Monday, February 13, 2012

Majina Ya Mitume 25 katika Quran


Pamoja na kwamba inasemwa kuwa idadi ya Mitume wanafika hadi 124,000 kutokana na baadhi ya mapokezi, lakini Hadiyth hizo zimedhoofishwa na hivyo hatuwezi kuzitegemea, ila kuna Hadiyth ambayo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyosimuliwa na Abu Dhar ambayo alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) idadi ya Mitume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akamjibu kuwa ni mia tatu na makumi kadhaa. Hadiyth hiyo imeelezwa usahihi wake na Imaam Al-Albaaniy kama ilivyo hapa chini:

  عن أبي ذر ، قال : قلت : يا رسول الله ! أي الأنبياء كان أول ؟ ! قال : آدم ، قلت : يا رسول الله ! ونبي كان ؟ ! قال : نعم نبي مكلم ، قلت : يا رسول الله : كم المرسلون ؟ ! قال : ثلاث مئة وبضعة عشر ؛ جما غفيرا . 
الراويأبو ذر الغفاري  -  خلاصة الدرجةصحيح  -  المحدثالألباني  -  المصدرمشكاة المصابيح  - الصفحة أو الرقم: 5669

Kutoka kwa Abu Dhar ambaye amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Allaah, Nabii yupi wa mwanzo? Akasema: ((Aadam)). Nikasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, alikuwa ni Nabii? Akasema: ((Ndio Mtume aliyesemeshwa)) Nikasema: Ewe Mjumbe wa Allaah. Wapo Mitume wangapi? Akasema: ((Mia tatu na makumi kidogo)) [Mishkaat Al-Maswaabiyh ikiwa na daraja ya Swahiyh]

Hata hivyo idadi iliyotajwa katika Qur-aan ni Mitume 25 pekee na dalili ni kauli ya (Subhaanahu wa Ta'ala):

((وَرُسُلاً قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلاً لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْك))

((Na Mitume tuliokwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia)) [An-Nisaa: 164] 

Watume 18 wametajwa kwa pamoja katika Aayah 4 zifuatazo zinazofuatana:

((وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَى قَوْمِهِ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاء إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ)) (( وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَقَ وَيَعْقُوبَ كُلاًّ هَدَيْنَا وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَى وَهَارُونَ وَكَذَلِكَ نَجْزِيالْمُحْسِنِينَ))   ((وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَى وَعِيسَى وَإِلْيَاسَ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ)) ((وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا وَكُلاًّ فضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ))  

((Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibraahiym kuhojiana na watu wake. Tunamnyanyua kwa vyeo tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na Mwenye ujuzi)). 
((Na tukamtunukia (Ibraahiym) Is-haaq na Ya’aquub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuuh tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daawuud na Sulaymaan na Ayyuub na Yuusuf na Muusa na Haaruun. Na hivi ndivyo tunavyowalipa wafanyao wema))
((Na Zakariyya na Yahyaa na ‘Iysaa na Ilyaas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema)) 
((Na Ismaa’iyl, na Al-Yasaa, na Yuunus, na Luutw. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu wote)) [al-An’aam:  83-86]
Manabii na Mitume waliotajwa katika Qur-aan kwa mpangio wa ujio nikama ifutavyo:

1.                  Aadam.
2.                  Idriys.
3.                  Nuuh.
4.                     Huud.
5.                        Swaalih.
6.                        Ibraahiym.
7.                           Luutw.
8.                           Ismaa'iyl bin Ibraahiym.
9.                           Is-haaq bin Ibraahiym.
10.                        Ya'quub bin Is-haaq bin Ibraahiym.
11.                        Yuusuf bin Ya'quub bin Is-haaq bin Ibraahiym.
12.                        Shu'ayb.
13.                         Ayyuub.
14.                         Dhul Kifl.
15.                         Muusa.
16.                         Haaruun nduguye Muusa.
17.                         Daawuud.
18.                         Sulaymaan bin Daawuud.
19.                         Ilyaas.
20.                         Alyasa'.
21.                         Yuunus.
22.                         Zakariyya.
23.                         Yahya bin Zakariyya.
24.                         'Iysaa bin Maryam.
25.                         Muhammad. (Swalla Allaahu 'alayhim wa sallam)
Na Allaah Anajua zaidi

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget