Monday, February 13, 2012

Masihi Isa/Yesu (Amani iwe naye)

Kupandishwa Nabii 'Iysa ('alayhis-salaam) mbinguni ni jambo ambalo limewatia shaka watu wengi. Na wengi waliotia shaka hawakubaliani na mafunzo ya 'Aqiydah sahihi yanayopatikana dalili zake katika Qur-aan na Sunnah. Hivyo imewafikisha kukufuru kwani ni kama kukanusha maneno ya  Allaah سبحانه وتعالى .


 Na sababu kubwa ya kuwafanya hadi wafikie katika hali hiyo ni kutokana na kupenda kujadiliana sana mambo ya Allaah سبحانه وتعالى  kwa kuyatilia shaka na kugeuza usemi huu na ule kutokana na fikra zao wakati tumeamrishwa kuwa tusiwe tunauliza sana mambo mengine ambayo Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى Ameyakidhia kwa Hikma Yake na ambayo Hayakuyaelezea zaidi bali tunatakiwa tuyapokee na kuyaamini kama yalivyotujia katika Qur-aan na Sunnah.
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَسْأَلُواْ عَنْ أَشْيَاء إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُواْ عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللّهُ عَنْهَا وَاللّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ))     ((قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُواْ بِهَا كَافِرِينَ))  
((Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapoteremshwa Qur-aan mtabainishiwa. Allaah Amesamehe hayo. Na Allaah ni Mwenye maghfira Mpole)) ((Waliyauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa wenye kuyakataa)) [Al-Maaidah: 101-102]
Ukweli ni kuwa Nabii ‘Iysa ('alayhis-salaam) aliishi kwa muda katika hii ardhi, kisha akapandishwa mbinguni kisha atarudishwa na Allaah سبحانه وتعالى  katika mwisho wa zama ili kutekeleza mambo fulani kama Anavyotaka Muumba Mwenyewe. Baada ya umri wake kumalizika atakaporudi, atakufa na kufufuliwa kama watu wengine.
Na kufanya hivyo Allaah سبحانه وتعالى  Anatuonyesha tena uwezo na nguvu Zake ya kuwa Anaweza kufanya chochote Anapokiamrisha kiwe basi huwa.  Anafanya Anavyotaka wala Yeye Haulizwi. Na kuwa katika Itikadi yetu kama Waislamu ni kwamba Allaah سبحانه وتعالى  ni Muweza wa kufanya Alitakalo. Kuweko 'Iysa ('alayhis-salaam) mbinguni ni kutuonyesha miujiza Yake na uwezo Wake na kwetu ni mtihani mkubwa sana kwani tusipoamini tutakuwa na hasara hapa ulimwenguni na Kesho Akhera.
DALILI KUTOKA KATIKA QUR-AAN  
((إِذْ قَالَ اللّهُ يَا عِيسَى إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُواْ وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُواْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ))
((Pale Allaah Aliposema: Ewe 'Iysa! Mimi Nitakufisha, na nitakunyanyua Kwangu, na Nitakutakasa na wale waliokufuru, na Nitawaweka wale waliokufuata juu ya wale waliokufuru, mpaka Siku ya Qiyaamah. Kisha marejeo yenu yatakuwa Kwangu, Nikuhukumuni katika yale mliyokuwa mkikhitalifiana)) [Al-'Imraan:55]
((وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَكِن شُبِّهَ لَهُمْ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُواْ فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلاَّ اتِّبَاعَ الظَّنِّ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا))   ((بَل رَّفَعَهُ اللّهُ إِلَيْهِ وَكَانَ اللّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا))   ((وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلاَّ لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا))  
((Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuua Masihi 'Iysa, mwana wa Maryam, Mtume wa Mwenyezi Mungu-nao hawakumuua wala hawakumsulubu, bali walifananishiwa tu. Na hakika waliokhitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuua kwa yakini)) ((Bali Allaah Alimtukuza kwake, na hakika Allaah ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima))((Na hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao)) [An-Nisaa:157-159]
ATAKAVYO HUKUMU NABII ISSA (A.S.).
Mitume wote waliotangulia pamoja na Mtume wetu Muhammad S.A.W. walitumwa ili kumpwekesha Mwenyezi Mungu S.W.T., na kwa kufanya hivyo mtu anakuwa amesalimisha nafsi yake kwa Mola wake au anakuwa amesilimu na kuitwa Mwislamu. Na Nabii Issa A.S. atakapoteremka atasimamisha hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad SAW.. Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira RAA na iliyotolewa na Muslim, “
“Vipi nyinyi akiwashukieni (Nabii Issa) Ibn Maryam awahukumuni?” Pia Hadithi iliyotolewa na Ibn Abii Dhi`ib (kumwambia Waliid bin Muslim) na iliyotolewa na Muslim kasema, “Unajua nini “AMMAKUM MINKUM?” Nikajibu: “Niambie” Akasema: “Awahukumu kwa Kitabu cha Mola wenu (Qurani) na sunna ya Mtume wenu (Muhammad) S.A.W..”

NABII ISSA A.S. KUMWUA MASIHI DAJJAAL.
Kitu cha kwanza atakachokifanya Nabii Issa atakapoteremka ni kupambana na Dajjaal. Baada ya kuteremka atakwenda moja kwa moja Baitil Muqaddas (Falastini) ambapo huko Dajjaal atakuwa amezungukwa na Waislamu, atawaamrisha wafungue mlango. Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Abii Umamah na iliyotolewa na Ibn Maajah na Ibn Khaziima, “Atakapoondoka, Issa A.S. atasema: “Funguweni mlango.” Wataufungua na nyuma yake (ule mlango) yupo Dajjaal (na) pamoja naye (wako) Mayahudi sabini elfu.
Wote wenye panga (upanga) zilizopambwa na saji. (Nabii Issa) atakapomtazama Dajjaal atayayuka kama chumvi inavyoyayuka katika maji (kwa khofu) na ataondoka akikimbia. Atampata kwenye mlango wa Mashariki. Atamuua, kisha Mwenyezi Mungu atawashinda Mayahudi...”

KAZI YA NABII ISSA BAADA YA KUMWUA DAJJAAL. 
Baada ya Nabii Issa kumuua Dajjaal na kuzitokomeza fitina zake, watatokea Yaajuuj na Maajuuj. Nabii Issa atamuomba Mola wake awaangamize, dua yake itakubaliwa, na Mwenyezi Mungu S.W.T. atawaangamiza wote Yaajuuj na Maajuuj. Na ndipo baada ya hapo ataanza kazi yake kubwa aliyoijia nayo ni kuangamiza kila ushirikina na kumpwekesha Mola wake na kuanzisha sheria ya Kiislamu. Mtume SAW kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na iliyotolewa na L-Bukhari na Muslim, “Naapa kwa (jina la Mwenyezi Mungu) ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, inakukaribieni kukuteremkieni (Nabii Issa A.S.) mwana wa Maryam atahukumu (kwa sheria ya Kiislamu) (na) muadilifu, basi atavunja misalaba (ya Wakristo makanisani) na atauwa nguruwe, na ataondosha (atazuiya) vita, na mali itazidi kuwa nyingi hata hakuna atakayeikubali (kwa kuogopa Kiyama). Na hata itakuwa kusujudu mara moja ni bora kuliko dunia na kilichomo ndani yake (kwa kukiogopa Kiyama).”


MUDA WA KUWEPO NABII ISSA A.S. DUNIANI.
Nabii Issa A.S. ataishi duniani muda wa miaka arobaini baada ya kuteremka kwake kutoka mbinguni. Katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira RAA na iliyotolewa na Abu Daud kasema, “
“Atakaa (Nabii Issa A.S.) katika dunia miaka arobaini, kisha atakufa, na watamsalia Waislamu.”
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلمamesema: ((Mitume ni ndugu katika sehemu, mama zao ni tofauti lakini dini yao ni moja. Mimi nina haki zaidi kwa 'Iysa  mwana wa Maryam kuliko mtu yeyote kwa sababu hakukuwa na Mtume baina yake na yangu. Atateremka, na mtakapomuona mtamtambua: Ni mwenye mwili uliojengeka, (rangi ya ngozi yake) ni baina ya nyekundu ya nyeupe. Atateremka akiwa amevaa nguo mbili ndefu za rangi ya manjano khafifu. Kichwa chake kitakuwa kinachuruzika maji, japokuwa hakikuguswa na umande. Atavunja misalaba, ataua nguruwe na ataondosha Jizya na atawaita watu katika Uislamu. Katika muda atakaokuwepo, Allaah Ataziangamiza dini zote isipokuwa Uislamu. Na Allaah Atamuangamiza Masiyhid-Dajjaal (Masihi Muongo). Usalama utajaa ardhini hadi kwamba simba watachanganyika pamoja na ngamia, chui na ng'ombe na mbwa mwitu na kondoo. Watoto watacheza na nyoka bila ya kuwadhuru. 'Iysa atabakia miaka arubaini kisha atakufa, na Waislamu watamswalia Swalah ya Janaazah)) [Ahmad na Abu Daawuud] .
عن أبي هريرة؛ أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((لا تقوم الساعة حتى ينزل الروم بالأعماق -أو بدابق-فيخرج إليهم جيش من المدينة من خيار أهل الأرض يومئذ، فإذا تصافّوا قال الروم: خلوا بيننا وبين الذين سَبَوا منا نقاتلهم. فيقول المسلمون: لا والله لا نخلي بينكم وبين إخواننا. فيقاتلونهم، فينهزم ثلث لا يتوب الله عليهم أبدًا، ويُقْتَلُ ثلثه أفضل الشهداء عند الله  عز وجل  ويفتح الثلث لا يفتنون أبدا فيفتتحون قسطنطينية، فبينما هم يقسمون الغنائم قد عَلَّقوا سيوفهم بالزيتون، إذْ صاح فيهم الشيطان: إن المسيح قد خلفكم في أهليكم. فيخرجون، وذلك باطل. فإذا جاؤوا الشام خرج، فبينما هم يُعدّون للقتال: يسوون الصفوف، إذ أقيمت الصلاة، فينزل عيسى ابن مريم فأمَّهم فإذا رآه عدوّ الله ذاب كما يذوب الملح في الماء، فلو تركه لانذاب حتى يهلك ولكن يقتله الله بيده، فيريهم دمه في حَرْبته))   مسلم
Kutoka kwa Abu Hurayrah  رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلمamesema: ((Qiyaamah hakitasimama hadi Warumi watakapomiliki Al-A'maaq au  Daabiq. Jeshi kutoka Madiynah litakuwa lenye watu bora kabisa katika ardhi. Watakapokutana uso kwa uso, Warumi watasema: "Tupigane na wale waliotuteka baadhi yetu". Waislamu watasema: "Hapana! Wa-Allaahi hatutawaachilia nyinyi muwateke ndugu zetu". Watapigana nao. Thuluthi ya jeshi la Waislamu litakimbia kwa sababu ya kushindwa, nao ni ambao Allaah Hatawasamehe. Thuluthi nyingine watauliwa, nao ni mashahidi bora kabisa. Thuluthi ya mwisho watakuwa ni washindi na hawa ndio hawatofitinika abadan na wataiteka Constantinople (Istanbul). Watakapokuwa wanagawa ngawira baada ya kutundika mapanga yao juu ya miti ya zaituni, shaytwaan  atapiga kelele baina yao na atasema: 'Al-Masihid-Dajjal yuko pembeni ya watu wenu". Wataondoka kukutana na Ad-Dajjal Shaam. Huu utakuwa ni wito wa udangayifu na watakapofika Shaam Ad-Dajjaal atatokea. Waislamu watakapokuwa wanasawazisha safu zao za vita na Swalah itakapoadhiniwa, 'Iysa mtoto wa Maryam atateremka na kuwaimamisha Swalah. Adui wa Allaah atakapomuona, (Masihi muongo) atayeyukakama chumvi inavyoyayuka katika maji na ikiwa bado atabakia ataendelea kuyeyuka mpaka atakufa. Allaah Atamuua kwa mkono wa 'Iysa na atawaonyesha Waislamu damu yake katika mshale wake))[Muslim]
Mji atakaoteremka:
حديث النواس بن سمعان : (( فَيَنْزِلُ عِنْدَ الْمَنَارَةِ الْبَيْضَاءِ شَرْقِيَّ دِمَشْقَ بَيْنَ مَهْرُودَتَيْنِ وَاضِعًا كَفَّيْهِ عَلَى أَجْنِحَةِ مَلَكَيْنِ، إِذَا طَأْطَأَ رَأْسَهُ قَطَرَ، وَإِذَا رَفَعهُ تَحَدَّرَ مِنْهُ مِثْلُ جُمَانِ اللُّؤْلُؤ، لَا يَحِلُّ لِكَافِرٍ يَجِدُ رِيحَ نَفَسِهِ إِلَّا مَاتَ، وَنَفَسُهُيَنْتَهِي حَيْثُ يَنْتَهِي طَرَفُه))  مسلم
Hadiyth kutoka kwa An-Nawaas bin Sam'aan ((Atateremka karibu ya mnara mweupe Mashariki ya Damscus. Atavaa nguo mbili zenye rangi ya zaafarani (manjano) khafifu, mikono yake ikiwa katika mbawa mbili za Malaika wawili. Kila atakapoinamisha kichwa chake, matone ya maji yatamdondoka. Kila atakapoinua kichwa chake, mapambo ya thamani yatamuanguka. Hakuna kafiri atakayesalimika na pumzi za 'Iysa, na pumzi zake zitafika umbali wa upeo wa macho yake)) [Muslim]
Maelezo kuhusu kupandishwa kwake:
Ibn Haatim amesimulia kwamba  Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما  amesema: "Kabla ya Allaah Kumpandisha 'Iysa mbinguni, 'Iysa alikwenda kwa Maswahaba zake kumi na mbili katika nyumba. Alipofika, nywele zake zilikuwa zikichuruzika maji akasema:"Kuna miongoni mwenu ambao watanikufuru mara kumi na mbili baada ya kuniamini". Kisha atasema: "Nani atakayejitolea abadilishwe umbo lake liwe kama langu ili auliwe badala yangu na atakuwa pamoja na mimi Peponi?" Mmoja wao aliye mdogo kuliko wote alijitolea lakini 'Iysa akamuambia akae chini. Kisha 'Iysa akauliza tena atakayejitolea na kila mara ilikuwa ni huyo huyo kijana mdogo aliyejitolea lakini 'Iysa akamuambia akae chini. Kisha tena kijana huyo akajitolea tena na mwisho 'Iysa akasema : "wewe utakuwa ni huyo mtu". Akafananishwa na 'Iysa na 'Iysa akapandishwa mbinguni akipaa juu katika uwazi  (uliofunuka juu ya sakafu ya nyumba). Mayahudi walipokuja kumtafuta 'Iysa wakamuona huyo kijana (wakidhani kuwa ni 'Iysa) wakamuua (kwa kumsulubu) Baadhi ya maswahaba wakamkufuru mara kumi na mbili baada ya kumuamini. Kisha wakajigawa katika makundi matatu. Kundi la mwanzo Al-Ya'aqubiyyah (Jacobites) wamesema: "Allah Amebakia na sisi Alivyojaalia kisha akapanda juu". Kundi la pili An-Nasturiyyah (Nestorians) wamesema: 'Mtoto wa Mungu alikuwa na sisi alivyojaaliwa kisha Allaah Akampandisha mbinguni. Kundi la tatu Waislamu wakasema: "Mja na Mjumbe wa Allaah amebakia na sisi Alivyomjaalia Allaah, kisha Allaah Akamchukua Kwake". Makundi mawili yaliyokufuru wakaungana dhidi ya Waislamu na wakawua. Tokea ilivyotokea hivyo, Uislamu ukafunikwa, hadi Allaah Alipomleta Muhammad  صلى الله عليه وآله وسلم "[Usimulizi huu una isnaad sahihi inayofikia hadi kwa 'Ibn 'Abbas na An-Nasaiy amesimulia kutoka kwa Abu Kurayb ambaye amepokea kutoka kwa Abu Mu'aawiya – Ibnu Kathiyr: 3-28-29]    
Na kama inawashangaza wengi kupandishwa kwake na baadhi yao wenye kutumia akili zao juu ya dini badala ya kufuata Qur-aan na Sunnah, wanapaswa wakumbuke kuwa kwa Allaah سبحانه وتعالى hilo si kubwa, kama Alivyomleta duniani kwa kuzaliwa na mama yake bila kuingiliwa na mwanamume,
((إِذْ قَالَتِ الْمَلآئِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ))    )) وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلاً وَمِنَ الصَّالِحِينَ))   (( قَالَتْ رَبِّ أَنَّى يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ قَالَ كَذَلِكِ اللّهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاء إِذَا قَضَى أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ((  
((Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake Masihi 'Iysa mwana wa Maryam, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa waliokaribishwa (kwa Allaah)))  ((Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utuuzima wake, na atakuwa katika watu wema))   ((Maryam akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Allaah Akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Allaah Huumba Apendacho. Anapohukumu jambo, Huliambia: Kuwa! Likaw)) ni[Al-'Imraan: 45-47] 
Na pia kupewa uwezo mbali mbali wa kufanya mambo ya ajabu  kamaAnavyoyaelezea Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah ifuatayo:
((وَرَسُولاً إِلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللّهِ وَأُبْرِىءُ الأكْمَهَ والأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَى بِإِذْنِ اللّهِ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ))
((Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Allaah. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Allaah, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini) [Al-'Imraan: 49]
Kwa hiyo vile vile kufanya asife na kupaishwa juu hilo pia kwa Allaah سبحانه وتعالى sio kubwa! 

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget