Wednesday, April 4, 2012

Unataka Kupata Nuru na Mwangaza Katika Maisha Yako?


Imekusanywa na

 Abu ‘Ammaar – Abdurrazzaaq K. Khiari

Basi Sali kwani Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam Amesema:

“Sala ni Nuru”
Unataka kujiepusha na maovu na maasi?

Basi Sali kwani Allah Subhaanahu Wataa’ala amesema:

Hakika Sala inamkataza mtu na mabaya na maovu


Unataka kurahisishiwa hesabu za amali zako siku ya kiama ?

Basi Sali kwani Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam amesema:

“Jambo la mwanzo atakalohesabiwa mja siku ya kiama ni Sala. Zikipita, basi na amali zake nyengine zote zitapita”


Unataka kupata cheo na hadhi ya kipekee?

Basi Sali kwani Allah Subhaanahu Wata’ala amesema:

Simamisha Sala jua linapopinduka mpaka giza la usiku, na Quraan ya alfajiri. Hakika Quraan ya alfajiri inashuhudiwa daima

Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya sunna hasa kwako wewe. Huenda Mola wako akakunyanyua cheo kinachosifika


Unataka kuisimamisha dini yako?

Basi Sali kwani Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam amesema:

“Hakika sala ni nguzo ya dini mwenye kuisimamisha ameisimamisha dini na mwenye kuiacha ameivunja dini.”

Unataka kuzungumza  moja kwa moja na mola wako?

Basi Sali kwani Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam amesema:

“Hakika mmoja wenu anaposali, huwa anazungumza na mola wake”


Unataka mwili wako utoharike na maovu?

Basi Sali kwani Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam amesema:

Mnaonaje kama mto ukipita  mbele ya nyumba ya mmoja wenu na anajitoharisha  kila siku mara tano. Atabakiwa na uchafu? Wakasema ; “hatobakiwa na chochote” Mtume akasema: “ (Huo ni) mfano wa Sala tano, Allah huzifutia madhambi”


Unataka msaada?

Basi Sali  kwani Allah Subhaanahu Wata’ala amesema:

Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu


Unataka kuijua amali iliyo bora?

Basi Sali kwani Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam alipoulizwa kuhusu amali bora alisema:

“Sala inayosaliwa kwa wakati wake”


Ndugu yangu katika Imani, kumbuka Wasia wa mwisho wa  kipenzi chetu Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam kabla ya kuondoka duniani.  

Alituusia tumuogope Allah Subhaanahu Wata’ala katika suala zima la kuSALI.

Hivyo tujihimu kuitikia wasia wa  Mtume wetu kwa kuSali kabla wengine hawajatusalia.



No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget