Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munnajid
Imetafsiriwa Na ‘Abdun-Naaswir Hikmany
Kuna zaidi ya maoni hamsini ya kiwanazuoni yenye maana ya Masiyh. Wanasema kwamba neno hili linatumika sehemu zote kwa Aliyemkweli [Masiyh wa Kweli, yaani (Yesu)] na mpotoshaji aliye muongo [dhidi ya ‘Kristo’ ama Dajjaal]. Masiyh ndiye Mkweli, ‘Iysaa bin Maryam (Yesu mwana wa Mariyamu), Masiyh wa uongofu, aliyewaponya wale waliozaliwa vipofu ama viguru, na kuwafanya wafu kuwa hai kwa uwezo wa Allaah.
Masiyh wa kuigiza (al-Masiyh ad-Dajjaal) ni muongo anayewaongoza watu kwenye uovu, Masiyh wa upotovu atawadanganya watu kwa namna alizojaaliwa, kama vile kuteremsha mvua, kuihuisha ardhi na kuifanya kuchipua mimea, na ‘miujiza’ mengineyo.
Kwa hivyo, Allaah Amewaumba Masiyh wawili, ambao mmoja wao ni tofauti kwa mwengine.
Wanazuoni wanasema kwamba sababu ya kwanini Dajjaal akaitwa Masiyh ni kwasababu moja kati ya macho yake ni mamsuuh (kimaana ni ‘lililo futika’; lililo tandazika au lililo kwaruzika, yaani atakuwa ni kipofu wa jicho moja ama halifanyi kazi). Au imesemwa kwamba ni kwasababu atakagua au kuzuru ardhi yote (yamsah) kwa siku arobaini... Maelezo ya awali ndio sahihi zaidi, kwasababu ya yale yaliyosemwa ndani ya Hadiyth iliyopokelewa na Muslim kutoka kwa Anas bin Maalik, aliyesema: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Dajjaal atakuwa kipofu (mamsuuh) katika jicho lake moja , na baina ya macho yake kutaandikwa ‘kaafir’...”
Neno Dajjaal limetolewa kutoka kwenye maneno “Dajjala al-ba’iir (amemtia alama ngamia)”, ikimaanisha pale wanapopaka kwa lami.
Mzizi wa [neno la Kiarabu la] dajala linamaanisha mchanganyo. Neno dajala linatumika kumaanisha kwa makusudi kuchanganya mambo na kuwa mbabaifu na mtatanishi. Dajjaal ni yule anayezungumza kwa ubabaifu, anayesema uongo mwingi na kuwadanganya watu wengi.
Neno “Dajjaal” limekuja kuwa ni sifa anayopewa muongo, mwenye jicho moja, Masiyh muongo. Dajjaal anaitwa hivyo kwasababu ataficha ukafiri wake mbele za watu kwa kuwaambia uongo, kuwachanganya na kuwababaisha.
Dajjaal atakuwa ni mtu miongoni mwa watoto wa kiume wa Aadam. Atakuwa na sifa nyingi ambazo zimeelezwa ndani ya Hadiyth nyingi kuwafafanulia watu kuhusiana naye na kuwaonya kuhusiana na uovu wake. Kwa hivyo pale anapokuja, Waumini wataweza kumtambua na hawatapotoshwa kutokana naye; watazitambua sifa zake ambazo Aliye Mkweli (Mtume - Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuelezea. Sifa hizi zitamtenganisha na watu wengine, ili kwamba hakuna mtu atakayelaghaiwa naye isipokuwa wale walio kuwa wajinga na uoni wao umeshaamuliwa (wapotofu). Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atujaalie kuwa salama na wenye upambanuzi.
Atakuwa ni mtu kijana mwenye ngozi ya wekundu, mfupi, nywele nyingi za mawimbi, uso mpana, na kifua kilichotanuka, kipofu au mlemavu (mamsuuh) wa jicho moja. Jicho halitanyanyuka wala kuzama, na litakaa kama ni zabibu inayoelea.
Jicho lake la kushoto litakuwa na kipande cha nyama chembamba kilichoota pembezoni mwa jicho lake. Kumeandikwa baina ya macho yake mawili “Kaaf, faa na raa’ (K-F-R)”, kwa herufi (za Kiarabu) zisizoshikana. Au “Kaafir”, kwa herufi zilizounganishwa. Zitasomeka kwa kila Muislamu, mwenye kujua ama asiyejua kusoma.
Sifa zake nyengine ni kwamba atakuwa tasa, hatozaa mtoto.
Kutoka kwa ‘AbduLlaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu), aliyesema: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Wakati nikiwa nimelala, nilijiona nikifanya tawaaf kuizunguka Ka’bah, ambapo nilimuona mtu anayengara akiwa na nywele ndefu, akiwa amesimama baina ya watu wawili, na maji yakidondoka kutoka kichwani mwake. Nikauliza, “Huyu ni nani?” Wakasema, “Mwana wa Maryam.” Baadaye nikageuka na kumuona mtu mwenye ngozi ya wekundu, mwili uliojaa, akiwa na nywele za mawimbi, kipofu kwenye jicho lake la kulia, na jicho lake likionekana kama zabibu inayoelea. Nikauliza, “Huyu ni nani?” Wakasema, “Huyu ni Dajjaal.” Mtu ambaye amefanana naye sana ni Ibnu Qatan.” (Imepokewa na Al-Bukhaariy; Ibn Qataan alikuwa ni mtu kutoka Banu Mustalaq kutoka Khuzaa’ah).
Pia imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amelitaja (jina la) Dajjaal kwa watu na kusema:
“Allaah Hana jicho moja, lakini Masiyh wa uongo (al-Masiyhud-Dajjaal) ni mwenye jicho moja (chongo), kipofu na mlemavu kwenye jicho lake la kulia, na jicho lake likionekana kama ni zabibu inayoogelea...” (Imepokewa na Al-Bukhaariy).
Kwenye Hadiyth refu iliyopokewa na an-Nawwaas bin Sam’aan (Radhiya Allaahu ‘anhu) inasema: “Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtaja Dajjaal (wakati wa) asubuhi moja. Mara nyengine akimuelezea kwamba ni mtu asiye muhimu na mara nyengine akimuelezea kwamba ni mtu aliye muhimu hadi kufikiria kwamba alikuwa kwenye sehemu ya shada la miti ya tende...” Moja kati ya sifa za Dajjaal alizozielezea zilikuwa:
“Atakuwa ni mtu kijana mwenye nywele zilizopindana pindana (pilipili), akiwa na jicho lenye kuogelea. Ni kana kwamba anaonekana kufanana na ‘Abdul-‘Uzza bin Qataan.” (Imepokewa na Muslim).
Imepokewa kutoka kwa ‘Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Nimekuelezeni mengi mno kuhusu Dajjaal na kwamba (bado) ninahofia hamutafahamu. Atakuwa ni mwenye jicho moja, jicho lake likiwa halijatokeza nje wala halijazama. Iwapo mutapata utata kuhusiana naye, basi kumbukeni kwamba Mola wenu sio mwenye jicho moja.” (Imepokewa na Abu Daawuud. Hadiyth hii ni sahihi – Swahiyhul-Jaami’ as-Swaghiyr).
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“... ama kwa Masiyh muongo, atakuwa ni mwenye jicho moja, akiwa na ubapa wa uso ulio mpana na mwenye kifua kipana, na atakuwa ni mwenye kibiongo...” (Imepokewa na Ahmad).
Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Dajjaal atakuwa ni mwenye jicho moja, kipofu na mlemavu kwenye jicho lake la kushoto, akiwa na nywele nyembamba. Atakuwa pamoja naye pepo na moto, lakini moto wake utakuwa ni pepo na pepo yake itakuwa ni moto.” (Imepokewa na Muslim).
Kwa mujibu wa Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu), Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Hakuna Mtume aliyeletwa isipokuwa aliwatahadharisha watu wake kuhusu (mtu) aliye na jicho moja (na aliye) muongo. Yeye ni mwenye jicho moja, lakini Mola wenu sio mwenye jicho moja, na baina ya macho yake kutaandikwa ‘Kaafir’” (Imepokewa na Al-Bukhaariy).
Kwa mujibu wa simulizi nyengine:
“Baina ya macho yake kumeandikwa ‘kaaf Faa Raa’.” (Muslim).
Kwa mujibu wa simulizi iliyopokewa na Hudhayfah:
“Haya yatasomeka na kila Muumini, aliyesoma ama asiyesoma (anaye/asiye jua kusoma na kuandika).” (Muslim).
“Hivyo tukakimbilia kuelekea katika nyumba ya mtawa, ambapo tulimuona mtu wa maajabu tusiyepata kumuona, akiwa amefungwa na minyororo tusiyopata kuiona.” (Imepokewa na Muslim).
“Tokea kipindi cha kuumbwa Aadam hadi Saa itakapoanza, hakutakuwa na uumbaji mkubwa kuliko wa Dajjaal.” (Imepokewa na Muslim).
Hivyo atakuwa ni mwenye ulemavu kwenye macho yake yote la kulia na jicho lake la kushoto; kila jicho litakuwa ni pofu, yaani, lisilofanya kazi, kwa sababu neno la Kiarabu lililotumika ndani ya Hadiyth,a’war, linatumika kuelezea chochote ambacho hakifanyi kazi na haswa linatumika kwa kuelezea macho yasiyofanya kazi. Jicho moja litakuwa halifanyi kazi na jicho jengine litakuwa ni lenye ulemavu (bovu).”
An-Nawawiy amekubaliana na mjumuisho huu ulioshauriwa na al-Qaadhi ‘Iyaad, na al-Qurtubiy pia amekubaliana nao.
Dajjaal atatokezea upande wa mashariki, sehemu za Khurasaan, kutoka miongoni mwa Mayahudi wa Kisfahani. Kisha atatembea sehemu mbali mbali duniani na hatoacha mji isipokuwa ameuingia, isipokuwa kwa Makkah na Madiynah, ambayo hatoweza kuingia kwa sababu Malaika wanailinda.
Kwa mujibu wa Hadiyth ya Faatwimah bint Qays (Radhiya Allaahu ‘anha), Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusiana na Dajjaal:
“Atatokezea upande wa bahari ya Syria au kutoka sehemu za bahari ya Yemen ... Hapana, inawezekana upande wa mashariki...” – na aliashiria pande za mashariki. (Imepokewa na Muslim).
“Dajjaal atatokezea kutoka ardhi ya upande wa mashariki inayoitwa Khurasaan.” (Imepokewa na at-Tirmidhiy. Ameisahihisha al-Albaaniy, Swahiyh al-Jaami’ as-Swaghiyr).
Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Dajjaal atatokezea kutoka miongoni mwa Mayahudi wa Kisfahani, na pamoja naye watakuwepo Mayahudi sabini elfu, wakiwa wamevalia mataji.” (Imepokewa na Ahmad).
Amezuiliwa Dajjaal kuingia Makkah au Madiynah pale atakapotokezea mwishoni mwa Saa (uhai wa dunia), kwa sababu Hadiyth zilizo sahihi zimepokewa kwa uthibitisho huo. Kwa namna zilivyo sehemu nyenginezo, ataziingia moja baada ya nyengine.
Katika Hadiyth ya Faatwimah bint Qays (Radhiya Allaahu ‘anha), amesema:
“[Atasema Dajjaal:], ‘Ni karibuni nitaruhusiwa kutokezea. Kisha nitatokezea na kutembea pembe za dunia kwa siku arobaini, na sitoacha mji wowote bila ya kuuingia, isipokuwa kwa Makkah na Madiynah, ambayo nitazuilika kuiingia kwa sababu kila nikijaribu kuingia, kutakuwepo Malaika aliye na panga lisilo na ala (lililo wazi) mkononi, akinizuia kuingia. Kwenye kila mlango kutakuwa na malaika wakiihami.’”(Imepokewa na Muslim)
“Nilikuja kwa mtu kutoka miongoni mwa Maswahaabah wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: ‘Nielezee Hadiyth ambayo umeisikia kutoka kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Dajjaal.’ Aliitaja Hadiyth hiyo, na kusema: ‘Atakaa miongoni mwenu kwa siku arobaini, ambazo ndani yake atakwenda katika kila pembe (ya dunia) isipokuwa kwa Misikiti minne: Masjidul-Haraam (Makkah), Msikiti wa Madiynah, (Msikiti wa) Sinai na Masjidul-Aqsaa.’”
Wengi miongoni mwa wafuasi wa Dajjaal watakuwa wanatoka miongoni mwa Mayahudi, Wafursi na Waturuki, na mchanganyiko wa watu wengine, zaidi ni Mabedui na wanawake.
“Wafuasi wa Dajjaal kutoka miongoni mwa Mayahudi wa Kisfahani watafikia idadi ya sabini elfu, wakivaa maguo mazito na zenye mistari.” Kwa mujibu wa simulizi iliyopokewa na Imaam Ahmad:“Mayahudi sabini elfu, wakiwa wamevalia mataji.”
“Dajjaal atakuja kwenye ziwa hili la Marriqanaat – bonde lililopo Madiynah – na wengi wao watakaotoka pamoja naye watakuwa ni wanawake, hadi itafikia mtu kumuendea mama mkwe wake, mama yake, binti yake, dada yake na shangazi yake, na kuwafunga pamoja (mfano kamba) barabara kwa kuhofia kwamba watatoka pamoja naye.” (Imesimuliwa na Ahmad).
Fitnah za Dajjaal zitakuwa ni za daraja ya juu tangu kuumbwa kwa Nabii Aadam ('Alayhis Salaam) hadi Saa itakapoanza. Hii ni kwa sababu ya miujiza mitukufu ambayo Allaah Atamuumba pamoja naye, ambayo itazifanya akili za watu kupigwa na butwaa na kuishangaa.
“Dajjaal atakuwa na jicho moja, pofu kwa upande wake wa kushoto, na atakuwa na nywele nyembamba. Atakuwa na pepo na moto pamoja naye, lakini pepo yake itakuwa ni moto na moto wake utakuwa ni pepo.” (Imepokewa na Muslim).
“Ninajuwa ni kipi ambacho Dajjaal atakuja nacho pamoja naye: atakuwa na mito miwili yenye kututurika (maji). Mmoja utaonekana kwa uwazi kama ni maji na mwengine utaonekana wazi kama ni moto uwakao. Iwapo yeyote kati yenu atayaona hayo, basi na achague mto wenye kuonekana kama ni moto, kisha mwaachie afumbe macho yake na ainamishe kichwa chake na anywe kutoka humo, kwani utakuwa ni (wenye) maji baridi.” (Imepokewa na Muslim).
“Sehemu ya fitnah yake ni kwamba atamwambia Bedui: ‘Je unafikiri kwamba iwapo nitamfufua baba na mama yako kwa ajili yako utanishuhudia kwamba mimi ni mola wako?’ Atasema: ‘Ndio.’ Hivyo majini mawili yatajitokeza kwake katika sura ya baba na mama yake, yakisema: ‘Ewe mwanangu, mfuate kwani yeye ndiye mola wako.” (Imepokewa na Ibn Maajah. Imethibitishwa usahihi wake na Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyhul al-Jaami’ as-Swaghiyr).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameufunza Ummah wake kuhusiana na yale ambayo yatawakinga dhidi ya fitnah za Masiyh wa uongo (al-Masiyhud-Dajjaal). Ameuacha Ummah wake kwenye njia ambayo ipo wazi, na hakuna anayepotea nayo isipokuwa kwa yule aliyeangamia. Hakuacha kitu chochote kizuri bila ya kukitaja kwa Ummah wake, au ovu lolote bila ya kuwatahadharisha dhidi yake. Miongoni mwa vitu alivyotutahadharisha dhidi yake ni fitnah ya Dajjaal, kwa sababu ya fitnah yake kubwa ambayo Ummah utakutana nayo hadi Saa itakapofika. Kila Mtume aliutahadharisha Ummah wake dhidi ya Dajjaal mwenye jicho moja, lakini Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni Mtume pekee aliyeutahadharisha Ummah wake zaidi kuhusiana naye. Allaah Alimfahamisha (Mtume) sifa nyingi za Dajjaal ili apate kuwatahadharisha Ummah wake. Hakuna shaka yoyote Dajjaal atatokezea ndani ya Ummah huu, kwa sababu huu ndio Ummah wa mwisho, na Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiye hitimisho la Mitume.
Zinafuatia Baadhi Ya Miongozo Ambayo Mtume Mteuzi (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Alizifafanua Kwa Ummah Wake Ili Kwamba Ujiepushe Dhidi Ya Fitnah Hii Kuu, Ambayo Tunamuomba Allaah Atukinge Na Atupatie Hifadhi:
(i) Kushikamana na Uislamu, kuwa na imani thabiti na kujifunza Majina na Sifa Nzuri zilizo Bora za Allaah Ambazo hazipatikani kwa mwengine yeyote. Mtu atambue kwamba Dajjaal atakuwa ni binaadamu aliye hai mwenye kula na kunywa, na kwamba Allaah Yupo mbali kabisa na hilo; Dajjaal atakuwa na jicho moja lakini Allaah Hana jicho moja; hakuna yeyote atakayemuona Mola wake hapa duniani hadi afariki, lakini Dajjaal atakapotokezea ataonekana na watu wote, Waumini na vivyo hivyo makafiri.
“ALlaahumma inni a‘uudhubika min ‘adhaabil-qabri, wa a‘uudhubika min fitnatil-Masiyhid-Dajjaal, wa a‘uudhubika min fitnatil-mahyaa wa fitnatil-mamaat. ALlaahumma inni a‘uudhubika minal-ma’tham wa ‘alal-maghram.
(Ee Allaah, najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda Kwako kutokana na fitnah ya Dajjaal, na najilinda kwako kutokana na mitihani ya uhai na kifo. Ee Allaah, najilinda Kwako kutokana na dhambi na deni).” (Imepokewa na Al-Bukhaariy).
“Pindipo mmoja wenu anaposoma Tashahhud, basi na aombe hifadhi ya Allaah kwenye mambo manne, na aseme: “ALlaahumma inni a‘uudhubika min ‘adhaabi Jahannam wa min ‘adhaabil-qabri wa min finatil-mahyaa wal-mamaat wa min sharri fitnatil-Masiyhid-Dajjaal
(Ee Allaah, najilinda Kwako kutokana na adhabu ya Moto, kutokana na adhabu ya kaburi, kutokana na mitihani ya uhai na kifo, na kutokana na uovu wa fitnah ya Dajjaal).” (Imepokewa na Muslim).
“Yeyote miongoni mwenu anayemuona (Dajjaal), basi na asome Aayah za mwanzo za Suuratul-Kahf.”.
“Yeyote anayehifadhi aayah kumi za mwanzo za Suuratul-Kahf atakingwa kutokana na Dajjaal” – yaani kutokana na fitnah zake. Muslim amesema: “Shu’bah amesema: ‘kutoka mwisho wa al-Kahf.’ Hammaam amesema: ‘kutoka mwanzoni mwa al-Kahf.’”
An-Nawawiy amesema: “Hoja ya hili ni kwa sababu mwanzoni (mwa Suurah hii), kumetajwa maajabu na alama, na yeyote anayezikubali, hatahadaiwa na fitnah za Dajjaal. Na mwishoni mwa Suurah, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema (maana ya maneno): {{Je, wanadhani waliokufuru ndio wawafanye waja wangu ndio walinzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo mahala pa kuteremkia makafiri.}} [Suuratul-Kahf 18:102].” (Sharh Swahiyh Muslim, 6/93).
“Yeyote anayeisoma Suuratul-Kahf siku ya Ijumaa, itakuwa ni mwangaza kwake kutoka Ijumaa moja hadi nyengine.” (Al-Mustadrak, 2/368. Imesahihishwa na al-Albaaniy kwenye Swahiyhul-Jaami’ as-Swaghiyr).
Kila Muislamu atie himma ya kuisoma Suurah hii, na kuihifadhi na kuikariri kuisoma, haswa siku bora ambayo jua linachomoza (Magharibi), nayo ni Ijumaa.
“Yeyote anayemsikia Dajjaal, basi na ajiweke mbali naye, kwani (itafikia) mtu atamjia (Dajjaal) na kudhani kwamba yeye (Dajaal) anasema ukweli kwa sababu ya maajabu yaliyofikishwa kwake.”
Dajjaal atafariki mikononi mwa Masiyh ‘Iysaa bin Maryam ('Alayhis Salaam), kama ilivyooneshwa ndani ya Hadiyth Swahiyh. Dajjaal atatokezea ardhini na atawakumba wafuasi wengi, akisambaza fitnah zake kwa mapana na marefu. Hakuna mtu atakayekimbia fitnah yake isipokuwa wachache miongoni mwa Waumimi. Kwa hatua hiyo, ‘Iysaa bin Maryam ('Alayhis Salaam) atashuka katika mashariki ya mnara wa Damascus , na waja Waumini wa Allaah watamzungukia. Atawaongoza kwa Dajjaal, (Dajjaal) ambaye wakati anaposhuka ‘Iysaa ('Alayhis Salaam) atakuwa anaelekea Baytul-Maqdis (Jerusalem ). ‘Iysaa ('Alayhis Salaam) atakutakana naye katika lango la Ludd (Lod), sehemu iliyomo ndani ya Palestine karibu na Baytul-Maqdis. Pale Dajjaal atakapomuona, ataanza kuyayuka kama vile chumvi inavyoyayuka ndani ya maji. Lakini ‘Iysaa ('Alayhis Salaam) atasema kumwambia: “Nina kazi na wewe, hutonikimbia.” Kisha atapambana naye na kumuua kwa ala yake. Wafuasi wake (Dajjaal) watakimbia, (hata hivyo) watakimbizwa na Waislamu, ambao watawaua, na miti na mawe yatasema, ‘Ewe Muislamu, Ewe mja wa Allaah, kuna Yahudi nyuma yangu – njoo na umuue!’ – (wataweza kujificha) mbali ya (mti wa) gharqad (miashoka), kwani ni mmoja kati ya miti ya Mayahudi.
Zinafuatia Baadhi Ya Hadiyth Zilizopokewa Kuhusu Kifo Cha Dajjaal Na Wafuasi Wake:
Muslim amepokea kwamba ‘AbduLlaah bin ‘Amr (Radhiya Allaahu ‘anhuma) amesema: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Dajjaal atatokezea miongoni mwa Ummah wangu na atakaa kwa siku arobaini... Kisha Allaah Atamleta ‘Iysaa bin Maryam, anayeonekana kama ‘Urwah bin Mas’uud, na atapambana naye na kumuua.”
“Mwana wa Maryam atamuua Dajjaal langoni mwa Ludd.”
“... Kila kaafir atakayenusa harufu ya (‘Iysaa ['Alayhis Salaam]) atakufa, na harufu yake itasambaa umbali wa namna atakavyoweza kuona. Kisha atamtafuta (Dajjaal) hadi atamkuta kwenye lango la Ludd, ambapo atamuua.”
“Dajjaal atatokezea enzi ambazo utiifu wa Diyn ni wa chini na elimu imepungua... Kisha ‘Iysaa bin Maryam atashuka kabla ya mawio na kuwaita watu, akisema: “Enyi watu, ni kipi kinachowazuia kutoka na kupambana dhidi ya muovu huyu muongo?” Watasema, ‘Mtu huyu ni jini’, kisha wataondoka. Pale watakapokutana na ‘Iysaa bin Maryam, muda wa Swalaah ukawadia na iqaamah ikakimiwa, na itasemwa kwake: ‘Nenda mbele (kuongoza Swalaah) Ewe Roho ya Allaah.’ Atasema:“Muacheni Imaam wenu aende mbele na kuwaongozeni katika Swalaah.” Watakapomaliza kuswali alfajiri, watatoka kwenda kukutana naye (Dajjaal) na watamuona muongo (mkubwa), ataanza kuyeyuka kama chumvi ndani ya maji. ‘Iysaa atapambana naye na kumuua. Hadi miti na mawe yataita: ‘Ewe Roho ya Allaah, hapa kuna Yahudi!’ Na hakuna yeyote mwenye kumfuata yeye (Dajjaal) atakayebaki, wote watauliwa.”
No comments:
Post a Comment