Wednesday, April 4, 2012

NASAHA - UNAPOKUWEPO KAZINI


Anasema Allah Subhaanahu Wata’aala katika Quraan Suuratul Hajr / 92-93 kwamba:

                                        فَوَرَبِّكَ لَنَسْـَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ - عَمَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ

Basi Naapa kwa Mola wako ! Tutawahoji wote . Kwa waliyo kuwa wakiyatenda

Wengi wetu tumekuja katika nchi hizi zisizokuwa za kiislamu kwa minajili ya kutafuta rizki ambayo Allah(Subhaanahu Wata’aala) ameitandaza katika ardhi kama anavyosema katika Suuratul Mulk/12

  النُّشُورُ هُوَ الَّذِى جَعَلَ لَكُمُ الاٌّرْضَ ذَلُولاً فَامْشُواْ فِى مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ وَإِلَيْه

Yeye ndiye aliyeidhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.

Hivyo tutakuwa wizi wa fadhila kama hatutamshukuru Allah Subhaanahu Wata’aala kwa kutuwezesha kufanikisha azma yetu hii na pia kwa kutupa uwezo na afya /uzima wa kuweza kufanya kazi . Pia tutatakiwa kuzingatia yafuatayo wakati tupo kwenye hizi ajira zinazotupatia rizki zinazokwenda kwenye matumbo yetu , na ya ahli, watoto na wote wanaotutegemea kwani mwisho wa aya Allah (Subhaanahu Wata’aala) anatutanabahisha kwamba kutakuwa na kufufuliwa na kuulizwa  kwa kila jambo mpaka hili la rizki inayoingia kwenye matumbo yetu. Kama hadithi ya Mtume  inayosema :

“Hautoinuka mguu wa mja siku ya kiama mpaka aulizwe juu ya mambo mane: Umri wake jinsi alivyoutumia, ujana wake vipi alivyoupitisha na mali yake wapi alipoichuma na wapi alipoitumia na elimu yake jinsi alivyoifanyia kazi”

                                                                                 Attirmidhiy

Hivyo

1                   Mkumbuke Allah(Subhaanahu Wata’aala) na utawakkal kwake kila wakati na hasa unapokuwepo kazini.Unaweza kuleta dhikr na kumtaja huku unafanya kazi au kusoma Quraan kama umehifadhi ikiwezekana na hata kujikumbusha hadithi za Mtume  na mengineyo kwani sehemu nyingi za kazi zimetawaliwa na haramu ya aina kwa aina kama miziki na mfano wake.

2                   Fanya kazi kwa Ikhlaas.

Hakikisha unapofanya kazi unafanya kwa ikhlaas nako ni kufanya kazi ipasavyo. Kigezo hiki ndicho kinachogeuza kazi hii na kuwa si kazi tu bali pia ni ‘ibada. Kusiwe na kutegeategea au kwa kumuogopa  msimamizi(supervisor) na huku Allah(Subhaanahu Wata’aala)  tunaetakiwa kumuogopa anatuona .  Lile pato tutakalojaaliwa tuwe tumelipata kihalali na kwa mujibu wa jasho letu..

3                   Fanya kazi kwa ufanisi kama  inavyotakikana

Tukifanya kazi vizuri ndipo tutakapopendwa na Allah (Subhaanahu Wata’aala) pamoja na Mtume wake  kwani Mtume  ametukumbusha katika hadithi kwamba:

 Hakika Allah anampenda mja wake akifanya amali huifanya kwa ufanisi.  

4          Kumbuka kufanya Da’awah kazini.

Kuwalingania wasiokuwa waislamu kwa kauli na vitendo ni moja katika mambo ambayo sheria yetu imeturuhusu kuishi katika nchi zisizokuwa za kiislamu. Jenga mfano bora wa kuigwa kitabia na kivitendo kazini.Pia uwalinganie wengine kwa njia nzuri kwa kadri ya elimu kidogo uliyojaaliwa.

5          Heshimu mkataba. Suuratul Maaidah/1

                           يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَوْفُواْ بِالْعُقُودِ

                  Enyi mlio amini! Timizeni ahadi

Na Pia suuratul Israai/34

                           وَأَوْفُواْ بِالْعَهْدِ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْؤُولاً

           Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa

Kumbuka si miongoni mwa tabia ya muislamu kutoheshimu                          mkataba aliosaini kwa khiari yake kwani kufanya hivyo ni kupatikana chembe chembe za unafiki kwani ni moja katika alama za watu wanafiki wakitoa ahadi huwa hawatimizi. Unaposaini mkataba unatoa ahadi ya kutekeleza yaliyomo kwenye mkataba ule. .

6           Jiepushe na dhambi za kimwili.

Kuchanganyika na wanawake, kuiba (kumbuka utakachokichukua ni amana na utakwenda kuulizwa) Annisaa/58

                      إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤدُّواْ الْأَمَانَةَ إِلَى أَهْلِهَا

 Hakika Allah anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe

                         

7           Jiepushe na dhambi za ulimi

Tahadhari sana ukiwepo kazini kutumia lugha ya matusi(wengine tunaona fahari kuiga) kusengenya, kufitini, kuzua na kadhalika kwani zote hizi ni dhambi na hazibadiliki kuwa halali kwa sababu ya kumtukana asiye muislamu au kwa kisingizio cha kuishi katika mazingira yanayoruhusu utamaduni huu.

8           Hakikisha kazi yako haiwezi kukukosesha mambo ya wajibu   

        katika dini.

  Kama kuzisali sala tano kwa wakati wake, kusali sala ya Ijumaa (ni fardhi ya lazima) na haiwezi kukuathiri katika kutekeleza funga ya Ramadhan ni moja katika nguzo tano za kiislamu na pia  kwa mwanamke kukufanya uvue vazi zuri alilokutaka Allah (Subhaanahu Wata’aala) ujistiri nalo (hijaab).

وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجاً - وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لاَ يَحْتَسِبُ  

            وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

Na anaye mcha Allah humtengezea njia ya kutokea Na humruzuku kwa njia asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Allah yeye humtosha.

Wabillahi Ttawfiyq

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget