Monday, April 2, 2012

Tunahitaji ‘UN’ ya Waislamu!


Na Twahir Rashid 
Upande! 
Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa. Neno "Upande" ni lugha ya Kiswahili ambapo Kiarabu ni "Kibla" (2:177). Nalo neno hili kibla (upande wa kuelekeza nyuso zetu) limebatizwa na huitwa (Capital City) mji mkuu. 

Kibla! 
Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa. Kauli hii "tunahitaji "UN" ya Waislamu", labda tusema "UN-dhana" ni ya madume matano yenye Turufu (VETO). Bali tunahitaji "UN" ya walimwengu wote. 

Na hapa tuingize fikra hii. Kwamba Mwenyezi Mungu hakuna kitu alichokiacha bila kukiweka wazi ndani ya kitabu chake (Quran). "UN ya Mataifa yote ilishaundwa na Mwenyezi Mungu na kUtiwa zege na Mtume Muhammad (s.a.w.) pale alipogeuzwa katika kibla akipendacho (2:144) nao ni upande wa msikiti mtakatifu, kwa kuacha upande (kibla) (kiini cha zamani) Baitil -Magdis. Na ni kwa nini alekee Makka? Basi fahamu kuwa "Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu ni ile iliyoko Makka, yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote." (3:96) Basi yule atakayekuwa maongozi yake hutokea mji huu, kwa maana wale wanaoelekea Makka kwa ajili ya maongozi ya maisha ya dunia yao na baraka; hao ndio wafuasi wa Mtume Muhammad (s.a.w.) (2:143).Kwa hiyo shibe na amani (106:3-4) watapata. Ili hali watakaoelekea mji mwingine usiokuwa huu(k.m. New York); njaa na khofu zitawasibu (106:3-4). Ndio Khaswa Mwenyezi Mungu atufanyiza Kampeni (anatuita)katika Nyumba (Ikulu) ya amani (10’25) - lakini watu leo tumefikishwa katika nyumba (Ikulu) ya Maangamizo (14:28) humo tukaagizwa kuwa watoto na moja kwa moja dini kuvurugwa (6:137). 

Kwa hiyo kuwa na Katibu Mkuu (Khalifa) ndio sawa. Ila Kofi 
Anan ahame kutoka Ikulu ya Maangamizo (14:28) (New York), ahamie Ikulu Kongwe (22:29) (Makka), kwani Katibu Mkuu (Khalifa) hana lake jambo ila kufuata Buku atakalolikuta katika Nyumba atakayosimama (2:125). 

Kwa hayo jua basi, Waislamu ni wale ambao mji wao mkuu (mji wanaowatajia watoto wao) ni Makka kwa hiyo Kofi Anan wao makao (ofisi) yake yapo Makka (27:91).Kinyume na hivyo ni kushirikisha (6"148). 

Ndio hivyo tunapo ambiwa turejee kwa Menyezi Mungu maana yake ni kwamba sasa hivi tupo katika uongozi wa Majumba (Ikulu) ya shetani (UN-New York) (ambavyo Ikulu hii imeshikana Ikulu yote ya kila nchi mpaka ofisi za vijiji). Kwa hiyo tutoke humo turejee katika (Ikulu ) ya Mwenyezi Mungu (UN-Makka). Na tayari UN-Makka ina ofisi zake mpaka Vijijini nayo ndio misikiti (72:18). 

Misikiti! 
Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa. Ndugu yangu Said Rajab swali lako. Je! Waislamu wa dunia nzima, wakati haujafika tu wa kuwa na "UN’ ya Waislamu.....? Basi fahamu kuwa kizazi cha Israel kilichukuwa ahadi (2:40) (lakini) waliificha haki (2:42, 2:146) nayo ni kuelekea Makka (2:144, 2:147) kwa maongozi ya dunia nzima (3:96). 

Wao wakaasi na kuruka mipaka pale walipokataa (maongozi)ya Mwenyezi Mungu na kuwaua manabii. Kwa hiyo wakapingwa juu yao chapa ya dhila na umasikini (2:61) mpaka leo hawana nchi. Wamepigwa chapa ya dhila popote wanapokuweka, ila (kwa kushika)kamba (dini) ya Mwenyezi Mungu (uogozi wa UN-Makka) au kamba ya watu (UN-New York) (Amerika Inawasaidia).... (3:112) na imewasimika Palestine. 
Kwa hiyo juhudi zimefanyika kuficha ukweli huu wa UN ya walimwengu wote (3:96) ambayo ndiyo tengenezo la maisha ya watu (5:97) baada ya kuharibiwa (2:12-11). Hivyo maongozi ya watu (Serikali) Majeshi, Mashule, na Nyumba za Mungu (Makanisa, Misikiti, Mapagoda n.k.)vyote vimehujumiwa (17:64) zimeshikwa na shetani. Na kutumiwa kupotosha ukweli. 
Wanaostahiki kuamirisha misikiti (ofisi za Mwenyezi Mungu) kwa ajili ya uongozi khaswa (2:120) ni wale 
1. Wanaomuamini Mwenyezi Mungu 
2. Na siku ya Mwisho 
3. Husimamisha swala 
4. Hutoa zaka 
5.Hawamuogopi yeyote ila Mwenyezi Mungu (9:18). 
Eh! Mola wangu, mimi ni mja wako 
Mikono nimekunyoshea 
Thelathini na sita miaka, tangu kijijini eti nini? nikatafute elimu. 
Na hivi imetimu ishirini na tano 
Miaka, tangu wanibwage mjini (2:61) 
Kufanya kazi ndiyo dini yangu 
Yote hayo wanisumbuliani? Tumbo? 
Unyonge umekithiri, umasikini ndio usiseme. Manabii wa leo (Mbwechai) wauawa (2:61) neno la Mwenyezi Mungu kosa. 
Ilivyokuwa kwa mfalme wa Yemen ndivyo hivi leo. Mfalme wa Marekani kafanya aliyoshindwa Mfalme wa Yemen na watu wote hata Saudia na Iran wana wajumbe wa kudumu katika Kibla cha New York Wamegeuzwa bila kujua (40:63). Ni nguvu ya mkono wako sasa tunayoienzi. Kwa sababu mfalme hupambana na mfalme mwenzake. Watu wanakutaka sasa uwaongoze uwatoe katika giza uwapeleke katika Nuru (2:257)

Mji maarufu kuliko yote leo duniani, ni mji huu wa New York.Hapo ndipo ambapo Baraza Kuu la Ulimwengu liliposimikwa, nalo ni Baraza la Umoja wa Mataifa. Baraza hili liko katika nyumba ya Umoja wa Mataifa badala ya kuwa katika nyumba isiyo na kushirikisha (22:26). Na haya sio kwa kubahatisha. La. Bali ni mpango maalumu ili watu wageuzwe bila wao kujua. Na imekuwa hivyo. Siri hii New York maana yake ni "Kiini Kipya". Sasa hicho kiini cha kale ni kipi? (22:29) 
Hivi kusema New York kwa maana ya kiini kipya, Waingereza wenyewe wangaliita New Center. Sasa la kujiuliza ni kwamba ni ipi iliyokuwa Old Center? 


Zingatia uone kwamba katika huo mji uitwao New Center ipo nyumba inayoeleweka na walimwengu wote kwa maongozi na baraka (ruzuku). Kwa hiyo, tukisema ipi hiyo Old Center la kuangalia hapa ni kutafuta kuijua nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya ulimwengu wote (Umoja wa Mataifa wa kweli) yenye maongozi na baraka (3:96). Na jambo hili la uongozi limefichwa. (2:159, 2:146). Uongozi wa walimwengu wote ndio Uongozi (2:120) 
Nyumba hii ya Umoja wa Mataifa bandia iliyoko kiini kipya ndiyo ambayo Mola wetu anaiita "nyumba ya maangamizo". (14:28). Hutuamrisha kuua watoto (6:1379) (Uzazi wa mpango) kwa hiyo utaratibu wa maisha unavurugwa. Lengo la maisha ya watu limekuwa ni kuboresha mazingira yao binafsi bila kujali litakalo tokea. 
Kwa maana hii ituyakinie kwamba hivi leo duniani upande (kibla) watu wanapoelekea sio kiini cha kale (Makkah). Bali ni kiini kipya (New York). Jambo ambalo Mola wetu ametuasa kuwa tusifuate upande (kibla) wa wale waliopewa Kitabu (2:145) kwani tukifanya hivyo, tutakuwa "madhalimu". Kwa kuelekea leo kibla cha New York hakuna maana nyingine bali sisi tulioko Makanisani na Misikitini tumekuwa madhalimu bila kujua. 


Wito wa Allah (s.w.): 
Na Mwenyezi Mungu anatuita katika nyumba ya amani (The Old Center) (10:25) (kwani) amani itakuwa juu ya wale wanaofuata uongozi (Wake) (20:47). Hapo ndipo ilitakiwa liwepo baraza la (Usalama 2:124). 
Jambo ambalo wale waliopewa Kitabu wanalijua kama wanavyo wajua watoto wao (2:146). Lakini kwa dhulma yao (4:160) (huzua kwao kibla kingine 2:145) watu walioko Makanisani na Misikitini, tunafuata kibla hiki, kwa hiyo nasi sote tumekuwa madhalimu. (Ole wetu) siku ambayo itatufikia adhabu aseme wale waliodhulumu. "Mola wetu tuakhirishe muda kidogo, tutaitikia wito wako na tutawafuata Mitume ..." (14:44). Kwani huku kumfuata Mtume ni nini? 


Tujiulize kwanza, hivi leo anayefuatwa ni nani? Mtume leo hayupo, lakini kile alichokuja nacho kipo. Na ni agizo kwetu kuwa tuwaite watu kwa Mola wetu na mtu yeyote asikuzuie kufuata aya za Mwenyezi Mungu (28:87). Na ni nani dhalimu kuliko yule anayekumbushwa aya za Mola wake akawa anazipuuza, na akayasahau yaliyotangulizwa na mikono yake. (18:57) Watu badala ya kukampeni jina kwa ajili ya Allah (s.w.) wao hukampeni kwa ajili ya majina yasiyokuwa jina Hili. Basi wasituzuie (kukampeni kwa ajili ya Rais wetu Allah) wale wasioamini na wafuatao matamanio yao. (20:16). Kwa kufuata matamanio yao (kibla chao 2:145) tumekuwa madhalimu pasipo kujua (30:26). 
Kumfuata Mtume! 


Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume wawili na akawazidishia nguvu kwa Mtume wa tatu; lakini watu waliwakadhibisha (36:14) kwa kuendelea kufuata mila za wakuu wao (7:88-89). Basi akaja mtu akisema "enyi watu wangu wafuateni mitume hawa" (36:20). Kwa sababu kwa kuwafuata Mitume ndio kumuabudu Muumba (36:22). Usipowafuata Mitume utashika Miungu mingine badala Yake (26:23) na huo ndio kuwa katika upotofu uliodhahiri (36:24). Udhalimu maana yake (31:11). 


Tusijesema "Wallahi", kwa yakini tulikuwa katika upotofu ulio dhahiri, tulipokuwa tukikufanyeni sawa na Allah. Na si wengine hawa wanaofanywa sawa na Allah ila ni (watu) waovu (26:97-99). Nao ni wakuu wa miji (6:123). 


Kwa kuwafuata wakuu wetu wa miji, ndio upotofu uliodhihiri. Kwani wao ofisi zao huelekea Ikulu iliyoko mji mkuu. Na Ikulu hiyo iliyopo mji mkuu imeelekea Ikulu ya dunia iliyoko Kiini Kipya. Hivyo, kwa ulaini maongozi ya Allah yametiwa kapuni. Ni kwa kuelekea Ikulu ya dunia iliyoko Makkah ndio Kumfuata Mtume (2:44) ili tuongoke (2:150). 


Said Rajab. Nyanyua mikono tuombe, kwani si mwingine bali ni wewe uloleta hoja hii adhimu. "Mola wetu tumesikia na tutatii tunakuomba msamaha. 
Na marejeo ni kwako. (2:285). Mola wetu usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na utupe rehema itakayo kwako. (Wallah jambo hili la mji mkuu wa dunia (Makkah) limefichwa) hakika Wewe ndiye Mpaji Mkuu (3:8). 
Mola wetu usiendelee kututesa kwa kusahau kwetu (tukakosea na kufuata maongozi ya New York). Hivyo, usitubebeshe mgizo kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Usitutwike tusiyoyaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tusaidie juu ya makafiri. (2:286). Hali yetu ni mbaya. Tuko Misikitini na Makanisani na tunafanywa kugombana, kumbe kikulacho kiko nguoni mwako.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget