Wednesday, April 4, 2012

Nasaha Kwa Muwaidhishaji Na Mwenye Kuwaidhiwa


Fudhail aliwahi kusema katika maneno yake ya busara kwamba, Muumini wa kweli humfichia (siri na makosa ya) ndugu yake wa kiislam na kumuwaidhi lakini mwenye kuasi humuaibisha na kumtangazia
Hapa Fudhayl anatuonesha tofauti kati ya kuwaidhi na kupakazia kwani kuwaidhi kunafungamana na usiri na  kuaibisha  kunakwenda sambamba na kumtangazia muislamu maovu yake badala ya kumuwaidhi kwa kutumia hekima, nasaha na busara .
Salaf ( waislamu wa mwanzo mwanzo) walikuwa hawapendezwi na kutumia njia hii katika kuamrishana mema na kukatazana maovu ;wao walipendelea kazi hii ifanyike kwa faragha kati ya muwaidhishaji na mwenye kuwaidhiwa kwani lengo kuu la mwenye kuwaidhi ni kujaribu kurekebisha na kutengeneza na si kutangazia maovu ya mwenye kuwaidhiwa na hivyo kumfanya aadhirike au aaibike mbele ya jamii.
Kwa kutangazia maovu kuna hatari ya kuingia katika yale yaliyokatazwa na Allah(Subhaanahu Wata’ala) Suuratu Nnuur 19-20
إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَـحِشَةُ فِى الَّذِينَ ءَامَنُواْ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِى الدُّنْيَا وَالاٌّخِرَةِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ وَلَوْلاَ فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ                                                                                                            
Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Allah anajua na nyinyi hamjui
Na lau kuwa si fadhila ya Allah juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Allah ni mpole, mwenye kurehemu
عنَ تَمِيمِ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلم قالَ:"الدِّينُ النَّصِيحَةُ". قُلْنَا: لِمَنْ ؟ قالَ: "للهِ، ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ"                                                    
رَوَاهُ مُسْلِمٌ    
Kutoka kwa Tamim Addaarriy (Allah amuwie radhi) :  Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam)  amesema:
Dini ni nasiha.  Tukauliza: Kwa nani? Akasema kwa Allaah, Kitabu chake, na Mtume wake, na kwa Viongozi wa Waislamu, na watu wa kawaida (kuusiana mema na kukatazana mabaya kwa njia nzuri).
Imesimuliwa na Muslim
Muwaidhishaji  kama tulivyosema ana lengo anataka kulifikia nalo ni kujaribu kumuondoa muislamu mwenzake katika uovu, maasi, uchafu au dhambi ambao tayari anaifanya na pia kumsaidia kuepukana na uovu huo. Sasa kwa kumtangazia au kumpakazia sidhani kama itakuwa rahisi kulifikia lengo hili . Ndiyo maana Allah (Subhanahu Wata’ala) anamsifia Mtume wake (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) katika Attawbah/128
لَقَدْ جَآءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُمْ بِالْمُؤْمِنِينَ                    
                                                                                                                         رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana(ili apate kukuondoeni kutoka katika makosa na dhambi). Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.
Na pia Allah(Subhaanahu Wata’ala) anawasifia masahaba wake Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) katika Suuratul Fat-h/29
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّآءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَآءُ بَيْنَهُمْ                               
Muhammad ni Mtume wa Allah. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao
Nasaha hizi ni maalum kwa muwaidhishaji kwenda kwa mwenye kuwaidhiwa as individuals - mtu kwa mtu na sio kwa Imaam au Sheikh au kiongozi wa waislamu kama akiyataja matendo maovu yanayofanywa na jamii kwa ujumla kwa lengo lile lile la kuyarekebisha.
Wabillahi Tawfiyq

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget