Leo Mwanamke amekuwa ni bidhaa isiyo na thamani. Kila mtu anaweza kununuwa
bidhaa hio kwa thamani ndogo kabisa kwa lengo la kujistarehesha, Mwanamke ni
fitna kubwa katika jamii, pindi akijiweka mbali na mafundisho ya Allah. Jamii
nyingi zina haribikiwa kwasababu ya maadili na tabia mbaya za wanawake. Athari
ya Mwanamke ni kubwa sana katika jamii na kwa Umma wote. Katika Khutba ya leo
tutaangazia suali hili muhimu la Fitna za wanawake, na jukumu la Waislamu
katika kupambana na fitna hizo.
Mwenyezi Mungu ametuusia sisi na watu waliotangulia
kumcha yeye. Na ushahidi wa hayo. Amesema Mwenyezi Mungu (SW) katika
Quraan tukufu:
{{ Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo
mbinguni na vilivyomo ardhini, na kwa hakika tuliwausia waliopewa kitabu kabla
yenu, na nyinyi pia kwamba mumche Mwenyezi Mungu na mkikufuru hakika ya
Mwenyezi Mungu ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini na Mwenyezi Mungu ni
mkwasi na mwenye kusifiwa}}. Amrisho hilo la kumcha Mwenyezi Mungu ni kwa wote
wanaume na wanawake. Lakini kwa vile wanaume ndio wasimamizi wa wanawake
inapaswa juu yao kuwalazimisha wake zao juu la suala la kumcha Mwenyezi Mungu
kwa njia yoyote ile iliopaswa kisheria. Ushahid wa haya; Anasema Allah (SW):
{{ Wanaume ni wasimamizi wa wanawake kwa vile
walivyofadhilishwa na Mwenyezi Mungu baadhi juu ya baadhi na kwa mali
wanayotoa}}. Na yote hayo ispokuwa kwa sababu za kimsingi kama utoaji na
utazamaji wao wa mambo kibusara. Amesema Shankiti: Mwenyezi Mungu ameashiria
kua mwanamume ni mbora kuliko mwanamke kutokana na utukufu na ukamilifu
alionao, na mwanamke ana upungufu wa kimaumbile kutokana na kujipamba.
Inafahamika kua wanawake waliokuwa katika zama hizi
wanatofautiana na wanawake wa zama za Mtume (SAW). Mbali na wanawake wetu
hawatafautiani na wanawake wasiokuwa na dini na kukhalifu miongozo ya dini kwa
mfano:
b) - Kutangamana na wanaume katika vyuo vikuu
Vyote hayo yameharamishwa na ushuhuda wa hapo ni pindi
alipotoka Musa na kuelekea Madyana kufika kisimani alikuta pote la watu
wanaywesha wanyama wao na akawakuta wanawake wawili wanazuia wanyama wao
wasitangamane na wanyama wengine. Akauliza sababu ya kufanya jambo hilo.
Wakasema hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao kunywesha (yote hayo ni kutokana
na unyonge wetu na kutopenda kutangamana na watu).
Amesema Mwenyezi Mungu kusimulia tukio hilo ndani
ya Quraan tukufu:“ Na alipoyafikia maji ya Madyana alikuta umati wa watu
wanaywsha (wanyama wao) na akakuta karibu yao wanawake wawili na wanyama wao
akawauliza mna nini? Wakasema hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao kuchunga, na
baba yetu sisi ni mzee sana”. Zingatieni msimamo huo ulinganishwe na yanayo
fanyika leo.
Na katika hadith
ya Mtume (SAW): [ Waamrisheni watoto wenu kusali hali wakiwa na umri
wa miaka saba, na wapigeni wakifika miaka kumi na watenganisheni katika
malazi]. Hadith hii inamaanisha
kutengamana kati yaa mwanamume na mwanamke.
Na miongoni mwa ukiukaji wa maaadili ya kiislamu ni
wanawake kudhihirisha mapambo yao jambo amblo linapelekea katika uasharati na
kwani Mwenyezi Mungu kaamrisha kuvaa hijabu, kuhifadhi macho na kukataza
kujishaua na kudhihirisha mapamabo yake. Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
{{ Na waambie waumini wanaume wainamishe macho yao
na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao kwa unao dhihirika, na
waangushe shungi zao kwa mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo
yao ila kwa wanaume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao, au
watoto wa waume zao,au kaka zao,au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao,
au wanawake wenziwao, au wale ilyowamiliki mikono yao ya kiume au
wafuasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyokhusu
ukwe wala wasipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao.
Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi waumini ili mupate kufanikiwa}}.
Wamesema wanazuoni: macho ndio mlango mkubwa wa moyo, na
ndiyo kuimarika kwa hisia kwa ajili hiyo tunapaswa kutahadhari nayo (macho) na
kuhifadhi tupu, ima ni kujilinda na uzinifu au kuhifadhi uchi, na wasionyeshe
uzuri wao isipokua kwa wale walio ruhusiwa kama Aya iliyotangulia. Imethubutu
katika Musnad ya Imam Ahmad kwamba Abu Hureira amepokea hadithi kutoka kwa
Mtume (SAW) akisema: (Aina mbili za watu wa motono na mmoja wao ni
mwanamke avaae nguo nyepesi isiositiri na inaonyesha uchi).
Wanawake wema waliotangulia walikua wakijiheshimu na
wakivaa hijabu na kumcha Mwenyezi Mungu, tazama kisa cha Uzushi, pindi Mama
yetu Aisha hakumsemesha swahaba Swafuwan hata neno na hivyo ndivyo walivyo fika
Madina. Na pindi walipoamrishwa kuvaa hijab waliitikia kwa haraka wito huo bila
ya kuchelewa. Ummu salama asimulia akisema pindi ilpoteremka Neno lake Mwenyezi
Mungu: "Wateremsha nguo
zao". Wamefika wanawake wa kianswaar kama juu ya vichwa vyao kuna kurabu,
na wakivaa vazi jeusi Mwenyezi Mungu mkubwa kwa kuitika wito wake na wito wa
Mtume wake.
Imepokewa na Ummu Salama kua akisema mwanamke akimwambia
Mtume (SAW) kua mimi ni mwanamke kurefusha vazi langu na natembea katika maeneo
yenye uchafu? Akasema Mtume (SAW): [ itatwahirika baada yake]. Amesema kua mwanamke huyo anakusudia kuficha nguo zake
pindi anapotembea kama iliyoada ya waarabu. Wanawake wetu na
mabanati wetu wakiachwa bila ya muongozo wa dini watafanya maovu na Mwenyezi
Mungu kajalia kuwa wanaume ndio wasimamizi wao kutokana na upungufu wa akili na
dini amabalo hilo Mtume
(SAW) anausia wanaume akisema: [ Na kusieni kuwafanyia
wema wake zenu kuweni ni wasiadizi wenu].
Ndugu Waislamu, tumeona khatari kubwa ya Fitna za
Wanawake na athari mbaya katika jamii. Nijukumu lakila Muislamu kujitolea
kubadilisha hali mbaya tunaoishi kwasasa katika jamii yetu. Ikiwa ni mkeo,
mamako, bintiyako, binti wa muislamu mwenzako, wote nijukumu la kila muislamu
kuwafundisha wanawke maadili na tabia njema. Tukifanya hivyo, kwahakika jamii
yetu itabadilika na tutapata rehma za Allah (SW) pamoja na hifadhi yake
kutokana na kila fitna. Namuomba Mwenyezi Mungu atulinde na fitna za
wanawake, na awalinde wao na moto uumizao, Ewe Mwenyezi Mungu tupe mema hapa
duniani na kesho akhera.
No comments:
Post a Comment