Monday, February 13, 2012

Ukweli juu ya Masihi Dajjal/Fake Messiah


Ukweli juu ya “Masihi Dajjal” yaani  “mtu wa mfano wa Yesu Kristo”
Siku moja hadhrat ali (a.s.) mwishoni mwa hotuba yake katika msikiti wa kufa aliwaomba watu wamwulize maswali wanayotaka kabla yeye kufariki dunia.
sasa bin sawhan akasimama na kuuliza: "eh kiongozi wa waumini! wakati gani hadhrat hujjat atatokeza"? hadhrat ali (a.s.) akajibu: "kwanza zitatokeza alama nyingi moja baada ya moja. sikiliza kwa makini kuhusu hizi alama na uzikumbuke. watu watapotosha dhana ya ibada, watakhini amana, watahalalisha uongo, watakula riba, watakuwa waovu, na waasharati na hawatawapenda jamaa zao, wataona fahari kufanya dhuluma, watapamba qur’an tukufa, misikiti yenye minara mirefu itajengwa, wataheshimiwa waovu na wadhalimu, misikiti itajaa watu wa kuswali lakini watu hao hawatakuwa na umoja, watawashirikisha wake zao katika biashara ili kupata utajiri, wataamini maneno ya waasi na kuwatii, waovu na wapotovu watakuwa viongozi wa majamii, wataweka vifaa vya ghina (muziki) (gita na piano), wanawake watapanda farasi (baiskeli) na kuwaiga wanaume (kwa mavazi ya kiume), watu watajishughulisha na kutekeleza mambo ya dunia kabla ya kuswali faradhi na kuonekana waungwana lakini mioyo yao itakuwa imejaa ufasiki”.



 Alipofika hapo asbag bin nabata akauliza, dajjal ni nani? imam ali (a.s.) akajibu: "jina la dajjal ni sayad bin sed. waovu tu ndio watamfuata na waungwana watamkimbia. dajjal atatokea yahudiyya mjini isfahan-iran. atakuwa na jicho moja na hilo jicho litakuwa kwenye paji la uso na litang’aa sana. mboni ya jicho lake.
Litakuwa wekundu na karibu na jicho lake litakuwa limechorwa neno  kafiri ili lisomeke na wote. mbele yake kutaonekana mlima wa moshi na kisogoni kwake kutaonekana kilima cheupe. yeye atatokeza wakati wa njaa kali, watu watababaika na vilima hivyo kufikiria hiyyo ni vyakula na kumkimbilia huyo dajjal. atapanda punda rangi ya majivu ambaye hatua yake moja itakuwa sawa na masafa ya maili moja.
akipita karibu na mto wowote maji yake yatakauka. kwa sauti kubwa itayosikika na watu na majini wote yeye atanadi, "eh nyinyi rafiki zangu, njooni kwangu mbio. mimi ni muumba wa vyote ulimwenguni. nimeumba vitu katika maumbile mbalimbali na mimi ndiye mtoa riziki mimi ninawaita kwenye maongozi yangu kwa sababu mimi ni mungu na nina uwezo juu ya vitu vyote."


hadhrat ali (a.s.) tena aliendelea kuwatahadharisha watu kwamba yule adui wa mungu ni mdanganyifu wa nafsi yake kwa sababu yeye anakula na kunywa. zaidi ya hayo mungu wenu siye chongo, wala hali wala kunywa, hana mwili na haondoki kutoka pahala pamoja na kwenda pengine. mjitahadhari! wafuasi wa huyo mwovu watakuwa watoto wa haramu na mayahudi. hadhrat mehdi (a.s.) atamwua dajjal huko sham kwenye mlima mkubwa unaoitwa tallu affik siku ya ijumaa saa tatu baada ya jua kuchwa.


baadaye kutatokeza tukio kuu. akasoma aya kutoka qur’an tukufu isemayo: "na sisi tuliwasimulia kwamba kuna mtu hutembea kwa wepesi na kuzungumza nao". (27.28). mtu huyo (imam a.s.) atatokeza kutoka mlima wa saffa uliopo makkah. atakuwa amevaa pete ya nabii suleiman na kushika asa ya nabii mussa.
 atagusa paji la uso la waumini kwa pete hiyo na papo hapo kutachoreka maneno "hadha mu'min" (huyu ni mtu aliyeamini).
atagusa paji la uso la makafiri na papo hapo patachoreka maneno "hadha kafir (huyu kafiri). juwa litachomoza kutoka magharibi na yeye atanyanyua kichwa mbele ya juwa na watu_wote duniani wataweza kumwona. wakati huo mlango wa toba utafungwa na vitendo havipatiwi jazaa ila vya wale walio amini kabla ya tukio hilo kwa sababu imani bila amali haikamiliki.”


Katika kitabu kimoja cha kisunni, kamaluddin, abdulla bin umar amesimulia kwamba siku moja baada ya swala ya asubuhi mtume mtukufu (sa.w.w.) pamoja na masahaba zake walikwen­da kutembea mjini. mtume (s.a.w.w.) akasimama karibu na nyumba moja na kugonga mlango wa nyumba hiyo. alitoka mwanamke mmoja aliyemtambua mtume (s.a.w.w.) na kumwuliza kwamba angeweza vipi kumsaidia mtume (s.a.w.w.). mtume akamjibu kwamba alitaka kuonana na mwanae, abdulla. mama huyo alijibu kwamba mwanae alikuwa mgonjwa wa akili na kwa hivyo huchafua nguo zake na kuzungumza maneno ya kiburi mara kwa mara. mtume (s.a.w.w.) akaomba ruhusa ya kuingia ndani kumwona huyo mgonjwa. mama huyo akamruhusu mtume (s.a.w.w.) lakini aliomba asamehewe ikiwa mwanawe huyo atazungumza vibaya na mtume. (s.a.w.w.).


Mtume (s.a.w.w.) akaingia ndani pamoja na masahaba. yule maluuni alikuwa amevaa nguo nene na kuzungumza peke yake. mama yake akamwambia anyamaze kwa sababu mtume mtukufu (s.a.w.w.) alikuja kuonana naye. kusikia hivyo akanyamaza. mtukufu mtume (s.a.w.w.) akasema: "ingelikuwa huyo mama asingemwambia kunyamaza, mngelisikia anayosema na mngeelewa hali nilivyoeleza". tena mtume (saw.w.) akamwuliza kwamba anaona nini. alijibu, "mimi ninashuhudia haki na ubatili na nina ona arsh ya mungu inaelea juu ya maji". bwana mtume (s.a.w.w.) akamsihi atoe shahada juu ya upweke wa mungu na unabii wake. naye akajibu, "ninatoa shahada juu ya upekee wa allah na mimi mwenyewe ni mtume wa mungu kwa sababu wewe hustahili utume zaidi yangu." mtume (s.a.w.w.) akaondoka.


Siku ya pili mtume mtukufu (s.a.w.w.), pamoja na masahaba wake walikwenda kumwona tena nyumbani kwake. kwa idhini ya mama akaingia ndani na wakamwona amekaa juu ya mtende anapayukapayuka tena mama yake akamgombeza na kumwambia akae kimya na kuteremka chini. siku hiyo tena mtume akachukiwa na akasema "ingekuwa mama yake asingemwambia kunyamaza, nyinyi mngeamini kwamba huyo ni dajjal mfasiki, ambaye nimekwisha watahadharisheni naye” mtume (s.a.w.w) akaondoka.
mtume (s.a.w.w.) tena pamoja na masahaba wake akaenda kumwona siku ya tatu na alipoingia ndani akamwona huyo abdulla akicheza na mbuzi waliokuwa karibu naye.
  Mtume (s.a.w.w.) akamsihi akubali upekee wa mungu na unabii wake na akamwambia aseme mtume (s.a.w.w.) alikuwa na wazo gani. huyo akasema “addhukh adhukh" (dukh maana yake mvuke na siku hiyo hiyo suratul dukhan iliteremshwa na mtume (s.a.w.w.) alisoma sura hiyo aliposwalisha swala ya alfajiri. mtume (s.a.w.w.) akamjulisha ‘atakayo mungu ‘ ndivyo huwa na wewe hutafikia mradi wako."


Mtume mtukufu (sa.w.w.) baadaye akawaeleza masahaba "wake kwamba huyo abdulla ndiye dajjal mfasiki ambaye habari zake alikwishawaeleza. atatokeza duniani siku za mwisho na kabla ya hapo mungu atakuwa amemweka mahabusu katika kisiwa kimoja. atawaletea watu utatanishi mkubwa siku za mwishoni. manabii wote kabla ya mtume mtukufu (s.a.w.w.) waliwatahadharisha wafuasi wao kuhusu dajjal. kadhalika, mtume wetu (s.a.w.w.) ametutanabahisha sisi kuhusu huyo dajjal na akaongeza "msidanganyike na huyo: mungu wetu siyo chongo, wala hana mwili na huyo mwovu (dajjal) atajitokeza siku za mwisho amepanda punda”.


Dajjal atajitokeza siku za mwisho na ataishi kwa muda wa siku arubaini na atatembelea kila sehemu ya dunia juu ya punda wake. mwisho atauliwa huko syria kwa mikono ya Nabii Issa(a.s.).

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget