Tuesday, April 3, 2012

NDOA KATIKA UISLAMU


    1. MANENO  MAWILI

Namshukuru Allah swt,Mtume Mtukufu s.a.w.w. pamoja na Ahli Bayt Tukufu a.s. kwa kunijaalia niweze kufanikisha juhudi zangu hizi katika kukitayarisha kitabu hiki juu ya maudhui haya ya ndoa katika Islam.

2.UTANGULIZI

Zipo riwaya nyingi mno ambazo zimenakiliwa kutoka Mtume s.a.w.w. na Maimamu a.s. ambazo zinasema kuwa mwenye kuoaanakuwa amejidhibiti  vyema katika Islam na nusu ya sehemu ya imani inambidi afanye jitihada ili aweze kuiimarisha.Mwenye kuoa rakaa mbili za mwenye kuoa ni afadhali kuliko rakaa' sabini za mtu asiyeoa. Aliyeoa ni mpenzi wa Allah s.w.t.

Mtume s.a.w.w. amesema kuwa mtu asifanye uchelewesho katika kuoa  kwani watoto watakaozaliwa watakuwa wakimtii na kumtukuza Allah s.w.t. ambapo ujira wake utakuwa ukipatiwa wazazi wao  na mema yao pia yatakuwa yakilipwa wao.Vile vile amesema kuwa tuuendeleze Ummah wake ili aweze kuwa na fak­hari Siku ya Qiyama.

Iwapo mwanamke mimba yake itaanguka basi  Siku ya Qiyama mtoto wake huyo atakataa kuingia Jannat (Peponi) hadi  hapo wazazi wake waingizwe nae pamoja.Limetolewa onyo kuwa "kufa bila ya kuoa  ni vibaya mno."

Imam Jaafer as-Sadiq a.s. amenakiliwa akisema kuwa "Iwapo nitakuwa na dunia  pamoja na vitu vyake vyote vikawa vyangu bila ya kupitisha usiku mmoja bila mwanamke,basi mimi siridhii hayo yote.Ni afadhali ku­kosa vyote hivyo kuliko kukosa mwanamke. Vile vile sala ya aliyeoa ni afadhali kuliko sala  za kila siku pamoja na saumu za asiyeoa."

Vile vile kuna riwaya isemayo kuwa mtu atakapo kujitakasa mbele ya Allah swt,basi inambidi  afanye harusi na kuoa katika hali  ya umasikini na ufukara ni kuthibitisha imani na uaminifu juu ya Allah s.w.t. kwani Al­lah s.w.t. amesema "Oeni hata katika hali ya umasikini na ufukara kwani nitawaghaniisha."

Ipo katika riwaya kuwa muoe wake wazuri na mtu atakayeoa mwanamke kwa sababu ya tamaa ya mali au uzuri,basi atakosa vyote.Na atakayeoa  kwa kuangalia dini na imani ya mwanamke,basi atapata mali na uzuri vyote.

Katika  kumsifu mwanamke,ni bora kuliko dhahabu na fedha na mwanamke mwovu ni mbaya sana kwani hata mchanga ni afadhali kuliko  yeye. Mwanamke mwenye gharama ndogo na vilevile anazaa watoto kwa ura­hisi na mwanamke mwenye mahari ndogo basi ni mwema na mwanamke mwenye  gharama kubwa na mwenye kuzaa watoto kwa mushkeli na mwenye mahari kubwa,basi mwanamke kama huyo si mwema.

Ni Sunnah kusoma nikah wakati wa usiku,kwani Allah s.w.t. ameufanya usiku kuwa  mapumziko na starehe na inapoangukia Qamar  dar Aqrab (nyota iwapo katika Nge) basi msifanya nikah na kunapokuwa joto ka­li,iwapo kutakuwapo na ndoa,basi kunauwezekano wa kuachana.Vile vile kusifanywe ndoa siku ya jumatatu kwani siku hiyo ni  mbaya mno na iwapo itakuwa  ni siku ya kuzaliwa kwa Ma'sum a.s. au Idd basi hakuna shida yoyote.Haifai kuoa katika tarehe  26,28 na 30 za kila mwezi.

Kuoa si faradhi lakini  iwapo kuna hatari ya  kutumbukia katika maasi,basi itakuwa ni faradhi kuoa,na kwa mjane kolewa si vibaya,kwani kubakia pekee mara nyingi inakuwa mushkeli kimaisha na hivyo haitakiwi kujitumbukiza katika magumu ya maisha ambapo tunaweza kujiepusha.Kwa hakika ni jambo la kusikitisha kuona katika jamii yetu wajane wakitupwa bila kujali na kudharauliwa kama ni wenye nuksi ambapo inatubidi sisi kuwajali na kuwatunza na kuwaoza  inapowezekana ili wao nao waweze kuishi maisha kama wengineo wote.

Ipo Hadith inayosisitiza mno kabisa kumfanyia na kumgharamia mtu harusi na nikah kwani inayo thawabu adhimu.Kila neno litakalosemwa na  kila  tendo litakalotendwa na kila hatua itakayochukuliwa,Allah swt atampa thawabu za  sala za usiku  na saumu  za mwaka mzima.Na huko Jannat atampatia Hur al-Ain elfu moja wakiwa na majumba yaliyorembeshwa kwa  Yaquti na vito vya thamani.

Ipo riwaya inayosema  kuwa  atakayemwozesha  mjane, basi Siku ya Qiyama atakuwa miongoni mwa wale
waliorehemiwa na Allah swt.

Atakaye suluhisha baina ya bibi na bwana,basi Allah swt  atamjaalia thawabu za mashahidi elfu na hatua zo­zote zile atakazozichukua katika kufanyisha suluh na matamshi yote yatakayotoka atapatiwa thawabu za ibada za mwaka mzima.


SEHEMU YA KWANZA

3. NDOA NA MAISHA YA STAREHE


1. Mafunzo ya awali

Iwapo mimi nitataka niwe daktari au niwe mhandisi basi itanilazimu kwa mfululizo kwa kiasi cha miaka miwili, au mitatu au mitano, kumi au kumi na tano nisome kwa kupitia vyuo mbalimbali, kufuatia mazoea tofauti tofauti hadi niweze kuwa daktari au mhandisi ambaye nitaweza kukabili hali ya kazi zangu bila matatizo na vile vile iwapo nitapata matatizo nitakuwa ninajua njia za kuweza kuyarekebisha, kusahihisha na kuleta maendeleo mazuri katika fani yangu.Lakini katika zama hizi ni jambo la kusikitisha mno kuona kuwa wanaume wanataka kufuzu na kupata stashahada ya kuwa yeye ni mume bila ya kupitia mafunzo na kujitayarisha vyema kwa ajili ya mustakabali huo mpya.  Kwa hakika mwanamme au mwanamke akitaka kuwa bwana na mwanamke akitaka kuwa bibi inawalazimu wajifunze mambo mengi na namna ya kukabili mustakabali huo mpya hivyo inawabidi wapitie mawaidha, nasiha na mazungumzo ya wazee na kujionea maisha yalivyo na wakati waliopo, lakini tunaona wengine wanaoa kimchezo na baadaye maisha yanakuwa magumu huko mbeleni na hatimaye ndoa zao kuvunjika na hivyo maisha ya pande zote mbili kuharibika  kujaa kwa chuki na kukosa raha kabisa. 

Hivyo katika taarifa zinazofuata nitajaribu kuzungumzia namna ya kutengeneza ndoa yetu ikawa raha na mustarehe.

2.  Ndoa ni kazi ya kikundi.

Ndoa ni sawa na farasi wawili wakivuta kigari. Kama utakavyokuwa ukiwaona farasi wawili wamefungwa kigari nyuma yao utaelewa zaidi vile wanavyotembea kwa sababu farasi wote wawili itawabidi wainue miguu yao kwa mpangilio na wote itawabidi waelekee upande mmoja, huwezi kuona farasi mmoja anakata kushoto au mwingine kulia gari hilo likaweza kwenda, farasi wote wawili watabaki hapo na kigari kitabaki hapo hapo. Hivyo tumeona katika maisha yetu ya ndoa kuwa baada ya kuoana bwana anakwenda kushoto na bibi anachukua mwelekeo wa kulia kwa hivyo lile gari lao wanalolivuta haliwezi kutembea, wote wataangamia, na kwa hakika hii sio sababu ya ndoa.  Kwani sababu kubwa ya ndoa ni bibi na bwana kushirikiana na kwenda hatua kwa hatua pamoja kuendeleza maisha yao na ya familia yao hapo baadaye.

 

3.  Kuendesha maisha ya ndoa.

Kwa hakika ndoa iliyofanikiwa na yenye raha inamgeuza mtu akajihisi kama yuko peponi na hiyo ndiyo baraka kubwa ya Allah swt, na neema kubwa wajitahidi kiasi wawezacho kujionyesha kama kweli wao wako katika mazingara hayo ili mazungumzo wanayozungumza, vitendo wanavyotenda vionekane kama ni kweli, mfano kunaweza kuwekwa mchezo wa kuigiza vile watumwa walivyokuwa wakipigwa na kuteswa katika zama za wakoloni, lakini vile vitendo wanavyovitenda pale wakiwa kwenye jukwaa vinawavutia watu kiasi kwamba wanahisi kwamba kweli hivi ndivyo ilivyokuwa kwa hiyo na sisi ili kuonyesha maisha yetu inatubidi tufanye kila njia kufikia hayo malengo yetu ya maisha.Kwa hivyo mtu anaporudi kutoka ofisini inambidi aje nyumbani na uso wenye bashasha hata kama amekumbana na mambo mengi yaliyomuudhi, yaliyomvuruga wakati akiwa ofisini na kwa hakika akija na uso wenye bashasha nyumbani, nyumba nzima watakuwa wachangamfu watakuwa wakicheka atapenda aongee wajadiliane wazungumze wabadilishane mawazo na kwa hakika hiyo itamfanya huyo bwana asahahu uchovu wake wa siku nzima, lakini fikiria ukija umenuna,umevimba uso kama papai nyumbani wakishakuona tu umekuja umepandisha wote watakukimbia, hata kama mmoja wa familia atakuwa amewazia ukija azungumze kitu fulani hatazungumza mtu yeyote na wewe maana wanajua wakikuzungumzisha wewe ni sawa sawa na kuwatemea moto; kwa hivyo mtu huyo mmoja tu ukija nyumbani unaweza kuigeuza nyumba yako ikawa bustani nzuri au unaweza kuitengeneza nyumba yako ikawa ni chumba cha adhabu kwa sababu kila mmoja anakuogopa wote wamenuna umewatia katika adhabu na huu sio uadilifu kwa upande wa mwanamme. Na hakuna sababu ya mwanamme kuleta hali mbaya kama hii katika nyumba mwanamme inambidi akirejea kutoka  nje arudi na furaha ndani.

4.  Furaha ya milele.

Mwanamme ni bingwa katika utumishi wake lakini mtumishi aliyebobea katika utumishi daima anatenda kiasi cha kumfurahisha mwanamke na kujiona yeye ni mtu maarufu.Bibi na Bwana wanaelewana vizuri kuliko mtumishi, lakini inawabidi wote wawili wawe ni watumishi waliobobea katika fani yao bibi kwa bwana na bwana kwa bibi. Kamwe usimfanye mke wako ahisi kuwa wewe unaelewa kasoro zake na wala asifanye hisia kuwa anaelewa kasoro zako daima kila mmoja awe akimfunika mwenzake.Kwa hakika maisha ya furaha yanaweza kupatikana katika ndoa pale bibi na bwana wanapokuwa na moyo wa kutoa na wala si wa kuchukua.

 

5.  Tofauti ya maoni.

Ni jambo la lazima kuwapo na tofauti ya maoni na uhodari wa mabishano miongoni mwa watu waliokuwa wanaishi pamoja.  Hasira ni jambo la kutokea lakini haibidi pande zote mbili kuwa na hasira labda wakati mmoja awe huyu wakati mwingine awe mwenzake (yaani mmoja awe na hasira kwa wakati mmoja, wote haiwabidi kuwa na hasira kwa wakati mmoja). Kwa hivyo yule anayeweza kwanza adhibiti na mara nyingine mwenzake.  Kwa sababu mmoja anapokuwa ameingiwa na hasira na mwenzake akawa ametulia hapo balaa na maafa mengi yataweza kuepukwa. Kwa hakika nimeona maneno ya kupooza magomvi katika majumba yetu ni machache na matamu sana yaani kusema:  "samahani nisamehe, "na kwa hakika mtu anayesema samahani nisamehe  maneno hayo ni mtu mwenye busara sana na anahisi raha moyoni mwake, hasa wakati anajua yeye hayuko kwenye hatia hana makosa lakini anaomba msamaha; na kuna msemo mashuhuri  usemao 'anayetoa msamaha kwa mwenzake ni mpenzi wa Mungu'. Kwa hakika mtu mwenye moyo mkubwa ni yule anayekubali makosa yake, anayekubali lawama na kuomba msamaha.  Jambo lingine linalostahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu ni kamwe usimlaumu mwenzako.  Njia nionayo iliyo rahisi kwa ajili ya kuelewana katika magomvi kutoelewana sura mbali mbali ni kwanza ukubali maelewano japo kuwa liwe ni jambo dogo baada ya kutua na mambo kutulia mnaweza kuendelea mkafanya marekebisho na maongezi zaidi katika maelewano yenu hayo, na hatimaye kila mnapokuwa mkiendelea kupanua maelewano yenu itafika wakati mtaona kuwa mambo ambayo mliokuwa hamkuelewana yatatoweka kutakuwa na uelewano tu.

6.  Kamwe usikemee bali ushukuru.

Kamwe usiwaseme vibaya upande wa mke wako au upande wa mume wako:  Kwa sababu iwapo  mwanamme atakuwa akiwasema vibaya jamaa za mke wake basi mke ataanza kuwachukia jamaa wa mume wake.  Kamwe usiwe na hasira dhidi ya mwenzako na wala usikubali hisia kama hizo ziingie mwilini mwako.  Daima uwe ukishukuru, ukionyesha furaha sio kwa sababu ya mambo mazuri ya mwenzako bali hata upande mbaya ni muhimu sana.  Kwa kufikiria mambo mazuri tu unaweza kupitiwa na mambo mabaya.

7.  Kufukia tofauti ndogo ndogo.

Kutofautiana kwa maoni na mawazo na magomvi ni sehemu ya maisha.  Mshairi mmoja maarufu amesema:  "Je maisha ni nini, Je mauti ni nini, na kufufuka ni nini?"  Urafiki wako, magomvi yako, na kukutana kwako tena."
Kisha hakikisha kuwa ugomvi wenu haubakii mpaka wakati wa chakula kinachofuata yaani mkigombana asubuhi mpaka chakula cha mchana kiwe kimeshakwisha , na wewe hutakiwi kukwepa mlo huo. Ni lazima ukubali kuwa Allah swt ametujaalia neema kubwa ya muda huo wa kula chakula pamoja ambamo tunaongezea uhusiano wetu, uelewano na kumaliza tofauti na ugomvi wetu, lazima tuwe tahadhari kuwa kamwe tusianze mazungumzo ambayo yataleta ubishano mkali wakati tukiwa tunakula. Kwa sababu kunaweza kuanza na mazungumzo ambayo yanaweza kuleta mzozo na watu wasiweze kula chakula chao hivyo kila mtu aachilie mbali mazungumzo hayo hadi baadaye ili wote waweze kula vizuri washibe  ili waweze kumudu maisha yao na kazi zao hapo baadaye.

8.  Mapenzi na mapenzi ya kusuhubiana.

Kupendana na kucheza kwa bibi na bwana ni moja ya siri kubwa ya ufanisi wa maisha ya ndoa na kwamba inaweka hai moyo wa ndoa. Kamwe usijitupe ukajisahau bali inakubidi daima uwe ukijiweka vyema, vizuri kiasi cha kumvutia mwenzako ili daima awe akikutamani na kukupenda bila ya  kujali umri wako. Kusuhubiana kwa bibi na bwana ni gurudumu moja muhimu katika mtambo huu wa maisha ya ndoa.  Kusuhubiana kutakuwa na mafanikio na raha zake zitapatikana pale bibi na bwana watashirikiana katika mazingara hayo.  Inabidi ikumbukwe pia unapokuwa na mawazo mengi kunapokuwa na mvurugano na mtu anapokuwa na matatizo raha na hamu ya kusuhubiana  hufa. Hivyo hamu na raha ya kusuhubiana inapatikana katika hali ya mtu kuwa mchangamfu na namna ya kujiweka mwenye raha.Mtu anapochokozana kimapenzi na mwenzake basi kimchezo mchezo mapenzi yao yanaongezeka na hatimaye yanafika mbali mathalani bibi na bwana wanaweza kuwa wamelala katika mazungumzo, wanaweza kuanza mapenzi ya mmoja kumbusu mwenzake na wakawa na hamu wakaingiwa na hamu kwa wote wawili hadi kufikia hatua ya kusuhubiana kwa furaha kwa sababu pande zote mbili wanakuwa na hamu.  Vile vile ni jambo la muhimu sana kila mmoja yaani bibi na bwana kukumbuka tarehe ya mwenzako kuzaliwa ili inapofika tarehe yake ya kuzaliwa unaweza kumpa salamu za kuzaliwa au ukampa zawadi ni jambo linalovutia kuona kweli unamfikiria au kukumbuka tarehe ya ndoa mambo haya ni muhimusana kuona kuwa unamjali sana mwenzako.  Kamwe vioja vidogo vidogo na tofauti ndogo ndogo ambazo haziishi zikaleta balaa kubwa nyumbani tuwe na moyo wa kusameheana na wala tusiwe na moyo wa kukomoana kwa sababu kila hasira na chuki zikiongezeka ni sawa na kumwaga mafuta juu ya moto.

9.  Mabishano na ugomvi mbele ya watoto.

Panapokuwa na watoto katika familia ni lazima kabisa kwa bibi na bwana kuheshimiana na kuonekana kuheshimiana mbele ya watoto wao na kamwe wasionyeshe tofauti zao mbele ya watoto. ugomvi na mzozano  wa bibi na bwana mbele ya watoto unaathari mbaya kabisa kwa watoto kwa ajili ya siha ya akili zao jambo ambalo ni muhimu sana kwa watoto kuliko siha ya mwili.Vile vile matishio ya kumpiga mke ni mambo ambayo hayawezi kusameheka.

10.  Kusahau yaliyopita.

Hakuna faida ya kukalia makosa yaliyopita au mambo yaliyopita itakuwa ni vyema lau utasahau na kusameheana ili mjenge maisha mema.

11.  Mkaidi dhidi ya kuvumiliana.

Ukaidi hauleti manufaa yoyote kwa bibi na bwana na familia nzima kwa ujumla, lakini kuvumiliana na kupeana mkono kwa bibi na bwana ni jambo moja ambalo linasaidia kusukuma gurudumu la maisha bora na utengemano ambavyo hatima yake ni ya bibi na bwana kuelewana vyema na kuishi maisha ya starehe.

12.  Kugawana kazi.

Nyumba ni mahala pa mke na biashara au kazi au taaluma ni maswala ya bwana.Hivyo kama mwanamke anaishi nyumbani tu anafanya kazi za nyumbani na mwanamme anafanya kazi za biashara au ofisini basi wasiingiliane bali kila mmoja amwachie mwenzake aendeshe kazi inayompasa hiyo haimaanishi kuwa bwana asiwe na picha ya mazingara ya nyumbani na mwanamke asiwe na picha ya mazingara ya kazi bali kila mmoja inabidi wasaidiane washirikiane waishi maisha mazuri ili bibi aweze kuendelea na kazi zake vizuri na bwana aweze kuendelea na kazi zake vizuri  bila ya kuzozana.

13.  Yote yale yang'aayo.

Ni kweli kuwa umbali unavutia.  Kwa hivyo utaona bibi na bwana wanatuvutia na wanaonekana kwamba wao wanaishi vizuri kuliko sisi kwa hiyo tukazane kuwa sisi hatuishi vizuri hatuelewani kama wale wanavyoishi kwa raha na starehe la sivyo hivyo inawezakana wao wakajua siri ya bibi na bwana kwa hivyo mbele ya watu hawaonyeshi bali wanaonyesha wako raha starehe na hakuna tofauti baina yao, kunaweza kuwepo raha na starehe pamoja na tofauti miongoni mwao hivyo kwa kuwatazama wengine tusianze kuzua magomvi kwetu vile vile usione wengine wanaishi maisha kifahari na sisi baada ya kuyaona tukatamani kuishi hivyo bila kujali hali ya uchumi wa waume wetu au matatizo mengine yanayokabili familia kwa ujumla.

4.MAMBO YANAYOBIDI BIBI NA BWANA WAYAJUE.

1.  Wazoeane na kuambiana ukweli.

Mtu anapoposa ni kipindi kimoja ambacho kila upande unafanya njia ya kuvutia mwenzake.  Siku hizi tunazuzuliwa kwa kuiga mambo ya sinema kiasi kwamba wengine wanajifanya ni waigizaji wa sinema ili mradi wawavutie wenzao.
Baada ya ndoa bibi na bwana wanakwenda kutembea safari ambapo ni bibi na bwana tu na hakika hilo ni jaribio mojawapo zuri na muhimu. Mara nyingi utaona bibi na bwana wanaona aibu na wanakuwa hawana uzoefu wa kuishi maisha kama hayo ni mambo ya kuvutia pia. Wakati mmoja, wakati bibi na bwana wako katika matembezi haya baada ya harusi mwanamke alipojaribu kupiga pasi nguo zake aliziunguza kwa sababu wengine mambo haya wanakuwa hawayafanyi na katika hali hiyo alishtuka sana kiasi kwamba alitaka kumficha bwana wake asipate kujua lakini kadiri muda unavyoendelea kupita watazoeana na hali kama hiyo itakwenda inapungua.Hata hivyo baadhi ya nyakati nyingine mambo kama haya yanaendelea na kwa hakika hizo ndizo sura za matatizo. 

2.  Uwe mwangalifu na usichukue mambo kwa pupa.

Iwapo kutokuelewana kwa kiasi kidogo kidogo kutakuwa kukiendelea na kuongezeka basi yanakwenda yanazaana.  Milima inatengenezwa kwa punje ndogo ndogo,na ukianza kuzikusanya utashtukia unapata mlima.Hivyo mashitaka na tuhuma dhidi ya mwenzako yatajenga nyumba katika mioyo ya bibi au bwana. Watu kama hawa ukiwashindilia kabisa na kuwauliza yaliyotokea wiki iliyopita yaani juma lililopita utawasikia wakianza kutupiana lawama ambazo zimewaka moto kweli kweli.Kwa kutokuelewana, kwa kutotosheka katika hali kama hiyo hata ukifanya ishara yoyote basi mwenzako atakwambia wewe umenisengenya hivi ilhali wewe mwenyewe huna maana hiyo unayoambiwa na hivyo utaongeza moto huo wa kutokuelewana katika mioyo yenu. Hatua za pupa ziepukwe mtu yeyote anayempiga mwenzake ni mwehu, katili ni mnyama na mtu asiye na maendeleo kwa sababu amekiuka misingi ya kuheshimu na kumhifadhi mke wake.

3. Kutokuelewana kudhibitiwe na kuelezwa.

Kutokuelewana kati ya bibi na bwana ni vitu vya kawaida katika ndoa ambapo shaka haijatokezea.Katika hali hiyo inatakiwa maswala kama haya yachukuliwe kwa busara na kuelezwa kwa kiakili sio kwa mtu mwenyewe bali kwa mwenzake pia.Mara nyingine hatua hii haiwezekani hivyo kuna wazee wanaoweza kusaidia katika maswala ya ndoa. Hivyo ndiyo maana Islam imetoa amri kuwa kabla ya kutoa talaqa ushauri wa watu wenye hekima katika mambo ya ndoa waingilie kati na kujaribu kusuluhisha tofauti baina ya bibi na bwana.  Kwa ushauri bora kusiwe na upande wa mwanamke au upande wa mwanamme bali wawe ni watu wa nje ya watu hawa wawili kwa sababu mtu asiweze kuvutia upande wa jamaa zake. 

4.  Mawasiliano na uaminifu.

Ninapenda kuwasisitizia kuwa mawasiliano ni muhimu kabisa katika ndoa yenye furaha na starehe. Bila ya mawasiliano baina ya bibi na bwana hofu inaendelea, mashaka inaongezeka na hali ya kutokuelewana itatokezea. Hivyo kuelewana lazima kuwepo na njia za kuwasiliana kuanzia wanapooana mwanzoni ili kwamba hata bibi na bwana wakiwa ni watu mashuhuri  sana lakini waweze kuzungumza na kuelewana. Njia hii inawezekana isiwe rahisi lakini kama bibi na bwana wanajuana basi kuna mahali popote wanaweza kukutana katika maisha yao na kuzungumza. Daima uwepo na inakubidi uwe ukijaribu kuyaangalia matatizo yako,na muwe mkiheshimu uaminifu miongoni mwenu ujue namna ya kushukuru kitu chochote  kidogo kile na uache kutoa shutuma za aina zozote kwa hivyo mawasiliano yatakuwepo.Itakubidi uanzishe mazungumzo yatakayomfurahisha mwenzako ili umvutie ashiriki katika mawasiliano yenu na wala usianze na mazungumzo na mashitaka na magumu ya maisha yako magumu ya kila siku kwa sababu utamfanya yeye achukizwe na mazungumzo yako asizungumze na wewe.Baadhi ya wanawake wanashitaki kuwa waume zao hawawashirikishi katika kazi zao au katika maisha yao ya kiofisi au kibiashara. Na hali hii ni kwa sababu wanatambua kuwa nyumba ni Jannat ambapo mwanamke yupo na hivyo anapotoka kwenye shughuli zake anakuja nyumbani apumzike na afarijiwe na mke wake mara nyingi, utaona wanaumme baada ya kuja nyumbani wanawaambia mambo mengine ya kazi zao ya ofisini au ya kibiashara hii haimaanishi kwamba anahitaji ushauri kutoka kwa mke wake bali anajaribu kupunguza uzito katika akili yake na kichwa chake na kwa sababu anakuwa na imani ya uaminifu na amana hiyo anayoiwekesha kwa mke wake anajua hatafanya khiana wala kumgeuka.

Katika maisha ya ndoa sio lazima kuwa ni maongozi tu yanayotakiwa kila siku kwa wakati mwingine hata kumgusa kidogo mwenzako au hata kuminya mkono kidogo yana mawasiliano ya aina yake na yana athari zaidi kuliko ya maneno.Hivyo mnapokutana baada ya bwana kushughulika ofisini na bibi kushughulika nyumbani mnapoonana mnazungumza nakidogo kujichangamsha, jambo ambalo litaweka njia ya mawasiliano kuwa bora na mazuri;na jambo lingine ambalo ni zuri kabisa katika mawasiliano ni hizi silabi tatu:"mimi ninakupenda sana." Na lau utaongezea maneno mengine mawili ya asante sana hapo litakuwa jambo zuri sana.

5.Kula chakula na maongezi.

Shughuli za kuridhisha za chakula na maongezi yanaunganisha familia pamoja.Baba anaweza kuwafurahisha kwa kuhadithia ujana wake, akiongelea mambo mengi yenye faida kama kuendesha baiskeli,kuroa samaki na kupanda farasi siku za Jumapili, vile vile mama pia anaweza kuanzisha mazungumzo juu ya utoto wake na ujana wake.Katika majumba mengine muda unakwenda mwingi wakati wanapokuwa mezani wanakula kwasababu familia wanapokuwa wanakula pamoja wanazungumzia mambo ya siku yaliyotokea mwingine anaongelea aliyoyasikia au kuyaona na mambo mengineyo hata wengine huzungumzia matukio mengine na kuzungumzia matukio ya Qurani,Hadithi n.k.
Hivyo inabidi wakati wa kukaa kula mazungumzo yatakayotokea yawe yenye kufurahisha na kupendeza na ichukuliwe tahadhari kuwa mtu yeyote asianzishe mazungumzo yale ambayo yanaweza kusababisha kutokea ugomvi au kutokuelewana wakati wa chakula.

6. Kuwa pamoja na familia.

Wazazi wawaulize watoto wao walichofanya shuleni na wamefanya na akina nani, na walichojifunza nacho. Na hali hii itakuwa ni ya kufurahisha mno kwa mzazi na watoto kwa sababu watajikuta wazazi katika mazungumzo na watoto wao.

Kuwachukua familia katika matembezi inawabidi wazazi watumie muda mwingi pamoja na familia yao na kuwachukua familia yao kimatembezi. Kuwafanya wao wakiwa ni moja ya shughuli zao. Kwa kuchukua nje ni njia moja nzuri kabisa kwa sababu inafungamanisha familia kwa pamoja na kufanya maisha ya ndoa yakawa ya raha na mustarehe.

Inawabidi wazazi waangalie kwa makini mavazi ya watoto na usafi wao na yote hayo uyafanye kwa sauti ya kuvutia na kupendeza, uwafundishe wao namna ya kufanya vyema zaidi kwa kuvutia.

Kufikiria shughuli za siku nzima, usikalie kusoma magazeti tu au kuangalia matatizo yako inakubidi pia ufikirie kuhusu familia yako vile utakavyoweza kuiendeleza na kutatua matatizo na kuleta ushirikiano na uelewano mwema miongoni mwa familia nzima.

5. UHAKIKA ANAOTAKIWA MUME KUZINGATIA.

(a)Je unajua na kutambua kuwa wewe umechukua kitu bora kabisa kilichoumbwa na Allah swt? Roho,maisha ya mwanamke na mapenzi ya kiajabu kabisa !.

(b).Tumewafaradhishia wanaume kuwafanyia wema wazazi wao. Mama yake alimhimili katika maumivu na kumzaa katika maumivu.

(c). Macho yoyote yanayomwangalia mwanamke kwa nia mbaya ni sawa na kufanya zinaa.

(d) Bora miongoni mwenu kuliko wote ni yule mtu ambaye ni mwenye huruma na mwenye ukarimu kwa familia yake, na mimi niko vivyo hivyo kwa familia yangu.Mtume Mtukufu s.a.w.w.

(e) Wanawake wanaheshimiwa na wale watu tu ambao ni wanaume wenye huruma na wenye fahamu zao imamu na hakuna anayewakashifu na kuwatukana isipokuwa kwa wale ambao ni waovu na wapotofu.

1. Mwanamke anahitaji kuhifadhiwa:

Daima ukumbuke kuwa mwanamke ni kitu kimoja kilicho chepesi kuliko mwanamme hivyo inabidi ahifadhiwe katika kila hali ya maisha na apewe yale anayoyahitaji. Mume bora ni yule ambaye anathamini mahitajio ya mke wake na iwapo mke wake atamuomba bwana wake kitu chochote basi bwana afikirie kuwa amepewa heshima hiyo ya kumpatia mke wake alichoombwa.

2.  Muwajie kwa maongezi mema.

Daima mfanye mke wako awe na hisia kuwa yeye ni mtu muhimu kabisa katika maisha yako na kamwe usiache kudhihirisha hivyo. Kwa kutoa lawama na kutumia lugha chafu na kuhamaki kila hapa na pale yaongezea katika uelewano mbaya baina ya bibi na bwana, na haisaidii chochote katika kuleta unyumba wenye raha na starehe.

3.  Kupeana zawadi.

Zawadi, lau ikiwa ndogo kiasi gani, atakayopewa mke kutoka kwa bwana wake kwa hakika itaongezea mapenzi na uvutano baina yao na kwa hakika hili jambo ndilo linaleta raha zaidi kimapenzi.

4.  Umchukulie vyema.

Mwanamke ni kiumbe kilicho nyororo na hivyo ndivyo inavyobidi kumchukulia. Kwa kumdharau, kwa kutumia maneno maovu, kwa kumchukua vibaya kutasababisha uharibifu wa akili yake hapo mbeleni ingawaje kwa wakati huo haitajulikana hivyo.

Mwanamke ni kiumbe cha ajabu kwa hiyo kila utakavyomuwia vyema ndivyo atakavyokuwa na akili timamu siku za mbeleni na ukianza kuchafua akili zake, siku za mbeleni hiyo akili itaharibika na unyumba wako utaanza kuwa katika matatizo.

5.  Usimtatanishe katika matendo yake.

Usijaribu kumfaidi mwanamke kwa sababu ya udhaifu wake na maumbile yake.  Kimaumbile mwanamke ni mama na daima anapenda kuhifadhiwa na kutumika kama mama. Mara nyingi utaona tabia yake ikibadilika ikawa ya kiwakati,anatakiwa awe kama mke, hivyo usijali mambo kama hayo kwa sababu ni maumbile yake yalivyo.  Kwa hakika hana nia mbaya hivyo hakuna ubaya wowote.

6.  Usishangae juu ya furaha zake.

Maisha mazima ya mwanamke yanategemea juu ya bwana, maendeleo, afya, furaha yake n.k. Mara nyingi utaona akivutiwa na mambo mengi kama vile bwana anavyokua naye kuhusu kazi yake. Katika hali hii mambo yanatakiwa yawe ya kuzingatia vyema.

7.  Mapenzi ya mama na mtoto yasilete husuda.

Mama kwa mtoto ni muhimu sana na vile vile tutambue kuwa mtoto ni wa baba pia.  Kwa hivyo angalia kusitokee husuda baina yako na watoto wako kwa mama wa nyumba.

8.  Mawazo ya ofisini uyaachilie mbali.

Itakubidi lazima ujifunze namna ya kuacha mawazo ya ofisini mwako wakati unapowasha gari lako ili uweze kukutana na familia yako kwa uso wenye bashasha na wenye furaha. 

9.  Kwenda matembezi

Uwe mwangalifu sana wakati fulani wewe na mke wako muwe mkienda matembezi mkiwa peke yenu kutembea. Kwa mwanamke ni muhimu sana kwenda nje ya mazingara ya nyumba na jiko kwa sababu vitamletea siha nzuri na ile waka na wasiwasi vitamtoka.  Kwa wanaume wanaokaa nje ya nyumba kwa siku nzima hawawezi kutambua vile mwanamke anavyokuwa amefungiwa nyumbani kwa siku nzima kwa sababu mwanamme anapokuwa nje anaona vitu vingi tofauti tofauti, anakutana na watu wengi anafanya kazi nyingi mbalimbali kwa hiyo hahisi kama yeye yuko kama mfungwa lakini mwanamke mwenye mbio zake chumbani, sebuleni, jikoni, kwa siku nzima anahisi kuwa yeye yuko katika kifungo na kwa kumchukua nje kwa ajili ya matembezi kutaleta siha nzuri ya afya yake ya mwili na kiakili.

6.UHAKIKA  ANAOTAKIWA  BIBI KUZINGATIA.


(a) Kuwa mcheshi, kuimarisha na kufundisha. Na haya ndiyo maneno yenye busara kubwa.

(b)  Unatakiwa uwe na uhusiano wa pembe tatu.Sio pembe tatu ile ya kidunia bali pembe tatu hiyo iwe imetengenezwa kwa kona tatu pembe ya kwanza ni Allah swt, bwana wako na wewe mwenyewe.

(c)  Vita vikuu vya dunia vilivyopiganwa lau ukitaka nikwambie wapi na lini hautaipata katika ramani ya ulimwengu, ni vita vilivyopiganwa na akina mama kwa wanaume. 

(d)  Tafuta vitabu, magazeti, maprogramu na mambo ambayo yatakufanya wewe uwe mke mwema zaidi, mama mwema, rafiki bora na Mwislamu bora.

(e)  Qurani Tukufu inatuambia sura An-Nisaa, 4 : 34
"....Basi wanawake wema ni wale wenye kutii,wanaojihifadhi wasipokuwapo waume zao..."

Vile vile Qurani Tukufu inatuambia katika sura  Al-Ahzab  33 : 59
"Ewe Mtume ! Waambie wake zako,na binti zako na wanawake wa Kiislamu, wajiteremshie uzuri nguo zao."

1. Ndoa nzuri ni muujiza wa maisha.

Kwa hakika katika siku yako ya harusi akili yako inageuka kwa siku za baraka zijazo. Ndoa nzuri ni muujiza wa maisha yote. Kwa hakika wewe na bwana wako hamuwezi kujua vile maisha yenye baraka na fanaka yatakavyokuwa mbeleni.

2.  Uwe mke sio mama.

Mke mpenzi, daima uwe ni kama mke kwa bwana wako na wala usiwe kama mama yake kwa sababu bwana wako aliyekwisha kua anahitaji mke na wala si mama. Na juhudi yoyote ya kujifanya kuwa wewe ni mama mbele ya bwana wako italeta athari mbaya kuliko nzuri. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuwa mama na mke kwa mtu mmoja papo hapo kwa hivyo kwa bwana wako uwekama mke wake.  Utambue wazi kuwa bwana wako anaye mama wake na lau wewe ukitaka kujifanya kama mama yake basi ujue kuwa utakuwa ni kama mama wa kambo.

3.  Ushangilie juhudi zake wala usimbishie.

Kwa hakika mwanamme amezaliwa akiwa mjeuri, na hivyo mwanamke inambidi awe mcheshi ili kuendesha maisha yao vyema. Mwanamme amezaliwa kuongoza na inavuruga akili na kumvuruga yeye pale anapoamrishwa na mke wake atii amri za mke wake.

Mwanamke hodari ni yule ambaye anaweza kumuathiri bwana wake kwa mbinu mbali mbali kiasi kwamba bwana wake asiweze kuhisi iwapo yeye anaelekezwa au anashutumiwa au anaburutwa na mke wake.Bwana yeyote hawezi kukubali kutii amri kutoka kwa mke wake na lau akichafuka mambo yanaweza kuwa mabaya kabisa kwa hivyo mwanamke mwenye busara anajaribu kujiepusha na majanga ya maisha ya ndoa ili yasiharibike bali yaendelee vizuri na yenye mustarehe.

4.  Kuonyesha hisia.

Inambidi mwanamke amfanye bwana wake ahisi kuwa mke wake ni mtu mmoja ambaye anamjali kabisa maishani mwake.Unaweza kuwa na mawazo na matatizo mengine ya familia na watoto lakini baba watoto lazima apewe nafasi ya kwanza, kiasi kwamba asihisi kuwa yeye ametupwa,haumjali.Hivyo pamoja na kuwa na shughuli za nyumbani nyingi zilizokutinga kamwe usisahau kumjali bwana wako pale anapoondoka kwenda kazini katika harakati za kutafuta riziki, na kwa hakika mwanamke mwenye busara atamsindikiza hadi mlangoni na ataweza kumuaga vyema. Vile vile atakaporejea kutoka kazini uwe ni wakati muhimu katika maisha yako inakubidi umpokee kama shujaa na unamkaribisha kama mgeni muhimu kwako huku ukijionyesha umefurahia sana na kurudi kwake kwa moyo wako na bashasha usoni.

5.  Usimkaribishe kwa matatizo yako.

Kamwe, usianze kuongea mambo ya matatizo yako pale bwana wako anaporudi kutoka kazini. Kwa sababu bwana wako atakuwa ametoka katika vurugu za maisha matatizo na mawazo ya siku nzima yaliyokuwa yakimzonga akilini huku akiwa amerudi nyumbani ikiwa kama ni peponi hivyo bibi umkaribishe vyema na furaha.  Mkaribishe vyema ajihisi kama kweli amepata utulivu katika moyo wake na akili yake,na baadaye kadiri muda unavyokwenda  atakujali vyema.

6. Usiwe mtafuta makosa.

Kamwe usiwe mtu mwenye mzozo, usiwe mtu mwenye kuzua mizozo na katika maswala nyeti na bwana wako kamwe usiseme:“Je si nilikwambia hayo .........".

7.  Nyumba ni ngome yako usiiache.

Kamwe usiiache nyumba yako katika hali ya mzozo wowote ukaenda nyumbani kwa mama yako. Hii nyumba ni ya kwako hivyo itakubidi ufanye marekebisho kuliko kuiacha. Magomvi na mizozano yote itakuwa imepoteza makali yote siku inayofuata yaani mambo yatakwenda yanatulia kila muda utakavyokuwa unaendelea kupita.

8.  Familia ndio wajibu wako

Mwanamke aliyeelimika na kuerevuka lazima akumbuke kuwa iwapo yeye anataka familia, maisha ya kifamilia basi itambidi kujitolea mhanga ya utaalamu wake kwa sababu ya bwana wake na watoto wake yaani iwapo mwanamke ni mhandisi au mwalimu au ni mtaalam katika fani yoyote ile na iwapo anataka familia na lau itambidi abaki nyumbani kuitunza familia yake basi itambidi atoe mhanga wa utaalamu wake kwa ajili ya familia yake hiyo.  Kwa hakika kimaumbile mwanamke ni mtu mwenye kuheshimiwa na makusudi ya maisha yake ya msingi ni kuzaa watoto, kuwalea na kutengeneza nyumba yake.  Adhma yake katika maisha ni kuwa mke na mama.

9.  Uonekane mwenye kuvutia.

Daima itakubidi uwe mwenye kupendeza na kuvutia mbele ya mme wako hakuna mtu yeyote anayeweza kujigeuza au kutokujali mbele ya mwanamke anayependeza na kuvutia yaani kila mwanamme anavutiwa kwa mwanamke anapopendeza na anapovutia lau wewe hautaweza kumuweka katika mvuto wako basi utambue wazi kuwa kuna mwingine atamvutia. Itabidi tukumbuke kuwa hakuna mwanamke aliye ovyo isipokuwa huyu mwanamke hajui namna ya kujirembesha na kujifanya mwanamke mwenye kuvutia na kupendeza.

10.  Uridhike kwa kidogo.

Bwana wako anaweza kufanya kila juhudi kwa uwezo wake ili akupatie kile kilichobora kabisa. Lazima daima uwe unafikiria kuwa wewe uko katika hali ya afadhali kuliko mwanamke mwingineyo.  Kitu kikubwa, majumba ya fahari na gari ,havifanyi maisha ya bibi na bwana yakawa ya furaha na mstarehe hata kidogo isipokuwa kinachofanya nyumba ya bibi na bwana kuwa raha na mstarehe ni kule kuridhika hata kama kitakuwa ni kiasi kidogo kwa sababu tumeona kuwa kuna familia nyingine matajiri kabisa lakini hawana raha nyumbani, bibi ana njia yake na bwana ana njia yake. Pamoja na kuwa na gari, majumba ya fahari kila kitu wanacho lakini ile raha ya maisha ya ndoa hawana.  Na vile vile tumewaona watu wengine wanatoa maisha kwa tabu tabu lakini wanaishi kwa mapenzi wanapendana na humo ndimo kuna baraka za  Allah swt.Kwa sababu wote wawili wanaishi maisha ya kutosheka wanakinai. Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w. kuwa:"Asiyekinai kwa kidogo hashibi kwa kingi." Inatubidi tutosheke, turidhike kwa kile alichotupa Allah swt na hii ni neema moja kubwa ya Allah swt na wala usisikitike kwa kile usichonacho.  Daima uwe na moyo wa kusema kuwa wewe unacho kila kitu na moyo kama huu ndio utakupa maisha mazuri.

11.  Malengo ya maisha yawe kujirekebisha.

Kamwe usijaribu mawazo yako potofu yakakufanya uwe mwenye fahari mbele ya mwenzako katika maisha ya unyumba, daima uishi vile nafasi yako juu ya familia ilivyo yaani isiwe wewe mwanamke unataka kujifanya wewe ukachukua nafasi ya mwanamme katika nyumba nafasi ya mwanamme iko nafasi yake na wewe mwanamke una nafasi yako hivyo kila mtu ana cheo chake. Na hii ndiyo itahakikisha maisha yawe mema kwa sababu tunaona magomvi makubwa ndiyo hayo, bwana ataanza kusema mimi mke wangu anataka kuniendesha anataka kunitawala ananitolea amri mbali mbali mimi siwezi mwanamke kama huyu na hatima yake ni kuachana na kuishi katika hali ya  ugomvi na kutokuelewana.

12. Daima uwe ukishirikiana naye

Daima uwe mcheshi pale unapomuona ametingwa na mawazo anamzigo kwenye akili yake ambao unamzuzua. Lazima umpunguzie uzito wake mwilini pale unapoona amelemewa.Uwe ukitoa mashitaka machache sana iwezekanavyo kiasi unachoweza kupunguza upunguze katika mashitaka yako kwa bwana wako daima uwe ukitafuta njia yenye mafanikio katika kumkaribia na katika maongezi yako na yeye. Inakubidi uitengeneze nyumba iwe ni mahari ambapo kwa hakika yeye ndipo anapotaka kwenda yaani unaweza kuigeuza nyumba yako ikawa ni mahala ambapo yeye akija amechoka anakuja anaona anaweza kupumzika na akatuliza akili yake na wala usiigeuze nyumba ikawa ni mahala akija ndio kunaanza vita na ugomvi. Kwa kifupi hiyo nyumba uigeuze iwe Jannati au Jahannam uamuzi ni wako utaona utakavyoweza kufanya wewe.

13. Mfanye akufurahie.

Kwa kumtukuza ni jambo muhimu sana na kila bwana anapenda kuwa mke wake amkubalie na kukubali mambo yake,ubashasha wa mke wake na shukurani zake. Na pale utakapoona unaweza kutimiza yale mambo yaliyo moyoni mwake basi utambue wazi kuwa daima atakuwa anakupa kila kitu kilicho bora kabisa. Iwapo bibi atamtukuza bwana wake kwa hiyo bwana ataona kuwa nikitaka kufanya kitu hiki atasema hapana mke wangu ananipenda na kunitukuza hivi basi wacha nimpe kitu kilicho bora zaidi hivyo tunaona hata hawa masikini wanaokuja kuomba mitaani na majumbani,akikuona hakwambii nisaidie shilingi moja,hapana, huyo masikini kwanza ataanza kukusifu ahaa bwana habari za siku nyingi hujambo?vipi watoto nyumbani hawajambomama hajambo! ehee siku hizi vipi nasikia ulikuwa unaumwa anakuzungumzisha kidogo unafurahi baadaye kidogo anakwambia haloo bwana nina shida nisaidie senti kidogo; kwa hiyo utafikiria kuwa bwana kuliko kumpa shilingi moja huyu mtu bwana nimezungumza naye vizuri badala ya kumpa shilingi moja ngoja nimpe shilingi kumi au mia moja basi hii ndivyo ilivyo unamthamini mtu kufuatana na kauli yake,katika sura nyingine mtu mpumbavu anapokuuliza je mimi ni mpumbavu lau utamwambia kuwa wewe ndiye mpumbavu wa mwisho duniani nadhani wewe ndiye utakuwa adui wake wa mwisho na mtagombana sana. Na iwapo utamwambia kuwa nani amekuambia kuwa wewe ni mpumbavu wewe ni mtu mmoja mwerevu sana katika watu ninaowajua na ninaowaheshimu wewe mtu mmoja mwenye busara sana basi utaona pale anacheka na anafurahi na kweli kwa hakika wewe ndiye utakuwa rafiki yake sana atakuheshimu pamoja na upumbavu wake ule lakini atakuheshimu;kwa hivyo itakubidi wewe kama mwanamke ushirikiane naye katika kujenga mazingara ya nyumba hiyo yenye ndoa.

14.  Hata wapenzi wa kweli wana matatizo.

Kwa hakika hata mapenzi ya kweli hayana dhamana ya kukosa matatizo. Hata kama bibi na bwana wanapendana kiasi gani haiwezi kusemwa kuwa hakuna matatizo miongoni mwao, lakini jambo la ajabu ni kwamba wao pamoja na kuwa na makosa na matatizo miongoni mwao wameshikamana vyema na wanasonga mbele.  Na hayo ndiyo maendeleo ya kweli.

15.  Uwe mpishi bora.

Kujishughulisha na mambo ya vyakula unachukua masaa mengi kwa siku na kwa juma kuliko kazi nyingine zozote za nyumbani. Katika hali hii kuna sura mbili:

1. Ama kuchukia na kusababisha kupika chakula songa mbele.
2. Kufurahika na kazi ya mapishi na katika hali hii lau utapika mapishi kwa furaha na moyo mkunjufu basi utapika bila kuona tabu yoyote na utaweza kupika vyakula vya aina  aina ambavyo vitafurahisha nyumba nzima .
Upishi unaonekana kwamba ni jambo ambalo ni kubwa sana katika baadhi ya majumba lakini mimi ninaona upishi ni fani moja kubwa yenye kufurahisha na yenye kumchangamsha, jambo ambalo linadumu maisha.

Na kutaka kuwa mpishi mzuri au mtaalam kwanza itakubidi utambue umuhimu wake. Pili itabidi ujifunze na kutambua, na tatu inabidi utende kimatendo yaani uyapike hayo mapishi.

Je hatuelewi sisi umuhimu wa mapishi katika maisha ya ndoa ya ustarehe na yenye fanaka?  Je hayana umuhimu katika kujenga familia zinazoishi kwa raha?  Wanaume wengi sana nimewaona na kuwasikia wanapotoka majumbani mwao wanakwenda kunywa chai katika vioski na mahotelini wakati wamewaacha wake zao nyumbani wamelala usingizi mnono na mtu ambaye hana habari na kinachotendeka. Vile vile wako wanaume wengine wanaoamka na kujipikia chai yao na vitafunio.Loh!Jambo la kushutua sana na la kuaibisha.  Inawezekana mwanamke huyo haimbidi kuamuka mapema kiasi ambacho mwanamme anaamka lakini anaweza kutumia ustaarabu huo wa kuamka na kumtengenezea chai na vitafunio bwana wake anywe ashibe aende kazini akafanye kazi vizuri, na baadaye anaweza kurudi chumbani kulala au anaweza kulala mchana.  Hebu fikiria chai na kitafunio kilichotengenezwa na bibi wako mcheshi mwenye roho nzuri mwenye moyo wenye kukupenda wewe na huku akitoa maongezi matamu matamu asubuhi itakavyokusaidia wewe katika siku yako hiyo nzima na hapo ndio mwanzo wa siku kumekucha kwa ajili ya siku hiyo, bwana anatoka nyumbani amefurahi, siku nzima yake itakwenda vyema kabisa.Na bwana kama huyo ambaye amepata chai na vitafunio na maneno matamu ya mke wake jioni anaporudi anakutana na mke anamchekea vizuri anaongea naye vizuri na kukuta amepikiwa chakula chake vizuri cha jioni basi mimi hapa sina maneno ya kuelezea hali ya starehe na ya ufanisi wa maisha ya ndoa inavyokuwa.

16.  Wajibu wa mama kwa binti.

Mama anaweza kuwaathiri watoto sana katika mapishi na kazi za nyumbani.  Inawabidi akina mama wachukue muda wao katika kuwafunza binti zao kuhusu mapishi na kazi za nyumbani wafanye nao.

Akina mama watambue wazi kuwa watoto wao wanapoolewa wanapokuwa na mikono yao myeupe haimfurahishi bwana isipokuwa kazi anazozifanya nyumbani na kutunza nyumba na ule mpango na akili na moyo wa kufanya na kufanyisha kazi ndio unaopendwa na bwana kwa hiyo mwanamke ambaye hafanyi kazi na nyumba inakuwa chafu na kupika hapiki au hajui kupika basi unyumba wake unamatatizo hali hii magomvi hayawezi kuisha.Inawabidi akina mama watumie akili na busara yao kutaka kuishi maisha mema wawafundishe mabinti wao vitu hivyo ili wao pia wakienda kwa mabwana wao waweze kuishi maisha mema na mazuri.Hakuna mama anayetaka binti wake akiolewa apate taabu huko, hivyo ili kuepukana na swala hili itabidi muwafundishe mabinti wenu mapishi, kazi za nyumbani, mapenzi ya bwana na ufamilia, ili kuhakikisha maisha yao yatakwenda vizuri. Watoto wa siku hizi wanalelewa vibaya na wazazi wao na hatimaye tunaona magomvi ya familia hayaishi, na mara nyingi watoto wengine wanarudishwa kwa wazazi wao kwa sababu ya kukosa uhodari katika fani hizo. 

17.  Kufanya kazi nje ya nyumba.

Akina mama inawabidi kufanya kazi, na miaka ya nyuma walikuwa wanafanya kazi ngumu na masaa mengi. Wanawake walikuwa wakifanya kazi katika maduka madogo au mashambani. Wanawake walikuwa wakifanya kazi pamoja na mabwana zao na watoto wao wote walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja.  Kwa hivyo kila wakati alikuwa pamoja nao. Yeye alikuwa daima akipatikana pale alipokuwa akihitajika na mtoto wake aliweza kuwaacha baba na watoto dukani akaenda nyumbani kumshughulikia mtoto wake. Na kazi yake ilikuwa ni kwa mujibu wa kutaka kuishughulikia familia yake na ilikuwa ni kazi za kifamilia.
Lakini kazi za siku hizi ni kazi tofauti kabisa ni mbali na nyumba, ni mbali na bwana (na kwa kawaida kazi hizo ni pamoja na mabwana wa wanawake wengine).Na mara nyingi wanaume wanapokosa mapenzi na uvutano wa wake zao, wanaingia katika mtego wa wanawake wengine.

18. Mama anapofanyia kazi ni mbali mno na watoto. 

Kwa hivyo walezi wa watoto wanakaa wanabadilika mmoja baada ya mwingine. Kwa hiyo katika maendeleo ya mtoto hafaidiki kiasi anachotakiwa na upole na mapenzi ya mama hayapatikani pale mtoto anapokuwa mgonjwa au anapokuwa katika shida. Hali hizi kwa siku hizi ndizo zinazoleta matatizo makubwa katika familia zetu hizi. Lakini ninaona kuwa akina mama inawabidi watambue hivyo kabla ya kukubali kufanya kazi kama hiyo.Labda inawezekana wakatafuta njia nyingineyo ya kupata mapato ili hali bado wakiwa nyumbani.  Daktari Habibu Nathan kutoka Chuo kuu cha Florida amefanya utafiti juu ya matokeo ambapo mama anapomuacha mtoto wake nyumbani kabla ya kuanza shule. Yeye amegundua kuwa kuna matokeo mengi sana ambayo ni kinyume na tabia za kijamii kwa mfano udanganyifu,wizi na uporaji, kutokuwa na adabu ya kutambua baina ya usawa na ubaya, uharibifu na mara nyingi wakiwa wakijishughulisha wenyewe na miili yao.Na watoto kama hawa mara nyingi imeonekana hawapendelei kujitambulisha na wazazi wao.

Ukitaka kusoma zaidi juu ya maudhui haya,rejea sehemu ya pili ya kitabu hiki juu ya muta'.

7.  HIKI NA KILE KATIKA MAISHA YA NDOA.

Kwa vijana.

1. Uvumilivu, hisia na kijana ambaye hana uzoefu anaweza kuona kuwa anajitwisha mzigo wa matatizo ulio hafifu kuliko pale anapokuwa peke yake.Lakini ule moyo na hali wa kutaka mtu kuunganisha na mwenzake ndio siri kubwa ya maisha ya ndoa ambayo itafanya maisha hayo kuwa kama bustani ya maua mazuri ya kupendeza.

2.Katika maisha ya awali ya ndoa kunakuwa na mawazo kuhusu mapato ya familia hasa fedha za kununulia vitu vya nyumbani na gharama zinginezo. Na katika hali ya kushirikiana, maswala ya kifedha ni ya wote wawili na bibi na bwana wanaweza kuunganisha vichwa vyao kwa pamoja na kuweza kutatua maswala yao kwa pamoja yanayowazonga kimapango, kifedha n.k.Ni lazima tukumbuke kuwa mwanzoni mwa maisha ya ndoa hakuna mtu ambaye ana mapato ambayo yanaingia tu bila yeye kutafuta na kushughulikia na ni jambo la furaha mno kuona mtu anakusanya senti moja moja hadi hapo wanafanikiwa hata kujenga nyumba.Usisahau kuwa wazazi wako pia wameanza vivyo hivyo na wao kamwe hawakuwa na chochote kile wanachokihitaji pale ulipokuwa bado mdogo. Na kwa hakika ni jambo la kawaida kuwa sisi inatubidi tujue namna ya kuweka akiba na maswala ya akiba ni nyeti katika maisha ya familia ili kujenga maisha ya baadaye kwa ajili yetu na kwa ajili ya watoto wetu.

3. Katika kupunguza mawazo na mvutano wa maisha, watu wengi wanakuwa na mapenzi katika mambo fulani fulani ambayo kwa hakika hatuwezi kuelezea umuhimu wake katika maisha ya ndoa hususani mapenzi au mazoea ya tabia baina ya bibi na bwana wanaweza kushirikiana kwa pamoja. Lau tabia ya mapenzi kama hayo yataanzia katika ujana wao kwa wote pamoja kwa hakika litakuwa ni jambo  la kufurahisha mno katika miaka ya baadaye. 

Umri wa kati.

4. Katika umri wa kati bibi na bwana wanakuwa katika umri wao mzuri sana na maisha yao yanaweza kuwa maisha ya peponi. 

5. Hapo kunaanza kutokea matatizo ya watoto wanaokua lau itakumbukwa kuwa watoto ni matokeo ya ushirikiano wao na hivyo ni wajibu wa kila mmoja wao katika kuwaongoza na kuwaelekeza kwa hivyo hakutakuwa na matatizo yoyote katika umri huu na hivyo itafanya maisha yao yawe yameimarika zaidi.

6.Katika miaka ya kukua mwanamke anaweza kukabiliana na matatizo kwa sababu uzazi wake unakwisha  na mwili wake inabidi ubadilike kwa ajili ya hali hiyo. Na katika hali hii ya kipindi kifupi anaweza kujisikia mzito asiye na raha na asiyejipenda na asiyependa hata maisha kwa sababu atakuwa haoni raha katika kila hali hivyo wakati huu ndiyo utunzaji bora na mapenzi ya bwana wake ndiyo yanayoweza kumsaidia akapita kipindi hiki ingawaje na daktari anaweza kusaidia katika swala hili.

Kwa kifupi, kila mabadiliko ya mwili wa mwanadamu iwe bibi au bwana, wanatakiwa wawe tayari  kama waokozi wa mwenzao katika hali itakayo kuwa ikimghalibu mwenzao.Bibi akiona bwana anapita katika kipindi fulani anamsaidia na kumfariji na kumpa hima na vile vile bwana pia itabidi kufanya vivyo hivyo.

7. Katika umri huu wa katikati mwanamme ndio huwa yuko katika kilele cha wajibu wake kama bwana au baba akiwa kama mkuu wa familia kwa ujumla hivyo ataonekana yuko mashughuli sanakatika kutimiza malengo na mipango ya kifamilia ambayo alikuwa akiadhimia akiwa anayo adhma kutoka muda uliopita. Hivyo inambidi huyo bwana awe akitia maanani pia kuwa familia inamhitaji hata wakati huo hivyo asijisahau na kuisahau familia yake. Kuwa na uwiano sawa na shughuli na familia ndio kutaleta maendeleo mazuri katika maisha ya kifamilia, hivyo haitakuwa vyema kushindwa upande mmoja wa vita vya nyumbani kwa ajili ya upande wa pili.Kwa sababu tunaelewa vyema kuwa athari, mapenzi maongozi na maongezi ya baba katika familia kwa ajili ya watoto wake na kama bwana kwa ajili ya mke wake ni vitu ambavyo vina umuhimu sana katika familia na lau watoto watakosa vitu hivi watakuwa na hasara kubwa sana na wataathirika vibaya mno, mambo ambayo hayana suluhisho katika maisha ya mbeleni.

Miaka hii ndiyo wakati mwanamme yaani mme au akiwa kama baba anaanza kuweka msingi wa maisha ya watoto ya baadaye wakati huu ndio bwana anamalizia mipango ya kujenga nyumba kwa ajili ya mke wake, na watoto wake na wakati  huu ndio watoto wanapokuwa wamekua kidogo kwa hiyo yupo katika mipango ya kuwasomesha masomo ya juu zaidi au kuwatia katika masomo ya fani mbalimbali hivyo ndivyo vinavyomtinga kwa kipindi hiki.  Namna ya kukabili mambo hayo yote na namna ya kutimiza adhma aliyokuwa akiipangia miaka yote iliyopita. Ushirikiano wa mke na watoto kwa bwana au baba katika hali hii ni jambo moja jema kabisa ambalo litamsaidia kutimiza malengo haya kwa uzuri na vyema kabisa, bila ya kuhisi kuwa amebeba mzigo huo peke yake. 

8. Wakati huu ndio tunawaona wanawake wengi wakiwa wajane wanafiwa na mabwana zao hivyo tunawaona na tuombe kwa Allah swt asiwajaalie wake zetu kupata matatizo.

Kuna wajane wengi sana wanaozurura mitaani, wanaofanya kazi vilabuni, wajane kila mahali tunakutana nao, na hayo hawapendi kuyafanya lakini kwa sababu ya mazingara magumu wanapotoka njia zao.

Kwa ajili ya uzeeni

9.Kuna msemo wa wahenga usemao kuwa:"Mwanamke ni mzee vile aonekanavyo na mwanamme ni mzee kama vile mishipa yake inavyoonekana, ni kweli."  Kwa sababu mwanamme ni mzee kiasi kile anachokihisi yeye na kuhisi mwenyewe ni jambo moja muhimu sana katika maisha ya mwanadamu na hiyo hisia ndiyo inayobadilika kuwa jambo la ukweli linaloonekana kwa hivyo iwapo mwanamme atapendelea ajionyeshe kama kijana na akajiweka kama kijana basi atakuwa anaonekana kama kijana kabisa, na mishipa yake ya damu ya mwili iwe minyororo inawezekana kwa kuzingatia mambo ya vyakula na mazoezi.
10.Ni jambo la kawaida kwetu sisi kuona mtu ameishi miongo sita au zaidi kuwa ni mzee na mambo ambayo tunaona kuwa huyu mtu anastahili kustaafishwa hata kazini. Kwa hakika hili zoezi sio sahihi. Tusiangalie mtu ameishi miaka mingapi ili tujue uzee wake bali tuangalie ameishi namna gani, ndilo jambo lililo la muhimu mno. Tunawaona watu wengi sana wanasayansi pia na watu wanaotoa mihadhara na wataalamu katika fani mbalimbali ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa mno na kwa muda wa miaka mingi katika fani zao na wametoa michango yao katika kuiendeleza fani zao hizo ambao baada ya kupita miaka yao hiyo ya uzee sisi tunaouhesabia na bado wako wachangamfu na wakakamavu. 

Kwa hiyo kama tunasema mtu miaka sitini ndio anastaafu sio sahihi kwa sababu katika miaka hiyo sitini hatujui ni miaka mingapi amefanya kazi, kinachotakiwa kuangalia ni miaka mingapi amefanya kazi ana uwezo bado kwa sababu mimi naona mtu mwenye biashara yake kamwe hakujistaafisha katika umri huo bado anaendelea vizuri kabisa na miaka mingi itakayokuja.

11.Utafiti wa siku hizi umegundua kuwa mtu ambaye anajiweka mkakamavu kiakili na kimwili katika shughuli mbalimbali basi anakuwa amejiepusha na matatizo ya uzeeni, au hata mwisho wa maisha yake kwa ufunguo wa ujana wa milele na kuwa na nguvu ni kuendeleza shughuli katika hali yoyote ile, iwe ya kiakili au kimwili. Hivyo maisha ya ndoa ambayo yanaendelea daima ni baraka na neema kubwa ya Allah swt. Na kukua kwa watoto kusiwaletee hofu na mashaka kwa upande wao. Iwapo mtu atataka maisha yake yawe mema na mazuri zaidi atokane na tamaa ya umashuhuri,kujitakia nafasi, kutaka mamlaka au pesa kwa hakika raha ya maisha itaweza kupatikana na mwenzako ambaye ameshirikiana na wewe katika hali tofauti tofauti za maisha.

Inabidi mtu aende na maisha yake au aende na wakati mtu anapokuwa kijana anaweza kujitafutia nafasi, pesa, nguvu na umashuhuri n.k. kwa sababu ana uwezo wa kufanya mambo kama haya na anakuwa na nguvu za kukabiliana na mambo kama haya na matatizo yoyote yatakayotokana nayo na vile umri wake unavyoendelea kukua ile nguvu ya kustahimili ya kukabiliana na mambo kama hayo inapungua pia nguvu kama hizo zinapungua mwilini mwake.Hivyo yanapotokea matatizo yoyote yanamuathiri sana kiakili na kisiha mara nyingine katika hali ya uzee mtu anapata ugonjwa wa moyo,au hata kupoteza fahamu (akili) n.k.na kukosa usingizi ni mambo ya kawaida, hivyo inabidi mtu kupunguza kasi zake hizo za harakati za  ujana ili anapozeeka akili yake isiwe inaathirika ambayo itahatarisha maisha yake ya uzeeni. 

12. Lakini mara nyingine, amani na udugu kama hiyo inapotea.Kwa sababu kuna kanuni zingine zisizo za kistaarabu ambazo zimembainisha mtu kuwa ni mzee ati kufikia tarehe fulani ya kuzaliwa kuonyesha kuwa amezeeka. Na hali hii inaweza kuleta athari mbaya sana kwa mtu ambaye mpaka siku hiyo amekuwa daima akijishughulisha na gurudumu hili la maisha na ghafla anakatizwa na mpangilio wake na tabia aliyoizoea katika maisha.Lakini inaweza hali hii ikamsaidia mtu kama alikuwa ameisha jiandaa na utaratibu mwingine baada ya kuachana na utaratibu aliokuwa akiendelea nao kwa miaka mingi.Kwa sababu tumeona watu wengi waliokuwa wakifanya kazi na kuishi vizuri nje na ndani ya nyumba baada ya kustaafishwa wanaona ni mshutuko sana katika maisha wanaona maisha yanakuwa magumu hawana raha na mstarehe ndani na nje ya nyumba zao. Na katika watu kama hawa wanajiona kwamba wao hawako miongoni mwa watu kwa sababu wanakaa wanaota kila wakati ndoto za siku zilizopita na mambo yalivyokuwa mema wakati huo.  Na vile vile anaona vigumu sana kuchanganyikana na watu wengine anakosa uchangamfu na badala yake anaona afadhali abakie nyumbani tu. Hivyo kwa matokeo yake atakuwa amejipoteza kwake mwenyewe kwa familia na jumuia yake nzima kwa pamoja.Hivyo inambidi mke wake ajitayarishe katika kumtayarisha bwana wake na kumpa hima katika hali hiyo ya kustaafishwa ili kujalibu kupunguza athari mbaya baada ya kustaafu,jambo lisilozuilika. Mwanamme daima amekuwa ni mtu wa kuhisi kuwa yeye ni mkubwa na mtu ambaye ana uwezo wa kila aina katika miaka ya nyuma na lau leo atakuwa amestaafishwa hivyo katika maswala ya mapato na mambo mengineyo atakuwa amekwama na katika hali hii mwanamke (mke wake) itambidi aendelee kumtukuza na kumpa heshima vile vile alivyokuwa.Mapenzi ya mke yanahitajika sana wakati huo.Kumshutumu na kumsuta katika umri huu kwa matendo yaliyopita yana athari mbaya kabisa.Na hali hii ya bwana kuadhirika ni kwa muda mfupi tu, na lau mke wake atashirikiana naye vizuri katika kipindi hiki inaweza kuwa kipindi kifupi zaidi na katika kipindi hicho maisha yanaweza kuwa mazuri na yenye raha na fanaka bila ya kujali uzee wanaopitia.

13. Kama nilivyoelezea awali kuna mapenzi katika fani mbalimbali hasa katika umri huu wakati mtu anaona hana shughuli ya kufanya anapitia katika kipindi kigumu baada ya kustaafu kwa kustaafishwa inambidi awe na mapenzi ya jambo fulani ili kupoteza mawazo yake mfano mtu mwingine anakuwa na tabia au mapenzi ya uchoraji kuna mfano wa mtu mmoja ambaye katika miaka ya mbeleni alikuwa mchoraji, na uchoraji huu ameuanza alipokosa kazi maana mawazo yalikuwa yakimsumbua kwa hiyo akajitafutia hoja ya kujituliza kimawazo akawa mchoraji na kwa hali hii alinunua kibokisi kimoja cha rangi na brashi kidogo na makalatasi mengi na akaanza kazi ya uchoraji. Na baada ya kutayarisha vitu hivi akajiingiza katika fani hii ya uchoraji hivyo maisha yake yakawa yanaendelea vizuri bila kuharibikiwa na akili.  mambo kama haya wote tunaweza kuyafanya.

14.Imesemwa kuwa ujana wenyewe unavutia lakini bora zaidi uko pale ni kuwa na shukurani katika uzeeni.

8.  MAMBO KATIKA MAISHA YA NDOA.

1. Bibi na bwana kustiriana.

 Allah swt  anatuambia katika Qurani Tukufu  sura  Al-Baqarah, 2 :  187:
"... Wao ni (kama) nguo kwenu, na nyinyi ni kama (nguo) kwao."

Familia inaanza katika bibi na bwana wenye mpangilio wa maisha ambayo yanawaelekeza wote wawili katika njia iliyobora hapo mbeleni, tunaona katika jamii ya siku hizi kuwa kuna mapambano katika jamii zetu, baina ya Mashariki na Magharibi mawazo haya yanatofautina au tunaweza kusema kuna tofauti baina ya mawazo ya Kiislamu na mawazo dhidi ya Uislamu, kwa sababu jamii ya Kiislamu imeeleza waziwazi vile mfumo wa familia unavyotakiwa kuwapo na kwa kuwa watu wanaacha tabia na tamaduni zao za Kiisilamu na kukimbilia tamaduni za kimagharibi au zile zisizo za Kiisilamu ndipo matatizo na upotofu unapoanza hivyo ni ushauri kwa wote kwanza wazingatie mfumo wa jamii katika Uislamu ndipo hapo baadaye wajaribu kuingia katika mfumo wa kimagharibi halafu shauri lake kama atapata kupotoka au atapenda kurekebisha maisha yake ili hadi mwisho wake, yawe yenye fanaka na baraka.

2.  Kimaumbile shughuli za mwanamme na mwanamke.

Ni wazi wazi kuwa Allah swt  amemuumba mwanadamu,ana mambo mawili ya kuyafanya,
1.Kuendeleza kizazi ili kisiishe, binadamu waendelee kuzaana.
2. Kutimiza mahitaji yao.
Kwa upande mwingine tunaona Allah swt amegawanya wanadamu katika makundi mawili mwanamme na mwanamke.Naona kwa  maumbile mwanamme ameumbwa kwa ajili ya shughuli za nje za kutafuta mahitaji na kutafuta riziki kwa ajili yake na familia yake nzima wakati mwanamke hakupewa uwezo huo.  Papo hapo tunaona kimaumbile mwanamke ametengenezwa makhsusi kwa ajili ya uzazi na malezi. 

Itakuwa ni jambo lenye ugumu sana kwa mwanamme kufanya kazi za kulea na kutunza familia na kupika chakula na mambo mengineyo ambayo mwanamke anayafanya vyema zaidi na vile vile kimaumbile mwanamke inamuwia vigumu sana kufanya kazi ngumu za kupambana na maisha katika kuchuma fedha kwa ajili ya kuilisha familia yake.  Na nyanja zote hizi mbili zinapingana.

Kwa mwanamme kubaki nyumbani na kulea watoto na kutunza nyumba na usafi n.k. anaweza akachoshwa katika muda wa madakika tu na papo hapo anaweza kukumbana na maswala magumu zaidi akiwa nje ya nyumba katika kutafuta riziki na kutafuta mahitajio ya familia yake hayo mambo mazito na magumu hatayajali bali atayakabili na kuyapita, na upande mwingine mwanamke kutoka nje ya nyumba kwenda kutafuta mapato kwa ajili ya riziki na mahitajio ya familia yake ni kazi moja ngumu sana kwake kimaumbile lakini anaweza kushinda nyumbani siku nzima, akilea watoto, akifanya usafi  na mapishi n.k. bila kusikia uchungu au uchovu wowote.Hivyo mwanamme awe ni mwanamme na mwanamke abakie kuwa ni mwanamke.

3.  Faida za ndoa.

Mazungumzo yaliyotangulia yametuonyesha waziwazi katika maswala haya ya ndoa hivyo tuendelee na mazungumzo yetu kuhusu faida za ndoa ni kama ifuatavyo:-

(a)  Faida ya kwanza

Kazi anazoziweza mwanamke na zile asizoziweza mwanamke, hivyo hizo ndizo faida za mkataba wa ndoa katika mkataba wa ndoa mwanamme anachukua jukumu la kufanya shughuli fulani na mwanamke anakubali kufanya shughuli fulani.  Ili familia iweze kuishi kwa baraka, amani na fanaka. Mwanamme atatumia uwezo na nguvu zake zote katika kutafuta mapato kwa ajili yake na familia nzima na mwanamke atatimiza wajibu wake upande wa nyumbani na hivyo sehemu zote mbili zitakuwa sawia. Allah swt anatukumbusha jambo hili katika  Qurani sura  An-Nur, 24 : 32:
"...kama watakuwa mafakiri,Allah atawatajirisha katika fadhila Zake..."

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema kuwa riziki na baraka ipo pamoja na wanawake na wale wanaowategemea. "Usemi huu unasema uhakika kuwa fani ya unyumba ni uhifadhi wa mwanamke na kwa ufanisi wao katika fani hii wanaweza kufanya mapato ya mwanamme yakafika mbali sana. "

 

(b)  Faida ya pili

Pande zote mbili baada ya kuungana kwa ndoa inawabidi wahakikishe uendelezaji na ubakiaji hai wa binadamu.Ingawaje mzigo mkubwa uliomuhimu katika hatua hii upo juu ya mabega ya mwanamke, lakini haiwezekani shughuli hii ikafanyika kuanzia mwanzoni iwapo mwanamme hatashirikishwa.

Ni faida hii ambayo Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema katika Hadithi mashuhuri, "Muoe,musaidiane, mustarehe na muongeze idadi yenu."

(c)  Faida ya tatu.

Faida ya tatu ya ndoa ni kutimiza mahitajio ya hamu ya mwanadamu kwa njia zilizo za heshima (tusiwe kama wanyama tukaanza kutumia njia kama za mbwa n.k.).

Ingawaje watu wengi mara nyingine wanajaribu kutimiza mahitaji yao ya jinsia bila ya ndoa, lakini faida mbili zilizoelezwa hapo juu zitakuwa vigumu sana kuzitimiza bila ndoa, na wakati mwingine haiwezekani kabisa, kupata bila ya ndoa.  Na kwa sababu hizi ndipo hata makabila au watu wasioendelea duniani wanatimiza ndoa hawaishi bila ndoa na wanaiheshimu sana.

Na kwa sababu kama hizi na faida kama hizi ndipo Mtume s.a.w.w. amesema:  "Mtu mbaya au mtu mwenye bahati mbaya kabisa katika watu waliokufa miongoni mwenu ni yule ambaye hajaoa au hajaolewa."(Watu wengi wanasema kuwa mtu anapokufa bila kuoa au kuolewa basi hata Mwenyezi Mungu hampokei kule na katika tamaduni mbalimbali swala hili linashughulikiwa kitofauti, katika tamaduni za Wahaya mtu anapokufa bila ya kuoa au kuolewa wanamzika na mgomba ati akiwa mwanamke huo mgomba ni bwana wake na lau yeye ni mwanamke basi huo mgomba utakuwa ni mme wake kwa hivyo wanathamini sana kuoa na kuolewa lakini mazingara ya uchafuzi wa akili zetu ndizo zinazotufanya tutupilie mbali maswala ya kuoa tusiyape umuhimu, kwa sababu mafunzo ya dini tumeyaacha, mila na desturi za mababu zetu tumeziacha tumeingia katika desturi na mila za kigeni ambazo zinatupotosha ).

Hivyo labda tunaweza kuilewa Aya ya Qurani  Sura  Al-Baqarah  2: 187
"... Wao ni (kama) nguo kwenu, na nyinyi ni kama (nguo) kwao."

Kwa kutaja mavazi tunaelezwa madhumuni matatu inapendeza, inafunika sehemu za mwili na inamuhifadhi mtu kwa baridi na joto.

Bibi na bwana kwa kuungana pamoja wanajaribu kufunika maswala madogo madogo wanayokumbana nayo, na umoja huu ndio unaowahifadhi dhidi ya magumu na matatizo ya mtu anapokuwa peke yake;"nuru ya furaha na fanaka inang'ara katika maisha yao."Na wote kwa pamoja kwa juhudi zao za pamoja wanatimiza wajibu wao kama zilivyo katika sheria za kibinadamu.

9.  MIPAKA YA KIISLAMU.

Hadi sasa hivi sisi tumekuwa tukiangalia mipaka ya kikudura ya wajibu wa mwanamme na mwanamke (Yaani wajibu wa bibi na bwana).Sasa hebu tuangalie vile Uislamu unavyoweza kutuongoza katika mipaka ya Din.

Kama iliyoelezwa hapo mwanzoni kuwa Uislamu unataka kumwelimisha kijana wa kiumme ili anapokuwa awe mtu wa matendo: na kuwaelimisha wasichana ili wanapokuwa wawe malkia wa nyumba.

Hadithi hii ifuatayo itawapa mfano wa kanuni za Kiislamu. Imam Muhammad Baqir a.s. amesema: 

"Kwa hakika Fatima a.s. alichukua jukumu la wajibu wa kazi zote za nyumbani kama kusaga unga, kupika mikate, na usafi wa nyumba kwa ujumla; na Ali a.s. alichukua wajibu wa kazi zote za nje ya nyumba, kama kuleta kuni za kupikia na kuleta vitu vya kupika, n.k. "
(Biharul Anwaar, Jalada 10).

Kwa mujibu wa Hadithi hii tuliyoisoma tunaona mipaka baina ya wajibu wa bwana na bibi ni ukuta wa nyumba. Mwanamke ni mkuu katika chochote kile kilichopo katika kuta nne za nyumba na mwanamme ni mkuu katika mambo yote yaliyo nje ya kuta hizo.
Uislamu umemkomboa mwanamke dhidi ya matatizo na michafuko yote ya dunia;ili kwamba aweze kuzingatia na kutimiza wajibu wake vyema katika mambo ya unyumba.

10.  HAKI ZA MWANAMME


Qurani Tukufu imekusanya kanuni zote za maisha ya nyumbani.Kama ilivyoelezwa hapo awali kimaumbile mwanamke ni jinsia dhaifu.Kwa hivyo asitegemewe kujitia katika machachari ya kutafuta maisha;badala yake mwanamme ndivyo inavyombidi atafute kwa ajili ya wote. Iwapo nyumba ni ufalme basi mwanamme ni mfalme na mwanamke ni waziri mkuu.Aya hii inatuelezea vitu vitatu vilivyo vya hakika.Hebu tujaribu kuangalia na kuchambua :-

Allah swt amempatia mmoja zaidi kuliko mwingine; Aya hii inatuelezea vile nguvu zilivyo za mwanamme katika kumlinganisha mwanamke. 

Mwanamme na mwanamke:  Tofauti ya uwezo wao.

Ni ilimu ya kawaida na inajulikana kisayansi kuwa mwili wa mwanamke kwa wastani uko dhaifu kuliko ule wa mwanamme. Ulinganishi ufuatao utasaidia kidogo kuelezea swala hili:-

1. Moyo:

Uzito wa moyo wa mwanamme ni baina ya gramu 280 hadi 340 wakati uzito wa moyo wa mwanamke ni kutoka gramu 230 hadi 280. Ujazo wa moyo wa mwanamme anapokuwa na umri wa miaka hamsini (50) anapofikia c.c.290, wakati upande wa mwanamke kwa baadhi yao ni 50c.c yaani chini ya 50c.c. (Gray's anatomy, chapa ya 28, 1945 ; uk.  672). 

2.  Misuli.

Farid Wajid Afind (Misri ) anaandika katika kitabu chake mwanamke nguvu na uwezo wa mishipa ya mwanamke ni nusu ya ile ya mwanamme; na huo ndiyo uwiano wa vile mishipa inavyofanya kazi.

3.  Urefu.

Wastani urefu wa mwanamke upo chini ya sm 12 (kiasi cha inchi 4 3/4) kasoro ya mwanamme. 

4.  Uzito.

Kwa kawaida  wastani wa uzito wa mwanamke ni kilo 5 kasoro ya uzito wa mwanamme.

5.  Damu.

Idadi ya chembe chembe nyekundu katika mraba wa milimita ya damu ya mwanamme ni milioni 5 na mwanamke ni milioni 4 1/2.  (Gray's anatomi).

Tofauti baina ya nguvu zao.

1.Farid Wajid Afind ananakili kwa mamlaka kuwa sehemu tano za hisia za mwanadamu (kuona, kusikia, kunusa, kuonja na kugusa, ambavyo ndivyo muhimu katika kuhisi) vya mwanamke ni dhaifu kuliko vya
 mwanamme.
2. Akili, kwa wastani uzito wa akili ya ubongo wa mwanamme ni kiasi cha gramu 1380; na wa mwanamke ni kiasi cha gramu 1250 (Gray's anatomi, jalada la 28, 1945; uk. 1024) uwiano wa ubongo wa mwanamme kwa mwili wake mzima ni 1: 40; na wa mwanamke ni 1:44.

Kama tulivyoona vitu hivi vitano ndivyo vinavyofanya mwili wa mwanadamu  uwe umekamilika.
Lau vitu hivi vitano vya mwanadamu vitakuwa dhaifu basi bila ubishi tutaona kuwa huyo mwanamke ni dhaifu kabisa kimaumbile.

Farid Wajid Afind ananakili kuwa akili ya mwanamke ni kama za mtoto.  Mtoto ataanza kulia atakapokumbana na hali ya kumtatanisha; na ataanza kurukaruka na kufurahi sana anapokuwa na furaha. Na ndivyo hivyo ilivyo hali ya mwanamke ambaye ukulinganishwa na mwanamme anaathirika sana na hisia kama hizo.

Allah swt amemuumba mwanamke awe mwenye hisia kali kuliko mwanamme ni kwa sababu alivyoumbiwa yaani mama. Mwanamke anatoa maamuzi yake haraka kwa mujibu wa hisia zake bila ya kutumia busara, akili au uhodari wake.  Na labda kwa sababu hizi na undani mwa swala hili ndio maana Qurani Tukufu inachukulia ushahidi wa wanawake wawili kuwa sawa na ushahidi wa mwanamme mmoja.

Ni jambo la masikitiko sana kuona kuwa jamii zisizo za Kiislamu zimemlazimisha huyu mwanamke dhaifu kujitwisha mzigo mara dufu juu ya mabega yake, kwa kutapeli uonevu huu ati kwamba ni kushirikishwa kwa wanawake na haki zake sawa na  manaume. 

Je kushirikishwa huku kuna maanisha nini?

Mwanamke bado anahitajika kutimiza wajibu wake wa kimaumbile wa kushika mimba, kuzaa na kulea watoto.Wakati mwanamme hafanyi hivyo na wala mwanamme hawezi kushirikiana naye katika kumbebea mwanamke mimba, kunyonyesha watoto, kuwalea, au kuangalia watoto na kufanya kazi zote zinazojulikana kama kazi za akina mama; hali hii mwanamke ndiye anayebeba mzigo huu lakini pamoja na wajibu huu nyakati zote, mwanamme bado anamwambia mwanamke  "tushirikiane kutafuta mapato ya kuendesha maisha yetu."Kwa kifupi jinsia mwenye nguvu amemkomboa jinsia dhaifu katika kubeba mzigo wake bila ya yeye kumsaidia mwanamke mzigo wake  Masikini mwanamke bado anazuzuliwa kwa sauti zinazopaazwa za uhuru na ushirikishwaji wa wanawake bila ya kutambua njama na mbinu za mwanamme za kumtwisha mzigo wake.Kwa kweli sitakuwa na nafasi ya kuorodhesha maafa -kijamii,kinyumbani na kiuchumi -unaotokana na mwanamke kujiingiza katika harakati hizi za kuchuma mapesa.

11. NAFASI YA MWANAMKE NI NYUMBANI

Vyovyote vile,mwanamme amefanywa kuwa mlinzi wa mwanamke, kwa sababu ya mwili wake wenye nguvu na akili na busara yake na kwa sababu amewajibishwa kumstiri na kumshughulikia mke wake. Hivyo kwa sababu  hizi na zinginezo mwanamke amelazimishwa kumtii bwana wake.

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:"Wanawake waliotukuzwa kuliko wote mbele ya Allah swt ni wale ambao ni watiifu kwa mabwana zao na ambao wanabakia katika mipaka ya nyumba zao."

Iwapo wanawake watabakia katika mipaka yao kimaumbile na kwa kuwatii mabwana zao na kutimiza wajibu waliowekewa na Allah swt, watatimiza wajibu wao na kwa hakika ndio wale wanaostahili kuitwa wanawake wanaotukuzwa kuliko wengine.

Tunaelewa kuwa leo taasisi yoyote au kikundi chochote kiwe cha siasa au hata michezo inahitaji kiongozi. Hivyo ni jambo la kustaajabisha mno kuona kwa wale wanaotetea usawa wa jinsia (yaani usawa wa mwanamke na mwanamme) wanapokanusha kuwa mwanamme si kiongozi katika unyumba.Je nyumba inakwenda kiholela au kuna mipango inayopangwa na kutekelezwa kwa ushirikiano wa wawili hivyo kuwapo kwa kiongozi mwenye maamuzi ya mwisho ni muhimu sana hata kama itakuwa ni maswala ya nyumbani.

Wataalamu wa mambo ya kale wanasema:"Katika zama za kale mwanamke alikuwa huru alikwenda alikotaka, alifanya kile alichokitaka yaani kwa kifupi alikuwa ni bwana mwenyewe. Lakini katika zama hizo za kale alikuwa hana heshima yoyote wala utukuzo wowote, kwa sababu kulikuwa hakuna familia kila mmoja alikuwa akiishi peke yake.

Lakini familia zilipoanza kutokezea,hali ilianza kubadilika kutokezea mizunguko ya familia, mwanamke alipoteza uhuru wake na ilimbidi akubali kanuni na vishindikizo vingine vya kifamilia, lakini papo hapo alijipatia heshima na utukuzo wa hali ya juu mambo ambayo alikuwa hakuyafikiria hapo kabla.

Katika nchi za Magharibi ushirikishwaji wa mwanamke umewafanya wanawake wengi sana kuacha kuolewa, kwa kifupi mwanamke mfanyakazi wa nchi za Magharibi amepoteza ile hali na matamanio ambayo mwanamke kimaumbile wa umri wao anatakiwa awe nayo. Kwa sasa wao si wanaume wala wanawake kwani wao ni kikundi cha katikati baina ya mwanamme (yaani si mwanamume wala si mwanamke ). Wao si wanaume kwa sababu wanatofautina kimaumbile na wala wao sio wanawake kwa sababu hisia zao, mawazo yao  na shughuli zao zinatofautiana na zile za mwanamke.

Mtu hawezi kupanda jahazi mbili kwa wakati mmoja hivyo lau yeye atajiingiza katika mambo ya kuchuma mapesa basi watoto wake watanyimwa haki yao ya mapenzi ya utunzwaji wa mama.

12.  UBORA WA MWANAMME.

Kama tulivyoona mapema wazazi ni mabwana wa watoto.Hadi hapo vijana wanaume wanapohusika sheria hii inaendelea.Ama wasichana,baada ya kuolewa ubwana wa wazazi wao unakwisha na wao wanaingia chini ya hukumu za mabwana wao.

Mwanamke mmoja alimwuliza Mtume s.a.w.w.:"Ewe Mtume wa Allah swt, je ni nani anayo haki zaidi juu ya mwanamme?"Mtume s.a.w.w.alimjibu:  "Wazazi wake."Baadaye alimuuliza:"Je nani mwenye haki zaidi juu ya mwanamke?" Mtume s.a.w.w. alimjibu:  "Bwana wake."

Wakati mmoja walimwuliza Mtume s.a.w.w.:"Sisi tunawaona baadhi ya watu wakiwasujudia baadhi ya watu wao." Mtume s.a.w.w.aliwajibu:"Iwapo mimi ningekuwa na uwezo wa kumruhusu mtu yeyote kumsujudia mtu mwingine basi ningemwamurisha mwanamke amsujudie bwana wake."

Imam Jaafer Sadique a.s. amesema: "Allah swt alimtumia ujumbe Mtume s.a.w.w., mwambie Fatima a.s. daima amtii Ali a.s. kwa sababu iwapo Ali a.s. hataridhishwa, basi mimi sitaridhishwa."

Na kwa sababu hii ndiyo maana Mtume s.a.w.w.alimwambia Fatima  a.s. :-
"Ewe Fatima, iwapo mwanamke atafanya ibada ya Allah swt kwa miaka sabini lakini atakufa  katika hali ya kutomtii bwana wake (na bwana wake atakuwa  hakufurahishwa naye ), basi mwanamke huyo atakuwa miongoni mwa  wakazi wa Jahannam."

13.  UTIIFU  KWA  MISINGI  YA MAPENZI.


Itatubidi lazima tukumbuke sheria iliyo ya uchokozi na udhalimu, kamwe hawezi kuwa sahihi. Hivyo misingi ya mamlaka ya bwana yamewekwa kwa mapenzi na wala sio vitisho na uonevu. Allah swt anatuambia katika Qurani Tukufu sura  Ar-Rum  30:21
"..... naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu..."

Katika Aya hii tunaona maneno mawili mapenzi na huruma,yametumika katika mapenzi ya unyumba.Kwa kawaida mwanamke tukiongelea ukweli anampenda bwana wake zaidi mno. Yeye yuko tayari, kujitolea  nafsi ,mwili wake kwa ajili ya mume  wake. Hivyo mapenzi ndivyo yanavyotelezea hali hiyo.

Kwa upande mwingine mapenzi ya mwanamme kwa mke wake yana sura tofauti kimaumbile - hapo hakuna swala la kujitolea. Na hivyo ndivyo huruma inavyotumika.

Vyovyote vile mapenzi, utiifu na huruma ndio mambo ya kutimiza katika maisha ya mwanadamu: Kudhatiti mambo ya nyumbani na uzazi.

14.  KUDHIBITI MAMBO YA NYUMBANI.

Kwanza kabisa ni muhimu kuwa mwanamke aweze kuweka maanani mapato ya bwana wake kuliko dunia nzima.

Ndipo hapo itambidi aweze kuweka malengo ya matumizi katika misingi hiyo.  Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Allah swt atamjalia nguo sabini elfu huko Jannah yule mke ambaye atakuwa ameridhika kwa kiasi cha mapato mume wake anachokipata kwa uwezo wake."

Kwa wale wanaokwenda kinyume na busara hii,Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: -
"Hakuna mwanamke ambaye anamuomba mume wake zaidi ya uwezo wake, na asiyetosheka kwa  kile anachopata  cha kuishi - kiwe kidogo au zaidi - wala kutosheka na neema anayojaliwa na Allah swt, isipokuwa atakuwa ni miongoni mwa wale ambao matendo yao mema hayakubaliwi, na madhambi yao hayatasamehewa na Allah swt atakuwa daima akiwachukia hadi hapo hao wanawake watakapotubu."

Ni ukweli kwamba matatizo ya kinyumbani yanamchukiza mtu sana kiasi cha kwamba wakati fulani hata subira yake inashindikana, ni kwa sababu hii kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w.ameahidi baraka kwa watu wenye maswala kama hayo, amesema: -

Iwapo mwanamke atatokwa na machozi wakati wa kupika kwa sababu ya moshi, Allah swt atamwandikia thawabu za shahidi  (waliouawa katika njia ya Allah swt)  ambao macho yaoyanatokwa na machozi kwa hofu ya Allah swt.

Na iwapo mwanamke huyo anaye msaidizi katika mambo ya nyumbani na hivyo anapata fursa kidogo basi asiupoteze huo wakati; badala yake, muda huo utumike katika shughuli zingine zenye manufaa katika mipaka yake ya nyumbani.Mtume Mtukufu s.a.w.w.amesema:"Kazi nzuri kabisa ya mwanamke ni ufumaji; kwa sababu kwa kila uzi mmoja anasamehewa dhambi moja na kupewa thawabu moja."

Mwanamke amevutiwa katika utunzaji wa nyumba bora katika maneno yafuatayo:- 
"Mwanamke yeyote katika nyumba ya mme wake, anapohamisha kitu kutoka nafasi moja hadi nafasi ya pili kwa nia njema, Allah swt anamwangalia (kwa baraka), na yeyote yule anayetazamwa na Allah swt kwa rehema, basi kamwe haadhibiwi."

Kwa hivyo tunaona katika maswala ya nyumbani mwanamke inambidi aangalie mambo yote mazuri kwa nia njema ya kuendeleza nyumba ya bwana wake na anayekuwa na nia mbaya ya kusema anachukua vitu nje ya nyumba yake bila ya bwana wake kujua kwa nia mbaya basi huyo naye atapata adhabu za  Allah swt.

15.  UZAZI.


Uendelezaji wa binadamu na asili ya kuwapo kwake na kwa ujumla ni wajibu wa kila aina, vyote viko pamoja na mwanamke. 

Kwa hakika mwanamke amebarikiwa jambo hilo, yeye anatimiza wajibu wake kwa binadamu kwa ujumla.

Uislamu haujapitiwa vile mwanamke anavyobeba mzigo huu na maswala kama hayo katika jambo hili. Uislam umemuahidi thawabu kubwa kabisa na rehema na baraka za kila aina katika jambo hili gumu kabisa. Mwanamke inambidi apitie hatua nne katika swala hili, kwanza kushika mimba;pili kuzaa  tatu kunyonyesha na nne uleaji malezi bora ya watoto.

Mwanamke anapata thawabu za kudumu katika kila hatua hizi, na kwa mujibu wa Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

Hatua ya kwanza
"Wakati mwanamke anaposhika mimba, katika kipindi hicho ni sawa na yule anayefunga saumu daima,anayesali  na anayepigana Jihad  kwa nafsi na kwa mali yake katika njia ya Allah  swt."

Hatua ya pili:  
"Wakati mwanamke anapozaa, anapata thawabu kupita kiasi kwamba hatuwezi kuzielezea kwa sababu ya tendo hili jema."

Hatua ya tatu: 
"Wakati mwanamke anapomnyonyesha mtoto wake maziwa, Allah swt anamjalia thawabu sawa na kumfanya huru mtumwa  (kutoka kizazi cha Mtume Ismail a.s. ) kwa kila mara anaponyonyesha."

Hatua ya nne: 
"Uleaji wa watoto - swala hili linazungumziwa zaidi katika maswala ya haki za watoto."

Taarifa ifuatayo kutoka Hadithi tukufu lazima isomwe kwa uangalifu sana:  "Mtume Mtukufu s.a.w.w. alimwambia binti yake, Bi. Fatima a.s. :-

"Ewe Fatima mwanamke asimletee chochote kile mbele ya bwana wake asichokipenda; daima awe mtunzi muhifadhi wake; lazima awe mkweli na mtiifu mbele na anapokuwa hayupo; aukate (ukali na majeraha) ya ulimi wake (dhidi ya bwana wake); amtazame vyema pale anapohitajika bwana wake kutazamwa na kutunzwa; amtimizie mahitaji yake yote na daima aangalie ahali yake; kwa sababu kumtazama bwana wake ni ibada; na kamwe asimkaribishe mtu katika chakula isipokuwa napokuwa ameruhusiwa na bwana wake; na daima mwanamke awe akiridhika na kile alichojaaliwa na Allah swt; na kamwe asimwache bwana wake, na kama atamwachia, basi sala zake, saum na zaka hazitakubaliwa na Allah swt hadi hapo bwana wake atakapokuwa  amemridhia."

16.  HAKI ZA MKE.


Quran Tukufu inafafanua misemo ya kuwazulia Waislamu juu ya utumwa wa wanawake katika Islam swala ambalo wanamagharibi waliomajahili ndio wanaotumia kama silaha dhidi ya Waislamu.Ilikuwa ni dharura katika kuimarisha na kudhibiti hali bora ya nyumbani ili kumdhatiti mwanamme katika mamlaka sawa sawa juu ya wanawake. Na Aya hiyo ya Qurani ndivyo inavyofanyia ishara juu yake. Mbali na haya sehemu zote mbili yaani bibi na bwana wamepewa haki zilizo sawia.  Kila sehemu wamepata nusu sawa sawa.

Kama iliyoelezwa hapo awali kwa mujibu wa akili na kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, mwanamme ndiye anayewajibika kwa ajili ya kumgharimia na kumtafutia mahitaji yote ya mke wake, na katika mtazamo huu wa uwajibikaji ambao upo katika mapenzi.

Inaonekana kutoka juu kuwa chochote kile anachotaka mwanamke kwa ajili ya utulivu wa akili yake kuwa bora kiroho, na kuridhika na mahitajio yake, vinaweza kutenganishwa katika makundi mawili:
1.  Mapenzi halisi.
2.  Kutizamwa vyema.
Lau mtu atakaa kupitia orodha ya madai ya wale wenye kutetea ukombozi wa wanawake, basi utagundua kuwa haki hizo zote ambazo zinakubaliana kiakili utaona yako katika makundi haya mawili.

Islam imewaamrisha kwa kuwasisitiza wanaume kuwapa uhuru wake zao kufurahi haki zao bila ya kubugudhiwa vyovyote vile. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:  
"Mwanamke yeyote atakayembughudhi mume wake kwa ulimi wake....atakuwa ni wa kwanza kuingizwa Jahanam. Na, vivyo hivyo, iwapo bwana wake hatamfanyia haki."

Mapenzi na baraka.

Imam Jaafer Sadiq  a.s. amesema:
 "Mimi nina uhakika kuwa mtu anapokuwa bora zaidi katika imani na Islam basi vivyo hivyo ndivyo mapenzi ya wake zake inavyozidi."

Aya isemayo:  Allah swt ameweka mapenzi na huruma baina yenu, inaonyesha kuwa mapenzi ya kindoa ni baraka za Allah swt; na vile mtu atakavyokuwa na imani zaidi katika Allah swt, na ndivyo vivyo hivyo rehema na baraka zaidi za Allah swt zitakuwa juu ya jozi hiyo (yaani bibi na bwana ).

Na kwa sababu hii Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:”Miongoni mwa desturi za Mitume ni mapenzi ya wanawake."

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema, "Ijulikane mtu bora miongoni mwenu ni yule ambaye ni bora kwa wake zake na mimi ni bora kwa wake zangu."

Vivyo hivyo ,ameendelea kusema: "Rehema na baraka za Allah swt ziwe juu ya mtumwa wake ambaye anawafanyia wema baina yake na mke wake kwa hakika, Allah swt amempa mamlaka zaidi juu ya mke wake na kwamba amemfanya awe ni mtu mwenye kumhifadhi mke wake."

Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, imesisitizwa kuwa mwanamme anapokuja nyumbani aje na uso wenye bashasha, mchangamfu. Nyumba hiyo itakuwa ni Jannah iwapo sheria kama hizi zitafuatwa kwa makini.

Haki za kutimiza

Katika aya za Qurani Allah swt anawaambia wanaume kuwatendea wema wake zao. Mbali na aya hiyo ya hapo juu ipo aya nyingine inayosema: "Qurani,sura An-Nisaa, 4 : 19   "...Na kaeni nao kwa wema ..."

Kuwatendea wema kwa mujibu wa Hadithi inamaanisha kuwa kile ambacho atapatiwa mwanamke, kwa kiasi kinachowezekana, hali na desturi alivyokuwa akiishi katika majumba ya wazazi wake; ili kwamba asipate kukabiliana na hali ya kutoishi kwa raha na vile vile asipate ugumu wa kupata magonjwa ya akili kwa sababu ya kukosa raha katika majumba ya mabwana zao.

Na iwapo bwana, kwa sababu za uchumi wake kuwa kiasi,anashindwa kumpatia hali hiyo bora basi hawezi kulaumiwa. 

Qurani Tukufu inatuambia katika sura Al-Baqarah  2 : 236
"... Mwenye wasaa kadiri awezavyo,na mwenye dhiki kadiri awezavyo..."

Imam Jaafer Sadiq a.s. anatuambia: "Wale wote wanaomtengemea bwana ni wafungwa wake, na mtumwa wa Allah swt aliyebora kuliko wote mbele ya macho ya Allah swt ni yule ambaye anawatendea wema wafungwa wake."

Vivyo hivyo Imam Musa al-Kadhim a.s amesema:"Wale wote wanaomtegemea mwanamme ni watumwa wake. Kwa hivyo iwapo Allah swt anamjalia baraka zake mtu yeyote, basi itambidi na yeye aitumie zaidi kwa ajili ya wafungwa wake; na lau hatafanya hivyo, basi neema na baraka hiyo itatoweka.

Kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, malipo, matumizi au posho ya mwanamke ni malipo ya utiifu wake. Iwapo huyo mwanamke hamkatalii mume wake haki zake, basi ana haki zake zote za kuruzukiwa.Iwapo bwana, kwa sababu ya matatizo yake ya kiuchumi, anashindwa kumtimizia posho na ruzuku za mke wake, basi atabakia na deni hilo akidaiwa na mke wake; na hivyo itambidi kumlipa mara moja pale apatapo mapesa n.k.Kwa kifupi kumtimizia mwanamke haja zake ni juu ya misingi nipe na nikupe, na mwanamme itambidi alipe kwa hali yoyote ile.Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:  "Amelaaniwa yule mwanamme ambaye hawajali wale wanaomtegemea."

17.  USAMEHEVU.


Kama iliyoelezwa hapo awali, hisia za mwanamke ndizo zinazotawala akili zao. Iwapo msichana hatakuwa amelelewa vyema kwa mujibu wa desturi na tamaduni za Kiislamu, basi kuna uwezekano mkubwa sana kuwa atakuwa ni msichana mwenye hasira na ulimi mkali.

Kwa upande mwingine mwanamme sio wa desturi hiyo kwa hivyo, Uislamu umemfaradhia mtu awe na subira na usamehevu wakati wa hasira za mke wake.Inambidi mwanamme amvumilie mke wake kwa kuweka maanani udhaifu wake na kwa kukumbuka kuwa mwanamke anatawaliwa na hisia zake.

Allah swt anatuambia katika Qurani tukufu sura  An-Nisaa  4 :19
"... na kaeni nao kwa wema..."
Hatuwezi kukanusha kuwa kazi hii ya kupewa ni ngumu sana na wakati mwingine inataka subira nyingi sana.

Allah swt anatuambia katika Qurani sura  Al-Baqarah  2 : 201
"... Mola wetu! Tupe mema duniani na mema Aakhera,na utulinde na  adhabu ya Moto."

Miongoni mwa ufafanuzi zaidi wa aya hii, Imam Amir -al- Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:
"Mema katika dunia hii inamaanisha mwanamke mwenye silka nzuri,na mema katika Aakhera inamaanisha hurul-ain na adhabu za moto inamaanisha mwanamke mwenye silka mbaya." (Tafsiri -Safi ).

Kusema kwa mwanamke mwenye tabia, silka na desturi mbaya, mke mwenye hasira kali ni adhabu ya motoni inawakilisha uhakika kwa njia inayowezekana.  Lakini inatubidi sisi pia tuwe tukiitazama hii Hadith:-

"Kwa hakika Mtume Ibrahimu a.s. alimlalamikia Allah swt dhidi ya hasira za mke wake Sarah. Hapo Allah swt alimtumia ujumbe ukimwambia kuwa kwa hakika mfano wa mwanamke ni mfano wa ubavu;iwapo utajaribu kuunyoosha utavunjika; na lau iwapo utauachia ubavu wako ulivyo basi utafaidika nao."

Kwa kifupi aya nyingi mno za Qurani tukufu na Hadith nyingi mno zinatuusia, zinatuamrisha kuwa muugano wa bibi na bwana uimarishe na kufanya madhubuti mapenzi yao na umoja wao kiasi wanapokuwa wameungana kindoa, hata kama itabidi mmoja ajinyime kiasi fulani na vile vile kujaza kwa subira inayozidi uwezo wa mtu mwenyewe. Na kwa kufuata kwa kanuni kama hizi ndipo wanadamu wataweza kufaidi matunda ya amani humu humu duniani  vile vile Aakhera.

18.  KUTOKUELEWANA  NA MAGOMVI.


Uislamu unatambua waziwazi kuwa hii njia ya kubuni mambo tu haisaidii kuwa mema. Isipokuwa kanuni zinazotumika na desturi miongoni mwa bibi na bwana ndizo zinazoleta amani katika nyumba.Hotuba kubwa kubwa hazitamsaidia mtu wa kawaida iwapo hayatakuwa kwa mujibu wa akili na vile vile lau hazitakuwa katika uwezo wake.

Ndoa bora za Kiislamu ni zile ambazo bibi na bwana wanapendana na wanaheshimiana na kila mmoja kuheshimu haki za mwenzake.

Lakini dunia hii haipo na watu wacha mungu na wenye kufahamu tu bali imejaa zaidi kwa watu wenye mioyo migumu na wanawake wa aina hizo; wao hawajali uharibifu wanaouleta katika jamii ya Kiislamu kwa sababu ya matendo yao na kuchezea maamrisho ya Sharia za Kiislamu. Hivyo ilikuwa ni lazima kutengenezwa Sharia ili kurekebisha desturi zao.

Kwa nini ugomvi.

Chanzo kikuu cha magomvi ni kupuuzia kwa wajibu wa mtu mmoja kwa ajili ya mwenzake.Dharau hiyo inawezekana ni upande wa bwana au upande wa mke, au pande zote mbili. Islam kwa kuzingatia maswala nyeti kama hayo imeweka Sharia kwa kila hali itakavyotokezea.

Wakati mke anapokuwa na hatia.

Iwapo mke ataacha wajibu wake na kumsumbua bwana wake, basi Allah swt  anaelezea laana za aina tatu kwa ajili yake, katika sura   An-Nisaa  4 : 34
"... Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu waonyeni na waacheni peke yao katika vitanda na wapigeni"

Hatua ya kwanza: 
"Itambidi kwanza bwana ajaribu kumuelimisha mke wake na kumshauri abadilishe desturi ya tabia zake. Mwanzoni nasiha na majadiliano baina yao inaweza kuleta matunda mazuri,wakati ambapo hatua kali zikichukuliwa zinaweza kuleta mwelekeo ulio mgumu zaidi."

Hatua ya pili: 
"Iwapo hilo litashindikana, inamaanisha kuwa ugonjwa huo umechukua mizizi ndani zaidi.Hivyo itambidi bwana amwache mwanamke huyo kitandani mwake.Inawezekana mgomo huu baridi ukamrudishia mwanamke huyo akili zake; na akajirudia na ugomvi ukaisha."

Hatua ya tatu: 
"Lakini, iwapo upuuzaji wake huo umezidi, na mawaidha, nasiha na mgomo wako huo haukumuathiri, basi matibabu madogo hayawezi kuwa na faida yoyote.  Katika hali ya kuzidi kabisakama hii, bwana ana ruhusa ya kumpiga mke wake. Kuna msemo usemao iwapo hatua nzuri zitashindwa kuamsha hisia nzuri za mwanamke, kinachobakia ni kumwijia kwa mabavu."

Lakini kumwijia kwa mabavu huko lazima kuwe ni kwenye hali nzuri na nidhamu bora.  Imam Muhammad Baqir a.s. amesema: 
"Kwa hakika, mjeledi kwa mswaki wa meno. Sharia inasema kuwa isiwe unampiga ngumi kiasi cha kuvunja mfupa au kuacha doa jekundu au michubuko, na kamwe mwanamme haruhusiwi kumpiga usoni mwanamke, na wala mahala pamoja kupigwa mara nyingi."

Iwapo matibabu haya yataondoa sababu za ugomvi, basi inambidi mwanamme (bwana ) amwie kwa wema na atimize haki zake zote kwa mara moja.Lau katika hali hii ya ugomvi na kujaribu kumrudisha mke katika hali yake akaomba msamaha na akatubu kosa lake basi inambidi mwanamme na hasira zake na ugomvi uishie pale pale, na mrudishie haki zote za mwanamke anazostahili yaani mapenzi, haki na mambo mengine yote kama tulivyokwisha kuelezwa hapo nyuma. Sentensi ya mwisho ya Aya ya hapo juu inatuambia hivi: 
( baadaye, wanaporudi katika utiifu, basi  usiwatendee tena hasira).
"... Na kama wanakutiini msiwatafutie njia ( ya kuwaudhi bure)."

Wakati mwanamme anapokuwa katika hatia.

Na iwapo kwa upande mwingine bwana ndiye yuko katika makosa na amepuuzia wajibu wake kwa mke wake, basi mwanamke itambidi kwanza ajaribu kuleta uelewano baina yao

Allah swt anatuambia katika Qurani tukufu katika sura  An-Nisaa  4:128
"... Na kama mke akiona kwa mume wake kugombanagombana na kutenganatengana,basi si vibaya kwao wakitengeneze baina yao sulhu...."

Na iwapo njia hii haitawezekana kuleta matunda mazuri basi mwanamke ana haki ya kuchukua mashitaka yake mbele ya Hakim-i-Sharia (kadhi au mujtahid ) ambaye ana mamlaka ya kila aina katika usuluhishi wa mfarakano kwa mujibu wa Sharia na maadili.

Bibi na bwana wanapokuwa na hatia.

Iwapo bibi na bwana watapuuzia haki zao, basi hapo kwa kweli kuna haja ya msaada wa mtu mwingine ili kumaliza mzozo wao. Hivyo Allah swt ametuamrisha katika Qurani tukufu sura An-Nisaa  4:35

"... Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basi pelekeni, mwamuzi mmoja katika jamaa za mwanamme, mmoja katika jamaa za mwanamke."

Uadilifu na maamuzi kama haya yanaweza kufikiwa katika hali mbili zilizotangulia pia, wakati mmoja tu anapokuwa katika hatia.

19.  MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.


1.Si haramu kusuhubiana na mke anapokuwa na mimbalakini iwapo kutakuwa na hatari kwake yeye au mtoto aliye tumboni,basi katika hali hii itakuwa ni haraam kusuhubiana.Hata hivyo wataalamu wanapinga kusuhubiana wakati  mwanamke anapokuwa na mimba.

2.Wazee waliwauliza Maulamaa iwapo watoto watazaliwa vile yalivyoelezwa hapo awali,lakini walijibu kuwa hayo yote yapo mikononi mwa Allah swt.

3.Maelezo yote yalivyoelezwa kama ni makruh (karaha) basi yachukuliwe ni karaha na kama yameelezwa kuwa ni haramu basi yachukuliwe vile vile ilivyo hukumu za haramu.Ni mwiko kubadilisha haram kuwa makruh!

4.Iwapo mwanamke alikuwa katika hali ya janaba na hakuwahi kuoga ghusl-i-janaba  na akaingia katika haidh,au baada ya kutoka haidh lakini kabla ya kufanya ghusli Haidh akaingia janaba(akatakiwa kufanya ghusli janaba) yaani anatakiwa kufanya ghusli zote mbili :Janaba na Haidh .Katika swala hili hatakiwi kufanya ghusli mbili mbalimbali isipokuwa atafanya nia moja tu ambayo itafaa kwa ghusli zote mbili.

5.Kutoa manii kwa mkono ni haraam na vile vile madaktari pia wanapinga mno kwani kunadhoofisha uwezo wa mtu na hatimaye kupoteza nguvu za kiume.

6.Kuingilia kwa njia ya  nyuma ni haramu na ni yenye madhara makubwa sana.

7.Kutalazimika kufanya ghusl-i-janaba iwapo kutatokwa na manii kwa njia yoyote ile ya kutumia mkono,kusuhubiana au kuingilia kwa sehemu ya nyuma au katika usingizi.

8.Iwapo mtu ataota ndoto ya kusuhubiana na mwanamke lakini hakutokwa na manii,basi halazimiki kufanya ghusl-i-janaba.

9.Ni lazima  kusuhubiana mara moja katika miezi minne lakini ni sharti kuwa kusiwepo na udhri wowote wa kisheria wala asiwe amekwenda safarini.

10.Ni swala mashuhuri miongoni mwa Maulamaa kuwa usiku saba ni makhsusi kwa ajili ya mwanamke aliyeolewa bikira na usiku  tatu kwa mwanamke asiye bikira.

11.Ni hukumu kwa ajili ya wanaume kutoziweka nywele za sehemu zao za siri kwa zaidi ya siku arobaini (na wazikate kabla  ya siku hizo) na wanawake wasiziweke zaidi ya siku ishirini (na wazikate kabla ya siku hizo). Ipo riwaya ya Imam Jaafer as-Sadiq a.s. isemayo:"Msiziweke nywele zenu za sehemu zenu za mwili zinazotakiwa kukatwa i.e.mashurubu, kwapani ,na sehemu za siri,na muziondoe kwa kutumia nurah.

12.Kuna faida mno kusuhubiana na mwanamke ambaye ametoka katika haidh na ameoga  ghusl-i-haidh.

13.Wapinzani wa swala hilo juu wanasema ni vyema kujiepusha na mwanamke ambaye ametoka haidh kwa siku kumi ambavyo hatapata udhaifu na siku ishirini zilizobakia  ni nzuri ambamo siku kumi za katikati ndizo nzuri mno.

14.Imeruhusiwa kumwoa msichana mdogo,lakini iwapo hatakuwa ametimiza umri wa miaka tisa au kuzidi basi ni  haraam kusuhubiana naye.

15.Iwapo mwanamme atamwoa msichana asiyefikia au kutimiza umri wa miaka tisa na akasuhubiana naye basi atambue kuwa ametenda tendo la dhambi na iwapo amemjeruhi katika sehemu zake za siri yaani iwapo sehemu ya kike kuungana na sehemu ya haja ndogo au sehemu ya kike kuungana na sehemu ya choo (njia ya nyuma) basi atambue kuwa huyo mwanamke atakuwa haraam kwake yeye kwa umri mzima.Lakini Maulamaa wanasema kuwa nikah (ndoa) haivunjiki kwa hivyo  kamwe hataweza kusuhubiana naye kwani atakuwa haraam kwake kusuhubiana naye.Na iwapo hali kama hiyo itatokea kwa mke wake ambaye amekwisha timiza umri wa miaka tisa au zaidi basi hatakuwa haraam kusuhubiana naye.

16.Mtu hawezi kumwoa dada wa mke wake aliye bado hai na iwapo atathubutu kufanya hivyo (yaani kuwaoa dada wawili wakiwa ni wake zake wawili) basi ni dhambi na nikah hiyo itakuwa batil na watoto watakaozaliwa watakuwa ni waladuz-zinaa.

17.Iwapo mwanamme atasuhubiana na mwanamke aliye na bwana ambaye yu hai au mwanamke ambaye hakumaliza kipindi chake cha Iddah basi kamwe hataweza kumwoa huyo mwanamke mbeleni.

18.Iwapo mtu alisuhubiana na mwanamke asiye na bwana (ingawaje ni dhambi la zinaa aliyojipatia)  lakini iwapo atataka kumwoa,basi anaweza.

19.Iwapo mwanamke (mwenye bwana) atafanya zinaa na bwana mwingine nje ya ndoa yake au mwanamme (mwenye mke) atafanya zinaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa yake basi wote wanakabiliwa na adhabau ya kukalishwa shimoni na kupigwa mawe hadi kufa. Na iwapo ni mwanamke asiye na bwana au mwanamme asiye na mke basi watachapwa viboko mia moja.

20.Iwapo ni mwanamke  aliyepewa talaqa basi hakuna mtu atakayeruhusiwa kumwoa kabla hajamaliza kipindi chake cha Iddah na iwapo mtu yeyote atathubutu kufanya hivyo,basi mwenye kuoa, kuolewa na wote walioshiriki katika kufanikisha hivyo wanalaaniwa na Allah swt na wanajitafutia adhabu zake. Na iwapo watasuhubiana basi hiyo ni zinaa na mtoto akizaliwa atakuwawaladuz-zinaa na atambue waziwazi kuwa kamwe hawezi kumwoa hata kama atataka hivyo.

21.Iwapo mwanamme atafanya tendo la kubaka (atamwingilia kwa nguvu) mwanamke basi atambue waziwazi kuwa kamwe hawezi kumwoa (aliyebaka) huyo mwanamke wala hawezi kumwoa mama,dada na binti yake.

22.Mwanamme atakaye kuwa amempa mke wake talaqa tisa kwa mujibu wa Shariah,basi atakuwa haraam kwake daima.

23.Iwapo mwanamme atakuwa amesuhubiana na wifiau shanghazi yake,basi hawezi kuwaoa mabinti  wao (watoto wa shanghazi na watoto wa wifi) .

24.Iwapo kutakuwa na mume ambaye ameishi na mwanamke kwa kipindi cha miaka thelathini au hamsini au hata zaidi ya hayo lakini kwa ndoa ya muda  (muta') na atakapokufa mmoja wao basi hakuna atakayemrithi mwenzake.

25.Haki ya urithi wa kutoka mali ya baba  kwa ajili ya watoto itakuwa sawa kabisa kwa mujibu wa Shariah za Dini iwapo watakuwa wamezaliwa na mama aliyeolewa kwa ndoa kamili,au ndoa ya muda au amezaliwa na kijakazi wa baba yake.

26.Iwapo mwanamme  atampa mke wake talaqa,basi itabidi ishuhudiwe na waadilifu wawili ndipo hapo sigha hiyo itakaposomwa na nikah ya mwanamke haivunjiki hapo hadi mwanamke huyo kutimiza kipindi cha Iddah yake (ndipo hapo atakapokuwa huru kuolewa) na iwapo ataolewa,basi ndoa hiyo itakuwa haraam na  iwapo watasuhubiana basi hilo ni tendo la zinaa.Hata hivyo siku hizi kuna mtindo wa kupeana talaqa za haraka haraka ilimradi mmojawapo anataka kuoa mwingine basi atafanya kila aina ya hila ya kujifanyia njia saheli ili mradi afanikiwe katika adhma yake,lakini ikumbukwe wazi kuwa iwapo Shariah za dini ya Islam kama hazikufuatwa na kutimizwa basi mambo yote yatakuwa ni haraam.Kutoa na kupewa talaqa kuna masharti maalum na yenye msimamo na mipangilio yake.

27.Iwapo bibi na bwana walikuwa mushrik na wote kwa pamoja wakawa Waislaam,basi ndoa yao itahala­lika na kuwa ya daima lakini iwapo mmoja wao atakuwa Mwislaam na baada ya kupita kipindi cha Iddah hawi  Mwislaam basi nikah inavunjika na haitawezekana kamwe hadi awe Mwislam.

28.Iwapo bwana atakuwa Mumiin na mke akiwa mushrik,na iwapo mke hatabadilisha imani yake (akawa Mwislam) basi itakuwa ni swala kama la hapo juu kwani huyo bibi hatakuwa mke halali wala bwana hatakuwa halali kisharia.Kwa kifupi  wote wanakuwa wametoka katika nikah.

29.Iwapo mke atakuwa Mumiin na bwana atakuwa mushrik,basi hukumu yake ni kama ilivyozungumzwa hapo juu katika na.28,yaaniuhusiano wao unakuwa umevunjika kindoa.

30.Bwana Mushrik anapokubalia Islam na akawa Mwislaam lakini mke akabakia mushrik, na baada ya kupita kipindi mke akawa Mwislaam,basi katika hali kama hii kwa mujibu waShariah,ndoa yao ilikuwa imekwishavunjika (hawakuwa na ndoa) na bwana haelewi masuala haya na anamchukulia mke wake kama yu halaali kwake,na siku atakapokuja kujua masuala hayakishariah basi itambidi afanye nikah haraka.

31.Watu wengi sana wanadai kuwa wao wamekuwa Waislaam lakini wake zao wanakataa kata kata kuwa Waislaam na ilhali wameshazaa nao watoto hivyo hawawezi kuwapa talaqa wake zao kwa sababu kama hizo na lawama na aibu kutoka kwa jamaa zao.Kwa hivyo "Mungu atatusamehe tu,sisi tufanyeje?".

Sisi tujiulize kuwa hapo kosa ni la nani na anayetakiwa kulaumiwa ni nani.Hivyo itawabidi wasiwachukulie wake kama hao kama ni wake zao na wala wasi suhubiane nao na hivyo tu ndivyo watakavyoweza kujiepusha na madhambi.

Sasa tuzungumzie swala la toharah kwani chakula anachokipika ni najis na nguo na vyombo anavyoviosha pia ni najis kwa hivyo ni haraam na sala zitakuwa batil  hivyo itambidi kuchukua hatua za kujitoharisha kishariah na kuchukua hatua zote za tahadhari ili aweze kusali na kufunga saumu bila ya kuhatarisha amali zake za ibadah.

Iwapo hatafanya hivyo na kuishi na mke wake mushrik na vyote atakavyopatiwa na mke wake kwa ajili ya wudhuu,ghusli, sala na saumu basi vyote vitakuwa ni batil. Hivyo mwenyekujitakia hayo,itambidi atafute ufumbuzi wake. Ama sivyo matokeo yake yapo bayana.

Watu wengi wanasema "Je mwenye kukubali matendo yetu ni  Allah swt au ni Mashekhe wetu?" Kwa kweli huku ndiko kujidanganya nafsi zetu na kujihadaa kwani Shariah kuhusu sala,saumu na mengineyo ni ya Allah swt na wala si yetu hivyo ni kwa mujibu wa hayo tu, hakuna Shariah ya aina yoyote ile ambayo mtu anayo ruhusa kuibadilisha kwa mujibu wa matakwa yake.Je ni Sheikh yupi ambaye anataka kujitumbukiza bure katika moto wa Jahannam kwa kumsingizia Allah swt,Mitume a.s. na Maimamu a.s? Hivyo sisi pia inatubidi kufanya utafiti zaidi juu ya masuala ya Din kwani ni fardhi yetu kujua masuala yote ya Din.
32.Ingawaje Islam imeruhusu kuoa wake wanne kwa wakati mmoja lakini imeweka Shariah kali mno ya  kutimiza na kuhakikisha uadilifu miongoni mwao.Itambidi mtu atafiti zaidi juu ya masuala haya katika fiqh.

33.Mke hawi haraam baada ya kumpatia talaqa, illa baada ya kupita kipindi cha Iddah.Iwapo mume atataka kumrejea mke wake kabla ya kipindi cha Iddah kuisha, na iwapo atakuwa na uhusiano wa mume na mke,basi talaqa itavunjika na hakuna haja ya kusoma nikah tena.

34.Iwapo mume atampa talaqa mke wake na baada ya kupita kipindi cha Iddah atataka kumrejea tena mke
wake basi itambidi kusomewa nikah tena.
Si lazima kuwa mwanamke huyo aolewe na kusuhubiana na mwanamme mwingine na kupewa talaqa ndipo bwana wa kwanza aweze kumrejea.

35.Mwanamme hawezi kumpa talaqa ovyo mwanamke kwa sababu zisizo na msingi kishariah.Hivyo itambidi mtu kutafiti vyema masuala ya talaqa katika Shariah kwa pande zote mbili kwani kuna mambo mengi ya kuzingatia na kuyatekeleza yakiwemo pamoja na haki ya mke na watoto.Hivyo tusidhani kuwa tutakapomwambia mke "nimekupa talaqa" basi siyo kwamba amepata talaqa bado anakuwa amebakia katika nikah au kwa kupewa talaqa mahakamani,kwani haki zake zote bado zipo juu ya bwana wake.Shariah za Kiislamu ni Shariah halali hivyo Shariah za nje ya Islam hazitabadilisha msimamo wa Islam.

20.  UFUMBUZI WA MASUALA MENGI

1. Wanaume kuingiliana na malaya

Wanaume wengi mno wenye ndoa huwa na tabia ya kuingiliana  pamoja na wanawake nje ya ndoa yao (malaya) ilhali wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume na Shariah za Dini na ni ghunah-i-kabirah (dhambi kubwa mno).Pamoja na hayo kuna madhara mengi mno ya kimwili pia na hatimaye mtu kufikia hatua ya hatari kwa siha yake.Ni dhahiri kuwa raha na starehe za huyo malaya pia zinatolewa na mke wake na mke wa nyumbani huweza kutoa  hata zaidi ya hayo.

Tumeona daima kuwa wanaume waendao na malaya huwa wanaadhiriwa na kudhalilika katika jamii inayothamini ndoa halali na hatima yao huwa mbaya kwani huwa wamefilisika kimali na vile vile miili yao pia inakuwa imekwisha.Yaani kudhoofika na kupatwa kila aina ya magonjwa kama magonjwa ya ngozi,ukhanisi na siku hizi ugonjwa wa ukimwi, kwani malaya huwa hana bwana mmoja illa kila mwenye chochote ndiye bwana wake,ukitoka wewe ataingia mwingine kwani wao wanataka kila wakati wapate 'kipya' nao pia hawataki kula pilau kila siku kama wewe unavyodai. Baada ya mwanamme huyo kujitumbukiza na kujiangamiza yeye mwenyewe katika magonjwa mabaya kabisa huwaambukiza wake na watoto wake na hata familia yake nzima inaweza kuteketezwa kwa kutokana na maovu yake.Hivyo inampasa kila mwanamme amwangalie mwanamke malaya kama nyoka mwenye sumu kali na hivyo inambidi kujiepusha naye kabla hajapata sumu hiyo mwilini na maishani mwake.

Mara nyingi mno sababu za kumfanya bwana aende kwa malaya huwa ni wake zao nyumbani.Kwani kwa kutokana na magomvi au kutoelewana vyema baina ya bwana na bibi au kwa kutokuwa na programu nzuri ya maisha ya nyumbani.Vile vile imewahi kuonekana kuwa huwa mmoja wao hataki kusuhubiana wakati fulani ambapo mwenzake anataka kwa nguvu,na katika hali kama hii ndipo inamfanya kufikiria njia ya kutaka kwenda nje kujiridhisha.

Hivyo inambidi bibi na bwana kuwajibika vyema katika masuala haya.Na daima tukumbuke kuwa katika maisha yetu yote mapenzi na bibi au bwana ni nguzo mojawapo ilipojengeka maisha yetu,na iwapo itadhoofika nguzo hiyo,basi itaweza kuporomosha maisha yetu.Na swala la kusuhubiana ni nyeti mno katika maisha ya ndoa.
Tujaribu kuelewa falsafa ya 'kuridhika' na 'kutosheka' ndipo maisha yetu yatatengemaa.Iwapo katika tembeatembea yako umeona gari moja ambalo limekupendezea na ukawa unao uwezo wa kulinunua,na ukalinunua hilo gari. Basi utajisikia una raha mno wakati ukiliendesha ambapo kabla yake ulikuwa unapata shida kubwa ya usafiri na huduma zinginezo. Lakini ikifika siku ukaanza kuidharau,basi utaanza kutukana badala ya kuisifu kama hapo awali na raha uliyokuwa ukiipata sasa itakuwa imegeuka kuwa udhia na kuanza kula kichwa chako.Utaanza kutamani magari mazuri mno ya watu wengine wakati uwezo hauna.Sasa jee utakwenda kuiba ambapo unajua hatima yake ni kule kushikwa gari na wewe kwenda kizimbani--maisha yako kupotea na kuteseka?

Maisha yetu kuhusu kusuhubiana huwa ni sawa na kula, kunywa na kulala.Iwapo mtu atakuwa mroho katika kula na kunywa ambapo kamwe haridhiki,basi utaona anapenda kula kila mahala na kila wakati yaani anakuwa mroho asiyekinaika.

2. Kuhusu kusuhubiana mara ngapi

Wataalamu na madaktari wanasema iwapo mtu atataka kuitunza siha yake vyema na kujilinda kabisa,basi inambidi asuhubiane mara moja kwa mwaka,lakini kipindi hiki ni kirefu mno ambapo nadhani hakuna mtu afanyaye hivyo.

Hata hivyo kumwaga manii mara moja kila siku ingawaje haishauriwi,lakini inawezekana kwani manii huwa inakusanyika sehemu tatu.Kumwaga mara moja kunapunguza sehemu moja ya manii iliyokomaa ambapo kunakuwa bado sehemu mbili zinazoendelea kukomaa.Na kumwaga kwa mara ya pili kunatokwa na manii iliyo bado kukomaa na kumwaga kwa manii mara ya tatu kunatokwa na manii changa kabisa na kumwaga kwa mara ya nne,ni kutoa damu tu.Hivyo kumwaga manii kwa zaidi ya mara moja kunamdhoofisha mwanamme na hatimaye kuwa khanisi .Kuna watu wengi mno ambao siku hizi hawaoni raha ya kusuhubiana na wake zao hadi hapo watazame filamu za watu uchi wakifanya hayo.Watambue wazi wazi kuwa mwelekeo wao ni mbaya. Bwana anaanza kuwatamani wake wa nje na bibi kuwatamani wanaume wa nje na vile vile kuna hatari kubwa mno ya mwanamme kupoteza nguvu zake za kiume.Sasa raha za dakika chache tu zikikufikisha katika hatari hiyo,je litakuwa ni jambo la busara? Hebu tukae na kutafakari swala hili vyema ili tusije tukajikuta tumeangamia kabisa.

Kama vile ilivyokwisha elezwa hapo awali,wazazi ambao wanapenda sana kusuhubiana, kizazi chao kitakuwa dhaifu na hivyo wazazi wanawajibika mno kuhakikisha kuwa vizazi vyao vinakuwa vyema na vyenye mustakbali mzuri.

3. Kumwaga manii kwa mikono

Ni ghunah-i-kabiirah kuchezea sehemu ya uume wa mwanamme hadi kutokwa na manii kwa sababu tu siyo kuwa inadhoofisha mishipa yao bali inaleta madhara makubwa mno ambayo ni hatari zaidi kwa siha yao.Ikumbukwe vyema kuwa vijana wanamwaga na kuzitupa jawhari kutoka mwilini mwao.Na anapoingia katika tabia kama hii anakuwa ndiye muuaji wake mwenyewe bila hata ya yeye mwenyewe kutambua hivyo anajifurahisha kipuuzi kwa kupoteza uzima wa milele.

Tabia kama hiyo haina mipaka kwani kila wakati tu atakuwa akitamani kujitoa manii ambapo ni hatari kwa siha yake.Akifanya utafiti ataona kuwa anajitoa damu tu na jee kwa kujitoa damu si kutamponza tu? Sasa mwanamme mzima akiupoteza uume wake atakuwa na faida gani?Kwa kutokwa na manii kupita kiasi kutampatia tabia ya kutokwa na manii haraka mno wakati wa kusuhubiana ambapo atakuwa daima hakutimiza hamu ya kusuhubiana.Si kwamba yeye tu atakuwa hana raha vile vile mke wake atakuwa na hamu isiyotoshelezwa ,hivyo si kutamwelekeza mke wake kutafuta wanaume wengine? Je mtu atapendelea hivyo?
Fikiria wewe ni mtu mmoja uliyesoma sana na unaolewa na mwanamke ambaye anafurahi mno kusikia sifa zako.Lakini mutakapoingia kitandani kusuhubiana anakukuta hauna nguvu za kiumeza kumridhisha.Je mwanamke si atajiambia kuwa "afadhali ningeolewa na jahili ambaye anaweza kunitimizia haja yangu kuliko huyu aliyesoma ambaye hawezi kuniridhisha?"  Maisha yamepotea bure!

Kuna baadhi ya vijana wanatokwa na manii katika ndoto,mkojo au katika hali  ya ugonjwa au mshtuko na hali kama hii inatokea miongoni mwa vijana kwa sababu ya ugonjwa ambao unatokana na:(1).kujitoa manii, (2).kujiweka pamoja na wanawake na  (3).kuwa na mapenzi ya wanawake bila ya kuwapata.

Hivyo inawabidi vijana wote wajirekebishe na kuacha mbali tabia hizo mbaya ambazo zitamwangamiza na kupoteza nguvu za ujana wake.

Kile ukifanyacho sasa hivi bila ya kufikiria mbele ni hatari kwa maisha yako ya mbeleni,fikiria bado ni miaka mingapi utakayo ishi.Hebu chukua mfano wa mtu amwambie kijana wa miaka 18 kuwa amng'oe meno yake yote,sasa kijana huyo atafikiria iwapo atang'olewa meno umri huo basi ataufikiaje umri wa miaka 40 au 60 au zaidi bila ya meno?
Hivyo fikiria na uyajenge maisha yako kuanzia sasa kabla haujachelewa!

4. Ulawiti wa kila aina

Kwa  mujibu wa Shariah za Kiislam,ulawiti na wanawake kuingiliana wenyewe kwa wenyewe ni matendo ya Ghunah-i-Kabira na hivyo kiviwekea adhabu kali mno hapa duniani na Aakhera . Iwapo kutapatikana watu wakifanya hivyo,basi wote wachinjwe. Hapo Hakim-i-Sharah (Hakimu wa Kidini) anaweza kutoa amri ya ya kuchinjwa kwa panga,kufungwa mikono na miguu na hatimaye kutupwa kutoka juu,au kuchomwa moto,kupigwa mawe hadi kufa au kuangushiwa ukuta. Vile vile anaweza kutoa adhabu zingine  pamoja na kuchomwa moto.

Ulawiti baina ya mwanamke mmoja na mwanamke mwingine pia inachukuliwa na Shariah kuwa ni dhambi kubwa kabisa kama vile ilivyo ulawiti baina ya wanaume. Iwapo wanawake wenye kutenda hivyo ni wenye akili na fahamu timamu,basi wapigwe viboko mia moja kila mmoja. Adhabu hii imewekwa kwa ajili ya wanawake wote wale walioolewa na wasioolewa.

Iwapo mwanamke atapatikana na makosa kama haya kwa mara ya nne,basi atachinjwa. Na iwapo mwanamke atakapopatikana na kosa kama hili,na akakiri na kutubu,basi Imam anaweza kumsamehe au kumpangia adhabu.Vile vile Naibu wa Imam  anayo mamlaka kama haya. Lakini siku hizi hakuna ad­habu kama hizi.

5.Kutafuta mwenzako katika ndoa

Binadamu anafanya kila aina ya utafiti na jitihada ya kutafuta mwenzi wa kila moja kuwa watoto watakaozaliwa na farasi,ng'ombe na mbwa wawe madhubuti na wenye siha nzuri lakini jambo la kushangaza kuona kuwa sisi tumejipuuza kutafuta mwenzetu katika swala hili !

Lakini leo tunatafuta bibi na bwana kwa kuzingatia  urembo na utajiri halafu hata kama mmoja wao atakuwa na tabia mbaya au magonjwa ya kuweza kurithiwa katika watoto.

Iwapo hawa watu wawili yaani mwanamme na mwanamke wanapotaka kuoana watakuwa ni watu wenye kasoro fulani za kitaalam ambazo zinajulikana basi hawashauriwi kuoana, huyu mwanamme asimuoe huyo mwanamke na huyo mwanamke asiolewe na huyo mwanamme. Hata hivyo watu wengi hawawezi kuelewa vile magonjwa ya kurithiwa yaliyomo miongoni mwao yaani mwanamme hawezi kuelewa mwanamke anayetaka kumuoa ana magonjwa gani ambayo yanaweza kurithiwa na watoto au mwanamke hawezi kuelewa mwanamme anayo magonjwa gani yanayoweza kurithiwa na watoto wao; basi watu wanaoana.

Umuhimu juu ya mali, kabila na mambo mengine na mara nyingi ndoa kama hizi ndiyo sababu kubwa za kuzaliwa kwa watoto waliodhaifu kwa sababu katika kuchagua, afya au siha iliachwa.Mwanamme aliye na siha nzuri anastahili kumuoa mwanamke aliye na siha nzuri, bila ya kujali kuwa huyo mwanamme ni tajiri au amesoma au ni mpumbavu, kwani  jambo kubwa ni siha.

Ndoa ndiyo msingi wa furaha za maisha ni jambo la kipumbavu kupanga ndoa baina ya watu wawili bila ya kutazama mambo ya mbele na nyuma. Inabidi wahusika wa sehemu zote mbili watilie maanani siha zao tofauti kati ya umri na silka zao kabla ya kukubaliana baina yao kwa sababu siha na silka au tabia zinazooana baina yao ndizo zinazofanya maisha yakawa yenye furaha na kama siha na silka zao zitatofautiana basi maisha yao yamepotea na kila mara watakuwa katika mizozo.  Mambo mengi sana yapo ya kuzingatia kabla ya mtu hajakubaliana na mwenzake kuoana. Litakuwa ni jambo la kipumbavu kutafuta msichana mwenye umbo zuri,kiuno kidogo mwembamba kama sindano ati huyo ndiye anaonekana  mzuri.Hakika mwanamke kama huyo hawezi kuzaa watoto wenye afya nzuri.

Kwa kifupi mtu anapochagua mwenzake akiwa mwanamke au mwanamme  asiangalie utajiri, urembo na ukabila ilimradi macho yake yanamdanganya, lakini inambidi amwangalie mwenzake ana siha gani. Na tabia zake zimeoana kama tabia zake, silka yake na silka ya  huyo mwenzake ziko sawa ili waweze kuelewana hapo mbeleni. Na iwapo ataoa mwanamke mrembo au  tajiri lakini asiye na siha nzuri,basi hatakuwa na faida naye. 

6.  Uislamu haujakataza kupanga ndoa ya utotoni 

Yaani watoto wanapokuwa wadogo katika mila nyingi wanapanga ndoa Uislamu haujakataza lakini kuna mambo mengi ya kuzingatia yaliyo na faida na yenye hasara katika hali hii.Ndoa hizi za kupangwa za utotoni zimesababisha vijana hawa wawili wakose kuendelea na masomo yao na maendeleo mengi hawawezi kuyafikia kwa sababu wanaoana bado wakiwa wadogo. Vile vile wanapokuwa wadogo wanaweza kuwa wanacheza pamoja, wanaweza kuwa marafiki sana kwa sababu wanakuwa na akili ya kitoto bado lakini vile wanavyoendelea kukua na baada ya kuwa wakubwa mara nyingi unaona wanatofautiana kwa mawazo na mmoja anakuwa na tabia tofauti na mwenzake na mara nyingine mmoja anaweza kumpenda mwenzake wakati mwingine anamchukia kwa sababu wakati huo wanaakili timamu kwa hivyo kuna uwezekano wa hali hiyo kutoendelea vyema. Kwa hakika ndoa kama hizi zinaishia katika hali ya vurugu na mara nyingi kupeana talaqa.

Kuna hali nyingine za ndoa ambazo zinapangwa na wazazi au ndoa zingine zinapangwa na wataalam katika fani hii ya kuoza na katika sura hii mwanamke na mwanamme yaani bibi na bwana mara nyingi sana wanakuwa hawana raha ya maisha kwa sababu mwanamme na mwanamke wanatoka mahala tofauti na inawezekana mara nyingi hawajuani wanashtukia wameshapangiwa ndoa au bibi ameshatafutiwa bwana au bwana ameshatafutiwa bibi,ilhali anaona wakubwa wake wameshamtafutia anakubali! Lakini mawazo na mapendo yao yanatofautiana, mwingine anakuwa na tabia tofauti na mwenzake kwa hiyo daima wanakuwa katika hali ya vurugu. Na katika maisha ambayo hayana raha, uelewano, mapenzi, uwiano baina ya bibi na bwana kuna sababisha watoto watakaozaliwa wasiwe watoto kamilifu kwa sababu watoto akiwa bado tumboni mama akili zake zinakuwa zimevurugika kwa sababu mama huwa hafikirii mambo mengi mazuri kila wakati utamuona mara ana hasira mara anafikiria matatizo anayoyapata sasa  na vitu vinamuathiri mtoto na hata mtoto akishazaliwa hawezi kupata mapenzi ya baba na mama kwa sababu wote wawili wako katika hali ya mvurugano kwa hiyo hata watoto mawazo yao yanakuwa yameharibikiwa. Ama wao wale wanaoolewa wakiwa bado wadogo kabla ya kufikia ubaleghehawawezi kuzaa ingawaje katika hali ya usichana msichana wa miaka kumi na moja imerekodiwa kuzaa watoto. Hata hivyo kifugo cha msichana wa umri huo haijatangamaa kikamilifu kwa hivyo tusitegemee kuwa mfuko wa mama huyo ambao haujatengamaa sawa sawa ukaweza kuzaa mtoto na kumlisha mtoto kikamilifu.Kwa sababu mfuko wake bado unakasoro sio madhubuti kwa hivyo mtoto huyo hatapata mahitajio yake sawasawa yungali tumboni.

7.  Hali ya kutooa kabisa.

Kwa mwanadamu kimaumbile alivyoumbwa na  Allah swt anategemewa aishi kama binadamu na hivyo mwanamme au mwanamke anapokataa kuoa au kuolewa kwa hakika hapo ni kinyume na kimaumbile aliyoumbiwa na Allah swt.Wataalam wamedadisi kuwa watu wanaooa au wanaoolewa wanaishi maisha marefu zaidi kuliko wale ambao hawaoi wala kuolewa.Na wale wasiooa wana uwezekano wa kupata magonjwa mengi ya hatari kuliko wale wanaooa hivyo ni jambo la busara kuoa au kuolewa pale mtu anapoingia katika umri wake huo.  Ni jambo la kudura za Allah swt kuwa mwanamme na mwanamke wanatamaniana.

8.Dua za kuomba watoto 

Zipo Dua nyingi mno kwa ajili ya mwanamke kushika mimba  na hapa chini nitawaleteeni Dua chache ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa wale bibi na bwana ambao kwa bahati mbaya hawakujaaliiwa watoto ninatumaini na ni sala zetu pia kwa kusoma duaa na kwa kufuata miongozo michache ifuatayo Allah swt atawajaalia hiyo neema.

Mtume s.a.w.w. amesema: "Watoto ni sawa na maua ya peponi kwa hivyo uwema wa mtu ni kutokana na vile anavyozaa watoto."

Mtu ambaye hajabahatika kupata watoto, aende katika hali ya sujuda na asome Dua ifuatayo:-
Rabbi habli min ladunka dhurriyatan tayyibatan Innaka samiud-Dua', Rabbi  la-tadharni fardan wa anta Khayrul Warithiin.

Na mtu ambaye anataka mke wake ashike mimba  basi inambidi baada ya sala ya Ijumaa asali rakaa mbili  na katika kila rukuu na sujuda arefushe na baada ya sala asome Dua ifuatayo:-
Allahumma inni as-aluka bima sa-alaka bihi Zakariyya:Rabbi la tadharni fardan wa anta khayrul warithiin,habli minladunka dhurriyatan tayyibatan,Innaka akhadhtaha fa fadhayat fi rahimiha waladan,fajalhu ghulaman mubarakan zakiyyan wala taj'al lishaytani fihi shirkan wala nasiban.

Mtu mmoja alimwijia Imam Muhammad Baqir a.s. na kumwambia:"Ewe mjukuu wa Mtume! Mimi sina watoto," hapo Imam a.s. alimjibu kuwa : "Kila usiku au kila wakati wa mchana usomeIstighfaar mara mia moja na Istighfaar ifuatayo ndiyo itakuwa vyema zaidi. 'Astaghfirullah  rabbi wa-atubu ilaihi'.

Ili kutaka watoto kwa wale ambao hawajabahatika inawabidi daima asubuhi na jioni wafanye ifuatavyo:  asome mara kumi
Astaghfirullah  rabbi wa-atubu ilaihi  na baadaye asome mara tisa Subahanallah na baadaye asome mara moja  Astaghfirullah rabbi wa-atubu ilaihi. 

Mwenye kuripoti mmoja anaelezea kuwa watu wengi wamefanya  majaribio hayo na wameweza kuzaa watoto wengi.

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema kuwa mtu yeyote mwenye kutaka watoto, kila anapoamka asome Istighfaar mara mia moja na lau atasahau hapo baadaye asome kwa nia ya Qadhaa

Mtu mmoja alisema:"Ewe Imam mimi sina watoto."Imam a.s.       alimwambia:"unapopanga kusuhubiana na mke wako soma duaa ifuatayo : Allahumma inruzaktana dhakaran sammaytuhu Muhammadan.

Mtu mmoja alimwijia Imam Ridhaa a.s na kumwambia: "Ewe mwana wa Mtume ! Mimi daima huwa niko mgonjwa na sina watoto."Hapo Imam a.s alimjibu: "Uwe ukisoma adhaan nyumbani kwako kwa sauti kubwa. Yule mtu baada ya miaka kupita alimwijia Imam na kumwambia:"Mimi nilikuwa nikifanya hivyo na ninamshukuru Allah swt nimepona  na nimekuwa mzima na sasa hivi nina watoto wengi."

Mtu mmoja alikuja kwa Imam Jaafer Sadiq a.s. na kuleta malalamiko yake,  "Ewe mwana wa Mtume ! Mimi sipati mtoto wa kiume." Hapo Imam a.s. alimjibu:  "Popote pale unapokuwa umepanga kusuhubiana na mke wako (kumuingilia mke wako) basi usome Aya ifuatayo mara tatu na baada ya kusoma mara tatu ndio usuhubiane na mke wako. Allah swt atakujaalia watoto wa kiume.Na Aya yenyewe ni hii ifuatayo:-Wadhannuni Idhdhahaba mughadhiban fadhanni an lan nakdir Ilayhi fanaada fidhdhulumaati,'an-Lailaha illa Anta Subhanaka inni kuntu minadhdhalimiin, fastajabna lahu wa najjainahu minal ghammi wa kadhalika nunjil mu'miniin,Zakariyya idhnaada Rabbahu Rabbi la tadharni fardan,wa anta Khayrul warithiin.

Katika Hadith inapatikana kuwa mtu yoyote ambaye hapati watoto inambidi afanye niyyat kama ifuatavyo:- "Iwapo mimi nitapata kijana wa kiume jina lake nitaliweka Ali"  basi  Allah swt atamjaalia mtoto wa kiume.

Imam Zeinul Abeidin a.s. amenakiliwa akisema mtu yeyote atakayesoma Dua ifuatayo atapata chochote kile akitakacho lau atataka mali, au watoto na wema wa dini na dunia, basi Mwenyezi Mungu atamjalia vyote hivyo na Dua yenyewe ni kama ifuatavyo:-
 Rabbi la tadharni fardan,wa anta Khayrul warithiin wajalni minladunka wayarithuni fi hayati wayastaghfiruli baada mauti waj-alha khalqan sawiyyan wala taj-al lishaytani fiha nasiban.Allahumma Inni astaghfiruka wa atubu ilayka,Innaka antal ghafurur-Rahiim.
Na kwa hakika imependekezwa mno kusoma Dua hiyo mara sabini kwa ajili ya wale wanaotaka watoto.

Mtu mmoja alimwijia Imam Muhammad Baqir a.s. na alikuja akilalamika kuwa anao watoto wachache.  Hapo Imam alimjibu: "Kila siku kwa muda wa siku tatu baada ya sala ya asubuhi na sala ya Isha usome subahanallah  mara sabini na Astaghfirullah  mara sabini.  Na baadaye usome Dua inayofuata:- Astaghfiru Rabbakum Innahu kana Ghaffara,yursilussama' alaykum midraara,wa yumdidkum bi amwalin wa baniin wa yaj-alkum anhaara.

Baada ya kukamilisha utaratibu huo kwa muda wa siku tatu kwa usiku huo wa siku ya tatu ndio usuhubiane na mke wako na Allah swt atakujaalia  watoto wema kwa ajili yako.

Mtu mmoja alikuja kwa Imam Jaafer Sadiq a.s. na kumwambia: "Ewe mjukuu wa Mtume! Allah swt amenijaalia wasichana wanane lakini mpaka leo sijabahatika kuona sura ya mtoto wa kiume. Imam a.s. alimwambia: "Wakati wa kusuhubiana, ukae katikati ya miguu ya mke wako, wakati huo mkono wako wa kulia uwe upande wa kulia mwa kitovu chake na usome sura ya Inna-An- zalnahu ... mara saba na baada ya kusoma ndio usuhubiane na mke wako.Mtu huyo anasema  kwa kufanya hivyo Allah swt alimjaalia watoto saba wa kiume. 

Imam Hasan a.s. amesema: "Yeyote yule anayependa kuzaa watoto wa kiume basi inambidi afanye Istighfaar kwa wingi kabisa."

Hapo tumeona duaa za kupata watoto vile vile kuna mambo mengine yanayochangia katika sura hii.

Wakati mzazi anapopata mimba hali yake ya kiakili na siha yake ya kimwili  inaathiri sana mwili na akili ya mtoto aliyetumboni.

Inamlazimu mwanamke akae mbali na bwana wake katika kipindi cha haidh.Mfano wa gogo liki­tupwa mtoni halirudi nyuma bali linaendelea mbele (yaani halirudi kule maji yanakotoka bali huenda kule maji yanakokwenda), vivyo hivyo iwapo manii zitaingizwa ndani ya mwanamke haitafika katika sehemu za kushika mimba  hivyo hakutakuwa na maana ya kusuhubiana.  Na lau kimaajabu mwanamke akitokea akashika mimba katika hali hiyo ya kusuhubiana wakati akiwa katika kipindi chake cha damu ya  siku za mwezini mtoto ataweza kufa azaliwapo.  Iwapo mimba itashika siku ya pili mtoto atazaliwa akiwa na kasoro ya viungo na umri wake utakuwa mdogo sana.  Na mimba itakayoshikwa baada ya kumalizika kwa damu hiyo mtoto atakuwa mzima mwenye siha nzuri na maisha mazuri. 

Mwanamke anayokumbana nayo kiakili na kimwili akiwa na mimba  yanamuathiri sana mtoto aliye katika tumbo.Hivyo inashauriwa sana kwa wanawake kuweka akili zao safi na wayaondoshe mawazo yao mabaya na wasijiingize katika mambo machafu, vile vile inawabidi wavae mavazi mazuri, masafi yenye kupendeza, wajipake manukato mazuri waonekane nadhifu,wajiepushe na harufu mbaya na mawazo ya kutisha.Mwanamke huyo asile vyakula vilivyoharibika au vilivyolala. Inambidi asitoke toke nje ila kikazi na aende katika mazingara ya kupendeza na kamwe asiende katika mazingara ambayo yanatisha yenye mashetani, majini n.k. na kamwe asipige makelele na mayowe na wala asijitaabishe kimwili pia, kwa muhtasari inambidi ajiepushe na kila aina ya tabia na hali ambayo itamuathiri vibaya mtoto tumboni.

Mwanamke mwenye mimba  asilale juu ya vitanda virefu. Inambidi kitanda anacholalia kiwe na nafasi ya kutosha na ni lazima kuwa matandiko yawe mazuri na masafi.  Na inambidi alale na mavazi mepesi, chakula chake kiwe cha kawaida na chenye afya yaani kiwe na mahitaji ya kutengeneza chakula cha mtoto tumboni.

Mwanamke mwenye mimba huwa na matamanio na yasipotimizwa yanamuathiri sana mtoto.Masikitiko,hasira, kutoridhika na mambo yote kama haya yanayoathiri akili  na ubongo wa mtoto aliyetumboni.

Imeshauriwa sana kwa mwanamke kujiepusha na:-
1.  Kupanda farasi au tembo.
2.  Kupanda miinuko mikubwa.
3.  Kufanya mazoezi magumu
4.  Kwenda kwa mwendo wa haraka haraka au kuruka ruka
5.  Magomvi ya kila aina
6. Kula vyakula vyenye harufu mbaya au kula vyakula vilivyo moto na kula
    vitu vichachu sana na  vile vile kula vyakula ambavyo ni vizito.
7. Kuchuchumaa na mambo kama hayo.

Inashauriwa ale matunda kwa wingi zaidi kiasi awezavyo.

Baada ya kushika mimbamwanamke anakuwa na hamu sana ya kula aina nyingi ya vyakula.  Na lau matamanio yake hayo yatatimizwa basi atazaa mtoto mwenye siha nzuri sana, lau matamanio yake hayo hayatatimizwa basi inawezekana akazaa mtoto mwenye kasoro nyingi tu.

Wazazi tabia zao pia zinaathiri sana akili na hali ya watoto.  Iwapo wazazi watakuwa wakigombana wakati wa kushika mimba  ,basi kuna uwezekano wa mtoto atakayezaliwa atakuwa mgomvi.Walevi mara nyingi wanazaa watoto wenye kasoro na wasio na maendeleo.Inatokea pia kwa watoto wanaozaliwa mwanzoni wanakuwa wamepoa na wenye fikara kidogo za kinyuma nyuma wakati watoto wengine wanaoendelea kuzaliwa wanakuwa hodari na wenye siha nzuri.Sababu zote hizo tunaweza kuzipata katika mazungumzo tuliyoyazungumza huko nyuma na mengineyo mengi. Kwa hivyo inatulazimu sisi twende na wakati kwa sababu iwapo tutataka watoto wazaliwe wenye siha nzuri wenye akili nzuri wema wenye sifa nzuri basi itatubidi tujirekebishe katika kipindi hicho, tuwe tahadhari na hali ya baadaye.

9. Khatna yaani kumkalisha sunna mtoto

Imefaradhishwa katika Islam kukata sehemu ya ngozi ya mbele ya uume wa mtoto mwanamme.  Kufanya hivyo kuna faida nyingi sana ambazo zinaelezwa hata na madaktari wa siku hizi.Daima kunakuwa na maji yenye kunatanata na yenye harufu mbaya mbele ya uume wa mwanamme. Lau itaachwa hali hiyo uchafu huo uendelee kuwepo hapo basi kuna hatari ya kutokezea vipele na kuzuka magonjwa mabaya yatakayo athiri uume wa mwanamme.  Hivyo iwapo hiyo ngozi ya mbele itakatwa basi hakutakuwa na utaratibu wa kubakia uchafu hapo mbele na hivyo sehemu ya uume wa mwanamme daima utakuwa  msafi na utakuwa hauna hatari ya kupata madhara kama haya.

Mwanamme aliyetahiriwa  yaani aliyekatwa ngozi ile ya uume ya mbele anatoa manii kwa nguvu zaidi ya yule mwanamme ambaye ngozi yake haijakatwa.Manii iliyomwagwa haibakii katika sehemu ya ngozi ya mwanamme sehemu ya mbele kwa wale waliokatwa ngozi na wale wasiokatwa ngozi uchafu huo unabaki pale pale na unaweza kuleta madhara makubwa zaidi.  Wale wanaume ambao hawajakatwa ile ngozi ya mbele (kutahiriwa) hawawezi kusafisha ndani mwa sehemu hizo hivyo kuna hatari nyingi ya kufuga magon­jwa hapo na vile vile kuna uwezekano mkubwa sana wa kufuga magonjwa yanayotokana sehemu za siri za mwanamke na mwanamme. 

Hivyo Sharia za Uislamu zina hekima , zina busara, na zimefanywa kwa ajili ya masilahi na ubora wa binadamu kwa yeyote yule atakayeweza kufuata atapata mafanikio na wala hakuna hasara au ubaya ndani yake. 

10. Pombe

Katika Uislamu unywaji wa pombe na zinaa vyote hivi ni katika madhambi makubwa.

Unywaji pombe umezungumziwa sana katika Quran na Hadithi na riwaya mbalimbali kabla ya kutaka kuzungumzia madhara na maovu ya pombe kwa mujibu wa dini ya Kiislamu tujaribu kuangalia sayansi na matibabu yanasemaje kuhusu haya.

Daktari mashuhuri Arnel-Wared anaandika katika mpangilio wa sayansi kuwa yeye alipokuwa akifanya kazi katika Hospitali mashuhuri ya Edinberg, hospitali yake ilikuwa ikiwanywesha pombe wagonjwa wenye magonjwa ya Pneumonia hivyo ilibidi watumie mabilioni ya mapaundi kwa ajili ya kuwanunulia wagonjwa pombe. Baada ya miaka michache kupita Profesa Sir Thomas wa Edinberg University alizuia matumizi ya pombe katika kutibu ugonjwa huo hivyo gharama ya matumizi ya pombe ilipungua sana ikabakia katika paundi chache tu.

Sababu kubwa yakukatiza utumiaji wa pombe katika kutibu ugonjwa wa pneumonia ni kwamba: "Pombe hiyo ilikuwa ikiwadhoofisha Phagocytes ambao wanasaidia sana katika kuua vijidudu vya Pneumonia. Kwa hakika hao phagocytes wanapokuwa dhaifu basi kuna uwezekano mdogo sana kwa mgonjwa kupona na hivyo hatima yake ni kifo.Baada ya uvumbuzi huo hospitali nyingi za Ulaya ziliacha kutumia pombe katika  matibabu ya ugonjwa huo na badala yake maziwa yalianza kutumika. Hata hivyo hawakosi madaktari wengi mno ambao bado wamekalia desturi ya kizamani ya kushauri wagonjwa wenye Pneumonia kutumia pombe. Hata hivyo katika hospitali nzuri na zenye maendeleo mazuri zinakataa utumiaji wa pombe kwa sababu pombe zinaaminiwa na inasadikiwa kuwa ni adui wa mwanadamu hadi leo hii.

Profesa Machincalf wakati wa maonyesho ya siha huko London katika mwaka 1906 alisema kuwa phagocytes ni kitu kimoja bora katika damu yetu, lakini inapopata sumu juu yake basi inaharibika.  Vile vile amethibitisha kuwa pombe inaiteketeza hiyo nguvu yake kama vile opium inavyofanya.

Wakati mtu anapoumwa na mbwa kichaa au anapopigwa sindano ya kichaa cha mbwa basi huyo mtu ambaye si mlevi inamsaidia vyema kabisa kuliko yule ambaye ni mlevi na mara nyingi haiwasaidii. Utumiaji hata kiasi kidogo cha pombe kinawateketeza phagocytes. Kwa hakika kwa unywaji wa pombe sisi tunateketeza uwezo wa mwili wetu wa kututeketeza sisi wenyewe. Baada ya uvumbuzi huo madaktari waliokuwa wakiamini kuwa pombe inasaidia katika kuivisha chakula mwilini wameondoa mawazo hayo ya kuwa pombe ni yenye faida badala yake wameamini kuwa pombe inaleta madhara  zaidi mwilini . 

Pombe inaathiri vibaya sana hali ya uzalishaji wa kemikali katika tumbo.  Kemikali hizi zinafanya kazi kubwa sana ya kutengeneza chakula chetu kuingia katika damu yetu. Hivyo kwa kunywa pombe kunaharibu nguvu za kemikali na hivyo kutukosesha sisi faida yote kutokana na vyakula vyote tunavyopata.

Athari za pombe kwa mama wanaonyonyesha maziwa


Miaka ya nyuma madaktari walikuwa wakiwashauri wanawake wanaonyonyesha maziwa watoto watumie pombe ili kuongeza maziwa katika matiti yao. Hata hivyo, wamebadilisha mawazo yao na maoni yao. Ni kweli kuwa pombe inaongeza kiasi cha maziwa katika matiti ya mama, lakini sio sababu nyingine isipokuwa ni sababu ya utumiaji wa maji, ambayo ndiyo inaongezea kiasi cha maziwa katika matiti ya mama. Kwa hivyo kuna vinywaji vingi sana vyenye afya na vyenye siha nzuri ambavyo vinaweza kutumika na vyenye manufaa zaidi kuliko pombe. Je kwa nini tuanze kumnywesha mtoto pombe yungali mchanga kwa kupitia katika maziwa ya mama? 

Pombe inakausha maji maji mwilini. Na hii ndiyo maana tunawaona wanywaji wa pombe kuwa wanahitaji kunywa maji mengi sana na wanakuwa na kiu kingi kuliko mtu wa hali ya kawaida. Sababu nyingine ya kiu kikubwa kama hicho ni kwamba pombe inaathiri vibaya sana kemikali zinazotengenezwa na tumbo kwa ajili ya kuivisha chakula na kufanya chakula kisiweze kuiva vizuri chakula kinageuka kuwa sumu kwa  mnywaji wa pombe.  Na sababu hii ni mojawapo ya kusababisha sumu hii kuingia katika damu kumfanya awe na kiu hasa ya vinywaji baridi.Na vile vile tumeona kuwa mtu mwenye homa huwa ana kiu sana kwa sababu ya sumu hiyo inayoingia katika damu yake.Hata hivyo ukinywa maji hiyo sumu iliyoko ndani ya damu ya mtu mwenye homa inapungua hivyo kila sumu inavyozidi kupungua katika damu  ndivyo vivyo hivyo homa inavyoendelea kupungua.

Mlevi wa pombe huwa anawashwa sana tumboni na ndio maana watu wengi utawaona wanakunywa pombe kwa kuiongezea maji na hii inakuwa na athari kidogo kuliko mtu anayekunywa pombe kavu kavu.Hata hivyo nawashauri hao watu waache kunywa pombe na wanywe maji tupu kwa sababu maji yanafaida sana kuliko pombe yao hiyo.

Sasa nitaomba tuangalie kidogo vipi Din yetu inatuambia nini kuhusu unywaji wa pombe.Sisi tumebahatika mno kuwa wafuasi wa Din ambayo imetuangalizia mambo mengi yenye faida na manufaa kwetu ambayo yote yanatuletea maendeleo katika maisha yetu.Vivyo hivyo Din yetu hii imetuambia mambo mengi yaliyo mabaya na maovu na yenye hatari  kwa ajili ya maisha yetu. Wataalamu katika fani ya madawa katika miaka ya nyuma walikuwa wakiwacheka Waislamu kuwa Din  yao imewanyima vitu vyenye faida kubwa kama vile pombe. Lakini baada ya utafiti kuendelea zaidi leo wanakubali kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w.  kwa hakika ametumia hekima na busara sana kwa kuwaharamishia Waislamu pombe kitu ambacho ni chenye madhara makubwa sana. 

Mtume s.a.w.w. amesema kuwa : "Watu wa vikundi vitatu hawataingia kamwe peponi , nao ni:-
1.  Wale wanaokunywa pombe daima
2.  Wale wanaotumia uchawi
3. Wale ambao wanavunja uhusiano na majamaa zao .
Mtu yeyote anayetumia pombe atapewa kinywaji kutoka mto unaoitwa Guta.  Kinywaji hiki kitakuwa kina uchafu na usaha kutoka kwa malaya na kitakuwa kikitoa harufu mbaya sana na kwa hakika kitakuwa kiki­wauma sana wale wote watakaokuwa wakiishi Jahannam.

Mtume s.a.w.w. amesema kuwa:"Mtu yeyote atakayekuwa akiwauzia pombe Mayahudi, Wakristo, au makafiri basi huyo mtu atakuwa anapata madhambi sawa na yeye mwenye kuinywa pombe hiyo.  Kwa hiyo mtu asiseme kuwa ninawauzia pombe makafiri hivyo mimi sina madhambi, pombe ni kitu kibaya kwa binadamu wa kila aina awe Mwislamu awe kafiri kwa hivyo atakayewauzia pombe hata makafiri atapata madhambi sawa sawa na mtu anayekunywa pombe yenyewe.Vile vile Mtume s.a.w.w. amesema kuwa:"Watu wasiende kumwangalia na kumjua hali mgonjwa ambaye ni mlevi na wala wasiungane katika mazishi ya mlevi huyo.Vile vile ameendelea kusema ushahidi wa mlevi usikubaliwe na wala msiwaoze watoto wenu kwa walevi.Ameendelea kusema Mtume s.a.w.w. kuwa:  "Chochote kile kisikubalike kutoka kwa mlevi."

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Mlevi siku ya Qiyama uso wake utakuwa umegeuka kuwa mweusi na ulimi wake utakuwa umevutwa ukining'nia mpaka mate yatakuwa yakimdondokea kifuani mwake. Mlevi huyo atakuwa akipatiwa maji au kinywaji kutoka kisima ambacho kitakuwa kimejaa usaha wa miili ya watendao maasi yaani malaya. Allah swt, Malaika, Mitume na waumini wote kwa pamoja wanawalaani walevi. Wakati mtu anapokuwa amelewa  imani yake inamtoka na nafasi hiyo inachukuliwa na mashetani.

Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:  "Mtu yeyote anapolewa ibada zake za siku arobaini hazikubaliki. Na lau hatasali basi atapata adhabu mara mbili."

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema kuwa: "Mlevi sala zake za siku za arobaini hazikubaliwi na iwapo atakufa katika kipindi hicho basi ataingizwa katika Jahannam moja kwa moja." 

Abu Salehe alimuuliza Imam Jaafer Sadiq a.s.iwapo kuna ubaya wowote katika kumnywisha mtoto mchanga azaliwapo pombe kwa sababu ilikuwa katika desturi na mila zao.Basi Imam a.s. alimjibu:"Allah swt  atawanywesha maji moto sana yakitokota wale wote watakaowanywesha watoto wa­changa pombe".

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Mtu yeyote atakayemuoza binti yake kwa mlevi, basi huyo mtu amejibu­ruta katika Jahannam. Vile vile amesema mtu yeyote asimuoze binti wake kwa mlevi na wala asimkubali binti wa mlevi kwa harusi na wala mtu yeyote asiende kumwangalia mlevi anapougua.  Mlevi siku ya Qiyama uso wake utaonekana mweusi, macho yake yakiwa majivu, uso wake ukiwa hauna sura nzuri ukiwa umeoza na ulimi ukiwa umening'inia chini. Amesema ni dhambi kabisa kunywa pombe. Mtu anapokunywa pombe anaacha sala, hamtambui mama, dada au binti yake na daima huwa amepoteza fahamu zake. 

Ameendelea kusema iko nyumba ya maasi na nyumba hiyo ina mlango uliotiwa kufuli na ufunguo wa nyumba hiyo ni pombe.  Kwa hiyo inamaanisha kuwa pombe ni mama wa maovu yote. Mtu yeyote anayekunywa pombe ni sawa na mtu anayeabudu miungu. Kwa sababu katika hali hiyo hakubali Quran kuwa ni kitabu kilicho kweli kwani lau akikubali kuwa ni Kitabu kilicho kweli na sahihi basi asingekunywa pombe kitu ambacho kimeharamishwa katika Quran tukufu.

Ameendelea kusema Imam a s. kuwa : "Mtu yeyote atakayempa mlevi  punje ya chakula au hata tone la maji, basi Allah swt atamuwekea kaburini nge mkubwa sana mwenye meno ambayo yatakuwa marefu kiasi cha mikono mia moja na kumi na atakuwa akipatiwa maji kutoka Jahannam Kutimiza mahitajio ya mlevi ni sawa na kuwaua waumini elfu moja na kuibomoa Al-Kaaba kwa mara elfu moja. Malaika elfu sabini wanamlaani yule mtu anayemsalimia au anayemheshimu mlevi.Jibrail, Mikail, Israfil,Mitume na Maimamu wote wanawalaani wale watu wote ambao wanachukua pombe hata tone moja.

Siku ya Qiyama atatokezea nge mkubwa mno katika uwanja na atasema:  "Wako wapi wale watu ambao walikuwa wakipigana na Allah swt  na Mtume wake?" Jibrail atamuuliza ni akina nani alikuwa akiwatafuta. Nge  huyo atasema:  "Yeye alikuwa akiwatafuta watu wa aina tano."
1.  Wale ambao wameacha sala
2.  Wale walioacha kulipa zaka
3.  Wale wanaopokea riba
4.  Wale walio na tabia ya kunywa pombe             
5.. Wale ambao wamezoea kuzungumzia mazungumzo ya dunia wakiwa misikitini.

Mtu mmoja alimwuliza Imam Jaafer Sadiq a.s. kuhusu kuwapo kwa pombe juu ya meza ya chakula.  Imam alimjibu: "Ni haramu kula chakula juu ya meza hiyo." Vile vile Imam a.s. amesema: "Watu wasiwe wakikaa na walevi kwa sababu walevi daima huwa wanalaaniwa na wale wanaokaa nao pia wataathirika kwa laana hizo."

Imam Mohammad Baqir a.s. amesema kuwa Allah swt anawalaani watu wa aina kumi wanao shirikiana ka­tika utengenezwaji wa pombe nao ni:-
1. Wale wanaopanda mbegu ya miti ambayo mazao yake yanatumika katika
 kutengenezea pombe
2.   Wale ambao wanaangalia na kuitunza miti hiyo.
3.   Wale wanaotengeneza juisi yake
4.   Wale wanaohudumia, wanaotawanya wanaogawa pombe
5.   Wale wanakunywa hiyo pombe
6.   Wale wanaopakia au kusafirisha hiyo pombe
7.   Wale wanaochukua hiyo pombe
8.   Wale wanaouza hiyo pombe
9.   Wale wanaonunua hiyo pombe
10.  Wale wanaolipia hiyo pombe.

Allah swt anazuia matendo mema yaliyofanywa na mtu katika kipindi cha miaka arobaini ya mtu ambaye anawasalimia au anawatolea heshima au anayepeana mikono na walevi. Ameendelea kusema: "Kumsaidia mlevi ni sawa sawa ni kuwasaidia wale ambao wanataka kuuvunja na kuuharibu Uislamu," na vile vile amesema : "Kumpatia mkopo mlevi ni sawa sawa na kumuua Mumiin."
Hivyo msomaji tumejaribu kuangalia kwa muhtasari tu kuhusu maovu na hatari na vile Uislamu unavyosema kuzungumzia pombe kwa kuwa kitabu hiki kidogo kinazungumzia mambo mengine kuhusu mambo ya ndoa n.k. hivyo hatuna muda wa kuzungumzia mambo juu ya pombe, hata hivyo maudhui haya yamezungumziwa na watu wengi Mashekh na madaktari kwa mapana zaidi na vile vile ukiweza kubahatika unaweza kutuandikia kwa anwani yetu juu ya kitabu kinachozungumzia mambo mawili ambayo yameungan­ishwa katika Quran: pombe na kamari maovu haya mawili katika jamii yetu ni maovu sana na mimi nimetunga kitabu kimoja juu ya kamari mbali peke yake na kipo kitabu kimoja kinazungumzia juu ya habari ya pombe,na anwani yangu ipo hapo nyuma katika ukurasa wa maneno machache.

Lau utapenda kupata kitabu hicho usisite kutuandikia tutajitahidi kukutumia. 

11. Zinaa

Kama vile Uislamu unavyolaani pombe vile vile inalaani vikali sana zinaa, kwa uchache ninawaletea mazungumzo na Hadithi juu ya suala hili.

Allah swt ametuamrisha katika Quran kuwa siku ya Qiyama mwenye kutenda zinaa ataadhibiwa mara dufu na daima atakaa katika moto wa Jahannam.

Imeelezwa katika kitabu Tafsir-i-Safi  kuwa miongoni mwa chemichemi za Jahannam moja inaitwa Asam ambamo badala ya maji inatiririka shaba iliyoyeyushwa.  Maumivu ya chemichemi hizi inazidi hata adhabu za ahera na adhabu za Jahannam. Wale watakaotupwa katika chemichemi hii inayotokota ni wale ambao wanamwabudu mtu mwingine mbali na Allah swt, na wale ambao wamewaua wale watu ambao wameharamishwa kuuawa na wale watu watendao zinaa.

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera
Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni:-
1.  Wanapoteza nuru 
2.  Wanakuwa maskini
3.  Maisha yao yanakuwa mafupi.

Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:-
1.  Allah swt atakuwa amewakasirikia mno
2.  Watahesabiwa siku ya Qiyama kwa Sharia kali
3.  Wataishi milele Jahannam.

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Manukato ya Jannat yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannat."

Kuna Hadithi isemayo kuwa mwenye kufanya zinaa na mwenye kufanya Ulawiti watakuwa wakinuka kama nyama ya mizoga siku ya Qiyama hadi watakapoingizwa Jahannam.  Na kwa kweli watu wataudhika na kud­hurika kwa harufu zao hizo mbaya. Na wala hakuna matendo yao mema yeyote yatakayokubalika na kwamba matendo yao yote hayo yatakuwa yametupiliwa mbali.Watapigiliwa misumari katika masanduku ya maiti.  Watakuwa wamepewa adhabu kubwa kweli kweli kiasi kwamba iwapo mishipa yao watafungwa watu laki nne wote watakufa kwa kuathirika na adhabu watakuwa wakipata watu kama hao.Na watu kama hao ndio watakaopata adhabu kubwa kabisa katika wakazi wa Jahannam.

Mtu yeyote iwapo ni mtumwa au mtu mwingine yeyote afanyapo zinaa na Mwislamu, Myahudi, Mkristo, au mwanamke mwingine, Allah swt atamfungulia milango laki tano katika kaburi ambamo wataingia nyoka, nge na miale ya mioto ambavyo vyote hivyo vitakuwa vikimuadhibu na kumteketeza humo hadi siku ya Qiyama wakati watu wote watakapokuwa wamekusanyika siku ya Qiyama, watu kama hawa watakuwa wakitoa harufu mbaya katika sehemu zao za siri, kiasi kwamba watu wengine wote watakuwa wakiona udhia, na harufu hii itaendelea kutoka hadi watakapoingizwa Jahannam. 

12. Magonjwa

Wanawake : Leucorrhoea

Kuna wakati wanawake wanatokwa na maji meupe au ya rangi ya njano yaani maji maji hayo ni kama usaha kutoka sehemu zao za siri na maji haya yanakuwa yenye kuondoa raha mwilini nayo yanaitwa Leucorrhoea
wanawake walio na ugonjwa kama huo wanaweza kuingizwa katika makundi manne yaani:-
                1.  Wasichana wadogo
                2.  Mabinti waliokua
                3.  Wanawake walioolewa
                4.  Wanawake wenye umri mkubwa

 

1.  Wasichana wadogo: 

Wasichana hawa wanaanza kutokwa na maji kama hayo kwa sababu ya uvimbe unaotokea katika sehemu zao za siri.Inaweza kuonekana iwapo msichana atalala kwa wima na ukiangalia sehemu yake ya siri utaona imevimba imekuwa rangi nyekundu na imejawa na usaha na maji maji kama haya na sababu kuu zinazofanya hali hii kutokea ni kama zifuatazo:-
(i)Kuna jarasimu za aina nyingi sana juu ya ardhi ambapo uchafu umechanganyikana hivyo jarasimu hizo zimeingia katika sehemu za siri za watoto kwa sababu wanapokuwa wakicheza kwenye udongo nje na wanakuwa hawakuvaa chupi na matokeo yake ni uvimbe wa aina hiyo.Na lau hali hii haitapewa umuhimu wa kutibiwa basi utaishia katika ugonjwa Leucorrhoea.

(ii)Kuna vijidudu vya aina fulani ambavyo vinaishi katika majumba ambayo haina upepo wa kutosha.Na minyoo hiyo inawauma watu wanapokuwa wamelala hivyo minyoo hiyo inapouma sehemu za siri za msichana pia inaweza kusababisha ugonjwa huo.

(iii)Majeraha  yanayopatikana kwa sababu ya ajali katika sehemu ya siri ya mwanamke pia inasababisha ugonjwa kama huo.

(iv) Hali ya baridi pia inachangia katika ugonjwa huu.

Katika kutibu sehemu hizi inabidi zioshwe vyema kabisa na kusafishwa na pamba au kitambaa safi kilichochovya katika maji ambamo borax imechanganywa. Borax ni aina ya dawa inayotumika katika matibabu kama haya na lau hakutaonekana dalili ya kupona ugonjwa huo basi inashauriwa kumuona daktari haraka sana iwezekanavyo.

2.  Wasichana wa makamu

Sehemu za siri za wasichana wasioolewa pia huwa inavimba na kutoa maji maji kama hayo wao pia hupata maumivu madogo madogo katika sehemu ya chini ya tumbo lao na huongezeka pale wanapokaribia vipindi vyao vya damu ya mwezi ( haidh ).Kwa sababu moja kubwa ya ugonjwa huo katika kikundi hiki kuwa matamanio yao yanakuwa hayakutimizwa.

Katika hali ya wasichana kama hawa hakuna matibabu yake.Hata hivyo wanatakiwa wapewe mapumziko, vyakula vizuri na vile vile wawe wakilala kwa kiasi wakiwezacho. Jambo tunaloshauri suluhisho kama hili ni kuwa msichana wa hali kama hii waozwe haraka iwezekanavyo.

3.  Wanawake walioolewa

Wanawake walioolewa wanapopata maumivu wakati wa kusuhubiana basi wajue kuwa ni onyo kuwa watapata ugonjwa huu. Hivyo waume zao inawabidi wawe wavumilivu na wenye subira kwa sababu kusuhubiana kupita kiasi kutaleta ugonjwa huu wa Leucorrhoea.

Wakati mwanamke anapozaa, mdomo wa kifugo chake unapanuka na moja ya sababu ya ugonjwa huo ni hiyo na lau mwanamke huyo atatibiwa vyema basi ataweza kuepukana na ugonjwa huo lakini kama hakupata mati­babu sahihi basi ugonjwa huu hautaweza kutokezea.

Mwanamke kutopata haidh, kusuhubiana wakati huo  na kushindiliana zaidi kunasababisha ngozi za sehemu za ndani ya sehemu za siri ya mwanamke kuvimba  na hii pia ni sababu mojawapo.

4. Wanawake wenye umri mkubwa

Si kwamba wasichana wadogo na wanawake ndio wanaopata ugonjwa huu bali hata wanawake wa makamu wanaathirika na ugonjwa huu. Kutokujali vyema katika umri wa vijana, ugonjwa wa kisukari na mabadiliko katika umri wa mwanamke huyo inachangia katika ugonjwa huu kwa wanawake wa makamu. 

Matibabu

Ugonjwa huu ni kwa sababu ya uvimbe unaotokana katika sehemu za siri ya mwanamke ndani mwake na sababu kubwa inatokana na damu yake kuwa chafu, kutoiva chakula vizuri tumboni, yabisi, n.k.Hivyo sababu hizi ziondolewe wakati huo huo kunapofanywa matibabu yaani dawa zake.

Inaonekana kuwa mwanamke anapata raha kidogo wakati anapochukua pamba iliyorowanishwa katika maji yenye kemikali ya borax na kuweka katika sehemu za siri za mwanamke kwa muda wa masaa ishirini na manne hadi arobaini na nane kwa hivyo iwapo hili halitamsaidia basi aonane na madaktari au awaulize wazee wanaoweza kumsaidia kwa madawa ya kienyeji ili akapona na aweze kujisikia raha starehe.

Wanaume

Spermatorrhoea

Imeonekana kuwa vijana wengi wana matatizo wa ugonjwa huo wa spermatorrhoea.  Kuna malalamiko ya aina mbili katika kupungua nguvu kwa kiume katika kusuhubiana, nazo ni :-
1.  manii  inamwagika wakati mtu akiwa usingizini au katika mkojo
2. Mwanamme, ingawaje anakuwa na hamu ya kusuhubiana na mwanamke hawezi kuusimamisha uume wake au anapousimamisha, hatokwi na manii. Hivyo katika kufanya matibabu ya magonjwa kama haya inabidi mtu afanye dawa ambayo itamsaidia.Hata hivyo kabla ya kufanya matibabuhayo inabidi mtu mwenye magonjwa ya yabisi n.k. ayatatue kwanza.Itambidi mtu aangalie hali ya hewa ya wakati na hali ya mwili wake na mazingara kabla ya kuingilia matibabu ya matatizo yake hayo.

21.  HUKUMU ZA NDOA.


Kwa mujibu wa fatawa za Alhaji Sayyed  Ali  Huseyn  Sistan, Najaf- Ashraf,Iraq.

Kwa sababu ya mkataba wa ndoa ndipo mwanamke anahalalishwa kwa mwanamme na vile vile mwanamme anahalalishwa kwa mwanamke,na mkataba huu upo wa aina mbili mkataba wa kwanza ni wa kudumu na mkataba wa pili ni muta'. Tofauti baina ya mikataba hii miwili ni kwamba katika mkataba wa daima mwanamke anapoolewa hautambulishwi muda fulani kwa hivyo inadumu umri wao mzima, na muta' humo kunatajwa muda wa kuishi kwa ndoa hiyo; yaani mtu wanaweza kuoana na mwanamke kwa mapatano ya kwa saa moja au siku moja au mwezi mmoja au mwaka mmoja au muda mwingine wowote; lakini muda huo usizidi umri wa mwanamke au umri wa mwanamme kwa sababu katika sura hii ndoa hii itakuja kuwa batil;  na ndoa hii inajulikana kama ndoa ya muta'. Ndoa hii ya muta' itazungumziwa peke yake katika kitabu hiki katika sehemu ya pili hivyo kwa habari zaidi na undani zaidi vitapatikana katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. 

(2372) Ndoa iwe ya kudumu au ya muda mfupi ni lazima sigha isomwe , kwa mwanamke na kwa mwanamme kuwa radhi nakuandika kwao hakutoshi. Itambidi mwanamke na mwanamme wasome wenyewe hiyo sigha ya ndoa ama wamtafute wakili ambaye atasoma kwa niaba yao.

(2373) Wakili huyo sio lazima awe mwanamme vile vile mwanamke anaweza akawa wakili wa upande wowote huo.

(2374)  Hadi hapo mwanamke na mwanamme watakapokuwa yakini kuwa mawakili wao wameisha soma sigha ya ndoa basi hapo huyo mwanamke na mwanamme watakuwa hawajahalalishwa na hivyo hawawezi hata kutazamana, na kwa kukisia kuwa mawakili wao wamesoma sigha vile vile haitoshelezi lakini mawakili wao wakisema tumesoma sigha lakini wao kama hawakuridhika au hawakuyakini basi kuamini ni swala la mashaka. 

(2375)  Iwapo mwanamke atamteua wakili wake amsomee sigha amsomee nikah na mtu fulani kwa muda wa siku kumi na hakumtajia mwanzo wa siku kumi hizo basi wakili siku atakayoichagua ndio itakuwa mwanzo wa siku kumi hizo, lakini iwapo wakili huyo atajua mwanamke huyo alikuwa akikusudia siku fulani au saa fulani basi itambidi asome hiyo sigha kwa mujibu wa yule mwanamke alivyotaka.

(2376)  Katika ndoa ya daima au ya muda mfupi inawezekana mtu mmoja akawa wakili wa upande wa mwanamke na mwanamme na vile vile mtu anaweza kuwa wakili wa mwanamke wakati yeye mwenyewe anamuoa huyo mwanamke lakini ni ehtiyate mustahab kuwa ndoa isomwe na watu wawili.

Namna ya kusoma sigha ya ndoa.


(2377) Iwapo mwanamme na mwanamke watapenda wajisomee wenyewe sigha ya ndoa yao basi itawabidi kwanza watambulishe kiasi cha mahari yao na ndipo mwanamke aseme: "Zawwajtuka nafsi alaa sidaaqil ma'alum" yaani mimi kwa mahari ambayo imekubaliwa nimejifanya mke wako.

Hapo mwanamme atasema Qabiltu tazwija-yaani mimi nimekubali wewe kuwa mke wangu.  Na katika sura hii ndoa yao ni sahihi.

Iwapo ndoa hii sigha ya ndoa hii itasomwa na wakili yaani iwapo jina la mwanamme ni Ahmad na jina la mwanamke ni Fatima na hapo wakili wa mwanamke akasema: "Zawwajtu muwakkilaka Ahmad muwakkilati Fatima 'ala sidaaqil ma'alum" na katika upande wa wakili wa mwanamme atasema "Qabiltu tazwija li-muwakkili Ahmad 'alaa sidaaqil ma'alum"  Na hapo ndoa hiyo itakuwa sahihi.Vile vile ni ehtiyat-i-mustahab kuwa itambidi mwanamme au wakili wa mwanamme atamke maneno kwa mujibu wa maneno yaliyotamkwa na mwanamke au wakili wake,mfano iwapo mwanamke atatamka "zawwajtu" basi mwanamme naye itambidi aseme "Qabiltu tazwija" na wala asiseme  'Qabiltu nikah.'

(2378)Iwapo mwanamme na mwanamke watapenda wajisomee sigha ya ndoa yao hivyo baada ya kuafikiana muda na mahari wanaweza kujisomea wenyewe. Hivyo mwanamke ataanza "zawwajtuka nafsi fi muddatil ma'alumat 'alaal mahril ma'alum"  na hapo akimaliza mwanamme atasema "Qabiltu."  Kwa hapo ndoa itakuwa sahihi na iwapo wataweka mawakili wao basi wakili wa mwanamke atamwambia wakili wa mwanamme "zawwajtu muwakkilati fil muddatil ma'alumati 'alaal mahril ma'alum." na hapo wakili wa mwanamme baada ya kusubiri kwa punde atasema: "Qabiltu tazwija  limuwakkili ha-kadhaa " na ndoa yao itakuwa sahihi.

Masharti ya ndoa.


(2379). Ndoa ina masharti na machache ndiyo yameorodheshwa kama ifuatavyo:-

1. Katika misingi ya ihtiyat, sigha isomwe katika Kiarabu kilicho sahihi na lau mwanamke na mwanamme hawataweza kusoma katika Kiarabu basi wanaweza kusoma katika lugha nyingine wanayoijua wao vyema ambamo maana ya maneno  zawwajtu au Qabiltu  inafahamika vyema kwao.  Na si lazima kuweka wakili.

2. Mwanamme au mwanamke au mwakilishi wao, ambaye anasoma nikah yao, awe na nia ya 'insha'  (yaani ikifanywa kutekelezwa papo hapo).  Katika maneno mengine iwapo mwanamme na mwanamke wanasoma wenyewe nia ya mwanamke anaposema zawwajtuka nafsi ikimaanisha kuwa amekuwa mke wake papo hapo; na mwanamme kwa kusema Qabiltu tazwija basi huyo mwanamme amemkubalia papo hapo huyo mwanamke kama mke wake.Na iwapo wakili wa mwanamke na mwanamme ndiye anaye soma nikah ndoa, nia zao wanaposema zawwajtu na Qabiltu ziwe kwamba mwanamke na mwanamme waliowateua wao kuwawakilisha, papo hapo wamekuwa mtu na mke wake.

3.Mtu yeyote asomaye nikah ama iwe yake mwenyewe au awe wakili wa mtu mwingine, lazima awe mtu mwenye akili na fahamu timamu, na kwa tahadhari, awe baleghe pia.

4.Iwapo nikah inasomwa na mawakili au walezi wa mwanamke na mwanamme, lazima wawatambulishe mwanamke na mwanamme kwa kuwataja majina yao au kwa kutoa ishara ya kuwatambulisha wao.Hivyo iwapo mtu ana mabinti zaidi ya mmoja na yeye akamwambia mwanamme:  zawwajtuka ihda banaati  (yaani nimekuoza mmoja wa mabinti wangu kuwa mke wako) na mwanamme akasema Qabiltu  yaani nimekubali  (hapo ndoa hiyo itakuwa batil kwa sababu hakuna msichana aliyetambulishwani  msichana yupi.

5.Ni lazima mwanamme na mwanamke wawe radhi kuingia katika mkataba wa ndoa.Lakini iwapo mwanamke ataonekana akisita kutoa ruhusa ya ndoa hiyo, lakini inaonekana kuwa kimoyo amekubaliana nayo, basi ndoa hiyo iko sahihi .
(2380) Iwapo katika kusoma nikah hata herufi moja ikisomwa isivyo sahihi, kubadilika kwa maana, basi ndoa hiyo itakuwa batil.

(2381) Mtu yule ambaye anasoma nikah na anajaribu kuleta maana kwa ujumla, wakati akiwa na nia ya maana hiyo hiyo, hiyo ndoa itakuwa sahihi.  Si lazima kwa mtu huyo kuelewa maana halisi ilivyo ya kila neno au kujua kanuni za lugha ya Kiarabu.

(2382)  Iwapo ndoa ya mwanamke itasomwa bila ya ruhusa yake lakini baadaye mwanamme na mwanamke wakakubaliana na ndoa hiyo wakaridhiana, hiyo ndoa ni sahihi.

(2383) Iwapo mwanamme na mwanamke au mmoja wao, amelazimishwa kuingia katika mkataba huo, na wakaridhia baada ya nikah kusomwa basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi, ingawaje ni vyema iwapo nikah hiyo itasomwa tena.

(2384)  Baba au babu wanaweza kufanya mkataba wa ndoa kwa ajili ya mvulana au msichana walio wadogo, au kwa niaba ya mvulana au msichana aliye na akili kasoro, lau watakuwa wamebaleghe na baada ya watoto kubaleghe au huyo mwenye akili kasoro akawa na akili timamu, basi wao wanauwezo wa kuiweka hiyo ndoa ikaendelea au kuikatisha iwapo kuna mambo maovu yaliyopo katikati.Lakini iwapo mmoja wa watoto hawa ambao bado hawajabaleghe watakataa hii ndoa, basi katika hali hii udharuri wa tahadhari talaqa au kusomwa tena kwa ndoa, hali itakayokuwapo lazima isomwe.
(2385)  Iwapo msichana atafika wakati wa kubaleghe na bado yu bikira na yuko Rashida (yaani anaweza kuamua kwa ajili ya masilahi yake) anataka kuolewa, basi itambidi apate ruhusa ya baba wake au ya babu wake mzaa baba, ingawaje atakuwa yeye akijitazama mwenyewe katika maswala yake.Hata hivyo si lazima kwake kwa msichana huyo kupata ruhusa ya mama au  kaka yake.

(2386)  Katika sura zifuatazo haitakuwa lazima kwa mwanamke kupata idhini ya baba au babu mzaa baba kabla ya kuolewa:

1.   Iwapo yeye si bikira
2.   Iwapo yeye ni bikira lakini baba au babu mzaa baba yake wanamkatalia
     idhini ya kuolewa na mwanamme ambaye ni mwema katika macho ya
     Sharia na vile vile katika tamaduni na desturi zao.
3.   Iwapo baba na babu mzaa baba hakubali kushiriki katika ndoa.
4.   Iwapo baba au babu mzaa baba hawako katika hali ya kutoa idhini, mfano
      hawana akili timamu, n.k.
5. Haiwezekani kupata idhini yao kwa sababu ya kutokuwapo kwao, au kwa
    sababu zingine kama hizi, na mwanamke anataka kuolewa haraka.

(2387) Iwapo baba au babu mzaa baba watafanya mkataba wa ndoa kwa niaba ya mtoto wao wa kiume ambaye hajabaleghe bado na huyo mtoto wa kiume atakapobaleghe itabidi kumlipia gharama zote mke wake.Na hata kabla ya kubaleghe kiasi kwamba huyo anakuwa na umri wa kuweza kuona raha ya mwanamke huyo na mwanamke asiwe mdogo sana kiasi kwamba asiweze kuwa na uhusiano wa kusuhubiana na bwana wake. Na katika hali mbali na hizi, kuwe na dalili za kuthibitisha kuwa anahitaji kugharamiwa mume wake hivyo kuwepo na maafikiano ikiwa ni njia ya tahadhari.

(2388)  Iwapo baba au babu mzaa baba wataingia katika mkataba wa ndoa kwa niaba ya mtoto wao asiyebaleghe itawabidi walipe mahari iwapo mtoto hana uwezo wake , au iwapo mmoja wao atakayechukua jukumu la kulipa mahari hayo. Katika hali nyingineyo, baba au babu mzaa baba wanaweza kulipa mahari kutoka milki ya mtoto, lakini kisizidi kiasi cha mahari ya kawaida inayotolewa katika sura kama hii.Lakini iwapo hali ya wakati huo itadai kulipiwa mahari zaidi, basi watalipa kutoka milki ya mtoto, na sivyo vinginevyo, hadi hapo mtoto mwenyewe atakapokubaliana nayo baada ya kubaleghe.

Bibi  na bwana wanaweza kuvunja ndoa

(2389)  Iwapo mwanamme atakuja kujua baada ya kusomewa nikah (ndoa) kuwa mke wake wakati wa kusomewa mkataba wa ndoa alikuwa na kasoro mojawapo ya sita zifuatazo basi anaweza kubatilisha ndoa:-
1.  Kichaa (hata kama kinakuja kwa muda fulani),
2.  Ukoma
3.  Magonjwa mabaya ya ngozi
4.  Kipofu
5.  Mlemavu, hata kama sio kiasi cha kutambaa ardhini,
6.  Kuwapo kwa kipande cha nyama au mfupa katika ndani mwa sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo linaweza au lisiweze mwanamke kuingiliwa au kushika mimba  na iwapo mwanamme atatambua kuwa mke wake wakati wa kusomewa nikah, alikuwa ana ugonjwa unaoitwa Ifza' -yaani njia ya mkojo wake na vipindi vya damu vimekuwa moja au njia yakupitia damu ya haidh na njia ya kupitia choo imekuwa moja, katika sura hii mwanamme hawezi kubatilisha ndoa yake. Kwa tahadhari ya lazima itambidi kumpa talaqa iwapo itabidi kuvunja ndoa hiyo.

(2390)  Mwanamke anaweza kubatilisha ndoa katika sura zifuatazo hata bila ya kupewa talaqa:
1. Iwapo atajua kuwa mume wake hana sehemu zake za siri (uume wa
   mwanamme).
2.  Iwapo atajua kuwa uume wa bwana wake umekatwa kabla au baada ya
    kusuhubiana.
3.  Iwapo bwana wake ana ugonjwa unaomfanya asiweze kusuhubiana, hata
   kama ugonjwa huo umetokezea  baada ya ndoa  au baada ya kusuhubiana.

(2391). Iwapo mwanamke atavunja ndoa kwa sababu ya mume wake hawezi kusuhubiana naye, basi itambidi mume ampe nusu ya mahari waliyopatana. Lakini iwapo mwanamme au mwanamke atavunja ndoa kwa sababu ya kasoro moja au nyingine kama zilivyoelezwa hapo juu, na kama hawajasuhubiana, basi mwanamme hatatakiwa kumlipa chochote mwanamke.Lakini iwapo bibi na bwana walisuhubiana, basi itambidi mwanamme amlipe huyo mke wake mahari kamili.Iwapo mwanamme atavunja ndoa kwa sababu ya kasoro kama zilivyoelezwa katika  mas'ala 2389, basi katika sura hii kama hawajasuhubiana mwanamme hatatakiwa kulipa chochote. Na iwapo mwanamme alisuhubiana na mke wake basi itambidi amlipe mahari kamili. 

Wanawake ambao kuwaoa ni haramu.

(2392)  Wafuatao ambao ni mahram kwa mwanamme ni haramu kuwaoa, nao ni:- Mama mzazi, dada yake, binti yake, shanghazi na wifi  wake,binti wa kaka yake, binti wa dada yake na mama mkwe.
(2393)  Mwanamme anapomuoa mwanamke kuanzia hapo mama mkwe bibi mzaa mke wake, bibi mzaa baba yake na wanawake wote walio katika mstari huu ni mahram wake,( maana yake ni wale wasioruhusiwa kuolewa nayeye), hata kama huyo mwanamme atakuwa hakusuhubiana na mwanamke huyo aliyemuoa.

(2394)  Mtu anapooa mwanamke, na akasuhubiana naye, basi watoto wa huyo mke wake na wajukuu wa mke huyo (wa wanaume au wasichana ) na kizazi mfululizo kinachotokana hapo kuanzia huyo mwanamme wote kwa pamoja wanakuwa mahramBila ya kujali kuwa hao wote walikuwapo wakati wa kusomwa ndoa au walizaliwa baada ya ndoa yao. 

(2395) Iwapo mwanamme ataoa mwanamke, na hakusuhubiana, basi ni tahadhari ya lazima kuwa muda utakao dumu ndoa yao, asimuoe mtoto wa mke huyo. 

(2396)  Shanghazi na wifi  wa mwanamme kwa upande wa baba na mama yake, na shanghazi na wifi kwa upande wa baba yake, na shanghazi na wifi wa mababu zake, na shanghazi na wifi wa mama yake na shanghazi na wifi wa bibi mzaa mama, na vile mfululizo unavyoendelea nyuma, hao wote ni mahram wake.

(2397) Baba na babu wa mume, hata mfululizo huu utakavyo kwenda ni mahram wa mwanamke wa bwana huyo.Vivyo hivyo watoto wa kiume na wajukuu wa kiume (watoto wa watoto wa kike ), vyovyote vile mfululizo huu utakavyokwenda chini, pia ni mahram wakebila kujali iwapo hao walikuwapo wakati wa ndoa yake au walizaliwa baadaye.

(2398) Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke, (iwapo ndoa yao ni ya kudumu au ndoa ya muta') kamwe hawezi kumuoa dada wa mke wake, wakati mwanamke huyo bado ni mke wake.

(2399) Iwapo mwanamme atampa mke wake talaqa inayoweza kurudiwa, kama vile itakavyokuwa inaelezwa katika Sharia zinazohusiana na talaqa, basi hawezi kumuoa dada wa mke wake wakati mke akiwa katika Iddah. Lakini iwapo hiyo ni talaqa inayoweza kurudiwa, basi anaweza kumuoa dada wa mke wake.Na kama ni Iddah ya muda mfupi  (muta'),tahadhari ya lazima ni kuwa mtu hapaswi kumuoa dada wa mke katika kipindi hicho.

(2400)  Mwanamme haruhusiwi kumuoa binti wa kaka au dada wa mke wake bila idhini ya mke wake.  Na lau kama ataoa bila idhini ya mke wake, na hapo baadaye mke wake akaridhia ndoa hiyo, basi itakuwa ni sahihi.

(2401) Iwapo mwanamke atakuja kufahamu hapo mbeleni kuwa bwana wake ameoa binti wa dada yake au kaka yake huyo mwanamke na akakaa kimya, na hapo baadaye akaridhia ndoa hiyo, itakuwa ni sahihi. Na lau mwanamke huyo hataridhia  hapo baadaye ,ndoa hiyo itakuwa batil.

(2402) Iwapo mwanamme kabla ya kumuoa binti wa shanghazi au wifi yake (Mungu atuepushe nayo ) akasuhubiana na mama mkwe, basi hawezi kumuoa huyo msichana kwa misingi ya tahadhari.

(2403) Iwapo mwanamme ataoa watoto wa wifi au watoto wa shanghazi wake na baada ya kusuhubiana na mke wake akasuhubiana na mama wa mke wake huyo, basi tendo hili halitakuwa sababu ya kuachana (ndoa yao itaendelea). Na Sharia kama hii itatumika iwapo huyo mwanamme atasuhubiana na mama wa mke wake baada ya kusomewa ndoa, lakini kabla  hajasuhubiana na mke wake, ingawaje tahadhari iliyosisitizwa mno katika sura hii ni kwamba huyo mwanamme ajitoe mbali kwa kumpa talaqa

(2404) Iwapo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke mbali na shanghazi na wifi wake, ni tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa asioe binti wa mama. Kwa hakika, na kama atamuoa, na atafanya zinaa na mama wa mke wake kabla ya kusuhubiana na mke wake, basi tahadhari iliyosisitizwa mno ni kwamba ajitenganishe naye, lakini iwapo huyo mwanamme akasuhubiana mke wake baada ya ndoa, na hapo baadaye ndipo akaja akafanya zinaa na mama wa mke wake, basi katika sura hii sio lazima kwake kutengana na mke wake. 

(2405) Mwanamke wa Kiislamu hawezi kuolewa na mwanamme asiye Mwislamu, na vile vile mwanamme wa Kiislamu hawezi kumuoa mwanamke asiye Mwislamu ambao sio katika Ahlul kitab.hata hivyo hakuna ubaya kwa kuingia katika mikataba ya ndoa ya muda mfupi (muta'') pamoja na Mayahudi pamoja na wanawake wa Kiyahudi na wanawake Wakristo, lakini tahadhari ya lazima mwanamme wa Kiislamu asiwachukue hawa katika ndoa yao ya kudumu.  zipo baadhi ya madhehebu kama Khawarij, Ghulat, na nasibi ambao wanajitambulisha na kudai kuwa wao ni Waislamu, lakini wametenganishwa kuwa si Waislamu. Wanaumme Waislamu na wanawake hawawezi kuoa au kuolewa ndoa ya kudumu au muta' pamoja na watu hao.

(2406) Iwapo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke ambaye yupo katika Iddah ya talaqa inayoweza kurudiwa, kama tahadhari huyo mwanamke atakuwa ni haramu kwa ajili yake. Na iwapo huyo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke ambaye yupo katika Iddah  ya muda mfupi, au ndoa isiyoweza kurudiwa, au katika Iddah ya kifo cha mume wake, basi anaweza kumuoa huyo mwanamke hapo baadaye, ingawaje ni tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa yeye asimuoe mwanamke huyo. 

Maana za talaqa za kurudiwa na kutokurudiwa, na Iddah za muta'na Iddah za kifo, zinazungumziwa vyema katika vitabu vya fiqh katika sura za talaqa.

(2407) Iwapo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke ambaye hajaolewa na ambaye hayuko katika Iddah yoyote ile, kama tahadhari huyo mwanamme hawezi kumuoa huyo mwanamke hadi hapo amefanya tawba  ya Allah swt na ameomba msamaha kwake.Lakini iwapo atatokezea mtu mwingine wa kumuoa huyo mwanamke kabla ya mwanamke huyo hajafanyatawba ya kuomba msamaha kwa Allah swt,basi hakuna mushkeli. Iwapo mwanamke huyo akaja kujulikana kuwa ni malaya katika sura hii haitaruhusiwa kumuoa huyo mwanamke hadi hapo amefanya tawba wazi wazi na kuomba msamaha wa Allah swt. Na katika misingi hiyo hiyo haitaruhusiwa kuolewa na mwanamme ambaye anajulikana kuwa yeye anajihusisha katika mambo ya malaya hadi hapo huyo mwanamme atubu kidhahiri na aombe msamaha wa Allah swt.Na iwapo mwanamme atataka kumuoa mwanamke ambaye amejulikana kufanya zinaa pamoja naye au amezini pamoja na mwanamme mwingine basi itambidi kwa misingi ya tahadhari,asubiri hadi huyo mwanamke awe tohara kutokana na haidh.

(2408)  Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke ambaye yuko katika Iddah ya mwanamme mwingine, na lau wote kwa pamoja wanajua au mmoja wao anajua kuwa Iddah ya mwanamke huyo haijaisha, na wanatambua waziwazi kuwa kuoa mwanamke akiwa katika Iddah ni haramu, hivyo huyo mwanamke atakuwa ni haramu kwa milele kwa ajili ya mwanamme huyo hata kama huyo mwanamme baada ya kusomewa ndoa atakuwa hajasuhubiana na mwanamke huyo.

(2409)  Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke ambaye yuko katika Iddah ya mwanamme mwingine, na atasuhubiana naye, basi mwanamke huyo atakuwa haramu kwa ajili yake milele, hata kama yeye mwanamme atakuwa hakujua yeye mwanamke alikuwa katika Iddah, au hakujua kuwa ni haramu kumuoa mwanamke akiwa katika Iddah.

(2410)  Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke huku akijua kuwa mwanamke huyo anaye bwana, basi itambidi ajitenganishe naye na asimuoe kamwe maishani mbeleni.  Na Sharia kama hiyo ndiyo itatumika katika misingi ya tahadhari, kama yeye mwanamme hakujua kama yeye mwanamke ameolewa na anaye bwana, na vile vile huyo mwanamme alikuwa amesuhubiana na mwanamke huyo baada ya ndoa yake.

(2411)  Iwapo mwanamke aliyeolewa akafanya zinaa, yeye katika misingi ya tahadhari, atakuwa ni haramu wa milele kwa mtu aliyefanya zinaa naye, lakini hatakuwa haramu kwa mume wake aliyeolewa na ndoa halali.Na lau huyo mwanamke hatafanya tawba, na ataendelea na tabia yake hiyo ya kufanya zinaa basi itakuwa ni afadhali kwa bwana wake ampe talaqa, ingawaje itambidi amlipe na mahari yake.

(2412) Katika sura ya mwanamke ambaye amepewa talaqa au mwanamme ambaye yuko katika ndoa ya muta' na bwana wake amekiachia kipindi kilichobakia, au iwapo kipindi cha ndoa ya muta'kimekwisha, na baada ya muda akaolewa na bwana mwingine na hapo akaijiwa na shaka iwapo wakati wa ndoa yake ya pili lau Iddah ya bwana wake wa kwanza ilikwisha au haikuisha, basi itambidi apuuzie shaka hiyo.

(2413)  Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake.  Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti ni kijana ambaye hajabaleghe.  Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme  umeingia katika sehemu za choo au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake.

(2414)  Iwapo mwanamme atamuoa mama au dada wa kijana mvulana, na akamulawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.

(2415) Iwapo mwanamme ambaye yuko katika hali ya ihram (ni amri moja wapo inayotimizwa wakati wa kuhiji)  akaoa mwanamke, basi ndoa hiyo ni batil, na lau alijua kuwa kuoa katika hali ya ihram ni haramu, basi mwanamme huyo hawezi kumuoa mwanamke huyo

(2416) Iwapo mwanamke ambaye yuko katika hali ya ihram ambaye hayuko katika hali ya ihram, basi ndoa yake ni batil.  Na iwapo mwanamke huyo alielewa kuolewa katika ndoa ya Ihram ni haramu, katika misingi ya tahadhari ya faradhi, yeye mwanamke hawezi kamwe kuolewa na mwanamme huyo tena.

(2417)  Iwapo mwanamme hafanyi tawaf-un-nisa (ni amri mojawapo ya kutimizwa katika Hajj na umra mufrada ) basi mke wake na wanawake wengine watakuwa haramu kwa ajili yake, vile vile iwapo mwanamke hatafanya tawaf-un-nisa, basi bwana wake na wanaume wengine watakuwa haramu kwa ajili yake .Lakini ,iwapo wao (mwanamme au mwanamke )watatekeleza tawaf-un-nisa  hapo mbeleni, basi watakuwa halali.

(2418)  Iwapo mwanamme atafunga ndoa pamoja na msichana ambaye bado hajabaleghe ni haramu kusuhubiana naye kabla hajatimiza umri wa miaka tisa. Lakini iwapo atasuhubiana naye basi huyo msichana ambaye ni mke wake hatakuwa haramu kwa ajili yake hapo atakapobaleghe, hata kama atakuwa amedhurika na Ifza (sura iliyoelezwa katika hukumu Na,2388) ingawaje katika misingi ya tahadhari itambidi, ampe talaqa.

(2419)  Mwanamke ambaye amepewa talaqa mara tatu, atakuwa haramu kwa ajili ya mume wake.  Lakini ataolewa na mwanamme mwingine, kwa mujibu wa Sharia na kanuni zinazoelezwa vyema katika vitabu vya fiqh katika sura ya talaqa, bwana wake wa kwanza anaweza kumuoa baada ya bwana wake wa pili kufariki, au kumpa talaqa mwanamke huyo na itambidi akamilishe kipindi chaIddah

Hukumu za ndoa ya kudumu.


(2420)  Kwa mwanamke ambaye ameolewa katika ndoa ya kudumu, ni haramu kwa ajili yake kutoka nje ya nyumba yake bila ya idhini ya bwana wake, ingawaje kutoka kwake huko nje hakutavunja haki za bwana wake.Vile vile itambidi ajitolee kwa ajili ya kusuhubiana na bwana wake, na kamwe asimuzuie mume wake kusuhubiana naye bila ya kuwa na sababu ya kiadilifu.  Na kiasi kwamba mwanamke huyo hataondoka katika misingi ya kutimiza wajibu wake, ni wajibu kwa mume wake kumpatia chakula, mavazi na nyumba ya kuishi. na lau bwana wake hatampatia vitu hivyo, bila ya kujali kama ana uwezo wa kumpatia vitu hivyo au hana basi atakuwa anadaiwa deni na mke wake.

(2421)  Iwapo mwanamke hatimizi wajibu wake wa kindoa kwa mume wake, basi hana ulazimisho wa chakula, nguo au nyumba kutoka kwa bwana wake hata kama akiishi naye.Lakini iwapo atagoma kumtii katika nyakati mbalimbali basi hukumu ya kiakili yetu inasema kuwa huyo mwanamke hatakuwa na haki ya kudai chochote kutoka kwa bwana wake. Lakini hukumu hii ni swala la ishkal.  Katika sura yoyote ile haimaanishi kuwa inapoteza haki zake za mahari.

(2422).  Mwanamme hana haki ya kumlazimisha mke wake kufanya kazi za nyumbani.

(2423) Gharama za usafiri za mwanamke ni lazima zilipwe na bwana wake, iwapo zitazidi kuliko gharama za nyumbani na iwapo atakuwa amesafiri kwa ruhusa ya bwana wake. Lakini kwa gharama za kusafiri kwa gari au kwa ndege n.k. na gharama zinginezo ambazo ni dharura katika safari, zitachukuliwa na mke mwenyewe, isipokuwa wakati ambapo bwana mwenyewe atataka kumchukua mke wake pamoja naye katika safari, ambapo katika sura hii bwana ndiye atakayegharimia gharama zote.

(2424) Iwapo bwana ambaye anawajibika kumlisha na kumtunza mke wake, hatimizi wajibu huo kwa mke wake, basi mke huyo anaweza kutoa gharama zake za maisha kutoka kwa milki ya bwana wake hata bila ruhusa ya bwana wake.  Na lau sura hii haitawezekana, na atalazimika mwanamke huyo kufanya kazi na kujilisha mwenyewe, na mwanamke huyo hawezi kupeleka swala lake mbele ya mujtahid  (kadhi au Hakimu wa Sharia) ambaye atamlazimisha huyo mwanamme (hata kwa kumtishia kwa kifungo cha jela, kulipa gharama za mwanamke, basi kuanzia pale mwanamke huyo atakapoanza kuchuma maisha yake haitakuwa faradhi kwa mwanamke huyo kumtii bwana wake.

(2425) Iwapo mwanamme kwa mfano ana wanawake wawili na hupitisha usiku kwa mmoja wao, hivyo ni wajibu kwake yeye kupitisha usiku mmoja kati ya usiku nne kwa mke wa pili; katika hali mbali na hii,si wajibu  kwa mwanamme kuwa pamoja na mke wake. Hivyo, ni lazima kwa mwanamme kutojitenga na mke wake kabisa. Na katika misingi ya tahadhari inambidi mwanamme apitishe usiku mmoja kati ya usiku nne akiwa pamoja na mke aliyemuoa kwa  ndoa ya kudumu.

(2426) Hairuhusiwi kwa mwanamme kutokusuhubiana kwa zaidi ya miezi minne pamoja na mke wake kijana na ambaye ameolewa kwa ndoa ya kudumu isipokuwa wakati kusuhubiana kule kunaleta madhara kwake au inahitaji nguvu na juhudi zaidi, au wakati ambapo mwanamke mwenyewe anakubali kutokusuhubiana kwa kipindi hicho au sharti liliwekwa na bwana wakati wa kufunga ndoa.Na katika Sharia hii, hakuna tofauti ya sura ya bwana anakuwapo au anapokuwa safarini au mwanamke huyu ameolewa kwa ndoa ya kudumu au kwa ndoa  ya muta'
(2427) Iwapo katika ndoa ya kudumu mahari hayajaafikiwa, basi ndoa hii ni sahihi na katika hali hiyo bwana alisuhubiana na  mke wake, basi itabidi amlipe mahari yote kamili ambayo itakuwa kwa mujibu kuwa mahari anavyolipwa mwanamke kwa kawaida kwa daraja lake.  Ama kuhusiana na muta'' hata hivyo kama mahari haijaafikiwa kuanzia mwanzoni basi ndoa hiyo itakuwa batil

(2428)  Wakati wa nikah ya ndoa ya kudumu, kulikuwa hakujaafikiwa wakati wa kulipa mahari, basi mwanamke ana ruhusa ya kumzuia bwana wake asisuhubiane naye hadi hapo atakapomlipa mahari yake, bila ya kujali iwapo bwana wake anaweza kumlipa au hana uwezo wa kumlipa.  Lakini iwapo huyo mwanamke atamkubalia mume wake asuhubiane naye kabla ya kupokea mahari, na mume wake akasuhubiana naye, basi kuanzia kusuhubiana kwao kwa mara ya kwanza mwanamke huyo kamwe hawezi kumzuia mume wake asisuhubiane naye bila ya kuwa na sababu za kuridhisha.

Muta'


(2430)Kufanya muta' (ndoa ya muda mfupi) pamoja na mwanamke ama kwa ajili ya kutaka raha ya kusuhubiana, au kwa sababu nyingine yoyote ile, basi ni sahihi.

(2431)Ni tahadhari ya faradhi kuwa mwanamme asikose kusuhubiana naye mwanamke aliyefanya naye muta' kwa kipindi cha miezi minne yaani inambidi isipite kipindi hicho bila kusuhubiana na mwanamke aliyefanya naye muta'.

(2432)Iwapo mwanamme aliyefanya muta' na mwanamke, ataweka shuruti kuwa mume wake huyo hatasuhubiana naye basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi na vile vile shuruti lake hilo pia linakubalika, kwa hivyo mume atafaidika kwa starehe zinginezo tu bila ya kusuhubiana naye.Hata hivyo iwapo atakubali kusuhubiana naye hapo baadaye,mwanamke anaweza kusuhubiana na bwana wake huyo, na sharti hili linatumika katika ndoa ya kudumu.

(2433)Mwanamke aliyeolewa kwa muta'hawi mustahiki wa kupewa gharama zake hata kama atashika mimba .

(2434))Mwanamke aliyeolewa kwa muta' hastahiki kulala na bwana wake, na wala hana urithi na bwana wake na wala bwana wake pia hamrithi mke wake aliyeolewa kwa muta'.Hata hivyo iwapo mmoja wao anaweka sharti na kurithiana basi swala hilo ni ishkal, lakini hata hivyo lazima ichukuliwe tahadhari katika kuweka maanani na utekelezaji wake.
(2435)Iwapo mwanamke ambaye ameolewa kwa muta' alikuwa hajui kuwa yeye si mustahiki wa gharama wala kulala na bwana wake lakini ndoa yake itakuwa sahihi bado, na kutokujua huko yaani kubakia katika hali ya ujahili vile vile atakuwa na haki ya kudai chochote kwa bwana wake.

(2436)  Iwapo mwanamke aliyeolewa kwa muta' atatoka nje ya nyumba bila ya ruhusa ya bwana wake na kwa vyovyote vile haki ya bwana wake itakuwa imevunjwa basi kutoka kwake nje ni haramu. Na iwapo haki ya bwana wake itakuwa imesalimika ichukuliwe tahadhari iliyosisitizwa kuwa mwanamke huyo asitoke nje ya nyumba bila ya ruhusa ya bwana wake.

(2437) Iwapo mwanamke atampa ruhusa mwanamme ya kuwa wakili wake katika kusoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo kwa kipindi fulani na kwa kiasi fulani cha mahari, na badala yake huyo mwanamme yaani wakili akasoma nikah ya kudumu pamoja na mwanamke huyo au anasoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo bila ya kubainisha wazi wazi kipindi cha muda au kiasi cha mahari, basi ndoa hiyo itakuwa batil. Lakini iwapo mwanamke ataridhia na kutoa ruhusa kwa mapatano hapo mbeleni basi ndoa hiyo itakuwa sahihi.

(2438)Ili kutaka kuwa mahram (yaani  ambaye huwezi kumuoa na anakuwa ni jamaa wako wa karibu ), baba au babu mzaa baba wanaweza kumuingiza mtoto wao asiyebaleghe au msichana wao asiyebaleghe  katika ndoa pamoja na mtu mwingine kwa kipindi kifupi,ili mradi haitatokezea ufisadi.Hata hivyo, iwapo wao watamuoza mvulana mdogo au msichana mdogo ambaye kwa vyovyote vile hawezi kupata starehe ya kusuhubiana katika kipindi hicho, basi katika sura hii usahihi wa ndoa kama hiyo ni ishkal.

(2439) Iwapo baba au babu mzaa baba wa mtoto asiyekuwapo, wakamuoza kwa mtu ili kutaka kuwa mahrambila kujua iwapo  mtoto yuko hai au amekufa, basi kusudi litapatikana iwapo katika kipindi katika ndoa, mtoto atakuwa na uwezo wa kusuhubiana. Iwapo hapo baadaye itakuja kujulikana kuwa mtoto huyo hakuwa hai wakati wa kusomwa ndoa hiyo basi itachukuliwa kuwa ni batil.Na wale wote ambao walikuwa ni mahram sasa watakuwa si mahram

(2440)Iwapo bwana atakuwa amempatia zawadi bibi wake aliyemuoa kwa muta' katika kipindi hicho, na atakapokuwa amemuachia na kama alikuwa amesuhubiana naye basi itabidi ampatie vitu vyote vile alivyokuwa ameahidi kumpa. Na lau kama alikuwa hajasuhubiana naye basi itambidi ampe nusu ya mahari yake, ingawaje achukue tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa itambidi ampemahari kamili.

(2441)Iwapo mwanamme ataingia katika muta' pamoja na mwanamke na mwanamke atakapokuwa katika kipindi cha Iddah kabla ya kuisha basi inaruhusiwa mwanamme kumuoa mwanamke huyo kwa ndoa ya kudumu au   ndoa ya muta'.

Kuwatazama wale wasio  mahram


(2442) Ni haramu kwa mwanamme kutazama mwili au nywele kwa mwanamke ambaye siyo mahram bila kujali iwapo ana nia ya kuona raha au sivyo, na kama kuna hatari ya kuangukia katika tendo bovu la kutenda madhambi au siyo. Vile vile ni haramu kutazama juu  uso na mikono  mpaka kufika katika vipingili vya mkono wa juu, ya wanawake kwa nia ya kuona raha au kuna hatari ya kuangukia katika madhambi, na katika hatua ya tahadhari iliyosisitizwa ni kuwa mtu asitazame sura zao au mikono yao hata kama ni bila sababu kama hizo. Vivyo hivyo ni haramu kwa mwanamke kutazama mwili wa mwanamme asiye mahram kwake, isipokuwa sehemu zile ambazo kwa kawaida  huwa hazifunikwi, kama uso,mikono, kichwa, shingo,na miguu. Mwanamke huyo anaweza kuona sehemu hizi za mwanamme bila ya kuwa au kutaka raha au iwapo kutakuwa au kama hakutakuwa na hatari ya kutumbukia katika matendo ya madhambi.

(2443)Kuangalia mwili wa mwanamke ambaye hajali kuhusu hijab hata kama atakuwa ameshauriwa si haramu, ili mradi haitamtumbukiza mtu katika matendo ya madhambi au raha ya kusuhubiana au kushangazwa, wala si kwa nia; na katika Sharia hii, hakuna utofautisho baina ya mwanamke wa Kiislamu au mwanamke asiye Mwislamu; na vile vile sehemu zile kama uso mikono ambayo kwa kawaida huwa haifunikwi,na sehemu zinginezo za miili yao.

(2444) Inambidi mwanamke afunike mwili wake na nywele zake kutokana na mwanamme ambaye sio mahram kwake na tahadhari iliyo faradhi,kuwa ajifunike mzima dhidi ya wavulana ambao hawajabaleghe na ambao wanaweza kutambua baina ya mema na mabaya na labda wanaweza kuvutiwa katika mambo ya kusuhubiana.Lakini anaweza kuacha uso wake na mikono mpaka juu kidogo viganja visifunikwe mbele ya mtu ambaye sie mahram kwake, ili mradi huku kusimpelekee mtu katika mtego wa madhambi, kwa macho  mabaya au yeye kufanya jambo lolote ni haramu; kwa hali zozote hizi itambidi yeye afunike sehemu hizo zote.Ni haramu kutazama sehemu zake za siri za Mwislamu aliyebaleghe,hata kama itatazamwa nyuma ya kioo au kutokana na kioo kwa mbele, au maji safi yaliyotulia n.k.Kama tahadhari ya lazima, ni haramu vile vile kutazama sehemu za siri za mtu ambaye si Mwislamu,na kijana ambaye hajabaleghe na ambaye anaelewa mema na mabaya.Hata hivyo bibi na bwana wanaweza kutazama mwili wa mwenzake.

(2446)Iwapo mwanamme na mwanamke ambao ni mahram kwa kila mmoja, hawana nia ya raha ya kusuhubiana, wanaweza kuona mwili mzima wa mtu na mwenzake isipokuwa sehemu zake za siri.

(2447) Mwanamme hatakiwi kuangalia mwili wa mwanamme mwenzake kwa kupandwa na matamanio ya Ulawiti, na vile vile ni haramu kwa mwanamke kutizama mwili wa mwanamke mwenzake kwa nia ya kutaka kuingiliana naye.

(2448)Iwapo mwanamme anamfahamu mwanamke ambaye siye mahram kwake, basi itambidi kama tahadhari asitazame hata taswira yake n.k.,ili mradi mwanamke huyo hayupo miongoni mwa wanawake mwa wale wasiovaa hijab.

(2449)Iwapo mwanamke anataka kumpiga enema  mwanamke mwingine au mwanamme mbali na bwana wake, au kusafisha sehemu za siri za mwanamke au za mwanamme kwa maji, basi itambidi avishe kitu mikono yake ili mikono yake isiguse sehemu hizo za siri za mwanamke au mwanamme. Na vivyo hivyo inatumika kwa mwanamme ambaye anataka kumpiga enemamwanamme au mwanamke mwingine mbali na mke wake, au kusafisha sehemu za siri za mwanamke au  mwanamme kwa maji.

(2450) Iwapo mwanamke atakuwa ameugua na anaweza kutibiwa na mganga wa kiume vyema zaidi, basi anaweza kutibiwa naye.Na iwapo daktari huyo mwanamme itabidi amtazame ili kumtibu, au kumgusa mwanamke huyo kwa sababu hizo basi hakuna ishkal yoyote.Hata hivyo,iwapo ataweza kumtibu kwa kumwangalia itambidi asimguse, na kama ataweza kutibu kwa kumgusa mwili wake, basi asimtazame mwanamke huyo.

(2451) Iwapo mtu itambidi atazame sehemu za siri za mgonjwa wake akiwa mwanamke au mwanamme kwa ajili ya matibabu, basi itambidi katika misingi ya tahadhari iliyo faradhi, aweke kioo mbele yake mbele ya mwanamke au mwanamme. Hata hivyo, na kama hakuna njia nyingine bila kuangalia moja kwa moja katika sehemu za siri za mwanamke huyo au mwanamme, basi hakuna mshikeli.Vivyo hivyo iwapo kutachukuliwa muda zaidi kuangalia sehemu hizo za siri kupitia kioo kuliko kumwangalia moja kwa moja, basi anaweza kumtazama moja kwa moja.

Hukumu mbalimbali kuhusu maswala ya  ndoa.


(2452)  Iwapo mtu atakuwa ametumbukia katika matendo (zinaa)  ambayo yameharamishwa kwa sababu ya kutokuwa na mke, basi ni  faradhi  kwake yeye kuoa.

(2453) Iwapo bwana ataweka sharti kabla ya ndoa kuwa mwanamke lazima awe bikira, na baada ya ndoa ikaonekana kuwa si bikira, basi anaweza kuvunja ndoa hiyo.Hata hivyo,anaweza kukata kiasi cha mahari yanayolipwa kwa kawaida kwa ajili ya mwanamke aliyebikira au asiyebikira.

(2454) Ni haramu kwa mwanamke na mwanamme ambao si mahram kuwa pamoja katika sehemu zile ambazo hakuna mtu mwingine, iwapo kuna hofu ya kutumbukia katika ufisadi, au hata kama ni mahari ambapo anaweza kutokezea mtu kwa ghafla. Lau kutakuwa  hakuna hatari yoyote ya ubaya basi hakuna mushkeli wowote.

(2455)Iwapo mwanamme ndiye atakayepanga mahari ya mwanamke wakati wa ndoa, lakini hana nia ya kumlipa, basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi lakini atakuwa ana deni na mke wake.

(2456)  Mwislamu ambaye anaukana Uislamu na kuingia katika dini ya wale wasio Waislamu, ni kafiri na hao ni wa aina mbili;fitri na milli . Kafiri fitri ni yule ambaye wazazi wake au mmoja wao alikuwa Mwislamu alipokuwa amezaliwa, na yeye mwenyewe alikuwa Mwislamu hadi hapo alipofika umri wa kutambua baina ya mema na mabaya na hapo baadaye akaja akawa kafiri. Na kafiri milli ni mtu aliyetofauti kabisa.

(2457) Iwapo mwanamke atakuwa kafiri baada ya ndoa, ndoa yake itakuwa batil,na iwapo mume wake atakuwa hajasuhubiana naye, basi hatakiwi kubakia katika Iddah. Na hali hii itakuwa vivyo hivyo iwapo yeye atabadilika baada ya kusuhubiana na mume wake, au yeye amefikia ugumba   ( Ya'isa), au alikuwa bado mdogo. Na lau kama  atakuwa hajafikia ugumba, basi itambidi atimize Iddah kama vile inavyoelezwa katika hukumu za talaqa. Na ni jambo la kawaida iwapo yeye atakuwa Mwislamu tena akiwa katika kipindi cha Iddahndoa yake itasalimika.Hata hivyo,inaweza kuchukuliwa kuwa sahihi, na hivyo tahadhari isiachwe. Mwanamke anayeitwa Ya'isa ni yule ambaye amefikia umri wa miaka hamsini (50) na kwa sababu ya umri huo mkubwa anaacha kupata haidh  na wala hategemei kuyapata maishani mwake.

(2458) Iwapo mwanamme atakuwa kafiri fitri baada ya ndoa, mke wake atakuwa haramu kwa ajili yake; na huyo mwanamke hatakiwi kuingia katika Iddah baada ya kifo cha mume wake maswala ambayo yanaelezwa vyema katika Sharia za  talaqa.

(2459)Iwapo mwanamme atakuwa kafiri milli baada ya ndoa, ndoa yake itakuwa batil. Na kama alikuwa hakusuhubiana na mke wake, au mwanamke huyo amekuwa Ya'isa, au kama bado ni mdogo basi hatatekeleza Iddah. Lau kama huyo mwanamme ataingia katika ukafiri baada ya kusuhubiana na mke wake, mke wake akiwa katika hali ya mwanamke yule  ambaye anapata haidhkama kawaida, basi itambidi aingie katika  Iddah ya talaqa, maswala ambayo yanaelezwa vyema katika maswala ya talaqa. Inachukuliwa kawaida iwapo bwana wake atakuwa tena  Mwislamu kabla ya huyo mwanamke kumaliza Iddah basi ndoa yao itasalimika. Hata hivyo haitegemei kuwa hii itakuwa sahihi, lakini tahadhari isiachwe.

(2460) Iwapo mwanamke wakati wa ndoa ataweka sharti kuwa bwana wake asimchukue nje ya mji (utakaotajwa), na mwanamme akakubalia hilo sharti, basi asimchukue mke wake nje ya mji huo bila ya idhini yake.

(2461).Iwapo mwanamke ana mtoto wa bwana aliyemtangulia huyu bwana, basi huyo bwana anaweza kumuoza huyu binti kwa mtoto wake wa kiume, ambaye si mtoto wa mke huyo. Vivyo hivyo iwapo mke atamuoza mtoto wake kwa msichana, basi yeye akiwa kama baba anaweza kumuoa mama wa binti huyo.

(2462) Iwapo mwanamke atashika mimba  kwa sababu ya zinaa, basi haruhusiwi kuangusha mimba hiyo.

(2463) Iwapo mwanamme atafanya zinaa na mwanamke asiye na bwana, wala yeye hayuko katika Iddah, na baadaye akamuoa na mtoto akazaliwa wakiwa bado pamoja na hawajui iwapo huyu mtoto ameingia katika mimba  ya mama akiwa wamesuhubiana kihalali au kiharamu basi mtoto huyo atachukuliwa kama mwana halali.

(2464) Iwapo mwanamme hajui kuwa mwanamke huyo yu katika Iddah na akamuoa na mwanamke huyo vile vile hajui kuwa yeye yuko katika Iddah  na mtoto akazaliwa kwao, basi huyo mtoto atakuwa ni mwana halali kwa mujibu wa Sharia ni mtoto wao wote. Hata hivyo iwapo mwanamke anajua kuwa yeye alikuwa katika Iddahna katika kipindi hicho cha Iddah ndoa hairuhusiwi mtoto atakayezaliwa atakuwa ni mtoto wa baba,na kwa hali yoyote ile ndoa yao itakuwa batil na wao watakuwa ni haramu kwa kila mmoja.

(2465)Iwapo mwanamke atasema yeye kuwa amekuwa gumba (Ya'isa), maneno yake yasikubalike lakini akisema kuwa yeye hana bwana basi maneno yake yakubalike, isipokuwa pale anapojulikana kuwa haaminiki, katika hali hiyo uchunguzi utahitajika. 

(2466)Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke baada ya mwanamke kusema kuwa hana bwana, na ikatokezea mtu mwingine akaja akadai kuwa huyu ni mke wake basi madai yake hayatakubaliwa hadi hapo ithibitishwe kwa mujibu wa Sharia.

(2467) Hadi hapo msichana au mvulana anamaliza umri wa miaka miwili, baba yake hawezi kumtenganisha na mama yake.Na kama tahadhari, mtoto asitenganishwe na mama yake hadi umri wa miaka saba.

(2468) Iwapo mtu anayetaka kuoa anajulikana kwa wema na imani yake, basi inasisitizwa kuwa ombi lake hilo lisikataliwe.Mtume Mtukufu s.a.w.w. ameripotiwa kusema: "Popote utakaposikia, popote utakapopokea maombi ya kumuoza mtoto wako kwa mwanamme ambaye sifa zake na ucha Mungu wake unakufurahisha wewe, basi muoze mtoto wako. Na lau hautafanya hivyo, basi ufisadi na maovu yatajaza dunia."

(2469)Iwapo mwanamke ataafikiana na mume wake kuhusu mahari yake, kwa masharti kwamba mwanamme huyo hataoa mwanamke mwingine, basi ni faradhi kwa mwanamme kutokuoa mwanamke mwingine,na kwamba mwanamke huyo asidai  mahari yake tena.

(2470)Iwapo mwanaharamu ataoa, na mtoto atazaliwa basi mtoto huyo atakuwa ni mwana halali.

(2471)Iwapo mwanamme atasuhubiana na mke wake katika funga za mwezi wa Ramadhani au wakati mwanamke huyo atakuwa katika vipindi vyake vya mwezi (haidh), mwanamme atakuwa ametenda dhambi lakini iwapo mke atashika mimba  katika hali hiyo basi mimba hiyo ni halali.

(2472)Iwapo mwanamke atakuwa na uhakika kuwa bwana wake amekufa akiwa safarini,na akaolewa na mwanamme mwingine baada ya kukamilisha Iddah ya kifo,(mambo yanayoelezwa vyema katika maswala ya talaqa) na baadaye mume wake wa kwanza akatokezea kutoka safari, basi itambidi mwanamke huyo papo hapo ajitenganishe na bwana wake wa pili,na huyo mwanamke atakuwa ni halali kwa bwana wake wa kwanza. Lakini iwapo bwana wake wa pili atakuwa amesuhubiana naye, basi itambidi atekeleze Iddah na bwana wake wa pili itambidi ampe mahari yake kamili kwa mujibu wa mwanamke wa kikundi hicho, lakini hastahiki kulipiwa gharama na bwana wake wa pili katika kipindi hicho cha Iddah.

22.  ADABU  ZA  KUSUHUBIANA.


1.Mtume s.a.w.w. amesema:
"Msisuhubiane na wake zenu kama kuku.Fanyeni mapenzi ya kutosha,mubusu na hatimaye  munapojawa na raha ndipo musuhubiane”.

2.Watu wengi wanachukulia mambo ya kishetani katika kusuhubiana huku wakipuuza njia aliyoihalalisha Allah swt. Wao wanaingilia  njia ya  nyuma i.e. panapopitia choo kwa kisingizio cha kupata raha zaidi kumbe kunakujitumbukiza katika hatari ya kuweza kuambukizwa magonjwa hatari kabisa kwa sababu hiyo ni nafasi ya kupitia uchafu mtupu uliojaa magonjwa ya kila aina. Kwa msomaji ni ushauri wangu kuwa aonane na mganga ili aweze kupata ukweli na uhakika wa swala hili ili aweze kuelewa vyema falsafa ya Islam katika swala hili.

3.Manukato ya maua  na mafuta mazuri yanaweza kuwafanya kustarehe zaidi katika kusuhubiana.

4.Kwa kubaki mbali na mke kwa kipindi kirefu bila ya kusuhubiana naye au kwa udhuru mwingine wa kisheria haifai kumtukana au kumuudhi kwani kunaweza kwa urahisi kumfanya mke aende nje kwa waume wengine na hapa bwana ndiye atakaye wajibika.

5.Wataalamu wanasema kuwa bibi na bwana wanaposuhubiana,inawabidi wasiingiliane tena  illa baada ya siku tatu au hata zaidi.Ingawaje hakuna ushahidi wa  kuleta madhara.

6.Haifai kusuhubiana wakati tumbo likiwa limejaa (ameshiba) au likiwa tupu  (njaa) bali baada ya kula iwapo utakuwa umepita muda wakutosha,basi hakuna madhara.

7.Baada ya kusuhubiana kwa bibi na bwana,wasioshe sehemu zao za siri kwa maji baridi wala wasioge kwa maji baridi kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuwaingiza katika magonjwa mengi mno na kuna uwezekano mkubwa wa mishipa kulegea.Lakini kusafisha kwa kitambaa chenye maji si vibaya.Bibi na bwana hawatakiwi kusafisha sehemu zao za siri kwa kutumia kitambaa kimoja tu kwani kunapunguza mapenzi baina yao.

8.Baada ya kusuhubiana wote wawili wanashauriwa  kujisaidia haja ndogo (kukojoa mkojo) na kwa kufanya hivyo mishipa haitalegea.

9.Kusuhubiana kwa kijana mwenye umri mdogo na mwanamke mwenye umri mkubwa ni hatari  sana kwa siha ya mwanamme kwani ni sawa na sumu kali sana.

10.Umri wa mwanamke: kuanzia miaka kumi na miwili hadi ishirini ni kama bibi harusi,na katika umri huu anaweza kutoa  uridhisho mzuri kabisa katika kusuhubiana.Vile vile  kuanzia umri wa miaka ishirini hadi thelathini anaweza kutoa uridhiano mzuri na bwana pia anaweza kuridhika. Na mwanamke kuanzia thelathini hadi arobaini si mbaya. Kuanzia arobaini hadi hamsini huwa hisia zimekuwa sugu,hata hivyo hana madhara.

11.Mtume s.a.w.w. alimwambia Imam Ali a.s. "Ewe Ali! Unapomleta mke wako nyumbani mwako,ondoa viatu vyake ili aweze kuketi vyema na uoshe vikanyagio vya miguu yake na kumwagilia maji hayo mlangoni  na kona zote na kuta za nje ya  ya nyumba;kwa kwa kufanya hivyo kutaondoa  mawazo na shida sabini  elfu na kutakuletea  baraka na rehema sabini elfu za Allah swt.Na vile vile kila kona ya nyumba itakuwa imebarikiwa na bibi harusi atakuwa amehifadhika na ugonjwa wa kichaa,kubabuka ngozi kichwani na ukoma.Usimpatie kwa siku saba za kwanza maziwa,siki,giligilani na tufahachachu.Alipouliza Imam Ali a.s. sababu yake,alijibiwa:"kwa kula vitu hivyo,mwanamke anapoteza nguvu za kushika mimba  na hawezi kuzaa mtoto.Kipande cha mkeka kilichotupwa nyumbani ni bora kuliko mwanamke asiyezaa."

23.  WAKATI WA KUSUHUBIANA

(1).  Wakati  usiopendekezwa


1.Ni haramu kusuhubiana na mwanamke anapokuwa katika haidh  (mwanamke anapotokwa na damu ya kila mwezi) au nifas (damu inayotoka baada ya kuzaa),na vile vile si vyema kumgusa kuan­zia sehemu zake za siri hadi magoti yake.

2.Hairuhusiwi kusuhubiana na mwanamke baada ya kufunga damu ya haidh na nifas na  kabla ya mwanamke hajaoga (hajafanya ghusl)  Maulamaa wengi wanasema kuwa ni haramu kusuhubiana na kwa hakika ndivyo inavyotakiwa lakini iwapo mtu atataka kusuhubiana,basi itawabidi wasafishe vyema sehemu hizo ndipo waweze kusuhubiana.

3.Iwapo mtu atapenda kusuhubiana na mwanamke aliye katika Istehadha (zisizozidi siku zaidi ya haidh) basi itambidi huyo mwanamke  aoge istehadha na kukamilisha masharti yote yaistehadha ndipo hapo atakapoweza kusuhubiana naye.

4.Kila wakati mwanamme anaposuhubina na mke wake haruhusiwi kumwaga nje manii (shahawa au mbegu za kiume) nje ya uuke wa mke bila ya ruhusa ya mke wake na baadhi ya Maulamaa wanasema kuwa ni haramu kufanya hivyo.Lakini hata hivyo anaposuhubiana na kijakazi wake anayo ikhtiyari  ya kufanya hivyo.Lakini wataalamu wanapinga kumwaga nje manii.

5.Haitakiwi kusuhubiana usiku wa kuamkia jumatano kwani iwapo atachukua mimba,basi kuna uwezekano wa kuanguka kwa mimba kabla ya kufikia muda wake na iwapo itakamilika basi kunaweza kuzaliwa kwa mtoto mwendawazimu au mwenye ugonjwa wa yabisi.

6.Haitakiwi kusuhubiana siku za mwanzoni,katikati na mwishoni mwa kila mwezi kwani vile vile kuna hatari ya kuanguka kwa mimba  changa na iwapo atazaliwa mtoto basi kunauwezekano wa kuwa mwendawazimu au mwenye yabisi.

7.Wakati wa kusuhubiana haitakiwi kuzungumza  kwani kunauwezekano wa kuzaliwa kwa mtoto kiziwi.

8.Wakati wa kusuhubiana hairuhusiwi kuangalia sehemu za siri kwani kunahatari ya kuzaliwa kwa mtoto kipofu,lakini katika riwaya nyingine inaelezea kuwa hakuna ubaya wowote ule.Mbali na wakati wa kusuhubiana,hapana  makatazo ya aina yoyote ile katika kutazamana.

9.Iwapo kutakuwa kumepakwa khizaab,basi haitakiwi kusuhubiana.

10.Vile vile hairuhusiwi kusuhubiana  wanapokuwa  katika maji.
11.Hairuhusiwi kusuhubiana mbele ya watoto kwani kuna hatari ya kuzaliwa mtoto  mzinifu.

12.Iwapo kutakuwa na aliye macho au asikiaye sauti za wakati wa kusuhubiana,basi haitakiwi kusuhubiana wakati huo.

13.Iwapo mtu atasuhubiana na kijakazi wake mmoja na kuwa na hamu ya kusuhubiana na kijakazi wa pili basi itambidi afanye wudhuu (kutawadha)  kwanza.

14.Hairuhusiwi kuwalaza wanawake wawili (iwapo mtu atakuwa na wake wawili) kwa pamoja kitanda kimoja lakini anaruhusiwa kwa ajili ya vijakazi wawili.

15.Hairuhusiwi kusuhubiana huku uso au mgongo ukielekea Qibla.

16.Vile vile hairuhusiwi kusuhubiana wakati wanapokuwa wakisafiri katika meli au jahazi.

17.Iwapo mtu alitokwa na manii bila ya kusuhubiana, (akiwa usingizini au kwa sababu zinginezo) basi itambidi kwanza afanye ghusl-i-janaba, ndipo aweze kusuhubiana  kwani bila ya kufaya hivyo kuna uwezekano wa kuzaliwa mtoto mwendawazimu.

18.Ni haramu kusuhubiana wakati wa kupatwa kwa jua na mwezi au kunapotokea mtetemeko au jua lionekanapo kuwa rangi njano.

19.Kusuhubiana wakati wa adhuhuri kunaweza kuzaliwa mtoto mwenye macho makengeza.

20.Imam Ali a.s. amesema:"Iwapo utamwona mwanamke wa nje na iwapo utaghalibiwa na Sheitani hata ukatamani kusuhubiana na mke wako,basi usithubutu kufanya hivyo kwani ujiambie kuwa kile alichonacho huyo hata mke wako pia anacho.Na iwapo atakuwa hana mke,basi inambidi asali rakaa mbili na kumwomba Allah swt amjaalie mke,naye atapata kuoa."

21.Iwapo watasuhubiana wakiwa wamesimama,basi kunauwezekano wa  mtoto kuzaliwa akiwa na tabia ya kujikojolea kitandani hata akiwa na umri mkubwa.

22.Iwapo kutasuhubiwa katika usiku wa Idd ul-Fitr, mtoto atakayezaliwa atakuwa na maovu mengi mno.
23.Vile vile inabidi kujiepusha na kusuhubiana usiku wa Idd ul-Adh-ha kwa sababu kunauwezekano wa kuzaliwa mtoto mwenye vidole vinne au sita.

24. Kwa sababu ya kusuhubiana chini ya miti ya matunda, mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa  kiongozi wa dhalimu.

25. Haitakiwi kusuhubiana wakati miale ya jua ikiwaelekea kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye wasiwasi hadi kufa kwake.

26. Hairuhusiwi kusuhubiana baina ya Adhaan na Iqamah mtoto atakayezaliwa  atakuwa daima mwenye kutaka kumwaga damu yaani muaji.

27. Kutaka kusuhubiana na mwanamke mwenye mimba, inabidi mwanamme awe katika hali ya wudhuu kwani  bila hivyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye roho ngumu na mchoyo.

28. Haitakiwi kusuhubiana usiku wa tarehe kumi na tano ya Shaaban, kwani mtoto atakayezaliwa hatakuwa
 mwenye bahati na atakuwa na madoti meusi usoni mwake.

29. Hairuhusiwi kusuhubiana  katika siku za mwisho za mwezi wa Shaaban kwani mtoto atakayezaliwa  atakuwa jambazi na mwenye ukatili na kuna hofu ya kuwaua watu wengi mno.

30. Hairuhusiwi kusuhubiana juu ya paa za nyumba kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mlaghai na asiye na imani.

31.Haitakiwi kusuhubiana usiku wa kuamkia safari kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye kutumia vibaya mali ya watu na watu kama hao ni ndugu wa masheitani.

32.Atazaliwa mtoto asiye na raha kwa sababu ya kusuhubiana wakati wanapokuwa wazazi katika safari  isi­yozidi siku tatu.

33.Iwapo kutasuhubiana wakati wa mwanzoni mwa usiku basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mchawi na ambaye ataithamini dunia kuliko Aakhera.

34. Hairuhusiwi kusuhubiana  mahala ambapo ni wazi kama chini ya mbingu.

35.Allah swt,Mitume  na Aimma a.s.,Malaika pamoja na wanaadamu pia hulaani vikali mno kule kusuhubiana barabarani au njiani ambapo hupitwa na watu.

36.Iwapo mtu atakuwa anatakiwa kuoga ghusl-i-Mayyit basi hatakiwi kusuhubiana na iwapo atataka kufanya hivyo,basi itambidi afanye wudhuu

37.Iwapo mtu atapenda kusuhubiana kwa mara ya pili baada ya kwanza,basi itambidi afanye wudhuu.

38.Iwapo mtu atataka Shaitan asiwe mshiriki  katika kusuhubiana kwao,basi aiseme kikamilifu "Bismillah".

39.Baada ya ndoa,haifai kusuhubiana kwa mara ya kwanza katika 'tahtush-shoaa' (usiku mbili au tatu za mwisho za mwezi ambapo mwezi hauonekani).

40.Ni haraam kusuhubiana wakati mwanamke anapokuwa katika haidh na nifas, na kwa kukiuka kunatakiwa kulipa kaffarah yake.

41.Mtume s.a.w.w. amesema iwapo atazaliwa mtoto mwenye ugonjwa wa ukoma,basi wazazi ndio watakaojilaumu.

42.Ipo riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Imam Jaafer as-Sadiq a.s."Adui wetu sisi Ahlul-Bait a.s. ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. ama atakuwa ni waladuz-zinaa au waladul-Haidh. Hivyo mtu akiona  kuwa moyoni mwake anayo mapenzi ya Ahlul-Bayt a.s. basi  amwombee kheri  mama yake mzazi kwa kutomzaa mwana haramu." Ipo riwaya moja  isemayo "alikuwa baba mmoja akisema  kuwa mtu mwenye mapenzi ya Ahli Bayti a.s. ni mwana halali na mwenye uadui nao ni waladuz-Zinaa. Basi mtoto wake alimwambia baba yake kuwa yeye alikuwa adui mkubwa wa Ahli-Bayti a.s. Sasa jee yeye alikuwa ni waladuz-zinaa ?

Baba yake alimwambia akamwulize mama yake kwani yeye anavyoelewa, alikuwa kweli mwana haramu kwa sababu baba yake alifanya mapenzi na mama yake na walisuhubiana kabla ya ndoa, na mama yake akashika mimba . Baadaye walifanya tawba na kufunga ndoa.Hivyo,kwa kifupi alizaliwa kabla ya wao kufunga ndoa.

43.Haifai kusuhubiana na  mke mmoja mbele ya mke wa pili lakini haina shida iwapo kutasuhubiana na ki­jakazi mbele ya kijakazi mwingine.

44.Haifai kusuhubiana katika hali ya kuwa uchi kabisa bila kujifunika kwani kunawafukuza Malaika.Lakini walimwuliza Imam Musa al-Kadhim a.s. iwapo nguo ikisogea,naye alijibu kuwa hapakuwa na matatizo.

45.Iwapo mtu atasuhubiana na mwanamke aliyepakaa rangi kichwani,basi mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa khanisi.

46.Inambidi mtu aondoe pete alizovaa ambazo zimechongewa majina matukufu au  naqshi kabla ya kusuhubiana.

47.Haifai kusuhubiana iwapo kuna shida ya kupata maji kwa ajili ya kufanya ghusli

48.Ni makrooh (karaha) kusuhubiana wakati wa alfajiri kabla hapajapambazuka au kuchwa kwa jua kamili.

49.Ni vyema kufunga macho wakati wa kusuhubiana.

50. Hairuhusiwi kusoma Quran Tukufu katika kitanda ambapo wamesuhubiana bibi na bwana na bado hawajaoga ghusl-i-janabakwani kutaweza kusababisha adhabu ya Allah swt kuwaadhibu wote wawili.

(2).  Wakati unaopendekezwa:


1.Ni Sunnah kusuhubiana usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani.

2.Mtoto atakayezaliwa kwa kusuhubiana usiku wa jumatatu basi atakuwa (hafidhi Quran) mwenye kuihifdhi
Quran kwa moyo na Allah swt atakuwa amemwia radhi na kwa bahati yake njema.

3.Mtoto atakayezaliwa kwa sababu ya kusuhubiana usiku wa jumanne,iwapo ni mvulana atapata ufalme wa Din ya Islam yaani  atakuwa mwema mno na roho yake itakuwa yenye huruma,mikono yake madhubuti na ulimi wake utakuwa umehifadhika na  ghibah na  buhtan  (kusengenya na kusingizia) watu.

4.Kwa kusuhubiana usiku wa alhamisi (kuamkia ijumaa),na mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa Hakimu wa Shariah au atakuwa Aalim.

5.Kwa kusuhubiana wakati  wa mchana wa siku ya Ijumaa mtoto atakayezaliwa atakuwa amekaa mbali na Shaitan na Allah swt atamjaalia usalama wa Din na dunia.

6.Ukimwona mtoto ni mzungumzaji wa lugha tamu na msomaji wa khutbah basi ujue kuwa huyo ni matokeo ya kusuhubiana usiku wa Ijumaa.

7.Mtoto atakayezaliwa kwa kutokana kusuhubiana baada ya adhuhuri ya Ijumaa ,basi atakuwa akijulikana kwa  ukarimu wake.

8.Kwa kusuhubiana baada ya salat al-'Ishaa ya siku ya Ijumaa,mtoto atakayezaliwa atakuwa ni mwenye wadhifa katika Din

24.  TALAQA.


Kuna baadhi ya mizozo na sura katika maisha ya ndoa ambazo zinashindikana kutatuliwa katika misingi mbalimbali, na hali ya maisha ya kifamilia inakuwa haivumiliki.  Katika hali kama hizo, kunakuwa na njia mbili tu za kufanya ambazo zinakuwa zimebakia:
1.Kumwachia bibi na bwana katika hali hiyo hiyo walivyo, ambavyo kwa mujibu wa aya ya Qurani tukufu ni adhabu ya motoni
2.Kuwaachanisha na kuwatenganisha na mfungamano wa ndoa (talaqa), ili kwamba kila mmoja wao atafute mwenzake atakayeweza kupatana naye ili maisha yao yawe mema na mazuri. 

Akili zetu zinakubaliana na utaratibu wa na. 2 na ndivyo vivyo hivyo Uislamu pia unaunga mkono.

Ukristo unapendelea hali ya kwanza yaani kuwalazimisha bibi na bwana waishi pamoja hata kama watachukiana kiasi gani,na hoja hii inatokana na maneno ya Yesu:-

Biblia inatuambia katika Mathayo,  5 : 31 - 32.
"...Kila mtu amwachaye mkewe,isipokuwa kwa habari ya uasherati,amfanya kuwa mzinzi; ...

Tujiulize sisi kama binadamu iwapo zinaa peke yake ndiyo inayoharibu maisha ya ndoa?  Je hasira kali au kutafuna haki ya mwenzako au ndizo pia zinazoleta mfarakano katika maisha ya ndoa, Je kudharau kumjali mke kwa kumpa haki zake, uaminifu, kumgeuka mke au kutojali havitoshelezi kufanya nyumba yako ikawa Jahannam?

Ni lazima hapa sisi tujaribu kujua busara ya talaqa ilivyo katika maswala mengi yaliy onyeti, kama ilivyoruhusiwa katika Islam. Leo hata wale watu ambao hawakubaliani na talaqa wanaiambia Serikali katika bunge ipitishe Sharia na muswada kuhusu talaqa, katika Sharia za nchi, mambo ambayo mara nyingi yanapingwa na Kanisa na dini nyinginezo kwa sababu dini hizo hazina mwanya zaidi katika maswala haya.
Dini ya Hindu haitambui talaqa; nao pia katika nchi ya India wametengeneza Sharia na muswada katika Sharia zao za nchi.

Waangilikana nao pia wanapinga talaqa; nao kwa kupitia Sharia ya bunge (ambamo Askofu ndio mhusika mkuu -member) Wamekubali kutenganishwa na mahakama yaani talaqa.  jambo la kuvutia hapa ni kwamba mkuu wa nchi, mtawala ni mkuu wa Kanisa la Kiangilikana; ambaye anapinga talaqa na papo hapo akiwa katika wadhifa wake wa mkuu wa nchi, anaidhinisha Sharia ya bunge ikiruhusu talaqa.

Je kwa nini Mfalme Edward VIII alimuoa mwanamke aliyepewa talaqa,  na papo hapo maelfu kwa maelfu ya raia wake walikuwa wakipewa talaqa chini ya  mamlaka yake?  Je inamaanisha kuwa dini ya Kikristo inasheria mbili ?  Sharia zake; moja kwa ajili ya watu wakubwa na Sharia nyingine kwa ajili ya watu wa kawaida?

Kanisa la Roman Katholiki linapinga kabisa talaqa.  Lakini wamelazimishwa kwa ukweli sugu wa maisha kiasi kwamba wametafuta njia ya kuvunja ndoa bila ya kuita talaqa. Iwapo mtu anasubira ya Job (Ayub) na fedha na mapesa ya Qarun anaweza kupata baada ya kuomba amri kutoka Vatikan, kuwa ndoa yake ilikuwa imekwisha na batil kuanzia mwanzoni.

Mastaajabisho au siyo?  Jambo lililogumu hapa ni kwamba atakayepata ni yule tu ambaye yuko katika tabaka la matajiri."Katika miaka ya karibuni, Papa Paulo wa VI ameonyesha utaratibu .....kuwa inaweza kutatua hata ya kesi ya miaka 20. Pamoja na Vatikani za kuweka malipo, gharama za Rot zimebakia juu sana, mara nyingine katika maelfu ya dola na ikiwafanyia wale wenye utajiri."

Iwapo ndoa hiyo itasemwa kuwa hiyo ndoa tokea mwanzoni ilikuwa ni batil sasa watoto waliozaliwa katika kipindi hicho watakuwa na nafasi gani katika Sharia zao? Je tutasema watoto hao ni wana haramu?
Italia chini ya shinikizo la Vatikan imejaribu kuzuia Sharia ya uhalalishaji wa talaqa. Lakini kule Italia pia Sharia imeshapitishwa yaani muswada umepitishwa na imeshakuwa Sharia. Mara pale Sharia ilipopitishwa ya talaqa maelfu ya watu waliomba wapatiwe talaqa, wengi ambao walikuwa wameachana na wake zao miaka 20 au 30 iliyopita.

Ndio tunaona binadamu anavyoweza kuteseka kwa kanuni na Sharia kama hizo.Sio kutaabika na kuteseka tu kunakotokea bali kunawashawishi na kuwasukuma watu kujiingiza katika madhambi (zinaa).Je inawezekana bibi na bwana walioachana kienyeji miaka 20 au 30 iliyopita wakabaki bado wako safi? Bila shaka kila mmoja wao yaani bibi na bwana watakuwa wametaka kutimiza haja zao za kijinsia pamoja na watu wa nje ambao hawakuolewa nao na wengineo humo watakuwa wamewazaa watoto wengi na bila shaka katika kipindi cha miaka 20 - 30 wengine wamekuwa mababu wa wajukuu na watoto wanaharamu ambao amezaa mtoto na mjukuu nje ya ndoa.

Kwa hiyo tukiangalia maswala kama hayo tunaona kweli kuwa Uislamu umetoa mwongozo ulio sahihi na mambo ambayo yanakubalika na akili yetu ili kufanya maisha yetu yakawa mazuri na fanaka.

Kwa kuwa kitabu hiki kinazungumzia mambo ya ndoa hivyo maudhui ya talaqa sitayazungumzia zaidi lakini nimeonelea nigusie kidogo ili tupate kidogo fununu juu ya desturi na  Sharia za Kiislamu ni kwa ajili yetu na ubora wetu na kwa ajili ya mustakbali, hivyo msomaji iwapo atapenda kufanya utafiti juu ya swala la talaqa anaweza kujiendeleza au Insha Allah nikifanikiwa nitajaribu kutayarisha kitabu juu ya talaqa na mirathi.


Kitabu kimeandikwa naAmiraly M.H.Datoo  

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget