Ni mara chache sana kumekuwa na mafanikio ya kuwabadilisha Waislamu kuingia katika Ukristo, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Waislamu wamekuwa wagumu sana kuingia katika dini nyingine ama iwe katika zama za Ukoloni au hata sasa. Harakati za kuwafikia Waislamu kwa lengo la kuwabadili itikadi zao haswa zilianza wakati wa ukoloni.
Wamisionari wa makanisa mbalimbali walifanyakazi bega kwa bega na Serikali za Kikoloni, miongoni mwa majina maarufu sana ya Wamisionari kwa Waislamu ni kama yafuatayo: Henry Martyn, Pfander na William Cary India, Lafigerie huko Algeria na Samuel Zwemer na William Gairdner katika ulimwengu wa Kiarabu walitumia muda wote wa maisha yao bila hata kupata Muislamu mmoja aliyesilimu.
Baada ya kuona kwamba harakati zao hazikuzaa matunda wamisionari waliitisha mkutano wa Misri uliofanyika CAIRO mwaka 1906 ili kuweka mikakati zaidi ya kuwasilimisha Waislamu.
Ikielezewa kama ni ukurasa mpya wa harakati za kuwasilimisha Waislamu Mkutano huo wa Misri ulihudhuriwa na wawakilishi 60 kutoka katika makanisa takribani 30. Mkutano huo wa CAIRO ulifuatiwa na ule wa Edinburgh MWAKA (1910), Lucknow (1911) na Mkutano uliofanyika Jerusalem (1924).
Mikutano hiyo kwa kiasi kikubwa ilipelekea kuchuliwa hatua mpya mfano maeneo ya Waislamu yaligawanywa kwa makanisa hayo na wamisionari wakaanza harakati zao za Ukoloni wa kiroho ambao hata hivyo ulishindwa kuonyesha mafanikio katika ulimwengu wa Kiislamu isipokuwa Indoniesia.
Lakini wamisionari walionyesha uhai (nguvu) katika maeneo mengine ya Asia na Afrika. Mnamo mwaka 1985 takribani robo million ya wamisionari wa Magharibi walikuwa katika Afrika na Asia pekee wakiwakilisha jumuia 3500 za wamisionari huko Magharibi mwa Afrika. Nchi za Magharibi hutumia kiasi kingi sana cha fedha kwa shughuri ya kueneza Ukristo kwa mujibu wa David Warren Mhariri wa Enyclopedia ijulikanyo kama World Chrestiani Enyclopedia (yaani insaiklopidia ya ulimwengu wa Kikristo).
Misheni walitumia Us 70 billion mwaka 1970, $1003 billion mwaka 1980 na matarajio ya bajeti kwa mwaka 1985 yalikuwa dola $127 billion.
Wamatumia kila chombo wanachoona kinafaa ili kuweza kuzifika. Mwaka 1984 palikuwa na Radio zao 21000 zikitanga kwa lugha mbalimbali. Mwaka 1984 walisambaza vitabu agano jipya kiasi cha nakala 64 million. Wastani wa idadi ya nakala zilizoenezwa bure katika miaka 60 iliyopita mpaka kufikia mwaka 1984 zilifikia nakala 43 million.
Kwa kutumia vivutio kama huduma za jamii shule Mahospitali juhudi zao zilipata mafanikio kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka katika Misionari kinasema kwamba watu 115.9 million waliweza uingia katika Ukristo wakati wa Miongo saba ya karne hii. Pamoja na kukumbana na ugumu wa kuwabadili Waislamu wamisionari hawakukatia tamaa katika harakati zao hizo.
Tunakuta katika kipindi cha hivi karibuni mkutano wa Lausanne juu ya uenezwaji wa Injili duniani uliofanyika mwaka 1974 ulilitazama kwa makini suala la kufikia katika maeneo yasiyofikiwa hasa maeneo ya Waislamu.
Miongoni mwa watu bilioni tatu ambao walikuwa hawafikishiwi ujumbe (Ukristo) 24% walikuwa Waislamu.
Mkutano huo wa Lausanne uliofatiwa na ule wa Pasadena uliofanyika mwaka 1977, Pia Pasadena ukafuatiwa na Willowbank mwaka 1978 na mwisho mkutano wa Amerika ya Kaskazini ulilenga kufikisha Ukristo kwa Waislamu uliofanyika Gleni Eyrie Colorado kwa muda wa wiki moja mwezi Oktoba.
Watu 150 kutoka sehemu mbalimbali duniani walihudhuria Mkutano huo kutokana na mkutano huo taasisi iliyojulikana kama Smuel Zwemer ilianzishwa huko Califonia ya Kusini na Bw. Mc Curry akiwa ndiye mkurugenzi wa taasisi hiyo.
Taasisi hiyo ndiyo ilikuwa na jukumu la kuratibu harakati zote za kuwafikishia Waislamu injili.
Leo hii kuna Misheni nyingi mia kwa mamia zinazoshughurika na harakati za kuwafikishia Waislamu Injili. Baadhi yao ni kama vile Gairdner ambayo sasa inajulikana kama (People international), operation mobilazation operashen mobilaizeshen, Evangiliko Misionari feloship, Feloship of feirz to Muislim n.k.
Wamisionari wao wanaamini kwamba Uislamu ni dini ya shetani na hii siyo itikadi ya zamani kama Wakristo wanavyotutaka tuamini hivi sasa kwamba waliokuwa wakiamini hivyo ni Wakristo wa zamani hata hivi sasa Wakristo wanaamini hivyo.
Hebu tunukuu maelezo yafuatayo ya mmoja wapo wa washiriki wa mkutano ule wa Colorado mwaka 1978,
Bw. W. Stanley Moone han Mkuu wa shirika lijulikana kama World Vision. Alinukuliwa akisema: “Mapambano yetu si dhidi ya damu au mwili, maadui hawa ni kama nyenzo tu katika mikono ya bwana katili ambaye amekusudia kuwashikilia ndugu zetu kwa kutumia siraha za Ustawi wetu tunaweza kabisa kuzuia adui huyo.
” Mojawapo ya harakati za wamishionari hao za kutaka kutuokoa kutoka katika mikono ya shetani ni zile za (RsmT) Read sea Mission Team jumuia ambayo inafanyakazi za kuwafikia waliobaki nyuma kimaendeleo, wasio na elimu na mafukara, tasisi hiyo ya (RsmT) hufanya kazi kwa siri kubwa.
Kwa mara ya kwanza niligundua shughuli za taasisi hiyo miongoni mwa Waislamu pale nilipokuwa Uingereza mnamo January mwaka 1983. jitihada zilizofanywa na mimi binafsi na marafiki zangu kupata moja ya nakala za katiba/malengo ya Taasisi hiyo zilishindikana.Katika siku zilizofuata ilikuwa January 17 1983
BW. John Oakfield alafu na mkurugenzi wa taasisi hiyo au mkurugenzi mkazi aliniambia kwamba wao hawapo tayari kutoa nakala ya malengo ya taasisi yao kwa mtu ambaye hawapo naye pamoja yaani mtu ambaye hawana imani kuwa anakubaliana na malengo ya taasisi yao.
” Utafiti wangu (wa mwandishi wa makala haya) uliendelea mpaka pale Mwenyezi Mungu aliponijalia kuzikamata nakala 10 za (RsmT) zilizo kusudiwa kupewa wafanyakazi.
Katika vitabu hivyo vipo vingine vilivyokuwa na vichwa vya habari “Waislamu watasikia kufungua mlango.
” Pia Masomo juu ya Uislamu na jinsi ya kuwashuhudia kufikia Waislamu” vitabu vilivyoandikwa na Jack Budd.”
Kauli mbinu ya (RsmT) ni kwamba “Waislamu watasikia”Ni taasisi mashuhuri iliyo kusudia kuwahubilia Injili ya Yesu kwa Waislamu,
(RsmT) inatilia mkazo uenezaji wa Injili wa mtu binafsi kupitia (a) Mahospitali (b) Katika maeneno ya elimu (c) Katika nyanja maeneo ya kilimo (e) Tafsiri katika lugha mbalimbali n.k. (RsmT) iliasisiwa na Dr. Lionel Gurney mwaka 1951 huyu bwana alitumai miaka 17 katika kazi yake hiyo ya Umishionary huko Mashariki ya mbali, kiongozi wa sasa ni Bw.Wolfang Stumpf amabaye office yake iko 87 Alcester Road Mosley Bir mingham. B 13 8E B.
(RsmT) ina office Australia Canada, Ujeruman, Uholanzi, Korea, Newzeland, Sweden, Uk na U.S.A. chanzo cha fedha kwa taasisi hiyo hakikuwekwa wazi wala taasisi hiyo haitoi matangazo ya kuomba Misaada ya fedha.
Kazi ya (RsmT) ilianza Aden na Arabia ya Kusini wakati huo ukiwa chini ya uthibiti wa Uingereza ambao uliendelea mpaka 1972. kuanzia mwaka 1956 – 1978 (RsmT) ilishaingia nchini Ethiopia.
Pia kule Eritrea. Mwaka 1969 Taasisi hiyo ilifanya kazi katika jamhuri ya watu wa Yemen Mpaka mwaka 1981 ilipoondoka.
Pia kuna ushahidi kuwa taasisi hiyo inafanya kazi zake nchini Somalia. Mnamo mwaka 1975 timu hiyo ilianza kazi zake nchini Djibouti iliyokuwa wakati huo na wakazi 350,000 ambapo 100% asilimia mia ya wakazi wake walikuwa Waislamu shughuli zao zilikuwa zikifanyika katika duka la vitabu lililojulikana kama “Libraries Emmanuel” Duka hilo la vitabu lilikuwa liendeshe masomo ya lugha ya Kifaransa, Kingereza na pia masomo ya fasihi.
Timu hiyo ya wafanyakazi wa (RsmT) imekuwa ikitafsiri Biblia katika lugha za Afar na Pia kuandika dikshorani (kamusi) ya English/Afar/French.
Kazi hiyo ya Tafsiri ya Biblia imekuwa ikifanywa na Yvonne Genet kwa msaada wa watu wawili kutoka kabila la Afar mmoja kati yao ni Mwislamu, na yule mwingine alikuwa mkomunist.
Mwandai wa kamusi hiyo alikuwa ni Bw. Enid. Parker.
Hii ni njia moja muhimu na isiyo na upinzani ya kuingia nchi ili kuweza kujifanyia mambo ambayo mhusika anakusudia kuyapata timu hiyo ya Djibouti pia huandaa kanda za kaseti na kisha kuwapa watu ambao huzisambaza kanda hizo katika maeneo mbalimbali.
Mnamo mwaka 1987 nchini Djibouti kulikuwa na wafanyakazi 29 wa (RsmT).
Watu hao wamesema kwamba kwa kutumia mbinu hiyo watu wengi wameingia katika Ukristo.
Djibouti ni (RsmT) tegemeo ni moja ya mpango uliotoa mafanikio mkubwa amesema Bw. Stumpf,
kikundi hicho cha watu 29 ni mashuhuri zaidi katika maeneo matano nchini Djibouti nayo ni (a) Mji Mkuu wa Djibouti (b) Hanley (bonde la Hanley) karibu na Yoboki (c) Adailou, (d) Randa na (e) Ali Subieh.
Wawili kati ya wafanyakazi 29 wanafanyakazi katika hospital na wako katika wodi za kina mama wadi yenye vitanda 40. katika eneo la Ali Sabieh.
Katika ripoti yao kwa Uongozi wa (RsmT) wafanyakazi hao wa hospitali wanaandika: “Tunamuomba Mungu wetu atupe maarifa zaidi juu ya namna ya kumpendeza yeye ili tuweze kushughulika na wale tunaowahudumia hapa na pia wale tunaofanya nao kazi pamoja. Kadili suala lugha linavyopatiwa ufumbuzi hivi sasa uwezo wa kuwasiliana na watu umeongezeka sana na mahusiano baina yetu na wenyeji yamekuwa mazuri, wakati wa sikukuu ya Krismasi huwa tunawaalika baadi ya wenzetu (watu) kuja kusherehekea ambao huweza kupata habari malimbali za historia ya sikukuu hiyo ingawa bado hupajawa na mafaniko makubwa sana lakini tuna amini kwamba tupo katika kipindi cha kulima na kupanda.”…
(RsmT) Pakistan’s open Door anasema wamisionari wa Kikristo waliokuwa wakitoa huduma hiyo huko Pakistani mwaka 1833.
Hivi sasa kuna jeshi la watu 500 nchini Pakistan ambao hata hivyo hawajafika maeneo mengi bado kuna eneo kubwa sana ambalo halijafikiwa.
Miongoni mwa wafanyakazi (RsmT) walioko Pakistan ni hawa: Ian na Dorca, Denness, Anitra Lockwood, Edda Dohm (kutoka Ujeluman Magharibi), Rod na Miriam Vardy RsmT wanafanya kazi zao miongoni mwa wabaluchi 600,000 Karachi na katika Kijiji jirani na Mardan NWFP.
Vile vile katika eneo linalojulikana kama Jacobabad Baluchistan.Wameanzisha huduma ya matibabu katika eneo hilo la Baluclustan, maili chache kutoka Jacobabad eneo lenye wakazi wengi sana likiwa na mabwanyenye (mabepari) wanaomiliki mashamba makubwa makubwa na wafanyakazi vibarua wenye kukodi mashamba kwa kulipia ambao wengi ni fukara.
Ni katika maneno hayo ya watu mafukara ambako wafanyakazi hao wa RsmT hupenda kufanya kazi zao moja ya shughuli zao ni kutafsiri Biblia katika lugha ya kibaluchistan.
Kwa mujibu wa ripoti ya (RsmT) kwa mwaka 1987 kundi hilo hufanya kazi pia kwa watu wenye ukoma wa Afghan katika eneo la mpakani.
Mkurugenzi mkazi wa RsmT U.K. Bw. Peter Draper anasema katika barua yake mwaka 1987 kwamba “matatizo tunayokabiliana nayo katika maeneo ya Waislamu wa Pakistani ni kule kushindwa kujua matokeo ya huduma zetu baada ya muda fulani (yaani hawawezi kutabiri matokeo ya kazi zao)
”Nchini Sudan kundi la wafanyakazi wa (RsmT) limekuwako huko tangu mwaka 1978 miongoni mwa watu wa kabila la Beja linasemekana kwamba lilikuwa katika hali ya kukata tamaa, lilikuwa gizani, halikuwa na matumaini kabisa ndio wao wakaamua kuanza kazi yao kwa kabila hilo kwa sababu wanaamini kwamba ni rahisi sana kufikisha ujumbe wao na wakakubaliwa.
Kundi hilo lilikuwa na nguvu sana katika eneo linalojulikana kama Port Sudan na maeneo yanayozuguka mpakani mwa Misri.
Kiongozi wa kundi hilo Bw. Stumpf akiongoza kongamano lililojadili kazi ya kueneza Injili katika eneo la Port Sudan mwaka 1986. Kundi hiko lilianzisha Koloni katika sehemu inayoitwa Bir Eit jirani na Port Sudan ambapo walianzisha kliniki na bustani.
Tunasoma katika ripoti zao kina Loek de vette kutoka mwezi wa (11 – 1985) na Mary Grundy ambaye alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha afya cha Sudan na Loek de vette akifanya kazi kama tabibu.
Lengo la kazi zao kama Mary anavyosema: “Ni jambo jema si kwa upande wa suala la chanjo kwa pekee bali pia inatia moyo kuona kwamba mawasiliano na watu yamekuwa mazuri sala zangu zote huwa ninaomba kwamba uchu huo uendelee ili kwamba watu wengi zaidi wawezi kupokea Injili.”
Hapa Loek anaelezea kwamba pamoja na kufanya kazi ya utabibu lakini jukumu kubwa alilonalo ni kuhakikisha kwamba anaeneza Injili. RsmT Pia iliingia hadi Tumalah na Kol koi (wadi Amur) lakini baada ya muda wafanyakazi wa taasisi hiyo walifukuzwa na wananchi.
Timu hiyo ya (RsmT) ulianzisha huduma ya hospital katika eneo la Amur. Mwaka 1985 lakini hospitali hiyo ilifungwa muda mfupi baada kufunguliwa kwa sababu wakuu wa kijiji hicho walikataa kuwapa ruhusa wafanyakazi wa RsmT kuishi katika eneo lao.
Baada ya kukataliwa kuwapo katika eneo la Amur hatimae walikimbilia katika eneo jingine lililojulikana kama Eit ambalo lipo jirani na (wadi Amru) kiasi cha mwendo wa masaa (2) kwa gari katika maeneo yote ya Waislamu eneo ambalo lilikuwa rahisi au watumishi wa RsmT hawakupata upinzani ni Mali ambapo kabila la Serakile linalopatikana upande wa Kaskazini Magharibi ndilo lililokuwa shina la harakati zao hizo.
Licha ya Mali timu hiyo ya watu wa (RsmT) pia ilikuwa inafanya kazi zake katika maeneo ya Ulaya Magharibi na Canada Miongoni mwa wahamiaji Waislamu majukumu yao ni kuwasiliana na wahamiaji wanafunzi wageni na makundi mengine ambapo walianzisha urafiki nao kwa lengo la kuwafikishia Injili. Lakini kuna dalili katika Makaratasi (kumbukumbu) zao kuwa kwa uchache sana wameweza kuyafikia maeneo ya Kiarabu ndio maana tunasoma katika moja ya taarifa za RsmT juu ya Helen Hislop kule Sharjah na mahitaji ya kuongeza wafanyakazi zaidi.
Mfanyakazi mwingine wa (RsmT) kwa jina Magda Bach tangu alipotimuliwa Yemen baadae akaenda Misri katika eneo lililojulikana kama Aswan 40km Mashariki ya Aswan.
Mara kwa mara hufanya kazi katika Hospital moja huko Aswan. “Watu wengi huja katika Hospitali yetu na kuweza kusikiliza Maneno ya Mungu.” Anasema Magda.
Watumishi wengi tu wa RsmT inasemekana wanajifunza Kiarabu huko Amman Jordan. RsmT inajaribu kufanya kazi (2) kwa wakati mmoja kueneza habari za Ukristo na wakati huo huo kuwasaidia wale wasio na uwezo (kuwapatia watu mahitaji muhimu kama elimu Matibatu).
Kwa hiyo ndio kusema RsmT huweza kusambaza Ukristo kwa njia ya uanzishwaji wa mashule hospitali n.k. kuwavuta watu waweze kuja katika maeneo yao na hapo kazi ya kuwafikishia neno huanza. Ni kazi ya kiroho ambayo ndiyo lengo la juhudi zetu zote hizi lakini hata hivyo pia inabidi kazi hiyo ya kiroho iambatane na misaada ya kawaida. Kiongozi wa RsmT Bw. Stumpf alisisitiza: “Kama lengo la kuwafikishia watu wengi neno la Mungu basi tutakuwa tumepoteza haki ya kusikilizwa.”
RsmT huwatafuta watu wa kujitolea katika maeneo ya (nyanja) za kielimu, kilimo, Matibabu, Uhandisi na ujenzi stadi.Katika moja ya taarifa zilizogunduliwa kutoka RsmT zile zinazosema kwamba wale wanataka kuwa wawakilishi wa RsmT lazima wapitie mafunzo ya mwaka kabla ya kufanywa kuwa Mwakilishi/mtumishi wa RsmT.
Wamisionari katika harakati zao wanawalenga sana wale watu ambao waliokuwa nyuma kimaendeleo na wasiokuwa na elimu miongoni mwa jamii ya Waislamu.
Mtego wanaoutumia kuhakikisha wanawanasa watu hao ni kwa kuanzisha huduma ya misaada katika kilimo, elimu pamoja na huduma za afya. Ili kuweza kuanzisha kanisa sehemu wamisionari hao kwanza huwatafuta wenyeji kama wawili hivi au mmoja katika eneo husika kisha humsomesha mtu yule na kumpa msaada wa fedha ili kuweza kuifanya kazi hiyo sawasawa.
Kwa kuwa mtu yule ni mwenyeji wa pale atajua nani rahisi kupokea ujumbe kwani ataifanya kazi hiyo akipata mtu mmoja wataunganika nakuwa wengi hasa ukizingatia watakuwa na huduma za jamii. Lakini wamisionari waliofanya kazi ya chini Djibouti wanakili kwamba kumekuwa na ugumu sana katika kuwapata waumini mfano wanasema kwamba wakati wakiwa Djibouti wale watu waliokuwa wakija kwao kupata huduma za shule, matibabu na huduma zingine huwa wanasema kabisa “sisi ni Waislamu hivyo hatupo tayari kuingia katika Ukristo.
” Hili ni jambo la kufurahisha kuona kwamba Waislamu wamekuwa madhubuti katika itikadi (dini yao) na bila shaka itawaamsha Waislamu. Mirianne Leuriberger ambaye alikuwa anaendesha kriniki moja huko Haule Valley Djibouti anasema: “wakati Fulani huwa nakatishwa tamaa kabisa na jinsi watu hao walivyo na msimamo katika imani yao, lakini hata hviyo najua kwamba itachukuwa sana ili kuweza kukubalika kwa sababu lengo letu si afya tu kuwapatia huduma za afya pekee bali pia kuwafanya wampokee Kristo.” Ernst Leuenberger, Pia katika hilo la bonde la Haule anasema: “Kwa hakika hata baada ya muda wa miaka yote ya utumishi hapa hapajawa na mafanikio ya wazi katika kazi yangu ya kiroho watu wamekuwa wakihitaji huduma zitolewazo nasi wala siyo ujumbe wa Injili.
” Loek de vette anaendelea kusema kwamba hapana ushahidi wa kutosha kuwa watu wamempokea Kristo huko Port Sudan. Katika maombi ya kutaka aombewe ili kazi yake iwe rahisi de vette anasema: “giza bado linawazuguka watu wa Port Sudan kwa sababu hawajampokea Kristo.” Kuhusu wale wanaobahatika kuwapata kuingia katika Ukristo de vette anaongeza kusema kwamba watu huwa hawadumu katika imani na hurejea tena katika dini yao ya awali Uislamu.
Hakuna sababu ya kufarijika na ukweli kwamba Waislamu wamekuwa wagumu kuingia katika Ukristo kwa sababu hatari iliyopo bado ni kubwa, ni wajibu wa kila Mwislamu wenyewe elimu kuutanabaisha Ummah wa Kiislamu juu harakati hizo za watu hawa.
No comments:
Post a Comment