Saturday, February 25, 2012

WAZANZIBARI MAARUFU


TIPPU TIP

Akiwa ametiwa ila sana na "magazeti ya wavumbuzi," shujaa huyu jasiri wa kizanzibari ambaye jina lake hasa aliitwa Hamed bin Mohammed Marjebi alijulikana zaidi kama Davy Corocket au Francis Drake wa Afrika ya Mashariki kuliko  mfano wa mwanafunzi mtundu ambaye tabia zake zilizompa umaarufu zaidi ni vile kuwa na ugomvi wa mara kwa mara na wavumbuzi wa kidini kutoka Ulaya wa wakati ule. Aliwatumikia Sultani wake kwa zaidi ya miaka 50, huku akibeba bendera na ustaarabu wao katika kila pembe ya mipaka yao.

Katika nyakati tafauti, alifanya kazi kama mvumbuzi, kiongozi, mfanyabiashara, askari mwanadiplomaisa, hakimu na gavana.  Aliwatumikia jumla ya Sultani 8 wakati wa maisha yake baadaye akastaafu na kubakia nyumbani kwake katika Mji Mkongwe.  Alifariki mwaka 1905 akiwa hakuwahi kuhalifu kazi zote alizopewa na watawala wake.





SITI BINTI SADI.

Akiwa Nyota wa kwanza mkubwa wa kurikodi Taarab tokea miaka ya mwanzo ya santuri, Siti aliweza kuifanya Taarab kuwa maarufu kutokana na muziki wake mtamu na nyimbo za mapenzi zilizobeba ujumbe wa nguvu za kijamii na uchambuzi wakisiasa.  Jambo moja lililoifanya kazi yake kuwa ya kiharakati ni vile kuimba kwake kwa kutumia lugha ya watu wa kawaida.  Baada ya kuishi kwa muda mrefu katika mitaa ya Ng'ambo mjini Zanzibar, baadaye Siti alitembelea nchi mbali mbali za Afrika ya Mashariki akiimba na kuuza rekodi zake.  Lililompa umaarufu zaidi miongoni mwa watu ilikuwa ni muziki mpya uliorekodiwa katika lugha yao wenyewe.  Baada ya  wasomo wanadai kuwa rekodi hizi za zamani zilichangia sana kuieneza lugha ya Kiswahili.

Akiwa mtoto wa watumwa, Siti alianza  maisha kwa akali ya kitu, lakini kwa juhudi yake mwenyewe na sauti  yake ya ajabu, aliweza kwanza kuimba taarabu  ya kawaida, baadaye katika makasri  na kumsifu Mfalme, na hata  kuimba kwa Kiarabu.  Baadaye aliigeuza midundo na mifumo ile ya kishairi na kuwa katika vinanda vya kawaida.  Matokeo yake, Taarab ya Kiswahili ilimfanya awe Nyota na yeye kuifanya taarab iwe aina ya sanaa ambayo bado ni maarufu visiwani na isiyokosekana katika harusi na sherehe zote za Kizanzibari ..



BARGHASH  BIN SAID

Huyu ni Mfalme wa Tatu wa Zanzibar, aliyetawala kuanzia mwaka 1870 mpaka 1888.  Mama yake alikuwa mtumwa (aliyewachwa huru kwa kuzaliwa yeye), Sultani wengi wa Zanzibar walikuwa watoto wa wanawake watumwa.  Baba yake, Seyyid Said bin Sultan, alikuwa mfalme mlowezi wa Sultan wa mwanzo wa Zanzibar.  Barghash anasifika kwa ujenzi wa miundo mbinu ya Mji Mkongwe, ikiwemo maji ya bomba, vituo vya polisi, barabara, bustani, hospitali na majumba mengi ya kiutawala kama vile Beit el Ajaib.  
Pengine alikuwa  Sultan wa mwisho kuweka kipimo cha uhuru wa kweli dhidi ya udhibiti wa Wazungu. Alishauriana na "Washauri" kadhaa wa kizungu ambao walikuwa  na ushawishi mkubwa, lakini alibaki kuwa mtu imara waliyepambana naye kumdhibiti alipambana na wanadiplomasia kutoka  Uingereza, America, Ujerumani, Ufaransa na Ureno na mara kwa mara aliweza kuiangusha kitaalau nchi moja baada ya nyengine katika kinyang'anyiro cha kabla ya Ukoloni.  Ni mtoto wake, Khalid, ambaye katika    mchuano wa kurithi ufalme, alishindwa katika Vita vifupi kabisa katika histora.



SHEIKH ABDALLA SALEH FARSY

Alikuwa ni mfano wa karne ya Ishirini, katika safu ndefu ya Ulamaa wa Kiislam kutoka Zanzibar.  Mchango wake maarufu katika uislamu ni kuchapisha QUR'AN TAKATIFU, yenye kurasa 807, ambayo ni tafsiri ya mwanzo kamili inayokubalika katika lugha ya Kiswahili  Sheikh Abdulla Saleh Farsy vile vile alikuwa kabobea katika sarufi ya Kiarabu.  Akiwa katika umri wa miaka ya ishirini, alikuwa anaandika mashairi kwa kiarabu, jambo linaashiria ukubwa wa kiwango cha elimu ambacho ulamaa  wa Zanzibar walikuwa wanasambaza nyakati zile.

Sheikh Abdulla aliteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa shule za msingi za Unguja na Pemba mnamo mwaka 1949, Mkuu wa Shule ya Lugha ya Kiarabu mwaka 1957 na Kadhi Mkuu wa Zanzibar mwak 1960.  Aliondoka visiwani baada ya Mapinduzi ya 1964 na akafia Omani Novemba 9 mwaka 1982.







TARIA TOPAN

Mfanya biashara, "mwana mfalme" wa kihafidhina, ambaye alijipatia utajiri wa mailioni kutokana na biashara ya karafuu na mamilioni  mengine zaidi wakati alipokuwa anafanyakazi kama mkusanyaji Ushuru wa Forodha katika bandari ya Unguja na Pemba.  Katika dhamana ile, alitakiwa kumlipa Sultani kiwango kikubwa kisichobadilika cha ada kila mwisho wa mwaka, kutokana na fursa aliyopata kwa kuteuliwa mkusanyaji mapato.  Alipiga mahesabu na kuona kuwa angeliweza kukusanya pesa nyingi zaidi kuliko zile ambazo angelilipa, kama ikiwa biashara ingekwenda vyema.  Na kwa wakati ule, biashara Zanzibar ilikuwa nzuri.  Bei ya karafuu na viungo vyengine ilikuwa juu, mahitaji  yalikuwa makubwa na bidhaa za viwandani ambayo vitu hivi zilifanyiwa biashara zilionyesha kushuka kupungua kila mwaka, kwa vile vitendea kazi na mbinu za kutendea kazi vilikuwa rahisi katika nchi za Magharibi.
Kwa utajiri wake huu, Topan aligeuka kuwa mfadhili Mkuu wa mji.  Aliweka Wakfu na kujenga Kituo cha Afya kilichonakishiwa ambacho kipo Kaskazini kabisa mwa Bandari ya Mji Mkongwe.  Vile vile  alitoa  "Wakf" vikataa vya ardhi vilivyokusudiwa kuwanufaisha wazee wasiojiweza.


 NAHODHA "SMITH WA ZANZIBAR"
Yeye hakuwa Mzanzibari, lakini alikuwa rafiki wa mwanzo wa Kimarekani kuja Zanzibar.  Alifanya biashara kwa mapana katika mwambao wa Afrika Mashariki kwenye miaka ya 1800.  Akiwa  mfanyabaishara kutoka Salem, Massachussets, aligundua kitu kilichomuunganisha na wafanyabiashara wa Zanzibar ambao Utajiri wao ulitokana na mfanya biashara mwerevu na wa kuaminika.  Pamoja na manahodha wafanya biashara hawa, alifanyanao mapatano ya bei na kuweza kuwa marafiki haraka sana.
Wamarekani wao waliuza nguo za pamba (Mrekani) na kununua vipusa, viungo na sandarusi ambayo ilitumika kutengeneza vanishi kwenye viwanda vya New England.  Kwa kufanya biashara na Marekani, kuliifanya Zanzibar kuwa kituo Kikuu cha Biashara katika maeneo haya..  Hata kufikia mwaka 1830, katika kipindi cha miezi 18, jumla ya vyombo 32 kutoka Amerika vilishatia nanga katika bandari ya Zanzibar.Mnamo mwaka 1836 kiwango cha biashara baina ya nchi mbili hizi ilihakikisha kuanzishwa Balozi za Amerika za kudumu katika Mji Mkongwe.  William Smith alisafiri "kuzunguka pembe" ya Afrika mara nyingi katika safari ndefu za kutoka Amerika na visiwani kiasi cha kujulikana kama Smith wa Zanzibar katika pande zote za ikweta

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget