Wednesday, May 2, 2012

OIC yalaani kuchomwa moto Qur’ani huko Marekani

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali kitendo kiovu cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu katika jimbo la Florida huko Marekani.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu imesema kuwa dharau ya mtu anayejiita kasisi wa Kanisa la Dove World Outreach Center katika mji wa Gainsville jimboni Florida Marekan dhidi ya Qur'ani ni matokeo ya uhasama na chuki binafsi na ni kinyume na mwenendo wa watu waliostaarabika.
Taarifa ya OIC imesisitiza kuwa mhalifu huyo anapaswa kuchukuliwa hatua. Ihsanoglu amesema kuwa inatarajiwa kuwa viongozi wa dunia hususan huko Marekani watalaani kitendo hicho kiovu.
Kasisi Terry Jones wa Marekani Jumamosi iliyopita kwa mara nyingine alichoma moto nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani mbele ya Kanisa la Dove World Outreach Center katika mji wa Gainsville jimboni Florida akiwa pamoja na watu wengine karibu 20.
La kustaajabisha zaidi ni kuwa polisi wa mji wa Gainsville waliokuwa mahala hapo hawakuchukua hatua yoyote ya kuzuia uhalifu huo.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget