Saturday, February 11, 2012

UTUMWA KATIKA ZAMA ZA KALE


"Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na wana-mume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari." (Qur'an 49:13).
Utumwa sio taasisi iliyoanzishwa na Ukristo au Uislamu. Ni Utumwa ulikuwepo kwa muda mrefu hata kabla ya kuanzishwa hizi dini mbili. Kwa mtazamo wa haraka kuhusu utumwa wa kale, ninamnukuu Jaji Ameer Ali:
"Shughuli ya Utumwa ina rika moja sawa na kuwepo kwa binadamu. Kihistoria dalili zake zinaonekana katika kila zama na kila taifa... Wayahudi, Wayunani, Warumi na Wajerumani wa kale, watu ambao taasisi zao za kisheria na za kijamii zilizoathiriwa mno na tabia na desturi za kisasa, walizitambua na kuzifanya aina zote za utumwa, utumwa wa kazi za kiuchumi na wa kazi za nyumbani. Baada ya kuanzishwa kwa makundi ya washenzi wa Magharibi na Kaskazini katika mabaki ya dola ya Warumi, zaidi ya utumwa wa mtu binafsi, utumwa wa taifa moja kulifanya taifa lingine kuwa mtumwa, ambao haukujulikana sana kwa Warumi, ukashamiri kwenye nchi zote mpya zilizo kaliwa... kanuni za kishenzi, kama zile za Warumi, ziliona utumwa kama hali ya kawaida ya binadamu; na kama mtumwa alipewa ulinzi, ilikuwa kwa sababu mtumwa alikuwa mali inayo milikiwa na bwana wake, ambaye ni yeye peke yake baada ya nchi, alikuwa na mamlaka juu ya uhai na kifo kwa
7
7
UTUMWA
mtumwa.1
Katika nchi ya Uajemi (Persia) ikulu ya Mfalme ilikuwa na watumwa wanawake elfu kumi na mbili. Wakati Mfalme wa Byzantine anaketi kwenye kiti chake cha enzi, maelfu ya watumwa walikuwa tayari kutoa huduma kamili na mamia ya watumwa waliinama kuonyesha heshima wakati mfalme anainama kuvaa viatu. Huko Ugiriki au Uyunani, idadi ya watumwa ilikuwa kubwa zaidi ya watu walio kuwa huru, licha ya kwamba Ugiriki ilitoa watetezi wakubwa wa ubi-nadamu na haki. Kila jeshi la Kiyunani ambalo lilirudi nyumbani na salamu za ushindi, lilifuatwa na kuindi la watumwa. Aristotle, mwanasalsafa maarufu wa zamani, alipokuwa anazungumzia suala la iwapo kila mtu alikusudi-wa na maumbile kuwa mtumwa au la, anasema: "Hakuna ugumu katika kujibu swali hili, katika misingi yote miwili, ya akili na kweli.
Ya kwamba watu baadhi fulani watawale na wengine watawaliwe si tu kwamba ni jambo muhimu bali ni kitu chenye manufaa kuanzia saa ya kuzaliwa kwao, watu wengine wameumbwa ili wawe watumwa, wako kwa ajili ya kutii tu, na wengine wameumbwa kwa ajili ya kutawala." Halafu anahitimisha; "... watu wengine kwa asili wako huru, na wengine ni watumwa, na kwa utumwa huu (uliotajwa) wa mwisho, wote ni wenye manufaa na haki."2Katika utawala wa Rumi, utumwa wa kale ulifika kilele chake, lakini Dola ya Kirumi ilipoanza kuanguka, watumwa wengi wakaanza kuwa na hali nzuri kwa kiwango kidogo.
1 Ameer Ali, Spirit of Islam (London: University paper back, 1965), PP. 259-261; pia angalia Will Duratnt, The Story ofa Civilisation, juzuu ya III (New York, 1944), P.397.
Aristotle, Politics, Book one, Sura ya 5 (New York: Modern Library, 1943), uk. 58-60.
UTUMWA
Lakini uovu wa utumwa ulionekana wazi kabisa. Uovu huu ulishinda ujuzi wa uhalali wa Kiyunani kama ambavyo imeshinda falasfa stadi ya Kigriki.
Kuonyesha mapenzi kwa watumwa lilionekana si tendo la hisia za kawaida lakini ilikuwa tabia pekee ya mtu mwenyewe binafsi. Mtumwa hakuonekana kama binadamu, hakuwa na haki, hakuwa na roho.3Wakati huo wa ujio wa Uislamu (mnamo karne ya 7 CE) utumwa ulikwisha enea kote kote huko India, Ajemi, Rumi, Rasi ya Arabia, Romania na Ugiriki. Watu waliokuwa na hali nzuri na nafasi nzuri na wasomi wa nchi hizi hawakuwatilia maanani watumwa kustahiki kupatiwa hata angalao pia haki za msin-gi za kibinadamu. Mtumwa alikuwa anaonekana kama bid-haa isiyo na thamani zaidi kuliko hata ya ng'ombe.4Mara nyingi mtumwa aliuzwa kwa bei rahisi kuliko kondoo na mbuzi. Kwenye hafla maalum za kijamii wageni waheshimiwa wa nchi walikuwa na tabia ya kukusanyika pamoja na Kiongozi wa Nchi kutazama michezo ya kupi-gana watu na katika michezo hii watumwa walifanywa wapigane kwa kutumia mapanga na mikuki kama vile maonyesho ya mapigano ya jongoo wawili na kware katika kipindi cha zamani cha jamii ya kikabaila. Watu walis-hangilia kwa kupiga makofi hadi mtu mmoja miongoni mwa wapiganaji aliuawa. Watazamaji walimshangilia sana mshindi.5
Kwa upande mwingine, Rasi ya Arabia ilizunguukwa na nchi ambazo bado zilikuwa na dalili za ufahari wa ustaaraabu wa Kirumi na Kiyunani uliokuwa unaporomoka,
3  Durant, W., op.cit., Juzuu ya III uk. 397, Juzuu IV (New York), uk. 29).
4  Ibid
5   ibid.
9
9
UTUMWA
na kwa upande mwingine, ilizunguukwa na nchi zilizogu-bikwa na imani za dini za "Zoroastria" na "Uhindi." Kama ilivyo tajwa hapo juu, kwenye nchi zote hizi utumwa ni taasisi iliyo tambuliwa.
Vibao kumi na mbili vya maandiko (ya sheria zao) vilitoa mhuri wake rasmi kuithibitisha taasisi hii. Ukali usiopungu-ka wa matatizo na ukatili ambao watumwa walifanyiwa, haukupungua, lakini, kwa namna yoyote ile, watumwa sasa walikubaliwa kama wanyama (hayawani) ambao hatima yao ilikuwa ni kufanya kazi na kufa tu kwa manufaa ya hao walio wamiliki. Sina nia ya kukifanya kitabu hiki kuwa his-toria ya unyama waliofanyiwa watumwa lakini itoshe tu kusema kwamba mtu lazima siku zote abebe hatia katika dhamira yake kwamba wakati fulani alijiingiza kwenye uovu wa utumwa.
UKRISTO NA UTUMWA
Ingawaje utumwa ulikuwa taasisi ya kale ambayo ilianza kabla ya historia ya binadamu haijaanza kuandikwa, ni sala-ma kusema kwamba ukubwa wa biashara hii ulifika kilele chake kwa kuendelezwa na mataifa ya Kikristo ya Ulaya na Amerika ambao kama ilivyo kawaida yao, waliigeuza kuwa biashara yenye utaratibu uliopangwa kwa uangalifu sana na wakaanza kuwakamata watumwa kwa maelfu. Kabla hatu-jaanza kutoa maelezo ya biashara hii mbaya sana ya utumwa ambayo ilianzishwa na Wareno, Wahispania na mamlaka zingine za kiubaharia za Kikristo kutoka Magharibi kwa ajili ya makoloni yao mapya, hebu tuangalie kwanza tuone kama Ukristo, kama mfumo na imani, ulifanya lolote wakati wa siku za mwanzo sana kupunguza ukali wa mateso kwa
10
UTUMWA
wengi wa watumwa. Jaji Ameer Ali anaandika kuhusu Ukristo:
Ukristo uliona utumwa kuwa ni taasisi iliyo tambuliwa na himaya (dola); na wenyewe ukakubali mfumo huu bila ya hata kujaribu kupunguza uovu wake, au kuahidi kukomesha polepole, au kuboresha hadhi ya watumwa. Chini ya sheria ya nchi, watumwa walikuwa kama mali inayo hamishika. Waliendelea kuwa hivyo chini ya utawala wa Kikristo. Utumwa ulishamiri miongoni mwa Warumi tangu zama za kale. Watumwa hao ama wamezaliwa wazalendo au wamezaliwa kutoka nje, ama walipatikana kutokana na ushindi wa vita au kununuliwa, walijulikana kama mali tu ya kuhamishika. Mabwana zao walikuwa na mamlaka na uwezo wa kuamua juu ya uhai au kifo kwao. Ukristo ulishindwa kabisa kukomesha utumwa au kupunguza uovu wake.6
Will Durant anatoa maelezo kuhusu nafasi ya Kanisa kama ifuatavyo. Kanisa halikulaani utumwa. Kanisa la Orthodox na waasi, Kanisa la Rumi na washenzi wote walidhani taasisi hii ilikuwa ya kawaida na haingeharibiwa. Sheria za kipagani zilimwingiza utumwani mwanamke yeyote aliye huru ambaye aliolewa na mtumwa; sheria za Mfalme Constantine (Mfalme Mkristo) ziliamuru mwanamke wa aina hiyo kuuawa kwa kukatwa kichwa, na mtumwa mwanamume kuchomwa moto akiwa bado yu hai.
Mfalme Gratian alitoa amri kwamba mtumwa yeyote aliye mshitaki bwana wake kuhusu kosa lolote isipokuwa uhaini dhidi ya serikali, lazima achomwe moto akiwa bado yu hai
6 ameer Ali, op. cit., uk. 260-261
11
UTUMWA
mara moja bila hata kufanya uchunguzi ili kupata uhalali wa shitaka.7
Rekebisho moja tu lililoagizwa na Ukristo linaonekana kati-ka barua ya Mtakatifu Paulo kwa mtu fulani aitwaye Filemoni alipomrudisha mtumwa wake, aliyeitwa Onesimo, na kupendekeza amfanyie wema. Hakuna zaidi ya hapo. Inavutia kuona kwamba neno "slave " ("mtumwa") la asili ya lugha ya Kiebrania limebadilishwa na kuwa "mtumishi wa nyumbani" kwenye toleo la Biblia liitwalo "Authorised Version of the Bible," na likabadilishwa kuwa "mtumwa mtumishi" katika toleo liitwalo "Revised Standard Version," kwa sababu, katika maneno ya "The Concise Bible Commentary," neno hili (yaani mtumwa) limeachwa kutumiwa kwa sababu ya maana yake.8Mtu hushanga iwapo mtarjumi anayo haki ya kubadilisha asili ya neno kwa sababu tu ya maana zake au ukumbusho wake?"
Itavutia kuona hapa kwamba neno "slave" ("mtumwa") ni la asili ya Wazungu. Lilianza kuwapo na kutumika wakati Wajerumani (Franks) walipokuwa wanajishughulisha na kulipatia "Washenzi" soko la watumwa la Wahispania, na mateka hao walio wengi walikuwa Waturuki kutoka jimbo la Slovakia (sasa ni sehemu ya Czecoslovakia). Watu hawa huitwa "Slav" na kwa hiyo mateka wote wakaitwa "slaves."
Nukuu ifuatayo inaonyesha dhahiri mtazamo wa Uislamu na Ukristo kuhusu suala la utumwa na rangi ya ngozi:
7.leeky, W.E. History of European Morals, Juzuu ya II ( New Yolk,
1926), kama ilivyonukuliwa na Will Durant, op. cit., juzuu ya IV, uik.
77.
8. Clarke, Rev. W. K. L, The Concise Commentary (London: S.P.C.K,
1952) uk. 976.
12
UTUMWA
"Mwondoshe mtu mweusi! Siwezi kuzungumza naye," alisema Archbishop Mkristo aliyeitwa Cyrus wakati Waarabu walioshinda walipowatuma wawakilishi wao wenye uwezo mkubwa ili wazungumze kuhusu makubaliano ya kusalimu amri mji mkuu wa Misri, ujumbe huu wa wawakilishi hawa uliongozwa na mtu mweusi aliyeitwa Ubaydah kama mtu mwenye uwezo mkubwa sana kuliko wote. Archbishop, alishangaa alipoambiwa kwamba mtu huyo mweusi alipewa ukubwa na maelekezo na Generali Amr, na kwamba Waislamu huwapa watu weusi na weupe heshima na daraja sawa na huwahukumia watu kwa tabia na si kwa rangi.9
Tukio hili linakupa tu maelezo kwa ufupi kile ninachotaka kueleza kwa urefu zaidi katika kitabu hiki.
UISLAMU UNASHAMBULIA UTUMWA
Uislamu mara nyingi umeelezwa na waandishi wa Kristo kwamba ni dini ambayo si tu kwamba ilifumbia macho utumwa bali pia iliuhimiza. Hii ni shutuma nzito sana iliy-oelekezwa dhidi ya Uislamu, na kwenye kitabu hiki nakusu-dia kuonyesha uwongo wake. Kama ingewezekana, ningechukua mtizamo wenye huruma kwamba shutuma dhidi ya Uislamu zinatokana na kutokujua ukweli, lakini nahuzunika kuona kwamba wakosoaji wengi wanaonyesha kuwa na mwelekeo wa chuki na uovu. Tumeeleza kwa ufupi msimamo wa Ukristo kuhusu utumwa, na maelezo mengi zaidi yatatolewa baadaye. Hapa, kwa kuanzia ngoja tuuan-galie Uislamu na mfumo wa kanuni zake. Kwa kadiri utumwa ulivyohusika, Waarabu katika siku za 9. Leeder, S.S., Veild Mysteries, of Egypt (London, 1912), Uk. 332.
13
UTUMWA
kabla ya Uislamu walikuwa wakosaji wabaya kama majirani zao. Watumwa walikuwa bidhaa ya biashara na utumwa ulikuwa ni asasi iliyokwisha anzishwa. Utumwa ulikuwa chanzo cha kupatia maisha kwa maelfu ya watu na chanzo cha kazi kwa maelfu ya wengi. Kwa watu wenye nafasi nzuri ya maisha idadi ya watumwa ndani ya kaya moja ilikuwa ni alama ya hadhi ya kaya hiyo.
Hii ndio hali iliyo kuwa wakati wa ujio wa Uislamu. Utumwa ulipinga msimamo wa Uisilamu kwa kiasi kikubwa kama ambavyo ibada ya masanamu inavyofanya. Lakini ambapo ibada ya masanamu ina mizizi yake katika mambo ya kiroho na kwa hiyo kuweza kukabiliwa na akili, utumwa mizizi yake ilikuwa katika biashara, katika muundo wa kijamii, katika miradi ya kilimo, na akili peke yake ilikuwa silaha dhaifu ya adui mwenye madhara mno na aliye jikita mizizi yake kwa ndani sana. Ni vipi basi utumwa ungeweza kukomeshwa?
Watu waliofahamishwa vibaya wanaweza kushauri kwamba Mtume wa Uislamu angeliweza kutumia nguvu. Lakini udhaifu wa nguvu kwa madhumuni haya unatambulika vizuri sana kwa wanafunzi wote wa elimu ya jamii wasio na upendeleo. Nguvu inaweza kufanikisha kusalimu amri, lakini bila kuepuka hufanikisha uadui. na mara nyingi uadui ni mkali sana kiasi kwamba mambo mengi mazuri yamepotea wakati nguvu ilipotumika kwa ajili ya maendeleo yake. Hali mbaya ya kusikitisha inayowapata watu weusi wa Marekani, ni mfano mmoja unaoonyesha jinsi gani matumizi ya nguvu yanavyoweza kuwa dhaifu wakati ikiwa lengo ni kupata mageuzi ya kijamii. Ukombozi wa watumwa haukubadilisha msimamo wa watu weupe kwa watumwa wao waliokom-bolewa, na uchungu ulioje wa urithi wa uhasama wa ubaguzi
14
UTUMWA
wa rangi ulioachwa katika jamii! Toynbee ameandika, "Watu weusi ambao walikomolewa kisheria kutoka kwenye utumwa huko Marekani (U.S.A) mnamo mwaka 1862, pamoja na sababu nzuri sasa wanayojisikia kwamba bado, zaidi ya karne moja baadaye, wananyimwa haki kamili za kibinadamu na raia wenzao walio wengi ambao ni Waamerika weupe. 10.
Vita vya Uislamu dhidi vya utumwa vililenga kubadili, msi-mamo na fikira kwa jamii yote, ili kwamba baada ya kukombolewa, watumwa wangekuwa wafuasi wake walio-funzwa na wenye uzoefu wa muda mrefu, bila ya kuwepo na haja yoyote ile ya kufanya maandamano, migomo, maasi ya kijamii na ghasia au fujo za ubaguzi wa rangi. Na Uislamu ulilipata lengo hili lilioonekana haliwezekani (kupatikana) bila vita yoyote ile kupiganwa. Kusema kwamba Uislamu haukupigana vita kwa sababu ya kukomesha utumwa itakuwa si maelezo sahihi. Uislamu ulipigana vita kwa sababu ya kuondoa utumwa, lakini, ni vita ambayo ilipigan-wa si kwa kutumia upanga, wala hakuna damu iliyomwagi-ka.
Uislamu ulilenga vita yake kwenye chimbuko la adui yake (yaani utumwa) na kuunda washirika wake kwa kuamsha hisia zilizo bora zaidi za wafuasi wake. Mashambulizi dhidi ya utumwa yaliendeshwa kwa kulenga pande tatu.
Kwanza, Uislamu ulikataza kununua watumwa na kuwami-liki. Kabla ya kuja kwa Uislamu, utumwa uliendeshwa
10. Toynbee A.J. Mankind and Mother Earth, (N.Y.: Oxford University Press, 1976), uk. 12.
15
UTUMWA
kiholela. Watu waliokuwa wanadaiwa walifanywa watumwa, mateka wa kivita, ama waliuawa. Kwenye mataifa yaliyo kuwa dhaifu, watu waliwindwa kama wanya-ma, wakauawa au kutekwa na kufanywa watumwa. Uislamu katika hali isiyo ya utatanishi, uliwakataza wafuasi wake kuwafanya binadamu wenzao watumwa kwa kisingizio cho-chote kile. Isipokuwa tu kwa yule adui mwabudu sanamu ambaye ametekwa kwenye vita ambayo ilipiganwa ikawa ama ya kujitetea au kwa ruhusa ya Mtume au warithi wake halali. Tofauti hii ilikuwa, kama anavyoieleza Jaji Ameer Ali: "Ili iwe kama dhamana kwa kulinda maisha ya mateka."
11.
Kama Allamah Tabatabai alivyokwisha eleza kwa undani na urefu zaidi, kabla ya Uislamu, watu wenye nguvu, na wapendao kutawala wengine kuwa watumwa, walikuwa na desturi ya kuwafanya watumwa binadamu wenzao waliod-haifu bila kusita. Sababu muhimu miongoni mwa sababu nyingi za kuwafanya watu wengine kuwa watumwa ni hizi zifuatazo:
Vita: Mshindi aliweza kufanya chochote anachotaka kwa adui aliye mshinda. Angeweza kuwauwa wapiganaji waliokamatwa mateka, angefanya kuwa watumwa au pengine kuwaweka chini ya mamlaka yake au makucha yake.
Utawala: Mkuu au mtawala angeweza kumtia utumwani, kutegemeana na hiari yake ipendavyo, mtu yeyote aishiye katika himaya yake.
Ulezi: Baba au babu alikuwa na mamlaka yote kwa kizazi chake. Angeweza kumuuza au kumtoa zawadi; angeweza 11. Ameer Ali, Muhammadan Law, j. 2, uk. 31.
16
UTUMWA
kumwazimisha kwa mtu mwingine, au kubadilishana na mtoto mwingine mvulana au msichana.
Uislamu ulipotokeza, ulibatilisha na kutangulia sababu mbili za mwisho kabisa. Hakuna mtawala au mlezi aliye ruhusiwa kuwafanya raia wake au watoto wake kuwa watumwa wake. kila mtu alipewa haki zake kikamilifu; mtawala na mtawaliwa, mzazi na mtoto walitakiwa kuishi katika mipaka iliyowekwa na dini; hakuna mtu aliye ruhusiwa kuchupa mipaka hiyo.
Na Uislamu ulikataza kwa ukali sababu ya kwanza, yaani, vita, kwa kuruhusu kuwafanya watumwa wale tu waliotek-wa kwenye vita iliyopiganwa dhidi ya adui aliye kafiri. Hapakuwepo na njia nyingine yoyote ambayo mtu ange-fanywa mtumwa. Wakati huo huo, Uislamu ulinyanyua hadhi ya utumwa na kunfikishia mtumwa hali ya kuwa mtu aliye huru na ukafungua njia nyingi za kuwakomboa watumwa.12.
Kabla biashara ya utumwa haijaanza kufanywa katika kiwango kikubwa na watu wa Magharibi (wakati ukoloni ulipoanza), ilikuwa ni katika kupigana vita tu ndipo watu walifanywa mateka. Lakini Uislamu haukuruhusu vita vya uvamizi. Vita vyote vilivyo fanyika wakati wa uhai wa Mtume, vilikuwa vya kujitetea. Si hivyo tu, mbadala ulianzishwa na kuanza kutekelezwa:
"kuwaacha mateka kuwa huru, ama kwa fidia yoyote au bila ya fidia yoyote." (Qur'ani 41 A) Kwenye vita vilivy-
12. al-Tabataba'i Sayyid Muhammad Husein, al-Mizan fi Tafsir'l Qur'an, j. 16, toleo la pili (Beirut, 1390/1971), uk. 338-358.
17
UTUMWA
olazimishwa kwa Waislamu, Mtume aliamuru mateka walioangukia kwenye mikono ya Waislamu wafanyiwe wema wa kibinadamu.
Wenye uwezo waliruhusiwa kununua uhuru wao kwa kulipa fedha kidogo, na baadhi yao waliachwa huru bila malipo yoyote.
Yote yalitegemea uamuzi wa Mtume au warithi wake halali, kwa kuzingatia usalama wa Waislamu na ukubwa wa hatari kutoka kwa adui. Mateka wa vita ya kwanza ya Kiislamu, yaani vita ya Badr, walipewa uhuru kwa malipo ya fidia (malipo yalikuwa fedha au kazi ya kufundisha watoto kumi wa Kiislamu kusoma na kuandika), ambapo mateka wa kabila la Tay waliachwa huru bila malipo yoyote yale ya fidia. 13.
Hata kwenye utumwa wa aina hiyo palikuwepo na sharti lililoambatanishwa kwamba mama asitenganishwe na mwanae, wala ndugu asitenganishwe na ndugu yake wala mume na mkewe wala mtu na ukoo fulani asitenganishwe na watu wa ukoo wake. Mtume na Imamu wa kwanza wa madhehebu ya Shia, Ali bin Abi Talib, walipitisha adhabu zilizokuwa kali sana kwa mtu yeyote yule aliyemfanya mtu huru kuwa mtumwa: adhabu hiyo ilikuwa kukata mkono wa mhalifu.
Ameer Ali anaandika katika kitabu chake kiitwacho "Mohammedan Law:
13. Al-Waqid, Muhammad bin Umar, Kitabul Maghazi, toleo la M. Jones, j. 1. (London: Oxford University Press, 1966), uk. 129; Ibn Sa'd, al-Tabaqatul Kabir, j. 11: 1 (Leiden: E. j. Brill, 1912), uk. 11, 14.
18
UTUMWA
"Kumiliki mtumwa kwa mujibu wa sheria za Qur'ani ilitegemea na sharti la aina ya vita ambayo Waislamu walip-igana, iliyo halisi, halali yaani vita ya kujitetea dhidi ya maadui waabudu masanamu; na iliruhusiwa kwa sababu ya kudhamini ulinzi wa maisha ya mateka... Muhammad ali-ikuta desturi hiyo ipo miongoni mwa Waarabu wapagani; alipunguza ubaya wa uovu huo, na wakati huo huo akaweka sheria kali kwamba isipokuwa kwa ukaidi wa wafuasi wake, utumwa kama anzisho la kijamii ungekoma kuwepo kwa kusitishwa vita ambazo taifa la Kiislamu lilihusika mwan-zoni.
Kukata mwili wa mtu vipande vidogo vidogo pia ilikatazwa kwa dhahiri na Muhammad, na taasisi ambayo ilisitawi huko katika falme ya Ajemi na falme ya Byzantine ilipigwa marufuku na iliwekewa masharti makali sana. Biashara ya utumwa haikujulikana wakati wa utawala wa makhalifa wanne wa mwanzo, "makhalifa waongofu," kama wanavy-oitwa na madhehebu ya Sunni. Hakuna ushahidi hata kido-go, wa kuaminika kimaandishi kwamba kuna mtumwa yey-ote alimilikiwa kwa kununuliwa wakati wa utawala wa makhalifa hao. Lakini baada ya ukoo wa Umayya kuchukua utawala wa ukhalifa, mabadiliko yaliingizwa kwenye msi-mamo wa Uislamu. Muawiyah ndiye aliyekuwa mtawala wa kwanza Mwislamu ambaye aliingiza katika ulimwengu wa Muhammad (wa Kiislamu) mpango wa kuwapata watumwa kwa njia ya kuwanunua. Pia Muawiyah alikuwa khalifa wa kwanza kutumia mila ya Byzantine ya kuwalinda wanawake zake kwa kutumia watu walio hasiwa. Wakati wa utawala wa ukoo wa Abbas, Imamu wa madhehebu ya Shia, Jafar al-Sadiq alihubiri dhidi ya utumwa, na fikira zake zilikubaliwa na Mutazila. Karmath, ambaye alisitawi wakati wa karne ya
19
UTUMWA
tisa kwa kalenda ya Kikristo... anaonyesha aliuona utumwa kuwa kinyume cha sheria.14.
Hivyo tunaona kwamba bidii ya Uislamu kujaribu kuwazuia wafuasi wake kupatana na kumiliki watumwa ilikwamishwa na Banu Umayyah. Na lazima niweke kwenye kumbukum-bu kuonyesha fedheha inayo endelea na kugusa idadi kubwa ya Waislamu, hawakujali kabisa maagizo ya Mtume na amri za makatazo za Qur'ani, na Waarabu pia walishirikiana na Wakristo wa Ulaya kwenye biashara inayo chukiza mno ya watumwa ya Afrika ya Mashariki. Biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi, yote ilikuwa katika mikono ya Wakristo wa Ulaya.
Pili, Uislamu ulianzisha kampeni kabambe ya kuwakomboa watumwa. Ukombozi wa watumwa ulitangazwa kuwa fidia ya kulipia dhambi kadhaa. Suala hili linahusiana na sheria za Uislamu lakini, tutaorodhesha chache miongoni mwao ili kuonyesha jinsi gani dhambi ndogo zilisamehewa kwa adhabu ya fidia ya kumwacha mtumwa huru. Mathalani, kama mtu alishindwa kufunga saumu bila sababu ya maana wakati wa mwezi wa Ramadhani, au kama alishindwa kufunga saumu ya itikafu au kiapo cha nadhiri, na kadhali-ka, fidia yake ilikuwa kumpa uhuru mtumwa mmoja kila siku aliyokosa kufunga, pamoja na kulipa kwa kufunga saumu baadaye. Vivyo hivyo, kwa kila kosa la nadhiri, mtumwa mmoja aliachwa huru kama fidia; au kosa la kuchana mtu nguo zake kama kuonyesha huzuni yake mtu kwa kufiwa na mke au mtoto; au kama mwanamke anajipi-gapiga au kujikata au kuvuta nywele zake kuonyesha huzuni ya kufiwa na yeyote; au kujiua kwa ajali na; wakati mwingine hata kwa sababu ya kumuua Mwislamu kwa 14. Ameer Ali Muhammadan Law, j. 2, uk. 31-2.
20
UTUMWA
kukusudia; au kama mume alimwambia mkewe kwamba alikuwa kwake kama mama yake, na kwa makosa mengine mengi.15. Kutoka kwenye mifano hii, mingine haina uzito lakini ilipenya kwa kina kwenye utamaduni wa Waarabu, mtu anaweza kuona jinsi gani sheria za kidini zilivyofung-wa kwa lengo la kuwakomboa watumwa, na hatimaye kukomesha kabisa laana ya utumwa katika jamii.
Inawezekana pia ikahojiwa kwamba kwa kuamrisha ukom-bozi wa watumwa kama kafara ya dhambi, Uislamu ulikuwa unaruhusu taasisi ya utumwa iendelee kudumu. Hii haikuwa hivyo. Kwa kila namna ya ukombozi wa mtumwa kulikofanywa kama kafara, aina nyingine vile vile ya kafara ilielekezwa badala yake - ikionyeshwa wazi kwamba lengo la Uislamu lilikuwa katika wakati muafaka wa kujenga jamii iliyo huru kutokana na taasisi hii yenye madhara. 16.
Pia Uisilamu ulitangaza kwamba mwanamke yeyote mtumwa ambaye anazaa mtoto na bwana wake anayemmili-ki, ilikuwa si ruhusa kumuuza, na kama mzazi mwenzake (mmiliki wake) akifa, mwanamke huyo anakuwa huru moja kwa moja.17. aidha, kinyume na mila zingine zote za huko nyuma, Uislamu uliamuru kwamba mtoto aliyezaliwa na mama mtumwa kutokana na bwana wake anayemmiliki, basi lazima mtoto afuate hadhi ya baba yake.
18. Watumwa walipewa haki ya kujikomboa wenyewe ama kwa malipo ya fedha au kufanya kazi kwa mapatano ya
15. Al-Khu'i, Sayyid Abu'l Qasim, Minhajus-Salihin, toleo la tatu, j. 11 (Najaf, 1974), uk. 328-331, vile vile tazama Qur'an: 4:92, 5:89 na 58:3.
16. Ibid.
17.  al-Amili, Hurr, Wasa'ilu'sh-Shi'ah, j. 16 (Tehran, 1983), uk. 128.
21
UTUMWA
kipindi cha makubaliano. Kauli ya makubaliano ya kisheria huitwa mkataba. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'ani:
"Na wanaotaka kuandikiwa wapate uhuru katika wale
ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni...." (Qur'an 24:33)
Neno kitab kwenye maana yake ni makubaliano ya maan-dishi baina ya mtumwa na mmiliki wake unaojulikana kama "Mukatabah - hati ya mkataba." Jambo la muhimu kwenye mukatabah ni kwamba pale ambapo mtumwa anataka kufanya makubaliano ya maandishi ya aina hii, bwana wake lazima akubali.19. Kwenye aya iliyonukuliwa hapo juu, Mungu amefanya wajibu kwa Waislamu kuwasaidia watumwa katika kujikomboa.
Mtumwa anapotaka kujikomboa, bwana wa mtumwa si tu kwamba akubali, lakini pia anatakiwa amsaidie mtumwa kiasi fulani kutoka kwenye utajiri wake mwenyewe,20. kiasi tu cha utoaji wa kuridhisha katika hali ambayo
18. Ibid.
19.  al-Amili, op. cit., j. 16, uk. 101
20.Ibid.
22
UTUMWA
mtumwa ataweza kuishi maisha ya kuheshimika baada ya kupewa uhuru wake.
Hivyo, miaka 1400 iliyopita, Uislamu ulishughulika katika njia ya ufanisi zaidi kuangamiza utumwa. Pia Uisilamu ulielekeza kwamba watumwa waliokuwa wanataka kujikomboa, kuwa uhuru lazima wapewe msaada kutoka hazina ya taifa (baytul mal).21Hivyo, kama tegemeo la mwisho, Mtume na warithi wake wa haki walitoa fidia ya kuwapa uhuru watumwa kutoka kwenye hazina ya taifa. Qur'ani inatambua ukombozi wa watumwa kama ni njia moja wapo ya ruhusa ya matumizi ya sadaka na misaada.
(Angalia (Qur'ani 9: 60, 2:177)
Na inafaa kukumbuka kwamba mtumwa anakuwa uhuru moja kwa moja kama bwana wake akimkata sikio lake au kumpofua jicho lake.22. Pia kama watumwa anayeishi kwenye nchi ya Kiislamu, wakikubali Uislamu mbele ya wamiliki wao, basi, watakuwa huru moja kwa moja. Kama mtumwa akiwa kipofu au akipata kilema chochote ataachwa huru.23. kwa mujibu wa Imamu Jafar al-Sadiq (amani iwe juu yake.), kama mtumwa ni Mwisilamu na amefanya kazi kwa miaka saba, basi alistahili kupewa uhuru wake. Kumlazimisha mtumwa huyo kuendelea kufanya kazi hairuhusiwi.24. Ni kwa sababu ya hadithi hii kwamba wanachuoni wa kidini wana maoni kwamba kumpa uhuru mtumwa baada ya kufanya kazi kwa miaka saba ilikuwa ni tendo la wema linalopendekezwa sana. Kwa nyongeza katika njia hizi za lazima, na za hiyari za
21.Ibid., uk. 121-2
. al-Hilli, Muhaqqiq, Sharaya'ul Islam, (kitabul-'Itqad), vile vile tazama Encyclopaedia of Islam, j. 1. (Leiden: E. J. Brill, 1960), uk. 31. 23.Ibid., uk.31-3 24. Ibid, uk. 43-4.
23
UTUMWA
kuwakopmboa watumwa, ilitajwa kama muundo safi sana wa sadaka. Imamu Ali aliwakomboa watumwa elfu moja, aliwanunua kwa fedha yake mwenyewe.25. Imamu wa saba - Musa al-Kazim naye aliwakomboa watumwa elfu moja. Imamu wa nne, Ali bin Al-Husein, alikuwa na tabia ya kumpa uhuru kila mtumwa aliyekuwa chini ya miliki yake kila Sikukuu ya Iddi (adhimisho la kila mwaka la Waislamu.) Ni muhimu kuzingatia kwamba katika matukio yote yaliyotajwa hapo juu, watumwa wote waliopewa uhuru walipatiwa njia za kutosha za kuwawezesha kujipatia riziki katika hali ya kuheshimika.
Uislamu ni ya kwanza na ndio tu dini ambayo iliagiza ukombozi wa watumwa kama jambo jema na likiwa ni shar-ti la mtu kutambulika kuwa ana imani ya kweli katika kumwamini Mungu. Hakuna dini nyingine zaidi ya Uislamu ambayo ilihubiri na kuamuru kwa njia ipi iliyo bora kabisa kuliko zote ya kuonyesha mapenzi kwa binadamu wenzetu walioko kwenye utumwa. Kwenye sura ya 90 ya Qur'ani, kumwacha mtumwa huru imeagizwa kama msingi mwema na ulio mkuu kabisa wa imani: "Hakika tumemuumba mtu katika taabu. " Je, anad-
25. Ibid., uk. 3.
24
UTUMWA
hani kwamba hapana yeyote mwenye uwezo juu yake? anasema: Nimeharibu mali nyingi (bure) je, anadhani kwamba hapana yeyote anayemuona? Je, hatukumpa macho mawili? Na ulimi na midomo miwili. Na tuka-muongoza njia mbili Lakini hakupita njia nzito Na nini kitakujulisha njia nzito ni nini! Ni kumwacha huru mtumwa: (sura 90:4-13)
Ni lazima ielezwe kwamba uachaji uhuru mtumwa ni jambo ambalo limependekezwa sana. Uislamu ulidhibiti utumwa kwa njia nzuri, yenye upendo na inayotekelezeka, hivyo kwamba ilifanya kumtunza mtumwa ilikuwa ni wajibu mkubwa sana kwa bwana wake, na wakati huo huo uliamu-ru kuwajali na kuwatendea wema mkubwa watumwa, hivyo kwamba mara nyingi watumwa walipoachwa huru hawaku-taka kuondoka na kutengana na wale walio wamiliki.
Tatu, Uislamu uliwarejeshea watumwa heshima na kun-yanyua hadhi zao kijamii. Uislamu haukutofautisha baina ya mtumwa na mtu aliye huru, na wote walitendewa kwa usawa, bila ubaguzi. Ulikuwa ukweli huu kwamba ndiyo siku zote ulivyo wavuta watumwa kwenye Uislamu. Inasikitisha na inaumiza moyo kuona kwamba wale wasioacha makelele yao yasiyo ya haki ya kuukosoa Uisilamu hawataki kuona msimamo huu wa usawa, ambapo hata wakati huu wa kipindi cha kuelimika zipo nchi zenye kutunga sheria zinazobagua umati wa walio wengi, na kuwaweka kwenye hali halisi ya utumwa.
Uislamu hautambui tofauti ya taifa au rangi ya ngozi, nyeusi au nyeupe, raia au wanajeshi, watawala au watawaliwa; wote hawa wapo sawa, si tu kinadharia bali katika hali halisi. Muadhini wa kwanza (mpiga mbiu wa mwito wa Sala) wa Uislamu, mfuasi mtiifu (mpenzi) wa Mtume na sahaba
25
UTUMWA
aliyeheshimika sana, alikuwa mtumwa mweusi (Mhabeshi). Qur'ani inaweka kipimo cha ubora wa mtu kwenye Aya ya 13 Sura ya 49. Maneno haya yameelekezwa kwa binadamu, umati wote wa dunia yote, na yanahubiri undugu asilia wa mwanadamu bila kutofautisha kabila, ukoo, taifa au rangi ya ngozi. Inasema: "Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na
mwanamune na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa mbali mbali na makabila mbali mbali ili mpate kujuana tu. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari." 49:13
Aya hii inaweka wazi mtazamo wa Uislamu kuhusu maisha ya binadamu hapa duniani. Inaweka kigezo kimoja tu cha ubora au hadhi na hicho ni uchaji Mungu, chenye maana ya utiii na unyenyekevu kamili kwa ayapendayo Mwenyezi Mungu. Aya hii inateketeza na kuangamiza kabisa tofauti zote zilizotengenezwa na binadamu na zilizo za bandia kuhusu taifa na rangi ya ngozi, ambazo tunaziona kila mahali duniani kote hadi sasa. Kuelzea ubora wa
26
UTUMWA
uchamungu, ngoja tuangalie Mwenyezi Mungu anavyose-
ma:
"Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa
Mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anayemuami-ni Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao na katika kuwakomboa watumwa na akawa ana shika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita hawa ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao." (Qur'ani 2:177)
Aya hii kwa wazi kabisa inaonyesha kwamba kwa yenyewe, hakuna wema maalum katika kuelekea upande wowote mahususi wakati wa Sala. (Umoja wa Qibla unaonyesha
27
UTUMWA
umoja wa imani ambayo hupelekea kwenye umoja wa kiro-ho na kufikia kilele cha ulinganifu wa kimwili.) Imani na ibada iliyoamrishwa katika aya hii ndio wema halisi, na mbali ya kuamriwa na Mungu, zinavutia kwenye fikra za mwanadamu. Tafadhali zingatia kwamba, "kutoa mali kwa upendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili... wale walioko kwenye utumwa," ni mojawapo ya wema huo. Katika hadithi ya Imamu Muhammad al-Baqir, inasemekana kwamba mtu anapompiga mtumwa wake (mwanamume au mwanamke), bila ya sababu yoyote ile ya halali, ipo njia moja tu ya fidia ya kosa hilo nayo ni kumpa uhuru hata kama tendo hilo la kupiga lipo katika mipaka iliyowekwa na Mungu. Katika hadithi nyingine, Zurarah alimuuliza Imamu huyo huyo kuhusu msimamo wa bwana kwa watumwa. Imamu akamjibu kwamba; "kitendo kinachofanywa na watumwa bila kukusudia hakistahili adhabu lakini watumwa wakikataa kumtii bwana wao mfululizo na kwa kukusudia, basi hapo ndipo wanapostahili kuadhibiwa." Itakuwa ni jambo la kuvutia kwamba, mtumwa alipewa haki ya kumshitaki bwana wake. Hadithi ya tatu kutoka kwa Imamu huyo huyo inasema kwamba mtu mwenye tabia nne zifuata-zo atasamehewa dhambi zake na atapandishwa na kuwekwa juu sana katika mazuri ya himaya za Peponi. (1) Mtu anayempa hifadhi yatima na kumtimizia mahitaji na kum-wondolea matatizo yake na anakuwa mwema kwake kama baba yake, anampa mapenzi ya wazazi wake; (2) mtu aliye mwema na mwenye huruma na anawasaidia wasio na uwezo; (3) mtu anaye toa matumizi kwa wazazi wake na ni mwenye huruma, mwenye kuwafikiria na kuwaangalia; (4) na mwisho, mtu ambaye hamkasirikii mtumishi au mtumwa wake na humsaidia kazi ambayo ameamriwa kuifanya na hampi kazi ambazo zipo nje ya uwezo wake kuzifanya. "Uisilamu umeagiza kwamba bwana amfanyie mtumwa
28
UTUMWA
wake kama mmoja wa jamaa ya familia yake, mtumwa laz-ima apate mahitaji yote ya muhimu katika maisha yake, kama anavyopata mtu mwingine katika familia hiyo. Mtume alikuwa na tabia ya kula pamoja na watumwa na wafanyakazi wake, na kuketi na kuzungumza nao, yeye mwenyewe Mtume hakula chakula kizuri zaidi kuliko wao wala hakuvaa nguo nzuri zaidi kuliko wao, wala hakuwabagua kwa namna yoyote ile.
"Wamiliki wa watumwa walilazimishwa wasiwape shida watumwa wao, ilikuwa si ruhusa kuwatesa, kuwatukana au kutowatendea haki watumwa. Watumwa walipewa fursa ya kuoana wao kwa wao (kwa ruhusa ya wamiliki wao), au na wanamume walio huru au wanawake walio huru. Watumwa waliruhusiwa kutao ushahidi, na kushiriki katika mambo yote pamoja na watu walio huru. Wengi katika wao wali-teuliwa kuwa magavana, makamanda wa jeshi na watawala.
"Mbele ya macho ya Uisilamu, mtumwa mcha Mungu anapewa nafasi ya juu zaidi kuliko mtu aliye huru lakini si mcha Mungu." 26.
Imeelezwa kwenye hadithi za kuaminika kutoka kwa Mtume kwamba, bwana ni lazima amlishe mtumwa wake chakula anachokula yeye na amvishe mavazi anayovaa yeye. Kwenye hotuba yake maarufu aliyo hutubia huko Arafat tarehe 9 Dhul-Hijjah 9 A.H. wakati wa hija yake ya mwisho, Mtume alisema; "...na watumwa wenu, zingatieni kwamba mnawapa chakula mnachokula nyinyi na muwav-ishe nguo ambazo nyinyi mnavaa.
Na kama wakifanya kosa ambalo hungependa kusamehe 26. at-Tabataba'i, op, cit, j. 338-358.
29
UTUMWA
basi wauzeni, kwani wao ni watumishi wa Mwenyezi Mungu na si vema kuwatesa.." 27.
Kusema kwamba Uisilamu uliwatendea watumwa wema kwa mujibu wa msingi wa usawa ni kutokusema ukweli wote. Kwa sababu, kwa kweli, kwa idadi fulani ya makosa, adhabu inayotolewa kwa mtumwa ilikuwa nusu ya ile iliy-otolewa kwa wengine.28.Hii ilikuwa tofauti na jinsi mataifa mengine yalivyo wapa adhabu kali zaidi watumwa kuliko watu wengine. Profesa Davis anaandika; "Sheria ya makosa ya jinai takriban kila mahali ilikuwa kali zaidi kwa watumwa kuliko watu huru." 29.
Mtume wa Uislamu kila mara aliwasihi wafuasi wake kuwa-tendea wema watumwa wao kama jamaa wa familia zao. Yeye na familia yake mara kwa mara waliwatendea wema watumishi wao.
Mtumishi mwanamke katika familia ya Fatimah, binti yake Mtume, anasadikisha kwamba, bimkubwa wake (Fatuma) alikuwa na desturi ya kugawana naye kazi zote ngumu za nyumbani na alisisitiza kwamba mtumishi lazima apumzike kila baada ya siku moja ambapo yeye, Fatimah, angefanya kazi zote. Hivyo, palikuwepo na mgawanyo sawa wa kazi baina ya bimkubwa na mfanyakazi wa ndani.
Pia imetaarifiwa kwamba siku moja Ali na mtumishi wake wa kiume Qambar walikwenda dukani ambapo Ali alich-agua nguo mbili, moja ilikuwa nguo ya bei ya chini na hafi-fu na nyingine nzuri na ghali.Ali alimpa Qambar ile nguo 27Ibn Sa'd, op, cit, j. 11:1, p. 133; al-Amili, op. cit., j. 16, 21.
28.al-Amili, op. cit., j. 18, uk. 401f. 527-8, 586-7; j. 19, uk. 73, 154f.
29.Davis, D.B., The problem of Slavery in Western Culture (N. Y: 1969), uk. 60.
30
UTUMWA
nzuri. Qambar akashtuka: "Ewe Bwana wangu!" Alisema: "Nguo hii ni nzuri zaidi na wewe ni mtawala wa Waislamu. Chukua wewe nguo hii." Ali akajibu, "Hapana, Qambar, wewe ni kijana na vijana sharti wavae nguo nzuri." Je? kitendo cha namna hii kingemfanya mtumishi ajihisi kuwa yeye ni mtu duni miogoni mwa watumwa? Wamiliki wa watumwa hawakuruhusiwa kuwapa watumwa wao kazi nyingi kuzidi uwezo wao. Waliagizwa kamwe wasiwaite watumwa wao wanaume na wanawake kwa majina ya kud-halilisha, lakini badala yake walitakiwa wawaite majina yenye huba zaidi kama: "kijana wangu," au "msichana wangu wa kazi" iliamriwa pia kwamba watumwa wote laz-ima wavae nguo na wale chakula sawa na wamiliki wao wa kiume na wa kike. Iliagizwa pia kwamba katika hali yoyote ile mama asitenganishwe na mtoto wake, wala kaka kutenganishwa na kaka yake, wala baba kutenganishwa na mtoto wake, wala mume kutenganishwa na mkewe, wala ndugu kutenganishwa na ndugu yake.
Sasa ngoja turejee kwenye Qur'an:
"Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe
31
UTUMWA
na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili, na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia (msafiri) aliyeharibikiwa, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi mwenye kiburi, ajivunaye." (4:36)
Mtukufu Mtume alimpa mtumwa Abu Dharr al-Ghifari kama zawadi yake na akamwambia amtunze katika hali iliyo bora kabisa, ampe chakula kile anachokula yeye, amnunulie nguo zozote zile anazozipenda yeye. Abu Dharr alikuwa na joho ambalo kwa haraka alilikata vipande viwili, na akampa kipande kimoja mtumwa. Mtume akasema: "vizuri sana!" Abu Dharr akamchukua mtumwa huyo hadi nyumbani kwake na akampa uhuru. Mtume akafurahi sana kwa kiten-do cha Abu Dharr na akasema: "Mungu atakulipa kwa hilo." Jinsi Imamu wa nne, Zaynul Abidin alivyomtendea -msichana wake mtumwa inajulikana sana katika historia ya Kiisilamu. Wakati fulani ilitokea mtumwa huyo msichana alikuwa anamtengea chakula Imamu, kwa bahati mbaya, akaangusha bakuli lenye mchuzi wa moto na ukamwagika juu yake. Mtumwa huyo wa kike alitambua dhara na mau-mivu aliyomsababishia Imamu. Mtumwa huyo alikuwa anajua tabia ya mtukufu Imamu na akaanza kukariri aya ya Qur'an:
"... Na wazuiao ghadhabu."
Imamu akajibu:
"Nimejizuia ghadhabu yangu,"
mtumwa akaendelea:
"na wanaosamehe watu;"
Imamu akasema:
"Nimekusamhe,"
32
UTUMWA
Hatimaye, mtumwa huyo msichana akasema:
"Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani;"
Imamu akajibu:
"Nimekuacha huru ili nitafute radhi ya Mungu."
Mtumwa huyo msichana alinukuu maneno hayo kutoka aya ya 134 Sura ya 3 ya Qur'an. Aya hii inasomeka ifuavyo: "Ambao hutoa katika (hali ya) wasaa na katika (hali ya) dhiki, na wajizuiyao ghadhabu na wanaowasamehe watu (na wawafanyiao ihsani); na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani."
Wakati fulani mtu mmoja alisema kwamba watumwa wa Imamu Zaynul Abidin huambizana wao wakisema kwa wao kwamba walikuwa hawamwogopi bwana wao. Aliposikia habari hii, Imamu alisujudu kwa Mungu kumshukuru na akasema: "Ninamshukuru Mungu kwamba viumbe wake hawaniogopi." Kutokana na yale ambayo tumeyasema hapo juu lazima ieleweke dhahiri jinsi gani watumwa walivy-opendwa na kutendewa wema na Mtukufu Mtume na Maimamu wa Ahlul Bait, na wale waliofuata maamrisho ya Qur'an na mifano iliyowekwa na Mtume na Maimamu.
Kuhusu msimamo wa bwana Mwislamu anaye miliki mtumwa na watumwa wake, Will Durant anasema: ".... Aliwatendea katika hali ya ubinadamu mchangamfu na wa huruma hali iliyowafanya wajione wanafuraha na labda pengine salama zaidi kuliko mfanyakazi wa kiwandani katika kipindi cha karne ya 19 huko Ulaya." 3°.
Mwishoni mwa karne ya 18, Mouradgead' Ohsson (chanzo
30. Hurgronje C., Muhammedanism, (N.Y., 1916), uk. 128, kama ilivy-onukuliwa na W. Durant, the story of Civilization, j. 4. (N.Y., 1960)
33
UTUMWA
kikuu cha taarifa cha waandishi wa Magharibi kuhusu ufalme wa Ottoman) alitamka:
"Labda pengine hakuna taifa ambalo mateka, watumwa, wavuja jasho katika manchani wana kirimiwa vizuri zaidi au kutendewa wema zaidi ya vile watendewavyo miongoni mwa wafuasi wa Muhammad." 31
P. L. Rwiere anaandika: "Bwana mwenye kumiliki mtumwa aliamuriwa kumgawia mtumwa wake riziki aliyopewa na Mungu. Lazima itambuliwe kwamba, kwa hili, mafundisho ya Kiisilamu yaliafiki heshima ya namna hiyo kwa utu wa mwanadamu na kuonyesha maana hasa ya usawa ambao ulitafutwa bila kupatikana katika kipindi cha ustaarabu wa kale." 32
Na si katika ustaarabu wa kale tu; hata pia wakati huu wa sasa wa ustaarabu wa Kikristo, imani iliyojengeka ya mam-laka ya juu sana ya kimbari bado ingali inajionyesha kila siku. A.J. Toynbee anasema kwenye kitabu kiitwacho "Civilazation on Trial, " "Kufutika kwa tofauti katika msin-gi wa kiambari (kitaifa) miongoni mwa Waisilamu ni moja ya mafanikio makubwa kabisa ya Uislamu, na katika dunia ya leo, kama inavyotokea kuna kilio cha haja, kwa ajili kuu-tangaza na kuueneza wema wa Kiisilamu.." Halafu anasema kwamba "katika jambo hili la hatari la kuendekeza kuji-hisi tofauti ya kiambari (kitaifa) hakuwezi hata kidogo kukataliwa kwamba (ushindi wa watu wanaosema Kiingereza) kumekuwa ni balaa." 33
Napoleon Bonaparte amenukuliwa akisema kuhusu hali ya
31. Kama ilivyonukuliwa katika The Encyclopaedia of Islam, j. 1 uk. 35.
32. Riviere P.L., Revue Bleaue (June 1939).
33. Tonbee, A.J., Civilization on Trial (New York, 1948), uk. 205.
34
UTUMWA
watumwa kwenye nchi za Kiisilamu: "Mtumwa hurithi mali ya bwana wake na anaweza kumuoa binti yake. Wengi wa watu wa vyeo juu waliwahi kuwa watumwa. Wengi wa Mawaziri Wakuu, wamamelukewote, Ali Ben Mourad Beg, walikuwa watumwa! Walianza maisha yao kwa kufanya kazi za mikono nyumbani kwa wamiliki wao na baadaye walipandishwa katika daraja kwa sifa zao au kwa upen-deleo. Katika nchi za Magharibi, kinyume chake, wakati wote mtumwa wa nyumbani; nafasi yake ni ile ya chini kabisa. Warumi waliwaacha huru watumwa wao, lakini kamwe watumwa walioachwa huru hawakulinganishwa na wazawa. Fikira za watu wa Mashariki na Magharibi zinato-fautiana sana hivyo kwamba ilichukuwa kipindi kirefu kuwafanya Wamisri kuelewa kwamba jeshi lote lilijumuisha watumwa walio milikiwa na Sultan al-Kabir.34.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget