Friday, April 20, 2012

Majina 99 ya Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu S.W.T. katuamrisha sisi Waislamu katika Kitabu Chake, Qurani Tukufu, tumuombe kwa kutumia majina Yake. Kama alivyosema katika Suratil Israa aya ya 110, “

 قُلْ ادْعُوا اللَّهَ أَوْ ادْعُوا الرَّحْمَانَ أَيًّا مَا تَدْعُوا فَلَهُ الأَسْمَاءُ الْحُسْنَى…

Maana yake, “Sema: “Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri…”

Pia Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil A`araaf aya ya 180, “

 وَلِلَّهِ الأَسْمَاءُ الْحُسْنَى فَادْعُوهُ بِهَا وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ…

Maana yake, “Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri mazuri; muombeni kwayo. Na waache wale wanaoharibu utakatifu wa majina Yake…”
Na Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi ilyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na iliyotolewa na Ahmad, “

‘‘إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمًا ، مِائَةً إِلاَّ وَاحِدًا مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الْجَنَّةَ’’

Maana yake, “Hakika Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa. Majina mia isipokuwa moja. Atakayeyahifadhi (majina haya na kujua maana yake) ataingia Peponi.”

Pia Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi ilyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na iliyotolewa na L-Bukhari, “

‘‘لِلَّهِ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ اسْمًا ، مِائَةٌ إِلاَّ وَاحِدًا ، لا يَحْفَظُهَا أَحَدٌ إِلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةَ’’

Maana yake, “Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa. Majina mia isipokuwa moja. Hakuna atakayeyahifadhi (majina hayo na kujua maana yake) isipokuwa ataingia Peponi.”

Ingawa Mwenyezi Mungu Mtukufu katuelezea kwamba majina Yake ni tisini na tisa, lakini hata hivyo majina Yake ni zaidi kuliko hivyo. Hakuna mtu yeyote yule hapa duniani anayeyajua majina Yake yote isipokuwa Mwenyewe Muumba wa mbingu na ardhi. Na Majina haya tisini na tisa yanatafsiri sifa Zake nzuri ambazo sifa hizo hazilingani na sifa za viumbe Wake. Ndio maana Mwenyezi Mungu S.W.T. katuamrisha wakati tunapotaka kumuomba basi kwanza kabla ya kuomba dua tumuombe kwa majina hayo, halafu tuombe tunachotaka kuomba. Na wakati wa kumuomba tuwe katika tohara na moyo na kiwiliwili vimnyenyekee Mola Mtukufu, wala tusijishughulishe na mambo mengine.

Ndio maana Mtume S.A.W. kasema,

“Mwenyezi Mungu hapokei dua ya mtu yule moyo wake umeghafilika wakati anapoomba.” 

Na majina hayo tisini na tisa yametajwa na Mtume S.A.W. kama yalivyokuja katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na Ttirmidhi.

Na anayetaka kuomba dua kwanza asome,

“AUDHU BILLAAHI MINA SHAITAANI RRAJIYM. BISMI LLAAHI RRAHMAANI RRAHIYM: ALLAAHUMMA INNIY ATAWAJJAHU ILAIKA BIASMAA-IKAL HUSNAA YAA MAN HUWA, “

‘‘اللَّهُ الَّذِي لا إِلَهَ إِلاَّ هُوَ ، الرَّحْمَنُ ، الرَّحِيمُ ، الْمَلِكُ ، الْقُدُّوسُ ، السَّلامُ الْمُؤْمِنُ ، الْمُهَيْمِنُ ، الْعَزِيزُ ، الْجَبَّارُ ، الْمُتَكَبِّرُ ، الْخَالِقُ ، الْبَارِئُ ، الْمُصَوِّرُ ، الْغَفَّارُ ، الْقَهَّارُ ، الْوَهَّابُ ، الرَّزَّاقُ ، الْفَتَّاحُ ، الْعَلِيمُ ، الْقَابِضُ ، الْبَاسِطُ ، الْخَافِضُ ، الرَّافِعُ ، الْمُعِزُّ ، الْمُذِلُّ ، السَّمِيعُ ، الْبَصِيرُ ، الْحَكَمُ ، الْعَدْلُ ، اللَّطِيفُ ، الْخَبِيرُ ، الْحَلِيمُ ، الْعَظِيمُ ، الْغَفُورُ ، الشَّكُورُ ، الْعَلِيُّ ، الْكَبِيرُ ، الْحَفِيظُ ، الْمُقِيتُ ، الْحَسِيبُ ، الْجَلِيلُ ، الْكَرِيمُ ، الرَّقِيبُ ، الْمُجِيبُ ، الْوَاسِعُ الْحَكِيمُ ، الْوَدُودُ ، الْمَجِيدُ ، الْبَاعِثُ ، الشَّهِيدُ ، الْحَقُّ ، الْوَكِيلُ ، الْقَوِيُّ ، الْمَتِينُ ، الْوَلِيُّ ، الْحَمِيدُ ، الْمُحْصِي ، الْمُبْدِئُ ، الْمُعِيدُ ، الْمُحْيِي ، الْمُمِيتُ ، الْحَيُّ ، الْقَيُّومُ ، الْوَاجِدُ ، الْمَاجِدُ ، الْوَاحِدُ ، الصَّمَدُ ، الْقَادِرُ ، الْمُقْتَدِرُ ، الْمُقَدِّمُ ، الْمُؤَخِّرُ ، الأَوَّلُ ، الآخِرُ ، الظَّاهِرُ ، الْبَاطِنُ ، الْوَالِيَ ، الْمُتَعَالِي ، الْبَرُّ ، التَّوَّابُ ، الْمُنْتَقِمُ ، الْعَفُوُّ ، الرَّءُوفُ ، مَالِكُ الْمُلْكِ ذُو الْجَلالِ وَالإِكْرَامِ ، الْمُقْسِطُ ، الْجَامِعُ ، الْغَنِيُّ ، الْمُغْنِي ، الْمَانِعُ ، الضَّارُّ ، النَّافِعُ ، النُّورُ ، الْهَادِي ، الْبَدِيعُ ، الْبَاقِي ، الْوَارِثُ ، الرَّشِيدُ ، الصَّبُوْرُ’’

ALLAAHU LLADHIY LAA ILAAHA ILLA HUWA (Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu), ARRAHMAANU (Mwingi wa rehema), ARRAHIYMU (Mwenye kurehemu), AL-MALIKU (Mfalme wa milele), AL-QUDDUWSU (Mtakatifu, ametakasika na sifa zote chafu), ASSALAAMU (Mwenye kuleta amani), AL-MU-UMINU (Mtoaji wa amani), AL-MUHAYMINU (Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo Yake), AL-`AZIYZU (Mshindi katika mambo Yake), AL-JABBAARU (Anayefanya analolitaka), AL-MUTAKABBIRU (Mkubwa), AL-KHAALIQU (Muumbaji), AL-BAARI-U (Mtengenezaji), AL-MUSAWWIRU (Mtia sura), AL-GHAFFAARU (Mwenye kusamehe), AL-QAHHAARU (Mwenye nguvu juu ya kila kitu), AL-WAHHAABU (Mpaji mkuu), ARRAZZAAQU (Mwenye kuruzuku), AL-FATTAAHU (Hakimu), AL-`ALIYMU (Mjuzi wa kila kitu), AL-QAABIDHU (Mwenye kunyima au kuzuia), AL-BAASITU (Mwenye kutoa), AL-KHAAFIDHU (Mfedheheshaji waovu), ARRAAFI`U (Mpandisha daraja), AL-MU`IZZU (Mtoa heshima kwa amtakaye), AL-MUDHILLU (Mnyima heshima kwa amtakaye), ASSAMIY`U (Mwenye kusikia), AL-BASIYRU (Mwenye kuona), AL-HAKAMU (Mwenye kuhukumu), AL-`ADLU (Muadilifu), AL-LLATIYFU (Mwenye kujua yaliyofichikana), AL-KHABIYRU (Mwenye kujua yaliyo dhahiri), AL-HALIYMU (Mpole), AL-`ADHIYMU (Aliye Mkuu), AL-GHAFUWRU (Mwingi wa kusamehe), ASHAKUWRU (Mwenye kushukuru), AL-`ALIYYU (Aliye juu), AL-KABIYRU (Aliye mkuu), AL-HAFIYDHU (Mwenye kuhifadhi), AL-MUQIYTU (Mlinzi), AL-HASIYBU (Mwenye kuhesabu), AL-JALIYLU (Wa hali ya juu), AL-KARIYMU (Mkarimu wa hali ya juu), ARRAQIYBU (Mchungaji), AL-MUJIYBU (Mwenye kujibu), AL-WAASI`U (Mwenye wasaa), AL-HAKIYMU (Mwenye hekima), AL-WADUWDU (Mwenye kupenda waja Wake), AL-MAJIYDU (Mwenye utukufu), AL-BAA`ITHU (Mfufuaji), ASHAHIYDU (Mwenye kushuhudia kila kitu), AL-HAQQU (Wa Haki), AL-WAKIYLU (Mtegemewa), AL-QAWIYYU (Mwenye nguvu), AL-MATIYNU (Aliye madhubuti), AL-WALIYYU (Mlinzi na Msaidizi), AL-HAMIYDU (Mwenye kusifika na kila sifa njema), AL-MUHSIYU (Mwenye kuhesabu), AL-MUBDI-U (Mwenye kuanzisha), AL-MU`IYDU (Mwenye kurejeza), AL-MUHYIYU (Mwenye kuhuisha), AL-MUMIYTU (Mwenye kufisha), AL-HAYYU (Mwenye uhai wa milele), AL-QAYYUWMU (Msimamia kila jambo), AL-WAAJIDU (Mtambuzi), AL-MAAJIDU (Wa kuheshimiwa), AL-WAAHIDU (Mmoja tu), ASSAMADU (Mwenye kukusudiwa kwa kuabudiwa), AL-QAADIRU (Mwenye uwezo wa kufanya au kutokufanya), AL-MUQTADIRU (Mwenye uwezo wa pekee juu ya kila kitu), AL-MUQADDIMU (Mwenye kutanguliza), AL-MU-AKHIRU (Mwenye kuakhirisha), AL-AWWALU (Wa Mwanzo), AL-AAKHIRU (Wa Mwisho), ADHAAHIRU (Wa Dhahiri), AL-BAATINU (Wa Siri), AL-WAALIYA (Mpanga mipango ya watu), AL-MUTA`AALI (Mtukufu Aliye juu), AL-BARRU (Mwema), ATTAWWAABU (Mwenye kupokea toba za waja Wake), AL-MUNTAQIMU (Mlipa kisasi kwa waovu), AL-`AFUWWU (Mwenye kusamehe madhambi), ARRAUFU (Mwenye huruma), MAALIKU L-MULKI DHUL JALAALI WAL IKRAAMI (Mfalme wa wafalme Mwenye utukufu na heshima), AL-MUQSITU (Mtoaji haki sawa kwa kila anayestahiki), AL-JAAMI`U (Mkusanyaji viumbe siku ya Mwisho), AL-GHANIYYU (Tajiri), AL-MUGHNIYU (Mwenye kutajirisha), AL-MAANI`U (Mwenye kuzuia viumbe visidhurike), ADHAARRU (Mwenye kudhurisha), ANNAAFI`U (Mwenye kuleta nafuu), ANNUWRU (Mwenye nuru), AL-HAADIY (Mwongozaji wa kheri), AL-BADIY`U (Mzuaji), AL-BAAQIYU (Mwenye kubakia milele), AL-WAARITHU (Mwenye kurithi kila kitu), ARRASHIYDU (Mwenye kuongoa waja kuiendea njia ya kheri), ASSABUWRU (Mwenye kusubiri).”

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget