifu ya Havard, na hapo
nilipata stashahada ya uzamili juu ya theolojia mwaka 1974, baada ya
kusimikwa kikamilifu katika ushemasi wa muungano wa makanisa ya
Methodisti mwaka 1972, na kwa kuwa, hapo kabla nilipata udhamini wa
masomo wa Stewart Scholarship kutoka muungano wa makanisa ya
Methodisti ikiwa ni kama nyongeza ya udhamini wangu wa Havard Divinity
School. Nikiwa katika elimu ya seminari, pia nilimaliza masomo ya nje ya
vipindi vya miaka miwili ya ukasisi wa mahospitalini katika hospitali ya Peter
Bent Brigham mjini Boston. Baada ya kumaliza masomo katika shule ya
utakatifu ya Havard, niliutumia wakati wa kiangazi nikiwa ni mchungaji wa
makanisa mawili ya Methodisti katika viunga vya Kansas, ambako
mahudhurio yalipanda juu kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana
katika makanisa yote hayo kwa miaka kadhaa.
Kwa nje ilionyesha kuwa, nilikuwa mchungaji kijana mwenye kutunza ahadi
sana ambaye amepokea elimu bora zaidi, kuvutia kundi kubwa la watu katika
ibada ya Jumapili asubuhi, na kulikuwa na mafanikio katika kila kituo
kwenye njia ya utumishi. Hata hivyo, kwa ndani ilionyesha, nilikuwa
napambana vita vya daima kudumisha msimamo wangu binafsi katika uso wa
majukumu ya utumishi. Vita hivi vilikuwa mbali sana na vile
vinavyotazamiwa vya kupambana na baadhi ya wainjilisti wa hivi karibuni
katika majaribio yasiofanikiwa ya kuendeleza utu wa kiroho na kingono.
Hivyo, ilikuwa ni vita tofauti sana na vile nilivyopambana na mapadri
Pedophilic waliotamba katika vichwa vya habari vya zama za sasa. Hata
hivyo, mihangaiko yangu ya kudumisha uadilifu wa utu wangu huenda ikawa
ni jambo la kawaida kukabiliwa na wanachama wa utumishi wenye elimu
bora sana.

34
Kuna aina fulani ya kejeli katika ukweli kwamba wale wanaodhaniwa kuwa
ni watumishi bora kabisa wanaochaguliwa kwa elimu bora kabisa ya
seminari, kwa mfano: wale wanaopewa ofa katika muda ule wa shule ya
Theolojia ya Harvard. Kejeli ni kuwa, kwa kupewa elimu hiyo, wanaseminari
wanawekewa wazi historia nyingi ya ukweli kama inavyojulikana: 1)-
maelezo ya kanisa la mwanzo, na vipi lilijengwa kwa siasa ya nchi kama
inavyoathiriwa na mambo ya kijografia. 2)- masomo “asilia” ya maandiko
mbali mbali ya Kibiblia, mengi yao yakiwa katika makindano makali na yale
yanayosomwa na Wakristo wengi wanapobeba Biblia zao, ingawa kidogo,
baadhi ya maelezo hayo hayajaharibiwa na kutiwa katika tafsiri mpya na bora
zaidi; 3)- mabadiliko ya itikadi hizo kama ya nafsi tatu kwa moja ya Mungu
na uwana wa Yesu, amani iwe juu yake; 4)- mambo ya wasiokuwa na dini
yapo katika kanuni za imani na mafundisho ya Wakristo wengi; 5)- kuwepo
kwa makanisa yote hayo ya mwanzo na harakati za Kikristo ambazo
hazikubali itikadi ya utatu wa Mungu, na ambazo kamwe hazikubali itikadi ya
uungu wa Yesu, amani iwe juu yake; 6)- mengineyo (baadhi ya matunda haya
ya elimu yangu ya seminari yanasimulia habari nyingi zaidi katika kitabu
changu kipya, Msalaba na Mwezi; mazungumzo ya imani mchanganyiko
kati ya Ukristo na Uislamu, yaliyochapishwa na Amana Publications
2001.)
Kwa hiyo, si ajabu kabisa kuwa wanaomaliza masomo ya seminari wengi wao
wanatoka kutoka katika seminari si kwenda “kujaza majukwaa,” sehemu
ambayo wataombwa wahubiri kile wanachokijua kuwa si cha kweli, lakini
kinyume chake wanajiingiza katika kazi mbali mbali za ushauri. Hali hiyo
ndiyo iliyonikumba, kwani nilijiendeleza ili nipate stashahada ya uzamili na
udaktari ya matibabu ya kisaikolojia. Niliendelea kujiita Mkristo, kwa sababu
hilo lilikuwa linahitajika kwa ajili ya kujitambulisha, na kwa kuwa nilikuwa
Mkristo, baada ya yote, ni mchungaji msimikwa, hata hivyo, kazi yangu ni
kazi ya kutibu magonjwa ya kiakili. Hata hivyo, elimu yangu ya seminari
ilikuwa ni kinga dhidi ya imani ya kuamini utatu wa Mungu, au uungu wa
Yesu, amani iwe juu yake. (Kura za maoni mara kwa mara zinabainisha kuwa
wachungaji wanaimani ndogo katika kuamini mambo hayo na imani
nyinginezo za kanisa kuliko walei (waumini wa kawaida) wanaowahudumia,
kwa sitiari, huku wakazi wa parokia wakifahamu jambo hilo kimaneno tu.)
Mimi nilikuwa Mkristo wa Krismasi na Pasaka.” Naenda kanisani mara moja
moja sana, kisha nikakerekeza meno yangu na kuuma ulimi wangu
nilipokuwa nasikiliza mahubiri yaliotetea kile nilichokijua kuwa hakikuwa
kadhia husika.

35
Hakuna hata moja katika hayo yaliyopita liwezalo kuchukuliwa ili lionyeshe
kuwa mimi nilikuwa nina upeo wa dini mdogo au uelewa wa kiroho mdogo
kuliko vile nilivyokuwa zamani. Nilikuwa ninasali kila siku, imani yangu kwa
Mungu Mkuu ilibaki imara na salama, na niliendesha maisha yangu binafsi
katika mstari pamoja na maadili niliyofundishwa kanisani na katika shule ya
Jumapili. Kiwepesi, nilikuwa ninajua lilobora zaidi kuliko kununua imani
zilizotengenezwa na mtu na mamlaka za kiimani za usharika wa kanisa,
ambazo zilikuwa zimeshehenezwa mambo mazito mazito ya kipagani, fikra
za kishirikina (kuabudu miungu mingi), na athari za kijografia za miongo
iliyopita.
Baada ya kupita miaka kadhaa, nimekuwa najihusisha zaidi na kupotea kwa
dini katika jamii ya Kimarekani. Dini ni uhai/roho inayopumua na wema kwa
kila mtu, na haitakiwi ichanganywe na ubabaishaji wa kidini, ambao
unajihusisha na ada za kidini, ibada, na kutunga sheria za baadhi ya vyama
vilivyopo, kama ilivyo kwa kanisa. Utamaduni wa Marekani unadhihirisha
kuwa unaendelea kupoteza utu na dira ya kidini. Ndoa mbili katika kila ndoa
tatu zinaisha kwa talaka; vurugu zimekuwa ni sehemu ya urithi uongezekao
mashuleni kwetu na mabarabarani; majukumu binafsi yamepungua; heshima
binafsi imedidimizwa na moyo wa “Kama unahisi ni kizuri, kifanye;”
viongozi na taasisi mbali mbali wa Kikristo zimesombwa na kashfa za ngono
na mali; na fikra za kujihalalishia tabia zao, vyovyote zitakavyochukiza.
Utamaduni wa Kimarekani umekuwa ni taasisi inayofilisika kiutu, nami
binafsi nilikuwa ninayahisi mambo hayo katika mikesha yangu ya kidini.
Ilikuwa ni hali hiyo iliyonifanya nianze mawasiliano na jamii za Kiislamu za
mtaani. Kwa miaka michache kabla ya, mimi na mke wangu kujishughulisha
kikweli kweli katika uchunguzi juu ya historia ya farasi wa Uarabuni.
Hatimaye, ili kupata tafsiri salama za nyaraka mbali mbali za Kiarabu,
uchunguzi huu umetupelekea tukaingia katika mawasiliano na Wamarekani
wa Kiarabu ambao walikuwa ni Waislamu, mawasiliano yetu ya kwanza
yalikuwa na Jamal wakati wa kiangazi cha mwaka 1991.
Baada ya mazungumzo ya awali kwa kutumia simu, Jamal alitembelea
nyumba yetu, na akajitolea kutufanyia tafsiri, na kusaidia kutuongoza katika
historia ya farasi wa Kiarabu katika mashariki ya kati. Kabla Jamal hajatuacha
mchana huo, alituomba kutumia, bafu yetu ili ajioshe kabla ya kutamka sala

36
zake za ratiba ya kila siku; na alituazima kipande cha gazeti ili akitumie kama
zulia la kuswalia, kwa hiyo, alitamka sala zake kabla hajaondoka na kuiacha
nyumba yetu. Na sisi, bila ya shaka, tulilazimika, lakini tulistaajabu kama
kungekuwa na kitu kizuri zaidi cha kutoa ambacho tungempa akitumie kuliko
gazeti. Sisi bila ya kutambua kitu kwa muda huo, Jamal alikuwa anafanya
aina nzuri sana ya Dawa (kuhubiri au kushawishi). Hakutoa maelezo yeyote
juu ya ukweli kwamba sisi hatukuwa Waislamu, naye hajatuhubiria chochote
kuhusiana na imani yake ya kidini. Yeye alitufikishia mifano ya imani yake
tu; mfano uliosema sauti kubwa, kama mtu alihitaji kuwa msikivu wa somo.
Baada ya miezi kumi na sita, kukutana na Jamal kuliongezeka kidogo kidogo
na kuwa mara kwa mara, hadi ikawa mara moja kila wiki mbili na kufikia kila
wiki. Katika safari hizo, Jamal kamwe hajanihubiria kuhusu Uislamu, kamwe
hajaniuliza kuhusu imani ya dini yangu au ninachokikinai, na kamwe
hajapendekeza kwa mdomo kuwa niwe Mwislamu. Hata hivyo, nilianza
kujifunza mengi. Kwanza kabisa, kulikuwa na mfano wa matendo ya daima
kutoka kwa Jamal wa kunionyesha vipindi vya sala zake za kila siku. Pili
kulikuwa na mfano wa kimwenendo wa namna Jamal alivyokuwa
akiyaendesha maisha yake ya kila siku kwa unyofu wa hali ya juu na tabia ya
maadili, anafanya yote mawili hayo katika ulimwengu wake wa kibiashara na
katika ulimwengu wake wa kijamii. Tatu, kulikuwa na mfano wa
kimwenendo juu ya namna Jmal anavyohusiana na watoto wake wawili. Kwa
mke wangu, mke wa Jamal alitoa mifano hiyo hiyo. Nne, daima kulikuwa na
wigo wa kunisaidia nifahamu historia ya farasi wa Uarabuni wa Mashariki ya
Kati, Jamal alianza kushirikiana nami: 1) visa vya Warabu na historia ya
Uislamu; 2) hadithi za Mtume Muhammad, rehema ziwe juu yake; na 3) aya
za Quran na mijadala yake inayozingatia muktadha na ifanyayo kituo juu ya
baadhi ya mitazamo ya Kiislamu, lakini daima alikuwa anaiwasilisha kwa
istilahi za kunisaidia kifikra ili nifahamu muktadha wa Uislamu katika
historia ya farasi wa Uarabuni. Kamwe sijaambiwa kuwa “hivi ndivyo vitu
vilivyo”, nilikuwa naambiwa “hivi ndivyo Waislamu wanavyoamini” tu. Kwa
kuwa sikuwa “nahubiriwa,” na kwa kuwa Jamal kamwe hajataka imani
yangu, sikuhitaji kujisumbua na kujaribu kutetea upande wangu. Mambo yote
yalifanyika kiakili, na si kama mbadilishaji dini.
Kidogo kidogo, Jamal alianza, kututambulisha kwa familia za Waarabu
wengine katika jamii ya Waislamu wa mtaani. Kulikuwa na Wa’eli na familia
yake, Khalidi na familia yake, na wengine wachache kwa unyofu, niliona mtu
mmoja na familia ambazo zilikuwa zinaishi maisha yao kwa maadili ya hali

37
ya juu, yaliyo sawa sawa kuliko jamii ya Kimarekani ambayo kwayo sisi sote
tulikuwa ndani yake. Huenda kulikuwa na jambo katika matendo ya Uislamu
niliyokuwa nayakosa wakati nilipokuwa mwanachuo na katika siku za
seminari.
Hadi Desemba, 1992, nilianza kujiuliza baadhi ya maswali makali juu ya
wapi nilipokuwepo na nilikuwa ninafanya nini. Maswali hayo yalichochewa
na nadhari zifuatazo. 1) Baada ya kozi ya awali ya miezi kumi na sita, maisha
yetu ya kijamii yalianza kukua katika kutilia maanani wigo wa Waarabu wa
jamii ya Kiislamu ya Mtaani. Kufikia Desemba, karibia 75% ya maisha yetu
ya kijamii yalikuwa yanajumuisha na kupitishwa na Waislamu wa Kiarabu.
2) Kwa maadili ya mafunzo na elimu yangu ya seminari, nilijua kuwa kuna
kuharibiwa vibaya kwa Biblia (mara nyingine nilijua kwa hakika kabisa lini,
wapi, na kwa nini), sikuwa na imani yeyote juu ya utatu wa Mungu, na
sikuwa na imani ya chochote zaidi ya sitiari tu “Uwana” wa Yesu, amani iwe
kwake. Kwa ufupi, huku nikiwa namwamini Mungu kikamilifu, nilikuwa nina
imani kali juu ya Mungu Mmoja kama rafiki zangu wa Kiislamu. 3) Thamani
yangu binafsi na akili yangu ya maadili iliyokuwa inaegemea sana kukaa na
marafiki Waislamu kuliko na jamii ya “Wakristo” iliyonizunguka. Baada ya
yote, nilikuwa na mifano isiyopingana ya Jamal, Khalid, na Wa’el ikiwa ni
vielelezo kwangu. Kwa ufupi, kiu yangu ya miaka mingi ya kupata aina ya
jamii ambayo nimekulia ilipatikana na kupendeza kutika jamii ya Kiislamu.
Jamii ya Kimarekani, imemomonyoka kimaadili, lakini ni jambo hilo
halikuwa tatizo kwa sababu ya ile ya jamii ya Waislamu ambayo
nimeshawasiliana nayo. Ndoa zilikuwa ni imara, wanandoa walikuwa
wanawajibika wao kwa wao, wema, uadilifu, msimamo, kubeba majukumu na
thamani ya familia ilitiliwa mkazo. Mke wangu alijaribu tuishi maisha yetu
kwa njia hiyo hiyo, lakini kwa miaka mingi nimehisi kuwa tulikuwa
tunafanya hivyo katika muktadha ombwe (tupu, wazi) wa kimaadili ya kiroho.
Jamii ya Kiislamu ilionekana kuwa ni tofauti. Nyuzi mbali mbali, zilifumwa
pamoja na kuwa kamba moja.
Farasi wa Kiarabu, malezi yangu ya utotoni, uvamizi wangu wa kuingia
uchungaji wa Kikristo na kuwasiliana kwangu na jamii ya Waislamu
yalikuwa ni mambo tata yanayosokotana. Kujiuliza kulifikia kichwani pale,
hatimaye nilipofikia kujiuliza kuna nini hasa kinachonitenganisha na imani ya
rafiki zangu Waislamu. Nikapendekeza kuwa niibue swali hilo kwa Jamal au
Khalid, lakini sikuwa tayari kuchukua hatua hiyo. Kamwe sijawahi
kujadiliana nao juu ya imani ya dini yangu mwenyewe, na sikufikiria kuwa

38
nilitaka kuitoa mada hiyo katika urafiki wetu. Kwa hiyo, nilianza kuegesha
pembeni rafu yote ya vitabu juu ya Uislamu ambavyo nilivipata nilipokuwa
chuoni na seminarini. Hata hivyo, kwa mbali imani yangu ilikua kutokana na
nafasi asilia ya kanisa, na ingawa nilienda kanisani mara chache lakini kwa
hakika nilihudhuria kanisani, na bado nilikuwa najitambulisha kuwa mimi ni
Mkristo, na kwa hiyo, niligeukia kazi ya uanazuoni wa Kimagharibi. Mwezi
huo wa Desemba, nilisoma nusu dazeni au zaidi ya vitabu juu ya Uislamu
vilivyoandikwa na wanazuoni wa Kimagharibi, kikiwemo kimoja cha historia
ya Mtume Muhammad, amani iwe juu yake. Zaidi, nilianza kusoma tafsiri
mbili za Kingereza zilizotofauti tofauti za maana ya Quran. Kamwe
sikuongea na rafiki zangu wa Kiislamu kuhusu huo uchunguzi wangu binafsi
wa kugundua mwenyewe. Kamwe sikutaja ni aina gani ya vitabu nilivyokuwa
navisoma, wala kuzungumzia kwa nini nilikuwa navisoma vitabu hivyo. Hata
hivyo, mara kwa mara nilikuwa nawapelekea maswali yenye mipaka
maalumu.
Huku nikiwa siwaambii rafiki zungu wa Kiislamu kuhusu vitabu hivyo,
lakini mimi na mke wangu tulikuwa na mijadala mbali mbali juu ya kile
nilichokuwa nakisoma. Kufikia wiki ya mwisho ya Desemba 1992,
nililazimika kukiri, kuwa sijapata upenyo wowote wa kukataa kimsingi kati
ya imani yangu ya kidini na mafundisho ya Kiislamu. Nilipokuwa tayari
kufahamu kuwa Muhammad, amani iwe juu yake, alikuwa ni Mtume
(mmojawapo aliyeongea kwa, au chini ya msukumo) wa Mungu, na
nilipokuwa sina uzito wowote wa kuthibisha kuwa hakuna Mungu kinyume
na Allah, Mtukufu aliyetukuka, nilikuwa bado ninasitasita kuchukua uamuzi
wowote. Tayari nilikuwa nimekiri katika nafsi yangu kuwa nilikuwa pamoja
sana na imani ya Kiislamu kama baadaye nilivyoifahamu, kuliko nilivyofanya
na mila ya Kikristo ya kuweka umoja wa kanisa. Nilijua vizuri sana kuwa
kiwepesi kabisa ningeweza kuthibitisha kutokana na mafunzo na elimu yangu
ya seminari, mambo mengi ambayo Quran ililazimika kuusema Ukristo,
Biblia, na Yesu, amani iwe juu yake. Hata hivyo, nilisita. Zaidi, nilitazama
kimantiki usitaji wangu kwa kujiendesha mimi mwenyewe kuwa kweli sikijui
kiini na suala la msingi na maelezo kamili juu ya Uislamu, na kwa hiyo,
maeneo yangu ya kuafiki yaliwekewa mipaka kwa dhana nzima. Kwa hiyo,
niliendelea kusoma, na kurudia kusoma.
Wazo moja la kujitambulisha, mimi ni nani, ni uthibitisho wenye nguvu zaidi
juu ya nafasi ya mtu binafsi ulimwenguni. Katika kazi zangu nizifanyazo,
mara kwa mara niliitwa kutibia tabia mbaya, zinazojipanga kuanzia, kuvuta

39
sigara, hadi ulevi, utumiaji wa madawa ya kulevya. Nikiwa ni tabibu, nilijua
kuwa msingi wa tabia mbaya za kiwili wili lazima utibiwe ili kuunda kinga ya
awali. Na hilo lilikuwa ni sehemu rahisi sana ya matibabu. Mark Twain
alisema: “Kuacha sigara ni kwepesi; nimeshaacha mara mia kadhaa.” Hata
hivyo, pia nilijua kuwa funguo ya kudumisha uzuiaji wa wigo wa muda
ilikuwa ni kumtibu mgonjwa tabia mbaya za kisaikolojia, ambazo kwa kiasi
kikubwa zilizunguka mzizi wa fikra za mgonjwa za kujitambulisha, yaani,
mgonjwa anajitambulisha kuwa yeye alikuwa ni “mvuta sigara,” au “mlevi”
na kuendelea. Tabia mbaya imeshakuwa ni sehemu na ni mfuko wa fikra hii
ya kujitambulisha, ilikuwa ni muhimu sana katika kurekebisha matibabu ya
kisaikolojia. Na hii ndiyo iliyokuwa sehemu ngumu sana kimatibabu.
Kubadilisha msingi wa fikra za mtu za kujitambulisha ni kazi ngumu sana.
Akili ya mtu inang`ang`ania mambo ya zamani na yaliyozoeleka, ambayo
yanaonekana ni yenye kutia raha sana kisaikolojia na ni yenye usalama sana
kuliko mambo mapya na yasiyozoeleka.
Kwa msingi wa kazi, nilikuwa na elimu hiyo, na niliitumia kila siku. Hata
hivyo, kwa dhihaka ya kutosha, sikuwa tayari kuutumia msingi huo kwa nafsi
yangu mwenyewe, na katika kadhia yangu ya kusitasita iliyozunguka
utambulisho wangu wa kidini. Kwa miaka 43, utambulisho wangu wa kidini
kimaridadi ulikuwa ni jina la “Ukristo” hata hivyo, sifa nyingi niliweza
kuziongeza katika jambo hilo kwa miaka mingi. Kuacha jina hilo la
kujitambulishia dhati binafsi, lilikuwa si rahisi. Lilikuwa ni sehemu na fuko la
namna nilivyofahamu kuwepo kwangu. Kupewa faida ya kung’amua, ni wazi
kuwa kusita kwangu kulihudumia lengo la kuhakikisha kuwa nitunze
utambulisho wangu wa kidini niliouzoea wa kuwa mimi ni Mkristo, ingawa ni
Mkristo ambaye anaamini kama wanavyoamini Waislamu.
Na ilikuwa mwishoni kabisa mwa Desemba, mimi na mke wangu tulipokuwa
tukijaza fomu za maombi ya pasipoti za US, kwa hiyo, safari
iliyopendekezwa ya kwenda mashariki ya kati imekuwa ni ya uhakika. Moja
ya swali lilikuwa ni kuhusu ushiriki wa kidini. Hata sikufikiria jambo hilo, na
bila kufikiri nikaangukia kule kule kwa zamani na mazoea, nilifungwa katika
“Ukristo.” Ulikuwa ni mwepesi na ulikuwa uliozoeleka, na wenye kutia raha.
Hata hivyo, raha hivyo ilikuwa ni ya muda tu na ilivurugika pale mke wangu
aliponiuliza vipi nilijibu swali la utambulisho wa dini katika fomu ya
maombi. Nami haraka haraka nilijibu “Mkristo”, na kuchekelea chini chini
kunakosikika. Sasa, moja ya nadharia ya udadisi ya Kifreudi inayosaidia

40
kufahamu nafasi ya mwanadamu ilikuwa ni kutambua kuwa kicheko mara
nyingine ni tiba ya mfadhahiko wa kisaikolojia. Hata hivyo, nadharia ya
udadisi ya Kifreudi inaweza ikawa katika mitazamo mingi ya nadharia yake
ya mwendelezo wa saikolojia ya ngono, utambuzi wake katika kicheko
ulikuwa katika lengo kabisa. Nilicheka! Nini kilikuwa mfadhaiko wa
kisaikolojia ambao nililazimika kuutuliza kupitia kicheko cha wastani?
Kisha haraka haraka niliendelea kumpa mke wangu maelezo mafupi
yanayothibitisha kuwa nilikuwa Mkristo na sio Mwislamu. Katika kujibu
hayo, naye kiungwana alinifahamisha kuwa alikuwa anauliza tu kama mimi
nimeandika “Ukristo”, au “Uprotestanti”, au “Umethodisti”. Kwa mujibu wa
kanuni za kazi, nilijua kuwa mtu hajitetei kwa lawama ya kitu asichokifanya.
(kama itakuwa katika mwendo wa baraza ya tiba za kisaikolojia, na mgonjwa
wangu akaropoka, na kusema “sijakikasirikia” na sijaanzisha habari za hasira,
ilikuwa ni wazi kuwa mteja wangu alikuwa na hisia za kujitetea dhidi ya
mashtaka ambayo bila ya kujijua alikuwa anayafanya. Kwa ufupi, huyo mteja
kwa hakika alikuwa na hasira, lakini hakuwa tayari kukiri kitu hicho au
kukishughulikia.) Kama mke wangu asingefanya tukio hilo, yaani “wewe ni
Mwislamu,” tukio hilo lingenitoka bila ya kujijua, kwa vile ndiye mtu pekee
aliyekuwepo. Nilikuwa macho na hilo, lakini niliendelea kusita sita. Jina la
dini ambayo imekita katika fikra zangu za kujitambulisha kwa miaka 43
ilikuwa haiwezekani kuondoka kirahisi rahisi.
Takriban mwezi umeshapita tangu mke wangu kuniuliza lile swali. Na
ilikuwa mwishoni mwa Januari ya 1993. nilipoweka pembeni vitabu vyote juu
ya Uislamu vya wanazuoni wa Kimagharibi, kwa kuwa nimevisoma
kikamilifu. Zile tafsiri mbili za Kingereza za maana ya Quran zilirejea tena
katika rafu, na nilikuwa nina kazi ya kusoma tafsiri ya tatu ya maana za
Quran. Uhenda katika tafsiri hii nitapata uthibitisho wa ghafla kwa….
Nilikuwa nautumia muda wangu wa chakula cha mchana kwa kutoka katika
kazi zangu binafsi na kuutumia katika mgahawa wa Kiarabu wa mtaani
ambao nimeanza kufululiza kuutembelea. Niliingia kama kawaida, nikakaa
katika meza ndogo, na nilifungua tafsiri yangu ya tatu ya Kiingereza ya
maana ya Quran kuanzia pale nilipoishia kupasoma. Nilifikiria kupata kusoma
kidogo wakati wa chakula cha mchana. Kwa kitambo baadaye, nilikuwa
macho kuwa Muhammad alikuwa mabegani mwangu, na anangojea kuchukua
oda yangu. Naye akakitupia jicho kile nilichokuwa nakisoma, lakini

41
hakusema lolote kuhusiana na hilo. Oda yangu ilichukuliwa, nami nikarejea
katika kisomo changu cha faragha.
Dakika chache baadaye, mkewe, Imani, Mwislamu wa Kimarekani, aliyevalia
hijabu na nguo za heshima ambazo nilizizoea kwa wanawake wa Kiislamu,
aliniletea oda yangu. Naye aliona kuwa nilikuwa ninasoma Quran, na kwa
adabu akaniuliza kama nilikuwa Mwislamu. Neno lilinitoka mdomoni kabla
halijarekebishwa na adabu za kijamii au kiungwana: “Hapana” Neno hilo
lilitamkwa kwa nguvu, na lilikuwa ni zaidi ya vidokezo vya kukasirika upesi.
Kwa ajili hiyo, Iman kwa adabu alijiondoa kutoka pale mezani kwangu.
kimenitokea nini? Nimefanya tabia mbaya na uchokozi. Mwanamke
amefanya nini cha kustahiki apate ufedhuli ule kutoka kwangu? Hili halikuwa
linalonistahiki. Kwa kupewa malezi ya utotoni, naendelea kutumia “bwana”
na “ma’am” nilipokuwa natambulisha makarani na makeshia ambao
walikuwa wananingojea madukani. Nilijifanya kudharau kicheko changu
mwenyewe kuwa ni kitulizo cha mfadhaiko, lakini sikuweza kuanza kudharau
aina hii ya tabia ya kutojitambua niliyoianza. Nikaweka pembeni kule
kusoma, na kiakili nililewa na aina hii ya matukio kupitia chakula changu,
kila nikiongezeka kuchukuliwa na kile chakula ndiyo nikiongezeka kuhisi
uovu juu ya tabia yangu. Nilijua kuwa wakati Imani atakaponiletea cheki
baada ya kumaliza chakula, nitahitajika kufanya marekebisho. Kama si kwa
ajili nyingine, ila kiwepesi kwa ajili ya uungwana ukiwa unanifanya nifanye
hivyo. Zaidi, nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa juu ya kiwango cha uadui
nilichomfanyia kwa swali lake lisilo na madhara. Kilichokuwa kinaendelea
upande wangu ni kuwa nimejibu kwa hasira sana lile swali lepesi na la wazi
lisilo na mitego? Kwa nini lile swali moja, swali lepesi limepelekea aina ile ya
tabia mbaya upande wangu?
Baadaye, Imani alipokuja na cheki yangu, nilijaribu kumuomba msamaha
kwa kusema: “nasikitika kidogo nilipagawa na kukujibu vibaya swali lako
pale mwanzo. Kama ungeniuliza iwapo ninaamini kuwa kuna Mungu Mmoja
tu, jibu langu lingekuwa ndiyo. Kama ungeniuliza iwapo ninaamini kuwa
Muhammad alikuwa ni mmoja wa Mitume ya Mungu, jibu langu lingekuwa
ndiyo.” Naye kwa uzuri kabisa na uvumilivu kabisa alisema: “Sawa; jambo
hilo linachukua muda mrefu kidogo kwa watu wengine.”
Huenda msomaji wa habari hii atakuwa mwadilifu vya kutosha kunukuu
mchezo wa kisaikolojia nilioucheza na nafsi yangu bila ya kujichekelesha

42
chini chini kwa sana katika mazoezi yangu ya kiakili na kitabia. Mimi
naelewa vizuri kuwa kwa njia yangu mwenyewe, ya kutumia maneno yangu
mwenyewe, nimeshatamka shahada, ushuhuda wa imani wa Kiislamu, yaani
“Ninashuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa
Allah, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah.” Hata hivyo,
baada ya kusema hivyo, na kutambua kile nilichokisema, bado niliendelea
kung`ang`ania mambo yangu ya zamani na niliyoyazowea ya jina la
utambulisho wa dini yangu, baada ya yote, sikusema kuwa nilikuwa
Mwislamu. Kwa wepesi kabisa nilikuwa Mkristo, ijapokuwa ni Mkristo wa
aina yake ambaye alikuwa anataka kusema kuwa kuna Mungu Mmoja tu, na
si utatu, na aliyekuwa anataka kusema kuwa Muhammad alikuwa ni mmoja
wa Mitume iliyopewa ufunuo na Mungu huyo huyo Mmoja. Kama Mwislamu
angetaka kunikubali kuwa mimi nimekuwa Mwislamu hilo lingekuwa ni juu
yake na ni jina lake la kunitambulisha mimi kidini. Hata hivyo, si kuwa mimi.
Nilifikiria kuwa nimeshapata njia ya kunitoa katika tatizo la utambulisho wa
kidini. Nilikuwa Mkristo niliyefafanua kwa uangalifu kuwa ninaafiki na
nilikuwa ninataka kushuhudia shahada ya imani ya Kiislamu. Baada ya
kutengeneza ufafanuzi wa mateso yangu, na baada ya kuianisha lugha ya
Kingereza karibu na kila nchi ya maisha yake, wenginewe wanaweza
kunibandika jina lolote watakalo. Na jina hilo ni lao wao, na si langu.
Sasa ilikuwa ni mwezi machi 1993, mimi na mke wangu tulikuwa tunafurahia
likizo ya wiki tano katika mashariki ya kati. Pia ulikuwa ni mwezi wa
Ramadhani wa Kiislamu, wakati ambapo Waislamu wanafunga kuanzia
alfajiri hadi kuzama kwa jua. Kwa kuwa mara nyingi tulikuwa tukikaa au
kusindikizwa na wanafamilia wa marafiki zetu wa Kiislamu nyumbani
Marekani, mimi na mke wangu tuliamua tufunge si kwa lengo lingine zaidi ya
adabu ya kikawaida. Katika kipindi hiki, vilevile nilianza kutekeleza swala
tano za Kiislamu za kila siku na marafiki zangu wa mashariki ya kati
niliowapata hivi karibuni, baada ya yote, kulikuwa hakuna kitu katika swala
hizo ambacho nilikipinga.
Nilikuwa ni Mkristo au hivyo ndivyo nilivyosema. Ingawaje baada ya yote,
nimezaliwa katika familia ya Kikristo, nimelelewa Kikristo, nimeshahudhuria
kanisani na shule za Jumapili kila Jumapili nikiwa mtoto, nimehitimu
masomo kutoka katika seminari yenye kuheshimika sana, na nilikuwa
mchungaji msimikwa katika madhehebu makubwa ya Kiprotestanti. Hata
hivyo, pia nilikuwa ni Mkristo: nisiyeamini utatu au uungu wa Yesu, amani
iwe juu yake, nilikuwa ni mtu anayefahamu vizuri jinsi ilivyoharibiwa Biblia;

43
na ni mtu niliyetamka shahada ya Kiislamu kwa maneno ya upambanuzi
wangu mwenyewe yenye uangalifu mkubwa; niliyefunga Mwezi wa
Ramadhani; niliyeswali swala za Kiislamu mara tano kwa siku; na ambaye
alishinikizwa sana na mifano ya mienendo niliyoishuhudia katika jamii za
Kiislamu, sehemu zote Marekani na Mashariki ya kati. (Muda na nafasi
haviniruhusu kutoa maelezo mapana juu ya mifano ya utu na mfumo wa
maadili niliyoyakabiliana nao mashariki ya kati.) kama ningeulizwa kama
nilikuwa Mwislamu ilinichukua dakika tano kutoa maneno binafsi marefu na
kuliacha swali halijajibiwa. Nilikuwa ninacheza mchezo wa maneno wa
kiakili, na nilifanikiwa kwa jamaa hao vizuri kabisa.
Na ilikuwa ni mwishoni mwa safari yetu ya Mashariki ya kati. Pale rafiki
mmoja mzee aliyekuwa hajui Kingereza, na nikiwa natembea katika njia
iliyopindapinda, njia ndogo, katika moja ya maeneo yaisioendelea kiuchumi
katika mji mkongwe wa ‘Amani, Jordan.’ Tulipokuwa tunatembea, kikongwe
kimoja kilitusogelea kutokea upande unaokabiliana nasi, na kusema, “Salam
Alaykum”, yaani “Amani iwe juu yenu”, na akatupa mikono. Tulikuwa watu
watatu tu sehemu hiyo. Sijui Kiarabu, pia rafiki yangu naye hajui, wala yule
mgeni haongei Kingereza. Yule mgeni, akanitazama, na akaniniuliza,
Mwislamu?
Katika kipindi hiki barabara, nilikuwa nimenaswa kikamilifu. Kulikuwa
hakuna mchezo wa maneno ya kiakili utakaochezwa, kwa kuwa nilikuwa
ninaweza kuwasiliana kwa Kingereza tu, na wao walikuwa wanaweza
kuwasiliana kwa Kiarabu tu. Kulikuwa hakuna mkalimani wa kunidhamini na
kunitoa katika hali hiyo, na kuniruhusu nijifiche nyuma ya mazungumzo
yangu ya Kingereza yaliyoandaliwa kwa uangalifu mkubwa. Sikuweza
kujidai kuwa eti sijaelewa swali, kwa kuwa lilikuwa wazi kabisa. Uchaguzi
wangu ulikuwa ni wa ghafla, usiotabirika, na usioelezeka na umepunguzwa na
kubakia mambo mawili tu: nisema “Naam” yaani “Ndiyo” au niseme “La”
yaani “Hapana”. Chaguo ni langu, na nilikuwa sina chaguo jengine. Kwa sasa
nililoazimika kuchagua; ilikuwa ni lepesi kabisa. Allah atukuzwe, Nilijibu
“Naam”.
Kwa kusema neno hilo moja, michezo ya maneno ya kiakili yote ilikuwa
nyuma yangu. Ikiwa michezo ya maneno ya kiakili ipo nyuma yangu, mchezo
wa kisaikolojia wa kuzingatia utambulisho wangu wa kidini nao ulikuwa
nyuma yangu. Sikuwa mmoja wa Wakristo wa ajabu nisiye wa kawaida.

44
Nilikuwa Mwislamu. Allah atukuzwe, mke wangu mwenye miaka therathini
na tatu akawa Mwislamu katika muda huo.
Na si miezi mingi baada ya kurejea Marekani kutokea mashariki ya kati, jirani
mmoja alitualika twende nyumbani kwake, na kusema kuwa anataka kuongea
nasi juu ya kubadili kwetu dini na kuwa Waislamu. Alikuwa ni mchungaji
mstaafu wa Kimethodisti, ambaye nilikuwa na mijadala naye mingi hapo
kabla. Ingawa mara kwa mara tulikuwa tukizungumza kijuu juu kuhusiana na
mambo kama uundwaji wa kibandia wa Biblia kutokana na vyanzo mbali
mbali vya mwanzo vilivyotengana, kamwe hatukuwa na maongezi ya kina juu
ya dini. Nilichojua ni kuwa amepata elimu madhubuti ya seminari, na alikuwa
anaimba katika kwaya ya kanisa la mtaani kila Jumapili.
Mwitikio wangu wa awali ulikuwa ni “Oh, oh, hilo linakuja”. Hata hivyo, ni
wajibu wa Mwislamu awe jirani mwema, na ni wajibu wa Mwislamu kutaka
kujadili Uislamu na watu wengine. Kwa hiyo, nilikubali ule mwaliko wa jioni
ifuatayo na nilitumia muda mwingi niliokuwa ni macho wa saa 24 zilizofuatia
katika kutafakari nanma nzuri ya kumwendea muungwana huyu katika mada
ya maombi yake. Muda tuliokubaliana ukafika, na tukaendesha gari yetu hadi
tukafika kwa jirani yetu. Baada ya muda mchache wa maongezi madogo,
yeye, mwishowe, aliuliza kwa nini nimeamua kuwa Mwislamu. Nilikuwa
ninalingojea swali hilo, na nilikuwa nimeshaandaa vizuri jibu langu. “Kama
ujuavyo ukiwa na elimu ya seminari, kuna mambo mengi yasio ya kidini
ambayo yametayarishwa na kuunda maamuzi ya Baraza la Nicaea.” Naye
kwa haraka haraka akanikatiza kwa sentensi nyepesi: “Wewe hatimaye
hukupendezwa na imani ya kuabudu miungu mingi, au siyo?” alijibu
kikamilifu kwa nini nilikuwa Mwislamu, naye hakupinga maamuzi yangu!
Yeye mwenyewe, kwa umri wake na nafasi yake maishani, alichagua awe
“Mkristo wa aina yake”. Allah anamtaka, na hadi kufikia sasa ameshamaliza
safari yake kutoka msalabani hadi mwezini.
Kuna muhanga unaotakiwa kutolewa kwa kuwa Mwislamu nchini Marekani.
Katika jambo hilo, kuna muhanga unaotakiwa kutolewa kwa kuwa
Mwislamu sehemu yeyote ile. Hata hivyo, inawezekana kuwa ni mikali sana
Marekani na hasa hasa miongoni mwa waliobadili dini katika Wamarekani.
Baadhi ya mihanga hiyo ni yenye kutabirika ikiwemo kubadili mavazi na
kujizuia na pombe, nguruwe, na kuvutiwa na pesa za mtu mwingine. Baadhi
ya mihanga hiyo haitabiriki kwa mfano, familia moja ya Kikristo, ambayo
ilikuwa ni mrafiki zetu wa karibu, ilitufahamisha kuwa hawatoshirikiana nasi

45
tena, kwa kuwa wao hawashirikiani na mtu yeyote “ambaye hamfanyi Yesu
Kristo kuwa ndiye mwokozi wake.” Kwa kuongezea, baadhi ya wafanyakazi
wenzangu wachache wamebadili tabia zao za kufungamana nami. Ima jambo
hilo lilikuwa la upatanifu au la pato langu la kazi, nalo lilipungua na kulikuwa
na takriban 30% inashuka katika pato langu kama matokeo ya hayo. Baadhi
ya mihanga hiyo isiyotabirika ilikuwa ni mikali mno kuikubali, ingawa
mihanga ilikuwa ni thamani ndogo sana kuilipa kwa kile kilichopatikana
kama malipo mbadala.
Kwa tafakuri zote hizo kuukubali Uislamu na kujisalimisha kwa Allah –
Mtukufu na Mpaji, kutakuwa na kujitoa muhanga tu katika njia yake. Mingi
ya mihanga hiyo kiwepesi ni yenye kutabirika, huku mingine huenda ikawa ni
ya kushangaza na isiyotabirika. Hakuna kukataa kuwepo kwa mihanga hiyo.
Uchambuzi wa mwisho kabisa, mihanga hiyo si muhimu sana kuliko fikra
zako za sasa. Allah anakutaka, upate mihanga hiyo ambayo ni sarafu rahisi
sana kuilipa ili kupata heri nyingi” utakazozinunua.
ﺓﺩﺎﻬﺷ ﺓﺭﻮﺻ

46
4 - SISTA KHADIJA “SUE” WATSON ALIYEKUWA
MCHUNGAJI, MMISHIONARI, NA PROFESA ANA
STASHAHADA YA UZAMILI YA MASWALA YA THEOLOJIA
(NI MMAREKANI MWENYE ASILI YA KIFILIPINO)
“Nini kimekutokea?” Kila siku hicho ndicho kitendo rejeshi cha kwanza,
ambacho nilikabiliana nacho. Wakati wanafunzi wenzangu wa zamani,
marafiki na wachungaji wenzangu waliponiona baada ya kuingia Uislamu.
Nadhani sikuweza kuwalaumu kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa sipendi
kabisa mtu abadili dini. Zamani, nilikuwa Profesa, mchungaji, mwasisi wa
kanisa na mmishionari. Kama kuna mtu yeyote aliyekuwa na msimamo mkali
kabisa, basi nilikuwa ni mimi.
Baada ya kuhitimu stashahada ya uzamili ya theolojia kutoka katika seminari
ya watu wenye vipaji na uwezo maalumu miezi mitano hapo kabla. Ilikuwa ni
baada ya wakati huo nilipokutana na bibi mmoja ambaye aliwahi kufanya
kazi nchini Saudi Arabia na ameshasilimu. Bila ya shaka nilimuuliza juu ya
namna wanavyotendewa wanawake katika Uislamu. Nilishutushwa na jibu
lake, kwani halikuwa ni lile niliolitarajia kwa hiyo, niliendelea kuuliza
maswali mengine yanayohusiana na Allah na Muhammad amani iwe juu yake
(S.A.W) 5. Naye akanifahamisha kuwa atanipeleka katika kituo cha Kiislamu
sehemu ambayo wataweza kujibu maswali yangu.
Baada ya kusali- yaani kumuomba Yesu anikinge dhidi ya Shetani na pepo
wabaya, ikionyesha kuwa kile tulichofundishwa kuhusu Uislamu kuwa ni dini
ya mapepo na mashetani. Kwa kuwa nimeshafundishwa uinjilisti nilikuwa
nimeshtushwa kabisa kabisa na ujaji wa Waislamu, kwani ulikuwa ni wa moja
kwa moja na usio na mizengwe. Hakuna vitisho, hakuna bughudha, hakuna
kutawaliwa kisaikolojia, hakuna kuvutwa bila ya kujihisi! Hakuna lolote
katika hayo, “Acha tukupatie mafunzo ya Quran nyumbani mwako”, iwe ni
kama mwenzi wa mafunzo ya Biblia. Sikuweza kuamini jambo hilo! Walinipa
baadhi ya vitabu na wakaniambia kama nitakuwa na maswali wao wapo
ofisini, tayari kuyajibu maswali hayo. Usiku huo nilisoma vitabu vyote
walivyonipatia. Na hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusoma kitabu juu
ya Uislamu kilichoandikwa na Mwislamu, tumeshajifunza na kusoma vitabu
juu ya Uislamu vilivyoandikwa na Wakristo tu! Siku iliyofuata nilitumia
masaa matatu pale ofisini kwao nikiuliza maswali. Tukio hilo liliendelea kila
5
Ni kifupi cha maneno ya Kiarabu na maana yake ni rehema na amani ziwe juu yake.

47
siku kwa wiki moja, kwa muda huo tayari nilikuwa nimeshasoma vitabu 12
na kujua kwa nini Waislamu ni watu wagumu zaidi duniani kubadili dini na
kuwa Wakristo. Kwa nini? Kwa sababu hakuna kitu cha kuwapa!! (Katika
Uislamu) kuna kufungamana na Allah, kusamehewa dhambi, uwokovu na
kuahidiwa maisha ya milele.
Kikawaida, swali langu la kwanza lilitilia umuhimu suala la Uungu wa Allah.
Ni nani huyu Allah ambaye Waislamu wanamwabudu? Sisi kama Wakristo
tumeshafundishwa kuwa huyo ni Mungu mwingine, Mungu wa uongo.
Wakati, kwa hakika yeye ndiye Mjuzi, Mwenye nguvu, na Aliye hai. Mmoja
asiye na mshirika wala aliye sawa naye. Ni jambo la kuvutia kujua kuwa
kulikuwa na maaskofu katika kipindi cha miaka mia tatu ya mwanzoni ya
kanisa ambao walikuwa wanafundisha kama wanavyofundisha Waislamu
kuwa Yesu (A.S) 6 alikuwa ni Mtume na si Mwana wa Mungu!! Na ilikuwa ni
baada ya mageuzi ya utawala ya mfalme Constantine kuwa yeye ndiye
aliyekuwa wa kwanza kutangaza na kujulisha imani ya utatu. Yeye alikuwa ni
mtu aliyebadili dini na kuwa Mkristo ambaye hajui lolote la kidini na
aliitambulisha itikadi ya kipagani ambayo historia yake inarejea zama za
Mababyloni. Kwa sababu nafasi hainiruhusu kuingia katika maelezo kwa
upana juu ya somo hilo insha-Allah, nitazungumza hayo mara nyingine. Kitu
pekee ambacho ni lazima nikizungumze ni neno utatu kuwa halimo katika
Biblia, katika tafsiri nyingi za Biblia wala halipatikani katika Biblia ya
Kigiriki au ya Kiyahudi!
Swali langu muhimu jengine lilitilia umuhimu juu ya Muhammad (S.A.W).
Ni nani huyu Muhammad? Nimegundua kuwa Waislamu hawamwabudu
kama vile Wakristo wanavyomwabudu Yesu. Yeye si mpatanishi na kwa
hakika ni haramu kumwabudu. Tunamuombea abarikiwe mwishoni mwa sala
zetu lakini vilevile Tunamuombea Abrahamu naye abarikiwe. Yeye ni Mtume
na ni mjumbe, Mtume wa mwisho. Kwa hakika, hadi sasa, ni miaka elfu moja
mia nne na kumi na nane imeshapita hakuna Mtume yeyote baada yake.
Ujumbe wake ni kwa watu wote ikiwa ni kinyume na ujumbe wa Yesu au
Musa (rehema ziwe juu yao) ambao walitumwa kwa Wayahudi. “Sikia ee
Israeli” lakini ujumbe wenyewe ni ule ule ujumbe wa Allah. “Yesu akamjibu,
Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;”
(Marko 12:29)
6
Ni kifupi cha maneno ya Kiarabu yenye maana Iwe juu yake amani.

48
Kwa kuwa sala ilikuwa ni sehemu muhimu sana ya maisha yangu ya Kikristo
nilikuwa navutiwa na nina udadisi wa kutaka kujua Waislamu walikuwa
wanakiswali nini? Tukiwa kama Wakristo tulikuwa tunapuuzia mtazamo huo
wa imani ya Kiislamu kama vile katika mitazamo mengine. Tulifikiria na
tulifundishwa kuwa, Waislamu walikuwa wanainamia Kaaba (iliyopo Maka),
na hiyo Kaaba ndiyo ilikuwa Mungu wao na ndiyo kiini cha huyo Mungu wa
uongo. Kwa mara nyingine, nililishtushwa kujua kuwa namna ya sala
imelezwa na Mungu Mwenyewe. Dua za sala, na yale ya kumtukuza na
kumsifu. Mwelekeo wa kuielekea sala (udhu au kuoga) kwa usafi upo chini
ya maelezo ya Allah. Yeye ni Mungu Mtakatifu na haifai kwetu sisi
kumwendea kwa hali ya kiholela holela lakini jambo la kiakili pekee ni kuwa
Yeye mwenyewe atwambie tumwendeeje.
Mwishoni mwa wiki hiyo baada ya kutumia miaka minane ya masomo ya
kitauhidi 7 ya kawaida nilijuwa kiutambuzi kabisa (head knowledje) kuwa
Uislamu ulikuwa ni ukweli. Lakini sikuuingia Uislamu kwa wakati huo kwa
kuwa sikuuamini moyoni mwangu, niliendelea kusali, kusoma Biblia,
kuhudhuria mihadhara katika kituo cha Uislamu. Nilikuwa ni mwenye ari na
bidii ya kuuliza na kutafuta mwongozo wa Mungu. Si rahisi kubadili dini
yako. Sikutaka kupoteza uwokovu wangu kama kulikuwa na uwokovu wa
kuupoteza. Niliendelea kushtushwa na kushangazwa kwa kile nilichokuwa
najifunza kwa sababu kilikuwa si kile nilichofundishwa kuwa Uislamu
unakiamini. Katika kiwango changu cha stashahada ya uzamili, profesa
niliyekuwa naye alikuwa ni mwenye kuheshimika kama ni mwenye
mamalaka ya juu ya Uislamu, mafundisho yake na Ukristo wake kiujumla
umejaa upotoshaji. Yeye na Wakristo wengi kama yeye ni waaminifu lakini
wao ni waaminifu wa kitu cha makosa.
Miezi miwili baadaye baada ya kuswali tena ili kutafuta maelekezo ya
Mungu, nilihisi kuna kitu kinanidondokea na kuniingia! Nilikaa kitako, na
hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kutumia jina Allah, na nilisema
“Allah, ninakuamini wewe kuwa ni Mmoja na ndiye Mungu wa pekee wa
kweli.” Kulikuwa na amani iliyonishukia na tangu siku hiyo ni miaka mine
imepita hadi kufikia sasa Kamwe sijajuta kuingia kwangu katika Uislamu.
Uamuzi huu haukuja bila ya majaribio. Nilifukuzwa kazi kwani nilikuwa
nafundisha katika shule mbili za Biblia kwa wakati huo, nilitenganishwa na
wanafunzi wenzangu wa zamani, maprofesa na wachungaji, nilikanwa na
7
 Tauhidi ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, yaani kumfanya Mwenyezi Mungu Mpweke- yupo mmoja tu
au ni somo la kumpwekesha Mwenyezi Mungu

49
familia ya mume wangu, nilifahamika vibaya na watoto wangu wakubwa, na
nilikuwa napelelezwa na serikali yangu mwenyewe. Bila ya kuwa na imani
ambayo inamuwezesha mtu kusimama kidete dhidi ya nguvu za shetani
nisingeweza kuhimili mambo yote hayo. Mimi ninamshukuru sana Allah kwa
kuwa mimi ni Mwislamu na naomba niishi na kufa nikiwa ni Mwislamu.
“Sema: “hakika Sala yangu, na ibada zangu (zote nyingine) na uzima wangu,
na kufa kwangu; (zote) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Muumba wa
walimwengu wote. (Likinisibu jambo limenisibu kwa kutaka Mwenyezi Mungu
si kwa kutaka viumbe vyake. Na yote ninayoyafanya nayafanya kwa ajili
Yake). Hana mshirika. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza
wa waliojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu).” Quran 8 6:162-163
Sista Khadija Watson anafanyakazi ya ualimu wa wanawake katika moja ya
vituo vya Da`wah (kuwaita watu waingie Uislamu) kilichopo Jeddah, Falme
ya Kiarabu ya Saudia - Arabia.
8
 Tafsiri za aya za Quran kwa kiswahili zimenukuliwa kutoka QURANI TAKATIFU ya marehemu Sheikh
Abdullah Saleh Al-Farsy

50
5 IBRAHIM KHALIL AHMED (IBRAHIM KHALIL
PHILOBUS) PADRI WA COPTIC NA NI MMISHIONARI
(MISRI).
Al-haji Ibrahimu Ahmad, zamani akiitwa Ibrahim Khalil Philobus, alikuwa ni
padri wa Coptic mwenye asili ya Kimisri aliyejifunza mambo ya itikadi na
kupata digrii ya juu katika chuo kikuu cha Princeton. Alijifunza Uislamu ili
apate mianya ya kuushambulia; kinyume chake akaingia Uislamu akiwa
pamoja na watoto wake wanne, mmoja wao kwa sasa ni profesa mwenye
kung’ara katika chuo kikuu cha Sorbonne, Paris Ufaransa. Kwa njia ya
kuvutia, anatumilia mitindo yake mwenyewe kwa kusema; “nimezaliwa
Alexandria 13/1/1919 na niliingizwa shule ya misheni ya Kimarekani hadi
nilipopata cheti cha elimu ya sekondari hapo hapo. Mnamo mwaka 1942
nikapata diploma katika chuo kikuu cha Asiyut na kisha nikajikita katika
masomo ya dini kama utangulizi wa kujiunga na kitengo cha itikadi. Ilikuwa
si kazi nyepesi kujiunga na kitengo hicho, kwani hakukuwa na mtu atakaye
kujiunga na akakubaliwa ispokuwa awe amepata kupendekezwa kwa
pendekezo maalumu kutoka umoja wa kanisani na vilevile, baada ya kupasi
idadi ya mitihani migumu. Nilipata pendekezo kutoka katika kanisa la Al-
Attareen la Alexandria na pendekezo lingine kutoka mkusanyo wa kanisa wa
Misri ya chini (maeneo ya kaskazini) baada ya kufaulu mitihani mingi ili
kujua uwezo wangu wa kuja kuwa mtu wa dini kisha nikapata pendekezo la
tatu kutoka mkusanyiko wa kanisa la Snodus ambalo linajumuisha makasisi
wa Sudani na Misri.
Kanisa la Snodus liliidhinisha niingie kitengo cha itikadi mwaka 1944 nikiwa
ni mwanafunzi wa bweni. Huko nilijifunza mikononi mwa walimu wa
Kimarekani na Kimisri hadi nilipohitimu mwaka 1948.
Nilipendekezwa, aliendelea, niajiriwe Jerusalemu kama kusingekuwa na vita
vilivyolipuka nchini Palestina mwaka huo huo, kwa hiyo. Nilipelekwa Esna
Misri ya juu (maeneo ya kusini). Mwaka huo huo nilijiandikisha kwa ajili ya
kusomea hoja katika chuo kikuu cha Marekani kilichopo Cairo. Jambo hilo
lilikuwa linahusiana na kazi za Kimishionari kwa Waislamu. Ujuzi na uzoefu
wangu juu ya Uislamu ulianzia katika kitengo cha itikadi nilpojifunza
Uislamu na mifumo yote ambayo kwayo tungeweza kuyumbisha imani ya
Waislamu na kuibua upotoshaji wa ufahamu wao wa dini yao wenyewe.

51
Mwaka 1952 nilipata stashahada yangu ya M.A. katika chuo kikuu cha
Priceton USA na niliajiriwa kama mwalimu katika kitengo cha itikadi huko
Asiyuti. Nilikuwa nafundisha Uislamu katika kitengo hicho hicho vilevile
hatia ya kueneza upotoshaji Uislamu kutoka kwa maadui zake na
wamishionari waliodhidi yake. Katika kipindi hicho niliamua kuongeza
masomo yangu juu ya Uislamu, kwa hiyo, sikusoma vitabu vya wamishionari
peke yake. Nilikuwa najiamini sana kiasi ambacho nikajidhatiti kusoma
mtazamo wa upande mwingine. Kwa hiyo, nilianza kusoma vitabu
vilivyoandikwa na waandishi wa Kiislamu. Vilevile niliamua kusoma Quran
na kuifahamu maana yake. Hili lilitokana na kuvutiwa na mapenzi yangu juu
ya elimu na kusukumwa na shauku ya kuongeza ushahidi zaidi dhidi ya
Uislamu. Matokeo yakawa, hata hivyo, ni kinyume kabisa. Nafsi yangu
ilianza kuyumba na nilianza kuhisi migongano mikali ya ndani kwa ndani
katika nafsi yangu na niligundua Uongo wa kila kitu nilichojifunza na
kukihubiri kwa watu. Lakini sikuweza kujikabili mimi mwenyewe kishujaa na
badala yake nilijaribu kuyashinda mambo hayo ya migogoro ya ndani kwa
ndani na niliendelea na kazi yangu.
Mnamo mwaka 1954, aliongeza bwana Khalil, nilipelekwa Aswan nikiwa ni
katibu mkuu wa misheni ya Ujerumani na Uswizi. Kazi hiyo ilikuwa ni nafasi
yangu ya dhahri lakini kazi yangu hasa ilikuwa ni kuhubiri dhidi ya Uislamu
katika Misri ya juu na hasa hasa kwa Waislamu. Mkutano wa wamishionari
ulifanyika muda huo huko Cataract Hotel mjini Aswani na nilipewa uwanja
wa kuongea. Siku hiyo niliongea kupita kiasi, nikirudia rudia upotoshaji wote
dhidi ya Uislamu; na mwisho wa maneno yangu, ule mgogoro wa ndani kwa
ndani ulinijia tena na nilianza kuipitia upya nafasi yangu.
Akiendelea na mazungumzo yake juu ya kile akisemacho migogoro, bwana
Khalil amesema: “Nilianza kujiuliza kwa nini nilisema na kutenda mambo
yote hayo ambayo nayajua kwa uhakika kabisa kuwa mimi ni mwongo, na
kuwa huo si ukweli? Nikachukua likizo kabla ya kuisha kwa mkutano na
kutoka nje hadi nyumbani kwangu. Nilikuwa ninayumba kikamilifu.
Nilipokuwa natembea kupitia bustani ya umma ya Firiyal, nilisikia aya ya
Quran redioni. Ilikuwa inasema: “Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi
moja la majini lilisikia (Qurani) likasema: ‘Hakika tumesikia Qurani ya
ajabu. ‘Inaongoza katika uongofu; kwa hivyo tumeiamini, hatutamshiriki
yeyote tena na Mola wetu.” (Qurani 72:1-2)

52
“Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini; basi anayemwamini Mola wake
hataogopa kupunjwa wala kutwikwa (kubebeshwa) dhambi (za mtu
mwengine).” (Qurani 72:13)
Nilihisi faraja ya kina usiku huo na niliporudi nyumbani niliupitisha usiku
wote nikiwa peke yangu katika maktaba yangu nikisoma Qurani. Mke wangu
alitaka nimjulishe lengo la kukesha kwangu usiku kucha na nilimweleza
aniache peke yangu. Nilisimama kusoma kwa muda mrefu nikifikiria na
kutafakari juu ya aya; “Lau kama Tungaliiteremsha hii Quran juu ya mlima,
ungaliuona ukinyenyekea (na) kupasuka kwa sababu ya hofu ya Mwenyezi
Mungu. Na hii ni mifano Tunawapigia (Tunawaeleza) watu ili wafikiri.”
(Qurani 59:21) na “Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu
(wengine) kwa Waislamu ni Mayahudi na wale mushirikina (wasiokuwa na
Kitabu), na utawaona walio karibu kwa urafiki na Waislamu ni wale
wanaosema: “Sisi ni Wakristo.” (Hayo) ni kwa sababu wako miongoni mwao
wanavyuoni na wamchao Mungu, na kwa sababu wao (Wakristo)
hawatakabari; (wakijua haki huifuata). Na wanaposikia yaliyoteremshwa
kwa Mtume (na yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona macho yao
yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema:
“Mola wetu! Tumeamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli
huu).” (Na wakilaumiwa kwa kusilimu kwao husema): “Na kwa nini
tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotufikia, na hali tunatumai Mola
wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema?” (Qurani 5:82-84).
Bwana Khalil kisha alinukuu nukuu ya tatu kutoka katika Quran Tukufu
isemayo; “Ambao wanamfuata Mtume, Nabii aliye Ummy (asiyejua kusoma
wala kuandika, na juu ya hivi atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya
Uislamu), ambaye wanamuona ameandikwa kwao katika Taurati na Injili
ambaye anawaamrisha mema na anawakataza yaliyo mabaya, na
kuwahalalishia vizuri na kuwaharamishia vibaya, na kuwaondolea mizigo
yao na minyororo iliyokuwa juu yao (yaani sharia ngumu za zamani na mila
za kikafiri). Basi wale waliomwamini yeye na kumuhishimu na kumsaidia na
kuifuata Nuru iliyoteremshwa pamoja naye (yaani Qurani) hao ndiyo wenye
kufaulu. Sema (Ewe Nabii Muhammad): “Enyi watu; Hakika mimi ni Mtume
wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote; (Mungu) ambaye anao ufalme wa
mbingu na ardhi, hapana aabudiwaye (kwa haki) ila Yeye; Yeye ndiye
Ahuishaye na ndiye Afishaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume
Wake, aliye Nabii Ummy (asiyejua kusoma na wala kuandika) ambaye

53
humuamini Mwenyezi Mungu na maneno Yake. Na mfuateni yeye ili mpate
kuongoka.” (Qurani 7:157-158).
Kwa sasa yaani usiku ule ule, Bwana Khalil kama mchezo wa kuigiza
alihitimisha: “Nilichukua uamuzi wangu wa mwisho. Wakati wa asubuhi
nilizungumza na mke wangu ambaye nilizaa naye watoto wa kiume watatu na
wa kike mmoja. Lakini haukupita muda mrefu hadi akadadisi kuwa mimi
naelekea kuingia Uislamu naye akalia na kuomba msaada kwa mkuu wa
misheni. Jina lake lilikuwa ni Monsieur Shavits kutoka Uswizi. Bwana huyo
alikuwa ni mtu mjanja sana. Aliponiuliza kuhusu mtazamo wangu wa kweli,
nilimwambia kinaganaga kile nilichokuwa nakitaka na kisha akasema: Hebu
jifanye kuwa upo nje ya kazi hadi tutakapojua nini kimekutokea. Kisha
nilisema: hii ndiyo barua yangu ya kuacha kazi. Alijaribu kunikinaisha
niahirishe jambo hilo, lakini mimi niling`ang`ania. Kwa hiyo, yeye
akatengeneza uvumi kwa watu kuwa nimekuwa chizi. Kwa hiyo, niliteseka
vikali kwa mtihani huo mkali na ukandamizwaji hadi nilipoondoka na
kuuacha mji wa Aswan kwa wema na kurudi Cairo.”
Alipoulizwa juu ya hali ya kubadili kwake dini alijibu: “Mjini Cairo
nilitambulishwa kwa profesa mmoja anaheshimika sana ambaye alinisaidia
kuyashinda majaribu yangu yaliyokuwa makali mno na alifanya hivyo bila ya
kujua chochote juu ya mkasa wangu. Alinitendea kama Mwislamu kwani
nilijitambulisha kwake hivyo ingawa hadi wakati huo nilikuwa sijaingia
Uislamu kirasmi. Huyo bwana alikuwa ni: Dr. Muhammad Abdul Moneim Al
Jamal ambaye ni mtunza hazina mkuu. Naye alikuwa anajishughulisha na
masomo ya Kiislamu na alitaka kutafsiri Quran Tukufu ikachapishwe
Marekani. Aliniomba nimsaidie kwa sababu nilikuwa nafahamu vizuri
Kingereza kwa kuwa nilipata stashahada yangu ya M.A katika chuo kikuu cha
Marekani. Pia alijua kuwa nilikuwa najiandaa kufanya uchunguzi wa
mlinganisho wa Quran, Taurati na Biblia. Tukashirikiana katika uchunguzi
huo wa mlinganisho na katika kutafsiri Quran. Wakati: Dr. Jamal alipojuwa
kuwa nimeacha kazi huko Aswan na kwa hiyo, sina kazi, alinisaidia kwa
kunipatia kazi katika shirika la Standard Stationary mjini Cairo. Kwa hiyo,
nilijiunda vizuri baada ya muda mfupi. Sikumwambia mke wangu nia yangu
ya kuingia Uislamu kwa hiyo, alifikiria kuwa nimeshasahau mambo yote na
sikuwa na lolote ila ni mgogoro wa mpito ambao haupo tena. Lakini, nilijua
vizuri kabisa kuwa kusilimu kwangu kirasmi na kuingia Uislamu kunahitaji
majaribio ya kutatanisha marefu na kwa hakika ilikuwa ni vita ambavyo

54
nilipendelea kuviahirisha kwa muda hadi pale nitakapoimarika na baada ya
kukamilisha uchunguzi wangu wa mlinganisho.”
Kisha Bwana Khalil aliendelea; “Mnamo mwaka 1955 nilikamilisha
uchunguzi wangu na mambo yangu ya kiuchumi na kimaisha yakaanza kuwa
mazuri. Nikaacha kazi kutoka katika lile shirika na nikaanzisha ofisi ya
kufundisha uagizaji wa vifaa vya kuandikia na vyombo vya mashuleni.
Ilikuwa ni biashara iliyofanikiwa sana kutokana na biashara hiyo nilichuma
pesa nyingi zaidi kuliko vile nilivyohitaji. Kwa hiyo, nikaamua kutangaza
rasmi kusilimu kwangu nakuwa Mwislamu rasmi. Mnamo 25/12/1959,
nilimtumia telegramu Dr. Thompson, kiongozi wa misheni ya Marekani
nchini Misri nikimjulisha kuwa nimeingia Uislamu. Nilipomweleza: Dr.
Jamal mkasa wangu wa kweli alishangazwa sana. Nilipotangaza kusilimu
kwangu na kuingia Uislamu, matatizo mapya yalianza. Watu saba miongoni
mwa jamaa zangu wa zamani katika misheni walijaribu kwa kila hali
kunishawishi niondoe tangazo langu, lakini nilikataa. Wakatishia kunitenga
na mke wangu na nikawaambia: yupo huru kufanya atakavyo. Wakatishia
kuniua. Lakini waliponikuta nipo imara waliniacha peke yangu na
wakaniletea rafiki yangu wa zamani ambaye naye pia alikuwa ni mwenzangu
katika misheni. Naye akalia sana mbele yangu. Kwa hiyo, nilimsomea mbele
yake aya zifuatazo kutoka katika Quran: “(Hayo) ni kwa sababu wako
miongoni mwao wanavyuoni na wamchao Mungu, na kwa sababu wao
(Wakristo) hawatakabari; (wakijua haki huifuata). Na wanaposikia
yaliyoteremshwa kwa Mtume (na yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona
macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua;
wanasema: “Mola wetu! Tumeamini, basi tuandike pamoja na
wanaoshuhudia (ukweli huu).” (Na wakilaumiwa kwa kusilimu kwao
husema): “Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotufikia, na
hali tunatumai Mola wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema?”
(Qurani 5:84).
Nikamwambia, “ulitakiwa ulie kwa unyenyekevu mbele ya Mungu kwa
kusikia Quran na kuamini ukweli ambao unaujua lakini unaukataa. Alisimama
na kuondoka na kuniacha kwa vile alivyoona kuwa hakuna njia. Kusilimu
kwangu kirasmi na kuingia Uislamu kulikuwa Januari 1960.”
Kisha bwana Khalil aliulizwa kuhusiana na mtazamo wa mkewe na watoto
wake, naye akasema: “Mke wangu aliniacha kwa muda huo na akachukua
vyombo vya nyumbani vyote akaondoka navyo; lakini watoto wangu wote

55
waliungana nami na kuingia Uislamu. Na aliyekuwa na shauku sana miongoni
mwao alikuwa ni mtoto wangu mkubwa Isaac ambaye alibadili jina lake na
kuwa Osmani, kisha mtoto wangu wa pili Joseph (Yusufu) na mwanangu
Samuel ambaye jina lake lilikuwa Jamal na binti yangu Majida ambaye kwa
sasa anaitwa Najwa. Osmani kwa sasa ni Dakitari wa falsafa anaefanyakazi ya
uhadhiri katika chuo kikuu cha Sorbonne mjini Parisi akifundisha masomo ya
utamaduni wa kimashariki na saikolojia. Pia ni mwandishi katika jarida la “Le
monde.” Kwa kumtazama mke wangu, aliiacha nyumba kwa miaka sita na
akakubali kurudi mnamo mwaka 1966 huku akisisitiza kuwa ataendelea na
dini yake. Nilimwambia: sitaki uwe Mwislamu kwa ajili yangu lakini ni baada
ya kukinai tu. Naye kwa sasa alihisi kuwa anaamini Uislamu lakini hawezi
kutangaza jambo hilo kwa kuiogapa familia yake lakini sisi tulimtendea kama
ni mwanamke wa Kiislamu na alikuwa akifunga Ramadhani kwa sababu
watoto wangu wanaswali na kufunga. Binti yangu Najwa ni mwanafunzi
katika kitengo cha biashara, Joseph ni Dakitari mtaalamu wa madawa na
Jamal ni injinia.
Katika kipindi hiki, ambacho ni tangu 1961 hadi muda huu nimeshachapisha
idadi kubwa ya vitabu juu ya Uislamu na mifumo ya kimishionari na
utaalamu wa mambo ya mashariki dhidi ya jambo hilo. Kwa sasa najiaandaa
na uchunguzi wa mlinganisho juu ya wanawake katika dini tatu huku nikitilia
umuhimu nafasi ya mwanamke katika Uislamu. Mwaka 1973 nilifanya hija na
ninafanya kazi za kuhubiri Uislamu. Ninafanya semina mbali mbali katika
vyuo vikuu na jumuia za wahisani. Nimepokea mwaliko kutoka Sudani
mwaka 1974 ambako nilifanya semina nyingi. “Muda wangu wote unatumiwa
kwa kuuhudumia Uislamu na shukrani ni za Allah kwa sababu kwa juhudi
zangu mapadri wengi na watu wengi wamesilimu na kuwa Waislamu.”
Mwisho kabisa Bwana Khalil aliulizwa juu ya vitu vilivyomvutia sana katika
Uislamu. Na kujibu: “Imani yangu katika Uislamu imeletwa kupitia kusoma
Quran Tukufu na historia ya Mtume Muhammad, amani iwe juu yake. Kwa
sasa siamini upotoshaji dhidi ya Uislamu na hasa hasa nimevutiwa na itikadi
ya Upweke wa Mwenyezi Mungu, kwani hiyo ndiyo picha muhimu sana ya
Uislamu. Mungu ni mmoja tu. Hakuna kitu kinachofanana naye. Imani hii
inanifanya niwe mja wa Mungu peke yake na si kwa mwingine. Upweke wa
Mungu unamkomboa mtu kutoka katika utumwa kwa mtu yeyote na huo
ndiyo uhuru wa kweli.

56
Pia ninapenda sana sheria ya kusamehe katika Uislamu na mafungamano ya
moja kwa moja kati ya Mungu na mja wake.
“Sema, “Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na
rehema ya Mwenyezi Mungu; bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi
zote; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu. “Na
rejeeni kwa Mola wenu na mnyenyekee Kwake kabla ya kukujieni adhabu
kisha hamtanusuriwa.” (Quran 39:53-54)
Chanzo: Habari za Kiislamu, San Francisco, (A 94141 – 0186)

57
6- MARTIN JOHN MWAIPOPO ALIYEKUWA KASISI MKUU
WA KILUTHERANI (TANZANIA).
Ilikuwa ni Desemba 23, 1986, siku mbili kabla ya Krismasi, wakati Askofu
mkuu Martin John Mwaipopo, alipotangaza kwa makutano yake kuwa
anauacha Ukristo na kuingia Uislamu.
Yale makutano yalipooza kwa mshtuko wa kusikia habari hiyo walishtushwa
sana kabisa kiasi ambacho msimamizi wake alisimama kutoka kitini kwake,
akafunga milango na madirisha na kutangaza kwa wanakanisa kuwa akili ya
Askofu imeganda, yaani amechizika. Vipi ashindwe kufikiria na kusema
hivyo, wakati katika kipindi cha dakika chache tu zilizopita, mtu huyo huyo
alichukua kifaa chake cha muziki na kuimba kwa kucheza cheza sana na
kuliimbia kanisa? Ni kidogo mno walichokijua cha ndani ya moyo wa Askofu
kama kulikuwa na uamuzi ambao utawapasua akili zao, na burudani ile
ilikuwa ni sherehe ya kuagana tu. Lakini hisia za makutano zilifadhaishwa
sana, naam! Wakawaita polisi waje wamwondoshe mwendawazimu”
Akawekwa kolokoloni hadi mida ya usiku wa saa sita ndipo Sheikh Ahmed
Sheikh, mtu aliyemwingiza katika Uislamu alipoenda kumtoa. Tukio hilo
lilikuwa ni mwanzo mdogo mdogo wa mshtuko uliojificha dhidi yake.
Magazeti yote ya habari za Qalam, Simphiwe Sesanti, yalizungumzia juu ya
mtu aliyezaliwa Tanzania na aliyekuwa Askofu mkuu wa Kilutherani Bwana
Martin John Mwaipopo, aliyeingia Uislamu amekuja na kujulikana kuwa ni
Al-Haji Abu Bakar Mwaipopo.)
Sifa lazima ziende kwa ndugu wa Kizimbabwe, Sufiyan Sabelo, kwa
kusababisha huu udadasi wa maandishi, baada ya kusikiliza maneno ya
Mwaipopo katika kituo cha Kiislamu cha Wyebank mjini Durban. Sufyan si
mpiga debe, lakini usiku huo lazima atakuwa amesikia kitu naye hakusimama
kuongelea kuhusu mtu huyo! Ambaye hataathiriwa baada ya kusikia hayo
naye ni Askofu mkuu, ambaye hakuwa na stashahada ya BA na Uzamili peke
yake, lakini pia alikuwa na stashahada ya udakitari wa falsafa, ya mambo ya
kiitikadi, mwishowe amebadilika na kuwa Mwislamu? Na kwa kuwa vigezo
vya kigeni ni muhimu sana kwake, basi huyo mtu alipata diploma ya uongozi
wa kanisa nchini Uingereza na baadaye digrii, mjini Berlin, Ujerumani! Mtu
ambaye, kabla hajakuwa Mwislamu, alikuwa ni katibu wa Baraza la makinisa
ulimwenguni kwa nchi za Afrika mashariki – zikiwemo Tanzania, Kenya,
Uganda, Burundi, na sehemu za Ethiopia na Somalia. Katika baraza la

58
makanisa, alikuwa anagusana mabega na mwenyekiti wa sasa wa kamishna
ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini. Bw. Barney Pityana na mwenyekiti
wa tume ya ukweli na maridiano, Askofu Dasmound Tutu.
Hiki ni kisa cha mtu aliyezaliwa miaka 61 iliyopita, mwezi februari tarehe 22
huko Bukoba, eneo linalopakana na Uganda. Miaka miwili, baada ya
kuzaliwa kwake, familia yake ilimbatiza, na miaka mitano baadaye,
walimtazama kwa jicho la fahari na wakitarajia kuwa atakuwa kijana wa
mageuzi. Kwa kumuona anamsaidia mchungaji wa kanisa, kuandaa “mwili na
damu” ya Kristo, walimjaza Mwaipopo fahari, na walimjaza Mwaipopo
mkubwa, wazo zuri juu ya mustakabali wa mwanawe.
“Nilipokuwa katika shule ya bweni, hapo baadaye, baba yangu aliniandikia”,
akieleza kuwa ananitaka niwe padri. Aliandika hivyo, katika kila barua
aliyoiandika” Anakumbuka bwana Abuu Bakri. Lakini Mwaipopo alikuwa na
mawazo binafsi juu ya maisha, ambayo ni kujiunga na jeshi la polisi. Lakini
alipofikia umri wa miaka 25, aliacha mawazo yake na akasalimu amri kwa
matakwa ya baba yake. Na hii ni kinyume na huko Ulaya ambako watoto
wanaweza kufanya watakavyo baada ya kufikia umri wa miaka 21, lakini
Afrika, watoto wamefunzwa kuheshimu matakwa ya wazazi wao kinyume na
matakwa yao binafsi.
“Mwanangu kabla sijafumba macho (sijafa), nitafurahi sana kama utakuwa
padri.” Hivyo ndivyo baba ya alivyomweleza mwana, na hivyo ndivyo mtoto
alivyoenenda, mwendo ambao ulimshuhudia akielekea Uingereza mnamo
mwaka 1964, kusomea diploma ya Uongozi wa kanisa na mwaka mmoja
baadaye alienda Ujerumani kusomea BA. Alipokuwa anarudi mwaka mmoja
baadaye, alisimikwa na kuwa Askofu anayetoa huduma.
Baadaye alienda tena kuchukua Stashahada ya Uzamili. “Muda wote huo,
nilikuwa nafanya vitu bila ya kuuliza.” Na ilikuwa pale alipoanza kufanya
‘uzamili wake’ ndipo alipoanza kuuliza vitu. “Nilianza kushangazwa … kuna
Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Ubudha na kila dini inadai kuwa yeye ndiyo ya
kweli. Ukweli ni upi? Nilitaka ukweli”, anasema Mwaipopo. Kwa hiyo,
akaanza uchunguzi wake, hadi alipopunguza dini hizo na kubakisha dini kuu
“nne.” Akajipatia nakala ya Quran, na kutabiri nini kitatokea?
“Nilipoifungua Quran, Aya za kwanza kabisa nilizozisogelea zilikuwa ni za
“surati Ikhlasi” “Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja (tu). Mwenyezi

59
Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe Vyake vyote kwa
kumwabudu na kumuomba na kumtegemea). Hakuzaa wala Hakuzaliwa.
Wala hana anaefanana Naye hata mmoja.” Anakumbuka jambo hilo. Na hiyo
ilikuwa pale mbegu za Uislamu, hazijulikani kwake na zilikuwa ni mara ya
kwanza kuonekana. Na ilikuwa ni hapo alipogundua kuwa Qurani ndicho
Kitabu cha pekee kisichovurugwa na wanadamu tangu kilipoteremshwa. “Na
katika kuhitimisha uchunguzi wangu wa uzamili nilisema hivyo. Sikujua
kama watanipa stashahada yangu ya uzamili au hawanipi – huo ndiyo
uliokuwa ukweli, na nilikuwa nautaka ukweli.”
Alipokuwa katika hali hiyo ya kiakili alimwita profesa wake ampendaye sana:
bwana Van Burger. “Nilifunga mlango, na kumwangalia machoni na
kumuuliza “katika dini zote duniani ni ipi ya ukweli?” Akajibu ni Uislamu.
“Kwa nini wewe si Mwislamu? Niliuliza tena. Akaniambia: “Mosi,
nawachukui Waarabu, pili, Je, unaviona vitu vya anasa vyote hivi
niliovyonavyo? Je, unadhani itakuwaje kama nitavitupa vitu vyote hivi kwa
ajili ya Uislamu?” Nilipofikiri kuhusu majibu yake, pia nilifikiria nafsi yangu
mwenyewe.” Anakumbuka Mwaipopo. Kazi yake, gari zake, vyote hivyo
katika taswira yake. Hapana, hatoingia Uislamu, na kwa mwaka mmoja
madhubuti, aliliweka jambo hilo nje ya akili yake. Lakini baadaye ndoto
zilikuwa zikimjia kwa kumsumbua, Aya za Quran ziliendelea kumtokea, watu
waliovalia nguo nyeupe waliendelea kumjia. “Hasa hasa siku za Ijumaa; hadi
alipofikiria kuwa hawezi kuvumilia tena jambo hilo.
Kwa hiyo, mnamo tarehe 22 Desemba, aliingia Uislamu kirasmi. Ndoto hizo
zilizomwongoza - Je, hazikuwa za “kishirikina” kama ilivyo kwa tabia za
Kiafrika? “Hapana, siamini kuwa ndoto zote ni mbaya. Kwani kuna zile
ambazo zinakuongoza katika mwelekeo sahihi, na kuna nyingine hazifanyi
hivyo, na za kwangu, kwa upekee kabisa zimeniongoza katika mwelekeo
sahihi, kuufikia Uislamu,” ametueleza.
Kwa hiyo, kanisa lilimnyang`anya nyumba na gari. Mkewe hakuweza
kuvumilia hayo, akafungasha virago vyake, akachukua watoto wake na
kuondoka, licha ya Mwaipopo kumuhakikishia kuwa halazimishwi awe
Mwislamu. Mwaipopo alipoenda kwa wazazi wake nao pia, walikuwa
wameshasikia habari zake. “Baba yangu aliniambia niukane Uislamu na
mama yangu, yeye alisema: “Hataki kusikia upuuzi wowote kutoka kwangu;”
alikumbushia Mwaipopo. Naye alikuwa kivyake vyake! Aliulizwa vipi
anajihisi hivi sasa kwa upande wa wazazi wake, anasema kuwa

60
nimeshawasamehe, kwa hakika alipata muda wa kusuluhishwa na baba yake
kabla hajaiaga dunia.
“Hao wazazi walikuwa ni wazee wasiojiweza. Walikuwa hawajui hata
kuisoma Biblia… Chote walichokijuwa ilikuwa ni kile walichokisikia
kikisomwa na mapadri” anaelezea. Baada ya kuomba akae kwa usiku mmoja
tu, mchana uliofuatia, alianza safari yake ya kuelekea kule kwenye asili ya
wazazi wake, Kyela, karibu na mpaka kati ya Tanzania na Malawi. Wazazi
wake walifanya makazi mjini Kilosa, Morogoro. Katika safari yake hiyo,
alikwamia Basale, kwa familia moja ambayo ilikuwa inauza pombe
zilizosindikwa nyumbani. Na ilikuwa ni hapo ndipo alipokutana na mkewe
wa baadaye, ambaye ni mtawa wa Kikatoliki, jina lake ni Sista Gertrude
Kibweya, kwa sasa anajulikana kwa jina la Sister Zainabu. Na ilikuwa ni
pamoja naye ndipo Mwaipopo aliposafiri hadi Kyela, ambako yule mzee,
aliyempa hifadhi kwa usiku uliopita alipomwambia kuwa hiyo ndiyo namna
Mwaipopo atavyowapata Waislamu wengine. Lakini kabla ya hivyo, wakati
wa asubuhi ya siku hiyo alipopiga adhana, kitu kilichowafanya wanakijiji
watoke, huku wakimuuliza mwenyeji wake kwa nini alikuwa anamuhifadhi
“mwendawazimu.” Alikuwa ni yule mtawa ndiye aliyeeleza kuwa mimi
sikuwa mwendawazimu, ispokuwa ni Mwislamu” anasema Mwaipopo. Na
alikuwa ni mtawa huyo huyo aliyemsaidia Mwaipopo hapo baadaye kulipia
ada ya matibabu katika hospitali ya Misheni ya Kianglikana, alipokuwa
mgonjwa sana, shukrani kwa mazungumzo aliyoyafanya na mtawa huyo.
Kisa chenyewe kinaenda hivi, Mwaipopo alipomuuliza mtawa huyo kwa nini
alikuwa anavaa shanga ya Rozali, naye akajibu kuwa ni kwa sababu Yesu
Kristo alisulubiwa msalabani. “Lakini, hebu sema, kama mtu amemuua baba
yako na bunduki, Je, utatembea huku umebeba bunduki kifuani kwako?”
Mmmhhh. Hilo lililmfanya yule mtawa afikirie, akili zake zikapata
“changamoto”, na Askofu wa zamani alimuomba amuoe hapo baadaye,
jawabu lilikuwa “sawa”. Walioana kwa siri, na wiki nne baadaye, huyo
mtawa aliandika barua kwa viongozi wake, akiwajulisha kuwa anaondoka.
Wakati yule mzee aliyempa hifadhi Mwaipopo, (mjomba wa mtawa)
aliposikia juu ya ndoa hiyo, na Mwaipopo na mkewe walipofika nyumbani
kwa mzee huyo, walishauriwa wahame nyumba hiyo, kwa sababu “yule mzee
alikuwa anashindilia bunduki yake”, na Baba wa yule mtawa alikasirika sana,
“alikuwa mkali kama simba”.

61
Kutoka katika kasri la Askofu, Mwaipopo alienda kuishi katika nyumba
aliyoijenga mwenyewe nyumba ya udongo. Kutoka alipokuwa akijipatia
matumizi ya maisha yake kwa kazi ya ukatibu mkuu wa baraza la makanisa
Duniani kwa nchi za Afrika mashariki, akaanza kujipatia pato la maisha yake
kwa kuuza kuni na kulimia mashamba ya watu wengine. Na wakati alipokuwa
hafanyi kazi hizo (anapomaliza) alikuwa anahubiri Uislamu wazi wazi. Hilo
lilimpelekea, kwa muda mfupi atiwe kolokoloni kwa kuhubiri kwa kuukashifu
Ukristo.
Alipokuwa Hija 1988, ulimpata msiba mkubwa, nyumba yake ililipuliwa kwa
bomu, na matokeo yake, vitoto vyake vitatu vilivyokuwa mapacha viliuwawa.
“Askofu, ambaye mama yake na mama yangu walikuwa ni watoto wa baba
mmoja, alishiriki katika njama hizo” anakumbushia Mwaipopo. Anasema
badala ya kumvunja moyo, tukio hilo lilifanya kinyume chake, kwani idadi ya
watu walioingia Uislamu, iliongezeka, na idadi hiyo ikijumuisha baba mkwe
wake.
Anasema kuwa kila siku anayoachwa huru, basi polisi walienda kumkamata
tena. Hebu tabiri ni kitu gani? “Wanawake wakasema: haiwezekani!
Watatumia nguvu dhidi ya polisi kuzuia asikamatwe. Pia, walikuwa ni
wanawake waliomsaidia kuvuka mpaka bila ya kujulikana. Walimvalisha
nguo za kike! Kwa mujibu wa kauli ya Mwaipopo. Na hilo ni moja ya sababu
inayomfanya awaheshimu sana wanawake.
“Wanawake lazima wapewe nafasi kubwa, lazima wapewe elimu bora katika
Uislamu. Vinginevyo, vipi mwanamke atafahamu kwa nini mwanamume
anaoa zaidi ya mke mmoja… Alikuwa ni mke wangu, Zainabu, aliyetoa
ushauri wa kuoa mke wa pili, Shela (rafikiye), wakati mke wangu
alipolazimika kwenda ng`ambo kusomea Uislamu.” Ni Askofu asemayo hayo.
Ndiyo?
Kwa Waislamu, Al-Haji Abuu Bakri Mwaipopo ana ujumbe huu: “Kuna vita
dhidi ya Uislamu… Epukeni dunia ya maneno matupu. Sasa hivi, Waislamu
tumefanywa tuone aibu kwa kuwa tunahesabiwa ni siasa kali. Waislamu
lazima tuache mifarakano. Waislamu lazima tuungane.
Chanzo: hhttp://mandla.co.za/al-qalam/sept97/bishop.htm

62
7- RAPHAEL NARBAEZ ALIYEKUWA MCHUNGAJI WA
MASHAHIDI WA YEHOVA (USA)
ﻪﺗﺭﻮﺻ
Latino, Raphael mwenye miaka arobaini na mbili ni mchekeshaji mwenye
kufanya maskani yake Los Angeles na ni muhadhiri wa chuo kikuu. Alizaliwa
Texas, sehemu ambayo ndiyo aliyohudhuria ushahidi wake na miaka minne
baadaye aliyaelekea makutano yake mwenyewe akiwa na miaka ishirini, na
alipewa nafasi ya uongozi kwa Mashahidi wa Yehova 904,000 laki tisa na
elfu nne nchini (USA). Aliiuza Biblia yake kwa Quran baada ya kupata
ushujaa wa kutembelea msikiti wa mtaani.
Novemba 1, 1991, aliingia Uislamu, huku akiiletea jamii ya Waislamu ujuzi
wa kuunda usharika na kuuzungumzia alioupata miongoni mwa Mashahidi
wa Yehova. Yeye huongea na Waislamu wapya kwa haraka haraka, lakini
yeye ni mmoja wa wale wanaoweza kuwafanya wanaohamia Uislamu
wajichekee.
Alisimulia kisa chake kwa mtindo wa kuigiza, nakumbuka wazi wazi
nilikuwa katika mjadala ambao sote tulikuwa tumekaa katika sebule ya
wazazi wangu na kulikuwa na baadhi ya Mashahidi wa Yehova wengine.
Walikuwa wanaongelea juu ya: “Vita kati ya wema na uovu; muda wa
Mwisho! Na Kristo anakuja! Na wajua tena, mvua ya mawe itakuwa na
matone makubwa kama gari ndogo! Mungu atatumia vitu aina zote vya
kuungamiza mfumo huu mbaya na kuondosha serikali! Na Biblia
inayozungumzia dunia itafunguka! Itameza magorofa ya mji mzima”
Naogopa sana kifo! Kwa hiyo, mama yangu alinigeukia: “Tazama
kitakachotokea kama hutobatizwa, na hutofanya matakwa ya Mungu? Dunia
itatumeza, au moja ya mawe hayo makubwa mno litakupiga juu ya kichwa na
litakuangusha, na hautoishi tena. Nami nitalazimika kutengeneza mtoto
mwingine.”

63
Sikutaka kuchukua nafasi ya kugongwa na moja ya mawe hayo ya mvua
yaliyo makubwa. Kwa hiyo, nikabatizwa. Bila shaka mashahidi wa Yehova
hawaamini kunyunyiza maji. Wao wanakuzamisha kabisa kabisa,
wanakuacha ndani ya maji hayo kwa sekunde moja, kisha wanakutoa.
Nilifanya hivyo nikiwa na miaka 13, Septemba 7, 1963 mjini Pasadena,
Calfornia, katika birika la Rose Bowl. Ilikuwa ni mkutano wa kimataifa
mkubwa sana. Tulikuwa watu 100,000 laki moja. tuliendesha magari kutokea
Lubbock, Texas.
Hatimaye nilianza kutoa maneno makubwa – dakika kumi mbele ya mkutano.
Na kundi la wahudumu wa sinema walinipendekeza nitoe muhadhara wa saa
moja ambao ulifanyika Jumapili walialikwa watu wengi. Wao kikawaida
huwa wanayahifadhi mahubiri hayo kwa ajili ya wazee wa makutano.
[Kwa sauti ya mamlaka:] “Kwa hakika ni ndogo, Lakini anaweza kukamata
jambo hilo. Yeye ni kijana wa Kikristo mzuri. Hana maovu, na ni mtiifu kwa
wazazi wake na anaonekana ana elimu bora na kubwa sana ya Biblia.”
Kwa hiyo, nikiwa na miaka kumi na sita nilianza kutoa muhadhara wa saa
moja mbele ya makutano yote. Kwanza kabisa niliandikwa katika kikundi
kilichopo Sweetwater, Texas, na Kaosha, hatimaye, mjini Brownfield, Texas,
nilipopata makutano yangu ya kwanza. Katika umri wa miaka ishirini,
nilikuwa ni kile wakiitacho mchungaji chipukizi (mtangulizi).
Mashahidi wa Yehova wana mpango wa mafunzo wa kisasa sana, wana aina
mfumo wa haki. Unalazimika kutenga masaa kumi hadi kumi na mbili kwa
mwezi ya kuhubiri nyumba kwa nyumba. Ni kama muuza biashara. IBM
haifai chochote kwa vijana hao.
Kwa hiyo, nilipokuwa mchungaji mtangazaji, nilitenga muda wangu mwingi
kufanya utumishi wa nyumba kwa nyumba. Nilikuwa nalazimika kufanya
hivyo kiasi cha masaa mia moja kwa mwezi, na nililazimika kuwa na masomo
saba ya Biblia. Nilianza kuwahubiria makutano mengine. Nilikubaliwa katika
shule ya Brooklyn, New York, ni shule ya tabaka bora sana waimilikayo
Mashahidi wa Yehova “the Crème de la crème, ni ya kwanza kwa kuwa na
asilimia kubwa. Lakini sikuenda.

64
Vitu vichache ambavyo kwa sasa haviniingii akilini. Kwa mfano, mfumo wa
sehemu ya haki. Jambo hilo linaonekana kama vile kila mara nilipotaka
kupinda kona nakujikuta katika nafasi nyingine ya majukumu, nililazimika
vitu hivyo vya kisekyula ili kuuthibitisha uungu wangu. Hiyo ni kwa kuwa
kama utafikia malengo ya sehemu yako ya haki ya mwezi huu, Mungu
anakupenda. Na kama hutafikia sehemu yako ya haki katika mwezi unaofuata
Mungu hakupendi. Jambo hilo halikuniingia akilini kabisa kabisa. Mwezi
mmoja ananipenda na mwezi mwengine hanipendi?
Kitu kingine nilichoanza kukiona ni mtazamo wa njia ya chini. Mashahidi wa
Yehova ni watu pekee watakaookolewa katika mpango mpya wa Mungu,
hakuna mtu mwingine atakayeokoka, kwa sababu, watu hao wanatekeleza
dini ya uongo. Sawa, nilifikiria: mama Tereza wa Kikatoliki. Huyo ni adui
yetu wa kutisha. Kwa hiyo, nilisema ngoja kidogo mama Tereza ametoa
maisha yake yote akifanya vitu alivyosema Yesu: kuwalea masikini,
wagonjwa na mayatima. Lakini hatopata huruma za Mungu kwa sababu ni
Mkatoliki?
Tulikuwa tunalikosoa kanisa la Kikatoliki kwa sababu Wakatoliki wana mtu
ambaye ni padri, wanamwendea na kuungama dhambi zao kwake. Na tuna
msemo “Usiende kwa mtu kuungama dhambi zako! Dhambi zako ni dhidi ya
Mungu!” Ndiyo sisi tulienda kwa baraza la wazee. Unaungama dhambi zako
kwao, na wao wanakuwekea mkono, na walisema [mzee ni kama oporeta wa
simu:] “Jizuie kwa dakika moja hivi … unafikiri nini, bwana? Hapana? …
sawa, samahani tumejaribu vya kutosha lakini wewe bado hujatibika vya
kutosha. Dhambi zako ni kubwa mno, kwa hiyo, ima upoteze ufuasi wako
kanisani au upelekwe majaribuni.”
Ikiwa dhambi ni dhidi ya Mungu, Je, sikupaswa nimwelekee Mungu moja
kwa moja na kumuomba msamaha?
Uhenda msumari uliogongelewa jeneza ulikuwa ni ule ule niliouna kuwa wao
waliianza kuisoma Biblia kidogo tu. Mashahidi wa Yehova wana vitabu vya
kila kitu ambavyo vimetayarishwa na mnara wa wachunguzi wa Biblia na
jumuia ya vitabu vya dini watu pekee katika sayari nzima ya dunia
wanaoweza kujua namna ya kutafsiri maandiko ya Biblia kisawa sawa ni
kundi la wanaume wa tume ya Brooklyn, ambao wanawaambia Mashahidi wa
Yehova ulimwengu mzima wavae vipi, waseme nini, watumie vipi maandiko
matakatifu, na wakati ujao utakuwaje. Mungu amewaambia wao, kwa hiyo,
wao nao wanaweza kutwambia sisi. Niliviheshimu vitabu hivyo. Lakini kama

65
Biblia ndicho kitabu cha elimu na ikiwa Biblia ni mafundisho ya Mungu,
vizuri, Je, hatupaswi kupata majibu yetu kutoka katika Biblia? Paulo
mwenyewe alisema jitafutie mwenyewe kile cha kweli na maneno ya Mungu
yanayokubalika. Usiruhusu watu kuyazuga masikio yako.
Nilianza kusema: “Usihofu sana juu ya kile kinachosemwa na mnara wa
wachunguzi – soma Biblia wewe mwenyewe.” Masikio yalianza kusimama na
kusikiliza kwa makini.
[Old Southerner`s drawl:] “Nadhani tumejipatia uasi hapa, hoji,. Yup.
Nadhani kijana huyu wa zamani ni {one taco short} la kitu fulani.”
Hata baba yangu alisema: “Bora uchunguze, wewe kijana, huo ni usemi wa
pepo wabaya huo. Hayo ni majaribio ya pepo wabaya kutaka kuingia na
kusababisha mgawanyiko.”
Nilisema: “Baba, hayo si mambo ya pepo wabaya. Watu hawahitaji kusoma
sana haya machapisho mengine. Wanaweza kupata majibu yao kwa kusali na
ndani ya Biblia.”
Kiroho sikuwa tena, nahisi wepesi. Kwa hiyo mnamo mwaka 1979, nikijua
kwamba sikuweza kuendelea, niliacha, sikuridhika na nikiwa nasikia ladha
mbaya mdomoni, kwa sababu nimeshayaweka maisha yangu yote, roho
yangu, moyo, na akili kanisani. Hilo lilikuwa tatizo. Sikuliweka kwa Mungu.
Nimeliweka katika mipango iliyosukwa na watu.
Siwezi kwenda katika dini nyingine. Nikiwa ni Shahidi wa Yehova,
nimeshafundishwa, kupitia maandiko, kuonyesha kuwa dini nyingine zote ni
za makosa. Yale masanamu ni kitu kibaya. Utatu wa Mungu haupo.
Mimi ni sawa sawa na mtu asiye na dini. Lakini sikuwa mtu asiye na Mungu.
Lakini wapi nitakapoweza kupaendea?
Mnamo mwaka 1985 nilamua kwenda Los Angeles na kujiunga na shoo ya
Johnny Carson na kufanya utambulisho wangu kuwa ni mwana maigizo mkuu
na ni mcheza sinema. Daima nilikuwa nahisi kuwa, kama vile nimezaliwa
kwa ajili ya kitu fulani. Sikujua kama kitapatikana, dawa ya kutibu kansa au
nitakuwa mcheza sinema. Niliendelea kusali na jambo hilo lilizuiwa kwa
muda mchache.

66
Kwa hiyo, nilienda katika kanisa Katoliki lilokaribu na nyumba yangu, na
nilijaribu kufanya jambo hilo. Nakumbuka siku ya Jumatano ya majivu hayo
ya msalaba katika paji la uso wangu. Nilikuwa najaribu kitu chochote
nilichokiweza. Nilienda kwa miezi miwili au mitatu, na sikuweza kufanya
hayo tena, awe mtu. Ilikuwa ni: Simama. Kaa.
Sawa, toa ulimi wako
Ungepata mazoezi mengi. Nadhani nilipoteza uzito kiasi cha paundi tano.
Lakini hilo lilikuwa ni juu ya jambo hilo. Kwa hiyo, kwa sasa nimepotea zaidi
kuliko nilivyokuwa.
Lakini jambo hilo halikupita akilini mwangu kuwa hakuna Muumba. Nina
namba ya simu yako lakini siku zote namba hiyo inatumiwa na watu wengine.
Nilipiga picha za sinema. Filamu iitwayo Azimio Baya. Tangazo la biashara
ya simu mjini Chicago. Tangazo la biashara la Exxon. Matangazo mawili ya
benki. Wakati huo huo ninafanya kazi za ujenzi sehemu nyingine.
Tumefanyakazi katika duka kubwa. Na huu ni msimu wa mapunziko, na wao
wameweka hivi vibanda vya ziada njia za ukumbini. Katika kibanda
kimojawapo kulikuwa na msichana mmoja, nasi tulilazimika kupita mbele
yake. Nilimwambia: “Habari za asubuhi, vipi hali yako?” Kama dada huyo
alisema kitu, kitu hicho kilikuwa ni “mambo.” Ni hilo hilo tu alilolisema.
Mwishowe nilimwambia: “Bibie, husemi lolote. Nilitaka kukuomba radhi
kama nimesema mabaya.” Naye akaniambia: “Hapana, unajua, mimi ni
Mwislamu.” “Wewe ni nani?” Mimi ni Mwislamu, na wanawake wa
Kiislamu, hatuongei na wanaume ispokuwa tuwe na kitu maalumu cha
kuongelea; vinginevyo hatuna kitu cha kufanya na wanaume.” Ohhhh yeye
akasema, “Ndiyo, tunatekeleza dini ya Kiislamu.”
Uislamu – vipi uanatamka herufi zake?”
“I-s-l-a-m.”
Kwa muda huo, nilichokijua ni kuwa Waislamu wote ni magaidi. Lakini dada
huyo hata hakuwa na ndevu. Vipi dada huyo anaweza kuwa Mwislamu?
Dini hii ilianza vipi?”
“Vizuri, kulikuwa na Mtume.”

67
“Mtume?” “Muhammad.”
Nilianza uchunguzi fulani. Lakini mimi nimetokea dini moja. Sina nia ya
kuwa Mwislamu.
Likizo ikaisha. Vibanda vikaondolewa. Naye akatoweka.
Niliendelea kuomba dua na kusali, na kuuliza kwa nini dua zangu hazijibiwi?
Mnamo Novemba 1991, nilikuwa nampeleka mjomba wangu Richie
nyumbani kutoka hospitalini. Nilianza kutoa vitu kutoka katika droo yake ili
nipakie vitu vyake na kulikuwa na Biblia ya Gideon. Nilisema, Mungu
ameshajibu dua zangu. Biblia hii ya Gideon. (Bila ya shaka, wameiweka
katika kila chumba cha hotel hii.) Hii ni alama kutoka kwa Mola kuwa yupo
tayari kunifundisha. Kwa hiyo, nikaiiba Biblia hiyo.
Nilienda nyumbani na kuanza kuomba: “Ee Mungu nisomeshe niwe Mkristo.
Usinisomeshe njia ya Mashahidi wa Yehova. Usinifundishe njia ya
Wakatoliki. Nifundishe nji yako! Wewe hujaifanya Biblia hii iwe ngumu sana
kasi cha watu wa kawaida waliowaaminifu katika sala washindwe
kuifahamu”.
Nilipita njia zote katika Agano Jipya. Nilianza Agano la Kale. Vizuri,
hatimaye kulikuwa na sehemu katika Biblia juu ya Mitume. Bing!
Nilisema, subiri dakika moja (kidogo) yule bibie wa Kiislamu alisema kuwa
wao wana Mtume. Vipi hiyo, na Mtume huyo hayupo humu?
Nilianza kufikiria, Waislamu – wapo bilioni moja ulimwenguni – hiyo maana
yake ni mtu mmoja kwa kila watu watano mtaani, kinadharia ni Mwislamu.
Na nilifikiria: watu bilioni moja! Jumuika , njoo, shetani ni mzuri. Lakini
yeye si mzuri hivyo.
Kwa hiyo, baadaye nilisema, nitasoma kitabu chao, ambacho ni Quran, na
nitaona aina ya uongo iliyopo ndani yake. Huenda kina mafundisho ju ya
kuficha bunduki aina ya AK – 47. Kwa hiyo, nilienda duka la vitabu vya
Kiarabu.
Wakaniuliza, “Tukusaidie nini?”
“Nataka Quran.”

68
“Sawa, hapa tunazo nakala za Quran.”
Walikuwa na nakala nzuri sana – kwa dola therathini, dola arobaini.”
“Tazama, nataka kusoma tu, sitaki kuwa mmoja wao, sawa?”
“Sawa, tuna huo hapo mdogo dogo kwa dola tano wenye jarada la karatasi.”
Nilirudi nyumbani, na kuanza kusoma Quran yangu kuanzia mwanzo, wa
Suratul Fatihah. Na sikuweza kuyatoa macho yangu kutoka katika Quran.
Oyaa, tazama hii. Inazungumzia juu ya Nuhu humu. Tunaye Nuhu katika
Biblia yetu pia. Oyaa, Inazungumzia Lutwi na Ibrahimu. Siamini. Kamwe
sijalijua jina la shetani kuwa ni Ibilisi. Oyaa, vipi kuhusu hayo?
Unapopata picha hiyo katika T.V yako na ikiwa na maelezo kidogo nawe
unabonyeza swichi ya kusafisha picha. Hilo ni jambo la hakika linalotoke na
Quran.
Nilipitia kila kitu. Kwa hiyo, nilisema: sawa; nimeshafanya haya, sasa kitu
gani utakachofanya baadaye? Vizuri, uende katika eneo lao la kukutania.
Nilitazama kitabu cha kurasa za manjano (kitabu cha kuelezea mambo mbali
mbali yanapopatikana) na mwishowe nilikipata kituo cha Kiislamu cha
Calfornia kusini, katika Vermont. Niliwapigia simu nao wakasema, “Njoo
Ijumaa.”
Sasa tayari nilianza kuchanganyikiwa, kwa sababu, sasa ninajua nitaanza
kukabiliwa na Habibu na bunduki yake ya AK-47.
Nataka watu wafahamu, Wakristo wa Marekani wapoje katika ujio wa
Uislamu. Nafanya mambo ya kitoto kuhusiana na AK- 47, lakini sijui kama
watu hao wana masime chini ya makoti yao, unajua? Kwa hiyo, nilienda hadi
mbele, na nina hakika vya kutosha, kuwa kulikuwa na huyu ndugu mwenye
(six-foot-three, 240-paundi) ndevu na kila kitu, na nilikuwa ni mwenye
heshima.
Nilitembea na kusema: “Samahani bwana.”
[Lahaja ya Kiarabu] “Rudi nyuma!”
Alidhani kuwa mimi tayari ni mwenziwao.
Nikasema; “Ndiyo bwana” [kinyenyekevu].
Sikujua kwa nini nilirejeshwa nyuma, lakini hata hivyo, nilirudi nyuma.
Walikuwa na hema na mazuria yaliyokuwa nje. Nilisimama hapo, kwa aina
fulani ya kuona haya, na walikuwa wamekaa chini na kusikiliza mahubiri. Na

69
watu wengine wakasema, nenda mbele, ndugu, kaa chini. Nami ninaenda,
hapana, shukrani, hapana, shukrani, ninawatembelea tu.
Kwa hiyo, mwishowe mahubiri yakaisha. Wote walipamga mstari ili waswali
na wakasujudu. Kwa hakika nilirejeshwa nyuma yaani nilikumbushwa kujua
mambo ya nyuma.
Nilianza kutia akilini, katika mishipa yangu, mifupa yangu, moyoni mwangu
na roho yangu. Kwani sala imeisha. Nasema, oyaa, nani atakayenitambua?
Kwa hiyo, nilianza kujichanganya kama vile mimi ni mmoja wao, na nilikuwa
natembea msikitini na ndugu mmoja anasema, “Assalaamu alaykum.” Nami
nafikiria, Je amesema: “Chumvi na nyama.”
“Assalaamu alaykum.”
Kuna mtu mwingine aliyeniambia “Chumvi na nyama.”
Sikujua kitu gani katika dunia hii wanachokisema, lakini wote walitabasamu.
Kabla ya mmoja wao kugundua kuwa mimi si mtu wa kuwa hapo na
akanichukua hadi chumba cha mateso, au cha kunikata kichwa, nilitaka kuona
mambo mengi niwezayo kuyaona. Kwa hiyo, hatimaye, nilienda maktaba na
huko kulikuwa na ndugu wa Kimisri; jina lake lilikuwa ni Omar Mungu
ameniletea mtu huyo.
Omar alinijia, na akasema, “samahani. Je, hii ndiyo mara yako ya kwanza
kuja hapa? Kwa hakika alikuwa na lahaja nzito.
Nikasema; eenhe, ndiyo.
“Oh, vizuri sana. Je, wewe ni Mwislamu?”
“Hapana, nasoma kidogo tu.”
“Oh, wewe unajifunza? Hii ndiyo mara yako ya kwanza kutembelea
msikitini?”
“Ndiyo.”
“Njoo, acha nikuonyeshe sehemu hii.” Na akaninyanyua kwa mkono, nikawa
natembea kwa nguvu ya mtu mwingine – tulikamatana mikono. Nilisema,
Waislamu hawa ni marafiki. Kwa hiyo, akanionyesha maeneo hayo.
“Kwanza kabisa, huu ndiyo ukumbi wetu wa kuswalia, vua viatu vyako katika
eneo hili.”
“Hivi ni vitu gani?”
“Hiki ni chumba kidogo, Hapa ndiyo sehemu ya kuweka viatu vyako.”
“Kwa nini?”

70
“Vizuri, kwa sababu wewe unasogelea eneo la kuswalia, na eneo hilo ni
takatifu sana. Huruhusiwi kuliingia na viatu vyako; sehemu hiyo inakuwa safi
kabisa muda wote.”
Kwa hiyo, alinichukua na kunipeleka eneo la wanaume.
“Na hapa, ndiyo sehemu tunayotilia wudhu.”
“Voodoo! Sijasoma chochote juu ya voodoo!”
“Hapana, sio voodoo. Ni wudhu!”
“Sawa, kwa sababu nilimuona mfanyakazi huyo akiwa na mwanasesere na
pini, nami sipo tayari kufanya ahadi ya aina hiyo.”
Yeye anasema; “Hapana, wudhu, hapo ni pale tulipojisafisha.”
“Kwa nini unafanya hivyo?”
“Vizuri, wakati unaswali mbele ya Mungu, lazima uwe msafi, kwa hiyo,
tunaosha mikono yetu na miguu yetu.”
Kwa hiyo, nikajifunza vitu vyote hivyo. Naye akaniruhusu niondoke, na
alisema, njoo tena. Nilienda tena na nikamuomba yule mtunza maktaba vitabu
vya swala, na nilirudi nyumbani na kuvifanyia mazoezi. Nilihisi kuwa
ninajaribu kutenda hiyo swala vizuri, Mungu ataikubali. Niliendelea kusoma
na kusoma na kuutembelea msikiti ule.
Nilikuwa na ahadi ya kutembelea Midwest katika umoja wa wanamaigizo.
Vizuri, nilichukua kizuria cha kusalia. Nilijua kuwa nilitakiwa niswali kwa
wakati maalumu, lakini kulikuwa na maeneo maalumu ambayo huruhusiwi
kusali, na mojawapo ni chooni. Nilienda chumbani kwa wanaume katika kituo
cha watalii na nikatandika zulia langu na nikaanza kusali sala zangu.
Nikarudi, na Ramadhani ilipofika, nilianza kupokea simu kutoka sehemu
mbali mbali za hapa nchini niende nikatoe muhadhara nikiwa ni mchungaji
wa Mashahidi wa Yehova aliyeingia Uislamu. Watu waliniona ni mgeni na ni
mpya. [Wahamiaji wawili waliongea:]
Kijana huyu ni kama epple pie na anaendesha (a Chevy truck). Yeye ni
Mmarekani Mwekundu Alikuwa ni Shahidi wa Yehova.”
“Watu hao walikuja asubuhi hiyo?”
“Ndiyo, hao hao.”
“Hilo, lilitufanya tusilale siku za Jumapili?”
“Ndiyo, kijana huyu alikuwa mmoja wao. Na sasa ni mmoja wetu.”

71
Hatimaye mtu mmoja alinijia na kusema [kwa lahaja za Kipakistani] “Oh
ndugu, mazungumzo yako yalikuwa mazuri sana. Lakini unajua wewe, katika
madhehebu ya Kishafii…”
Kisha kitu pekee nilichoweza kukifanya ni kuwageukia na kusema, “Ahaa,
wandugu, Samahanini sana, natumai ningejua hayo, lakini sijui chochote juu
ya Uislamu ispokuwa kile kilichopo katika Quran na Sunnah. 9
Mmoja wao aliduwaa na kusema; “Ha –ha! Maskini ndugu, hajui lolote.
Anajua Quran peke yake.”
Vizuri, hayo ndiyo yale ninayoyajua. Na hilo limekuwa ni kinga niipendayo
sana. Nadhani yote hayo yapo mikononi mwa Allah.”
                 http://www.newmuslims.tk
chanzo ni: habari za Kiislamu, San Francisco, CA 94141-0186
9
 Sunna ni maelezo yanayohusishwa na Mtume Muhammad (S.A.W), sawa yale aliyoyatenda, kuyasema au
kuyakubali.

72
8- GEORGE ANTHONY
KIKATOLIKI (SRI LANKA)
– ALIYEKUWA PADRI
WA
Fr. Anthony alikuwa ni padri wa Kikatoliki nchini Sri-lanka. Masimulizi yake
ya kuwa muumini wa kweli na kuchagua jina la Abdulrahmani ni jambo la
kuvutia sana. Kwani kwa kuwa padri wa Kikatoliki kwa hakika alikuwa na
ujuzi sana wa mafundisho ya Biblia. Alikuwa ananukuu Biblia mara kwa
mara pale alipokaa na kutusimulia safari yake ya kuingia Uislamu. Alipokuwa
anasoma Biblia aligundua migongano mingi ndani yake. Anaendelea kunukuu
Aya za Biblia kwa lugha ya Kisri-lanka na kuonyesha utata.
Ananukuu Esaih 29:12 isemayo: “Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na
maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.”
Aya hii ni utabiri wa Mtume Muhammad (S.A.W), kwa sababu Muhammad
(S.A.W), ndiye aliyekuwa Mtume asiyejua kusoma na kwa kuwa yeye ndiye
Mtume asiyejua kusoma na alipotakiwa na malaika Jibrilu asome ufunuo
mtakatifu wa kwanza mbele yake alisema; “Mimi si msomi” na hii ni
kinyume na imani ya Kikristo kuwa Yesu ni Mungu, huku Matendo ya
Mitume 2:22 ya Biblia Takatifu inayomchukulia Yesu kuwa ni mtu. Inasema;
“Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu
aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo
Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe
mnavyojua;”
Ukristo na dini nyinginezo, haziuelezei utume kwa uwazi kwa mujibu wa
kauli yake. Wala Ubudha na ukimya wake juu ya Mitume wengine. Kinyume
na hayo, kwani katika Uislamu ni lazima kuamini Mitume yote iliyotangulia
na kuwaheshimu. Kwa mujibu wa Abdulrahmani imani hii ni ya kukinaisha
kabisa na ni ya kupendeza kwa kila mtu. Abdulrahmani anasema kuwa
hakuna sababu ya kuwazuia mapadri wa Kikatoliki wasioe, wakati mapadri
wa madhehebu mengine ya Kikristo wnaoa. Abdulrahmani alikuwa
anatafakari juu ya mkorogeko wa imani ya Kikristo wakati huo huo alipata
mkanda wa kaseti wa padri wa Kikristo wa Kisir-lanka aliyesilimu Shareef D.
Alwis. Mkanda wa Ahmad Deedat pia ulimvutia. Juhudi zake za kuendelea
kuupata ukweli mwishowe zilitoa matokeo ya kumbadili dini na kuwa
Mwislamu. Fr. Goerge Anthony.

73
Abdulrahmani, anatokea kijiji cha Rathnapura Sri-lanka. Alikuwa anafanya
huduma zake kama padri katika kanisa la Katumayaka. Ana salio la miaka
kumi katika kufundisha upadri. Aliandika barua kwenda kwa mama yake
akimfahamisha Uislamu. Baada ya kusoma kwa miezi kadhaa naye alifuata
njia ya mwanawe na kuingia Uislamu. Dada pekee wa Abdulrahmani
anafanyakazi Ugiriki. Baba yake na dada yake bado ni Wakristo.
Abdulrahmani aliacha kazi yake inayoheshimika sana ya upadri kwa ajili ya
ukweli. Naye kwa furaha kabisa ametoa muhanga mapato yake ya mali kwa
furaha ya kiroho. Kwa sasa anafanyakazi ya ukufunzi katika tume ya
kutangaza Uislamu nchini Kuwaiti.

74
9-DR.GARY
MWANAHISABATI
(CANADA)
ﻪﺗﺭﻮﺻ
 MILLER(ABDUL-AHADOMAR)
NA MMISHIONARI WA KIKRISTO
Gary Miller (Abdul-Ahad Omar) anaonyesha jinsi tunavyoweza kuanzisha
imani ya kweli kwa kuweka viwango vya ukweli. Yeye anafafanua jambo
lepesi, lakini ni njia yenye kufanya kazi sana katika kuupata mwelekeo sahihi
katika uchunguzi wetu wa kusaka ukweli.
G.R. Miller ni mwanahisabati na ni mtaalamu wa mambo ya kitikadi.
Alikuwa ni mchapakazi katika umishionari wa Kikristo akifanyakazi katika
maeneo maalumu maishani mwake lakini punde tu alianza kugundua mambo
yasiyowiana katika Biblia. Mwaka 1978, ilimtokea kuisoma Quran akitarajia
kuwa nayo vilevile itakuwa na mchanganyiko wa ukweli na uongo.
Kwa mshangao, aligundua kuwa ujumbe wa Quran kwa usahihi kabisa
ulikuwa ni ule ule kama ilivyo asili ya ukweli alioutiririsha kutoka katika
Biblia. Akawa Mwislamu na tangu hapo amekuwa ni mchapakazi
mchangamfu katika kutoa mafunzo ya Uislamu kwa watu wengine ikiwemo
njia ya kutokea redioni na katika Tv. Pia, yeye ni mtunzi wa makala nyingi na
machapisho kadhaa juu ya Uislamu.
Mmishionari muhimu sana wa Kikristo ameingia Uislamu na amekuwa mpiga
debe mkubwa wa Uislamu, alikuwa ni Mmishionari mchapakazi sana na
alikuwa na elimu nyingi ya Biblia. Mtu huyo anapenda sana hisabati, na hiyo
ndiyo sababu kuwa anapenda mantiki. Siku moja, aliamua kusoma Quran ili
kujaribu kupata Kosa lolote ambalo atafaidika nalo wakati wa kuwaita
Waislamu waingie Ukristo… Alitarajia Quran itakuwa ni kitabu cha zamani
kilichoandikwa karne kumi na nne zilizopita, kitabu kinachozungumzia
jangwa na kadhalika… Alishangazwa na kile alichokikuta. Aligundua kuwa
kitabu hiki kina vitu ambavyo, vitabu vyengine ulimwenguni havina…
Alitarajia atakuta baadhi ya visa juu ya wakati mgumu aliokuwa nao Mtume
Muhammad (S.A.W), kama vile kifo cha mkewe Khadija (Allah amrehemu)

75
au kifo cha mwanawe na mabinti zake … Hata hivyo, hakukuta chochote
kama hivyo … na kile kilichomfanya achanganyikiwe zaidi ni kuwa alikuta
“sura” kamili katika Quran inaitwa “Mariamu/Maria” ambayo imeshamiri
heshima nyingi kwa Mariamu (amani iwe juu yake) jambo ambalo halipo
katika vitabu vilivyoandikwa na Wakristo na hata Biblia yao haina. Hakukuta
sura yeyote iliyoitwa “Fatuma” (binti ya Mtume) wala “Aisha” (mkewe),
Mungu awarehemu wote wawili. Pia alilikuta jina la Yesu (amani iwe juu
yake) limetajwa ndani ya Quran mara ishirini na tano, wakati jina la
Muhammad (S.A.W), limetajwa mara nne tu, kwa hiyo, akawa
amechanganyikiwa zaidi. Akaanza kuisoma Quran kwa uangalifu zaidi
akitarajia kugundua kosa, lakini alishtushwa pale aliposoma aya kubwa kabisa
ambayo ni aya namba 82 ya surat Al-Nisaa (Wanawake) isemayo:
“Hawaizingatii nini, hii Qurani? Na kama ingelitoka kwa asiyekuwa
Mwenyezi Mungu bila shaka wangalikuta ndani yake khitilafu nyingi.”
Dr. Miller anazungumzia aya hii: “Moja ya misingi ya kisayansi ni msingi wa
kugundua kasoro au kutafuta kasoro katika nadharia hadi itakapothibitishwa
kuwa ni sahihi (jaribio la kugundua uongo wake)… kile kilichomshangaza ni
kuwa Quran Tukufu inawaambia Waislamu na wasiokuwa Waislamu
wajaribu kugundua makosa katika kitabu hiki na kinawaambia watu hao kuwa
hawatagundua kosa lolote.” Pia anasema juu ya aya hii, hakuna mwandishi
yeyote ulimwenguni mwenye ushujaa wa kuandika kitabu na kusema kuwa
kitabu chake hakina makosa, lakini Quran, kinyume kabisa, inakueleza kuwa
haina kosa na inakutaka ujaribu kugundua hata kosa moja na kamwe
hutoligundua.
Aya nyingine ambayo Dr. Miller ameihakisi kwa muda mrefu ni aya namba
30 ya Surat “Al-Anbiya’a” (Mitume): “Je! Hawakuona wale waliokufuru ya
kwamba mbingu na ardhi vilikuwa vimeambatana, kisha Tukaviambua,
(Tukavipambanua). Na Tukafanya kwa maji kila kitu kilicho hai. Basi je,
hawaamini?”
Anasema: aya hii kwa hakika ni mada ya uchunguzi wa kisayansi ambayo
imeshinda zawadi ya nobel mwaka 1973 na ilikuwa ni juu ya nadharia ya
“Mlipuko mkuu.” Kwa mujibu wa nadharia yake, ulimwengu ulikuwa ni
matokeo ya mlipuko mkuu ambao umepelekea kuundika kwa ulimwengu
ukiwa na mbingu zake na sayari.
Dr. Miller anasema: “Sasa tumekifikia kile kinachoshangaza juu ya Mtume
Muhammad (S.A.W) ni kile kinachodaiwa kuwa ni msaada wa shetani juu

76
yake, Mungu anasema: “Wala mashetani hawakuteremka nayo (hii Qurani
kama wanavyodai kusema hao makafiri katika kuitukana). Wala haiwi kwao
(kuiteremsha Qurani inayovunja hayo mambo yao), na hawawezi. Bila shaka
wao wamezuiliwa kusikia (yanayosemwa na Malaika huko mbinguni).”
(Quran 26:210 – 212) na aya: “Na Tunapoibadili Aya kwa Aya (nyingine), na
hali ya kuwa Mwenyezi Mungu (Akulinde) na shetani aliyefukuzwa (katika
rehema yake Mwenyezi Mungu. Anza kwa kusoma Audhu).
Unaona? Je, hii inaweza kuwa ni njia ya shetani ya kuandika kitabu? Vipi
aandike kitabu kisha akwambie umuombe Mola akupe ulinzi dhidi ya shetani
kabla ya kukisoma kitabu hicho? Hizo ni aya za miujiza katika kitabu hiki cha
miujiza! Na kina jibu la kimantiki kwa wale wote wanaodai kuwa kitabu
hicho ni cha Shetani.” Na miongoni mwa visa vilivyomshangaza Dr. Miller ni
kisa cha Mtume (S.A.W) na Abu-Lahabi… Dr. Miller anasema: “Mtu huyo
alikuwa anauchukia sana Uislamu kiasi ambacho alikuwa anamfuatilia
Mtume popote aendapo ili amwaibishe. Kama atamuona Mtume
anazungumza na wageni, alikuwa anasubiri hadi anapomaliza kisha
anawauliza: “Muhammad amekwambieni nini?” Na kama alisema cheupe
basi yeye atasema kwa hakika ni cheusi na kama amesema ni usiku yeye
atasema ni mchana. Yeye anakusudia kumwambia Muhammad ni mwongo
kwa yote asemayo na kuwafanya watu wawe na mashaka juu ya kitu hicho.
Na miaka kumi kabla ya kifo cha Abu Lahabi, iliteremshwa Sura kwa Mtume,
iitwayo “Al-Masadi.” Sura hiyo inasema kwamba Abu Lahabi hatoingia
Uislamu. Katika kipindi cha miaka kumi, Abu Lahabi aliweza kusema:
“Muhammad anasema kuwa mimi sitokuwa Mwislamu na kwa hiyo, nitaingia
Motoni, lakini sasa ninawaambia nataka kuingia Uislamu na niwe Mwislamu.
Je, sasa mnaonaje juu ya Muhammad? Je, anasema ukweli au sio? Je, ufunuo
wake umetoka kwa Mungu? Lakini Abu Lahabi hakufanya jambo hilo,
kabisa, ingawa alikuwa ni mpinzani wa Muhammad (S.A.W) katika kila
jambo, lakini si katika jambo hili. Kwa maneno mengine, ilikuwa ni kama
vile Mtume (S.A.W) alikuwa anampa Abu Lahabi nafasi ya kuhakikisha
makosa yake! Lakini hakuthibitisha kwa miaka kumi yote! Hakuingia
Uislamu na hata hajajifanya eti ni Mwislamu!! Katika miaka kumi, alikuwa
na nafasi ya kuuharibu Uislamu kwa dakika moja tu! Lakini hilo halikutokea
kwa sababu hiyo Quran si maneno ya Muhammad (S.A.W) lakini ni maneno
ya Mwenyezi Mungu ambaye ni Mjuzi wa kilichofichikana na Anajua kuwa
Abu Lahabi hatokuwa Mwislamu.

77
Vipi Mtume (S.A.W) ajue kuwa Abu Lahabi atathibitisha kile kilichosemwa
ndani ya sura hiyo ikiwa huo haukuwa ufunuo wa Allah? Vipi Mtume
atakuwa na uhakika katika kipindi cha miaka kumi kuwa kile kilichomo
(ndani ya Quran) ni sahihi kama hajajua kuwa huo ni ufunuo kutoka kwa
Allah? Kwa mtu ajitiaye katika changamoto hatari kama hiyo, jambo hilo lina
maana moja tu: nayo ni kuwa huo ni ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
“Pana kuangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia.
Hayatamfaa mali yake wala alivyovichuma. (Atakapokufa) atauingia Moto
wenye mwako (mkubwa kabisa). Na mkewe, mchukuzi wa kuni (za fitina),
(fattani, anayefitinisha watu wasiingie katika Dini; atauingia Moto huo).
(Kama kwamba) shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa (anayochukulia
kuni za fitina hizo). (Quran 111:1-5).
Dr. Miller anasema kuhusu aya iliyomshangaza: moja ya miujiza ndani ya
Quran ni changamoto ya wakati ujao kwa vitu vile ambavyo mtu hawezi
kuvitabiri na kwa vitu hivyo “jaribio la kuona uongo wa kitu” inatumika,
jaribio hili linakusanya kutafuta makosa hadi pale kile kitu kinachojaribiwa
kinapothibitishwa kuwa ni sahihi. Kwa mfano, hebu tutazame Quran
imesemaje juu ya mafungamano kati ya Waislamu na Mayahudi. Quran
inasema kuwa Wayahudi ni maadui wakuu wa Waislamu na jambo hilo ni
kweli hadi hivi sasa kwani maadui wakuu wa Waislamu ni Wayahudi.
Dr. Miller anaendelea: hili linazingatiwa kuwa ni changamoto kubwa sana
kwani Wayahudi wana nafasi ya kuuangamiza Uislamu kirahisi kwa
kuwatendea wema Waislamu kwa miaka michache na baadaye waseme: Sisi
tunakutendeeni kama marafiki zetu na Quran inasema kuwa sisi ni maadui
zenu, Quran lazima iwe na makosa! Lakini hili halijatokea kwa miaka 1400!!
Na kamwe halitatokea kwa sababu hayo ni maneno ya Mmoja ambaye anajua
kisichoonekana naye ni Mwenyezi Mungu na si maneno ya wanadamu.
Dr. Miller anaendelea: Je, waweza kuona namna aya ambazo zinazungumzia
juu ya uadui kati ya Waislamu na Wayahudi zinaanzisha changamoto kwa
akili ya mwanadamu? “Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu
(wengine) kwa Waislamu ni Mayahudi na wale mushirikina (wasiokuwa na
Kitabu), na utawaona walio karibu kwa urafiki na Waislamu ni wale
wanaosema: “Sisi ni Wakristo.” (Hayo) ni kwa sababu wako miongoni mwao
wanavyuoni na wamchao Mungu, na kwa sababu wao (Wakristo)
hawatakabari; (wakijua haki huifuata). Na wanaposikia yaliyoteremshwa

78
kwa Mtume (na yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona macho yao
yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema:
“Mola wetu! Tumeamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli
huu).” (Na wakilaumiwa kwa kusilimu kwao husema): “Na kwa nini
tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotufikia, na hali tunatumai Mola
wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema?” (Qurani 5:82-84).
Aya hizi zilitumiwa na: Dr. Miller pia alipokuwa Mkristo lakini alipoujua
ukweli, aliamini na kuingia Uislamu na akawa ni muhubiri wa Kiislamu.
Mungu alitie nguvu.
Dr. Miller anasema juu ya mtindo wa kipekee wa Quran kuwa yeye anauona
ni wa kupendeza sana: hakuna shaka kuwa kuna kitu cha pekee na cha
kushangaza katika Qurani ambacho hakijatajwa sehemu yeyote ile, kwani
Quran inakupa maelezo maalumu na inakuambia kuwa ulikuwa huyajui hapo
kabla. Kwa mfano: Hizi ni habari za ghaibu Tunazokufunulia; nawe hukuwa
nao walipokuwa wakitupa kalamu zao ndani ya maji (kwa kura, wajue) nani
wao atamlea Maryamu, na hakuwa nao walipokuwa wakishindana. (Quran
3:44)
Hizi ni katika khabari za siri Tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala
watu wako, kabla ya hii (Qurani kuteremshwa). Basi subiri; hakika mwisho
(mwema) utawathubutikia wanaomcha Mungu.” (Quran 11:49).
Hizi ni katika khabari za siri Tulizokufunulia. na hukuwa pamoja nao
walipoazimia shauri lao, hali wakifanya vitimbi vibaya. (Quran 12:102).
Dr. Miller anaendelea: “Vitabu vitakatifu vingine havitumii mtindo huu,
vitabu vingine vyote vina maelezo ambayo yanakwambia maelezo hayo
yametokea wapi. Kwa mfano, wakati Biblia Takatifu iliyopotoshwa
inazungumzia juu ya kisa cha mataifa ya kale, inakusimulia kuwa mfalme
huyu aliishi katika eneo hili na kiongozi yule alipigana katika vita vile, na mtu
yule maalumu ana idadi kubwa ya watoto na majina yao ni … lakini kitabu
hiki (Biblia iliyopotoshwa) daima inakusimulia kuwa kama unataka kujua
zaidi, soma kitabu maalumu kwani maelezo hayo yamekuja kutoka katika
kitabu hicho.”
Dr. Miller anaendelea: “Hii ni kinyume na Quran ambayo inakupatia maelezo
na inakwambia kuwa ni mapya!! Na kile kinachoshangaza ni kuwa watu wa

79
Maka wa wakati huo-wakati wa ufunuo wa aya hizo walikuwa wanazisikia
aya hizo na changamoto iliyokuwemo katika aya hizo ambayo ni mpya na
ilikuwa haijulikani na Muhammad (S.A.W) wala watu wake wa wakati huo,
lakini licha ya hivyo, kamwe hawajasema: tunayajua hayo na hayo si mapya,
na hawajasema: tunapajua pale Muhammad alipozitoa aya hizo. Hilo
halikutokea, lakini kilichotokea ni kuwa hakuna mtu aliyethubutu kusema
kuwa Muhammad (S.A.W) alikuwa anawaongopea kwa sababu maelezo
hayo yalikuwa ni maelezo mapya kabisa, hayajakuja kutoka katika akili za
wanadamu lakini yamekuja kutoka kwa Allah ambaye anajua kisichoonekana
hapo zamani, na sasa na wakati ujao.”

80
10- REV. DAVID BENJAMIN KELDANI (ABDUL’L-AHAD
DAWUD) (IRAN).
ﻪﺗﺭﻮﺻ
Profesa Abdu ‘l-Ahad Dawud, B.d., mwandishi wa mtiririko wa makala kwa
sasa, zamani alikuwa ni Padri wa Roman Katoliki kwa jina la Reverend David
Benjamin Keldani, B.D., wa Uniate-Caldean sect. Alipoulizwa vipi aliingia
Uislamu aliandika:
“Kuingia kwangu Uislamu hakukuweza kumpa sifa mtu yeyote
aliyesababisha zaidi ya maelekezo ya Mwingi wa rehema. Bila ya mwongozo
huu mtakatifu juhudi zote za masomo na uchunguzi wa kutafuta ukweli
huenda zingepelekea mtu kupotea. Kipindi ambacho niliamini Umoja
kamilifu wa Mungu na Mtume wake Mtukufu, Muhammad amekuwa ni
sehemu ya mwenendo na tabia yangu.”
“Abdu ‘l-Ahad Dawud ni padri wa Roman Katoliki wa zamani kwa jina la
Rev. David Benjamin, B.D., wa Uniate – Caldean Sect. Alizaliwa 1867 mjini
Umia Persia alisoma shule ya watoto mjini mwake. Toka 1886-89 (kwa miaka
mitatu) alikuwa katika walimu wa Uaskofu wa Canterbury`s Mission to the
Assyrian (Nestorian) Wakristo wa Urmia. Mwaka 1892 alipelekwa na
Cardinal Vaughan hadi Rome, sehemu ambayo alipitia kozi ya masomo ya
falsafa na nadharia katika chuo cha Propandanda cha Fide, na mnamo mwaka
1895 alikuwa ni padri msimikwa. Katika kipindi hicho alitawanya mlolongo
wa makala katika vibao juu ya “Assyria, Rome na Canterbury”; pia Aryland
Akirekodi juu ya uthibitisho wa Torati.” Ana tafsiri nyingi za Eva, Maria
katika lugha tofauti tofauti, zimechapishwa kwa vielelezo vya Misheni ya
Kikatoliki. Alipokuwa njiani Constantinople kuelekea Pershia mwaka 1895,
alitawanya mlolongo mrefu wa makala za Kingereza na Kifaransa katika
magazeti ya kila siku, yaliyochapishwa sehemu hiyo chini ya jina la The
Levant Herald, kwa Makanisa ya mashariki mwaka 1895 alijiunga na misheni
ya Lazarist ya Kifaransa katika eneo la Urmia, na kwa mara ya kwanza
alichapisha katika historia ya misheni ndani ya jarida la muda maalumu kwa
lugha ya wenyeji Syriac iitwayo Qala-la Shara, yaani “Sauti ya Ukweli.”

81
Mwaka 1897 alikuwa ni mwakilishi kwa taasisi mbili. Uniate-Caldean
Archbishops ya Urmia na Salmas to espresent-le-Monial nchin Ufaransa chini
ya uongozi wa Cardunal Perrand. Jambo hili bila ya shaka lilikuwa, kwa
mwaliko rasmi. Nyaraka ziliosomwa mbele ya baraza la wazee na “Baba
Benjamin” zilichapishwa katika kumbukumbu za kihistoria za Baraza la
wazee la kalamu ya Bwana, liitwalo “Le Pelirin” kwa mwaka huo. Katka
waraka huo padri wa Cadean (hiyo ilikuwa ni amani yake rasmi) akisikitikia
mfumo wa elimu wa Kikatoliki miongoni mwa Nestorians, na alitabiri
kukaribia kutokea kwa mapadri wa Kirusi katika mji wa Urmia.
Mnamo mwaka 1898 baba Benjamin alirudi tena Pershia, katika kijiji chake
asilia, Digala, kiasi cha maili moja kutokea mjini, alifungua shule ya bure.
Mwaka uliofuatia alipelekwa na mamlaka ya makasisi kuchukua uongozi wa
dayosisi ya Salmas, pale migogoro mikali na kashfa kati ya Unitiate wa
Askofu, Khudabash, na mapadri wa Lazzarist ilipozidi kwa muda mrefu
amekuwa anaogopea mfarakano. Katika siku ya mwaka mpya 1900, padri
Benjamin alihubiri mahubiri yake ya mwisho na ya kukumbukwa sana kwa
makutano, wakiwemo, Waaramenia wengi wasio Wakatoliki na watu wengine
kutoka kanisa kuu la Mt.George. Khorovabad, Salmas. Maudhui ya mahubiri
yalikuwa ni “Karne mpya na watu wapya.” Alikumbushia ukweli kwamba
Wamishieni Wanestorian, kabla ya kudhihiri kwa Uislamu, wamehubiri Injili
katika Asia yote; wanazo taasisi mbali mbali nchini India (hasa hasa) katika
mji wa Malbar Coast). Tartary, China na Mongolia; na kuwa wametafsiri
Injili kwa Kituruki, Kiughurs na lugha nyinginezo; Wakatoliki, Wamarekani
na misheni za Kianglikana, ingawa wamefanya vizuri kidogo kwa taifa
Waassyro (Haldean) katika Elimu ya utangulizi, wameligawa taifa hilo dogo
na kuwa Pershia, Kurdistani na Mesopotamia, na kulitumbukiza katika uadui
wa aina mbali mbali na madhehebu; na kwa hiyo, juhudi zao zilikuwa ni
zenye kujaaliwa kuleta mporomoko wa mwisho kabisa. Kwa hiyo,
aliwashauri watu asilia wajitoe muhanga ili wasimame kidete juu ya miguu
yao wenyewe kama wanaume, na wasitegemee misheni za kigeni na
kadhalika.
Misheni kubwa tano za kujivunia – za Kimarekani, Kifaransa, Kijerumani, na
Kirusi – wakiwa na wenziwao, Magazeti yanayoungwa mkono na jamii za
dini tajiri, Mabalozi wadogo na Mabalozi. Walikuwa wanajitahidi
kuwabadilisha zaidi ya Waassyro – Chaldean laki moja wotoke kutoka katika
uasi wa kidini wa Nestorian na wawe katika kundi mojawapo miongoni mwa
makundi matano hayo ya uasi. Lakini misheni ya Kirusi punde ilizishinda

82
misheni nyingine, na ilikuwa misheni hiyo ambayo mnamo mwaka 1915
iliwasukuma au iliwalazimisha Waassyrian pia, makabila ya milimani ya
Kurdistani, ambao baadaye walihamia uwanda wa Salmas na Urmia, kusaidia
kuinua silaha dhidi ya Serikali yao inayoheshimika. Matokeo yalikuwa ni
kuwa nusu ya watu hao waliangamia vitani na waliobakia walifukuzwa
kutoka katika ardhi zao za asili.
 Swali kuu ni: Je, Ukristo, ukiwa na uma wake wote, maumbile na rangi zake
zote, na huku ukiwa na mambo ya bandia yaliyo madhubuti na maandiko
yaliyoharibiwa, Je, hiyo ilikuwa ni dini ya kweli ya Mungu? Wakati wa
kiangazi mwaka 1900 alistaafu na kuelekea katika nyumba yake ndogo
iliyopo katikati ya shamba la mizabibu karibu na chemchem ya sherehe ya
Chali-Boulaqhi mjini Digala, na hapo kwa kipindi cha mwezi mmoja alitumia
muda wake kwa kusali na kutafakari, akisoma na kumaliza maandiko
matakatifu katika maandiko yake asilia. Mgogoro uliishia kwa kustaafu
kikawaida kulikopelekwa hadi kwa Maaskofu wa Unite wa Urmia, na hapo
kwa uwazi alimweleza Mar (Mgr.) Touma Audu sababu ya kujitoa katika kazi
zake za kikasisi. Majaribio yote yaliyofanywa na mamlaka ya makasisi ili
aondoe uamuzi wake yalikuwa bila ya faida. Kulikuwa hakuna uadui wa
kibinafsi au mabishano kati ya Fther Benjamini na vigogo wake; yote hiyo
ilikuwa ni swala la dhamiri.
Aliajiriwa Tarbiz kwa kazi ya ukaguzi katika shirika la huduma za posta na
forodha la Pershia chini ya utaalamu wa Belgian. Kisha alichukuliwa katika
huduma ya Mtukufu mwana wa mfalme Alihammad Ali Mirsa kwa kazi ya
ualimu na ukalimani. Na ilikuwa ni mwaka 1903 ambapo kwa mara nyingine
alitembelea Uingereza na huko alijiunga na jamii ya Wakristo wasioamini
utatu. Na mwaka 1904 alipelekwa na Uingereza ikishirikiana na Umoja wa
Wakristo wageni wasioamini utatu, kuendeleza kazi za elimu na kuelimisha
miongoni mwa watu wa nchi yake. Akiwa njiani kuelekea Pershia alitembelea
(constantinople, na baada ya mahojiano kadhaa na Sheikh l-Islamu Jemalu d-
Din Effendi na Maulamaa wengine (wanazuoni wa Kiislamu), alisilimu na
kuingia Uislamu.

83
11- MUHAMMAD AMAN HOBHM MWANADIPLOMASIA,
MMISHIONARI NA MFANYAKAZI WA KAZI ZA JAMII
(UJERUMANI).
Kwa nini watu wa magharibi wanaingia Uislamu?
Kuna sababu nyingi juu ya hilo. Inayoshika nafasi ya kwanza, ni kuwa ukweli
daima una nguvu zake. Msingi wa imani ya Kiislamu ni ya uwiano sana, ni ya
kimaumbile sana na ni ya kuvutia sana kiasi ambacho mtafuta ukweli aliye
mwema hawezi kutovutiwa na hayo. Tuchukulie kwa mfano; imani ya kuwa
kuna Mungu mmoja. Namna inavyoinua heshima ya mtu na namna
inavyotuweka huru na ung`ang`aniaji wa mambo ya kichawi na ya hovyo
hovyo! Namna inavyoongoza kimaumbile kueleke katika usawa wa
kibinadamu, kwa kuwa binadamu wote wameumbwa na Mungu Mmoja na
wote ni watumishi wa Mola huyo huyo! Kwa Wajerumani, kwa sifa ya
kipekee, imani ya kumwamini Mungu ni chanzo cha ufunuo, chanzo cha
ushujaa wa kutokuwa na woga na ni chanzo cha kuhisi usalama. Kisha dhana
ya maisha baada ya kifo inapindua meza. Maisha katika dunia hii yanabakia
kuwa si lengo kuu tena, na sehemu kubwa ya nguvu ya mwanadamu
itolewayo kwa ubora wa ahera. Imani ya kuamini siku ya Kiama yenyewe
inampa mtu heshima ya kuacha matendo mabaya, na kufanya matendo mazuri
pekee ambayo yanaweza kuhakikisha uwokovu wa milele, ingawa matendo
mabaya yanaweza kustawi hapa duniani kwa kipindi chenye mipaka maalumu
tu. Imani ya kuamini kuwa hakuna mtu awezaye kukimbia matokeo ya
hukumu ya haki, na Mungu Mjuzi afanyaye mambo mawili kabla ya mtu
kufanya chochote kile kilichokibaya na kwa hakika huu ukaguzi wa milele ni
wenye kutenda kazi zaidi kuliko polisi wenye kufaa sana duniani.
Kitu kingine ambacho kinawavutia wageni wengi kuingia Uislamu ni
msisitizo wake juu ya kuvumiliana. Kisha sala za kila siku zinamfundisha mtu
awe anapanga wakati na mwezi mmoja wa kufunga unamuwezesha mtu
kufanya mazoezi ya kujimiliki juu ya nafsi yake na bila ya shaka kupanga
wakati na kuwa na nidhamu binafsi ni vitu viwili vya fikra muhimu sana ya
mtu mwema na mtu mbora.
Sawa, yanakuja mafanikio halisi ya Uislamu. Uislamu ni itikadi pekee
ambayo imefanikiwa kuingiza, kidogo kidogo, kwa wafuasi wake roho ya
kuona mfumo wa maadili na mipaka ya utu bila kulazimishwa na vitu vya nje.
Kwani Mwislamu anajua kwamba, popote alipo, anatazamwa na Mungu.

84
Imani hii inamwepusha na dhambi. Kwa kuwa binadamu kwa kawaida
anamili kwa Mwenyezi Mungu, Uislamu pia, unatoa amani ya moyo na akili
– na jambo hili limesahauliwa kabisa na jamii za Kimagharibi za hivi sasa.
Nimeshaishi chini ya mifumo ya maisha mbali mbali na nimeshapata nafasi
ya kujifunza itikadi mbali mbali, lakini nimehitimisha kuwa hakuna imani
yeyote iliyokamilika kama Uislamu.
Ujamaa una vivutio vyake, na hivyo hivyo kwa mfumo Kidemokrasia wa
Kisekyula na mfumo wa Kinazi. Lakini hakuna mfumo wowote katika hiyo
wenye kanuni kamilifu kwa maisha mema. Ni Uislamu pekee wenye
ukamilifu huo, na kwa hiyo, ndiyo sababu watu wazuri wanauingia Uislamu.
Uislamu si nadharia bali ni wa vitendo. Uislamu si jambo la kupita, Uislamu
unamaanisha utiifu mkamilifu kwa matakwa ya Mungu.
Kutoka “Islam, Our Choice = “Uislamu ndio Chaguo Letu”

85
12- PADRI MKUU VIACHESLAV POLOSIN (URUSI).
Viacheslay Sergeevich Polosin alizaliwa mwaka 1956. Mwaka 1979 alihitimu
kitengo cha falsafa cha MGU na mnamo 1984 alihitimu Seminari ya makasisi
Moscow. Alikuwa ni padri msimikwa na alihudumia parokia katika dayosisi
ya Asia ya kati na Kaluga ya RPTS. Mwaka 1990 alinyanyuliwa daraja ya
upadri mkuu. Mwaka huo huo alichaguliwa kaimu wa watu wa RSFSR
kutoka jimbo la Kaluga na aliongoza tume ya mamlaka kuu kabisa ya Soviet,
alihitimu katika shule ya kidiplomasia ya wizara ya mambo ya nje na kutetea
makala zake juu ya madai ya: “Kanisa la Kiothodoksi la Kirusi na hali ya
USSR, 1971-1991.” Kuanzia 1993 amekuwa ni mwajiriwa wa kazi za serikali
ya Duma katika Baraza la harakati za kidemokrasia ya Kikristo ya Kirusi na
ni mwanachama wa baraza la umoja wa Kikristo. Mwaka 1991, alienda likizo
kutokea dayosisi ya Kaluga na tangu mwaka 1995 hajasalisha katika Liturujia
(kawaida ya ibada ya usharika mtakatifu). Katika mahojiano yake na jarida la
Musulmane yeye, kirasmi alijiita Mwislamu: “Ninazingatia kuwa Quran ni
ufunuo wa mwisho duniani, ulioteremshwa kwa Mtume Muhammad. Hakuna
Mola ispokuwa ni Mungu Mmoja, Allah, na Muhammad ni Mtume wake.”
Viacheslav Polosin ni mtunzi wa kazi nyingi za kisomi juu ya mambo ya
kihistoria, kisiasa, kidini, na mada za kifalsafa. Mwezi Februari wa mwaka
huo alitetea makala nyingine juu ya mada: “Lahaja ya visa vya kubuniwa na
waundaji wa visa vya kubuni vya kisiasa.” Mawazo yake ya msingi ya
kifalsafa ni kukiwasilisha kitabu chake “visa vya kubuni, Dini, na hali.”
(Moscow, 1999).
Katika mahojiano na jarida “Musulmane;” VIACHESLAV POLOSIN
alisema kuwa Uislamu haujaanza kutokana na Ukristo lakini ni mapinduzi ya
pili na makuu ya imani ya Mungu Mmoja imani ya Ibrahimu. Ibrahimu
alikuwa anaamini Mungu Mmoja na alikuwa ni mtu wa kwanza kueleza
jambo hili wazi wazi. Alitangaza jambo hilo na alilithibitisha kwa mafanikio,
akawa “baba” wa waumini wote. Baadaye utamaduni huo ukakatizwa na
mkengeuko. Hilo linajulikana kwa kuwa Mitume yote na wengi wao vilevile
wanaitwa “waokozi”… wakiwakosoa watu kwa mkengeuko wao na
kutumbukia katika upagani na ukafiri. Na Mtume mkuu ambaye ni Yesu,
vilevile alikosoa watu kwa kukengeuka na kuingia ukafiri. Zaidi ya hayo,
Yesu yeye mwenyewe alijizungumzia nafsi yake kwa mafumbo kuwa
ametumwa na Mungu kufanya kazi maalumu. Kabla watu hawa kusema:
“Mitume ni watu kama sisi.” Lakini Mungu amempeleka Malaika wa Mungu

86
asiye na dhambi – katika Biblia malaika wanaitwa “watoto wa Mungu” (Job
38:7) – ambaye alikuwa ni Mtume mtakatifu kabisa lakini alikuwa hatiiwi.
Wao walifikiria hamu ya kumwangamiza. Naye alikosoa utawala ulioshindwa
kufikia malengo ya wakati huo na kusambaza habari njema za Mungu bila ya
mipaka ya mtu hata mmoja, kwa watu wote; hayo yalikuwa ni mapinduzi
makubwa ya Uyahudi. Uislamu ni mapinduzi ya pili, yaliyosafisha sana
Ukristo wa karne ya sita na saba kutokana na ukuaji wa upagani ambao
umeundika katika kipindi chake na kujipatia madaraka rasmi na kukubaliwa
kwa wingi mkubwa.
Kinachovutia katika Uislamu ni jambo lepesi tu Tauhidi (imani ya kuamini
Mungu Mmoja) kwa mfumo wake maridadi ili tusimfikiri Mungu katika tabia
isiyofaa. Napenda jambo hilo kwani hakuna kupingana na kuna hali ile ile ya
kimantiki. Quran Tukufu inasema papo hapo kuwa ukweli hauna kupingana.
Kuna mafundisho ya dini, Mungu mwenye miujiza, Muumba, Mwenye
nguvu, Mwenye Rehema na yote yaliyobaki lazima yawe yanaafikiana na
hayo. Kama kuna kitu kinapingana na haya, hilo linamaanisha kuwa jambo
hilo lazima liwe limefutwa.
        Nevasisimaia gazeta..religii, 2 June 1999
chanzo:http://www.edu/~psteeves/relnews/9906a.html#03

87
MAKASISI WAINGIA UISLAMU
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
  “Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wengine) kwa
Waislamu ni Mayahudi na wale mushirikina (wasiokuwa na Kitabu), na
utawaona walio karibu kwa urafiki na Waislamu ni wale wanaosema: “Sisi ni
Wakristo.” (Hayo) ni kwa sababu wako miongoni mwao wanavyuoni na
wamchao Mungu, na kwa sababu wao (Wakristo) hawatakabari; (wakijua
haki huifuata). Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume (na
yakawatulilikia kuwa ni kweli), utaona macho yao yanamiminika machozi
kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema: “Mola wetu! Tumeamini,
basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli huu).” (Na wakilaumiwa
kwa kusilimu kwao husema): “Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na
haki iliyotufikia, na hali tunatumai Mola wetu atuingize (Peponi) pamoja na
watu wema?”
[QURANI TAKATIFU, Surah Al-Maidah 5:82-84]

88
KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA MAPADRI, MAKASISI NA
WAHUBIRI WANAOINGIA UISLAMU, TAFADHALI TEMBELEA
TOVOTI HIZI:
HTTP://WWW.ISLAMTOMORROW.COM
HTTP://WWW.NEWMUSLIMS.TK
HTTP://WWW.THETRUELIGION.ORG
HTTP://WWW.WADEE3.5U.COM
HTTP://WWW.ISLAMWAY.COM
S.A.W: REHEMA NA AMANI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE.

89
Makasisi Waingia Uislamu
  Vyombo vya habari vya kuupinga Uislamu
vinawagawa Waislamu katika makundi yafuatayo:
“Magaidi” “Walipua Mabomu” Waporaji” na
            “Wateka Nyara”
Kwa hiyo, mtu atautazama vipi Uislamu?
Kwa nini mapadri na wahubiri wengi wanaingia
                 Uislamu?
Haya ni maswali mazuri ambayo tutayatolea majibu.
“Salam Alaykum” yaani “Amani iwe juu yenu”
Hili kava limetengenezwa na
   www.harunyahia.com
     kwa ajili ya kitabu
       (Yesu Atarejea)

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget