Wednesday, April 4, 2012

Kuyafurahia Mauti - Birthday


Je unajua kwamba unaposherehekea siku ya kuzaliwa (Birthday) unakuwa unafurahia kukaribia kwa mauti? Unalolifurahia ni jambo ambalo muislamu amepaswa kulizingatia sana na kujiandaa nalo. 
Mauti ni moja katika alama zake Allah (Subhaanahu Wata’ala). Utamaduni wa kuyafurahia mauti si utamaduni wa kiislamu. Anasema Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) katika hadithi iliyopokelewa na Abu Hurayrah, Allah amuwie radhi kwamba:
                                          أَكْثِرُوا ذِكْرَ هَاذِمِ اللَّذَّاتِ ‏"‏ ‏.‏ يَعْنِي الْمَوْت                                      
“Zidisheni katika kukumbuka kivunjacho Ladha (yaani mauti)”.
              
            Imesimuliwa na Attirmidhiy,Ibnu Majah, Annasaai
Anasema Allah(Subhaanahu Wata’ala) katika Quraan,  Yaasin /68
                                                                                        وَمَن نّعَمِّرْهُ نُنَكِّـسْهُ فِى الْخَلْقِ أَفَلاَ يَعْقِلُونَ    
Na tunayempa umri (mrefu) tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii?
Je katika kusherehekea huku kupewa umri na Allah (Subhaanahu Wata’ala) kunakuwepo mazingatio kama tulivyoagizwa katika Quraan? Mazingatio haya ni kufahamu kwamba kujiandaa na mauti ni wajibu wa kila muislamu na  dunia ni pahala pa kupita tu na kila umri unapopita ndio kuelekea uzeeni na kuelekea kwenye makaazi ya milele - Akhera. Suuratul Hajj/5
                                                وَمِنكُمْ مَّن يُرَدُّ إِلَى أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْلاَ يَعْلَمَ مِن بَعْدِ عِلْمٍ شَيْئاً….          
Na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua.
Lau kama siku hii waislamu wangelikusanyika kwa pamoja na kuyakumbuka mauti - badala ya kuyafurahia - kama alivyokuwa akifanya  Sahaba Abdullah ibn Umar (Allah amuwie radhi yeye na baba yake) alipokumbushwa kuhusu mauti, huwakusanya waliokuwepo miongoni mwa mafuqahaa (wasomi wa dini) na kuyazingatia na kuyakumbuka mauti wakilia mpaka wanaopita hudhani pana msiba!.

Ndugu yangu muislamu, ukibahatika kualikwa/ kuhusishwa/ kushirikishwa katika “sherehe” hizi tafadhali tanabahisha kwa kufikisha ujumbe huu muhimu kuwakumbusha waislamu kama tunavyoagizwa katika Quraan  Al A’alaa/ 9 -1
                                                    فَذَكّرْ إِن نَّفَعَتِ الذّكْرَى- سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَى- وَيَتَجَنَّبُهَا الاْشْقَى        
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. Atakumbuka mwenye kuogopa. Na atajitenga mbali nayo mpotovu.

Wabillahi Tawfiyq

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget