Ndugu katika imani, suali la mwanamke ni suali ambalo liliwashughulisha watu
wengi walio pita, na linendelea kuwashughulisha wengi katika zama zetu hizi.
Dini na mila mbalimbali zimezungumzia hali ya mwanamke katika jamii. Wasomi wa
ilimu na falsafa tafauti wamejaribu kuzugumzia cheo cha mwanamke katika jamii.
Lakini kila kundi linajaribu kuzungumzia mwanamke kwa misingi ya kufikia
malengo yao. Katika khutba hii tutajaribu kuangazia cheo cha mwanamke katika
jamii mbalimbali. Tutangalia hali ya mwanmke kabla ya kuja Uisalmu, na haliyake
katika Uisalmu, na haliyake katika mataifa ya magharibi.
Hali ya Mwanamke kabla ya kuja Dini ya kiislamu
Alikuwa mwanamke katika zama za ujinga akionekana kama
bidhaa ambao haina thamani. Kila mtu anaweza kumiliki bidhaa hio wakati wowote.
Wanaume wakiowa wanawake bila ya idadi maulumu na kuacha bila ya idadi ya
talaka. Mwanamke haruhusiwi kumiliki chochote, hana haki ya kurithi, anaweza
kuolewa na zaidi ya mume mmoja. Mwanamke hakuwa na cheo katika jamii ya
ujahiliyah, bali alikuwa akionekana ni mtu anaye leta aibu katika
jamii. Ikafikia hali hio, baaadhi ya wanaume kuwazika mabanati wao wakiwa
wadogo kuogopea kuleta aibu katika jamii. Mwenyezi Mungu (SW) Anatueleza hali
ya mwanamke Akisema:
قال تعالى:
{وإذا بشر أحدهم بالأنثى ظل وجهه مسودا وهو كظيم. يتوارى من القوم من سوء ما بشر به أيمسكه على هون أم يدسّه في التراب ألا ساء ما يحكمون}
{{ Na mmoja katika wao anapopewa khabari ya kuzaliwa
mtoto wa kike, unabadilika uso wake huwa mweusi na akajaa sikitiko. Anajificha
na watu kwa sababu ya khabari mbaya ile alioambiwa. (anafanya shauri) Je, akae
naye juu ya fedheha hiyo, au amfukie udongoni. Ni mbaya mno hukumu yao hiyo}}.
Hii ndio hali halisi ya mwanamke kabla ya kuja Dini ya kislamu. Na hali hii
ilikuwa sawa katika mataifa yote, sawa taifa la kiarabu na wasiokuwa
waarabu.
Baada ya mwanamke kuishi katika dhulma kwa mda mrefu,
bila ya kupata haki zake. Allah (SW) Alimtumiliza Mtume (SAW) wake kuja
kumkomboa mwanamke na dhulma na udhalilifu alikuwa akipata kutoka kwa jamii
anayo ishi. Dini ya kislamu inamtukuza mwanamke na inampa haki zake zote katika
jamii. Miongoni mwa haki hizo”-
قال تعالى: {من عمل صالحا من ذكر أو أنثى وهو مؤمن فلنحيينه حياة طيبة ولنجزينهم أجرهم بأحسن ما كانوا يعملون}
{{ Wafanyaji mema, wanaume au wanawake, hali yakuwa ni
Waislamu, tutawahuisha maisha mema, na tutawapa ujira wao mkubwa kabisa}}. Na
Mwenyezi Mungu (SW) alimfadilisha mwanamume kuliko mwanamke katika baadhi ya
mambo, kwasbabu ya majukumu mazito ya mwanamume katika kusimamia familiya.
وقال
سبحانه : { للرجال نصيب مما ترك الوالدان والأقربون وللنساء نصيب مما ترك الوالدان والأقربون مما قل منه أو كثر نصيبا مفروضا}
{{ Wanaume wana sehemu katika mali wanayoyacha
wazazi wao na jamaa waliokaribu. Na wanawaake pia wanayo sehemu katika yale
waliyayacha wazazi wao na jamaa waliokaribu. Sawa yakiwa kidogo au mengi. Ni
sehemu zilizofaridhishiwa (na Mwenyezi Mungu)}}.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu mabao mwanamke amepewa
katika Dini ya kislamu. Na hii ndio halihalisi ya mwanamke katika Uislamu.
Uislamu ilimrejeshea mwanamke haadhi na utukufu wake katika jamii, na ikatambua
mchango wake mkubwa katika kuandaa kizazi cha kesho na kulea viongozi wa
kusimamia Dini ya kislamu. Amesema Mtume
(SAW) katika Hija: [ Mcheni Mwenyezi Mungu katika kuwasimamia wanawake,
kwasababu wao ni wasaidizi wenu]. Mtume
anaweka wazi cheo cha mwanamke nacho ni wasaidizi wa wanaume, sio mtumwa au
mtumishi kama wanavyomdai watu wengine kwamba uislamu umefanya
mwanamke kuwa ni mtumwa hana haki yoyote katika jamii.
Enyi waja wa Allah, tumcheni Allah na tufanyeni bidii
kuwasimamia wake zetu kulingana na alivyo tufundisha Mwenyezi Mungu (SW).
Ndugu Waislamu, na wausieni na kujiusia nafsi yangu
kumuogopa Allah (SW), kwani wachaji Mungu ndio wenye kufaulu. Ndugu katika
imani, tuangalieni hali ya mwanamke katika nchi zilizoendelea kama wanavyo dai
nchi za kikafiri.
Hakika hali ya mwanmke katika nchi hizi ni mbaya sana
kushinda hali ya mwanamke katika zama za jahiliyah. Mwanamke amefanywa na
kivutio wa kila badhaa au biashara kwa kudhihirisha uchi wake bila ya kujali
wala kuona haya. Kila tukiangalia runinga, kusoma magazeti, internet
tunashuhudia mwanamke ndiye wakwanza kuonyesha hali akiwa uchi kabisa kwa lengo
la kuvutia watu katika biashara hio. Kwa kweli mwanamke amepokonywa haki zake
zote za kimsingi, haki ya kusimamia majukumu ya nyumba, kulea watoto, kuandaa
familya juu ya misingi ya tabia njema na maadili mazuri.
Leo mwanamke hana nafasi nyumbani, kazi yake kubwa
nikutoka nje na kwenda kushindana na wanaume, na kudai haki za wanaume katika
kazi. Imekuwa hakuna tafauti baina ya mume na mke. Na hili ndilo lengo kubwa la
makafiri kumtowa mwanamke nje na kumvunjia hishima yake aliopewa na Allah (SW).
Na baadhi ya wanawake wakislamu wameathirika na tabia mbaya za makafiri.
Wakaona haya ndio maendeleo na kuenekana umeendelea.
Ndugu waumini, ni wajibu wetu kama wazazi
kuwatahadharisha wake zetu mabanati wetu na kasumba mbaya za makafiri. Na
tujuwe makafiri hatokuwa radhi mpaka tufuate mila zao. Amesema Mwenyezi Mungu
(SW):
قال تعالى:
{ ولن ترضى عنك اليهود ولا النصارى حتى تتبع ملتهم قل إن هدى الله هو الهدى ولئن اتبعت أهوائهم بعد الذي جاءك من العلم مالك من الله من ولي ولانصير }
{{ Hawatukuwa radhi juu yako Mayahudi wala Wakristo mpaka
ufuate mila yao. Sema hakika uwongozi wa Mwenyezi Mungu ndio uwongozi wa sawa.
Na kama ukifuata matamanio yao baada ya yale yaliyokufikia ya ujuzi, hutapata
msaidizi yoyote wala mlinzi kwa Mwenyezi Mungu}}.
Mwisho ndugu Waislamu, tukumbuke malipo na fadhila
atakazo pata mwenye kumlea msichana malezi ya kislamu kisha amuuzeshe mume
mwenye taabia njema basi huyo amedhaminiwa kuingia peponi. Amesema Mtume (SAW): [ Mwenye kuruzukiwa mabinti wa tatu, na
akasubiri juu ya kuwalea, kwahakika mtu huyo amewajibika kuingia peponi.
Akasema mtu kumuuliza Mtume: vipi ukiwa na wasichana wawili?. Akasema Mtume na
wawili pia ni sababu ya kuingia peponi].Ndugu
waumini, angalieni rehma ya Allah juu yetu katika kusimamia majukumu ya Allah
kwa kuwalea wasichana kwa maadili mema na tabia njema, Allah atakulipa pepo
yake ambayo sirahisi ya kuingia kila mtu, ispokuwa watakao simamia majukumu
hayo.
Tunamuomba Allah atuafikie tuweze kutekeleza majukumu
yote kwa njia ya kumridhisha yeye peke yake. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu
awahifadhi watoto wetu na kila shari ilio dhahiri na siri.
No comments:
Post a Comment