Qur’aan tukufu ni maneno ya Allah aliyoteremshiwa Mtume Muhammad Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam na ikawa ni muujiza uliobaki milele wa kuonesha ukweli na hoja yenye nguvu ya dini ya kiislamuKutokana nayo waislamu, wanapata hukumu na muongozo wa maisha yao ya kila siku duniani na matarajio ya akhera na pia habari za umma zilizotangulia.MAANA YA QUR’AANAsili ya neno Qur’aan linatokana na Qa-ra-a – kusoma na Al Qur-aan ni chenye kuunganishwa pamoja au chenye kusomwaNi maneno ya Allah Subhaanahu Wata’ala aliyoteremshiwa Mtume Muhammad Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam kupitia Malaika Jibreel ‘Alayhi Ssalaam yaliyohifadhiwa katika vitabu na ni ibada kubwa kuisoma kwakeMiongoni mwa majina na sifa za Qur’aan
UBORA NA FADHILA ZAKEAnasema Allah Subhanahu Wata,ala katika Qur’aan(إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلاةَ وَأَنْفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرّاً وَعَلانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَنْ تَبُورَ) (فاطر:29) .Hakika wale wanaosoma kitabu cha Allah, wakasimamisha sala na wakatoa tulivyowaruzuku kwa siri na dhahiri watarajie bishara isiyokatika (Faatwir:29).قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :" ما اجتمع قومٌ في بيت من بيوت الله يتلون كتاب الله ويتدارسونه بينهم إلا نزلت عليهم السكينة وغشيتهم الرحمة وحفتهم الملائكة وذكرهم الله فيمن عنده ".رواه مسلمNa anasema Mjumbe wa Allah Salla Allahu ‘Alayhi WasallamHawakusanyiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allah wanasoma kitabu cha Allah na wanafundishana baina yao ila huteremka juu yao utulivu na hufunikwa na rehma na huzungukwa na Malaika na huwataja Allah mbele ya waliokuwemoMuslimوقال صلى الله عليه وسلم:" البيت الذي يُقرأُ فيه القرآن يتراءى لأهل السماء كما يتراءى الكواكب لأهل الأرض ".Na amesema Mjumbe wa Allah Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam“Nyumba inayosomwa Qur’aan inaonekana kwa waliokuwa mbinguni kama zinavyo onekana nyota kwa watu wa duniani”.وقال صلى الله عليه وسلم :" أفضل عبادة أمتي قراءة القرآن " .Na amesema Mjumbe wa Allah Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam“Bora katika ibadah za umma wangu ni kusoma Qur’aan”وقال صلى الله عليه وسلم :" الذي ليس في جوفه شيء من القرآن كالبيت الخَرِب ".Na amesema Mjumbe wa Allah Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam:“Yule ambaye hana katika kifua chake chochote katika Qur’aan ni kama jumba lilo hamwa.”وقال صلى الله عليه وسلم :" اقرءوا القرآن فإنّه يأتي يوم القيامة شفيعاً لأصحابه... " رواه مسلمNa amesema Mjumbe wa Allah Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam:“Someni Qur’aan hakika itakuja siku ya qiyama kuwaombea msamaha waliokuwa wanaisoma. Muslimوقال صلى الله عليه وسلمالماهر بالقرآن مع السفرة الكرام البررة رواه البخاري ومسلم.Aliye mahiri katika Qur’aan anakuwa pamoja na Malaika walio wakarimu walio wemaBukhariy na MuslimAbu 'AbdiRrahmaan |
Madhumuni ya blogu hii ni matatu: Kwanza:Kuelimishana sisi waislamu mambo yanayo tuhusu (uislamu) Pili:Kujulishana hitilafu zilizopo katika imani nyingine{ifahamike vizuri kuwa lengo sio kukashifu imani nyingine bali kuzitohoa hitilafu zilizopo katika imani hizo ili kuwa na upeo mkubwa wa uelewa utaowasaidia kutoshawishiwa au kutoritadishwa na makafiri (wasio waislamu)}. Tatu: Kuungana na waislamu wengine kwa kuweka makala au post zao hapa ili kusambaza ujumbe uliokusudiwa.
Wednesday, April 4, 2012
Qur'an- Maana,Ubora na Fadhila Zake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment