Ndugu yangu katika imaan,
Nimeipenda sana hoja hii iloandikwa na host wa HakiForums mpaka nimeona niiweke hapa nanyi muweze kupata wasaa wa kutafakari juu ya hili.
--------------------------
Assalaam aleykum,leo napenda tutazame viongozi wetu kutokuwa na maadili,swali ni je,tuliwaandaa na tunamikakati gani?
Kumekuwa na malalamiko juu ya baadhi ya waumini wetu wa kiislam wanafanya vibaya katika uongozi.
Siku hizi mazingira yamebadilika sana,aliyesoma madrasa unaweza kukuta hana tofauti na asiyesoma! Japo wengi waliosoma na kamua hujitahidi katika maisha yao.
Wengi waliosoma dini basi utakuta elimu ya mazingira hawana na wale ambao wanaelimu ya mazingira basi elimu ya dini hawana au wapo wachache sana.
Kutokana na kuwa na wasomi ambao hawajui dini yao ambao ndio haohao wanaotegemewa kuwa viongozi wakubwa wa nchi yetu na baada ya kuwa viongozi huitizama dunia na kufanya ufisadi tu. Kisha tunakaa pembeni na kulaumu kuwa wanauaibisha uislam kwani tuliwaandaa katika mazingira ya dini na kumtii Allah(s.w) na mtume wake?
Badala ya kuweka mikakati ya kuandaa vijana watu wamekalia utaasisi na madhehebu na kupigana vijembe na wakati mwingine hata kukwamishana katika maendeleo.
USHAURI WANGU
Kuwe na kamati maalum ya kuwafunda viongozi na hata kuwachukulia hatua ya kuwaonya na kama wataendelea basi watangazwe na watengwe katika jamii ya kiislam na endapo watakufa basi wasizikwe kiislam.
Waislam kwa umoja nchi nzima yeyote atakayekwenda kinyume na maadili kutoka nyumbani hadi katika utawala aadhibiwe kwa kutengwa na kutokuhudumiwa kwa chochote na waislam.
Waislam wote washikamane pamoja na atakayekengeuka basi waislam wamtenge abaki mwenyewe.
Kila wakati viongozi waandaliwe ili kuwafanya kumwogopa Mungu na kumtumikia Mungu badala ya kutumikia matamanio yao tu. Viongozi wapewe semina mara kwa mara ili wajengewe uwezo wa kiroho na imani.
Dini na siasa nisawa na binadamu na upumuaji wa hewa ya oksijeni au samaki na maji hivyo ni viitu visivyotengana kamwe,kimoja kikiondoka basi kingine hakina maisha.
Propaganda za kutenganisha elimu zimetumaliza ila sasa Alhamdulillah waislam wamefunguka na elimu zote zinasomwa kwa bidii. Propaganda nyingine inayotumaliza waislam ni hii ya kudanganywa kuwa kuchanganya dini na siasa ni dhambi na mwishowe tumetawaliwa kila nyanja.
Viongozi wetu mtakuwa mas'ul kwa kutupeleka ambako sio lengo,kwanza unganeni nasi waumini tutawafuata bila tabu. Viongozi ndio wanaoanzisha uhuishaji wa uislam na waumini tunafuata. Tukiamua kuanza kuwatenga wanaokwenda kinyume na uislam haraka sana tutafanikiwa kuinyoosha jamii yetu.
No comments:
Post a Comment