Wednesday, April 4, 2012

'Marekani inatekeleza hujuma za kigaidi Nigeria'

Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaki amesema Marekani ndio inayotekeleza hujuma za kigaidi kote Nigeria.

Katika mahojiano na Idhaa ya Kihausa ya IRIB, Sheikh Ibrahim Zakzaki amesema shirika la kijasusi la Marekani CIA ndio ambalo limekuwa likitekeleza hujuma za mabomu katika miji mbali mbali ya Nigeria.


Sheikh Zakzaky amesema Marekani inalaumu kundi la Boko Haram kuwa linahusika na hujuma za mabomu ili kuwadhoofisha na kuwagawa Waislamu Nigeria.
Sheikh Zakzaki amesema watu wanaodai kuwa wasemaji wa Boko Haram ni mamluki ambao hawana uhusiano wowote na itikadi za Kiislamu.
Sheikh Zakzaki ambaye ni mkuu wa Harakati ya Kiislamu Nigeria amesema Marekani inajaribu kuingilia mambo ya ndani ya Nigeria kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. 

Amesema Marekani ndio inayoibua magaidi. Katika miezi ya hivi karibuni, watu wengi wameuawa na kujeruhiwa katika hujuma za mambomu kote Nigeria.


SOURCE: http://kiswahili.irib.ir/index.php?option=com_content&view=article&id=23097:marekani-inatekeleza-hujuma-za-kigaidi-nigeria&catid=1:latest&Itemid=74

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget