Friday, April 6, 2012

UJIRANI NA HAKI ZAKE KATIKA UISLAMU

Ndugu zanguni Waislamu, kila mmoja anahitaji mazungumzo hayo, maongezi ambayo Jibril hakuacha kumusia Mtume (SAW) kuhusu jirani mpaka akadhani anahaki ya kurithi. Jirani ana haki zinapaswa kulindwa hizo haki na jirani huyo sawa awe muislamu au kafiri, mwema au muovu, rafiki au adui aliyekuwa karibu au mbali. Na kila mmoja ana daraja kuliko mwengine inazidi au inapungua kutokana na ukaribu wake, dini yake, tabia yake na ukaraba wake. Uislamu umeusia kuhusu jirani na kuhifadhi haki zake amabazo hazijatambuliwa na kanuni. Amesema Mwenyezi Mungu (SW):

قال تعالى : { واعبدوا الله ولا تشركوا به شيئا وبالوالدين إحسانا، وبذي القربى واليتامى والمساكين والجار ذي القربى والجار الجنب }
 {{ Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msishirikishe na chochote. Na wafanyeni ihsani wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na maskini, na jirani walio karibu au jirani walio mbali}}. Amepokea Ibn umar, amesema Mtume (SAW):  [ Hakuacha Jibril kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhani kuwa jirani atarithi]. Amepokea Abu Hureira hadithi kutoka kwa Mtume  (SAW) akisema: [ Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho azungumze mambo ya kheri au anyamaze, na anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho amkirimu jirani yake]. Amesema Sheikh Abuu Muhammad:  Kuhifadhi haki  ya jirani ni katika kukamilika kwa Imani. Na watu wajahilia walikuwa wakihifadhi haki za jirani na wakiusia kwa kuwafanyia wema mfano kumpa zawadi, kumtolea salamu, kumuonyesha uso wa furaha na kujua hali yake na kumsaidia anacho kihitaji.
4.    Kumrehemu anapo chemua
5.    Kumtembelea anapokuwa mgonjwa
6.    Kufuata jeneza lake anapo kufa




Ndugu zangu Waislamu ni haramu kuudhi majirani.  Mtume (SAW)  amesema: [ Mwenye kumuamini Mwenyez Mungu na siku ya mwisho basi asiudhi jirani zake].  Imepokewa na Shureyh amesema Mtume (SAW): [ Naapa kwa Mwenyezi Mungu Haamini! Haamini! Haamini! Akaulizwa: Nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?  Akasema:  Ni yule ambaye kwamba majirani zake hawasalimiki na shari zake]. Miongoni mwa sura za kuwaudhi majirani nikuwaudhi watoto wake, kuchezea milki yake kuinua sauti kama ya nyimbo na kumpangaisha mtu asiyeridhika nae.
Na kuwaudhi majirani kama kuwafanyia kinyama, kuwachunguza, kufuatilia aibu yake,  kuangalia maharimu zake,kupitia dirisha lake au kumtembelea mke wake. Imetolewa onyo kali kutoka kwa Mtume (SAW)  kwa mwenye kufuatilia aibu za jirani zake, Ibnu Masoud alimueleza Mtume (SAW) akisema: Ni dhambi gani kubwa? Ni kumkirisha Mwenyezi Mungu, kisha akasema ni dhambi gani? Akasema Mtume: ni kumuua mtoto wako kwa kuchelea kutomlisha, kisha akasema dhambi gani? Akasema ni kuzini pamoja na jirani yako”.  Amesema Mtume (SAW) : [ Kuzini mtu na wanawake kumi ni bora kuliko kuzini na mwanamke wa jirani yake].
Mcheni Mwenyezi Mungu, Enyi wenye kukhini jirani zenu ima kwa kuwapigia simu au kwa njia ya ujumbe au kwa njia ya kuangaliana.  Amesema Mwenyezi Mungu (SW):




يقول الله سبحانه وتعالى : {وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُبِينًا}
{{ Na wale wanaowaudhi wanaume Waislamu na wanawake Waislamu pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhahiri}}.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu kuwaudhi majirani kuna namna nyingi kama zifuatazo; kutumia milki ya jirani mwenzake kwa kumuudhi  mfano wake kuegemea matagaa ya mti wake kwa jirani mwenzake, kufanya kiwanda ambacho kinatoa moshi au sauti au upepo ambapo kinaudhi majirani wenzake yapaswa kuzuiwa mfano wa madhara haya.

Tahadhari na Mambo ya Futayo:-
a.    Kuwakodisha majirani wasio swali wala wasio muogopa Mwenyezi Mungu
b.    Kukodi duka au sehemu ya kuuza vitu vya haramu kama kaseti za nyimbo na nyenginezo
c.    Kumuzuia jirani kutoshughulika kwa milki ya jirani mwenzake kama kuweka mbao katika ukuta wa jirani mwenzake.
d.    Kuwakataza jirani wenzake kunufaika kwa mambo ya shirika ya watu wote mfano wake kuteka maji katika kisima au mto. Amesema Mtume (SAW)  : Watu ni washirika kwa mambo matatu:-
1.    Maji
2.    Moto
3.    Nyasi
e.     kuweka udhia katika njia.
Mcheni Mwenyezi Mungu na mubadilishane manufaa kati yenu na jirani zenu. Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
قال تعالى : {وتعاونوا على البر والتقوى ولا تعاونوا على الإثم والعدوان واتقوا الله إن الله شديد العقاب}
 {{ Na saidianeni katika wema na twaa, wala msiaidiane katika dhambi na uadui}}


Mfano Mwema wa Waja Wema Waliopita na Jirani Zao
Tarekhe ya kiislamu imejaa mifano iliyokuwa ya juu kwa namna ya kuaminiana kati ya majirani. Imamu Dhahabi ametaja katika kitabu chake kwamba jirani wa Abi Hamza. na huyu Walid Ibnu Kassim Bin Walid Hamdanii ameulizwa Ahmad Ibni Hanbal akasema ni mwaminifu, na akaulizwa Abi Yaala akasema ni mtu bora nay eye ni jirani yetu tangu miaka hamsini uliopita na hatukumuona ispokuwa na kheri.
Ndugu katika imani, huo ni mifano wa watu wema waliopita namana walivyo ishi na majirani kwa wema na kusaidiana. Nijukumu letu kuwaigiza watu wema na kufuata vitendo vyao, kwani huko ndio kufaulu. Asema Mshairi: Jifananisheni na watu wema hata kama hamtafanana na wao, lakini kule kujifananisha nawao nj kufaulu. Enyi Waumini fanyeni bidii kutekeleza haki za jirani kama alivyo tufundisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Mwisho
Ndugu Waislamu, tumeona wazi namna ya sheria ya Kislamu ilivyo himiza juu ya haki za jirani. Na adhabu kali kwa wale watakao keuka haki hizo. Kwasababu, mwanadamu nilazima atekeleze haki mbili; haki ya kwanza ni ya Allah, na haki ya pili ni ya viumbe wenzake. Haki ya Allah anaweza mwanadamu kupata msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Yeye ni mwingi wa kusamehe. Lakini haki za mwanadamu ni lazima kutekeleza hapa duniani na ukishindwa, utadaiwa siku ya kiama. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Atuwezeshe kutekeleza haki zote zake na za viumbe vyake

.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget