Wednesday, April 4, 2012

Hijab si Kikwazo cha Masomo kwa Mwanamke


Utangulizi

1.      Kwa kipindi kirefu pamekuwepo na fikra ambazo kikweli hazikujengwa kwenye msingi wowote wa kisayansi wala kimantiki kuwa vazi analowajibika kulivaa mwanamke wa Kiislamu i.e. hijaab kuwa ni kipingamizi na halifai kuvaliwa katika kada mbali mbali za masomo na kazi. Miongoni mwa kada hizi ambazo zimekuwa zikipinga kutumia vazi hili ni pamoja na kada ya uuguzi (au nursing kwa lugha ya Kiingereza).

2.      Makala hii fupi inajaribu kuonyesha kuwa hijaab haijawa kikwazo na wala haitakuwa kikwazo katika masomo ya uuguzi na hata kazi yenyewe. Katika kufanya hivyo tutaangalia kwa ufupi mambo yafuatayo: -

a.   Historia fupi ya uuguzi katika mfumo wake wa zamani na ule unaoitwa wa kisasa (modern nursing or Judeo-Christian or Westernized nursing).

b.   Uuguzi na athari ya ustaarabu wa jamii inayohusika.

c.   Hijaab kama mfumo wa jamii ya Kiislamu.

d.   Wanawake waliovaa hijaab katika vyuo vikuu vya afya.

e.   Wepesi na faida ya hijaab kwa wanafunzi wa kike.

f.     Vipi tuanze?

Historia fupi ya uuguzi

3.      Uuguzi ambao unaelezwa au kutafsiriwa kama “the process of caring for, or nurturing, another individual. More specifically, nursing refers to the functions and duties carried out by persons who have had formal education and training in the art and science of nursing”[1]. Kazi hii tukiiangalia kwa ukweli na uyakinifu tutakuta kuwa haikuanza miaka 500 wala 1000 iliyopita bali inakwenda sambamba na historia ya maisha au uhai wa binadamu hapa ulimwenguni.

4.      Jamii mbali mbali za binadamu zimekuwepo hapa ulimwenguni na zimeweza kuvuka vikwazo kadhaa vya zama tofauti kutokana na maarifa ambayo jamii hizo imekuwa ikizirithisha kutoka jamii moja hadi nyengine. Jamii hizo zote zimeweza kuuguza wagonjwa wao kwa viwango tofauti na wauguzi hao wote walifanikisha lengo la kazi yao hiyo. Ni kwa sababu hiyo ndiyo hadi leo jamii ya binadamu imekuwa ikiendelea kuwepo. Kila zama huongeza maarifa mapya katika baadhi ya mambo hayo kutegemeana na mazingira na ugunduzi katika jamii hizo. Lakini mote humo tunakubaliana kuwa wanadamu hao walikuwa wakitumia fani hii ya uuguzi kushughulikia wagonjwa wao kuanzia kwenye uangalizi, utoaji wa huduma, msaada wa matatibu wa zama zao n.k.

 

5.      Wanazuoni wa Kiislamu wamerikodi katika vitabu vyao matukio ya kihistoria ambayo yanawaonyesha wanawake watukufu wa Kiislamu wakati wa Mtume (s.a.w.) wakitoa huduma za uuguzi kwa masahaba waliojeruhiwa katika vita mbali mbali baina ya Uislamu na washirikina au makafiri wengine. Mfano mmoja ni ule wa Bibi Fatma (mtoto wa Mtume s.a.w.) na Bibi Safiyyat bint Abdimuttalib (shangazi yake Mtume s.a.w.) wakati wa vita vya Uhud. Wote hawa pamoja na wanawake wengine wa masahaba waliingia katika uwanja wa vita na kuwahudumia majeruhi wa jeshi la Kiislamu kwa kuwapatia maji, chakula, kuwafunga majeraha na kutoa misaada mengine.

6.      Maelezo ya ziada kwa upande mwengine tunayapata katika Encarta 97 Encyclopedia. Kulingana na muandishi wa makala hiyo, uuguzi katika zama za awali ulikuwa ukifanywa kwa njia ya kujitolea zaidi na wahusika walikuwa ni watu waliokuwa chini ya jumuiya za kidini. Kuna kipindi ambapo uchafu katika mahospitali yalifanya kada hii kuonekana haifai kwa wanawake wadogo wenye hadhi zao kijamii hivyo kazi hiyo ilishikwa na wafungwa ambao walipatikana na makosa ya ulevi na wale ambao hawakuwa na kazi nyengine ya kufanya[2].

7.      Ama kwa upande wa hiki kinachoitwa kama “modern nursing” au uuguzi wa kisasa tunasoma tena katika mtiririko huo maneno yafuatayo:

Modern nursing began in the mid-19th century with the advent of the Nightingale training schools for nurses. In the U.S., the Spanish-American War and, later, World War I established the need for more nurses in both military and civilian life. As a result, nursing schools increased their enrollments, and several new programs were developed. In 1920 a study funded by the Rockefeller Foundation and known as the Goldmark Report recommended that schools of nursing be independent of hospitals and that students no longer be exploited as cheap labor. Following the publication of this report, several university schools of nursing were opened.

During the depression of the 1930s, many nurses were unemployed, and the number of schools declined. World War II, however, brought about another increased demand for nurses. The Cadet Nurse Corps, established in 1943, subsidized nursing education for thousands of young people who agreed to engage in nursing for the duration of the war. Since the end of World War II, technological advances in medicine and health have required nurses to become knowledgeable about sophisticated equipment, to learn about an increasing number of medications, and to design nursing care appropriate for the health care delivery system during a period of rapid change[3].

8.      Ni vyema kabla ya kuanza sehemu nyengine kuhitimisha sehemu hii kwa kufanya majumuisho kutokana na kile tulichojifunza katika historia ya uuguzi katika maelezo yaliyopita. Mosi, tunaona kuwa uuguzi kama fani ya taaluma na kazi imeanza muda mrefu kabla ya inayoitwa “modern nursing”. Pili, kuna kipindi ambapo kazi hii ilifanywa zaidi na jumuiya ambazo zilikuwa ni za kidini zaidi kuliko jumuiya nyengine. Tatu, uuguzi kama fani ya elimu katika mfumo wa kisasa inahusishwa na nchi za Magharibi chini ya anayejulikana kama muanzilishi wa fani ya uuguzi – Bi Florence Nightingale.

 

Uuguzi na athari ya ustaarabu wa jamii inayohusika

9.      Uuguzi kama ilivyo kwa kada nyengine za kazi au taaluma ni zao la jamii ambayo kada hiyo imeebuka. Ulaya na Marekani kimaadili na kijamii ni matokeo ya ustaarabu wa Kiyunani, Kiyahudi na Kikristo (Greek-Judeo-Christian civilization). Chochote tukionacho katika jamii hii ya leo katika nchi za Magharibi hapana budi kukifuatilia kwenye asili yake ambayo inajionyesha katika hatua mbali mbali za maendeleo yake. Kwa kuwa lengo la makala haya ni kuangalia kivazi cha wauguzi wanawake, hapana budi kuangalia vipi mwanamke amekuwa akichukuliwa katika jamii ya Magharibi tokea huko nyuma hadi hivi sasa.

10.  Tunafanya hivi kwa sababu hapana tatizo wala shindikizo la aina yoyote kwa wauguzi wanaume kuhusiana na mavazi yao. Kama ilivyo kwa waimbaji wa miziki na wacheza “show”, wanaume siku zote huvaa vizuri na hapana dalili zozote za kufanywa vinyago wala kuvishwa nguo za kuwadhalilisha. Hali haiko hivyo kwa wanawake ambao mara nyingi huwekewa kivazi ambacho ukikiangalia kwa makini utakikuta kuwa kimelengwa kumfanya awe kivutio cha ngono kwa mwanamme na chombo cha kuburudishia macho.

11.  Katika kitabu chake Purdah and the Status of Woman in Islam, mwanazuoni wa Kiislamu – Abul A’la Maududi ana muhutasari ufuatao wa jamii tofauti na jinsi walivyokuwa na wanavyoendelea kumfanya mwanamke:

a.   Greece

The Greeks regarded woman as a sub-human creature whose rank in society was in every way inferior to that of man, for whom alone was reserved honour and a place of pride.... With the worship of the goddess of love in Greece, houses of prostitution became places of worship, prostitutes were considered like pious girls dedicated to the temples, and adultery was raised to the status of piety and invested with full religious sanctity[4].

b.   Rome

When the checks on public morality became weak, the flood of sexual licentiousness, nudity and promiscuity burst upon Rome. Theatres became the scenes of moral perversion and nude performance, dwelling places were decorated with nude and immoral paintings and prostitution became so widespread and popular that Ceasar Tiberius (14 AD – 37 AD) has to enforce a law prohibiting women of the Roman nobility from adopting prostitution. Flora became a popular Roman sport in which naked women competed in race contests[5].

c.   Ulaya ya sasa (chini ya ubepari wa kiutandawazi)

During this impious age of the individual’s revolt and aggressive sinfulness, it was impossible that the selfish people did not think of the weakest point of man, his urge for sex, which could be easily exploited for the purpose of coining money. And this weakness was fully exploited, in diverse ways. Services of beautiful women were obtained for theatres, ballrooms and film-making centres. They were made to appear nude before the people in order to arouse their sexual appetite and deprive them of their pockets. Some people hired out women and developed prostitution to the level of an organized international trade. Some others invented new ways and manners of make-up and publicized them widely so as to arouse the female urge for beautification to the point of craze with a view to making money. Others designed sex-arousing, semi-covering dresses and appointed charming women to wear and go about society with a view to tempting young men ... these dresses popular among young girls and the designers earned high profits ... Gradually things came to such a pass that no sphere of trade and commerce remained immune from the sex element... No hotel, no restaurant, no showroom could be imagined without a lady attendant in order to attract men[6].  

12.  Ni muhimu kumkumbusha msomaji wetu kuwa hali hii haikufikiwa kwa siku moja au mbili. Haya ni matokeo ya karne nyingi za kukua na kudidimia kwa ustaarabu wa nchi za Magharibi. Ulaya ya zama za kati (Middle ages) ilimuheshimu mwanamke kimavazi licha ya kumdhalilisha kwa namna nyengine. Hali hii ilikuja baada ya wanafalsafa wa Ulaya kumtangaza Mwenyezi Mungu kuwa amekufa (subhaana-llaahu) na wao wanakajiona kuwa wana uwezo wa kupanga maisha kulingana na zama na mahitaji yao. Hayo yalitangazwa na Friedrich Nietzsche (1844-1900) katika kujenga hoja za kuhalalisha kupitwa na wakati kwa mafunzo ya Ukristo.

13.  Kabla ya kufikia hatua hiyo na bado Ukristo ukiwa na athari na kukubalika, jamii za Ulaya zilimvisha mwanamke muuguzi nguo ya heshima iliyokuwa inavaliwa wakati huo na wanawake wote wenye heshima zao katika Ulaya na Marekani. Hebu tuangalie picha hii ya linaloitwa darasa la kwanza la somo la uuguzi katika ulimwengu wa Magharibi.

Class of 1896

The six women that composed the first graduating class of the Columbia University School of Nursing entered their profession at a time when there was little classroom preparation for nurses. Modeled after European programs, training was based on apprenticeship. Students provided low-cost labor to hospitals and gained invaluable practical experience. Enrollment in increasingly university-based, rather than hospital-based, nursing programs rose after the turn of the century as the need for nurses in both civilian and military life became more and more apparent[7].

14.  Picha hii inathibitisha kuwa si kweli kuwa muuguzi mwanamke lazima avae nguo iliyo juu ya mapaja na inayomuonyesha ujana-jike wake ndiyo aweze kufanya kazi yake. Zama na maadili ya jamii inayohusika ndiyo muamuzi wa kuilinda heshima ya mwanamke au kumdhalilisha kwa ajili ya maslahi ya wanaume wenye uchu wa kujistarehesha kwa uzuri wa wanawake wasio halali kwao. Kama alivyosema Abul A’la Maududi, tunaweza kukitafsiri kivazi anachovaa muuguzi mwanamke hivi sasa kuwa kimelengwa zaidi kuvuta biashara ya wamiliki wa hospitali (ukizingatia kuwa hospitali nyingi za Ulaya ni mali za watu binafsi) na suala la ushindani kibiashara. Hili ni eneo moja ambalo lingepaswa kuangaliwa na wale wanaodai kupigania haki na heshima ya mwanamke. Kwanini mwanamme avae vizuri lakini mwanamke akashifiwe?

 15.  Kuna kauli ambazo hatuwezi kuzithibitisha zinazoeleza kuwa kivazi anachovaa muuguzi mwanamke kimechaguliwa kwa lengo la kumliwaza mgonjwa ili kupata afueni haraka. Iwapo ni kweli, hoja hii inakwenda pale pale kuwa mwanamke ni chombo cha kumstarehesha na kumvuta mwanamme!!! Hapana shaka kuwa huu ni udhalilishaji wa dhahiri shahiri. Suala jengine; kwanini nao wauguzi wanaume wasitakiwe kuvaa nguo na kuwavutia wagonjwa wanaowauguza?

Hijaab kama mfumo wa jamii ya Kiislamu

16.  Muislamu ni katika viumbe ambao Mwenyezi Mungu amewapatia mfumo kamili ya maisha ambao umekamilika na hauhitaji msaada wa binadamu kama ilivyo kwa dini au mifumo mengine ya maisha. Hijaab katika Uislamu si vazi tu bali ni mfumo wa kijamii ambao unatenganisha maisha ya jinsia ya kike na kiume katika sehemu mbili tofauti. Kwa kuwa maisha hayakamiliki bila ya kuja pamoja viumbe hivi, Mwenyezi Mungu amewaekea utaratibu madhubuti wakati wanapokuwa mbali mbali na pale wanapokutana. Mtengano wa jinsia hizi mbili na mchanganyiko wao katika mfumo maalumu ndio unaoitwa hijaab.

17.  Hijaab kama nguo ambayo hukamilika kwa masharti tutakayoyaeleza hapa chini ina maana ya kujificha ili kuepuka kuonekana na asiyestahili. Aya zifuatazo zinawawajibisha (kuwalazimisha wanawake wa Kiislamu) kutekeleza amri hii: -

a.   Na wambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (ambavyo ni uso na vitanga vya mikono). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenziwao, au wale inayowamiliki mikono yao ya kiume, au wale wafuasi wanaume wasio na matamanio au watoto ambao hawajajua mambo yahusuyo wanawake. Wala wasipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao... (24:31)

b.   Ewe Mtume! Waambie wake zako na binti zako na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane na wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu. (33:59)

c.   Katika hadith iliyosimuliwa na Mama Aisha (r.a): siku moja alikuja Asma bint Abibakr kwa Mtume (s.a.w.) akiwa amevaa nguo nyepesi, Mtume aligeuza uso wake na akamwambia: “Ewe Asma! Mwanamke anapofikia balegh (utu-uzima) huwa hapaswi kuonekana chochote katika mwili wake isipokuwa uso na vitanga vya mikono”.

18.   Masharti ya hijaab kwa muhutasari ni haya yafuatayo: -

a.   Vazi la mwanamke ni lazima limuhifadhi sehemu zote za mwili wake isipokuwa zile zinazokubalika na Uislamu. Sehemu hizi kwa hapa kwetu ni uso na vitanga vya mikono.

 

b.   Vazi la mwanamke Muislamu linatakiwa liwe pana na kabisa lisiwe lenye kumbana ambalo halitaonyesha mviringano wa mwili wake.

c.   Vazi la mwanamke Muislamu ni lazima liwe zito ambalo haliruhusu kuonyesha mwili au nguo za ndani. Mavazi mepesi yanayoruhusu kuonyesha rangi ya mwili ni haramu.

d.   Vazi la mwanamke Muislamu lisiwe lile ambalo kwa asili yake ni urembo ambao unavuta hisia za wapita-njia. Vazi hili liwe ni la kawaida kama buibui ambalo halina vitoneo au vikorombwezo vinavyolitafautisha na mabuibui ya kawaida yasiyo na tashwishi.

e.   Vazi la mwanamke Muislamu halipaswi kulingana na nguo za mwanamme.

f.     Vazi la mwanamke Muislamu halipaswi kuwa lenye kulingana na mavazi ya makafiri kama hili linalovaliwa sasa. Kiasili vazi hili ni la ustaarabu wa Magharibi lenye lengo la kumdhalilisha mwanamke.

g.   Vazi la mwanamke Muislamu halitakiwi kuwa lenye kuvuta watu ama kwa rangi zake au mitindo yake.

h.   Vazi la mwanamke Muislamu halitakiwi kuwa lenye manukato yanayowashawishi watu kutaka kujua nani anayenukia hivi au vile.

Wanawake waliovaa hijaab katika vyuo vikuu vya afya

19.  Katika kuthibitisha kuwa vazi hili ambalo linazingatia amri ya Mwenyezi Mungu Muumba wetu si kikwazo kwa mwanamke yeyote anayesomea fani yoyote ya kielimu tumeamua kufanya mapitio katika mitandao na vitabu vya vyuo mbali mbali ulimwenguni. Hapa chini tutaweka picha kuthibitisha hilo. Picha hizi zinazojieleza zenyewe zinawaonyesha wanawake wa fani zinazohusiana na utabibu katika kiwango cha shahada ya kwanza na kuendelea katika vyuo vya Malaysia, Saudi Arabia, Pakistan nk. Nchi hizi zote tunalingana ustaarabu wetu hivyo tumeona ni vyema kuwaangalia wanafanya vipi katika suala hili.

Wepesi na faida ya hijaab kwa wanafunzi wa kike

20.  Picha hizo zilizopo juu ambazo zinawaonyesha wanawake wanafunzi wakiwa katika sehemu mbali mbali kuanzia darasani, majadiliano, wodi za wagonjwa, chumba cha mionzi na chumba cha upasuaji mkubwa wakifanya kazi zote zikiwemo zile za upasuaji ni kielelezo kuwa hakuna kazi za kitatibu wala kiuguzi ambazo haziwezi kufanywa na wanawake wakiwa katika kivazi ambacho wameamrishwa na Mola wao. Pamoja na ukweli huo, hijaab kama sare katika vyuo na skuli ina faida nyingi kwa jamii kama yetu. Miongoni mwa faida za vazi hili ni pamoja na: -

a.   Kuutangaza utamaduni wa Kizanzibari ambao kwa kila hali umefungamana na utamaduni wa Kiislamu.

 

b.   Kuondosha ugumu kwa wanafunzi wa familia za kimaskini katika suala la mashindano ya mavazi wakati wanapokutana na watoto wa familia za kitajiri.

c.   Kupambana na ugonjwa wa ukimwi ambao kwa sasa unaonekana kuzidi kuenea kutokana na kuongezeka kwa vishawishi vya zina.

d.   Ni kwenda sambamba na ukombozi wa mwanamke ambaye hapa tutampima kulingana na uwezo wake wa akili na kujifunza badala ya uzuri wa mwili wake.

e.   Na kubwa zaidi ni kutii amri ya Muumbaji wetu ambaye ametuahidi kuwa tutakapomtii (kumshukuru na kumcha) basi Yeye atatuongezea yale tuliyoyakusudia na kutupa utambuzi wa mambo.

Vipi tuanze?

21.   Baada ya maelezo hayo, hapana shaka suala linalofuatia sasa ni vipi tuanze kwani hilo halihitaji mjadala mkubwa. Sote ni Waislamu, wanafunzi wetu wengi wao ni Waislamu, jamii tunayoihudumia ni ya Waislamu, na hicho ndicho kilio cha watoto wa Kiislamu ambao ni wanafunzi na wauguzi wetu. Hapana shaka kuwa Wizara yetu ya Afya na Ustawi wa Jamii haitakuwa ni ya kwanza katika suala hili. Mifano ya hijaab imejaa tele kuanzia katika maofisi yetu ya Serikali na hata ya watu binafsi. Lakini kwa kusaidia tunadhani Wizara ya Elimu, Utamaduni na Michezo ni ya kupigiwa mfano kwani ina wanafunzi na walimu ambao tayari kwa zaidi ya miaka 15 sasa wanavaa hijaab madarasani, katika maabara na maktaba na hata maofisini. Tuna wahudumu wa Benki ya Watu wa Zanzibar na mifano mengine mingi.

22.  Mchango wa Ukuem katika hili ni: -

a.   Kuchagua kitambaa na rangi yoyote ambayo inahisiwa kuwa ni nzuri kwa wanafunzi wa afya na wauguzi.

b.   Kuchagua aina ya mshono ambao utahakikisha kuwa unafikia masharti ya hijaab kama tulivyoyaeleza katika ibara ya 18 hapo juu.

c.   Kutoa fursa kwa wale wanaotaka kuvaa hijaab kushona kwa mujibu wa maelekezo hayo kama ilivyo kwa wanafunzi wa vyuo mbali mbali chini ya Wizara ya Elimu.

d.   Wizara au Chuo kuchukua hatua zifaazo kwa wale ambao watataka kutumia nafasi au fursa hiyo kuharibu masharti ya vazi hilo au kukidhi matashi yao badala ya yale ya vazi hilo.

23.  Neno la mwisho ni kuwa hakuna lisilowezekana na binadamu ilivyokuwa limeamrishwa na Mwenyezi Mungu Muumba wetu. Mola hatuamrishi kitu isipokuwa ni kwa manufaa yetu. Kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyezi Mungu kwa lengo la kuwafurahisha binadamu ni kielelezo cha utumwa na kukosa dira kwa binadamu mwenye muongozo. Wazanzibari tuna historia ndefu ya ustaarabu wetu hata kabla ya kuja hao ambao hivi sasa tunalenga kuwafurahisha au kuwaiga. Hapana kosa kurudi katika ustaarabu wetu ambao kwa muda wote umekuwa ukimuheshimu mwanamke na kumpa hadhi ambao Mwenyezi Mungu Muumba wake amempa.

 

Imetayarishwa na:

Idara ya Elimu na Da’wah ya UKUEM,

Zanzibar,

--------------------------------------------------------------------------------

 

[1] Microsoft Encarta 97 Encyclopedia, 1993-1996 (ni programu ya computer). Maelezo haya yametolewa chini ya neno “Nursing”.

[2] Angalia “History of Nursing”.

[3] Encarta 97 Encyclopedia.

[4] Abul A’la Maududi, Purdah and the Status of Woman in Islam, Markazi Maktaba Islami, 1992, Delhi-6, uk. 4 na 6.

[5] Ibid. uk. 8

[6] Ibid. uk. 37

[7]"Class of 1896," Microsoft® Encarta® 97 Encyclopedia. © 1993-1996 Microsoft Corporation. All rights reserved.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget