Thursday, April 12, 2012

Haki za mwanaume


Qurani Tukufu imekusanya kanuni zote za maisha ya nyumbani.Kama ilivyoelezwa hapo awali kimaumbile mwanamke ni jinsia dhaifu.Kwa hivyo asitegemewe kujitia katika machachari ya kutafuta maisha;badala yake mwanamme ndivyo inavyombidi atafute kwa ajili ya wote. Iwapo nyumba ni ufalme basi mwanamme ni mfalme na mwanamke ni waziri mkuu.Aya hii inatuelezea vitu vitatu vilivyo vya hakika.Hebu tujaribu kuangalia na kuchambua :-

Allah swt amempatia mmoja zaidi kuliko mwingine; Aya hii inatuelezea vile nguvu zilivyo za mwanamme katika kumlinganisha mwanamke.

Mwanamme na mwanamke: Tofauti ya uwezo wao.
Ni ilimu ya kawaida na inajulikana kisayansi kuwa mwili wa mwanamke kwa wastani uko dhaifu kuliko ule wa mwanamme. Ulinganishi ufuatao utasaidia kidogo kuelezea swala hili:-

1. Moyo:
Uzito wa moyo wa mwanamme ni baina ya gramu 280 hadi 340 wakati uzito wa moyo wa mwanamke ni kutoka gramu 230 hadi 280. Ujazo wa moyo wa mwanamme anapokuwa na umri wa miaka hamsini (50) anapofikia c.c.290, wakati upande wa mwanamke kwa baadhi yao ni 50c.c yaani chini ya 50c.c. (Gray's anatomy, chapa ya 28, 1945 ; uk. 672).
2. Misuli.
Farid Wajid Afind (Misri ) anaandika katika kitabu chake mwanamke nguvu na uwezo wa mishipa ya mwanamke ni nusu ya ile ya mwanamme; na huo ndiyo uwiano wa vile mishipa inavyofanya kazi.
3. Urefu.
Wastani urefu wa mwanamke upo chini ya sm 12 (kiasi cha inchi 4 3/4) kasoro ya mwanamme.
4. Uzito.
Kwa kawaida wastani wa uzito wa mwanamke ni kilo 5 kasoro ya uzito wa mwanamme.
5. Damu.
Idadi ya chembe chembe nyekundu katika mraba wa milimita ya damu ya mwanamme ni milioni 5 na mwanamke ni milioni 4 1/2. (Gray's anatomi).

Tofauti baina ya nguvu zao.

1.Farid Wajid Afind ananakili kwa mamlaka kuwa sehemu tano za hisia za mwanadamu (kuona, kusikia, kunusa, kuonja na kugusa, ambavyo ndivyo muhimu katika kuhisi) vya mwanamke ni dhaifu kuliko vya
mwanamme.
2. Akili, kwa wastani uzito wa akili ya ubongo wa mwanamme ni kiasi cha gramu 1380; na wa mwanamke ni kiasi cha gramu 1250 (Gray's anatomi, jalada la 28, 1945; uk. 1024) uwiano wa ubongo wa mwanamme kwa mwili wake mzima ni 1: 40; na wa mwanamke ni 1:44.
Kama tulivyoona vitu hivi vitano ndivyo vinavyofanya mwili wa mwanadamu uwe umekamilika.
Lau vitu hivi vitano vya mwanadamu vitakuwa dhaifu basi bila ubishi tutaona kuwa huyo mwanamke ni dhaifu kabisa kimaumbile.
Farid Wajid Afind ananakili kuwa akili ya mwanamke ni kama za mtoto. Mtoto ataanza kulia atakapokumbana na hali ya kumtatanisha; na ataanza kurukaruka na kufurahi sana anapokuwa na furaha. Na ndivyo hivyo ilivyo hali ya mwanamke ambaye ukulinganishwa na mwanamme anaathirika sana na hisia kama hizo.
Allah swt amemuumba mwanamke awe mwenye hisia kali kuliko mwanamme ni kwa sababu alivyoumbiwa yaani mama. Mwanamke anatoa maamuzi yake haraka kwa mujibu wa hisia zake bila ya kutumia busara, akili au uhodari wake. Na labda kwa sababu hizi na undani mwa swala hili ndio maana Qurani Tukufu inachukulia ushahidi wa wanawake wawili kuwa sawa na ushahidi wa mwanamme mmoja.
Ni jambo la masikitiko sana kuona kuwa jamii zisizo za Kiislamu zimemlazimisha huyu mwanamke dhaifu kujitwisha mzigo mara dufu juu ya mabega yake, kwa kutapeli uonevu huu ati kwamba ni kushirikishwa kwa wanawake na haki zake sawa na manaume.

Je kushirikishwa huku kuna maanisha nini?
Mwanamke bado anahitajika kutimiza wajibu wake wa kimaumbile wa kushika mimba, kuzaa na kulea watoto.Wakati mwanamme hafanyi hivyo na wala mwanamme hawezi kushirikiana naye katika kumbebea mwanamke mimba, kunyonyesha watoto, kuwalea, au kuangalia watoto na kufanya kazi zote zinazojulikana kama kazi za akina mama; hali hii mwanamke ndiye anayebeba mzigo huu lakini pamoja na wajibu huu nyakati zote, mwanamme bado anamwambia mwanamke "tushirikiane kutafuta mapato ya kuendesha maisha yetu.
"Kwa kifupi jinsia mwenye nguvu amemkomboa jinsia dhaifu katika kubeba mzigo wake bila ya yeye kumsaidia mwanamke mzigo wake Masikini mwanamke bado anazuzuliwa kwa sauti zinazopaazwa za uhuru na ushirikishwaji wa wanawake bila ya kutambua njama na mbinu za mwanamme za kumtwisha mzigo wake.Kwa kweli sitakuwa na nafasi ya kuorodhesha maafa -kijamii,kinyumbani na kiuchumi -unaotokana na mwanamke kujiingiza katika harakati hizi za kuchuma mapesa.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget