Saturday, February 11, 2012

UGONJWA WA UKIMWI


Ukimwi ni maradhi hatari sana yaliyogubika ulimwengu mzima. Maradhi haya nitisho kubwa sana kwa maisha ya binaadamu kwa sababu mpaka sasa mabingwa wa sayansi ya tiba hawajagundua kinga wala tiba yake. Inakadiriwa kuwa takribani watu milioni 13 wamekwishaambukizwa virusi vya gonjwa hili hatari ulimwenguni kote. UKIMWI kwa kishwahili, AIDS kwa kiingereza herufi za neno UKIMWI ndizo zinazobeba na kuwakilisha jina la ugonjwa hu harati, U = Ukosefu, KI – wa kinga. MWI – mwilini. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuzawadia mwili wa binadamu jeshi miongoni mwa majeshi yake mengi "…….WALA HAPANA YOYOTE AJUAYE MAJESHI YA MOLA WAKO ILA YEYE TU…..” 74:31
Majeshi hayo yaliyojikusanya pamoja ambayo hayaonekani kwa jicho tupu ila kwa msaada wa darubuni maalumu hupambana na kukishambulia kila kirusi/bacteria/kijidudu chochote cha maradhi kinachojipenyeza ndani ya mwili wa binadamu. Majeshi haya yakizidiwa na kushindwa ndipo kirusi/bacteria huushambulia mwili na kusababisha maradhi mwilini. Maradhi haya hatari ya ukimwi yanapouvaa mwili ndio huyasagilia mbali majeshi haya yaliyowekwa mwilini kwa nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hapo ndipo mwanadamu huweza kushambuliwa kwa urahisi uhai wake. Haya ndio maradhi yajulikanayo kwa jina la UKIMWI (AIDS), maradhi ambayo yanautikisa ulimwengu mzima hivi sasa na kuwafanya wana sayansi kukesha katika maabara zao ikiwa ni katika jitihada za kujaribu angalau kugundua tiba au kinga yake ili kuikoa jamii ya wanadamu kutokana na janga hili la kutisha. Ulimwengu mzima unapiga kelele, wanasiasa, viongozi wa kidini misikitini na makanisani wote wanafanya juhudi za kuelimisha na kuitahadharisha jamii juu ya maradhi haya. Mapesa chungu nzima yametolewa na serikali na mashirika mblaimbali katika kuelimisha na kuupiga vita ugonjwa huu, vitabu vimetungwa na filamu zimeandaliwa sambamba na mabango. Hebu tujiulize ni nini hasa sababu ya yote haya? Ni kitu/jambo gani lililotumbukiza ulimwengu katika janga hili? Nani hasa wa kulaumiwa kutokana na janga hili?
Naam, ni ukweli usiopingika na ni hakika iliyo wazi dhahiri kwa kila mmoja wetu kuwa UKIMWI ni matokeo ya binadamu kulibadilisha umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu, ni natija ya kubadilisha na kukengeusha kanuni za maumbile ya ulimwengu huu, ni sababu ya kuzipa mgongo hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu.
Tusome kwa mazingatio ‘BASI UELEKEZE USO WAKO KATIKA DINI ILIYO SAWASAWA, NDILO UMBILE ALALH ALILOWAUMBIA WATU(Yaani dini hii ya kiislamu inawafikiana barabara na umbo la binadamu ) HAKUNA MABADILIKO KATIKA MAUMBILE YA VIUMBE VYA ALLAH. HIYO NDIYO DINI ILIYO HAKI, LAKINI WATU WENGI HAWAJUI" (3:30). Ukaidi wa binadamu kuipinga haki na kutokuifuata ndio ulioifikisha hapa tulipo leo, nguvu kazi (vijana ) ya jamii, muhimili (wazee) wa jamii na rasilimali ya jamii inapotea na kumezwa na janga hili la ukimwi.
Mpaka malaika (watoto wadogo) walionao matumboni mwa mama zao tayari wamshaambukizwa na kuathirika na maradhi haya mabaya. Ni nani anayedhulumu uhai wao malaika hawa, kwani ni dhahiri kuwa hawatakuwa na muda mrefu wa kuyafurahia maisha haya, kabla kifo hakijawarejesha kwa Mola wao. Bila shaka dhalimu hapa ni mwenye kukhalifu sheria ya Mwenyezi Mungu. Maradhi haya ndiyo jazaa ya uoni na uchafu anaoufanya mwanadamu, ni malipo ya kuenea na kutapakaa kwa dhambi ya zinaa na liwati, ni thawabu za kuingiliana kimwili wanamume kwa wanamume, ni zawadi ya klabu za usiku (makasino) ni tuzo ya uhuru wa kuchanganyika mwanaume na wanawake katika msingi ya kile kinachoitwa usawa. Hayo ndio matokeo ya maendeleo tunayoyaiga kutoka kwa watu walioendelea wa Magharibi watu waliofika mwezini na sasa wanajaribu kwenda katika sayansi nyingine. Hawa ndio watu huru, wasemao tuacheni tufanye tutakavyo maadamu hatuvunji sheria za nchi, tuoane wanamume kwa wanamume na wanawake kwa wanawake. Serikali zao zikawakubalia na mabunge yao ya kapitisha sheria wakawa na wawakilishi bungeni, na wanamume wakaoana kisheria na hati za ndoa kutolewa na ndoa hiyo kushuhudiwa pengine hata na viongozi wa kiserikali na picha zikapigwa uchafu huu na fisadi hii ndio iliyoufikisha na kuutumbukiza ulimwengu katika janga hili la maradhi mabaya ya ukimwi. Tusome na tuyafanyie kazi "UHARIBIFU UMEDHIHIRI BARANI NA BAHARINI KWA SABABU YA YALE ILIYOYAFANYA MIKONO YA WATU (maovu) ILI AWAONJESHE (adhabu ya) BAADHI YA MAMBO WALIYOYAFANYA, HUENDA WAKARUDI (wakatubia kwa Mola wao)” (30:41). tuzidi kuwaidhika: “NA MISIBA (majanga) INAYOKUPATENI NI KWA SABABU YA VITENDO VYA MIKONO YENU (Maoni) ….” (42:30). Tafsiri potofu ya uhuru itolewayo na Magharibi ndio kiini cha janga hili. Uhuru na ufuska si uhuru wa haki, uhuru wa kinyama si uhuru wa haki, uhuru hakika si mtu kufanya apendavyo na kutamani lakini uhuru wa kweli ni mtu kufanya atakiwayo kufanya (yaliyompasa). Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka katika ulimwengu huu, kila kitu kina mpaka wake maswahaba walimuuliza Bwana Mtume- Rehema na Amani zimshukie- kuhusiana na mtu kukutana na mkewe katika kipindi cha hedhi, ikashuka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwajibu "NA WANAKUULIZA JUU YA HEDHI; WAAMBIE HUO NI UCHAFU: BASI JITENGENI NA WANAWAKE WAKATI WA HEDHI (zao) WALA MSIWAKARIBIE MPAKA WATWAHARIKE. WAKISHAKUTWAHARIKA BASI WAENDEENI KATIKA PALE ALIPOKUAMRISHENI ALLAH. HAKIKA ALLAH HUWAPENDA WANAOTUBIA NA HUWAPENDA WANAOJIITA KASA.” (2:222)
Aya inahalalisha kuwaingilia wanawake, na sio kuwaingilia popote bali mahali pa shamba (patoapo mazao) tena muingiliano huo uwe ni kati ya mtu na mkewe wa halali. Lakini utakapofika wakati wa adha (hedhi) basi imempasa mume kujizuia na kuidhibiti nafsi yake mpaka mkewe atwaharike kwa kumalizika hedhi yake. Ama mtu kutenda kinyume cha hivi, akapaendea mahala pengine, mahala pa uchafu ambapo hapakuumbwa kwa ajili ya tendo hili la ndoa, mahala pasipootesha mimea huko ni kuyabadilisha maumbile ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanamume kuwa ni mfanywaji apandwe bali awe ni mfanyaji apande yeye wala hakuiumba duburi (utupu wa nyuma) kwa ajili ya kuingiliwa bali kwa kazi maalumu na muhimu. Kazi hii si nyingine ila kutoa nje makapi ya chakula yasiyohitajika mwilini ambayo kama hayakutoka binadamu hawezi kuwa binadamu mwenye afya na siha njema. Kila kiungo katika mwili wa binadamu kimeumbwa kwa lengo/kazi maalumu ambayo haiwezi kufanywa na kiungo, kingine ila hicho hicho tu, sasa kukitumia kiungo kwa kazi isiyo yake, huko si kubadilisha umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia waja wake? Ni ufundi huu wa binadamu kijifanya mjuzi kuliko Muumba wake na kubadilisha kanuni za maumbile ndio uliotufikisha kuogelea, katika bahari hii ya ukimwi. Kwa mtaji huu hatujui ni nini kitafuatia baada ya ukimwi! Historia inatuonyesha kuwa watu waliufanya ufundi huu wa kubadilisha umbile la mwenyezi Mungu nao si wengine bali ni kaumu ya Nabii Lutwi hawa ndio viumbe na kwanza kuanzisha uovu na uchafu huu wa kuingiliana wanamume kwa wanamume. Tusome na tuzingatie. “NA (tulimpeleka) LUTWI. BASI (wakumbushe watu wako) ALIPOWAAMBIA KAUMU YAKE JE! MNAFANYA JAMBO CHAFU AMBALO HAJAKUTANGULIENI YOYOTE KWA (jambo chafu) HILO KATIKA WALIMWENGU!”.(7:80)
Mwenyezi Mungu aliwapelekea waja wake hawa mtume wake Lutwi Amani imshukie awaite kwake na wauache uchafu huu Akawaambia (Lutwi): “MNAWAINGILIA WANAMUME KWA MATAMANIO MABAYA BADALA YA WANAWAKE? HAKIKA NYINYI NI WATU MFANYAO YA UJINGA KABISA” (27:55) Akawaambia tena: “NYINYI MNAWAENDEA WANAMUME KWA KUWA NDIO MNAOWATAMANI BADALA YA WANAWAKE! AMA NYINYI NI WATU WAFUJAJI”. (7:81) Akazidi kuwaasa, “ NA MNAWACHA ALICHOKUUMBIENI MOLA WENU KATIKA WAKE ZENU? KWELI NYINYI NI WATU MNAORUKA MIPAKA (mliyowekewa)” (26:166)
“…. BILA SHAKA WAO WALIKUWA WATU WABAYA, WAVUNJAO AMRI”. (21:74) Nabii Lutwi aliwasifia watu hawa kwa kila sifa mbaya kutoka na kitendo chao hiki kichafu, kisha akamuomba Mola wake amuepushe na watu waovu hawa walioitia doa historia nzima ya jamii ya wanadamu. Nae Mwenyezi Mungu akalikubali ombi la Mtume wake na akamuokoa na watu wa ule mji uliokuwa ukifanya maovu. Hakika hili ni janga na msiba, atakayesibiwa na msiba huu, akili humtoka, utu humvuka na mahala pake kukaliwa na unyama kwa maana ya unyama. Hawa walistahiki kufikwa na adhabu ya Mola wao na waliadhibiwa kwa adhabu ambayo Mwenyezi Mungu hajapata kuadhibu kwa adhabu kama hiyo kwa kaumu zilizowatangulia na zilizokuja baada yao ikiwa ni jazaa ya uovu na uchafu wao ambao haukupatwa kufanywa na ye yote kabla yao. Tusome, tuwaidhike na tuonyeke “BASI ILIPOFIKA AMRI YETU, TULIIFANYA (ardhi hiyo iwe juu chini) JUU YAKE KUWA CHINI YAKE NA TUKAWATEREMSHIA MVUA YA CHANGARAWE ZA UDONGO MGUMU (wa motoni uliokamatana) (changarawe) ZILIZOTIWA ALAMA KWA MOLA WAKO (kila moja kuwa ya mtu fulani)NA (adhabu) HII HAIKO MBALI NA MADHALIMU (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya)”. (11: 82 – 83)
Leo baadhi yetu wamerudia kuufanya uchafu huu ulioasisiwa na kaumu ya Mutme Lutwi, wakauonea fakhari na kuutangaza dhahiri bila kificho mpaka kufikia hatua ya kuuhalalisha kwa kuoana na kuwa na klabu zao maalumu na kujitangaza katika vyombo vya habari. Kiovu zaidi walichowashinda hawa wa leo wale wa zamani wa kaumu Lutwi ni kwamba hawa wa leo wana kanuni/sheria zinazowalinda na kuwahalalishia biashara yao hii chafu zilizotungwa na mabunge ya nchi zao na serikali zao kuwatoza kodi kwa mapato machafu wanayoyapata kutokana na biahara yao hii chafu. Kwa masikitiko makubwa yapo baadhi ya makanisa katika nchi fulani fulani yanathubutu kulibariki tendo hili chafu makanisa yanayojinasibisha na Nabii Isa mwana wa Mariam Amani imshuku ambaye alikuwa akisema "waliokuwa kabla yenu walikuwa wakisema usizini na mimi ninasema Atakayetazama kwa macho yake, atakuwa amezini". Hivyo ndivyo tunavyosoma katika Injili. Nabii Issa anaharamisha kutazama, vipi basi, viongozi hawa wa kamanisa wanajasiri kuhalalisha aliyoyaharamisha Mungu kupitia kwa Mitume wake wote akiwemo Nabii Issa ambao wao wanadai kumfuata?! Wanaupa baraka zote uchafu na uoza huu Ni ustaarabu gani huu?! Tunaelekea wapi?! Turudi ndugu zanguni, UKIMWI hauna dawa, tutakwisha, Kondomu sio kinga ya ukimwi, kinga na dawa pekee dhidi ya maradhi haya ya hatari ni kurejea kwa Mola wetu, tujisalimishe kwake kwa kufuata hukumu na sheria zake. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuhifadhi na kutukinga kwa mafundisho ya dini yake na hukumu za sheria yake na itikadi ambayo humfanya muumini kuwa imara kama jabali madhubuti mbele ya matamanio machafu na maovu kiasi cha kutokutetereka. Uislamu umemlea mwanadamu kuinamisha macho na kuhifadhi utupu wake, tusome na tunaisihike: WAAMBIE WAISLAMU WANAUME WAINAMISHE MACHO YAO (wasitazame yaliyokatazwa) NA WAZILINDE TUPU ZAO, HILI NI TAKASO KWAO, BILA SHAKA ALLAH ANAZO HABARI ZA (yote) WANAYOYAFANYA. NA WAAMBIE WAISLAMU WANAWAKE WAINAMISHE YAO NA WAZILINDE TUPU ZAO, WALA WASIDHIHIRISHE VIUNGO VYAO ISIPOKUWA VINAVYODHIRIKA (nao ni uso na vitanga) NA WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO NA WASIONYESHE MAPAMBO YAO….” (24: 30 – 31)
Uislamu umemlea muumini katika malezi ya kutochanganyika kimwili ila katika halali (ndoa) Mongoni mwa sifa walizosifiwa nazo waumini ndani ya Qur-ani ni: “NA AMBAO TUPU ZAO WANAZILINDA ISIPOKUWA KWA WAKE ZAO TU AU KWA (wanawake) WALE ILIYOWAMILIKI MIKONO YAO YA KUUME. BASI HAO NDIO WASIOLAUMIWA. (Lakini) ANAYETAKA KINYUME CHA HAYA, BASI HAO NDIO WARUKAO MIPAKA (ya Allah)” (23: 5 – 7)
Uislamu umemfungia muislamu milango na mianya yote ya haramu sambamba na kumfungulia milango ya halali …”BASI OENI MNAOWAPEMDA KATIKA WANAWAKE (maadamu mtakuwa waadilifu) WAWILI, AU WATATU AU WANNE (tu) NA MKIOGOPA KUWA HAMUWEZI KUFANYA UADILIFU, BASI (oeni) MMOJA TU…(4 : 3)
Sasa wanadamu wanapoyatupilia mbali mafundisho haya ya Mola wao na kufuata matashi na matamanio ya nafsi zao kwa kutneda yale ya haramu yenye kubadilisha umbile lao waliloumbiwa, hao wamestahiki kupata adhabu kali ya Mwenyezi Mungu aliye mkali wa kuadhibu. Mbali na zile adabu/adhabu za kisheria alizompa mamlaka kiongozi aongozaye kwa kutumia Qur-ani kuzitekeleza kama vile kumkata mkono mwizi, kumcharaza bakora mzinifu au kumpiga mawe mpaka afe na nyinginezo pia ana adhabu za kimaumbile zinazotawaliwa na nguvu yake ya utendaji. Maradhi haya ya ukimwi yanaingia katika kundi hili la adhabu za kimaumbile kama alivyotutanabalisha na hilo Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie katika hadithi iliyopokelewa na Ibn Maajah, Al-Haakim na Al-Bayhaqiy ikiwa ni upokezi wa Ibn Umar Allah awawie radhi kwamba Mtume aliwaambia maswahaba wake. “Enyi kusanyiko la Muhajirina, mtakapotahiniwa kwa mambo matano na ninajilinda kwa Mwenyezi Mungu msiyadiriki (na likawa la mwanzo la matano hayo) haukudhihiri uchafu (zinaa) katika kaumu katu (kabisa) mpaka wakautangaza wazi wazi ila itaenea kwao tauni na magonjwa ambayo hayakuwepo kwa wahenga wao walipita…”
Naam, ni kweli ukimwi nido tauni ya zama hizi na ni kweli kuwa maradhi haya mabaya hayakuwepo huko nyuma bali yamezuka hivi karibuni tu, ni kweli kabisa haya ni maradhi mapya. Watu wamezua uchafu na uovu na Mola wao amewazushia adhabu. Enyi mliopotea rudini, enyi waasi tubieni, Mwenyezi Mungu anajtuambia “NA MISIBA INAYOKUPATENI NI KWA SABABU YA VITENDO VYA MIKONO YENU, NA (juu ya hivi Allah) ANASAMEHE MENGI.” (42:30).
“….. ILI AWAONJESHE (adhabu ya) BAADHI YA MAMBO WALIYOYAFANYA HUENDA WAKARUDI (wakatubia kwa Allah)”. (42:41)
Yaani Mwenyezi Mungu anawazindua waja wake kwa adhabu za maradhi kama haya ya ukimwi ili warejee kwake. Basi,
·je, watarejea waliokengeuka?!
·Je, watatubia waasi hawa?!
·Je, wataongoka wapotevu hawa?!
·Je, wataongoka wapotevu hawa?!
·Je, watazinduka walioghafilika?!
·Je watatubia waasi hawa?!
·Je, wataongoka wapotevu hawa?!
·Je, watazinduka walioghafilika?!
·Je, wataamka wale wote waliolala?!
Tunasihike: "… BASI JE, MTAACHA (mabaya hayo).” (5:91)

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget