Sunday, February 12, 2012

KAFARA YA YESU


Kwa  Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema,Mwingi wa Ukarimu.


MAELEZO YA  KAFARA
Wakristo wadai kwamba Mwenyezi Mungu ana mwana, aliye
mwanawe wa pekee. Huyu mwana wa Mungu alijipa utu tumboni
mwa Maria. Maria na mumewe Joseph  seremala wakajulishwa hayo
na Malaika na baada ya muda mwana wa Mungu akazaliwa sawa na
mtoto wakibinadamu. Akalelewa kama mtoto wa wakibinadamu na
alipokua akafanya miujiza. Mwana huyo ndiye Yesu aliyezaliwa katika
Wayahudi ambao walimtesa na mwishowe wakamuua kwa kumtundika
msalabani. 
Hivyo ndivyo mwana wa Mungu aliyejipa utu alivyokufa
na akashukia jahanamu alikokaa siku tatu. Kisha akafufuka toka wafu
na sasa yuko mbinguni akikaa kuumeni kwa Mungu.
Yesu ingawa hakuwa na kosa lolote, hata hivyo alivumilia mateso
kwa ajili ya wanadamu ili kwa mateso yake awe kafara kwa dhambi
za wanadamu. Kwahiyo, yule anayemkubali hawezi kuadhibiwa kwa
ajili ya dhambi zake kwa  maana Yesu amejitwika dhambi zote za
watu. 
Wana wa Adamu wote ni wenye dhambi, ndivyo wasemavyo
Wakristo. Adamu na Hawa walifukuzwa toka bustanini kwa ajili ya
dhambi yao ambayo imerithiwa na wazao wao wote wanaozaliwa.
Kwa sababu hii, Wakristo wanasema, ndiyo maana mwana wa Mungu
hakuingia tumboni mwa Maria kwa njia ya mbegu ya mwanadamu,
bali Maria alitunga mimba bila kuguswa na mwanamume yeyote wasije
wakarithi dhambi ya Adamu kama wazao wake wengineo.

HAJA   YA  KAFARA
Baada ya kueleza asili na maana  ya  kafara kama wasemavyo
Wakristo, sasa nitaeleza haja yake kwa mradi wa fikara za Kikristo.
Wakristo wadai kwamba mwanadamu ni mwenye dhambi na mwisho
wa dhambi ni adhabu ya moto.  Mwenyezi Mungu  ni mwenye huruma6
Mungu  ni mwenye huruma na huruma yake yataraji kwamba
mwanadamu aepushwe kutokana na adhabu hii. Lakini pia Mwenyezi
Mungu ni mwenye haki na haki yake Mungu inataka itolewe adhabu.
Je, ingaliwezekana huruma na haki kutumika pamoja? Mwana wa
Mungu aliyekuwa hana kosa lolote akatoa jawabu la tatizo hili. Alitoa
jawabu kwa kujitolea kuadhibiwa mahala pa mwanadamu na
Mwenyezi Mungu akaridhia sadaka hiyo na kujitolea huko. Hivyo
haki na huruma ya Mungu vikafanya kazi pamoja. Adhabu  juu ya
madhambi ya watu ikatolewa na watu pia wakawa huru! Adhabu ya
dhambi za wanadamu ilikuwa nzito, lakini Yesu akajitwika. Kwahiyo
kuteswa kwa mwana wa Mungu kwalinganishwa  sawa na uzito wa
adhabu ya jumla ambayo wangepewa wanadamu wote.

KANUSHO LA IMANI HII
Hapa nataka kukanusha imani  hii ya Wakristo. Kwanza nitatoa
ushahidi wa akili na wa busara kuvunja itikadi hii.
Hoja  ya kwanza ni ule ukweli wa kukosa kuthibitika katika vitendo.
Hii itakuwa wazi zaidi ukifikiria mifano hii miwili ifuatayo: Nabii Musa
alikuwa mtu pekee na kwa vyovyote alionekana  dhaifu na mnyonge,
lakini,  alisimama imara mbele ya Firauni, mfalme wa Misri mwenye
nguvu na majeshi. Nabii Musa alimwambia Firauni, "Mimi ni Mtume
wa Mwenyezi Mungu. Watume wana wa Israeli pamoja nami. Ikiwa
utakataa, basi ujue kwamba utashindwa." Hivyo Musa mbele ya Firauni
alidai ya kuwa ni Mtume wa Mungu na pia akatabiri maangamio ya
Firauni. Bishara hii kubwa ilitimia sawasawa na ukweli kwamba Musa
a.s. alikuwa Nabii wa Mungu ukathibitika kwa vitendo.
     Nabii mtukufu Muhammad s.a.w. alidhihiri katika Bara Arab.
Waarabu wa siku hizo walikuwa wajinga waliopotoka  na washenzi.
Sayyidna Muhammad s.a.w. akawaambia "Nifuateni; mafundisho ya
Qur`an Tukufu yatawaleteeni  utamaduni na ustarabu, maarifa na elimu,
nanyi mtakuwa mshindao." Hivyo ndivyo ilivyokuwa  hasa. Hii7
ilithibitisha ukweli wa unabii wake kwa vitendo.
Mifano hii miwili ni ya kidini, hata hivyo napenda kuongeza  mifano
mingine ya kidunia. Kila Serikali hutunga sheria zenye kutoa adhabu
kwa hatia na pia zipo sheria zenye kutunukia tuzo kwa mwenye kutenda
kazi njema.  Daima twashuhudia sheria hizi zikitimizwa kwa vitendo.
Hebu natuangalie miaka 1900 iliyopita tangu Yesu alipotundikwa
msalabani na tuone kama itikadi hii ya kafara inaongoza kwenye
matukio yoyote yanayothibitika kwa vitendo.

Inasemekana kwamba Adamu na Hawa ndiyo waanzilishi wa
dhambi ya asili hapa ulimwenguni na kuwa haiwezi kuondolewa kwa
watu isipokuwa wanajifanya wenye kustahili wokovu kwa kuzingatia
imani ya kafara ya Yesu. Yafaa kwanza tuone ni adhabu gani waliyopewa
akina Adamu na Hawa kwa dhambi yao waliyofanya kisha tuone kama
wale  waaminio kafara ya Yesu  wamesamehewa. Kutoka katika Biblia
ni dhahiri kuwa adhabu aliyopewa  Adamu kwa dhambi yake ni: "Kwa
jasho la uso wako utakula." (Mwanzo 3:19). Na bibi Hawa naye
akaambiwa ,"Kwa uchungu utazaa watoto."  (Mwanzo 3:16).

Sasa nauliza, Je, yupo Mkristo yeyote awezaye kusema kwa
uaminifu kwamba yeye binafsi yu huru kutokana na adhabu hiyo ya
hao Adamu na Hawa? Nani anayesema ya kuwa kwa kuzingatia imani
ya kafara ya Yesu sasa yeye riziki hupata bila  kuitolea jasho?
Kadhalika yupo bibi yeyote wa Kikristo awezaye kusema kwa dhati
kwamba  kuamini  kwake  kuwa  Ye su   ni  mkomboz i  wake
kumemwondolea uchungu wa kuzaa na kwamba yeye sasa huzaa bila
ya uchungu? Hakuna Mkristo atakayeitikia `ndiyo`  kwa maswali  hayo
hapo juu. Hii yaonesha wazi kuwa hizi kazi zetu tufanyazo kila siku
zinaharamisha imani ya ndugu Wakristo  juu ya kafara ya Yesu. Iwapo
ni kweli kwamba Yesu alikomboa dhambi naye alibeba dhambi za
watu na kwazo akaadhibiwa na watu wanachohitaji ni kumwamini tu,
kwa nini basi wale  wanaoamini Ukristo wanaendelea kupata adhabu
ambapo Yesu alikwisha fika na kuondoa taabu hiyo? Hii inanifanya
niseme ya kuwa kafara ya Yesu haina manufaa yoyote, bali ni kitu cha
kudhania tu na daima twashududia kinyume chake.
Pindi mtu anaamini na kukubali ukombozi wa Yesu, bila shaka mtu8
huyo ana dhambi fulani fulani alizofanya kabla ya hapo na pia pana
dhambi zingine awezazo kufanya baadaye. Ikiwa imani katika kafara
ya Yesu ni kuleta msamaha wa dhambi hizo hapo  italazimu asiadhibiwe
kwa dhambi zake za zamani. Lakini matokeo ambayo daima tunaona
yapo kinyume na hayo. Hebu tuseme mtu huyu aliyebatizwa alikuwa
na hatia ya uzinifu na akawa na viini vya ugonjwa m`baya mwilini
mwake, lakini maradhi yenyewe yawe bado kudhihirika; kwa mujibu
wa imani ya kafara ni lazima Yesu aichukuwe adhabu ya dhambi hiyo.
Hivyo, viini vya maradhi ya uasherati kama tego na kaswende
vitalazimu vihamie mwilini mwa Yesu amkinge kutokana na shambulio
la viini hivyo vya maradhi  na kuwa salama salimini. Lakini hivi sivyo
ilivyo.

Ukweli ni kwamba imani ya Mkristo katika kafara ya Yesu
haimkingi kutokana na shambulio la viini hivyo vya maradhi ya uasherati
na matokeo ni haya tu kwamba Mkristo huyo huwa windo zuri la
maradhi ya tego na kaswende. Hii inaonesha kwamba imani katika
ukombozi wa Yesu haimwondolei mtu dhambi alizozitenda kabla ya
kubatizwa. Na kwa zile dhambi atakazozitenda baada ya kubatizwa,
tunaona kuwa Wakristo wanapotenda maovu huadhibiwa kwayo kama
watu wengineo. I wapi  faida ya kafara? Kafara isiyoondoa dhambi
za kabla ya ubatizo na zile za hatimae ina wokovu gani kwa watu?
   Upotovu wa imani hii hakuna haja kutazama kwa darubini bali upo
peupe. Imani ya kafara ya Yesu imeshindwa kabisa kutakasa nyoyo
za wanadamu. Kila mwaka nchi za Kikristo idadi kubwa za wakosefu
wenye hatia zinazidi. Ikiwa itasemwa ati hao hawafuati sheria , nasi
tutauliza, je, hii kafara ya Yesu matumizi yake kitu gani? Hata kama
isemwe kwamba mradi wa imani ya kafara ni kuondolea mbali uwezo
wa kutenda dhambi, sisi tunasema hii si kweli. Tukiacha kando wale
Wakristo wa kawaida, hata hivyo tutabaki na orodha ndefu ya hatia
chafu za wakuu wa Kikristo.

Inasemekana kwamba haki ya Mwenyezi Mungu haiwezi kutimizwa
ila kwa njia ya kafara. Lakini ukweli ni kwamba imani hii inabatilisha
haki. Yesu hakuwa na kosa lolote na ni udhalimu hasa kumtwisha mtu
asiye na kosa mzigo wa  mwenye dhambi.

Inawezekana kusemwa ya kuwa Yesu alimiliki uhai wake na
kwamba alijitoa kuwa kafara kwa hiyari yake mwenyewe. Hoja hii
itakuwa haina nguvu mbele ya Biblia. Biblia  inatuambia kuwa
hakupenda Yesu kifo cha kutundikwa msalabani, bali alimwomba
Mwenyezi Mungu ili amwepushe na kikombe hicho cha mauti.
Imeandikwa: "Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi,
akaomba, akisema, Baba yangu  ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke;
walakini si  kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe" (Mathayo
26:39). Tena pana kilio cha uchungu alicholia bwana Yesu kwa sauti
kubwa, "Eloi, Eloi, lamasabaktani? Yaani Mungu wangu, Mungu wangu,
mbona unaniacha?"  (Mathayo27:46).

Dua hizi zaonesha dhahiri kuwa Yesu hakutoa uhai wake kwa hiyari
kama watu wengine wanavyosema. Hata kama tukikubali kuwa alijitoa
kwa hiyari, twakuta swali jingine moja ambalo ni hili: Ikiwa Yesu alimiliki
uhai wake, je, Mwenyezi Mungu si mmiliki wa matendo yake
mwenyewe? Si yeye mmiliki wa hazina za neema na mibaraka? Ikiwa
Yesu aliweza kutoa uhai wake bila malipo, je, Mwenyezi Mungu hawezi
kutoa ukarimu wake bure? Kuadhibiwa kwa Yesu kwa sababu ati ya
dhambi za watu ni kitendo kinachokwenda kinyume na kanuni yake
Mwenyezi Mungu, mwenye Haki.

Imani ya kafara inamfanya Yesu kuwa yu mdhalimu pia. Dhambi
za mwanadamu zinakuwa za namna mbili. Mtu asipofanya wajibu
wake kwa Mwenyezi Mungu au mwanadamu mwenzie. Mtu
asipofanya wajibu wake kwa Mwenyezi Mungu , imani ya kafara ya
Yesu itamwepusha adhabu. Mwanadamu alimwasi  Mwenyezi Mungu,
Mwana wa Mungu alijitwika  adhabu ya  uwasi huo na mwanadamu
akawa huru. Lakini hebu natuangalie upande wa pili ambapo
mwanadamu anamkosea mwenzake. Tuseme pana mtu aitwaye John
ambaye ni mumini wa Yesu. Yesu anajitwisha dhambi zote za John
pamoja na ile ya wizi wa saa. Henry ambaye ndiye mwenye saa anabaki
akilia bila kupata saa yake. Je, sasa hamuoni kwamba upande wa
Henry , Yesu amekuwa yu mdhalimu kwa kujitwika adhabu ya John?
Hivyo kwa imani ya kafara, Yesu anapakazwa hatia ya udhalimu.10
Inasemekana kwamba kama Mwenyezi Mungu angaliwasamehe
watendao dhambi kwa huruma yake, bila ya kuwaadhibu  kwa  namna
yoyote, basi wangalizama katika madhambi wakiamini kuwa Mungu
atawasamehe tu. Lakini sisi tunaona ni itikadi hii ya kafara ya Yesu
ndiyo imfanyayo mtu kuzidi kudidimia katika dhambi na uwasi. Njia
ya kwanza inamweka mwanadamu katika hali ya wasiwasi kama
Mungu atamsamehe au la, Katika hali hii mwanadamu ataogopa
kumwasi Muumba wake. Lakini kwa mujibu wa njia ya pili, kafara ya
Yesu, inamfanya kuwa na hakika kwamba yuko huru kutenda  dhambi;
maana Yesu keshachukuwa kila kitu, bali  kitu kitakiwacho kwake ni
kuamini.  Kafara inampa mwanadamu nafasi ya kumwasi Mwenyezi
Mungu. Ndiyo sababu watu wa Ulaya na Amerika wamezidi maasi
na kuzama katika anasa za kidunia.

Mtu anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake kusudi la adabu hiyo
huwa kumwongoa huyo mwenye dhambi. Lakini kusudi hili haliwezi
kutimizwa iwapo mtu asiye na kosa lolote ataadhibiwa mahali pa yule
mwenye makosa. Tufanyapo wema hutumfadhili Mwenyezi Mungu
chochote. Na tufanyapo uwovu haimfikii dhiki yoyote. Ni sisi wenyewe
tunaofaidi wema wetu au kupata hasara kwa sababu ya uwovu wetu.
Laiti kama kutenda dhambi kwa wanadamu ni kumdhuru Mwenyezi
Mungu, hapo tungelazimika kumridhisha kwa kumlipa na inatosha hata
mtu mwingine ajitolee kulipa badala yake. Lakini hivi sivyo ilivyo.
Imani ya ndugu Wakristo  juu ya kafara inatukumbusha hadithi
moja ya Mfalme Chaupat. Siku moja mhalifu aliletwa kwa mfalme
Chaupat ili ahukumiwe. Mfalme aliamuru mhalifu huyo anyongwe.
Mfalme alipojulishwa ya kuwa upana wa kitanzi cha kamba ya
kunyongea ulizidi shingo ya mhalifu, mfalme akasema,  "basi mtu mnene
anyongwe badala yake". Kwa ufupi upotovu wa itikadi ya kafara ya
Yesu unakuwa wazi kwa vile kunamfanya Mwenyezi Mungu aonekane
mwenye kiu sana ya kuadhibu watu hata kama hawana kosa.
Wakristo wanasema mshahara wa dhambi ni mauti. Husema hivyo
wakifuatia mamlaka ya vitabu vyao. Kwa mujibu huu ingefaa basi
watu wote ambao mishahara ya dhambi zao  imelipwa na mtu mwingine,
wao wasife katu. Maana inajulikana kwamba kifo cha Yesu kilifidia11
dhambi za wale wanaomwamini, hivyo wafuasi wake hawangekufa
kwamwe.  Lakini mambo yamekuwa kinyume. Sisi tunawaona
Wakristo wakikabiliwa na mauti kama watu wengine wasiokubali
kafara ya Yesu. Hii inaonesha kwamba kafara ya Yesu haikuwafaa
chochote Wakristo hao.

Kusema kweli Wakristo hawakuelewa sifa hizi mbili: Haki na
huruma. Wamechukuwa huruma kuwa kinyume cha haki, ambapo
kinyume cha haki si huruma bali ni dhuluma. Maana ya haki ni kwamba
mtu atendewe uadilifu. Kwa kuwa imani ya Kikristo imejengwa juu
ya wazo kwamba huruma ni kinyume cha haki, basi inakuwa wazi
kuwa wao wamesimama juu ya msingi ulio mbovu sana na usiofaa
hata chembe.
Inasememwa  na Wakristo kuwa hapana njia nyingine yoyote ya
kuleta msamaha wa dhambi ila kafara ya Yesu. Lakini tunaona
Mwenyezi Mungu amejaalia uwezo wa kuondoa dhambi katika
maumbile. Mtu alapo chakula kibaya huwa anavunja kawaida na bila
shaka ataugua maradhi.  Lakini akigeuka na kutumia dawa ifaayo,
yumkini atapata ahuweni na maumivu yote yataondoka. Hii ni njia ya
ya kimaumbile kundoa maradhi yatokanayo na kuhalifu sheria na kanuni
za maumbile. Lakini je, ni  nani aliyemwona daktari amejiua mwenyewe
kwa sababu ya kuponyesha wagonjwa wake? Bila  shaka daktari
hodari hutafuta dawa na kuanza kuwatibu wagonjwa wake. Ni daktari
mzembe sana anayejitumbua kisu ili wagonjwa wake wapate afya.
Kafara ya bwana Yesu kwa kuokoa watu, tunaona inakwenda
kinyume na kanuni zote za Mwenyezi Mungu. Hapa duniani daima
tunaona, kwa mfano, vita. Vita askari wa kawaida hapigana safu ya
mbele kabisa, nao maofisa huwa nyuma ya hao hali amiri jeshi huchukua
mahali pa usalama zaidi,,ambapo mfalme huwa yupo salama salimini
ngomeni mwake. Askari hutoa maisha yao kwa ajili ya kapteni, naye
kapteni kwa ajili ya Kanali na huyu naye kwa ajili  ya Jemedari na
Jemedari kwa  ajili ya Amiri jeshi. Amiri  jeshi au mfalme hawezi
kutolewa kafara ili kuokoa maisha ya askari. Ni fundisho la ajabu tu la
hawa Wakristo kutuambia Yesu ambaye wanamwamini kuwa mwana
wa Mungu alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu wasiyo na thamani12
yoyote wakilinganishwa na Mwana wa Mungu.
Wanyama kama vile ng`ombe na mbuzi huchinjwa kwa ajili ya
manufaa ya mwanadamu. Mapanya waenezao tauni huuawa ili maisha
ya mwanadamu yasiwe katika hatari. Hatujaona   mwanadamu anakufa
ili kuhifadhi maisha ya wadudu . Basi mwana wa Mwenyezi Mungu
awezaje kujifanya kafara kwa ajili ya wanadamu? Ndipo tunaposema
imani ya kafara ya   Yesu ni kinyume na akili, kinyume na uchunguzi na
kinyume na kanuni za maumbile.

Ni uwongo kusema ya kuwa wanadamu wote huzaliwa wakiwa
na dhambi. Ulimwengu mzima hufikiria watoto hususan  wachanga
kuwa ni malaika, yaani hawana dhambi yoyote. Yesu pia aliwaita
watoto waende kwake. Akasema , "Waacheni  watoto wadogo waje
kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu
ni wao" (Luka 18:16). Kwa nini hakusema ufalme wa mbinguni  ni wa
yule anayeamini kafara yake?

DHAMBI  ZAONDOLEWA NAMNA GANI?
Kabla ya Yesu kufika njia ya kusamehewa madhambi  ilikuwa
maombi na kutorejea tena katika matendo mabaya. Katika wakati
wa Musa a.s. tunasimuliwa na Biblia kwamba wana wa Israeli
walipoona Musa a.s. anakawia kutoka huko mlimani, basi
wakajitengenezea ndama wa dhahabu wakamuabudu. Mwenyezi
Mungu akawakasirikia wana wa Israeli. Nabii Musa a.s. akasikitishwa
sana na jambo hilo. Upande mmoja akaamuru watu wake kuua kwa
mikono yao watu wale walioleta kufuru na upande mwingine akapenda
yeye mwenyewe awe kafara kwa ajili ya wafuasi wake, yaani auawe.
Lakini Mwenyezi Mungu akamjibu akasema, "Mtu yeyote aliyenitenda
dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu" (Kutoka 22:33).
Hii inatujulisha mpango wa Wakristo juu ya kafara ni jambo ambalo
wao wenyewe wamelipanga wala halipo katika kanuni ya Mwenyezi
Mungu. Mungu hawaadhibu wasio na makosa mahali  pa wale wenye13
dhambi. Ingawa Musa a.s. aliridhia kujitoa kafara kwa ajili ya watu
wake, lakini Mwenyezi Mungu alikataa ombi hilo. Kama kafara ya
mtu ndiyo inayotakiwa baada ya watu kutenda dhambi, basi Mwenyezi
Mungu hangeona ombi la Musa a.s. kuwa halina maana. Bali Mungu
angeweza kumwambia Musa a.s. kwamba kazi hiyo amejitwika Yesu.
Mwenyezi Mungu hakupata kumwambia Musa a.s.  au nabii yeyote
kwamba mwanawe ataadhibiwa kwa sababu ya dhambi za watu. Ni
ajabu tu leo tunaambiwa na Wakristo ati Yesu ni kafara ya dhambi za
watu!
Wakristo hawawezi kukana ya kuwa manabii wote wameokoka.
Je, manabii hao waliokolewa na kafara ya Yesu iwapo walifika hata
kabla ya Yesu mwenyewe?  Hakuna dawa ya kusamehewa ila kuomba
toba tu. Mwenyezi Mungu alimwambia nabii Suleiman hivi: "Ikiwa
watu wangu, walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba
na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka
mbinguni na kuwasamehe dhambi zao." (2 Mambo ya Nyakati 7:14).
Mwenyezi Mungu hakusema watu hawawezi kusamehewa dhambi
zao ila kwa kafara ya Yesu. Kwa nini watu wabaki kunga`ang`ania
imani hii? Kwa nini ndugu Wakristo hawawezi kufikiri kidogo na
kuangalia mambo yalivyo?
Yesu mwenyewe anazumgumza juu ya wokovu, anasema, "Ingieni
kwa kupita mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na
njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango
huo. Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani,
nao waionao ni wachache" (Mathayo 7:13:14). Katika maneno haya
Yesu anaonesha njia ya wokovu kuwa ni yenye taabu na yenye kuhitaji
uvumilivu na kujinyima. Lakini tuonavyo njia ya kafara si ngumu wala
si nyembamba. Kwa upande mwingine njia ya kafara ni mlango ulio
mpana sana. Fanya upendavyo na imani ya kafara itakuondolea dhambi
zako zote. Hushurutishwi kufuata sheria yoyote, bali kukiri kafara ya
Yesu tu!

DALILI ZA KAFARA ZINACHUNGUZWA
Haitakuwa vibaya kutaja hapa vifungu vya maneno ya Agano la
Kale na Jipya ambavyo Wakristo huvichukua kuwa vyenye kusaidia
fundisho lao la imani ya kafara! Yesu alisema ya kuwa ni mchungaji
mwema aliyeyatoa maisha yake kwa ajili ya kundi lake. Tena,
inasemakana, alipokaribia kusulubiwa aliketi karibu karibu na hao
thenashara ambao alikula nao  na akachukua mkate akaubariki.
Akawapa wanafunzi naye akasema, watwae wale na ya kwamba huo
ndio mwili wake Yesu. Kadhalika inasemwa Yesu alitwaa kikombe
na kuwaambia wanafunzi wake wanywe, kwa maana hiyo ndiyo damu
yake ya Agano Jipya imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa kuondoa
dhambi zao!

Hii ndiyo misemo ya pekee ambayo Wakristo huchukua kusaidia
imani yao ya kafara. Hata kama misemo hiyo imeaminiwa ya kuwa ni
ya asili katika Biblia, haihakikishi kuwa Yesu aliadhibiwa kwa ajili ya
wanadamu wote. Bali meneno hayo ni ya kawaida kwa kiongozi yeyote
wa kiroho. Kila nabii na  kila mtume huumizwa kwa ajili ya watu
wake. Si hayo tu, bali huvumilia kuumizwa hata na watu wake pia.
Lakini kwa nguvu za Sala na maombi, mizigo ya dhambi ya watu
huondolewa. Kama watu hawangezama dhambini, Mwenyezi Mungu
hangeleta mwonyaji.

Ni kweli Yesu alivumilia maumivu kama walivyovumilia manabii
wengine. Na kwa juhudi ya sala na maombi watu wa nabii Isa a.s.
(Yesu) walipata matunda mema kama vile sala na dua za Musa a.s.
zilivyoondoa  na kuwaokoa watu wake kutokana na maangamio.
Kadhalika iwapo Yesu alifika kuwaokoa watu wote wa ulimwengu
kwa nini katumia kwa "ajili ya wengi"  "Kwa ajili ya wengi" inaonesha
Yesu alikuwa anaongea juu ya watu wa taifa lake pekee ambao kwa
ajili yao Yesu alitumwa kuwaongoza na alipata taabu kuwaonesha
njia ya kufika kwa Mwenyezi Mungu.
Imeoneshwa kuwa pana vifungu kadhaa katika Agano la Kale
vyenye kupotoa imani hiyo ya kafara. Hata hivyo Wakristo hudhania
kuwepo maneno fulani katika Agano la Kale yenye kusaidia imani
yao.

Lakini ukweli ni kuwa maneno yenyewe hayo hayamhusu Yesu
wala kafara yake. Kifungu kimoja kinachodhaniwa kuunga mkono
imani yao ya kafara kinasema:-"Angalia siku zinakuja, asema BWANA,
nitakapofanya Agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
Si kwa mfano wa Agano lile nililofanya na baba zao ......  Baada ya
siku zile, asema BWANA, nitatia sheria yangu katika sehemu zao za
ndani na katika nyoyo zao nitaandika,  nami nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu ....Nitasamehe uwovu wao, wala dhambi
yao sitaikumbuka tena" (Yewremia 31:31-34).
Wakristo huwekea umuhimu mkubwa juu ya aya ya mwisho katika
kifungu hicho cha maneno wakidhania kuwa ndiyo yenye kuhakikisha
imani yao ya kafara. Lakini wanasahau kwamba katika Agano la Kale
mmeandikwa ya kuwa kulikuwapo msamaha wa dhambi. Msamaha
huo ulifika baada ya watu kutubu na kuombewa na  nabii wao. Hakuna
kitu kigeni katika aya hiyo kinachoweza kutufanya tufikirie kwamba
pamedokezea au kugusia kafara ya Yesu.Kama ingesemwa kwamba
hapo mwanzo Mwenyezi Mungu hakusamehe dhambi kabisa, yumkini
pangekuwapo sababu ya kufikiria kule kutajwa kusiko kwa kawaida
kwa njia  ya kuleta msamaha wa dhambi. Lakini tunaona kuwa
msamaha wa dhambi ulikuwapo miogoni mwa Israeli kabla na baada
ya aya hiyo. Basi kwa nini tufikirie kuwa mujibu wa msamaha  wa
dhambi uliotajwa katika aya hiyo ni kafara ya Yesu?

Ingawa ni hivyo, yapo maneno yenye kuashiria tukio la baadaye
.Moja ya aya hizo yasema: "Nitafanya Agano jipya na nyumba ya
Israeli, na nyumba ya  Yuda. Si kwa mfano wa Agano lile nililofanya
na baba zao." Akieleza juu ya aya  hii Mwenyezi Mungu anasema,
"Nitatia sheria yangu katika sehemu zao za ndani." Kwa mujibu wa
imani ya Kikristo ni dhahiri Yesu hakuleta sheria yoyote, lakini hakika
ni kuwa aya hizo zatabiri kuletwa kwa sheria mpya. Sheria hiyo moja
ni Qur`an Tukufu aliyofunuliwa Nabii Muahmmad s.a.w. ambayo
inawakumbusha wana wa Israeli bishara ambayo hivi punde tu
imesomwa hapo juu. Qur`an Tukufu inasema: "Enyi wana wa Israeli,
ikumbukeni neema yangu niliyowanemesheni nayo na itekelezeni ahadi
yangu nitatekeleza ahadi yenu na niogopeni  mimi tu" (Qur`an Tukufu
2:41). Aya hii ina mradi kwamba wana wa Israeli waikubali sheria16
hiyo mpya waliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu atawatekelezea ahadi
zake zote alizofanya katika Agano la Kale.

Wale waliokubali wito huu si kwamba walipewa neema za mbinguni
tu, bali hapa duniani pia walipewa heshima na wakawa watawala na
wafalme wenye nguvu. Waafghani na ndugu zao. Wakashimiri siku
hizi waaminiwa kuwa wazao wa Israeli ambao ni jumla ya yale makabila
kumi na mawili yaliyopotea. Hivyo kati ya hao wana wa Israeli
waliopotea waliikubali sheria mpya (Qur`an Tukufu) na matokeao yake
yakawa kwamba Mwenyezi Mungu hakuzikumbuka dhambi za baba
zao. Lakini wale waliokana kupokea sheria hiyo mpya, mpaka sasa
wako chini ya ghadhabu  za Mwenyezi Mungu.

USHAHIDI WA TAREHE WAIPINGA KAFARA
Nimekwisha kuonesha kwamba Biblia haina ushahidi wowote  juu
ya imani ya Wakristo ya Kafara ya Yesu. Sasa  yafaa tuchungue ukweli
wa itikadi hii katika msingi wa histora. Wokovu wa ulimwengu mzima
yasemekana wategemea juu ya imani kuwa Yesu alikufa msalabani na
baada ya hapo kutoka kwake katika wafu na kupaa ni matukio ya
shani katika historia ya ulimwengu ya kuwa wokovu wa watu
unategemea matukio hayo makuu. Lakini sisi twasema kuwa ikiwa
kifo cha Yesu msalabani kilikusudiwa na Mwenyezi Mungu  kwa
kuwakomboa watu wote wa ulimwengu, basi kifo hicho ingefaa
Mwenyezi Mungu akifanye wazi machoni pa walimwengu. Maandiko
ya historia yangepaswa kutoa ushahidi juu ya  ukweli kwamba Mwana
wa Mungu alizuru ulimwengu huu karne fulani na ya kuwa alikufa
msalabani kwa ajili ya wenye dhambi. Lakini sasa ushahidi tulio nao ni
ule wa Injili tu ambao humo pia jambo hili halimo katika sura ya ukweli
wala hauitaji kafara ya Yesu. Kadhalika hauwei kupinga hoja kuwa
maneno haya  "Alitoka kwa wafu" yanaweza kuwa na maana kwamba
alipata fahamu baada ya kuzimia.

Injili kama usome kwa makini wazi  itakuonesha dalili nyingi kuwa
Yesu aliepuka kifo cha laana cha msalaba. Lingekuwa jambo refu
sana kutoa hapa ushahidi wote wa Injili unaothibitisha kuwa Yesu
hakufa msalabani. Swali lifuatalo linatosha kuonesha upuuzi wa dhana
ya Wakristo  kuwa Yesu alifufuka toka wafu na akaruka kwenda
mbinguni. Ikiwa ni hivyo kwa nini Yesu alipofufuka toka wafu
alijifichaficha akachelea asije akakamatwa? Kwa nini alificha lile tendo
lake la mwisho, lile la kupaa mbinguni lisifanyike mbele na machoni pa
Mayahudi? Ingawa nyota haina uhusiano wowote na ukombozi wa
wanadamu, lakini iangukapo hushuhudiwa na watu wengi hata kama
hawakuwa wenye kungojea. Bali jambo la ajabu ni ukweli kwamba
hapana hata mtu mmoja katika wasiomwamini Yesu aliyeshuhudia
kupaa kwa yule aliyefufuka toka wafu. Hapana mtu mmoja anayedai
kwamba aliona mwanadamu akivurumika kuelekea mbinguni, iwe
pekee au kusindikizwa na kundi la malaika. Hata maroketi
yanaporushwa angani watu hupashwa habari  mapema  nao wanayaona.
Mbona Yesu hakutangaza?

Ukweli ni huu tu ya kuwa Yesu hakusafiri kwenda mbinguni. Kama
hadithi hii ya kusema Yesu amepaa mbinguni ni kweli, basi mradi wake
ni huu kwamba baada ya kuwaaga wanafunzi wake chini ya mlima,
Yesu alipanda mlima huo akinuia kufanya safari ndefu. Kule juu milimani
mawingu yalitanda, yakielekea mbinguni. Hapo wenye kukisia
wakasema Yesu amepaa mbinguni! Kwa wanafunzi wa Yesu kusema
hivyo ilikuwa sawasawa maana walikuwa na nia ya kuwazuia Mayahudi
wasimfuate Yesu wakamshika tena mara ya pili.

Wakristo wa madhehebu mengine wanaamini kuwa Yesu aliishi
duniani miaka 11 baada ya kusulubiwa. Wengine wanasema la, bali
aliishi miezi kadhaa. Waliobaki wananena, sivyo bali aliishi siku 40 tu.
Swali ni hili: Yesu alikuwa na haja gani kujifichaficha baada ya
kusulubiwa? Alikuwa ameshasulubiwa tayari, alikwisha onja kifo kile
alichofikia, akaingia Jahanamu na kazi ya ukombozi ikakamilika; kwa
nini tena aliendelea kuwa na udhaifu wa kibinadamu? Kwa nini
hakuwaendea Mayahudi na kuwaonesha makarama yake na uwezo
aliokuwa nao wa Kiungu ili nao wakamwamini?18
Ili kukanusha imani potevu ya Kikristo, Qur`an Tukufu inashambulia
kiini hasa cha dini hiyo. Imethibitika bila taabu kuwa Yesu hakufa kifo
cha laana cha msalabani na ya kuwa hakuwa mwana wa Mungu. Na
hii inatosha kuvunjilia mbali imani ya Kikristo juu ya ukombozi wa
kafara ya Yesu. Isitoshe, Qur`an Tukufu inakanusha imani ya aina hii
na kusema,"WALA NAFSI YOYOTE HAICHUMI (UBAYA) ILA
NI JUU YAKE, WALA M`BEBAJI HATABEBA MZIGO WA
MWINGINE.' (6:165)
Haikuwa lazima hapa kutaja imani ya kafara ya Kikristo, kwani
ikithibitishwa kwamba Yesu alikuwa mwanadamu na kuwa hakufa
kifo cha laana kile cha msalabani, bali alikufa kifo cha kawaida; yale
mawazo yote ya kipumbavu hususan ya kafara yake, hayo yatafutika
kabisa katika akili za watu.

KWA  NINI  TWAKATAA
Kama kuna manufaa yoyote katika itikadi ya kafara, bila shaka
tungalikubali. Lakini mbali na kutunufaisha imani hii, tunatokomezwa
kwenye matokeo maovu mno. Hapa upo mfano wa uwovu huo.
KWANZA: Imani ya kafara ni kinyume na akili zetu. Akili ya
mwanadamu inakataa wazo hili kwamba John ajipasuwe tumbo lake
ili amponyeshe Henry maradhi ya kichwa.
   PILI: Kukubali imani ya kafara ya Yesu ni sawa na kukataa Agano
la Kale, kwani inaonesha njia nyingine ya kuleta msamaha wa dhambi.
TATU: Ikiwa tutakubali kafara ya Yesu, basi  ni lazima tukubali kuwa
Yesu alilaaniwa, hali laana inamsukuma yule aliyelaaniwa mbali na
Mwenyezi Mungu  na kumsogeza karibu na shetani. Laana ni jina tu
lisilo na mujibu wake. Waila laonesha  hali ya roho na ambayo ni
dhambi kubwa  kuitaja kwa vyovyote kuwa nayo Nabii wa Mungu.
Wakristo wanaposema kuwa Yesu alilaaniwa, wao hawatishwi na
maana ya laana.19
NNE: Itikadi ya kafara inamfanya Mwenyezi Mungu kutokuwa
mwenye Haki, anaweza kumwadhibu mtu ambaye hakufanya kosa
lolote.
TANO: Kukubali imani ya kafara ni kukataa kuwa Mwenyezi
Mungu ni mwenye huruma, kwani hakutosheka na kutubu kwa
watu wake, bali aliona bora kumtoa Yesu aje amwadhibu kwa
ajili ya dhambi za wanadamu.
SITA: Ikiwa kafara ni njia ya kweli, basi Manabii wote waliopita
kabla ya Yesu wote watakuwa hawana ukweli, maana wao
walifundisha njia nyingine ya kupata wokovu.
SABA:  Ikiwa kafara ni kweli, basi watakatifu walioleta dini zote
hapo mwanzo watakuwa na makosa sababu hakuna hata mmoja
wao aliyefundisha itikadi hii.
NANE: Ikiwa Kafara ni kweli, baraza zote za sheria katika nchi
za Kikristo zina hatia ya dhambi ya uwovu mkubwa, kwani
hazitofautishi Wakristo na wasiyo Wakristo. Haifai kuwadhibu wote
sawa bila kujali kwamba dhambi za wale Wakristo zilifidiwa na kifo
cha Yesu na kwazo akaadhibiwa.
TISA: Kafara imewafanya Wakristo wa hali zote kuwa sawa. Kwa
mfano mmoja akiwa na 99 kwa mia ya matendo yake maovu, na
mwingine 50 kwa mia na mwingine moja tu kwa mia; lakini Kafara
inaondoa dhambi zao zote na wote wanawekwa katika daraja moja
ya usafi. Hivyo wale waliofanya wema zaidi wanakuwa sawa na wale
ambao hawakufanya wema wowote. Hii si haki abadan. Mtu awezaje
kuamini itikadi yenye udhalimu kama huu?
KUMI: Ikiwa Kafara yatosha, basi hapana haja ya kusali, maana
wokovu unapatikana tele kwa kuamini kafara tu. Yote tunayohitaji
kufanya ni kuamni ukombozi, na sala haina lazima. Hili ni ovu kuu
linalotufanya tuikatae imani ya kafara. Kwani Sala ndiyo uhai wa
waaminio. Mcha Mungu anawezaje kuishi bila ya kusali? Yesu
mwenyewe aliwafundisha wanafunzi wake kusali na hivyo ndivyo
ilivyokuwa kwa manabii wote wa Mwenyezi Mungu.
KUMI NA MOJA: Itikadi ya Kafara inamfanya mtu kuamini kuwa
hata Mungu alikufa. Wakristo wanamwamini Yesu kuwa Mungu.20
KUMI NA MBILI: Imani ya Kafara ina maana kwamba Mwenyezi
Mungu ni mwenye kiu ya damu na hatosheki na chochote ila damu ya
mwanadamu. Mungu ni lazima apate damu wala si kingine, haidhuru
damu hiyo iwe ni ya mwenye dhambi au asiye na dhambi.
KUMI NA TATU: Imani hii haina ushahidi wa historia.

CHIMBUKO  LA   KAFARA
    Itikadi ya Kikristo ya kafara inapingana na fikira za kawaida na
wala haisaidiwi na Injili au kauli yoyote ya Yesu. Daima watu wanauliza
chanzo cha imani hii ni nini? Ukweli ni kwamba Yesu na wanafunzi
wake wote ni wageni katika imani hii iliyovumbuliwa na Paulo. Ilikuwa
ni mwisho wa karne ya jana ambapo Injili mpya ilienezwa huko
Amerika. Injili hiyo inajulikana kwa jina la THE STORY OF
CURCIFIXION BY AN EYE WITNESS, yaani, maelezo ya
kusulubiwa na shahidi aliyeona kwa macho. Mwandishi wa Kitabu
hicho amesema wazi kuwa Yesu hakufa msalabani na kwamba alihamia
nchi nyingine baada ya kusulubiwa kwake.
  Shabaha ya Mayahudi, kama nilivyosema hapo mbele, ilikuwa
kwamba wamsulubu Yesu ili aonekane kuwa mtu aliyelaaniwa kama
ilivyoandikwa katika  Biblia, "Kwani aliyetundikwa amelaaniwa na
Mungu." (Kumbukumbu la Torati 21:23). Hivyo wanafunzi wa Yesu
walitatizwa. Kukubali kuwa Yesu alikufa msalabani wanaona
atafanywa amelaaniwa. Kusema kuwa Yesu aliponyoka na yupo
safarini kuelekea nchi nyingine ya mbali, hilo lilikuwa jambo la hatari
kubwa, maana serikali ingeweza kumshika tena Yesu na kumtia
msalabani na kumwua. Kwa ujanja Paulo akawabunia hila nao
hawakukataa kwa sababu waliliona hilo ni njia ya pekee ya kuondoa
tatizo lao gumu sana. Katika  maarifa yake, Paulo alikisia kuwa ni
kweli Yesu alikufa msalabani na kulaaniwa. Lakini hakuwa na kosa
bali alijitwika laana hiyo kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Hivyo kifo
cha msalaba hakikuwa cha fedheha, bali ni jambo lenye sifa njema na21
fadhila! Hapo basi ndipo  ndugu Wakristo wakawa na kitu cha kujisifia
wakapata jibu la kuwaeleza Mayahudi.

Uvumbuzi huu wa Paulo ingawa u hivyo, kwa  kweli hapo mwanzo
ulikuwa kama ngao ya Wakristo ya kukingia matusi ya Mayahudi,
lakini pole pole iligeuka kinga hiyo kuwa imani ya ukombozi ambayo
hivi leo inahubiriwa kote ulimwenguni. Kwa ufupi, Yesu haikuwa
afundishe imani ya kafara hii  inayosemwa juu yake wala hao wanafunzi
wake pia hawakueleza habari hizi. Bali mwalimu wa imani hii alikuwa
Paulo hata imekuwa kwamba Wakristo wenye kufikiri hujiuliza je,
Ukristo huu wa leo ni wa Yesu au ni wa Paulo?

Siku chache zilizopita  mtaalamu mmoja wa Kijerumani aitwaye
Dr. Arnold Meyer   aliandika kitabu juu ya Ukristo na imani zao kadha
zilizotiwa humo. Kitabu hicho kimefasiriwa kwa Kiingereza na kinaitwa
"Jesus or Paul?"  Yaani, Yesu au Paulo? Ndani ya kitabu hicho,
mtaalamu huyo wa Kijerumani amethibitisha kwamba "uungu wa Yesu
na Kafara yake ni  imani ambayo mwanzo wake ulitokana na ujanja
wa Paulo na ambayo Yesu na wanafunzi wake hawakujua aslan."
   Mayahudi kwa sababu ya uwadui wao na chuki walimchukulia Yesu
kuwa mtu aliyelaaniwa ambaye mwisho wake ungekuwa moto mkali
wa Jahanamu. Wakristo nao wakisukumwa na tamaa yao  ya kupata
wokovu kwa urahisi wanakubali kuwa Yesu alilaaniwa na akaingia
Jahanamu. Hivyo maadui na marafiki wa  Yesu wote wanaungana
pamoja na kumtumbukiza motoni. Mwenyezi Mungu ampe
Muhammad, Mtume Mtukufu wa Islam neema  na baraka zake nyingi,
ambaye ndiye aliyemwokoa Yesu katika shimo la moto na kuthibitisha
Yesu hakuwa mtu aliyelaaniwa, bali ni nabii wa Mwenyezi Mungu.
Nabii Muhammad s.a.w. si kwamba alimwokoa Yesu tu, lakini hata
Bi Mariamu pia alimwondolea mashitaka maovu aliyowekewa na
Mayahudi hata imekuwa siku hizi Wakristo wanaposhindwa kupata
thibitsho la usafi wa tabia ya Yesu hukimbilia Qur`an Tukufu ambayo
ina ushahidi murua. Qur`an Tukufu ndiyo iliyomfanya Yesu awe
mtakatifu na mtawa pamoja na mama yake. Kwa ufupi, Paulo ndiye
aliyepanda Ukristo huu wa leo kwani ndiye aliyejua kusoma  na
kuadika. Ama wanafunzi wengine wa Yesu hawakuelewa chochote.22
Akiongea juu ya ukombozi, mwanachuoni mmoja Mkristo
aliyeandika kitabu cha "History of  the Christian Religion and the
Church" akiri kwamba "itikadi ya kafara halikuwa jambo lililokuwa na
umbo dhahiri mpaka kwenye karne ya kumi na mbili. Karne hiyo ni
muhimu mno katika historia ya kuvumbuliwa kwa imani hii." (Jalada la
1 B,ukurasa 497 mtungaji Bwana Meander).

Hapa  pana swali la kawaida je, kuna dawa gani kwa dhambi?
Kwani maisha maovu ni heri mauti. Ni bahati njema kwa mwanadamu,
maana tatizo hili lilikwisha kufumbuliwa zamani  na mwanzilishaji wa
Islam, Mtukufu Mtume Muhammad s.a.w. kwa  njia yenye kukubalika.
Kufuatia kanuni za maumbile nasi tumekwisha kushuhudia
kurekebishwa kwa njia hii katika hali yake ya usafi na Seyyidna Ahmad
wa Qadian aliye mfuasi mwaminifu wa Mtume Muhammad s.a.w. si
katika madai yake yenye kukubalika tu, bali kwa ukweli uliohakiki juu
yake na ishara zake zenye nguvu.
Hadhrat Ahmad a.s. amesema "Tangu kuumbwa ulimwengu
pamekuwapo na kinga moja tu kwa dhambi. Mwanadamnu
alipotafakari juu ya hoja zinazokubalika na ishara zilizo wazi na kupata
hakika ya kuwapo kwa Mwenyezi Mungu  na kuthibitisha kwa yakini
kuwa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ni moto uunguzao, hapo ndipo
unapopata mwangaza wa utukufu toka mbinguni unaomfunulia kwamba
Mwenyezi Mungu ndiye hasa asili ya raha na malipo mema.  Au kwa
vingine, Mwenyezi Mungu hujidhihirisha kwenye moyo wa mwanadamu.
Hivyo, awezaye kuepuka dhambi ni yule tu aliye na yakini juu ya
kuwapo kwa Mwenyezi Mungu na ambaye daima huzingatia kwa
mapenzi na kumwogopa Yeye pekee.

"Uovu na  elimu ya yakini haviwezi kukaa ndani ya moyo mmoja.
Elimu ya yakini ndiyo ponyo la pekee kwa maradhi yako ya dhambi.
Kusulubiwa kwa yeyote hakuwezi kukuondolea mzigo wako wa
dhambi. Damu ya yeyote haiwezi kukuzuia usitawaliwe na tamaa
mbaya za kimwili. Vitu kama hivi havina uhusiano wowote na wokovu
wa kweli. Omba, jaribu kuelewa hakika na jifunze kutafakari juu ya
ukweli. Yajaribu haya  kama vile unavyojaribu mambo mengine ya
kidunia na kisha utakuja  fahamu kwamba elimu ya yakini ndiyo23
mwangaza wa pekee unaoweza kupenya ndani ya moyo  wenye giza.
Elimu ya yakini ndiyo dawa yenye  nguvu za kusafisha maumivu na
maradhi ya kutojua." (Review of Religions 1902).

Mwanadanmu anapojitahidi katika imani yake na kutenda matendo
mema na anakuwa tayari kumtii Mwenyezi Mungu na mitume wake,
basi  rehema za Mwenyezi Mungu huwa pamoja naye na kumwongoza
katika njia iliyo sawasawa. Katika kitabu kitukufu cha Qur`an Mungu
anasema,  "Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na mtume, basi hao
ni miongoni mwa wale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu - Manabii,
Masadiqi, Mashahidi na Masalih na hao ndiyo marafiki wema" (Sura
4:70). Tena baada ya kufanya kosa  kwa sababu ya udhaifu  wa
kibinadamu mtu anapasa ajiepushe   na dhambi  zile kubwa, sehemu
zile ndogo ziandamanazo  na dhambi   hizo zinasamehewa. Kama
mfano,  mtu amtazame mwanamke kwa kumtamani, halafu akurubie,
kishapo anuie kumjua. Katika hali hizi zote mtu huyo anahesabiwa
kama  atenda dhambi. Lakini iwapo baada ya kupitia katika hali hizo
zote za mwanzoni akatubu na kuacha kuendelea mpaka kileleni, bali
akafuata msamaha wa Mwenyezi Mungu; sehemu hizo zote za
mwanzoni husamehewa. Huu ndiyo mlingano ulio sawa kati  ya haki
na maumbile ya mwanadamu. Hayo yameelezwa katika sura 4:32,.
Qura`n Tukufu pia inasema "hakika mema huyaondoa mabaya"
(11:115). Ndiyo kusema usafi huondolea mbali uchafu.

Dunia hii yetu ni mfano wa ulimwengu wa kiroho na inavyo vielelezo
vingi vyenye kutuongoza kwenye dunia ya Kiakhera. Hivyo kutokuwa
na dhambi pekee hakumfanyi mtu kuwa mkombozi wa wanadamu.
Kuna sifa nyingine nyingi zinazohitajika katika cheo hicho. Nabii wetu
Mtukufu Muhammad s.a.w. si kwamba hakuwa na dhambi tu, bali
zaidi ya hivyo yeye alikuwa na sifa zote za lazima kuwa mwokozi.
Qur`an Tukufu  inamtangaza Mtume s.a.w. kuwa ni mtu asiye na
dhambi, hali nabii Isa a.s. (Yesu) haikuwa hivyo. Ingawa manabii wote
wa Mwenyezi Mungu wana usawa katika hali ya kutakaswa na
madhambi.

Kule kuwapo  kwa mtu mmoja tu mtakatifu miongoni mwa watu,
huwa ni sababu ya uombezi kwa wanadamu. Kwani Mwenyezi Mungu
huzuia adhabu yake mpaka mtakatifu huyo atoweke miongoni mwa
watu hao. Agano la Kale linalo mfano katika jambo hili.  Nabii
Muhammad s.a.w. alikuwa mwanadamu mtiifu na mtimilifu. Kulikuwa
na mwungano mkubwa kati yake na Mwenyezi Mungu. Mtume
Muhammad  s.a.w. alizama katika mapenzi ya Mungu hivi kwamba
matendo yake yote, hata kifo chake kilikuwa kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu. Nafsini mwake Mtume Muhammad s.a.w. hamkuwa na viungo
vya kidunia na roho yake ilianguka mbele ya Mwenyezi Mungu kwa
mapenzi kamili yaliyojaa moyoni. Kwa njia hii Mtume Muhammad
s.a.w . ametekeleza sharti moja iliyo  ya lazima kwa mwombezi. Sharti
lile ya pili pia Mtume Mtukufu amelitimiza kama inavyothibitishwa na
Qur`an kwa kusema, "kisha akakaribia na akateremka na ndipo akawa
umbali wa pinde mbili au karibu zaidi" (Sura 53:9-10). Ndiyo kusema
nabii  Muhammad s.a.w. katika hali ya kiroho alinyanyuka juu kwa
ukaribu zaidi kama inavyowezekana akipitia kila daraja katika
kumkurubia Mola wake hata akafikia upeo wa mwisho wa hali yake
ya kibinadamu na ile sehemu yake timilifu ya mapenzi yake juu ya
mwanadamu.

Kwa upande mmoja alikuwa na mapenzi ya upeo wa juu ya
Mwenyezi Mungu  na upande mwingine alikuwa na huruma ya upeo
wa juu ya wanadamu. Hivyo Mtukufu Mtume Muhammad s.a.w.
alikaribia sana ule mpaka baina ya vipeo vya mwisho vya utakatifu na
uwanadamu na akawa mfano wa nguzo baina ya matao mawili. Bila
shaka Mtume Muhammad s.a.w. alikuwa kielezo halisi cha asili zote
za uombezi kama isemavyo Qur`an Tukufu, "Na lau wangalikujia
walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha, bila shaka
wangemkuta Mwenyezi Mungu Mwenye kupokea toba, Mwenye
Rehema." (4:65). Kadhalika tunasoma katika Qur`an Tukufu, "Chukua
sadaka katika mali zao, uwasafishe kwayo na kuwatakasa na
uwaombee; hakika kuomba kwako ni utulivu kwao" (Sura 9:103).25
Aya  hizi na nyinginezo nyingi kama hizi zinashuhudia kwamba Nabii
Muhammad s.a.w;  alikuwa mwombezi kwa walimwengu na kwamba
uombezi wake utawaongoza wale walio wanyonge nao watapata
heshima.

Mwenyezi Mungu amewabariki sehemu ya cheo cha uombezi
wafuasi watii wa Nabii Muhammad s.a.w.  Kwa mfano Masihi
Aliyeahidiwa a.s. Hadhrat Ahmad  wa Qadian,  wakati wa uhai wake
alijaaliwa uwezo wa kuwaombea watu, wengine waliokaribia kufa,
lakini kwa dua zake wameweza  kuishi hata sasa  (wakati  mtunzi
alipokuwa hai) kama thibitisho  dhahiri la kukubaliwa kwa uombezi
wa Masihi Aliyeahidiwa a.s. na Mwenyezi Mungu.  Baada  ya Masihi
Aliyeahidiwa a.s.  imeendelea kushuhudia kutimizwa kwa uombezi
wa Makhalifa wake watukufu. Wamebarikiwa wale wote wenye
kuyakubali haya na kufuata njia iliyonyooka iongozayo kwenye uzima
wa milele.

Ewe Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote! Ziondoe kufuru za
kidunia na uwaongoze viumbe  wako katika njia yenye kuwaepusha
dhambi! Uwafunue macho yao waweze kuiona njia ya ukweli ili
waweze kuifikia chemchem ya elimu ya yakini wapate kunywa hapo
maridhawa! Amin.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget