“Ushahidi” wa Uungu wa Yesu
Kuna baadhi ya
mistari iliyotafsiriwa na makanisa ya Kikatoliki pamoja na Kiprotestanti kuwa
ndio ushahidi wa uungu wa Yesu Kristo. Hata hivyo, kwa uchunguzi wa kina kuhusu
mistari hiyo, imekuwa ni dhahiri kuwa, ama maneno yake ni tata, yanayoacha tafsiri
nyingi tofauti tofauti, au imeongezwa na haikuwepo katika miswada ya mwanzo ya
mapokeo ya Biblia. Ifuatayo ni baadhi ya mistari hiyo iliyotajwa sana :
1.
Mwanzo na Mwisho
Katika kitabu
cha Ufunuo 1:8, inadokezwa kuwa Yesu amesema yafuatayo kujihusu yeye mwenyewe: “Mimi
ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako
na atakayekuja, Mwenyezi”. Hizi ni sifa za Mungu. Kwa hiyo, hapa Yesu, kwa
mujibu wa Wakristo wa mwanzo, anadai uungu. Hata hivyo, hayo maneno yalitajwa
hapo juu ni kwa mujibu wa toleo la King
James Version. Ama katika toleo la Revised Standard
Version, wasomi wa Biblia wanarekebisha makosa ya kitafsiri na wameandika: “Mimi
ni wa mwanzo na wa Mwishom” asema Bwana Mungu,..”. Pia, marekebisho yalifanywa katika toleo la
New American Bible iliyotayarishwa
na Wakatoliki. Tafsri ya aya hiyo imerekebishwa ili iwekwe katika muktadha wake
ulio sahihi kama ifuatavyo: “Bwana Mungu
anasema: “Mimi ni wa mwanzo na wa Mwishom…” Ikiwa na marekebisho
haya, inadhihirika kuwa, mstari huu ulikuwa ni maelezo ya Mungu na sio maelezo
ya Mtume Yesu.
2.
Maisha ya kabla ya Kristo
Mstari
mwingine unaotumiwa sana
ili kuunga mkono uungu wa Yesu ni Yohana 8:58: “Yesu akawaambia, amin, amin,
nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.” Mstari huu
umechukuliwa na kuashiria kuwa Yesu alikuwepo kabla ya kudhihiri kwake duniani.
Uamuzi uliofikiwa kutokana na mstari huo ni kuwa Yesu lazima awe Mungu, kwa
kuwa kuwepo kwake kumetangulia tarehe ya kuzaliwa kwake duniani. Hata hivyo,
dhana ya kuwepo kabla ya kudhihiri kwa mitume, na kwa watu wengine, ipo katila vitabu
vyote viwili, Agano la Kale ,
vilevile katika Quran. Yeremia anajielezea mwenyewe katika Kitabu Cha Yeremia
1:4-5 kama ifuatavyo:
“Neno la
BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla
hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”
Nabii
Suleimani anaripotiwa katika Mithali 8:23-27, ya kuwa amesema, “Nalitukuka
tokea milele, tangu awali, kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwako
vilindi nalizaliwa, Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji. Kabla milima
haijawekwa imara, Kabla ya vilima nalizaliwa. Alipokuwa hajaiumba dunia,
wala makonde, Wala chanzo cha mavumbi ya dunia; Alipozithibitisha mbingu
nalikuwako…"
Kwa mujibu wa Ayubu
38:4 na 21, Mungu amemtambulisha Nabii Ayubu kama
ifuatavyo: “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa unafahamu.”
Katika Quran,
Sura ya Al-A’aaraf, 7:172, Mungu
anaeleza kuwa mwanadamu alikuwepo kiroho kabla ya kuumbwa ulimwengu wa kimwili.
"وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ
وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنفُسِهِمْ أَلَسْتَ بِرَبِّكُمْ قَالُواْ بَلَى شَهِدْنَا
أَن تَقُولُواْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ."
"Na pale Mola wako Mlezi alipowaleta
katika wanaadamu kutoka migongoni mwa kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya
nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani!
Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na
hayo." Al-A’aaraf, 7:172
Kwa hiyo,
maelezo ya Mtume Yesu, “Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko”. Hayawezi
kutumiwa kuwa ni ushahidi wa uungu wake. Katika muktadha wa Yohana 8:54, Yesu
amedaiwa kuwa ametamka kuhusu ujuzi wa Mungu kwa Mitume yake, ambayo inatangulia
tarehe ya kuumbwa kwao katika ulimwengu huu.
3.
Mwana wa Mungu
Ushahidi
mwingine uliotumiwa kwa ajili ya uungu wa Yesu ni kule kutumiwa sifa ya “Mwana wa Mungu” kwa Yesu.
Hata hivyo, kuna sehemu nyingi katika Agano la Kale ilipotumiwa sifa hiyo kwa watu wengine.
Mungu alimwita
Israeli (Nabii Yakubu) “Mwanawe” pale alipomuelekeza Mtume Musa aende kwa
Firauni katika Kutoka 4:22-23, “Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli
ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; nami nimekuambia, Mpe mwanangu
ruhusa aende, ili apate kunitumikia…”[1]
Katika 2
Samweli 7:13-14, Mungu anamwita Nabii Suleimani Mwanawe, "Yeye ndiye
atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake
nitakifanya imara milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu…"
Mungu
alimuahidi Nabii Daudi kumfanya mwanawe katika Zaburi 89:26-27: “Yeye ataniita,
Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Nami nitamjalia kuwa
mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana
kuliko wafalme wa dunia.”[2]
Malaika
wanachukuliwa kuwa ni “wana wa Mungu” katika kitabu cha Ayubu 1:6, “Ilikuwa,
siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za
BWANA, Shetani naye akaenda kati yao ”.[3]
Katika Agano
Jipya, kuna marejeo mengi ya “mwana wa Mungu” ya watu wengine wasio Yesu. Kwa
mfano, pale mtunzi wa Injili kwa mujibu wa Luka amewaorodhesha wahenga wake
hadi kwa Adamu, ameandika: Luka 3:38 “Wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa
Mungu”.[4]
Baadhi ya watu
wanadai kuwa kile cha kipekee kilichopo kwa Yesu ni kuwa yeye ndiye mwana wa
pekee wa kuzaliwa[5] Mwana
wa Mungu, huku hao wengine ni “wana wa Mungu tu.” Hata hivyo, Mungu
ananukuliwa akimwambia Mtume Daudi, katika Zaburi 2:7, “Nitaihubiri amri,
BWANA aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.”
Pia inapaswa ijulikane
kuwa hakuna hata sehemu moja katika Injili ambapo Yesu alijiita yeye mwenyewe
kuwa yeye hasa ndiye “mwana wa Mungu”.[6]
Badala yake, amenukuliwa kuwa amekariri kujiita “Mwana wa Adamu” (mfano Luka
9:22) kwa mara zisizohesabika. Na katika Luka 4:41, kwa hakika amekataa kuitwa
“Mwana wa Mungu”: “Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema,
Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa
ndiye Kristo.”
Kwa kuwa Wayahudi
wanaamini kuwa Mungu ni Mmoja, na hana mke wala mtoto kwa maana halisi yoyote
ile, ni wazi kuwa ibara “mwana wa Mungu” kwa Wayahudi ina maana ya “Mtumishi wa
Mungu tu” yaani mtu aliye karibu na Mungu, kwa sababu ya huduma yake ya
kiimani, akiwa kama mtoto kwa baba yake. Wakristo waliokuja kutoka katika
historia za kuwa walikuwa ni Wagiriki au Warumi, baadaye waliitumia vibaya
istilahi hiyo. Kwani katika urithi wao, “mwana wa Mungu” inamaanisha mungu ana
mwili au mtu aliyezaliwa kwa muungano wa kimwili kati ya mungu mwanamume na
mwanamke.[7] Wakati
Kanisa lilipoacha msingi wa Kiyahudi, lilitwaa dhana ya kipagani ya “mwana wa
Mungu”, ambayo kwa ukamilifu, ilikuwa ni tofauti na matumizi ya Kiyahudi.[8]
Kwa hiyo,
matumizi ya istilahi “mwana wa Mungu” inafaa ifahamike kuwa ni alama ya ufahamu
ya kisemintiki yenye maana “mtumishi wa Mungu”, na sio katika ufahamu wa
kipagani wa uhalisi wa kuwa kinda la Mungu. Katika Injili nne, Yesu anarekodiwa
akisema: “Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.” Mathayo
5:9.[9]
Vivo hivyo,
matumizi ya Yesu ya istilahi abba, “baba mpendwa” lazima ifahamike hivyo
hivyo. Kuna ubishani miongoni mwa wasomi wa Agano Jipya juu ya nini maana ya abba
kwa uhakika kabisa katika zama za Yesu na Wayahudi wa makundi mengine wa muongo
huo huo walilitumia kwa upana gani.
Hivi karibuni
kwa ukali kabisa, James Barr amedai kuwa hilo
halikuonyesha wazi wazi ufahamu wa kuwa hilo
lilikuwa linamuhusu yeye ila hilo
kiwepesi kabisa linaashiria “baba” tu.[10] Ili kufikiria kuwa Mungu ni “Baba yetu wa mbinguni” haina
maana mpya, kwa kuwa katika sala ya bwana amenukuliwa kuwa amewafundisha
wanafunzi wake kumtambulisha Mungu katika njia hii hii.
4.
Pamoja na Mungu
Wale wanaodai
kuwa Yesu alikuwa Mungu, wanashikilia kuwa yeye hakuwa Mungu
aliyetengeka, bali ni mmoja na ni Mungu yule yule mwenye mwili. Wao wanaunga
mkono imani hii kutokana na mstari wa 30 wa Injili kwa mujibu wa Yohana, sura
10, ambayo ndani yake Yesu anaripotiwa kuwa amesema, “Mimi na Baba ni kitu
kimoja.” Nje ya muktadha, mstari huu unaashiria uungu wa Yesu. Hata hivyo,
pale Wayahudi walipomtuhumu kwa kudai uungu, kwa kutegemea sentesi hiyo, Yohana
10:34 “Yesu akawajibu, Je, haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, Mimi
nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la
Mungu;"[11] Amewabainishia,
kwa mfano wa maandiko unaojulikana sana
kwao, kuwa yeye alikuwa anatumia lugha ya kistiari ya manabii ambayo haipaswi
kufasiriwa kwa kujipachika uungu yeye mwenyewe au kwa mtu mwingine yoyote.
Ushahidi zaidi
unachukuliwa kutoka katika mstari wa kumi na wa kumi na moja wa Injili kwa
mujibu wa Yohana, sura ya 14, pale watu walipomtaka Yesu awaonyeshe Baba, naye
inaaminiwa alisema: "Husadiki ya kwambi mimi ni ndani ya Baba, na
Baba yu ndani yangu; Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri
langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwambi mimi
ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa
sababu ya kazi zenyewe.”
Ibara hizi
zingeashiria uungu wa Yesu, kama sehemu
iliyobakia ya Injili hiyo hiyo inapuuzwa. Hata hivyo, aya tisa baadaye, katika
Yohana 14:20, pia Yesu anarekodiwa akiwaambia wanafunzi wake, "Siku ile
mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami
ndani yenu.” Kwa hiyo, kama maelezo ya
Yesu "Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; yanamaanisha
kuwa yeye ni Mungu, basi vivyo hivyo iwe kwa wanafunzi wa Yesu. Hii sentensi ya
kiishara inamaanisha umoja wa lengo na sio umoja wa asili. Tafsiri ya kiishara
inasisitizwa zaidi katika Yohana 17:20-21, pale Yesu aliposema, "Wala
si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote
wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao
wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe
uliyenituma.”[12]
5.
Amekubali kusujudiwa
Inadaiwa kuwa Yesu
tangu aliporipotiwa kuwa amekubali kusujudiwa na baadhi ya wafuasi zake, lazima
atakuwa ni Mungu. Hata hivyo, uchunguzi makini kuhusu andiko hilo unaashiria mambo mawili; tafsiri
wasiwasi, na tafsiri potofu. Istilahi “kusujudu” inaweza kupatikana katika King
Jemes Version na The Revised Standard Version yakielezea watu watatu
wenye busara waliokuja kutokea mashariki. Wameripotiwa katika Mathayo 2:2,
wakisema, "Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana
tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.”[13]
Hata hivyo, katika Biblia ya The New American Bible (Catholic Press,
1970), hilo
andiko linasomeka: "Yu wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa sasa?
Tumeona nyota yake ikichomoza na tumekuja kutoa heshima kwake.”
Katika The
Revised Standard Version, Yohana 9:37-38, "Yesu akawaambia, Umemwona, naye
anayesema nawe ndiye. Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia. [14]
Hata hivyo, katika The American Biblke, wafasiri wasomi wameongeza
tanbibihi inayosomeka: 9:38. Mstari huu, imefutwa kwa umuhimu wa MSS [miswada],
unaweza kuwa ni nyongeza kwa liturujia ya ubatizo.
Mistari hii
haipatikani katika miswada muhimu ya kale yenye Injili hii. Huenda ni nyongeza
ya baadaye iliyowekwa na waandishi wa kanisa ili yatumike katika huduma ya
ubatizo. Zaidi, kama alivyofafanua, mwenye
mamlaka makuu na adhima katika Biblia na lugha zake za asili, George M. Lamsa, “Neno
la Kiarama
sagad, sujudu, pia lina maana ya kuinama au kupiga goti kwa watu wa mashariki
wakati wa kusalimiana kwa kawaida ya kuinamisha kichwa au kuinama chini.[15]
“Alimsujudia” haiashirii kuwa yeye
alimwabudu Yesu kama vile mtu alivyomwabudu
Mungu. Tendo kama hilo
lilitakiwa lichukuliwe ni la kukufuru na la uvunjaji wa Amri ya kwanza mbele ya
macho ya Wayahudi, na huyo mtu angepigwa mawe. Lakini yeye alipiga magoti mbele
yake kwa kutoa heshima na shukurani.”[16]
Kitabu cha
mwisho, Quran, kinaeleza tukio la kuabudiwa au kutoabudiwa kwa Yesu, kwa
kunukuu mazungumzo yatakayotokea baina ya Yesu na Mungu siku ya Kiama. Allah
anaeleza katika Sura Al-Maa`idah, 5:116-117
"وَإِذْ قَالَ اللّهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ
قُلتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـهَيْنِ مِن دُونِ اللّهِ...، مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلاَّ مَا أَمَرْتَنِي بِهِ
أَنِ اعْبُدُواْ اللّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ..."
"Na
pale Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu:
Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu?..., (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika!
Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu…, Sikuwaambia lolote ila uliyoniamrisha,
nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi…"
Al-Maa`idah, 5:116-117
6.
"Hapo mwanzo kulikuwa na Neno"
Huenda
‘ushahidi’ wa uungu wa Yesu ulionukuliwa sana
ni Yohana 1:1 na 14, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa
Mungu, na Neno alikuwa Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi
tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana
pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” Hata hivyo, maelezo haya
hayakutolewa na Yesu Kristo, wala hayakuhusishwa naye na mtunzi wa Injili kwa
mujibu wa Yohana. Hivyo, mistari hii haiundi ushahidi wa uungu wa Yesu, hasa
hasa kuzingatia shaka inayoshikiliwa na wasomi wa Kikristo juu ya Injili ya
Nne. Wasomi wa Biblia waliotunga Injili tano: “Picha mbili zilizochorwa na
Yohana na muhtasari wa injili (yaani Injili ya Mathayo, Marko na Luka) zote
mbili haziwezi kuwa ubainifu wa kihistoria.[17] Neno
lilohusishwa na Yesu katika Injili ya Nne limeundwa na wainjilisti kwa sehemu
kubwa, na linaakisi mwendelezo wa lugha ya jamii ya Wakristo wa Kiyohana.[18]
Neno la Kigiriki
lilotumiwa na mtunzi wa Injili ya Nne asiyejulikana kwa “neno” ni logos.[19] Kwa
kufanya hivyo, huyo mtunzi anamtambulisha Yesu kwa logos la wanafalsa wapagani
wa Kigiriki, neno ambalo lilikuwa na lengo takatifu na thabiti lililojitokeza
ulimwenguni, huyo mtunzi akalipangilia neno hilo na kulipa mfumo na maana.[20]
Wazo la logos
katika fikra za Kigiriki huenda linarejea nyuma, kwa uchache hadi kwa
mwanafalsafa wa karne ya sita BC, Heracleitus, aliyependekeza kuwa, kulikuwa na
logos ulimwenguni anayetenda kwa mwanadamu kulingana na nguvu ya hoja. Baadaye,
Stoics[21]
analitambulisha logos kuwa ni tendo, mantiki, na kanuni ya kiroho inayosambaa
katika ukweli wote.[22] Mwanafalsafa
wa Kiyahudi anayeongea Kigiriki, Judaeus Philo wa Alexandria (15 BC -45 CE),
amefundisha kuwa logos alikuwa ni mpatanishi baina ya Mungu na ulimwengu, kwa
kuwa na sifa mbili za uwakala wa Mungu na ulimwengu, na kuwa na sifa mbili za uwakala wa viumbe na
wakala wa ambaye kupitia kwake akili ya mwanadamu inaweza kumfahamu Mungu.[23]
Maandiko ya Philo yalihifadhiwa na kutunzwa na kanisa, na kueneza ufunuo kwa
mafundisho ya kistaarabu ya tiolojia ya kifalsafa ya Kikristo. Aliacha
mafundisho ya fikra za Kipilato wakichukulia logos (Neno) na kuliita
“mtoto wa kwanza wa kuzaliwa na Mungu.”[24]
Utambulisho wa
Yesu kwa logos, uliendelezwa katika kanisa la kwanza ikiwa ni tokeo la
majaribio yaliyofanywa na wanatiolojia wa kwanza wa Kikristo pamoja na watetezi
kuielezea imani ya Kikristo kwa istilahi ambayo ingekuwa wazi kwa ulimwengu wa
Wayunani. Zaidi ya hayo, ilikuwa ni kuwavutia wasikilizaji wao na mtazamo wao
kuwa Ukristo ulikuwa unashinda, au mrithi wa wale wote waliokuwa wanafalsafa
bora wa kipagani. Kwa hiyo, katika kazi zao za utetezi na ubishani, Mapadri wa
Kikristo wa kwanza wameeleza kuwa Yesu alikuwa ni logos aliyekuwepo hapo
kabla.[25]
Neno la Kigiriki lililotumika kwa
maana ya ‘Mungu’ katika hiyo ibara ni “na Neno lilikuwa kwa Mungu,” lipo
katika mtindo wa “definite form- yaani mtindo uliowazi, au unaofahamika”
batheos, Linalomaanisha “Huyo Mungu, au Mungu maalum”. Hata hivyo,
katika ibara ya pili “na Neno alikuwa Mungu”, neno la Kigiriki lililotumika kwa
maana ya ‘Mungu’ katika ibara lipo katika mtindo wa “indefinite form-
yaani mtindo usiowazi, au usiofahamika” tontheos, Linalomaanisha
‘mungu yoyote, yaani mungu asiyejulikana, au mungu yoyote asiye maalumu’.[26] Kwa
hiyo, Yohana 1:1, kwa uwazi zaidi ilipaswa itafsiriwe, “Hapo Mwanzo kulikuwa
na Neno, na hilo Neno lilikuwa kwa Mungu, na hilo Neno lilikuwa mungu
mwingine.” Kwa hiyo, kama hilo
neno lilikuwa mungu mwingine kwa ufahamu wa kifasihi, itamaanisha kuwa kulikuwa
na miungu miwili na sio mmoja. Hata hivyo, katika lugha ya Kibiblia, neno
‘mungu – asiyefahamika’ linatumika kwa maana ya istiari ili kuashiria nguvu.
Kwa mfano, Paulo alimtaja shetani kuwa ni ‘mungu – asiyefahamika’ katika 2
Wakorintho 4:4, "ambao ndani yao
mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya
injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu." Pia, Musa
alitajwa kama ni ‘mungu – asiyefahamika’
katika Kutoka 7:1, "BWANA akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe
kuwa Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruna atakuwa nabii wako.[27]
Mawazo
ya kale
Kulikuwa na
mgogoro mkubwa kati ya tafsiri ya Pauline na ya Jerusalem kuhusu Yesu na ujumbe wake. Mgogoro
huo, baada ya kutokea pole pole kwa miaka mingi, hatimaye ulipelekea mpasuko
kabisa, katika mpasuko huo, ulipelekea kuundwa Kanisa la Wakristo wa Pauline, kwa
athari hiyo, dini mpya iliyojitenga kutoka Uyahudi. Kwa upande mwingine, Wanazareti
wa Jerusalem
hawakukata uhusiano wao na Uyahudi, bali walijizingatia kuwa wao ndio kiini cha
kuutekeleza Uyahudi, watiifu wa Torati, pia walimwamini Yesu, umbo la Masihi mwanadamu.[28]
Wakati uasi wa
Kiyahudi ulipopondwa pondwa na Warumi na mahekalu yao kuharibiwa mwaka 70 CE,
Wakristo wa Kiyahudi walitawanyika, nguvu yao na mvuto wao wa kuwa wao ndio
Kanisa Mama na kituo cha vuguvugu la Yesu zilifikia kikomo.[29]
Vuguvugu la Wakristo
wa Kipauline, vuguvugu ambalo mpaka mwaka 66 CE. Lilikuwa linapigania liendelee
kuishi, dhidi ya kutokubaliwa huko Jerusalem ,
sasa lilianza kusonga mbele.
Kanisa la Jerusalem ,
chini ya uongozi wa James, kiasili lilijulikana kuwa ni la Wanazareti, baadaye
likajulikana kwa jina la kupanga na la kuaibisha la Ebionites (Kwa kiyahudi evyonium,
“watu maskini”), jina ambalo baadhi ya Wanazareti walilitwaa kwa ufahari
wakilichukulia kuwa ni kikumbusho cha maneno ya Yesu yasemayo, “Wabarikiwe
maskini.” Baada ya Kanisa la
Graeco-Roman kushika hatamu, Wanazareti wakawa wanadharauliwa
na kuonwa kuwa ni waasi, kwa sababu ya kukataa kwao mafundisho ya Paulo.[30]
Kwa mujibu wa
historia ya kanisa la wahenga, Irenaeus (c. 185 CE,) hao watu maskini
walimwamini Mungu mmoja, Muumba, aliyefundisha kuwa Yesu alikuwa ni masihi, kwa
mujibu wa Mathayo, walitumia Injili tu, na kumpinga Paulo kwa kumwona kuwa ni
muasi aliyeasi Sheria ya Kiyahudi.[31]
Hao watu
maskini walijulikana kuwa waliishi mpaka katika karne ya nne. Baadhi yao walihama Palestina na wakaishi huko Transjordan na Syria na baadaye sehemu hiyo ikajulikana kuwa ni
Asia ndogo, Misri na Roma [32].
Kwa mfumo wa
kifalme,[33] vuguvugu
la Wakristo
wa Mataifa lilioendelezwa kipindi cha karne ya pili na ya tatu liliendelea kuwakilisha
mtazamo wa kuamini Mungu mmoja uliokithiri na ule wa Waibionia ‘watu maskini’.
Mtazamo huo ulishikilia kuwa Kristo alikuwa ni mtu, mimba yake ni ya kimuujiza,
lakini alikuwa ni “mwana wa Mungu” wa pekee kwa kuwa amejazwa busara takatifu
na nguvu. Mtazamo huu ulifundishwa huko Roma takriban mwishoni mwa karne ya
pili na Theodotus, aliyetengwa na Papa Victor, na ulifundishwa sehemu Fulani
hapo baadaye na Artemon, aliyetengwa na Papa Zephyrinus. Takriban mwaka 260 CE
mtazamo huo ulifundishwa tena na Paulo wa Samosata,[34]
Askofu mkuu wa Antokia huko Syria ,
ambaye alihubiri kiwazi wazi kuwa Yesu alikuwa ni mtu na kupitia kwake Mungu
ameongea maneno yake (Logos), naye kwa nguvu kabisa amethibitisha upweke
wa Mungu.
Kati ya mwaka
263 na 268 kwa uchache vikao vitatu vya baraza la kanisa viliitishwa huko Antokia
ili kujadili usahihi wa Paulo. Kikao cha tatu kililaani mafundisho yake na
kumvua madaraka. Hata hivyo, Paulo alifaidika na ulinzi wa Zenobia, malkia wa Palmyra , ambaye kwake
yeye, Antokia ilikuwa ndio mada, na haikuwa ila mpaka mwaka 272 pale mfalme
Aurelian alipomshinda Zenobia kwa kiwango ambacho madaraka halisi yakanyakuliwa.[35]
Mwishoni mwa
karne ya tatu na mwanzoni mwa karne ya nne, Arius (b.c 250, Libya – 336 CE), kasisi wa Alexandria ,
Misri, pia amefundisha maumbile yenye mipaka ya Kristo upweke kabisa wa Mungu,
jambo lililowavutia idadi kubwa ya wafuasi, mpaka alipotangazwa kuwa ni
mzandiki na baraza la Nicaea
mnamo Mei mwaka 325 CE. Wakati wa baraza hilo ,
alipinga kutia saini mfumo wa imani unaoeleza kuwa Kristo alikuwa na tabia ile
ile kama Mungu. Hata hivyo, akiwa ameshawishiwa
na wenzake wa Asia ndogo na kutoka Constantia, binti wa mfalme Constantine , alifanikiwa
kushawishi kurejea kwa Arius kutoka uhamishoni na kurudi kanisani.[36] Vuguvugu
alilodhaniwa kuwa amelianzisha, lakini kwa hakika lilikuwa ni kupanua imani ya
Wakristo wa kiyahudi Wanazareti wa Jerusalem, Vuguvugu hilo lilijulikana kama
Arianism na kuunda tisho kubwa ndani ya imani ya itikadi ya Wakristo wa
Kipauline juu ya uungu wa Yesu.
Kutoka mwaka
337 hadi 350 CE, mfalme wa Magharibi, Constans, alionyesha huruma kwa Wakristo
waoksodoksi, na Constantius wa pili, aliyekuwa mfalme wa Mashariki, aliwahurumia
Waarians. Ushawaishi wa Arian ulikuwa mkubwa mno kiasi ambacho katika baraza la
kanisa lililofanyika Antokia (341 CE), uthibitisho wa imani ulikuwa ndio jambo
lililoondoa kifungu cha kuwa Yesu alikuwa na maumbile yale yale ya uungu kama Mungu”. Mwaka 350 CE Constantius wa pili akawa
mtawala wa pekee wa himaya yote, na chini ya uongozi wake sehemu ya Nicene
(Wakristo Waoksodoksi) waliangamizwa kwa kiasi kikubwa. Baada ya kifo cha Constantius
wa pili mwaka 361 CE, Wakristo Waoksodoksi walio na wingi mkubwa huko Magharibi
waliimarisha nafasi yao .
Hata hivyo, utetezi wa kuwa na Mungu mpweke kabisa, na kukandamizwa kwa Wakristo
Waoksodoksi, imani ya utatu iliendelea huko Mashariki chini ya mfalme Arian
Valens (364-383 CE). Haikuwa ila mpaka pale Mfalme Theodosius wa kwanza
(379-395 CE) alipotwaa ulinzi wa imani ya Arius, hata hivyo, imani hiyo iliendelea
miongoni mwa makabila ya Kijerumani hadi mwishoni mwa karne ya saba.[37]
Mawazo ya kisasa
Leo hii, kuna wasomi
wengi katika Ukristo wanaoshikilia kuwa Yesu Kristo hakuwa Mungu. Mwaka 1977,
kikundi cha wasomi saba wa Biblia, akiwemo mwanatiolojia kiongozi wa
Kianglikana na wasomi wengine wa Agano Jipya, walichapisha kitabu kiitwacho The
Myth of God Icarnate, (Kisa cha kubuni cha Mungu mwenye mwili)
kilichosababisha fujo kubwa kwa makutano makuu ya Kanisa la Uingereza. Katika
utangulizi, mwandishi, John Hick, ameandika yafuatayo: “Waandishi wa kitabu
hiki wamekinaishwa kuwa mwendelezo mkubwa wa kitiolojia uitishwe katika muda
huu wa karne ya ishirini.
Dai linaibuka kutokana
na kukuwa kwa maarifa ya asili ya Ukristo, na kuhusisha kutambua kuwa Yesu
alikuwa ni (kama alivyowasilishwa katika matendo 2:21) ‘mtu aliyethibitishwa na
Mungu’ kwa kazi maalum kwa lengo la kiungu, na kuwa dhana ya baadaye juu
kumhusu yeye kama ni Mungu mwenye mwili, Nafsi ya Pili ya Utatu Mtakatifu
inayoishi katika maisha ya kibinadamu, ni ngano ya kubuni au njia ya kishairi
ya kuelezea umuhimu wake kwetu.”[38] Kuna
makubaliano makubwa miongoni mwa wasomi wa Agano Jipya kuwa, kihistoria Yesu
hajadai uungu ambao fikra ya Kikristo ilimfanyia; yeye hajajielewa kuwa yeye ni
Mungu, wala Mungu Mwana, mwenye mwili [katika mwili].[39] Askofu
mkuu wa hivi mwishoni Michael Ramsy, ambaye alikuwa ni msomi wa Agano Jipya,
ameandika kuwa “Yesu hajadai uungu.”[40]
Mwenzake wa zama moja, msomi wa Agano Jipya C.F.D. Moule. Amesema kuwa, “Kwa
hali yeyote ile ya Elimu ya Ukristo ya hali ya juu inayotegemea usahihi wa
madai ya Yesu mwenyewe, hasa hasa katika Injili ya Nne, kwa hakika atakuwa
hatarini.”[41]
Katika utafiti
mkubwa juu ya asili ya imani ya kuwa na mwili, James Dunn, anayethibitisha Elimu
ya Ukristo wa Kioksodoksi, anahitimisha kuwa “hakuna ushahidi wa hakika katika
mapokeo ya mwanzo ya Yesu kwa kile ambacho kwa uadilifu, kitaitwa ufahamu wa
uungu.”[42]
Tena, Brian Hebblethwaite, mtetezi kwa nguvu wa Elimu ya Ukristo ya mapokeo ya
Nicene-Calcedonian, anakiri kuwa “haiwezekani tena kutetea uungu wa Yesu kwa
kurejea katika madai ya Yesu.”[43] Hebblethwaite
na Dunn, na wasomi wengine kama wao
wanaoendelea kuamini uungu wa Yesu, wanadai kuwa licha ya kuwa Yesu
hakujijua kuwa Yeye alikuwa Mungu mwenye mwili. Haya yalijulikana baada ya
kufufuka kwake tu.
Wengine wengi
miongoni mwa Maaskofu wakuu mashuhuri wa Kanisa la Uingereza , wanoshuku
uungu wa Yesu, ni Kasisi asemaye wazi wazi Profesa David Jenkins, Askofu mkuu
wa Durham Uingereza, ambaye anaeleza kwa uwazi kuwa Yesu hakuwa Mungu.[44]
Makala
ifuatayo, ilitokoea katika The Daily News miaka iliyopita, kwa uwazi kabisa
inaonyesha kiasi gani cha shaka miongoni mwa wakuu wa kidini kuhusu uungu wa
Yesu.
Uchunguzi wa kushtusha
wa Maaskofu wa Kianglikana
Kura za
maoni za Maaskofu Waingereza 31, miongoni mwa Maaskofu 39, zinaonesha kuwa,
wengi wao wanaona kuwa, Miujiza ya Kristo, kuzaliwa na bikira na kufufuka
huenda hayo hayajatokea
Hiyo kura ya maoni
iliendeshwa na London Weekend Television's weekly religion show, Credo.
"DAILY NEWS"
25/6/84
|
[1] Pia tazama, Hosea
1:10, ya King James Version.
[2] Katika Revised
Standard Version, inasema: “Na mimi nitamfanya mzaliwa wangu wa kwanza, mkuu
wa wafalme duniani.” Pia tazama Yeremia 31:9, “Watakuja kwa kulia, na
kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia
iliyonyooka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na
Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.”
[3] Pia tazama, Job 2:1
na 38:4-7. marejeo mengine ya wana wa Mungu pia unaweza kupatikana katika
Mwanzo 6:2, Kumbukumbu la
Torati 14:1 na Hosea 1:10.
[4] Luka 3:38.
[5] Neno “wa kuzaa”
katika Kingereza cha Kale linamaanisha ‘kuzaliwa na baba’ na lilikuwa
linatumiwa kutofautisha kati ya Yesu, aliyechukuliwa kuwa ni mwana halisi wa
Mungu, na mfumo wa kistiari wa kutumia neno ‘mwana’ kwa “wana wa Mungu
walioumbwa”.
[6] Katika kitabu cha
Matendo cha Agano Jipya, kuna mihtasari ya hotuba za wanafunzi wa kwanza wa
Yesu, maneno ya tarehe zinazoanzia mwaka 33 CE., takriban miaka arobaini kabla
ya kuandikwa zile Injili nne. Katika moja ya hotuba hizi, Yesu anaaonyeshwa kwa
bayana kuwa ni andra apo tou theou: “yaani, mtu kutoka kwa Mungu.”
Matendo 2:22. Hakuna hata nara
moja kuungama huku kwa mwanzo kwa imani ukitumia maelezo wios tou theous:
“Mwana wa Mungu”, lakini wao wanaongea mara kadhaa kuwa Yesu ni mtumishi wa
Mungu na ni mtume Matendo 3:13, 22, 23, 26. Maana ya hotuba hizi ni kuwa hotuba
hizo kibarabara zinaakisi imani asilia na istilahi za wanafunzi wa Yesu, kabla
ya kubadilishwa kwa imani na istilahi chini ya ushawishi wa Dini ya Warumi na
Falsafa za Kigiriki. Wao wanaakisi mapokeo ambayo ni ya zamani kuliko yale
yanayotumiwa na Injili Nne, ambapo Yesu havikwi uungu wala umwana wa Mungu.
(Bible Studies From a Muslim Perspective, p. 12).
[7] Tazama
Matendo14:11-13. Katika mji wa Lystra (Uturuki), Paulo na Barnabas walihubiri,
na wapagani walidai kuwa Paulo na Barnaba walikuwa ni miungu wenye miili.
Walimwita Barnaba mungu wa Kirumi Zeus, na Paulo mungu wa Kirumi Hermes.
[8] Bible study from a
Muslim Perspective, p. 15.
[9] Mathayo 5:9.
[10] Journal of
Theological Studies, vol. 39 na Thewology, vol. 91, no. 741.
[11] Yesu ananukuu Zaburi
82:6 “Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.”
[12] Pia tazama Yohana
17:11.
[13] Pia tazama, Mathayo
2:8.
[14] Pia tazama Mathayo
28:9, "Na tazama, Yesu akakutana nao, akasema, Salamu! Wakakaribia wakamshika
miguu, wakamsujudia."
[15] Tazama, kwa mfano, 1
Samweli 25:23, "Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka
kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka
nchi."
[16] Gospel Light, (1936
ed.) p. 353, quoted in Jesus, p.21.
[17] Injili ya Yohana
kimsingi inatofautiana na Injili nyingine tatu (Injili za muhtasari) kiasi cha
kutilia shaka uhakika wake. Kwa mfano:
Injili za Ufupisho
|
Injili ya Yohana
|
Mahubiri ya Yesu kwa umma yalikuwa ni mwaka mmoja
|
Mahubiri ya Yesu kwa umma yalikuwa ni miaka mitatu
|
Yesu aliongea kwa ufupi kiasi cha mstari mmoja hivi,
na kwa mafumbo
|
Yesu aliongea kwa urefu na kwa mijadala ya kifalsafa.
|
Yesu amesema kidogo mno kujihusu yeye mwenyewe
|
Yesu aliakisi kwa upana zaidi juu ya kazi yake na haiba yake.
|
Kumtoa mbadilisha pesa nje ya hekalu ndio tukio lake la mwisho katika
kazi yake duniani
|
Kumtoa mbadilisha pesa nje ya hekalu ndio tukio lake la kwanza katika
kazi yake
|
Yesu alitetea maskini na wakandamizwaji
|
Yesu alikuwa na jukumu dogo au hakuwa na jukumu lolote kwa maskini na
wakandamizwaji
|
Yesu ni mtoa pepo
|
Yesu hajatoa pepo
|
Yesu alisulubiwa mnamo 15 Nisan
|
Yesu alisulubiwa mnamo 15 Nisan, siku ya Pasaka ya muhanga wa
Wayahudi.
|
[18] The Five Gospels, p.
10.
[19] Wingi wake ni logoi
nalo pia linamaanisha “hoja” au “mpango”.
[20] Dhana
inayotambulishwa na neno logos pia linapatikana kwa wanafalsafa wahindu,
Wamisri, na Wairani na mifumo ya kitiolojia. (The New Encyclopaedia
Britannica, vol. 7, p. 440)
[21] Stoics walikuwa ni
wanafalsafa waliofuata mafundisho ya mtambuzi Zeno wa Citicum (karne ya 4-3
BC).
[22] Wao wanaliita logos
majaaliwa ya Mungu, maumbile, mungu, na roho wa ulimwenguni.
[23] Kwa mujibu wa Philo
na wanafalsafa wa The Middle Platonists, waliofasiri kwa istilahi za kidini
mafundisho ya karne ya nne BC ya mwalimu wa falsafa wa Kigiriki Plato, logos
alizaliwa duniani kama ni msingi na wakati huo huo akili ya kiungu ya hali ya
juu. (The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 7, p. 44o)
[24] The New Fncyclopaedia
Britannica, vol. 9, p. 386.
[25] Ibid, vol. 7, p. 440.
[26] Kristo katika
Uislamu, pp. 40 – 1.
[27] Hili ni kwa mujibu wa
King James Version na the Authorized Version. Katika Revised Standard Version,
tafsiri ya mstari huu ni rejesho, “Na Bwana alimwambia Musa, ‘Tazama,
Ninakufanya uwe Mungu kwa Farao; na Aroni nduguyo atakuwa mtume wako.”
[28] - The Myth-maker, p. 172.
[29]Miaka
sabini baadaye Kanisa la
Kikristo lilijengwa upya huko Jerusalem , baada ya huo mji kuharibiwa na
Warumi kwa mara ya pili na kujengwa upya ukiwa ni mji wa Mataifa usio wa
Wayahudi ukiitwa Aelia Caitolina. Hili kanisa Jipya la Kikristo halikuendeleza
‘Kanisa la Jerusalem ’ lile la kwanza
lililongozwa na James. Wafuasi wake walikuwa ni watu wa Mataifa, kama anavyothibitisha Eusebius, na imani yake ilikuwa ni
ile ya Ukristo wa Kipauline. (Eusebius, Ecclesiastical History, III. V. 2-3,
iliyonukuliwa katika The Myth-maker, p. 174)
[30] The Myth-maker, p. 175.
[31] The New Fncyclopaedia
Britannica, vol. 4, p. 344.
[32] Ibid., vol 4, p. 344.
[34] The New Fncyclopaedia
Britannica, vol. 8, p. 244.
[35] The New Fncyclopaedia
Britannica, vol. 9, p. 208.
[36] Ibid., vol. 1, pp.
556-7.
[37] The New Fncyclopaedia
Britannica, vol. 1, p. 549-50.
[38] The Myth of God
Incarnate, p. ix.
[39] The Metaphor of God
Incarnate, pp. 27-8.
[40] Jesus and the Living
Past, p. 39.
[41] The Origin of
Christology, p. 136.
[42] Christology in the
Making, p. 60.
[43] The Incarnation, p.
74.
No comments:
Post a Comment