Tuesday, April 10, 2012

Wasemavyo Wanaharakati


UKOLONI uliupa unyonyaji jina lake. Ukaunyang’anya madhumuni yake. Mapinduzi yoyote ya kijamii ni lazima yatanguliwe na mapinduzi ya kiroho. Nchi za Kiislamu bado ni wateja wa nchi nyingine katika mawanda yote. 
Ufumbuzi wa matatizo ya Waislamu hautapatikana kwa kuukata mkono wa mwizi. 
Fikra za maana hubaki ni wino juu ya karatasi muda wakuwa hazijapata watu wa kuzifasiri katika matendo. 
Itikadi ya Kiislamu ni itikadi ya kimapinduzi katika mawanda yote. 
Ni lazima uwe Msikiti na majukwaa na vyombo vyote vya habari upande mmoja. 
Ufumbuzi wa Kiislamu wa matatizo ya wakati huu, hautapatikana ila kwa kuufungua mlango wa jitihada kwa kila anayeweza. 
Ufumbuzi wa Kiislamu ndio pekee unaovuka upande wa kimaada na kwenda upande wa kiroho. 
Kuzibadilisha silaha na zana nyingine, ni rahisi lakini ugumu wa kweli ni kumbadilisha na kumjenga mwanaadamu. 

Kinachowapungua Waislamu ni kufikiri na kutenda kwa ukweli.  
By Dr. Yousuf Alqardhawy.  

-------------------------------


Hatakuwa mtu ni mwenye kuamini dini hii mpaka afanye mafunzo yake ndiyo yanayo tawala. 
Maarifa katika dini yanageuka pale pale kuwa ni harakati. 
Ujuzi wa Uislamu hautakuwa na thamani mpaka ugeuke kuwa harakati. 
Mtazamo wa Kiislamu unatenganisha moja kwa moja kati ya tabia ya uungu na tabia ya ubinaadamu. 
Dini ni haja ya maumbile kwa wanaadamu. 
Uhalisi wa maisha ya kisiasa, ya kijamii, ya kiuchumi, ya kitabia na ya kielimu, hayatakuwa hayo ila ni tafsiri ya kimatendo ya Uislamu. 

Wale wanaozichukua aya za Qur’an wakienda nazo nyuma ya nadharia za kisayansi zilizoenea wakati huu, hao wanaifuata njia ya Kanisa lilivyokuwa mnamo karne za kati pasina wao kuelewa.  
Shaheed Sayyed Qutub.  

-------------------------------


Ni lazima awe mwanadamu ndio kipimo cha mambo yote. 
Uislamu ni dini ya maumbile. 
Kumwamini Mwenyezi Mungu ni hakika iliyothabiti, kutokana na kuthibiti hakika ambayo imetegemea juu yake, nayo ni kupatikana Muumba na muumbwa. 
Itikadi ina sehemu inavyobadilika wakati wote nayo ni sehemu ya sheria na mipango. 
Uislamu wanao msingi safi wa nguvu na maendeleo ya kibinadamu. 
Nafasi ya Waislamu ni kuwa mbele siku zote, na kushika hatamu za dola. 
Ni lazima Waislamu waiendeleze Fiqh ya Kiislamu ili iende sambamba na maisha ya sasa karne ya ishirini. 

Waislamu wanayo haja ya kuzijua nchi za Magharibi na kuzijua nguvu zao za kimaada.  
Ustadh Muhammad Qutbu  

-------------------------------


Uislamu unamtambua kiumbe mwanaadamu kama alivyo. 
Dini ni kumwabudu Muumba ambaye vitu vyote vinatokana na Yeye. 
Mwanaadamu katika mtazamo wa Uislamu ni kiumbe ambaye si malaika wala si shetani. 
Lengo kuu la juu ya Uislamu ni kujenga uwiano katika nafsi ya mtu. 
Uislamu unachukia kukosekana uwiano. 
Uislamu uko wazi katika kuyabadili ya mwanaadamu. 
Hapana mgongano kati ya Uislamu na kati ya maslahi ya mtu mmoja na jamii. 
Uislamu ulilipa kipaumbele suala la tabia njema. 
Hapana mgongano kati ya kazi na ibada. 
Kila wito mpya lazima ukabiliane na upinzani mkali. 
Kunawkati fikra huwa wzi kutokana na upinzani. 

Uislamu unachukia kuukimbia ukweli.  
- Alustadh Muhammad Qutub  

-------------------------------


Dini msingi wake ni uhusiano kati ya mtu na ulimwengu wote. 
Muislamu hagawanyiki kati ya dunia na akhera. 
Hapana katika Uislamu kuwa kunakosa lililorithiwa na wanaadamu wote. 
Hapana katika Uislamu utenganisho kati ya mambo ya Mwenyezi Mungu na mambo ya Caisar. 
Uislamu unampenda Muislamu anayefanya kazi na unamchukia yule asiyefanya kazi. 

Uislamu haukukusudia kwa kufaradhisha zaka kuifanya ndiyo ufumbuzi wa tatizo la umasikini.  
- By Abbas Mahmoud Al-Aqad  

-------------------------------


Ujumbe wa Uislamu katika misingi yake na matawi yake, ni jengo lililokamilika linalowiana na maumbile ya mwanaadamu. 
Uislamu ni jambo zima lisilogawika ima uchukuliwe wote au uachwe wote. 
Uislamu haukati mahusiano yake na wale ambao hawakuamini muda wa kuwa hawana vita nao. 
Uislamu unaihesabu kila kazi yenye manufaa kijamii kuwa ni Ibada muda wakuwa mtendaji wake amekusudia kheri. 
Jamii ya Kiislamu ni ile ambayo Uislamu unatekelezwa ndani yake itikadi, ibada, sheria, utaratibu, tabia na mwenendo. 
Mwanaadamu anaongozwa kwa ndani yake si kwa nje yake. 

Kuuhama ulimwengu na kuzama katika utawa kuna kwenda kinyume na mwongozo wa Uislamu.  
By Omr Duda Al-Khatib  

-------------------------------

Nusu ya Uislamu imekufa au imedumazwa, na nusu yake nyingine ndiyo iliyoruhusiwa kuishi na kufanyiwa harakati. 
Maadui wameviunganisha vita vya utamaduni na vita vya kijeshi dhidi ya Waislamu. 
Haukuparaganyika umoja wa Waarabu ila baada ya kuupza kwao kushikamana na dini yao na kitabu chao kitukufu. 
Itikadi ya Uislamu katika mjengo wa jamii ni kama moyo katika mwili wa mwanaadamu. 
Waislamu wameshughulika na maganda wameacha kiini. 
Ufukara wa Waislamu ni ufukara wa tabia njema na vipaji nasi ufukara wa rizki na uwezo. 
Kuzijenga nafsi na dhamiri kunatakiwa kuwe mwanzo kabla ya kujenga viwanda. 

Wameharibikiwa Waislamu leo kutokana na kujihusisha kwao na Uislamu kwa udanganyifu.  
By Sheikh Muhammad Al-Ghazaly  
-------------------------------

Maisha ya mwanaadamu ya kimaada hayatengani na maisha yake ya kiakili na kiroho. 
Ulimwengu ni alama ya kupatikana kwa Mwenyezi Mungu na ni onyesho la uwezo wake. 
Kuna uhusiano mkubwa kati ya nafsi na mwili. 
Uislamu hauipuuzi hali halisi ya ardhi, na wala haupuuzi ulimwengu wa maada, na historia ni shahidi mzuri juu ya hilo. 

Maisha ya ulimwengu ni mahangaiko, na usumbufu na taabu na kushirikiana kusiko koma kati ya watu na matukio.  
By Al-Ustadh Muhamad Qutub  

-------------------------------

Katika Uislamu hakuna ukudhani wala ukati na kati kati ya Muumba na viumbe. 
Uislamu hauna ugumu na sayansi na wala hauna chuki na wataalamu. 
Siyo lengo la swala na dua kuwa ni matamshi ya ulimi na harakati za viungo, bali lengo ni kuelekea kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya moyo. 
Uislamu siyo utaratibu uliyodumaa. 
Kufanya kazi ndiyo nyenzo pekee ya kupata haki ya kumiliki katika Uislamu. 
Uislamu unawachukia watu ufukara na umaskini. 
Muislamu haruhusiwi kujifunza mambo ya itikadi ila kwa Muislamu anayemwamini katika dini yake na ucha Mungu wake. 
Muislamu anaruhusiwa kujifunza mambo ambayo si ya itikadi kutoka kwa asiye Muislamu. 
Elimu haihusiki na elimu ya itikadi na mambo mengine yanayohusu dini, bali elimu katika Uislamu ina kusanya kila kitu. 

Umekuja Uislamu kumwendeleza mwanaadamu.  
By Sayyed Qutub.  

-------------------------------
Jamii ya Kiislamu ni huu umma ambao umekutana pambizoni mwa dini. 
Jamii za mashariki na magharibi hazikufanikiwa kuyatatua matatizo ya wanaadamu. 
Jukumu la Uislamu ni kuyaongoza maisha kwenye kumjua MwenyeziMungu. 
Si katika uadilifu kuutenga Uislamu na kuitenga jamii. 
Uislamu haufurahi mpaka watu watakapo yasimamisha maisha yao juu ya msingi wake. 
Imeweza jamii ya Kiislamu tokea kusimama kwake, kuvunja misingi ya ubaguzi wa namna zote. 
Uislamu unaleta usawa kati ya watu wote. 
Uislamu umeweka kipimo kipya cha ubora kati ya watu nacho ni uchaji. 
Uislamu unakubali kutofautiana kwa watu katika uwezo na vipaji. 
Uislamu haukubali mfumo wa matabaka katika jamii ya wanaadamu. 
Ukomunisti umeshindwa kuwafanya watu walingane katika mambo yote. 
Kuunganisha kati ya dunia na akhera ni katika utaratibu wa Uislamu. 
Uislamu unaona kuwa kuhangaika katika kutafuta riziki ni katika kuipigania njia ya Mwenyezi Mungu. 
Kufanya kazi ndiyo njia bora sana katika Uislamu na kujipatia chakula na mahitaji mengine. 
Kufanya kazi ndiyo njia iliyobarikiwa. 
Elimu katika mtazamo wa Uislamu ndicho kilele cha uongofu. 
Duara ya elimu katika Uislamu ni pana sana. 
Uislamu umeufanya ulimwengu wote kuwa ni uwanja wa utafiti. 
Siyo sahihi kuwa Uislamu unaona kuwa lililobora kwa mwanamke asiwaone wanaume na wao wasimuone yeye. 

Jamii ya Kiislamu inatofautisha kati ya pumbao na michezo iliyoruhusiwa na kati ya maradhi ambayo yanajipenyeza katika mawanja mbalimbali ya maisha yetu.  
By Dr. Mustafa Abdulwaheed  

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget