Askofu Mkuu wa Canterbury nchini Uingereza Rowan Williams ameunga mkono vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu na kutangaza kuwa vazi hilo ni chaguo la mtu binafsi kwa ajili ya wanawake Waislamu.
Tovuti ya On Islam imeripoti kuwa, Askofu Mkuu wa Cantebary Williams aliyasema hayo jana katika tamasha ya fasihi ya Oxford akijibu fikra zisizo sahihi zilizoenea katika jamii kuhusu vazi la hijabu.
Hii si mara ya kwanza kwa Askofu Mkuu wa Canterbury kutetea vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu.
Mwaka 2006 Rowan Williams pia aliwatahadharisha viongozi wa serikali ya Uingereza akisema kuwa kupiga marufuku vazi la hijabu na nembo nyingine za kidini ni jambo lenye hatari kubwa katika mtazamo wa kisiasa.
Mwaka 2008 pia kiongozi huyo wa kidini alitoa wito wa kutekelezwa sheria za Kiislamu kwa ajili ya Waislamu wa Uingereza ili kuboresha uhusiano wa nchi hiyo na Waislamu na akatangaza kuwa Uingereza inapasa kutambua uhakika kwamba baadhi ya wananchi wa nchi hiyo hawana uhusiano mzuri na mfumo wa kisheria wa Uingereza.
Karibu Waislamu milioni 2.5 wanaishi nchini Uingereza
No comments:
Post a Comment