Saturday, June 2, 2012

“JE, UISLAMU NI DINI YA UMASONIA (FREEMASONS AU FREEMASONRY)!?”




Makala hii imeandikwa nami Ndg. Lung’wecha,K. M.

    Ijumaa Mei 25, 2012.

Makala hii ni sehemu ndogo tu toka katika Sura ya 4 ya utafiti wa kitabu changu ninachokiandika
                       ambacho mpaka sasa kina kurasa 215, kiitwacho:
“JE, UISLAMU NI DINI YA UMASONIA (FREEMASONS AU FREEMASONRY)!?”

KWA MAONI:
E-mail: wecha2005@yahoo.com
Facebook: www.facebook.com/Lung’wecha
Mob. 0784 566 055
‘KARIBU!’
**************************************
FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI!

JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?
“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele
ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu
wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa
athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni
kama mmea uliochipua, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya
ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri.
Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na
ujira mkubwa.”
                                  (Qur’an 48:29)
“Basi ole wao wanao andika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka
kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyo
andika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayo yachuma”
                                   (Qur’an 2:79).
==================
Katika kitu ambacho nimeking’amua, viongozi wengi wa dini mbalimbali duniani nje ya Uislamu
ikiwemo ya kikristo, na waandishi wa vitabu akiwemo Mmasonia Robert Spencer [1] ambaye
nitabainisha tuhuma zake dhidi ya Uislamu hapo baadae, wamekuwa wakidhani au wakizusha
kuwa Uilamu ulianzishwa na Mtume karne ya 7 kitu ambacho sio kweli kwani uislamumu ulianza
tangu kwa Nabii Adam mamilioni ya miaka yasiyo na hesabu kamili inayofahamika na
mwanadamu kwa mujibu wa aya mbalimbali za Kuran Tukufu.
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


2
Pia, Mmasonia Bill Gates ambaye kwa makusudi kabisa aligharamia Dola za kimarekani 750
milioni kwa Chanjo zenye madhara kwa binadamu za ugonjwa wa malaria zilizotengenezwa
Marekani kwa ajili ya nchi masikini Tanzania ikiwemo [2]. Bill Getes pia ni mmiliki wa kampuni
kubwa ya kompyuta duniani ya Microsoft Corporation ya Marekani ambayo ndiyo
iliyotengeneza Encarta Encyclopaedia Standard ya 2004 ambayo inasema, eti Mtume
Muhammad (S.A.W) ndiye aliyeanzisha Uislamu duniani! [3] yaani akimaanisha eti Uislamu ni
dini ya juzi! uzushi kinyume kabisa na Qur’an.

JIM HARRIES
Mchungaji Jim Harries kwa jina lingine Jacob Otieno, wa Kenya 2007 alitunga kozi maalum ya
kufundishia wachungaji kwa kuwapotosha juu ya Uislamu na ili nao waje kuipotosha jamii hasa
ya kikristo juu ya maarifa ya Uislamu, somo ambalo wao huliita “Islamology” somo ambalo kila
mkristo anayesomea ukasisi wowote ule ni lazima alisome popote duniani ikiwa kama silaha
dhidi ya kuupindihsa Uislamu kwa kushika akili za waumini wao.
Bw. Jim Harries, aliitunga kozi hiyo aliyoiita “HALI YA UISLAMU, Maelezo ya kumsaidia Mkristo
aufahamu Uislamu” [4] ili itumike kufundishia makasisi wanaokwenda kusomea ukasisi katika
Chuo cha Teolojia cha Yala (Yala Theological Centre) huko Yala Kenya na Chuo cha Teolojia cha
Siaya (SiayaTheological Centre) huko Siaya Kenya mbapo mwandishi huyo anapotosha kwa
kusema eti kwamba, na hapa namnukuu:
“… Uislamu si dini kongwe, ni dini ya juzi iliyoanzishwa na Mwaarabu aitwae
Muhammad, baada mkewe wa kwanza, Bi. Khadija kufariki alioa tena wake kumi na
wawili. Muhammad aliuanzisha uislamu kwa maono yake tu ambayo alisingizia
kuletewa na malaika Jibril (Gabriel) yaani maandiko ya Kur’an…” [5]
“… mwanzoni Muhammad alitaka dini ya Uislamu iwe (sehemu ya) dhehebu la (dini
 ya) Wayahudi(Judaism), lakini sababu Wayahudi hawakumkubalia alibadilika na
 kuifanya dini ya kipeke yake inayojitegemea. Wakati ule aliacha kusema waombe
 wakielekea Yerusalemu, na aliamrisha maombi yawe wa watu wakielekea Maka,
 alipokuwa Madina aliweka misingi mingi ya dini - kwa mfano kuweka ijumaa siku ya
 kuomba, na Ramadhani mwezi wa kufunga. Alianzisha vita vilivyoendelea mpaka
 Waarabu wote wakawa chini ya Uislamu. Vitabu vitakatifu kwa waislamu vilikuwa
 104, lakini vilibaki vine tu yaani Taurati, Zaburi, Injili n Kuran sababu Wayahudi na
 Wakristo waliharibu vitabu vyao vingine [6]. Karibu mambo yote yanayofanywa
 katika Hija Maka ndio hayo hayo yaliyofanywa na Waarabu wapagani kabla ya
 kuanzishwa kwa Uislamu [7]. Jihadi ni kueneza dini ya kiislamu kwa nguvu (yaani kwa
 vita). Katika mafudisho ya kiislamu Hadith ni mafunzo yanayosisitiza umuhimu wa
 vita ili dini ya kiislamu iendelezwe, vita hivyo vinaitwa Jihad, na vinafanya watu
 wengi wauwawe Nigeria na Sudan siku hizi. Pia iko Jihad ya kulipa pesa kwa wale
 wanaogeuka (wanaosilimu) ili wawe Waislamu toka dini nyingine…” [8]
“… Muhammad alikuwa mtu mweupe (Mwaarabu) na watu weusi wote wanaotajwa
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


3
walikuwa watumwa, na alikuwa na mtumwa mweusi. Alikuwa mwepesi wa hasira na
mwenye dhambi sababu alienda kuomba msamaha kwa Mungu mara nyingi, dhambi
hizo ni pamoja na kuikata mikono na miguu ya watu, kuwatoa macho kwa chuma, na
kuwaua kwa kiu ya maji. Alikuwa na wake wengi, na wanawake wengine tena wengi
ambao hawakuwa wake halisi (yaani vimada), kuongea vibaya juu ya Muhammad
kunawaudhi Waislamu sana, sababu wanajaribu sana kuyaiga maisha yake …” [9]
“… sehemu ingine ya Qur’an haikuweza kuandikwa chini (yaani haikuandikwa ndani ya
 kitabu cha Kuran) kwa sababu walioifahamu peke yao walikufa kabla ya kuandika.
 Qur’an na Hadith inakubali sehemu fulani yake kuwa imepitwa na maneno ya baadaye
 (yaani imepitwa na wakati) inaondolewa (inafutwa). Wasuni wamegawiwa chini ya
 sheria aina nne: Hanafi, Maliki, Shafi na Hanbali. (Sheria ya Washia inafanana sana na
 hizi). Sheria za kiislamu zinadumaza wanawake (zinavunja haki za wanawake na
 kurudisha nyuma maendeleo yao). Sheria (hizo) ziliundwa kati ya mwaka 700 na 860
 AD, na sasa haziwezi kubadilishwa tena, kwa hivyo zimepitwa sana na wakati.
 Waislamu ambao wanaotaka sheria zisiwe kali hivyo, wanayahatarisha maisha yao.”
 [10]
“…Waislamu waliposema Yesu sio mungu,walipotea mbali na ukweli kabisa. Maandiko
 matakatifu ya Wakristo (Biblia) hayalingani na imani ya Waislamu. Waislamu husema
 wanaamini Taurati, Zaburi na Injili, lakini ukweli hawaviamini vitabu hivi. Wanaamini
 Wakristo na Wayahudi wameyachafua maandiko hayo (Taurati, Zaburi na Injili).
 Yaliyokuwepo (katika Biblia) yamechafuliwa na yale ya asili (halisi) yamepotea
 kulingana na Waislamu. Huo uwongo ni moja wa misingi ya dini yao. Uislamu ni dini
 ya chuki. Inafundisha kukuwa kwa uadui, na kulipa kisasi kwa anayekukosea,
 Waislamu wanaweza kukataa hivyo, sababu wanaruhusiwa kutaja uongo! Uislamu
 kama dini ni mtego. Kuingia ni rahisi lakini kutoka ni kifo. Ndio sababu Muislamu
 anamwogopa sana Mwislamu mwenzake. Waislamu hawana uhuru kuongea ubaya
 wowote juu ya dini yao. Badala yake wanalazimishwa kupiga kelele pamoja
 upingamizi wa dini yao unapotokea. Uislamu pia unajaribu kuzuia maendeleo mengi,
 sababu washirika (waumini) wanalazimishwa kuzifuata sheria ambazo haziambatani
 na maendeleo…” [11]
“…Waislamu kwa Afrika Mashariki wanapenda kutengeneza mihadhara, uhubiri wao
 hawahubiri Uislamu, ila wanaupinga Ukristo. Wengine wao wamefanya utafiti katika
 Biblia na wanajaribu kudhihirisha udhaifu wote wa imani ya Ukristo, ili waweze
 kuwavuta watu kuingia katika Uislamu. Inamhitaji Mkristo kuwa na msimamo dhabiti
 na ujuzi wa kutosha ili aweze kugundua uongo na udanganyifu wa Waislamu hawa.
 Hii inahitaji masomo zaidi, na ujuzi mzuri wa kibiblia…” [12]
Mwisho wa kunukuu.

FREEMASON ROBERT SPENCER
Miongoni mwa waandishi wakubwa ni pamoja na mmasonia (freemason) aitwae Robert Spencer
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


4
ambaye ni Mkurugenzi aliyeajiriwa katika programu ya kimasonia ambayo imeundwa maalum
na serikali ya kimasonia ya marekani ili kuupotosha uislamu, programu hiyo inaitwa “Jihad
Watch” inayoendeshwa na taasisi ya kimasonia iitwayo David Horowitz Freedom Center, taasisi
ambayo imeundwa maalum kwa kazi ya kuupotosha uislamu aghalabu kwa uandishi wa vitabu
chini ya serikali ya kimasonia ya Marekani iliyokua chini ya freemason Bill Clinton, George
Walker Bush na sasa Barack Obama. [13]
     ↑Mmasonia Bw. Robert Spencer
{Chanzo: www.amazon.com/Robert-Spenser}
Robert Spencer ambaye pia ni mwandishi wa kitabu kiitwacho “The Politically Incorrect Guide to
Islam (and the Crusades)” [14] yaani “Muongozo Potofu wa Kisiasa Katika Uislamu na Jihadi”
kama picha ya kitabu hicho inavyo onekana hapa chini, kitabu hicho kina kurasa 270, alikiandika
akishirikiana na freemason wa kike aitwaye Bi. Pamela Geller.
Spencer amekuwa akiendesha semina mbalimbali dhidi ya Uislamu na Jihadi kwa maafisa wa
jeshi la Marekani na katika Chuo cha Kijeshi (United States Central Command and General Staff
College, the U.S. Army's Asymmetric Warfare Group) na kwa maafisa wa kijasusi (FBI), Kikosi
Kazi cha kupambana na ugaidi na Jumuia za Kiintelijensia za huko Marekani. [15]
↑Kitabu cha Freemason Robert Spencer kinavyoonekana kwa nje, cha
   “The Politically Incorrect Guide to Islam (and the Crusades)”
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


5
{Chanzo: www.amazon.com}
Kazi kubwa anayoifanya Spenser ni kucheza au kuharibu saikolojia au akili (mind control) za
wamarekani na wakiwa kama raia na watumishi wa sarikali ya ki-freemason ya Marekani ili
hatimaye wauone kuwa Uislamu kuwa adui badala ya Freemasons duniani.
Spencer katika kufanikisha hilo, ameandika vitabu kumi na moja, makala zaidi ya mia tatu
akihusianisha dhana ya Jihad (neno la kiarabu likimaanisha kujitahidi au kufanya bidii) akisema
huo ndio “Ugaidi wa kiislam”. Spencer miongoni mwa vitabu vyake vingine ni pamoja na: “Islam
Unveiled: Disturbing Questions About the World's Fastest Growing Faith (Encounter)” yaani
‘Uislamu Uliovuliwa Hijabu: Maswali Sumbufu juu ya Kukabialiana na Dini/ Itikadi Inayokuwa
kwa Kasi Mno Duniani’ [16], kitabu ambacho kinaeleza wazi na kuthibitisha kwamba uislamu
ndiyo dini pekee inayaoongoza kwa kukua kwa kasi zaidi duniani hasa Ulaya na Marekani kuliko
dini yoyote na kwamba hilo ni tatizo na kwamba lazima hatua zichukuliwe kukabiliana na ukuaji
huo anasema [17].
 Spencer pia ameandika kitabu kinachoitwa “Onward Muslim Soldiers: How Jihad Still Threatens
America and the West”, yaani “Maaskari wa kiislamu wa Kesho: Kwa Namna Gani Jihad Bado
Inatishia Amani Amerika na Ulaya Magharibi” na pia ameandika kitabu “Religion of Peace? Why
Christianity Is and Islam Isn't” yaani “Kwa nini Ukristo ni Dini ya Amani Wakati Uislamu Sivyo?”
ambamo Spencer anaeleza kupinga kwake kukua kwa dini ya kiislamu huko Magharibi akitaka
kudhibitiwe zaidi na kudumisha maadili ya kiyahudi na kikristo tu. Anasema Spencer kwa hali
yoyote Uislamu ulivyo ni lazima udhibitiwe usikue huko Amerika na Ulaya Magharibi.
Pia aliadika kitabu chake kiitwacho “The Complete Infidel's Guide to the Koran” [18] yaani
“Muongozo Kamili wa Kikafiri katika Qur’an” kitabu chenye kurasa 260 akishirikiana na Daniel Ali
ambaye kabla ya hapo Daniel aliandika kitabu kiitwacho “Inside Islam: A Guide for Catholics
(Ascension)” [19] yaani “Ndani ya Uislamu: Muongozo kwa Wakatoliki (Kupazwa kwa Yesu
Mbinguni)”.
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


6
↑ Kitabu cha Freemason Robert Spencer kinavyoonekana kwa nje cha
          “The Complete Infidel's Guide to the Koran””
                 {Chanzo: www.amazon.com}
          {Chanzo: www.amazon.com/Robert-Spenser}
Vitabu vya Spencer vimekuwa vikifasiriwa katika lugha kadhaa duniani yaani: kihispania,
kitaliano, kifinland, kikorea na kibahasa cha Indonesia. Spencer pia na mwandishi katika Mradi
wa Uchunguzi wa Ugaidi wa Taasisi ya Steven Emerson (Steven Emerson's Investigative Project
on Terrorism). Makala zake dhidi ya Uislamu huchapishwa katika magazeti ya Marekani
yaitwayo: New York Post, the Washington Times, the Dallas Morning News, the UK's Guardian,
Canada's National Post, Middle East Quarterly, World Net Daily, First Things, Insight in the News,
National Review Online, na katika majarida mbalimbali. Spencer pia aliendesha mijadala juu ya
Jihad, Uislam, na Ugaidi katika warsha zilizodhaminiwa na idara maalum ya serikali ya kimasonia
ya Marekani (U.S. State Department) na wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani [20].
Pia Spencer alifanya vipindi mbalimbali katika runinga mbalimbali zikiwemo: BBC, ABC News,
CNN, Fox News's O'Reilly Factor, the Sean Hannity Show, the Glenn Beck Show, Fox and Friends,
PBS, MSNBC, CNBC, C-Span, France24 na Croatia National Television (HTV). Pia katika radio
mbalimbali kama: Bill O'Reilly's Radio Factor, The Laura Ingraham Show, Bill Bennett's Morning
in America, Michael Savage's Savage Nation, The Sean Hannity Show, The Alan Colmes Show,
The G. Gordon Liddy Show, The Neal Boortz Show, The Michael Medved Show, The Michael
Reagan Show, The Rusty Humphries Show, The Larry Elder Show, The Barbara Simpson Show,
Vatican Radio, na nyingine nyingi. [21]
Pia, amekaribishwa kama mzungumzaji katika vyuo na vyuo vikuu kama vile: Dartmouth College,
Stanford University, New York University, Brown University, the University of North Carolina
huko Chapel Hill, University of Virginia, College of William and Mary, Washington University ya
St. Louis, University of Wisconsin huko Madison, University of Wisconsin huko Milwaukee, na
kadhalika [22].
Spencer miongoni mwa vitabu vyake chini ya udhamini wa serikali ya Marekani ili kuupotosha
Uislamu ni pamoja na kitabu kiitwacho : The Truth about Muhammad, the Founder of the
World’s Most Intolerant Religion” [23], yaani “Ukweli Kuhusu Muhammad, Mwanzilishi wa Dini
Isiyovumilika Kabisa Duniani”, ndani ya kitabu hiki, Freemason Robert Spencer, Wamagharibi
humwita bingwa wao wa taaluma ya Uislam, ameupotosha Uislamu eti kwamba katika Uislamu:
Muhammad (S.A.W [24]) ndiye alianzisha dini ya kiislamu, (Upotoshaji huu pia umefanywa
katika Encarta Encyclopaedia Standard ya 2004 [25] ), kitabu hiki pia kiliongoza kwa mauzo huko
Marekani [26].
Anasema Spenser, eti kwamba, mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) yalitawaliwa na
vitisho, yanatokana na shetani, yanawalaani Mayahudi na Wakristo, eti yeye ni mroho wa
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


7
madaraka ya kisiasa na kijeshi, eti mafundisho hayo yalitawaliwa na matumizi ya mabavu yaani
alikuwa dikteta, eti yalitawaliwa na udanganyifu au utapeli kuwa atakae kufa vitani atakwenda
peponi, eti Qur’an inahalalisha vita dhidi ya kila asiye amini Uislamu na ili hatimaye isimamishe
sheria za kiislamu.[27]
Anasema Spencer kwamba kupitia mafundisho yake Mtume Muhammad (S.A.W) amehalisha
umalaya! na ukware! kwa kuoa wake wengi, eti kwamba yeye ni mkatili wa kijinsia na mbakaji
kwa kumuoa mtoto wa miaka 9 (akimaanisha Bi. Aisha!), eti kwamba Mtume Muhammad
(s.a.w) aliwalazimisha wasiowaislamu kuingia ktk Uislamu kwa nguvu chini ya utawala wa
kiislamu eti wa kidikteta, eti kwamba Uislam wa Mtume Muhammad (S.A.W) hauna demokrasia,
na Robert Spenser mwishoni anatoa wito kwa Waislamu kukifanyia marekebisho kitabu kitukufu
cha kiislamu ili kuondoa hayo aliyoyaita yeye kuwa ni mapungufu. [28] Samahani! naomba radhi
ndugu mpendwa msomaji kwa maneno haya makali niliyoyanukuu kama yalivyo.
       ↑ Kitabu cha Freemason Robert Spencer kinavyoonekana kwa nje cha
“The Truth about Muhammad, the Founder of the World’s Most Intolerant Religion”
                       {Chanzo: www.amazon.com}
Mbali na Robert Spencer, waandishi wengine wanaoupotosha Uislamu huko Magharibi ni
pamoja na Profesa Ergun Mehmet Caner, huyu ni Prof. katika fani ya taaluma ya teolojia na
Historia ya Kanisa (Theology and Church History) katika Chuo Kikuu cha Liberty (University) huko
Lynchburg, Virginia Marekani. Na ndugu yake Prof. Emir Fethi Caner ambaye ni Profesa katika
taaluma au fani hiyo hiyo ambaye ni mkuu wa chuo cha Truett-McConnell College huko
Cleveland, Georgia Marekani.[29]
Maprofesa hao wameandika kitabu kiitwacho: “An Insider’s Look of Muslim life and Beliefs,
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


8
Unveilling Islam”[30] , jina linalomaanisha: “Mtazamo wa ndani wa Maisha na Imani au Itikadi ya
Kiislamu, Kuuvua Hijab Uislamu”, kitabu hicho kina kurasa 288 ambamo wanasema katika kitabu
hicho kwamba wanaelezea mambo ambayo hayafahamiki juu ya imani, mila, vitendo na
utamaduni, na maadili ya Uislamu kwa ujumla yanayosikitisha ambayo hayafahamiki kwa
wakristo wakisema kwamba wao waliwahi kuwa waislamu walipokuwa wadogo, mambo gani
hayo? hawakuyabainisha katika utanguilizi wa kitabu hiki kupitia mtandao! Wanasema hayo ni
pamoja na tofauti kati ya Uislamu na Ukristo, wanasema lengo la kitabu chao hicho ni kumpa
Mkristo mpango mkakati (Strategic Plan) ambao anaweza kuutumia kujengea hoja katika
mdahalo dhidi ya waislamu na kuwawezesha wasiingie katika Uislamu kwa kile kinachoonekana
ni kukosa hoja.
Wanashindwa kujua kumbe swala hapa ni ukweli wa uhalisia wa mambo.
↑ Kitabu cha waandishi Prof. Ergun Mehmet Caner na Prof. Emir Fethi
                Caner kinavyoonekana kwa nje cha
  “An Insider’s Look of Muslim life and Beliefs, Unveilling Islam”
                 {Chanzo: www.amazon.com}
Mwandishi Prof. Ergun Mehmet Caner wa hapo juu pia ameandika kitabu kingine peke yake
alichokiita “Voices Behind the Veil” [31] yaani “Sauti za Wasio na Sauti Walionyuma ya Shungi
(Hijab)” chenye kurasa 218. Anaeleza katika kitabu hicho akiushutumu Uislamu eti kwamba
wanawake hawana sauti katika Uislamu na kwamba Uislamu unawakandamiza wanawake na
hivyo wanaishi katika maisha yao yote bila ya matumaini kwa manyanyaso, makandamizo na
kutendewa matendo yasiyo ya ubinadamu katika ulimwengu wa kiislam duniani kwa watoto,
wake, wakinamama, wakinadada, na kila muumini wa kiislamu wa kike duniani wakiwa zaidi ya
nusu bilioni dunia nzima, anasema haya yote yanafanyika nyuma ya shungi (Uislamu) [32].
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


9
↑Kitabu cha Prof. Ergun Mehmet Caner kinavyoonekana kwa nje
                          cha
                   “Voices Behind the Veil”
                {Chanzo: www.amazon.com}
Dr. Sproul, R. C. muasisi na rais wa taasisi ya kikristo inayoshughulika na elimu ya kikristo
iitwayo Ligonier Ministries iliyoko Orlando, Florida Marekani. Ambaye pia ni mhariri mkuu wa
Jarida la kikristo la “Tabletalk” na “Reformation Study Bible” na mwandishi wa vitabu na makala
zaidi ya 70 vya kikristo kupitia machapisho ya Injili kitaifa huko Marekani. Pia ni rais wa Chuo cha
Biblia cha Ligonier Academy of Biblical and Theological Studies and Reformation Bible College.
Pia anafanya kazi kama mhubiri na mwalimu wa Ukristo katika chuo cha Saint Andrew's in
Sanford, FL. [33]
Dr. Sproul mwaka 2003 aliandika kitabu chake alichokiita:” The Dark Side of Islam” [34] yaani
“Uovu uliojificha wa Uislam” ambacho kina kurasa 112. Anasema katika kitabu hicho kuwa
Uislamu ni dini ambayo haipaswi kutoitilia maanani, ni dini inayokuwa kwa kasi zaidi kuliko zote
duniani, na Uislamu umeingia huko Amerika ambako kwa sasa kuna Waislamu takriban millioni 5
hadi 7 na idadi hiyo inaongezeka kwa kasi sana kwa watu kuingia dini hiyo. Hivyo yeye
akisaidiana na Abdul Saleeb anayedai kuwa alitoka katika Uislam anasema lengo ni kuzuia kukua
huko kwa kasi kwa dini hiyo kwa kuwapa wakristo kuufahamu Uislamu na kupata msingi wa
kumjibu Muislamu anyeweza kukutana nae katika mazingira yake ili asije akatoka katika Ukristo
kwani eti Uislamu ni fujo na si amani katu. [35]
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


10
↑Dr. Sproul, R. C. mwandishi wa kitabu cha
        “The Dark Side of Islam”
      {Chanzo: www.amazon.com}
↑ Kitabu cha Dr. Sproul, R.C. kinavyoonekana kwa nje cha
              “The Dark Side of Islam”
            {Chanzo: www.amazon.com}
Dr. Qanta A. Ahmed, (MD) mwanamama toka Uingereza, kitaaluma ni daktari wa binadamu
aliandika kitabu chake alichokiita “In the Land of Invissible Women” [36] yaani “Katika Nchi ya
Wanawake Wasionekana” alichokiandika mwaka 2008 chenye kurasa 464 anaeleza katika kitabu
chake kuupotosha Uislamu kuwa eti ni dini ya kibaguzi kwani alipokuwa Saudi Arabia
alipomfanyia upasuaji mwanamke yeyote bado mwanamke mgonjwa alitakiwa bado awe
amemevaa ushungi wake, anasema hata kwenye kuhiji Maka eti kwamba alipata manyanyaso
toka kwa wafanyakazi. Anasema Uislamu unawakandamiza wanawake katika mambo ya ndoa,
mapenzi na kujamiiana, harusi, wajibu wa kimalezi wa familia zao, talaka, ajira urafiki wa ukaribu
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


11
na watu, na anamalilizia kusema kwamba Wamarekani ndio wanaochukiwa zaidi katika Uislamu
[37].
↑ Kitabu cha Dr. Qanta Ahmed kinavyoonekana kwa nje cha
         “In the Land of Invissible Women ”
            {Chanzo: www.amazon.com}
Jitahada nyingi za Freemasons zimefanywa ili kuipindisha au kuipotosha Qur’an Tukufu, lakini
kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hazikuzaa matunda, hizi ni pamoja na Mchungaji Terry Jones
wa Marekani katika mpango wake wa kuichoma moto Qur’an ili kuadhimisha miaka 9 ya tukioa
la ulipuaji wa majengo pacha ya Marekani [38].
Qur’an ni kitabu kilicho muongozo katika Uislam, na hakijawahi kubadilishwa hata mstari au aya
moja tangu kilipofikishwa duniani kupitia mitume mpaka leo.
Freemasons Juni, 1999 walijaribu kuandika Qur’an Feki ili kuupotosha na kuupindisha umma wa
kiislamu duniani, lakini walishindwa kabisa kwani katika Uislamu wapo wasomi wa dini ya
kiislamu ambao wamehifadhi (wameweka vichwani/ akilini yaani ‘mahafidhi’) Qur’an yote hata
akiamka usingizini na hivyo ni rahisi mno kubaini mabadiliko yoyote ya uwongo yanayoweza
kufanywa kwa hila toka ndani au nje ya Uislamu. Hivyo hila hiyo ikabainika mara moja, mpango
huo wa kuandika Kuran Feki hiyo uliratibiwa na serikali ya kimasonia ya Marekani chini ya rais
George W. Bush wa kipindi hicho na wamasonia wa kiyahudi, siri ya kuwepo kwa kitabu hicho
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


12
ilibainishwa na gazeti la liitwalo “Al-Usbn” la Juni, 2004 la nchini Misri [39].
Qur’an hiyo Feki wamasonia waliiita “The True Furkan” au “Al-Furqan Al-Haqq” na majina ya
waandishi yaliyo tumika ni ya kiarabu ili ionekane imeandikwa na Waislamu, majina hayo ya
waandishi ni “Alsaffee na Al-Mahdy A. Al-Radhy” ambayo ilichapishwa Marekani na kampuni ya
Wine Press Publishing kwa namba ya bidhaa ikiwa ni: ISBN 1579211755 – 978579211752,
iliandikwa kwa lugha mbili ndani ya kitabu kimoja yaani ya kiarabu na kiingereza kwa pamoja, na
kitabu hicho kilikuwa na mafundisho mengi toka katika Agano la Kale la Biblia na mambo
mengine yaliyoongezwa yaani kutungwa na wao [40].
Mwandishi wa kitabu hiko Al-Mahdy A. Al-Radhy ni mwanachama wa kamati kuu ya kimasonia
inayoitwa “Project Omega 2001. Baada ya kukitoa kitabu hicho ambacho kilikuwa kikiuzwa huko
Marekani kwa Dola za kimarekani 13.74, Al-Mahdy A. Al-Radhy alisema waislamu hawajawahi
kupata ujumbe wa kweli wa injili kama huo, akikisifu kitabu hicho na kuongeza kuwa, hiyo ni
zana ya kuwaweka waislam huru kwa kuwa eti wao ni watumwa katika dini yao waliotiwa
utumwani na Qur’an, kitabu hiki cha Kuran Feki kilipigwa marufuku kuuzwa India [41].
Qur’an hiyo feki ina kurasa 366 na sura 77 ikihesabiwa na utangulizi na hitimisho lake. Kitabu
hicho kwa jina linguine kinaitwa “21 Century Kuran” yaani “Qur’an ya Karne ya 21”. Kitabu hiko
cha “Qur’an Feki” kiligaiwa bure huko nchini Kuwait kwa wanafunzi wa shule binafsi zinazotumia
mtaala wa Kiingereza yaani “English Medium” lakini kilibainika kuwa si Qur’an halisi. Kuran hiyo
feki ina baadhi ya sura zinazoitwa kwa majina kama ya kwenye Qur’an Halisi, kuna Sura inayitwa
“Al Fat’ha”, “Al Jana”, na “Al-Injil” na kila sura haianzi na “Bismillah”bali huanza na Utatu
Mtakatifu yaani “kwa jina la baba, na la mwana na la roho mtakatifu, Amina!” na pia kitabu
hicho kinasema eti: ndoa za mitala ni haramu eti kwamba ni uzinzi! talaka ni haramu na Jihadi ni
haramu! [42].
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


13
Kuran Feki iliyotengenezwa na Freemasons Marekani 1999
{Chanzo: http://en.wikipedia.org/wiki/The_True_Furkan}

HITIMISHO NA TAFAKURI
Ndugu msomaji mpendwa uwe mkristo au muislam, umeshawahi kujiuliza ni kwanini wale
wanaoitwa ‘magaidi’ hupambana na maslahi ya Marekani tu duniani popote yalipo?! hii ni wazi
Uislamu hauna uadui dhidi ya dini yeyote duniani, kwani mafundisho yake ni kuto kudhulumu
wala kudhulumiwa wala kumlazimisha mtu awe muislamu, bali hizi ni chuki zilizopandikizwa na
Freemasons kwa utaratibu kama huu wa akina Spencer na wengine kwa usimamizi wa taifa kuu
duniani la ki-freemason la Marekani ambako shetani amesimika vibaraka wake mashetani-watu
ili kuitawala dunia chini ya usimamizi wake shetani.
Kama hao wanaoitwa ‘Magaidi’ wangelikuwa na uadui na Ukristo basi mahala pa kushambulia
sio Marekani kwani huko sio chimbuko la Ukristo bali wangeshambulia Ugiriki ambako ndio
waanzilishi wa Uorthodox duniani [43], na Italia ambako ndio chimbuko la ukristo wa Kikatoliki
kisha basi waelekee Ujerumani ambako ndio chimbuko la Ukristo wa Kiprotestanti duniani chini
ya Martin Luther (karne ya 16) [44] na ndiko chimbuko la Joseph Ratszinger yaani Papa Benedict
XVI wa Kanisa Katoliki duniani?
Kwanini kama hao wanaoitwa ‘Magaidi’ wanapigana na Ukristo basi hawalipui nchi ya Poland
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


14
taifa linaloongozwa kwa misingi ya Kikatoloki hadi leo na ambako pia ndio chimbuko la Papa
John Paulo II? Kwa nini sio Uingereza chimbuko la Uanglikana chini ya Mfalme Henry VIII [45]?
nk.
Kwahiyo Mpendwa msomaji funguka akili yako leo na uufahamu ukweli sahihi kwamba wale
waitwao “Magaidi” wanapambana na U-freemason sio ukristo baada ya wao waitwao “Magaidi”
kufahamu freemasons ni mawakala wa shetani katika kumuangamiza binadamu dhidi ya Mungu
na hivyo kujitoa kindakindaki kupambana nao.
Ikumbukwe kwamba, mtu kama Bilionea wa Saudi Arabia, Osama Bin Laden historia yake
inaonesha alikuwa rafiki mkubwa wa taifa la Marekani na alisoma vyuo vya kijeshi vya Marekani
na baadae alipigana vita ya Marekani dhidi ya Wakomunisti wa Vietnam (1965-1975) kwa
upande wa Marekani kwa kuwa hakufahamu kuwa Marekani lilikuwa ni taifa dhalimu la
kimasonia. Hii ni vita pekee niijuayo mimi ambayo Marekani ilishindwa. Lakini Osama baada ya
kutambua kuwa kumbe Marekani ni taifa dhalimu la kimasonia duniani basi ndio akaanzisha
harakati za kupambana nalo kwa kuanzisha Al-Qaeda mnamo 1988 na kuanza kuyawinda
maslahi ya Marekani popote duniani hasa baada Vita ya Ghuba 1992 (Gulf War) yaani Marekani
dhidi ya Iraq.
Hii inamaana ya kwamba, kupingana na hao waitwao “Magaidi” ni sawa na kupigania
maendeleo ya U-freemason bila ya kujua na hiki ndicho kinachofanyika baada ya umma wa
dunia nzima kuchotwa akili kupitia propaganda za vyombo vya habari vya kimasonia. Hawa
freemasons ni pamoja na marais wa Marekani wote ambapo katiba yao inamtaka kila mgombea
urais sifa ya kwanza awe “tajiri” hili neno halitumiki utajiri katika maana ya kawaida bali uwe
“milionea wa ki-freemason” ili uupiganie Umasonia duniani. Mfano mzuri ni Barack Obama
alipotangaza katikati mwa Mei, 2012 kuruhusu rasmi ushoga Marekani ikiwa ni miongoni mwa
sera zake katika kugombea tena urais 2012, pia Mwana Mfalme wa Uingereza mnamo mwaka
2011 kuzitaka nchi za Jumuia ya Madola ikiwemo Tanzania kuhalalisha ushoga na usagaji.
Marais wa Marekani akiwemo Bill Clinton, George W. Bush, Barack Obama wote ni freemasons
isipokuwa marais watatu ambao ni J. F. Kennedy aliyeuliwawa [46] 1963/4 , na Abraham Lincoln
 aliuliwa na Mmasonia Myahudi John Wilkes Booth (Botha) mnamo Aprili 14, 1865 huko
Washington D. C. Marekani [47]na Richard Nixon aliyelazimishwa kujiuzuru [48] baada ya
kukataa kuongoza taifa la Marekani kimasonia.
Hebu jiulize msomaji, Uislam ulikuwepo tangu binadamu wa kwanza alipoumbwa (Adam),
ukaendelea kuwepo enzi za akina Ibrahim, Ismail (Ishmael), Is-hak, Yaakub (Yakobo), Musa na
Issa (Yesu) tangu karne nyingi duniani na kukamilishwa na Mtume Muhammad (S.A.W) karne ya
7 kwa ushahidi wa aya mbalimbali toka katika Qur’an ikiwemo hii: “Semeni ninyi: Tumemuamini
Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na
Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Issa, na pia waliyo pewa Manabii
wengine (yaani akiwemo Adam) kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutofautishi baina ya yeyote
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


15
katika hao, na sisi tumesilimu (ni waislamu) kwake.”[49], iweje basi wale wanaoitwa “Magaidi”
kama kina Osama Bin Laden waanze kuyawinda maslahi ya Kimarekani kuanzia hasa miaka ya
1990?! Twende pamoja, fuatana nami ndugu msomaji hapa chini.
Ndugu yangu msomaji! propaganda za kimasonia dhidi Uislam duniani ni pamoja na wao
Freemasons kufanya matukio makubwa ya mauaji kwa kuyatengeneza yaonekane kana kwamba
yamefanywa na waislamu wanaoitwa magaidi, mfano mzuri ni tukio la Septemba 11, la mwaka
2001 ambalo kiukweli halikufanywa na Osama au Al-qaeda au muislamu yeyote. Na ushahidi wa
hili ni kama ifuatavyo:
Siri hii nzito Bw. David Duke, mnamo 8/10/2001 alieleza katika utafiti wake alioutoa kupitia
mtandao akiuita “THE BIG LIE, The True Reason Behind the Attack of September 11” [50] yaani
“UONGO MKUBWA, Sababu ya Kweli Juu ya Tukio la Septemba 11” yeye ni Mmarekani
msimamia ukweli mtafiti, msomi ambaye ni rais wa shirikisho liitwalo Europian-American Unity
and Rights Organization.
Mwingine ni Mmarekani mtafiti Bw. Mark Glenn, katika utafiti wake alioutoa kupitia mtandao
kwa jina la “Truth And Lies About September 11” [51] yaani “Ukweli na Uongo juu ya Tukio la
September 11”.
Pia Mchambuzi wa kitanzania aitwae Nizar Visram, katika makala yake chini ya kichwa cha
habari alichokiita “Miaka Tisa Baada ya 9/11 Wananchi Wanadai Ukweli” makala hiyo aliiandika
katika gazeti la Mwananchi la Jumatano Septemba 15, 2010 [52].
Wote hawa watatu wanaeleza kwamba tukio la Septemba 11 liliandaliwa na serikali ya
kimasonia ya Marekani chini ya rais wa wakati huo Bw. George W. Bush (Jr/ Mtoto) ili Uislamu
uchukiwe duniani na dunia nzima ikubali kupitisha Sheria ya Ugaidi ambayo aghalabu ni dhidi ya
Uislamu duniani, pia ili na kupata uhalali wa kuivamia Afghanstan na kwakweli walifanikiwa
katika haya!
Tukio hilo lilipangwa kama sinema, hebu fikiria ndugu yangu mpendwa, majengo pacha
yaliolipuliwa ni kitovu cha biashara duniani ambacho kilihamishwa toka London baada ya kuanza
Vita ya Pili ya Dunia (1939), kwahiyo wafanyabiashara mamilionea na mabilionea hawakosekani
humo muda wote, iweje leo waliokufa wote ni wafanyakazi tu na raia wa kawaida walikuwa na
mishughuliko humo? Hii maana yake ni kwamba, watu hao waliufahamu mpango huo mapema
na kujiweka mbali na eneo hilo, na raia wa kawaida kutolewa kafara katika tukio hilo na
wamasonia.
Hatimaye serikali ya Tanzania chini ya rais Benjamin W. Mkapa mwaka 2002 kwa shinikizo hilo la
kipropaganda wakaridhia sheria hiyo iliyoitwa “The Prevention of Terrorism Act” [53] yaani
“Sheria ya Kuzuia Ugaidi” kutokana uzushi huo.
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


16
Baada ya wamarekani kuujua ukweli huu wamefungua kesi ya kuidai serikali yao fidia kutokana
na vifo vya ndugu zao. [54] Swala hili halitangazwi katika vyombo vya habari hasa vya kimataifa
kwa sababu vyombo hivyo vinamilikiwa na freemasons hao. Na aghalabu vyombo vya habari vya
nchi zetu hutegemea habari za kimataifa toka katika vyombo hivyo.
Lakini pia Mwandishi wa habari wa kitanzania Bw. William Shao amelieleza swala hilo katika
kitabu chake cha 2011 alichokiita “HADAA: Unafiki Marekani, Ugaidi Duniani” anaeleza kwamba
Osama wala Al-Qaeda wala Uislamu ulioshiriki kulipua majengo pacha ya Pentagon huko
Marekani bali ni mpango wa G.W. Bush na serikali yake, na hapa namnukuu kwa ufupi:
    “Damu ya makumi ya maelfu ya wanadamu wasio na hatia
ilimwagika katika kipindi cha miaka kumi tangu 2001 hadi 2011 kwa
kile kinachodaiwa kuwa ni ‘ugaidi’ na VITA DHIDI YA UGAIDI.
Katika mwaka wa kumi wa vita hivyo, Marekani ikadai kuwa imemuua
kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda, Osama bin Laden,
ambaye wanadai kuwa ndiye aliyeandaa ugaidi dhidi ya Marekani
Septemba 11, 2001. Ukweli ni kwamba waliohusika na ‘ugaidi’ huo
hawakutajwa, na waliotajwa hawakuhusika. Osama bin Laden
hakuhusika kwa vyovyote na ugaidi huo dhidi ya Marekani. Hata
hivyo, kifo chake nacho kina utata mwingi. Mengi yaliyosemwa ni ya
kutungwa kwa kusudi la kuihadaa dunia. Mengi, au yote, yaliyodaiwa
kuithibitishia dunia kuwa Osama bin Laden alikuwa na hatia ya
kufanya ugaidi huo ni ushahidi wa bandia. Mwandishi wa Hadaa
ameweka wazi uchambuzi wa tafiti zilizofanywa kuhusu ugaidi huo
ulioitikisa dunia na udanganyifu uliotawala tukio hilo na mazingira ya
‘kifo’ cha Osama bin Laden.” [55]
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


17
Kitabu cha William Shao kinavyoonekana kwa nje.
        Chanzo: http://wshao.blogspot.com

UISLAMU UNAPIGWA VITA NA FREEMASONS DUNIANI SABABU YAKE
                          NINI?
Sababu yake ndugu msomaji ni kwamba, baada ya kumalizika kwa Vita Baridi (Cold War) 1990
duniani ambapo kitovu cha Mfumo wa Ukomunisti (USSR) kikasambaratika chini ya rais Mikhail
(Michael) Gorbachev wa Urusi kwa msingi kwamba yeye hakuwa mjamaa (mkomunisti) hivyo
akiwa madarakani akaibadili Urusi kuwa yenye uchumi wa kibepari (Kiliberali/ Soko Huria) na
kuachana na Ukomunisti ulioasisiwa na Baba wa Ukomunisti katika taifa hilo Bw. Lenin ambaye
chini ya uratibubu wake raia walimpindua Mfalme Tsar Nicolas, katika Mapinduzi ya Urusi ya
1917 ambaye yeye Lenin alikuwa mfuasi wa falsafa ya Umarx (Marxism) ilioanzishwa na
Mwanafalsafa wa kijerumani Carl Marx (1818-1883) mnamo mwaka 1848 [56] ambapo
mafundisho yake yalitaka mgawanyo sawa wa pato la taifa kati ya tabaka la wafanyakazi na
watawala na hatimaye wafanyakazi ndio washike hatamu ya kuongoza nchi na nyenzo zote kuu
za uzalishaji (viwanda) vimilikiwe na Umma sio watu wachache binafsi (mabepari) .
Hivyo huko Ulaya, sera hii ilionekana kuwa suluhisho la makandamizi na unyonyaji wa
walionacho (haves) yaani mabepari dhidi ya masikini wasionacho (have-nots). Mabepari huko
Marekani wengi wao ndio freemasons kama vile bilionea Bill Gates.
Kwa hiyo kwa maana nyingine vita baridi ilikuwa ni vita kati ya wakomunisti na freemasons chini
ya taifa ya kimasonia la Marekani, kwa hiyo ushindi wa ubepari dhidi ya Ukomunisti ni ushindi
wa freemasons kusonga mbele ili kutaka kuitawala dunia yaani “New World Order” kwa Kilatini
wanaita “Novus Ordo Seclorum” ambayo alama yake ni ndege tai ambaye pia yupo katika noti
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


18
ya dola ya Marekani [57]. Watu wengi huziamini habari za kipropaganda za vyombo vya habari
vya kimataifa kama vile BBC, VOA, RFI (Radio France International), CNN, RDW (Radio Deutch
Welle) nk. bila ya kujua kuwa asilimia kubwa ya vyombo vya habari vya kimataifa vinamilikiwa
na Freemasons duniani kama nyenzo za kuhalalisha propaganda na Ushetani wao ikiwemo
umagharibishaji (westernization) [58] ambao kwa lugha rasmi na ya mficho inaitwa Utandawazi
ambao aghalabu watu wengi hawajui kuwa ni propaganda sio uhalisia wa dhana hii.
Utandawazi si chochote bali ni Sera au mkakati danganyifu wa kipropaganda unaodaiwa eti
kukusudia kuleta maendeleo dunia nzima zikiwemo nchi masikini ziwe kama za Ulaya, sasa
kama ndio, mbona Ulaya pia masikini wapo hata ombaomba?! kwa nini wasingeanza huko?! huu
ni ulaghai mtupu, bali ukweli ni kwamba Utandawazi ni mkakati wa Mawakala wa Shetani
(freemasons) duniani waliouanzisha na kuutumia kama nyenzo ya kuupotosha ulimwengu ili
Umasonia kutawala dunia! ni pamoja na wao kujitajirisha zaidi, kuipotosha jamii kimaadili,
kifikra, kiuchumi kwa kuifukarisha jamii katika lindi la umasikini wa kutupwa [59] kwani mtu
akishakuwa masikini huwa aghalabu ni rahisi kumtumia au kumuendesha katika ‘ushenzi’ wa
kumuasi Mwenyezi Mungu namna watakavyo vile watakavyo wamasonia, hii ikiwa ni pamoja na
kubuni ajira za kumuasi Mungu eti ili watu uondokane na umasikini na lazima mtu utakubali,
mfano ni uhalalishwaji wa biashara za ngono huko Ulaya.
Ifahamike kwamba hata utamaduni ulioko sas huko Magharibi, sio utamaduni halisi wa mzungu
wa huko bali ni matokeo ya udhibiti wa Umasonia, kwa hiyo wamefanikiwa huko kwao sasa
wanaitaka dunia nzima.
Baada ya ya kumtokomeza adui yao huo Ukomunisti 1990, freemasons wakaona adui aliyebaki
ni Uislamu kama kikwazo kwa wao kuiharibu jamii duniani ikiwemo kushika kwao soko la mafuta
duniani, kusambaza mfumo wa Riba duniani, kukua kwa Uislamu Magharibi, kuwa na msimamo
na maadili ya dini yakiwemo mavazi, ulevi, uzinzi na kila kinachopingana na Mungu, na uislamu
kuonekana kikwazo cha kukuwa kwa “Ushetani” (Freemasonry) duniani.
Kwa hiyo kuanzia 1992 kwa urasmi kabisa taifa la ki-freemason Marekani kwa kutumia Taasisi
yake ya kimasonia ya kimataifa, yaani Umoja wa Mataifa (UNO) ambayo wengi wanadhani ni
taasisi ya mataifa yote duniani kumbe sivyo ila mali ya wamasonia! Marekani ikaanza kwa
kuivamia Iraq (nchi ya pili kwa kuzalisha mafuta duniani) chini ya Sadam Hussein (Gulf War)
baada ya kumgombanisha na muislamu mwenzake wa Kuwait na kujifanya anakwenda
kumsaidia kumbe ni ‘wagawe ili uwatawale’ (Divide and Rule) na ndio maana 2003 wakaja na
vita ya pili ya Iraq kwa kusingizia eti Saddam anatengeneza silaha za nyuklia, ambazo
hazikupatikana mpaka leo! na Sadamu akanyongwa kwa kukatwa kichwa siku ya Idd Kubwa ya
2003 na bado Marekani hadi sasa hataki kuondoka Iraq moja kwa moja, lengo ni ili andelee
kupata maslahi toka kwa vibaraka aliowapandikiza baada ya Saddam Hussein.
Freemasons wakati mwingine anapokuja unaweza kudhani ni mkristo kwa kuwa ni mmagharibi
jina lake lina asili ya kimagharibi kama vile la kigiriki, kilatini, kiingereza, kifaransa nk. kama lilivyo
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


19
chimbuko la ukristo wenyewe. Kiuhalisia, Ukristo katu sio kikwazo dhidi ya kukua kwa
U-freemason duniani kwani tayari freemasons wamefanikiwa kuudhibiti ukristo katika chimbuko
au kitovu chake huko Ulaya ndani ya makanisa kiasi kwamba wanaupeleka kwa kuupindisha vile
watakavyo kwani walishafanikiwa kujipenyeza katika kada mbalimbali za kanisa na uongozi wa
juu wa madhehebu mbalimbali duniani.
Na Freemasons wengine hata kuanzisha madhehebu au taasisi mbalimbali ndani ya makanisa
kufanikisha kuongoza kanisa kimasonia aghalabu bila ya waumini kujua wamasonia hao
wakijifanya kuwa viongozi wa kikristo, na kuweza kuhalalisha Ushetani kama vile ushoga, usagaji
na, uvaaji mavazi yasiostahili katika ibada ndani ya makanisa na mazingira kwa ujumla, kwa
mfano huko Uingereza katika Uanglikana na Marekani katika Usabato huko Marekani. Mfano
Askofu Michael Ingham wa Dayosisi ya New Westminster huko Uingereza ameruhusu na
kubariki ndoa za jinsia moja! [60]
 Mfano Ignatius Loyola mwaka 1534 ndani ya kanisa la Roma alianzisha Shirikisho aliloliita
“Society of Jesus” au “Jesuits” yaani “Jamii au Watu wa Yesu” ambalo lilipata baraka za Papa
baada kuaminishwa kuwa eti Loyola aliunda shirikisho hilo ili kuulinda Ukatoliki dhidi ya harakati
za zilizokuwa zimeibuka huko Ulaya Magharibi hasa Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa,
Hispania nk. kujitenga na Ukatoliki na kuanzisha Uprotestanti chini ya Martin Luther.
Lakini kumbe ukweli ni kwamba kwa mujibu wa mtafiti wa kimarekani Robert Howard anasema
Bw. Ignatius Loyola alikuwa Freemason ambaye ndiye aliyeanzisha “Iluminati” nae akawa mkuu
wa kundi hilo, yaani kundi la wanachama wa kimasonia wenye kuanzia daraja la 5 hadi la juu
yaani la 33 ambalo ni tabaka la wamasonia linaloaminika kuwa lenye elimu kubwa ya kimasonia
ambalo kwa kuanzia Loyola aliweka makao makuu huko Visiwani Malta ambao wanamwabudu
Shetani (Lucifer) [61]. Pia kwa mujibu wa mtafiti Kareena Kapoo kupitia mtandao wa intaneti
katika www.DesiHits.com/KareenaKapoor anasema kuwa Martin Luther alikuwa Freemason
ambaye ndiye aliyeupinga Ukatoliki duniani na kuasisi Uprotestanti ambapo alianzisha kanisa
lake la dhehebu la Lutherani duniani.
Mfano mwingine wa namna gani freemasons wamefanikiwa sana kuingia katika makanisa
hatimaye kuliongoza katika misingi isiyo ya kibiblia ni pamoja na kuingiza misingi ya “Riba”
kutumika katika makanisa huko Ulaya na hata Tanzania kwa sasa na maeneo mengine ya dunia.
Je mpendwa msomaji! unaikumbuka Taasisi iliyojiita “DECI Tanzania” iliyokuwepo takriban kati
ya 2006-2010? ambayo iliingia Tanzania, chimbuko lake kwa yakini baadaye ikaja kufahamika ni
Marekani toka katika kanisa la Pentekoste! siri iliyotolewa na wachungaji wa kanisa hilo baada
ya kukamatwa na jeshi la polisi la Tanzania baada ya Serikali ya Tanzania kuipiga marufuku
taasisi hiyo ambayo watanzania walikuwa hawajui kuwa ni ya kimasonia toka Marekani! na
wengi “walipanda” pesa zao (waliweka) ili zizae “Riba” baada ya wiki kadhaa, hatimaye DECI
ilifungwa na kwa kuwa ilikuwa haikusajiliwa kufanya kazi za kibenki na hivyo watanzania wote
waliopanda pesa hawakupata walichoweka wala riba walikuwa wanaisubiri kwa matumaini na
shauku kubwa.
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


20
Miongoni mwa mambo ambayo freemasons walifanikiwa kwa mujibu wa mtafiti Robert
Howard katika makala yake iliyoitwa “United States Presidents and The Illuminati / Masonic
Power Structure, Hard Truth/Wake Up America” kupitia mtandao wa intaneti:
www.forbiddenknowledge.com ni kuuharibu ukristo moja wapo kama mfano na ushahidi ni kile
kinachoitwa “Apocrypha” ambapo mwaka 1776 tabaka la vyeo vya juu la kimasonia (Illuminati)
huko Ulaya liliunda kamati maalum ya kuiharibu Biblia ambayo iliitwa “The Biblical Destruction
Group” ambapo pamoja na mambo mengine, walifanya kile walichokiita ‘To Eliminate the
Opiate" (out of print)’ kamati hii ilikuwa chini ya mmasonia aitwae Rabbi Antelman na
ilifanyakazi kwa miaka 50 [62] na walifanikiwa kufikia 1826 kufuta maandiko (vitabu) 14 toka
kwenye Biblia na kisha kuchapishwa toleo la Biblia lililoitwa toleo la Mfalme James yaani “King
James Version” [63] inayotumika hadi sasa, na sasa wana mpango kufuta maandiko yoye
yanayoonekana kama yanamkandamiza mwanamke, mpango ambao ulianza kupangwa mwaka
1988.
Pia vita dhidi ya Uislamu ni pamoja na wao kuanzisha taasisi maalum za kupambana na Uislam
kama hii ya Jihad Watch chini ya Robert Spencer. Kuchochea vita kwa kupandikiza vibaraka
katika nchi za kiislamu kwa kisingizio cha Demokrasia mfano yaliyotokea Palestina (kwa
kuwapandikiza wayahudi tangu 1947 na kuitumia yao ya kimasonia ya Umoja wa Mataifa -UNO
kuasisi taifa la Israel ambalo halikuwepo ndani ya ardhi ya wapalestina mwaka 1967 baada ya
kuwasukumia huko Ukanda wa Gaza nk. na mpaka leo Wayahudi wakiendea kujenga makazi ya
kudumu katika ardhi ya Wapalestina). Na yale yanayotokea 2011-12 Libya, Misri, Algeria,
Tunisia na Syria ni mkakati wa kimasonia wa “wagawe ili uwatawale” na sasa wakiwa katika
mkakati dhidi ya Sudan kwa Omar Al-Bashir na Iran kwa Mohammed Nejad.
Demokrasia ya Kimagharibi sio demokrasia ya kweli kama watu wanavyodhani, kuiamini na
kuichukulia kwani huzingatia utashi wa wengi tu, je wale wachache wanachukuliwaje? zaidi ya
kupuuzwa hata kama waliowengi hawako sahihi kimantiki katika kuchagua kwao?! na hatakama
kimantiki wachache wanasimamia uhalali na wengi wanasimamia udhalimu, hivyo kwa hali hii
dhana ya “Demokrasia ya Magharibi ni Udikteta dhidi ya wachache” [64] si vinginevyo ikiwa ni
moja ya nyezo ya njia wanayopitishia umasonia. Hivyo dhana ya Demokrasia ingelikuwa sahihi
kama ingezingatia ubora/ ufanisi wa mawazo ya wengi na wachache, sio uwingi wa waliochagua
kwani hata wengi wanaweza kusimamia ujinga au udhalimu, fikra ya kwamba ‘penye wengi
hapaharibiki neno haina nafasi katika eneo kama hili hili kwani kauli hii ni ya kubahatisha tu.
Mfano mzuri ni Libya ambapo hapakuwa na Demokrasia ya kimagharibi lakini Muammar
Gaddaffi (1942-2011) aliyeingia madarakani Libya 1969 akiwa na umri wa miaka 27 kwa
mapinduzi ya kijeshi kwa kumng’oa Mfalme Idrisa wa I aliyekuwa akiwajali kimaslahi
wamagharibi huku akiacha kutumia rasili mali za mafuta za nchi hiyo kwa ajili ya wananchi wake.
Pamoja na kwamba Gaddaffi hakufuata Demokrasia bali utawala wa kijeshi, alitumia vema rasili
mali za mafuta ya Libya kwa ajili ya wananchi wa nchi hiyo kuliko rais au dikteta yeyote duniani
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


21
kupata kutokea ambapo kila raia wake alipata huduma za msingi bure zikiwemo Elimu toka
chekechea hadi viwango vyote katika elimu ya vyuo vikuu (yaani mtu asome atakavyo), huduma
ya maji bure, umeme bure, nyumba bure na afya bure nk. Ni wapi duniani pameshawahi
kufanywa hivyo chini ya kiongozi gani?
Ikumbukwe pia Gaddaffi aliwahi kujitolea kugharamia mkutano wa Umoja wa Nchi za Afrika
(AU) uliowahi kufanyika Ethiopia, hii ni baada ya kuonekana mkutano huo usingefanyika kwa
ukosefu wa michango ya kifedha toka kwa nchi wanachama. Pia alitoa misaada mingi katika nchi
za kiafrika ya kijamii na kiuchumi na mpaka anaondoka madarakani Libya haikuwa na deni
linayodaiwa na taifa au benki yoyote duniani.
Waliosemekana eti waasi dhidi ya Ghadaffi ni wale wapinzani wa Ghaddaffi ambao waliokimbia
na kuishi uhamishoni kama vile Uingereza na hivyo wakatumika na wamasonia wa magharibi
kwa kupewa silaha na kusaidiana na majeshi ya kimagharibi ya NATO ili waje kuwa vibaraka
ambao nao sasa wamegawanyika, kuna wanaotaka serikali ya kidemokrasia, wengine ufalme na
kwa upande wa wananchi wengine wanataka serikali ya kiislam, wakati waasi wote mwanzo
walidai Gaddaffi hakuwa na Demokrasia kwa hiyo walikuwa wanpigania Demokrasia.
Kipi kilicho bora, ni demokrasia katika maisha duni, au maisha bora nje ya demokrasia ya
kimagharibi? Tafakari! Ifahamike sipingi demokrasia bali ile ya kimagharibi ambayo ni njia ya
kupenyezea umasonia duniani. Dhana ambao ilianzishwa na mwanafalsafa wa kale wa kigiriki
Bw. Arristotle (300BC, mwanafunzi wa Plato) na kuja kuendelezwa kisasa zaidi na wanafalsafa
wa falsafa ya Sheria yaani Jurisprudence wafaransa aliyeitwa Montesquieu na Jean Jacques
Rousseau katika karne ya 17-18 [65].
REJEA ZILIZOTUMIKA:
[1] SPENCER, Robert:” (2007)ktk: http: www.amazon.com
[2] Juri Lina, (2004) ktk uk. 532
[3] Tafuta “Prophet Muhammad”
[4] httpwww.jim-mission.org.ukarticlesuhali-ya-uislamu.pdf
[5]Jim Harries (2007 ktk uk. 3 . ktk: http://www.jim-mission.org.uk/articles/uhali-ya-uislamu.pdf
[6] Ibid ktk uk. wa 4.
[7] Ibid ktk uk. wa 6.
[8] Ibid ktk uk. wa 7.
[9] Ibid ktk uk. wa 10.
[10] Ibid ktk uk. wa 11.
[11] Ibid uk. 12.
[12] Ibidi uk. 12.
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


22
[13] www.amazon.com
[14] PENCER, Robert (2005) ktk http: www.amazon.com
[15] www.amazon.com/Robert_Spencer_Biography.
[16] Ibid.
[17] Ibid.
[18] SPENCER, Robert (2009) ktk http: www.amazon.com
[19] www.amazon.com/Robert_Spencer_Biography.
[20] Ibid.
[21] Ibid.
[22] Ibid.
[23] Op.Cit SPENCER, Robert (2007) ktk: http: www.amazon.com
[24] Swalallahu Alaih Wasalam (Amani iwe juu yake)
[25] Imeandikwa na Microsoft Corp. (Tafuta “Prophet Muhammad”)
[26] www.amazon.com
[27] Op.Cit SPENCER, Robert (2007) ktk http: www.amazon.com
[28] Ibid.
[29] www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam>Unveilling Islam
[30] Prof. Ergun Caner & Emir Caner ( 2009) ktk www.amazon.com /Books > Religion &
     Spirituality > Islam>Unveilling Islam
[31] Prof. Caner, Ergun Mehmet (2004) ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality >
     Islam> Voices Behind the Veil
[32] Ibid Prof. Ergun Mehmet Caner (2004)
[33] Dr. Sproul, R. C (2003) ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam> The
     Dark Side of Islam
[34] Ibid.
[35] Ibid.
[36] Dr. Qanta A. Ahmed:(2003) ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam>
     In the Land of Invissible Women
[37] Ibid.
[38] Gazeti la Mwananchi la 15/9/2010 ktk uk. 12.
[39] http://en.wikipedia.org/wiki/The_True_Furkan
[40] Ibid.
[41] Ibid.
[42] www.babalumra.com
[43] International World History Project kupitia: http://history-world.org
[44] Ibid.
[45] Encarta Encyclopaedia (2004)
[46] Juri Lina (2004) ktk uk. 126
[47] Ibid ktk 148-9
[48] Ibid ktk 210
[49] Qur’an Tukufu 2:136
[50] Tafuta ktk mtandao kwa kitafutio cha “Google ”
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


23
[51] Ibid.
[52] Mwananchi la 15/9/2010 Katika uk. wa 2
[53] Act Number 21/2002 (Sheria Namba 21 ya mwaka 2002).
[54] Op.Cit Mwananchi la 15/9/2010 Katika uk. wa 2
[55] Shao William (2011) utangulizi ktk: http://wshao.blogspot.com
[56] Op.Cit Encarta (2004) Tafuta “Carl Marx” na “Communist Manifesto”
[57] www.DesiHits.com/KareenaKapoor
[58] Op.Cit Juri Lina, (2004) ktk uk. 13
   Tembelea: http://en.wikipedia.org/wiki/Blessing_of_same-
    sex_unions_in_Christian_churches
   Pia:http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Christian_denominational_positions_on_homosexu
   ality#cite_note-Carey-3
   Pia: Gazeti la TAZAMA Tanzania la Jumanne, April 3-9, 2012 ktk uk. 14 chini ya Makala yenye
   kichwa cha habari “FREEMASONS WALITEKA KANISA LA WASABATO”.
[59] Joseph E. Stiglitz (2007), uk. 9
[60] Colin Coward (2004)
      Pia ktk: http://en.wikipedia.org/wiki/Blessing_of_samesex_unions_in_Christian_churches
[61] Robert Howard :United States Presidents and The Illuminati / Masonic Power Structure,
       Hard Truth/Wake Up America www.forbiddenknowledge.com
[62] Ibid.
[63] http://www.hiddenmysteries.com/redir/index9.html
[64] Dr. Jaafar Idris wa Sudan akijadili udhaifu wa Demokrasia ya kimagharibi akiwa Peace Tv.
            Mumbai India 2011.
[65] Encarta Encyclopaedia (2004) tafuta “Democracy”
BIBLIOGRAFIA:
A)VITABU:
1. Qur’an Tukufu.
2. Dr. Qanta A. Ahmed:” In the Land of Invissible Women”(2003), Sourcebooks, Inc. USA.
   Pia kinapatikana ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam> In
   the Land of Invissible Women
3. Dr. Sproul, R. C: ” The Dark Side of Islam” (2003), Crossway Books,USA.
  Pia kinapatikana ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam> The
   Dark Side of Islam
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


24
4. Microsoft Corp: “Encarta Encyclopaedia Standart”, (2004), Microsoft Corp. USA.
5. Juri Lina: ”The Architects of Deception”, 2004, Stockholm Sweden.
6. Jim Harries (Jacob Otieno):“HALI YA UISLAMU, Maelezo ya kumsaidia Mkristo
   aufahamu Uislamu” (2007), Kenya. ktk uk. 3 Pia inapatikana katika Intaneti ktk:
   http://www.jim-mission.org.uk/articles/uhali-ya-uislamu.pdf
7. Prof. Ergun Caner & Emir Caner: “An Insider’s Look of Muslim life and Beliefs Unveilling
   Islam”( 2009), Kregel Publications, USA.
   Pia kinapatika: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam> An
   Insider’s Look of Muslim life and Beliefs Unveilling Islam
8. Prof. CANER, Ergun Mehmet: “Voices Behind the Veil” (2004), Kregel Publications,
   USA.
  Pia kinapatikana ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam>
   Voices Behind the Veil
9. Shao William: “HADAA: Unafiki Marekani, Ugaidi Duniani”(2011) Tanzania
   Utangulizi ktk: http://wshao.blogspot.com
10. SPENCER, Robert:” “The Politically Incorrect Guide to Islam (and the Crusades)”,
     2005, Regnery Publishing, USA.
    Pia kinapatikana ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam> The
    Politically Incorrect Guide to Islam (and the Crusades)
11. SPENCER, Robert:” “The Complete Infidel's Guide to the Koran”,2009 ,Regnery
     Publishing, USA.
    Pia kinapatikana ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam> The
     Complete Infidel's Guide to the Koran
12. SPENCER, Robert:” The Truth about Muhammad ,The Founder of the World’s Most
    Intolerant Religion”,2007,Regnery Publishing,USA.
   Pia kinapatikana ktk: www.amazon.com /Books > Religion & Spirituality > Islam> The
    Truth about Muhammad ,The Founder of the World’s Most Intolerant Religion
13. Stiglitz, J.E: “Making Globalization Work”, (2007),W.W. Norton & Co. Ltd. London UK.
B) SHERIA:
1. The Prevention Of Terrorism Act, Act Number 21/2002
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


25
C) MAKALA:
1. Colin Coward (11 June 2004). "Canadian Church defers blessing decision and affirms
   adult same-sex relationships". Changing Attitude – Anglican Communion News.
   Retrieved 2007-05-13
D) TOVUTI:
1. http://en.wikipedia.org/wiki/Blessing_of_same-sex_unions_in_Christian_churches
2. http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Christian_denominational_positions_on_homosex
   uality#cite_note-Carey-3
3. International World History Project kupitia: http://history-world.org
4. www.forbiddenknowledge.com
5. http://www.hiddenmysteries.com/redir/index9.html
6. www.babalumra.com
7. http://en.wikipedia.org/wiki/The_True_Furkan
8. http://en.wikipedia.org/wiki/Blessing_of_samesex_unions_in_Christian_churches
E) MAGAZETI:
1. Gazeti la TAZAMA Tanzania la Jumanne, April 3-9, 2012 ktk uk. 14
  WALITEKA KANISA LA WASABATO”.
“FREEMASONS
2. Nizar Visram: Mwananchi la Jumatano, Septemba 15, 2010, ktk uk. 2 “Miaka Tisa Baada ya
   9/11 Wananchi Wanadai Ukweli”
*************************************
©Haki zote zimehifadhiwa na Mwandishi chini ya Sheria ya Haki Miliki
                      (Intellectual Property Law).
Ni ruhusa kuituma kwa yeyote au kui-print kwenye karatasi bila ya kupunguza
                             au kuongeza chochote.
===== ====== {word count = 7,560 in 25 pages} ====== =====
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?


26
Lung’wecha, K. M: FREEMASONS KATIKA UPOTOSHAJI WA UISLAMU DUNIANI! JE, MIMI NA WEWE TUNAWAJIBIKA VIPI?

1 comment:

  1. WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
    Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
    that will make you rich and famous in the world and have
    power to control people in the high place in the worldwide
    .Are you a business man or woman,artist, political,
    musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
    in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
    instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
    home.any where you choose to live in this world
    BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
    1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
    2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
    3.A Dream House bought in the country of your own choice
    4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
    destination.
    5.One year Golf Membership package
    6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
    Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
    account every month as a member
    9.One Month booked Appointment with Top 5 world
    Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
    If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
    or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com

    ReplyDelete

Twitter Bird Gadget