Thursday, April 5, 2012

Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya

Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuisoma dini yako.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuisoma Quran na Maana yake.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kutafuta sadaka ya kujitolea kwa ajili ya uislamu iwe muda, hali na mali.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya familia yako kuzungumza nayo mambo ya dini.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kutembelea ndugu jamaa na marafiki.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya mkeo kama umeoa na mumeo kama umeolewa.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kumfikiria Allah (sw) na maneno yake na makatazo yake, 
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuzifikiria neema na rehma alizokuneemesha mola wako.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kujiombea dua na usitegemee dua za misikitini na mikusanyiko.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuiendea riziki ya Allah aliokupangia na ukinai na kuridhika nayo.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuongeza ujuzi juu ya Elimu yako ya mazingira na jamii ikuzungukayo .
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuipata na kuitafuta elimu juu ya mwili wako na maumbile yako, kuepuka maradhi na madhara juu yake.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kujishughulisha na hidma mbalimbali kwa ajili yako, uislamu na jamii yako kwa ujumla.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kupumzika baada ya uchovu wa shughuli, mizunguko na fikra nzito.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuwakumbusha watu wako na wakaribu wako juu ya haya.
Ushauri huu utaendelea inshaalah, na mnaalikwa katika muendelezo huu kwa ajili ya kuusiana.


MUHIMU KUZINGATIA HAYA KWANI UJUMBE USHAWAFIKIA
WABILLAH TAWFIQ.



IMETOLEWA UDOMSA

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget