Wednesday, May 2, 2012

UN: Israel inakwamisha shughuli za kutetea haki za binadamu


UN: Israel inakwamisha shughuli za kutetea haki za binadamu
Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeuweka utawala haramu wa Israel katika orodha ya pande zinazozuia shughuli za mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani.
Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametoa taarifa akisema kuwa Israel imewekwa katika orodha ya pande zinazozuia shughuli za mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Siku chache zilizopita nchi wanachama wa Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa zilitoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina huko katika Ukingo wa Magharibi.
Jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu pia zimekuwa zikiikosoa vikali Israel kutokana na kuendelea kuwakandamiza raia wasiokuwa na hatia wa Palestina

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget