Monday, February 20, 2012

Kuitambua hadithi sahihi


Hii ni fani katika somo la Sayansi ya Hadiyth, somo ambalo lachukuliwa kwa muda usiopungua miaka minne kwa mwanafunzi ili kupata shahada ya kwanza.


Ama Hadiyth iliyo Swahiyh huwa na sifa zifuatazo:

1.     Isiwe inapingana na Aayah ya wazi ya Qur-aan.


2.     Ni lazima itaje kwa uwazi kabisa kuwa kitu kadhaa kilisemwa au kufanywa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).


3.     Mpokezi ni lazima awe shahidi kwa tukio analolisimulia.


4.     Ni lazima itolewe ushuhuda kuwa kila mpokezi alikutana na yule kabla yake katika Isnadi.


5.     Kila mpokezi katika Isnadi ni lazima awe ni mtu anayejulikana kwa uchaji Mungu, uaminifu, ukweli na utendaji wa ‘amali nzuri.


6.     Kila mpokezi katika Isnadi ni lazima awe anajulikana kwa kisomo na akili muruwa, na muweza wa kufahamu barabara na kuyafikisha kwa uaminifu na uhakika kwa wengineo yale aliyoyasikia.


7.     Ni lazima ithubutu kuwa wapokezi wote walikuwa katika zama ambazo walikuwa na uwezo wa kuyafahamu vilivyo yote waliyoyasikia.



Ama kinyume na hizo sifa inafanya Hadiyth kuwa dhaifu, munkar au iliyozuliwa.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget