Wednesday, April 4, 2012

UZURI WA SALA ZA SUNNAH (ZILIZOSISITIZWA)


Kutoka kwa mama wa waumini Ummu Habiybah, radhi za Allaah ziwe juu yake amesema; Nimemsikia Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallam akisema;  

Mja yeyote Muislamu anayeswali kwa ajili ya Allaah – kila siku rakaa kumi na mbili za kujitolea (Sunnah) ambazo sio za fardhi, Allaah Atamjengea nyumba peponi. [Muslim].

Maelezo:

Hadithi hii inahimiza na kuonyesha umuhimu wa Sala za Sunnah zilizokokotezwa, ambazo husaliwa kabla/baada ya Sala za fardhi.  Malipo yake ni kujengewa nyumba kwenye pepo kwa mwenye kuzitekeleza. 

Sala hizi ni kama ifuatavyo.

Rakaa mbili kabla ya Sala ya Alfajiri

Rakaa nne (mbili mbili au kwa pamoja*) kabla ya Sala ya Adhuhuri

Rakaa mbili baada ya Adhuhuri

Rakaa mbili baada ya Sala Magharibi

Rakaa mbili baada ya Sala ya ‘Ishaa 

Pia kuna Hadithi nyengine ya Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallam iliyopokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim ambayo inasema ni rakaa kumi ambazo ni sawa hizi ila kwa Adhuhuri huwa ni rakaa mbili tu kabla.

·         Kutokana na baadhi ya mapokezi inakubalika kusali rakaa nne za kabla ya Adhuhuri kwa pamoja zote na kwa Tashahhud moja tu na kisha kutoa Salaam. Na kuziswali rakaa mbili mbili ni bora zaidi; kila rakaa mbili unakaa Tashahhud na kutoa salaam ni bora zaidi kuliko kuziswali zote nne pamoja japo inaruhusiwa.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget