Thursday, April 12, 2012

Unataka mtoto?


Zipo Dua nyingi mno kwa ajili ya mwanamke kushika mimba na hapa chini nitawaleteeni Dua chache ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa wale bibi na bwana ambao kwa bahati mbaya hawakujaaliiwa watoto ninatumaini na ni sala zetu pia kwa kusoma duaa na kwa kufuata miongozo michache ifuatayo Allah swt atawajaalia hiyo neema.

Mtume s.a.w.w. amesema: "Watoto ni sawa na maua ya peponi kwa hivyo uwema wa mtu ni kutokana na vile anavyozaa watoto."

Mtu ambaye hajabahatika kupata watoto, aende katika hali ya sujuda na asome Dua ifuatayo:-
Rabbi habli min ladunka dhurriyatan tayyibatan Innaka samiud-Dua', Rabbi la-tadharni fardan wa anta Khayrul Warithiin.

Na mtu ambaye anataka mke wake ashike mimba basi inambidi baada ya sala ya Ijumaa asali rakaa mbili na katika kila rukuu na sujuda arefushe na baada ya sala asome Dua ifuatayo:-
Allahumma inni as-aluka bima sa-alaka bihi Zakariyya:Rabbi la tadharni fardan wa anta khayrul warithiin,habli minladunka dhurriyatan tayyibatan,Innaka akhadhtaha fa fadhayat fi rahimiha waladan,fajalhu ghulaman mubarakan zakiyyan wala taj'al lishaytani fihi shirkan wala nasiban.

Mtu mmoja alimwijia Imam Muhammad Baqir a.s. na kumwambia:"Ewe mjukuu wa Mtume! Mimi sina watoto," hapo Imam a.s. alimjibu kuwa : 
"Kila usiku au kila wakati wa mchana usome Istighfaar mara mia moja na Istighfaar ifuatayo ndiyo itakuwa vyema zaidi. 'Astaghfirullah rabbi wa-atubu ilaihi'.

Ili kutaka watoto kwa wale ambao hawajabahatika inawabidi daima asubuhi na jioni wafanye ifuatavyo: 
asome mara kumi
Astaghfirullah rabbi wa-atubu ilaihi na baadaye asome mara tisa Subahanallah na baadaye asome mara moja Astaghfirullah rabbi wa-atubu ilaihi.
Mwenye kuripoti mmoja anaelezea kuwa watu wengi wamefanya majaribio hayo na wameweza kuzaa watoto wengi.
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema kuwa mtu yeyote mwenye kutaka watoto, kila anapoamka asome Istighfaar mara mia moja na lau atasahau hapo baadaye asome kwa nia ya Qadhaa.
Mtu mmoja alisema:"Ewe Imam mimi sina watoto."Imam a.s. alimwambia:"unapopanga kusuhubiana na mke wako soma duaa ifuatayo : Allahumma inruzaktana dhakaran sammaytuhu Muhammadan.
Mtu mmoja alimwijia Imam Ridhaa a.s na kumwambia: "Ewe mwana wa Mtume ! Mimi daima huwa niko mgonjwa na sina watoto."Hapo Imam a.s alimjibu: "Uwe ukisoma adhaan nyumbani kwako kwa sauti kubwa. Yule mtu baada ya miaka kupita alimwijia Imam na kumwambia:"Mimi nilikuwa nikifanya hivyo na ninamshukuru Allah swt nimepona na nimekuwa mzima na sasa hivi nina watoto wengi."

Mtu mmoja alikuja kwa Imam Jaafer Sadiq a.s. na kuleta malalamiko yake, "Ewe mwana wa Mtume ! Mimi sipati mtoto wa kiume." Hapo Imam a.s. alimjibu: "Popote pale unapokuwa umepanga kusuhubiana na mke wako (kumuingilia mke wako) basi usome Aya ifuatayo mara tatu na baada ya kusoma mara tatu ndio usuhubiane na mke wako. Allah swt atakujaalia watoto wa kiume.

Na Aya yenyewe ni hii ifuatayo:-Wadhannuni Idhdhahaba mughadhiban fadhanni an lan nakdir Ilayhi fanaada fidhdhulumaati,'an-Lailaha illa Anta Subhanaka inni kuntu minadhdhalimiin, fastajabna lahu wa najjainahu minal ghammi wa kadhalika nunjil mu'miniin,Zakariyya idhnaada Rabbahu Rabbi la tadharni fardan,wa anta Khayrul warithiin.

Katika Hadith inapatikana kuwa mtu yoyote ambaye hapati watoto inambidi afanye niyyat kama ifuatavyo:- "Iwapo mimi nitapata kijana wa kiume jina lake nitaliweka Ali" basi Allah swt atamjaalia mtoto wa kiume.
Imam Zeinul Abeidin a.s. amenakiliwa akisema mtu yeyote atakayesoma Dua ifuatayo atapata chochote kile akitakacho lau atataka mali, au watoto na wema wa dini na dunia, basi Mwenyezi Mungu atamjalia vyote hivyo na Dua yenyewe ni kama ifuatavyo:-
Rabbi la tadharni fardan,wa anta Khayrul warithiin wajalni minladunka wayarithuni fi hayati wayastaghfiruli baada mauti waj-alha khalqan sawiyyan wala taj-al lishaytani fiha nasiban.Allahumma Inni astaghfiruka wa atubu ilayka,Innaka antal ghafurur-Rahiim.
Na kwa hakika imependekezwa mno kusoma Dua hiyo mara sabini kwa ajili ya wale wanaotaka watoto.
Mtu mmoja alimwijia Imam Muhammad Baqir a.s. na alikuja akilalamika kuwa anao watoto wachache. Hapo Imam alimjibu: "Kila siku kwa muda wa siku tatu baada ya sala ya asubuhi na sala ya Isha usome subahanallah mara sabini na Astaghfirullah mara sabini. 
Na baadaye usome Dua inayofuata:- 
Astaghfiru Rabbakum Innahu kana Ghaffara,yursilussama' alaykum midraara,wa yumdidkum bi amwalin wa baniin wa yaj-alkum anhaara.
Baada ya kukamilisha utaratibu huo kwa muda wa siku tatu kwa usiku huo wa siku ya tatu ndio usuhubiane na mke wako na Allah swt atakujaalia watoto wema kwa ajili yako.

Mtu mmoja alikuja kwa Imam Jaafer Sadiq a.s. na kumwambia: "Ewe mjukuu wa Mtume! Allah swt amenijaalia wasichana wanane lakini mpaka leo sijabahatika kuona sura ya mtoto wa kiume. Imam a.s. alimwambia: 
"Wakati wa kusuhubiana, ukae katikati ya miguu ya mke wako, wakati huo mkono wako wa kulia uwe upande wa kulia mwa kitovu chake na usome sura ya Inna-An- zalnahu ... mara saba na baada ya kusoma ndio usuhubiane na mke wako.
Mtu huyo anasema kwa kufanya hivyo Allah swt alimjaalia watoto saba wa kiume.
Imam Hasan a.s. amesema: "Yeyote yule anayependa kuzaa watoto wa kiume basi inambidi afanye Istighfaar kwa wingi kabisa."

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget