Monday, April 2, 2012

MARADHI YA KISAIKOLOJIA


Paraphilia 
Maradhi ya kisaikolojia ambayo yameivamia jamii yetu na yanaendelea kuwaathiri watu kwa kasi ya ajabu, hasa wanapokuwa nje ya kanuni na maadili ya Kiislamu.
Maradhi haya hujulikana kama
 Paraphilia ambapo mtu anakuwa na tabia za ajabu na mbaya,kama tutakavyoziona. 
Paraphilia zote hukithiri katika jamii ambayo watu wake wamezama kwenye zinaa.
Zinaa siku hizi katika jamii yetu imekuwa sio dhambi, na imekuwa ni jambo la kawaida lisilo hata na kificho. Matokeo yake watu wengi wamekuwa na maradhi haya ya kisaikolojia ya Paraphilia . Baadhi ya Paraphilianitakazozingumzia katika makala zangu ni hizi zifuatazo. 
1. Voyeurism. 
2. Sexual sadism. 
3. Frotteurism. 
4. Exhibitionism. 
5. Fetishism. 
6. Transsexualism. 
7. Transvestism. 
8. Pedophilia. 
9. Sexual Mosochism. 
10. Homosexualism/Lesbianism.
 
Usitishike na majina hayo kwa lugha ya kigeni. Kila kimoja tutajitahidi kukielezea kwa ufasaha wake katika lugha ya Kiswahili. 
Voyeurism: Tukianza na maradhi ya kwanza, Voyeurism ni maradhi ya kisaikolojia ambapo mwenye maradhi haya anakuwa na tabia ya kupenda kuangalia watu wasio na nguo. Mtu mwenye maradhi haya huitwa kitaalamu Voyeur (inasomwa vouya). Kwa Kiingereza cha kawaida, mtu huyu huitwa Peeping Tom, Waswahili humwita kozimeni. 
Mara nyingi Voyeur huwa na tabia ya kuchungulia watu walio kwenye faragha, na yeye roho yake hufurahi kuwaona watu walio wazi bila nguo, na furaha yake hufikia kilele kama atawaona mke na mume wako katika kitendo cha ndoa. 
Katika jamii yetu leo, maradhi haya yameingia kwa kasi. Tunao watu wengi waliozama hapa, na iko haja ya kupambana na maradhi haya, na hakuna anayeweza kupambana nayo bali Waislamu. Siku hizi, wenye maradhi haya huwezi kuwakuta wanachungulia madirishani au sehemu nyingine, kwa sababu wanaweza kushikwa na kuchomwa moto. Kuna mbinu mpya za kukidhi haja ya wenye maradhi haya. Zamani kulikuwa na senema za X. Siku hizi kuna kanda za video, hawa akina Peeping Toms hujifungia ndani na kuanglia kanda hizi. Hawa ni wagonjwa mahututi. 
Kuna wagonjwa wengine ambao sio mahututi, lakini nao pia ni ma Voyeur. Kwa mfano, binti wa Kiislamu anaweza akaomba avae hijabu shuleni, lakini wapo watu hawakubali binti huyu afunike viungo vyake. Utamkuta mwalimu anakuwa mkali kabisa, kwani na yeye ni miongoni mwa watu ambao roho zao haziridhiki mtu, hasa mwanamke anapojihifadhi. Hawa ndio wale wale ambao huandaa kile kinachoitwa "mashindano ya uzuri" na kuwapitisha mabinti waliovaa "vichupi" mbele ya kadamnasi, na mwisho huwapa zawadi. Kwa bahati mbaya sana, wenye maradhi hawa ni pamoja na viongozi wa nchi. Wao hufungua na kushiriki katika mambo haya ya kukodolea macho watu walio uchi. 
Mtume amesema: "Jinsi mlivyo, ndivyo mtakavyotawaliwa", kwa hivyo, kama viongozi wetu ni ma Peeping Tom na ma Voyeur, auMakozimeni, je wanaoongozwa. 
Kiboko ya maradhi haya hakuna zaidi ya Uislamu kwani ndio unaotekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu yasemayo: "Wala msiikurubie zinaa hakika hiyo ni uchafu na njia mbaya kabisa". (Qur. 17:32)  

SEXUAL SADISM
Hapo juu tuliona aina ya maradhi ya Paraphilia yaitwayo Voyeurims yaani maradhi ya mtu kupenda kukodolea macho au kuchungulia watu wasio na nguo. Sasa tuangalie Paraphilia nyingine ambayo vile vile inakuwa kwa kasi katika jamii yetu. Hiini Sexual Sadism,yaani maradhi ambayo aliyenayo huona raha mtu wa jinsia tofauti na yeye anapodhalilika au kuteseka kijinsia. 
Sexual Sadism ni maradhi ambayo yanawapata wake kwa waume, ingawaje maradhi haya hukithiri kwa wanaume. 
Mara nyingi wanaume wenye maradhi haya hutumia nguvu za kimaumbile au za kiutawala kuwadhalilisha wanawake kijinsia. Hawa huona raha wanapowadhalilisha wanawake kwa njia mbalimbali kama vile kuwashikashika bila ya ridhaa yao, kuwaangalia kwa jicho la fitna,a u kuwatolea lugha za kejeli na kuwaita majina yasiyofaa. Wengi katika hawa hufikia hatua ya kuwabaka wanawake kwa kuwakomoa tu au kuwadhalilisha, au ukomo wa raha yao huja pale wanapomfanyia mwanamke jambo linalomuudhi au kumuumiza. Hili ni kundi la wagonjwa mahututi. 
Kundi jingine ni la wanaume ambao, japo hawashiriki moja kwa moja katika udhalilishaji, hufurahia mwanamke anapodhalilika au kudhalilishwa kijinsia. Hawa husifia vitendo vichafu walivyofanyiwa wanawake, na huona waliofanya hivyo ndio wanaume. Mara nyingi unaweza ukawakuta vijana wahuni wakipongezana na kuwahadithia wenzao kwa ushabiki na furaha jinsi mwanamke fulani alivyodhalilishwa kijinsia, kwa kubakwa na kundi la wanaume, au kufanyiwa tendo lolote la kinyama na kihayawani. 
Mfano mwingine wa watu wenye maradhi haya ni wale wanaoshangilia kuona mwanamke anadhalilika kijinsia, labda kwa bahati mbaya. Kwa mfano, mwanamke anaweza kujikwaa na kuanguka kiasi cha kuonekana baadhi ya sehemu za siri na utakuta kundi la vijana (na wengine watu wazima) wakitoa mayowe na vifijo, wengine wakipiga miluzi kushabikia yaliyotokea. 
Au mfano mwingine ni pale labda mwanamke mgonjwa wa akili anapovua nguo na kutembea wazi, panapotokea wasamaria wema kumhifadhi utakuta wenye maradhi haya ya Sexual Sadism hukasirika wakilaumu kuwa wameondolewa sinema ya bure. 
Wapo wanawake vile vile wenye maradhi haya, japo wao mara nyingi hawawezi kutumia mabavu 
kuwadhalilisha wanaume. Baadhi yao ni wale ambao hujitoa nje katika hali ambayo wanajua kwamba wanaume watakaowaangalia watateseka kimaumbile. Hawa ni wendauchi ambao kwa makusudi hutumia maumbo yao kuwatesa wanaume majiani na mabarazani. 
Wendawazi hawa vile vile ni chanzo cha matukio mengi ya ubakaji, kwani wanaume wengine hushindwa kuendelea kuvumilia hali iliyosababishwa na uvaaji na uchochezi wa mwendawazi yule. Hivyo wabakwao wengi huanza kuwabaka wabakaji kisaikolojia. Jamii ya Kiislamu husalimika na maradhi haya kwa kusisitiza stara (hijab) kwa wanawake na wanaume. 
Ama suala zina la ugonjwa huu wa Sexual Sadism kunakuwa hakuna dawa kwa jamii kama hii yetu, yenye mfumo wa maisha wa kikafiri (kufru culture) ambapo hakuna sheria inayoongoza mahusiano ya wanaume na wanawake. Kila mmoja anadai uhuru wa kujiamulia mambo, kwa hiyo uhuru huo umetoa mwanya kwa wadhalilishaji kuwa huru kuwadhalilisha wenzao. Uislamu pekee ndio kinga dhidi ya Sexual Sadism na maradhi kama hayo. 
Jambo la kwanza, Uislamu hauruhusu michanganyiko ya holela ya wanaume na wanawake wasio ndugu. Hii hupunguza fursa (opportunity) ya watu wa jinsi tofauti hata kuongea, zaidi ya salamu ya amani. 
Pili, Uislamu unamtetea mwanamke hata anapokuwa amesingiziwa tu kuwa amefanya uovu. Msingiziaji hutakiwa apewe adhabu ya viboko themanini vya nguvu ( Qur’an 24:4). 
Tatu, Sheria ya Kiislamu ina adhabu kali dhidi ya wazinifu. Leo hii wadhalilishaji ni wengi kwa vile uzinifu umepewa leseni na umekuwa sio dhambi. Lakini kama wazinifu wangekomeshwa, wadhallishaji, wenye maradhi ya Sexual Sadism wangetokea wapi? 
Nne, wanawake na wanaume wamekatazwa hasa kudhalilishana. (49:11) 
Tano, Uislamu unakataza hata kukodoleana macho yanayoweza kuleta fitna, kwa kuwaambia wanaume na wanawake washushe macho yao chini (Qur’an 24:30) 
Sita, Uislamu umemtaka mwanamke ajihifadhi. Katika Uislamu mwili wote wa mwanamke ni uchi, isipokuwa uso na viganja. Hivyo mwanamke wa Kiislamu hawezi kuwadhalilisha wanaume, na ni vigumu kwake kudhalilika: 
Aya: "Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako na wanawake wa Kiislamu, wajiteremshie vizuri nguo zao. Kufanya hivyo kutafanya wajulikane (kuwa ni watu wa heshima) na wasiudhiwe..." (33:59) 
Kwa ujumla, jamii kufuata Uislamu ni kusalimika na kila janga la ulimwengu huu, hasa yale yanayosababishwa na sisi wenyewe kwa matendo yetu. Hivyo janga la kudhalilishana kijinsia vile vile litaondoka kwa kufuata sheria za Kiislamu.

FROTTEURISM
Hapo juu tuliangalia maradhi yaitwayo Sexual sadism yaani mtu wa jinsia moja anapoona raha kuona mtu wa jinsia nyingine akidhalilika au kudhalilishwa kijinsia. Sasa tuangalie maradhi mengine, ambayo pia huathiri maeneo ambayozinaa imeachwa huru kwa watu. Maradhi haya ni Frotteurism, yaani maradhi ya mtu kupenda kugusa, kushika au kujiminya (kujigandamiza) kwa mtu au watu wa jinsia tofauti na yeye - Wenye maradhi haya hupendelea michanganyiko ya kiholela ya wanaume na wanawake, na hawa hupenda sana miminyano ya kwenye mabasi, kwenye lifti za kupandia magorofani au sehemu zenye mikutano ya watu wengi, au hata kwenye foleni za huduma. 
Katika jamii yetu, maradhi haya yameanza kuingia kwa kasi kama ilivyokuwa kule Ulaya na Marekani. Wale wenye tabia ya kusoma magazeti wanakumbuka miaka michache iliyopita watu kadhaa walifikishwa mahakamani baada ya kukamatwa na kosa la kujiminya kwa wanawake hadi kufikia hatima ya kukidhi haja zao za kimaumbile. Maradhi haya huwatokea wanaume na wanawake kadhalika. 

Wanaume wenye maradhi haya katika nyoyo zao wana tabia kwanza kabisa ya kuangalia wanawake wapitao na kuanza kuchunguza ramani za maumbo yao. Kwa vile haya ni maradhi ya kisaikolojia, wanaume hawa hujaribu kuvuta picha ya kuwa na mwanamke amuonaye, na picha hii humpa liwazo la kiakili kama tayari anaye, ingawaje liwazo lile halifikii ukomo au kilele chake. Mgonjwa huyu huweza hata kufunga safari, akiacha shughuli zake, kumfuatilia mwanamke mwenye umbo lililompendezea hadi mwanamke huyo atakapofika kwenye nyumba na kuingia, ndipo bwana yule hurudi alikotoka, na akiona mwingine mwenye umbo lililomvutia huanza safari. Wanaume hawa ili kuficha maradhi yao, ukiwauliza wanaenda wapi, kwa vile wanajua hawana wanapokwenda zaidi ya kuvutwa na uhayawani wao, huwa na lugha ya "kunyoosha miguu". 
Tabia hii ndiyo huwafikisha watu kwenye Frotteurism na kuanza tabia ya kuwashika watoto wa kike na wake za watu.
Kesi nyingi za mahakamani sasa hivi ni za wanaume kuwatomasa wanawake bila ya ridhaa yao.
 Hawa ni wale wanaume ambao hawana nia ya kuwadhalilisha wanawake, bali roho zao hufurahi tu sehemu ya miili yao inapogusana na mwanamke. Wagonjwa hawa ni hatari kwa sababu saa nyingine maradhi yao huyapeleka hata kwa watoto wadogo wa kike, wakijifanya kucheza nao, hata kuwabeba na kuwabusu, kumbe hukidhi haja zao.
Tahadhari sana na mtu mzima mwenye tabia ya kuwaita mabinti "mchumba", wengine ni wagonjwa hawa. 
Wagonjwa mahututi ni wale sasa wenye kupenda kuminyana kwa mfano siku hizi kwenye madaladala wake kwa waume hukubali tu makondakta wanapowaambia wabanane. Utamkuta mtu mwingine ni mnene, na anapoambiwa akae anaona hapamtoshi, pakiwa na madume wenzake, atagoma kukaa, lakini kama ni wanawake atakwenda aminyane nao. Atajitia kulaani, lakini ndani ya moyo wake anaona raha. Vile vile wanaume wanaweza kuwa wamekaa kwenye siti, nafasi imebaki ndogo.
Akija mwanaume mwenzao, wanakuwa wakali kusogea, lakini akija mwanamke wanakuwa wepesi kuminyana ili nafasi kwake ipatikane. Na ukizingatia mambo ya wanawake sehemu za makalio huwa kubwa kuliko wanaume, basi wagonjwa hawa hufurahi zaidi mminyano unapozidi. 
Kama basi limejaa na watu wamesimama, hapo ndio utaona fedheha. Watu wameminyana, wake kwa waume, lakini kwa wenye maradhi ndio huona raha na ndio maana wengine yamewatokea kama ya wale waliopelekwa mahakamani. Wale walioshikwa ni wachache tu, wengi huteremka mabasi bila ya kujulikana hali zao. 
Kawaida ya utamaduni wa kikafiri (kufru culture) ni kutumia maradhi ya watu katika kupata faida. Ndio maana wenye kuchezesha madisko hutangaza "wanawake kuingia bure" kwenye madisko kule ndio wenye maradhi haya wako wengi, maana huko hukosi wa kuminyana naye, hata kama humjui atokako. Kwa hiyo waminyanaji wengi utawakuta kwenye majumba yanayoitwa ya starehe. Kuongezeka kwa madanguro haya na makasino kwenye jamii yetu ni dalili ya wazi kwamba waminyanaji (frotteurs) wameongezeka mno. 
Wanawake pia huugua maradhi haya ya uminyanaji kupenda tu kuminya minya kwa wanaume. Dalili ya mwanamke mminyaji ni kuwa na macho juu, na haoni haya kujichomeka au kupita na kupigana vikumbo vikumbo na wanaume. Halafu huona tabu kukaa kwenye vikao ambavyo wanaume na wanawake wametenganishwa. 
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba mzazi anaweza akawa na imani na shule ambayo kampeleka mtoto wake, kuwa ni shule ya wasichana watupu, au wavulana watupu, akadhani kuwa mtoto wake yuko salama, lakini shule hizi za watoto wa jinsi moja zina siku zao maalumu, wasichana wanapelekewa wavulana wa shule nyingine, au wavulana wanapelekewa wasichana, halafu wanacheza disko tena usiku. Siku hiyo ya disko ulinzi unakuwapo mkali ili wavulana na wasichana hao "wasitende dhambi", wacheze tu, kwa hiyo usiku kucha wavulana na wavulana watakumbatiana, kuminyana na kutomasana. Haya ndiyo wanayofundishwa watoto. Utakuta mwalimu wa mambo ya starehe amekaa na wasichana wanajadili eti wasichana wanataka waletewe wavulana wa shule gani. Je, hapa hatutengenezi jamii ya waminyanaji? 
Rafiki yangu mmoja, Mkristo safi, alinishutumu kwa kusema dini yetu, Uislamu ina ubaguzi, eti hata kwenye ibada tunawatenga wanawake, wao hukaanao bega kwa bega Kanisani kwa jina la Bwana. Alitaka nimpe sababu za sisi kuwaficha wanawake nyuma ya pazia hata kwenye ibada. 
Nilimueleza kuwa katika dini zote, Uislamu ndio unaofuata amri za Mungu kimatendo. Kwa mfano, amri ya kuiepuka zinaa ilikuja kwa manabii wote. Tukianza kwa Musa, katika amri kumi imo ile inayosema "usizini". Yesu alipokuja akasisitiza kuwa, imeandiwa usizini, lakini si hivyo tu, bali hata kuangalia kwa jicho la matamanio nako pia ni kuzini. Muhammad (s.a.w.) akaja na "Laa Taqrabuz-Zinaa" yaani usiikurubie zinaa. 
Nikamuuliza swali yule rafiki yangu. Kama kuangalia kwa tamaa pia ni kuzini, basi sisi tunazini sana, barabarani, sokoni n.k. Je? Tuzini hadi kwenye nyumba za Ibada? Ndipo wanaume na wanawake wanapotengana angalau kwa wasali kwa unyenyekevu. 
Hivyo, kuhamasisha wake kwa waume wasio ndugu kukaa mbalimbali kutapunguza wimbi la maradhi ya kupenda kuminyana minyana yaaniFrotteurism.  

FROTTEURISM
 Hapo juu tuliangalia maradhi yaitwayo Sexual sadism yaani mtu wa jinsia moja anapoona raha kuona mtu wa jinsia nyingine akidhalilika au kudhalilishwa kijinsia. Sasa tuangalie maradhi mengine, ambayo pia huathiri maeneo ambayozinaa imeachwa huru kwa watu. Maradhi haya ni Frotteurism, yaani maradhi ya mtu kupenda kugusa, kushika au kujiminya (kujigandamiza) kwa mtu au watu wa jinsia tofauti na yeye - Wenye maradhi haya hupendelea michanganyiko ya kiholela ya wanaume na wanawake, na hawa hupenda sana miminyano ya kwenye mabasi, kwenye lifti za kupandia magorofani au sehemu zenye mikutano ya watu wengi, au hata kwenye foleni za huduma. 
Katika jamii yetu, maradhi haya yameanza kuingia kwa kasi kama ilivyokuwa kule Ulaya na Marekani. Wale wenye tabia ya kusoma magazeti wanakumbuka miaka michache iliyopita watu kadhaa walifikishwa mahakamani baada ya kukamatwa na kosa la kujiminya kwa wanawake hadi kufikia hatima ya kukidhi haja zao za kimaumbile. Maradhi haya huwatokea wanaume na wanawake kadhalika. 
Wanaume wenye maradhi haya katika nyoyo zao wana tabia kwanza kabisa ya kuangalia wanawake wapitao na kuanza kuchunguza ramani za maumbo yao. Kwa vile haya ni maradhi ya kisaikolojia, wanaume hawa hujaribu kuvuta picha ya kuwa na mwanamke amuonaye, na picha hii humpa liwazo la kiakili kama tayari anaye, ingawaje liwazo lile halifikii ukomo au kilele chake. Mgonjwa huyu huweza hata kufunga safari, akiacha shughuli zake, kumfuatilia mwanamke mwenye umbo lililompendezea hadi mwanamke huyo atakapofika kwenye nyumba na kuingia, ndipo bwana yule hurudi alikotoka, na akiona mwingine mwenye umbo lililomvutia huanza safari. Wanaume hawa ili kuficha maradhi yao, ukiwauliza wanaenda wapi, kwa vile wanajua hawana wanapokwenda zaidi ya kuvutwa na uhayawani wao, huwa na lugha ya "kunyoosha miguu". 
Tabia hii ndiyo huwafikisha watu kwenye Frotteurism na kuanza tabia ya kuwashika watoto wa kike na wake za watu. Kesi nyingi za mahakamani sasa hivi ni za wanaume kuwatomasa wanawake bila ya ridhaa yao. Hawa ni wale wanaume ambao hawana nia ya kuwadhalilisha wanawake, bali roho zao hufurahi tu sehemu ya miili yao inapogusana na mwanamke. Wagonjwa hawa ni hatari kwa sababu saa nyingine maradhi yao huyapeleka hata kwa watoto wadogo wa kike, wakijifanya kucheza nao, hata kuwabeba na kuwabusu, kumbe hukidhi haja zao. Tahadhari sana na mtu mzima mwenye tabia ya kuwaita mabinti "mchumba", wengine ni wagonjwa hawa. 
Wagonjwa mahututi ni wale sasa wenye kupenda kuminyana kwa mfano siku hizi kwenye madaladala wake kwa waume hukubali tu makondakta wanapowaambia wabanane. Utamkuta mtu mwingine ni mnene, na anapoambiwa akae anaona hapamtoshi, pakiwa na madume wenzake, atagoma kukaa, lakini kama ni wanawake atakwenda aminyane nao. Atajitia kulaani, lakini ndani ya moyo wake anaona raha. Vile vile wanaume wanaweza kuwa wamekaa kwenye siti, nafasi imebaki ndogo. Akija mwanaume mwenzao, wanakuwa wakali kusogea, lakini akija mwanamke wanakuwa wepesi kuminyana ili nafasi kwake ipatikane. Na ukizingatia mambo ya wanawake sehemu za makalio huwa kubwa kuliko wanaume, basi wagonjwa hawa hufurahi zaidi mminyano unapozidi. 
Kama basi limejaa na watu wamesimama, hapo ndio utaona fedheha. Watu wameminyana, wake kwa waume, lakini kwa wenye maradhi ndio huona raha na ndio maana wengine yamewatokea kama ya wale waliopelekwa mahakamani. Wale walioshikwa ni wachache tu, wengi huteremka mabasi bila ya kujulikana hali zao. 
Kawaida ya utamaduni wa kikafiri (kufru culture) ni kutumia maradhi ya watu katika kupata faida. Ndio maana wenye kuchezesha madisko hutangaza "wanawake kuingia bure" kwenye madisko kule ndio wenye maradhi haya wako wengi, maana huko hukosi wa kuminyana naye, hata kama humjui atokako. Kwa hiyo waminyanaji wengi utawakuta kwenye majumba yanayoitwa ya starehe. Kuongezeka kwa madanguro haya na makasino kwenye jamii yetu ni dalili ya wazi kwamba waminyanaji (frotteurs) wameongezeka mno. 
Wanawake pia huugua maradhi haya ya uminyanaji kupenda tu kuminya minya kwa wanaume. Dalili ya mwanamke mminyaji ni kuwa na macho juu, na haoni haya kujichomeka au kupita na kupigana vikumbo vikumbo na wanaume. Halafu huona tabu kukaa kwenye vikao ambavyo wanaume na wanawake wametenganishwa. 
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba mzazi anaweza akawa na imani na shule ambayo kampeleka mtoto wake, kuwa ni shule ya wasichana watupu, au wavulana watupu, akadhani kuwa mtoto wake yuko salama, lakini shule hizi za watoto wa jinsi moja zina siku zao maalumu, wasichana wanapelekewa wavulana wa shule nyingine, au wavulana wanapelekewa wasichana, halafu wanacheza disko tena usiku. Siku hiyo ya disko ulinzi unakuwapo mkali ili wavulana na wasichana hao "wasitende dhambi", wacheze tu, kwa hiyo usiku kucha wavulana na wavulana watakumbatiana, kuminyana na kutomasana. Haya ndiyo wanayofundishwa watoto. Utakuta mwalimu wa mambo ya starehe amekaa na wasichana wanajadili eti wasichana wanataka waletewe wavulana wa shule gani. Je, hapa hatutengenezi jamii ya waminyanaji? 
Rafiki yangu mmoja, Mkristo safi, alinishutumu kwa kusema dini yetu, Uislamu ina ubaguzi, eti hata kwenye ibada tunawatenga wanawake, wao hukaanao bega kwa bega Kanisani kwa jina la Bwana. Alitaka nimpe sababu za sisi kuwaficha wanawake nyuma ya pazia hata kwenye ibada. 
Nilimueleza kuwa katika dini zote, Uislamu ndio unaofuata amri za Mungu kimatendo. Kwa mfano, amri ya kuiepuka zinaa ilikuja kwa manabii wote. Tukianza kwa Musa, katika amri kumi imo ile inayosema "usizini". Yesu alipokuja akasisitiza kuwa, imeandiwa usizini, lakini si hivyo tu, bali hata kuangalia kwa jicho la matamanio nako pia ni kuzini. Muhammad (s.a.w.) akaja na "Laa Taqrabuz-Zinaa" yaani usiikurubie zinaa. 
Nikamuuliza swali yule rafiki yangu. Kama kuangalia kwa tamaa pia ni kuzini, basi sisi tunazini sana, barabarani, sokoni n.k. Je? Tuzini hadi kwenye nyumba za Ibada? Ndipo wanaume na wanawake wanapotengana angalau kwa wasali kwa unyenyekevu. 
Hivyo, kuhamasisha wake kwa waume wasio ndugu kukaa mbalimbali kutapunguza wimbi la maradhi ya kupenda kuminyana minyana yaaniFrotteurism.

Exhibitionism
Hapo juu tutayachambua maradhi mengine yaitwayo
 Exhibitionism. Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huona raha kuonekana sehemu zake za mwili zisizotakiwa kuonekana. Hawa ndio wale tunaowaita kwa Kiswahili rahisi wendawazimu au wendauchi. Kitaalam mgonjwa huyu anaitwaExhibitionist.
Tutakumbuka kwamba katika matoleo ya nyuma ya gazeti hili tulichambua maradhi yaitwayo Voyeurism yaani mtu kupenda kukodolea macho watu ambao wako faraghani na hawana nguo (makozimeni). Hivyo hawa wagonjwa tunaowachambua leo hukidhi sana haja za ma-Voyeur (Keeping Toms). Kwani wengi wao ndio wale wanaotokea kwenye sinema za X, kwenye kanda za video zinazoonyesha ufuska, pamoja na kwenye magazeti yenye picha za wendawazimu (Ponographic magazines). 
Maradhi haya ya wendawazimu yameanza kuingia kwa kasi zaidi katika jamii yetu. 
Mara nyingi wendauchi huwa ni wanawake, ingawa na wanaume pia wapo wanaopenda kujiweka wazi waonekane na watu. 
Tukianza na wagonjwa mahututi, hawa huona raha tu watu wengine wanapoona "uwazi" wao, na roho zao hufurahi tu sehemu zao "nyeti" zinapoonekana. Kule Ulaya na Marekani, nchi ambazo zimeendelea kwa kila kitu, hadi ufuska, wendauchi wamefikia mpaka kuanzisha jumuiya zao, na wana sehemu zao maalum au kambi ambazo ukifika huko unaacha nguo mlangoni na unabaki wazi kama mnyama. Hawa wanaitwa "Nudists", na Marekani ambako kuna "uhuru" mkubwa wa kufanya mambo, kambi hizi za wenda wazi (nudist camps) zinajulikana na zinapewa baraka zote na serikali, na baadhi ya wananchama ni viongozi wakubwa wa serikali. Kuna hofu kwamba kwa vile nchi za Afrika zimekaa tayari kuiga kila kinachotendeka Ulaya na Marekani, huku kwetu nako kambi hizi zitakuja. 
Kwa hiyo kama tulivyo na mbuga za wanyama kama vile Serengeti, Manyara, Mikumi, n.k. hivi karibuni tunaweza tukawa na "mbuga za wendauchi". Nasema hivi kwa sababu madanguro (Casinoes) tayari yamo katika jamii yetu, na yamepewa leseni. 
Ugonjwa huu wa wendauchi unaongezeka kwa kasi Afrika. Kwa haraka haraka unaweza kuona hawa wendauchi wamefikia kuwekewa kumbi za kifahari, wakipita uchi mbele za mamia ya Makozimeni na mshindi wa kupewa zawadi ya mamilioni akapatikana. Haya ni mashindano ya urembo, na urembo wa mtu, hasa mwanamke ni mwili wake wote. Hivyo kuonyesha urembo ni kujiweka wazi, ukiwa umevaa vile wenyewe wanavyoviita "vichupi" hushangiliwa na kupewa zawadi, na tiketi ya kwenda Ulaya au Marekani, kuingia katika mashindano ya kimataifa ya wendawazi. Kwa hiyo, jamii yetu imefikia kutoa wendauchi mabingwa katika hadhi ya kimaaifa kwenda kugombea Uendawazi wa dunia. 
Dalili nyingine ya kuenea maradhi haya ni wendawazi kuenea kwenye matangazo ya biashara. Kama unataka bidhaa yako inunuliwe sana, basi weka picha ya mwendawazi wa kike, hata kama ni kibiriti mtu atanunua kumi akaviweke tu nyumbani. 
Dalili ya wazi nyingine ni ile ya wacheza ngoma wanaotokea kwenye video. Utakuta bendi ya muziki wanaume wote wamejisitiri tena kwa mashati na masuruali mapana kabisa, lakini wanawake wanenguaji wako wazi, na wanaona raha tu kuonekana hivyo. 
Mitaani ndio kumejaa hasa ma-Exhibitionist, hasa wa kike, ambao wanavaa visuruali vyembamba kama ngozi (skin tight). Sasa hao ndo wenye nafuu. Kuna wale ambao wanashona visketi vifupi, halafu ufupi wa visketi vyao hauwatoshi, wanaongeza kupasua nyuma. Hawa mimi huwafananisha na mbuzi ambaye kapewa kamkia kafupi, halafu kamkia kenyewe badala ya kulala chini kamhifadhi, kamekaa wima, kwa hiyo kanamuacha mbuzi wazi kabisa bila ya stara kama aliyonayo kondoo. 
Wanaume nao wapo wenye maradhi haya. Utamkuta mwanamume kavaa Kibukta , nywele zote za kifuani, tumboni na mapajani ziko nje, wala hashituki eti anapunga upepo. Wengine utawakuta mitaani na hivyo vibukta vyao, wala hawaoni tabu, ili mradi raha yake ni aonekane alivyotunisha misuli ya mapaja yake. 
Madhara ya Exhibitionism 
Uislamu dini iliyopo kwa maslahi ya wanaadamu unapokataza jambo basi ni lazima lina madhara kwa jamii. Sasa hivi duniani kuna maradhi yameingia, kwani tunaambiwa kuna dawa ya kuongeza nguvu za kiume inaitwa VIAGRA. Watu wanaishangilia bila kujua sababu ya kuja dawa hii. Dawa hii imekuja kwa vile wanaume wabovu wanaongezeka. Ubovu huu wa kupoteza ngvu za kijinsia unasababishwa zaidi na watu kuwa na tabia ya kwenda uchi. Sasa hivi imekuwa ni kawaida kwa mwanamke kupita mapaja wazi na wanaume wengi hawashituki. Yaani kumuona mwanamke yuko wazi ni kama kumuona mbuzi tu. Limekuwa ni suala la kawaida. Ule msisimko wa mtu kumuona mtu wa jinsia nyingine umekwisha. 
Nasaha 
Kwa kina dada: Kila kitu kina stara yake, hata ndizi. Ndio maana wauza ndizi huwa hawazimenyi kwanza ndio wakaziuza kwa sababu wanajua hakuna atakayezinunua, bali zitang’ong’wa na mainzi. Hivyo hivyo, wale wanawake waliojitoa stara ndio kama ndizi zinazotembezwa zikiwa zimemenywa. Sasa wale wanaowashangilia wakipita uchi si watu bali ni mainzi yanawang’ong’a. Msijidhalilishe kwa kujiweka wazi. 
Kwa Waislamu wote: Moja kati ya tofauti ya wanyama nawatu ni kuvaa nguo (kujistiri). Kila unavyozidisha stara, ndivyo unazidisha tofauti yako na mnyama. Na kila unavyopunguza stara ya mwili wako ndio unaukaribia unyama zaidi, yaani unapunguza ule utofauti wako na mnyama. Uislamu ndio unasisitiza stara ili kuwafanya binadamu wawe watu. Ndipo Mwenyezi Mungu akatuambia kwenye Qur’an: 
"Enyi wanadamu! Tumewaletea (tumewajaalia) nguo za kuficha utupu wenu (uwazi wenu) na za mapambo na zile za ucha Mungu. Hizo za ucha Mungu (utawa) ndizo bora zaidi. Hayo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu, ili (watu) wapate kukumbuka jukumu lao kama watu". (Qur’an 7:26)  

FETISHISM 
KATIKA toleo lililopita tulichambua aina ya maradhi ya Paraphilia yaitwayo Exhibitionism, yaani mtu kupenda, au kuona raha sehemu zake nyeti za mwili zinapokuwa wazi zikionekana na watu.

Sasa tuichambue
 Paraphilia nyingine iitwayo Fetishism. 
Fetishism ni maradhi anayokuwa nayo mtu aliyeelemewa na mawazo ya ngono hadi kuwa na tabia ya kupenda vitu ambavyo anavihusisha na mtu wa jinsia tofauti na yake. Kwa tafsiri finyu, mtu mwenye maradhi haya hususan mwanaume huwa na mapenzi na vitu vinavyohusiana na mtu mwingine, hususan mwanamke, kama vile nguo za ndani au hata viatu. Mtu huyu akiviona vitu hivi anaweza kuvifuga nyumbani kama ambavyo watu hufuga ndege. 
Kama ni nguo ya ndani, labda iliyosahauliwa bafuni au iliyoanikwa, au hata iliyochorwa tu kwenye picha, au iliyotundikwa dukani ikiuzwa, basi humsisimua na kumfanya katika mawazo yake kuona zaidi ya kile anachokiona wakati huo. 
Mgonjwa wa maradhi haya anaitwa Fetishist, na vile vitu vinavyomvutia vinaitwa Fetish. 
Kwa tafsiri pana, Fetishism ni maradhi ya kujawa na wazo la zinaa kwa kupitia kitu (Fetish) fulani. Ukiacha tafsiri za kwenye vitabu, ambazo zinachukulia Fetish kuwa ni nguo za ndani tu au vitu, kwa upana wake, Fetish ziko nyingi mno. Tukitoa Fetish hizi, nguo za ndani na viatu, nitaziorodhesha Fetish nyingine ambazo huwaathiri wagonjwa hawa. 
Umbile la mwili la aina fulani pia linaweza kuwa ni kivutio (Fetish) kwa Fetishist. Umbile hili ni la mwili, kwa mfano wanawake wenye maumbo makubwa hasa sehemu za makalio huwa ni Fetish nzuri sana kwa wagonjwa hawa, na ndio maana magazeti ya habari za kipuuzi na ngono ambayo sasa hivi yamejaa katika jamii yetu na yanapendwa mno na wenye maradhi haya, huwa na picha za kuchora zenye wanawake wenye makalio makubwa kupita kiasi ili picha iwe na mvuto fulani. Stara ya Hijab humsaidia mwanamke asiwe ni Fetish kwa wenye maradhi haya. 
Harufu: Pia inaweza ikawa ni Fetish , hususan manukato. Mara nyingi wenye maradhi haya wanaposikia harufu ya manukato inawapa hisia ya "mwanamke mzuri kama jini". Mara nyingi manukato hutumiwa na wanawake wanaopenda kujipamba wakitoka nje ili watu wawasifie au wawapende. Wanawake hawa huvaa nguo za fahari na nyingine fupi (hasa za wendawazi) na hujipaka manukato. 
Hivyo mtu anaposikia harufu ya manukato, hata kama haoni mtu, harufu hiyo humpa hisia ya wanawake walio katika hali fulani ya mvuto wa zinaa. Ndio maana wanawake wa Kiislamu huambiwa wapake kila aina ya manukato kwa ajili ya waume zao ndani, lakini wakitoka nje wanaambiwa wasijitie manukato makali, ili wasije wakawafanya watu wachemkwe kwa kupata harufu watakayoihusisha na mwanamke, hasa wale wenye maradhi katika nyoyo zao. 
Kwa wanaume wenye maradhi haya, sauti ya mwanamke pia huwa ni Fetish. Kwa kawaida sauti ya mwanamke huwa ni tofauti na ya mwanaume, kwani ya mwanamke ni nyororo. Hivyo utofauti huu humfanya Fetishist kushtuka asikiapo sauti ya mtu mke, au huburudika tu kusikia mwanamke akiongea, kulia au kuimba. Kwa tahadhari ya kuwahemsha watu wenye maradhi haya, wanawake wanaaswa kurembesha sauti zao kwa waume zao tu, na wanapoongea nje, wazikaze sauti zao, kama walivyoambiwa wake za Mtume (s.a.w.) katika Qur’an: 
"...basi msilegeze sauti, asije akatamani mtu mwenye maradhi katika moyo wake, na semeni maneno mazuri". (33:32) 
Kwa wagonjwa wengine, hata mwandiko huwa ni Fetish. Kwa kawaida, miandiko ya wanaume na wanawake huwa inatofautiana. Katika jamii yetu tumezoea kwamba mwandiko wa herufi zinazolalia kushoto ni wa kike, basi Fetishist akiwa mwanafunzi atakwambia daftari likiandikwa na mwanamke linasomeka na kueleweka vizuri zaidi. Vile vile, hawa wagonjwa hupenda marafiki wa kalamu, na wanaweka masharti kwamba rafiki huyo ni lazima awe mwanamke wa umri fulani, basi miandiko ile humridhisha, akawa hana kazi ya kufanya zaidi ya kusoma na kurudia kusoma barua za wanawake asiowajua. 
Fetish nyingine huwa ni picha, hasa za wendauchi. Wenye maradhi haya ukiingia vyumbani mwao utakuta wamebandika picha za watu waliovaa vichupi na sidiria tu. Hayo ndio mapambo waliyonayo. Pia wenye maradhi haya hupendelea magazeti ya picha za ngono (ponography), au magazeti ya upuuzi yenye manyang’unyang’u na mafindo findo na zile wanazoziita "chachandu" ili mradi maradhi haya ni kichaa cha aina fulani kilichowakumba watu wengi, wengi wao wakiwa ni wenzetu. 
Nyimbo za aina fulani pia huwa Fetish . Mara nyingi Fetishist hupenda kusikiliza na kuimba nyimbo zinazoamsha hisia za ngono. Hapa na wanawake pia wanakuwa Mafetishist . Katika jamii yetu, taarabu kwa mfano zilikuwa na nyimbo zenye mashairi mazuri yenye nasaha na maliwazo mbalimbali mazuri, lakini sasa hivi taarab imevamiwa na watu "wa kuja" ambao hawana asili na taarab, basi wamechafua taarab kwa kuingiza nyimbo za kifuska, na kwa bahati mbaya nyimbo hizo, hata redioni hazipigwi kwa ubaya wake, lakini utazikuta zinapigwa majumbani. Utamkuta mwenye maradhi kakaa anasilikiza, tena wengine na vibalaghashia vyao, anatingisha kichwa kwa raha ya wimbo wa matusi, na wanawake walio karibu, hadi mabinti wadogo nao wanaisaidia redio kaseti katika kumliwaza au kumhemsha mgonjwa. 
Sehemu ya mwili, hasa wa mwanamke, pia inaweza kuwa ni Fetish kwa wenye maradhi haya, hasa sehemu za mapaja na kifua. Hapa wenye maradhi haya hufaidi sana wanapoishi kwenye jamii yenye wendauchi. Nywele pia huwa ni Fetish ya ajabu. Utakuta wanaume wengi wa Kiafrika hupendelea nywele za Kizungu. 
Kasumba iliyojengeka miongoni mwa Waafrika malimbukeni ni kwamba kila kitu cha Kizungu ni kizuri, basi hata nywele. Kwa kujua hili, kwamba wanaume wa Kiafrika huvutiwa sana na nywele za Kizungu, ndipo wanawake wengi mno huzibadilisha nywele zao (kwa vile hufurahia kuwa Fetish Object), wakaweka dawa za ajabu ambazo nyingine huwafanya wanuke vibaya, nyingine huwanyonyoa nywele, na nywele zinaponyonyoka ndipo wanapoamua kuunganisha nywele za brashi au kuvaa manywele ya bandia (wigs). 
Ukimkuta mwanamke kavaa chupi ya mtoto ya mkojo kichwani ujue anaogopa nywele zake zikingiia maji zitaharibika na zikiharibika hawezi kuwa mteja wa Mafetishist. Mwanamke wa Kiislamu hawezi kufanywa chanzo cha starehe ya wanaume wenye maradhi ya Fetishism. Kwa hiyo huvaa hijab, inayomstiri mwili mzima, haonekani mapaja, kifua wala nywele zake. Kwa hiyo ni Uislamu tu ndio unaoweza kuleta ponyo ya maradhi haya na mengineyo.

TRANSSEXUALISM:
 Hapo juu tulizungumzia Paraphilia ijulikanayo kama Fetishism, yaani maradhi ya kisaikolojia ya mtu kupenda vitu vinavyoamsha hisia ya ngono, kama vile nguo za ndani na viatu au chochote kinachohusiana na jinsia nyingine. 
Sasa tuangalie maradhi mengine yaitwayo Transsexualism. Mwenye maradhi haya anaitwa Transsexual (inasomwa Trans - sekshual). Mgonjwa huyu huwa na tamaa ya kuwa na jinsia tofauti na ile aliyonayo, kwa mfano, mwanaume anatamani kuwa mwanamke, na mwanamke anatamani kuwa mwanaume. 
Wagonjwa wa Transsexual hufikia kiwango cha kutaka kubadilishwa maumbo yao, hata kwa njia ya operesheni au kwa kutumia madawa yanayoweza kubadilisha hali zao za asili. 
Kule Ulaya na Marekani, na sehemu nyingine zinazofuata nyayo za "maendeleo", ambako watu wamekubuhu katika fani ya ufuska, baadhi ya watu wamediriki kwenda hospitali na kufanyiwa operesheni kuondolewa sehemu zao za viungo zinazowanasibisha na jinsi yao asilia. 
Katika jamii yetu, japo hakuna hospitali za kubadilisha jinsi za watu, wapo wanaume wanaoonyesha silka za kike katika maisha yao. Mfano hai ni pale tunapowaona watu waliopewa majina ya "anti" fulani, au wale wanaoshiriki katika ngoma za "kibao kata". Hawa ni wagonjwa mahututi. 
Maradhi haya hupenyeza vile vile hadi kuingilia majukumu ya kijinsia. Kwa mfano, katika jamii yoyote ya watu waungwana, mahusiano ya ndoa huwa baina ya watu wenye jinsia tofauti, lakini tunasikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kwamba kule Ulaya, kwenye maendeleo wanaume kwa wanaume wanafunga ndoa, tena Kanisani; na vile vile mahusiano ya wanawake kwa wanawake (Lesbianism) ni jambo la kawaida lililopewa kibali na mamlaka ya nchi. 
Katika hali ya kimaumbile, viumbe hutofautiana kijinsia katika hali tatu tofauti, ambazo kitaalamu zinaitwa gender. Kuna viumbe vyenye hali ya kiume (Masculine gender), vyenye hali za kike (feminine gender) na vyenye hali haidi, yaani isiyo ya kike wala ya kiume (neutral gender).Transsexualism ni hali ya mtu kujibadilisha (kifikra au kifizikia) kutoka katika hali yake ya kijinsia ya asilia, na kujifanya kuwa na hali nyingine. Hivyo, hata kujitoa katika hali ya kike au ya kiume na kujiweka katika hali haidi (isiyo ya kike wala kiume) pia ni Transsexualism. 
Wapo wanawake, kwa mfano, waliotoka katika hali yao ya kike (feminine gender) na kuwa haidi (neutral). Hawa wamefikia hali hii baada ya kuielewa vibaya dhana ya "ukombozi wa mwanamke". 
Dhana hii ya "ukombozi wa mwanamke" ni dhana nzuri, kwani ni kweli wapo wanawake wengi wanonyanyaswa, kuonewa na kudhulumiwa kutokana na mila na mienendo ya jamii zao, lakini dhana ya "usawa" imewafanya wanawake wengi kutaka kuwa "sawa" na wanaume hata kimaumbile. 
Jamii za kinyonyaji zimechukua fursa (advantage) ya propaganda ya "usawa" wa wanawake na wanaume kwa kumtaka mwanamke amenyeke katika kazi sawa na wanaume bila ya kujali maumbile yake. Sasa hivi katika jamii yetu kumeletwa miradi mbalimbali, eti ya kuwakomboa wanawake, na kumeenezwa vitengo vinavyoshughulikia "mitandao" ya kijinsia, lakini ukweli wa mambo ni kwamba nchi hizo hizo zinazotaka kuleta ukombozi ndizo hizo zilizoleta ukoloni na zinatuletea ukoloni mamboleo, na ndizo hizo hizo zinatuletea dhana ya "ukombozi". Mimi sioni ukombozi unaofanyika zaidi ya kuwatia wanawake maradhi, hasa haya ya kisaikolojia kama vile Exhibitionism (wendawazi), Lesbianism (usagaji) na haya maradhi ya wanawake kutaka kuwa sawa na wanaume ambayo tunayaita kichaa cha kijinsia. Maradhi yanayosumbua nchi zao, na kuziparaganyisha familia zao wanaya leta huku kwetu. 
Sehemu nyingi za kikazi zilizokuwa mahsusi kwa wanaume sasa hivi zimeshikwa na wanawake, na jamii hizi zianzowafanyisha kazi wanawake sambamba na wanaume, chini ya nembo ya "usawa", hujisifia kuwa na idadi kubwa ya wanawake maofisini na viwandani, lakini watu, hata wanawake wenyewe, wamesahau kuwa mwanamke ana kazi kubwa ambayo katika Uislamu huhesabika kama Jihaad. 
Dunia leo ina mamilioni na mamilioni ya watu. Kila mwanaadamu unayemuona anatembea katika mgongo wa ardhi ni lazima alimtesa mwanamke. Mwanamke alimbeba binaadamu huyu tumboni mwake, kwa tabu na mashaka makubwa, kwa muda wa miezi tisa, na siku ya kujifungua, mwanamke alipata uchungu mkubwa unaosemekana kuwa unakaribia uchungu wa kutoka roho (na wanawake wengine hufa kwa uchungu huu). 
Baada ya hapo, mtoto anakuwa akitegemea kumnyonya mama yake kwa zaidi ya mwaka mmoja. Huyu mwanamke pia anakuwa mwalimu wa kwanza wa binaadamu. Ukifikiria yote haya ndipo inakuwepo hoja kuwa, mwanaume, ambaye hapati tabu katika mahusiano yake na mwanamke, zaidi ya raha za kimapenzi, inabidi yeye ndiye ahenyeke kwa uchungu na ugumu wa kazi za uzalishaji mali katika jamii, lakini mtu anang’ang’ania wanawake wawe sawa na wanaume katika uzalishaji mali, wakati yeye mwanaume hawezi kuwa sawa na wanawake katika uzalishaji watu. 
Kwa vile wanawake wamevamia uwanja wa uzalishaji mali sawa na wanaume, basi wengi wao wanaona iko haja ya kuepuka jukumu lao la kuzaa watoto, ili waweze kufanya kazi kwa nafasi, sawa na wanaume. Basi wanawake hawa hukwepa uzazi (asili yao) kwa kuzuia mimba, kunyofoa mimba au kuua watoto, maana wasiposhika mimba kama wanaume wasivyoshika mimba ndio watakuwa wachapakazi wazuri. Matokeo yake, wanawake wanatoka kwenye uanauke na kuwa hawawezi kuwa wanaume, wanabakia kuwa haidi (neutral). 
Kwa vile wanaume nao eti wanachangia sana katika "kuharibu" ufanisi wa wanawake, nao wanapigwa propaganda hadi wanakubali kufungwa kizazi. Utakuta mwanaume anafunga kizazi, eti kwa kuogopa "kumuathiri" mke wake. Basi mwanaume huyu naye huenda hospitali, akaonyoosha miguu, na wanaume wenzake wakamuondoa uwezo wake wa kuzaa. Anakubali kuwa haidi. Mwanaume anayejitoa uanaume kwa kuogopa kumzalisha mwanamke, ni wa ajabu sana. Kwa vile anajibadilisha kuwa haidi, basi na yeye anakuwa ni Transsexual, kwa vile kajitoa silka ya uume (masculinity) akajitia au akatiwa uhaidi (neutrality). 
Kuna suala la kuwa na mke zaidi ya mmoja, ambalo pia hupigiwa kelele. Eti watu hung’ang’ania usawa, mume mmoja kwa mke mmoja (one-to-one-function). Suala la kuzingatia hapa ni kwamba, kuhusu uzazi, mwanamke ana uwezo wa kushika mimba ya mwanaume mmoja tu kwa mwaka mzima (miezi tisa ya kubeba mimba na angalau miezi mitatu ya kunyonyesha kabla ya hali ya kubeba mimba nyingine haijawa tayari). Lakini mwanaume, katika mwaka huo mmoja ana uwezo wa kuwapa mimba wanawake wengi mno. Mwanaume mwenye nguvu anaweza kuwapa mimba hata wanawake watatu kwa siku moja. 
Lakini tumchukue mwanaume dhaifu, ambaye anaweza kumpa mimba mwanamke mmoja kila siku, ambaye yuko katika hali ya kuweza kushika mimba. Kwa hiyo, kwa wiki anaweza kuwapa mimba wanawake saba. Kwa mwezi wanawake 28. Kwa hiyo kwa mwaka, kama kila mwanamke atakayekutana naye atakuwa katika siku muafaka, ataweza kuwapa mimba wanawake 330 (28 mara miezi 12). 
Hivyo kinadharia, kama kungekuwa na kazi maalum ya kuzaa ili kuijaza watu jamii fulani yenye hatari ya kutoweka, basi mwanaume mmoja anahitaji wanawake 330 kwa mwaka, wakati mwanamke mmoja anahitaji mwanaume mmoja tu kwa mwaka. Sasa kutaka mwanaume awe na mke mmoja tu, hata kama kuna sababu ya kuongeza mwingine, angalau mmoja ni kubadilisha jinsi ya mwanaume . Na hii ni kumgeuzaTranssexual. Kimaumbile, mwanaume anahitaji zaidi ya mke mmoja, ibaki matashi yake tu na sababu nyingine za kiuwezo. 
"Usawa" na uwepo, lakini tusibadili asili ya maumbile ya mtu. Shetani hupenda kuwashawishi watu wabadilike kinyume na Mwenyezi Mungu anavyowataka wawe, ndio maana akasema: 
"Na nitawapoteza na nitawatumainisha na nitawaamrisha (ninavyotaka mimi) ... na nitawaamuru, nao watabadili umbile la Mwenyezi Mungu (alilowapa)..." (Qur’an 4:119) 
Waislamu tunatakiwa tuwe na msimamo wa Nabii Mussa, alipomjibu Firauni, kwa kumwambia: "Mola wetu ni yule aliyekipa kila kitu umbo lake kisha akakiongoza (kufuata kinachoafiki umbo lake hilo)". (Qur’an 20:50) 

 TRANSVESTISM
Hapo juu tuliyachambua maradhi yaitwayo Transsexualism, yaani kichaa cha mtu kupenda kuwa na silka au umbile la mtu wa jinsia tofauti na yeye, kwa mfano mwanaume kuwa na shauku ya kupata silka au umbile la kike, au mwanamke kuwa na shauku ya kupata silka au umbo la kiume.
Sasa tuangalie maradhi mengine yaitwayo Transvestism. Haya ni maradhi au kichaa cha mtu kupendelea mavazi au mapambo ya watu wa jinsia nyingine. Maradhi haya hurandana sana na yale ya Transsexualism, lakini wengi pia hupenda kujipamba kwa vipambo vya watu wa jinsia nyingine bila ya wao kuwa na silka za watu hao. Haya ni maradhi ya mwanaume kupenda kuvaa nguo au mapambo ya kike, au mwanamke kupenda kuvaa nguo za kiume. Mwenye maradhi haya huitwa Transvestite. (Husomwa Transevestait) 
Wenye maradhi haya walio wengi ni wanawake, hawa wale tuliowaelezea katika toleo lililopita kuwa wameielewa vibaya dhana ya "usawa". Ni nadra kumkuta mwanaume amevaa sketi na blauzi, lakini siku hizi tunawaona wanaume waliotoboa masikio na kuvaa hereni, na wengine huacha vifua wazi ili mikufu yao ya dhahabu ionekane. 
Wagonjwa wengi wenye maradhi haya wako kule Ulaya na Marekani. Wagonjwa walio huku kwetu mara nyingi huambukizwa maradhi haya kwa kupitia Mavazi mapachiko (Programmed Mind) kwamba chochote wanachokifanya watu wa Ulaya na Marekani ndiyo maendeleo, kwa hiyo vijana huiga yanayoonekana kwenye televisheni hata kama yanafanywa na wanaume mashoga. Hivyo, Trasvestite wengi wa humu kwetu huwa na maradhi mengine yanayoitwa Copycatism, ugonjwa wa kuiga bila ya kuelewa maana ya kinachoigwa. 
Wagonjwa wa kike wa maradhi haya mara nyingi huwa na michanganyiko ya maradhi. Mwanamke anayevaa nguo za kiume, hasa makaptula au suruali na shati, mara nyingi huwa na maradhi ya Sexual Sadium, kwa kupenda wanaume wahemkwe kwa umbile lake popote anapopita, kwa vile huziacha wazi sehemu zake za mvuto. Pili, mgonjwa huyu wa kike pia yawezekana kuwa ameathirika na wazo mpachiko la kuwa "sawa" na wanaume, kwa hiyo labda yeye ni Transsexual, na tatu inawezekana kuwa ni miongoni mwa malimbukeni ambao wako ndani ya hali ya kuchanganyikiwa kiasi cha kutojielewa afuate mila gani (Identity Crisis) na ndipo wanaishia kuwa Copycats kila siku wanaangalia Mzungu kavaaje ili na yeye avae hivyo. Kwa hiyo siku Mzungu akivaa gunia basi na yeye unaweza kumkuta mitaa ya Tandale akichagua magunia matupu akashone vazi aliloliona kwenye kabati la picha (tv). Wagonjwa wengine hurithishwa tabia ya kuvaa kiume tangu wadogo, hivyo wazazi malimbukeni huchangia sana katika kutengeneza jamii ya ma-Transvetite. Mara nyingi watoto wa kike tu ndio huzoeshwa kuvaa mavazi ya kiume, lakini sijapata kuona watoto wa kiume(waliofikia umri wa kukimbia) wakivalishwa vigauni au wakatogwa masikio. 
Wanaoshangaza zaidi ni wale wagonjwa wa kiume wanaotoga masikio na kuvaa hereni na vidani. Hawa nao huenda ni Transsexuals, wana shauku ya kuwa wanawake, ila tu kwa bahati mbaya huku kwetu hakuna hospitali za kufanyia operesheni, pengine wangependa kubadilishwa viungo vyao vya mwili vinavyowafanya wanaume. Kama sio madume jike (transsexuals) basi ni malimbukeni waliopapia miji. Au wako kwenye vurugu la mawazo ua kujitambua (identity crisis). Au pengine labda ameona wanawake wamependelewa kwa kuachiwa wapendeze peke yao, kwa hiyo na yeye anataka apendeze kama dada zake, au mabinti wa jirani. Cha kumuuliza ni: Unataka upendeze kama akina dada ili iweje? Halafu ukishapendeza watu wakikupenda, wafanyeje? Labda walete posa! 
Uislamu umechukua zaidi tahadhari kwa wanawake Waislamu wasije wakawaiga majahili katika kujipamba, kwa kuwaambia: 
"... Wala msijipambe kujipamba kwa majahili waliopita (yaani msiwaige majahili)" (33:33). 
Huyu Transvestite wa kiume sijaipata aya yake, nadhani haipo kwa sababu, labda haitegemewi kabisa mwanaume kujifananisha na mke au kuvaa kike. Lakini Abu Hurairah amesema kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.) amewalaani wanaume wanaovaa mavazi ya kike na wanawake wanaovaa mavazi ya kiume. (Abu Daud). 

PEDOPHILIA
Tuyaangalie maradhi yaitwayo Pedophilia. Maradhi haya ni ya mtu mzima (hususan aliyepea kiumri, yaani mtu wa makamo au mzee) kupenda mahusiano ya kijinsia na watoto wadogo, hususan wale ambao hawajafikia balegh. Tafsiri hii ni ya kawaida iliyozoeleka lakini kwa undani zaidi, Pedophilia ni maradhi aliyonayo mtu yeyote ambaye ni balegh, anayependelea mahusiano na mtu wa jinsia nyingine ambaye hajafikia balegh. 
Wagonjwa wa maradhi haya mara nyingi wanakuwa wanaume, ingawaje wapo wanawake ambao hujihusisha na kuwaghilibu watoto katika masuala ya maasi ya zinaa. 
Katika jamii yetu, maradhi haya yameenea kwani ni mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia au kusikia na kusoma habari kwamba mtoto mdogo, na wakati mwingine hata mtoto mchanga amenajisiwa. 
Nini chimbuko la maradhi haya au tuseme maovu haya? 
Jamii yetu hivi sasa imekumbwa na wimbi la wale wanaodhani mwanadamu yupo hapa duniani ili ale vizuri zaidi, anywe kwa israf, alale pazuri na avae vizuri zaidi. Ufupi wa maneno apate kustarehe. 
Dhana hii huendana na dhana nyingine ya kukimbia majukumu. Ndio maana leo watu wanahamasishwa wasizae maana wakiwa na watoto watabeba jukumu la kulea na hiyo kupunguza starehe zao. 
Dhana hizi zikishajengwa na kustawi katika fikra za watu, mambo makubwa mawili ni matokeo ya lazima. Kwanza ubinafsi na hali ya kutowajali wengine hustawi. 
Kwa hiyo hakuna atakayejali njaa ya mwingine wala janga jingine katika maisha. Na tunashuhudia leo katika jamii yetu wagonjwa wanavyotekelekezwa katika mahospitali kwa vile hawana fedha. Wenye madaraka serikalini wanavyotumia kodi za wananchi, wanatembelea magari ya fahari , kula na kusaza wakati wenyewe wananchi hawana madawa wala maji safi ya kunywa. 
Jambo la pili ni kiu isiyokatika wala isiyo na mipaka ya kutosheleza matamanio ya nafsi (kustarehe). Kila mtu hujiundia namnayake ya kustarehe. 
Wengine wataendekeza ngono ya jinsia moja, wengine watataka waparamie hata wanyama na wengine wataona starehe yao ipo katika kuwabaka watoto wadogo. 
Kwa mtu mzima kupenda kuwa na mahusiano ya kingono na watoto wadogo (Pedophilia) ni matokeo ya dhana nzima ya maisha inayopandikiza hisia kwamba lengo la maisha ni kustarehe. 
Watu wanahamanika leo kutaka kudhibiti wabakaji wa watoto wadogo na matatizo mengine kama matumizi ya madawa ya kulevya. Kosa halianzuii hapo. Hayo ni matokeo ya falsafa inayoongoza maisha katika jamii. 
Uislamu hautazami tatizo la ubakaji na tabia ya watu wazima kupenda mahusiano ya kingono na watoto wadogo kama tatizo au maradhi yenye kujitegemea. Wala si maradhi yanayoweza kuhusishwa na elimu nafsi bali ni matokeo ya lazima ya mifumo mibovu ya maisha. 
Dawa ya maradhi hayo ni kurejea kwenye mfumo sahihi wa maisha. Mfumo usio mtizama mwanadamu kama mnyama aliyeko hapa kwa ajili ya kustarehe, bali Khalifa wa Allah (s.w.) kwa ajili ya kumwabudu Muumba wake. 
Mtu aliyelelewa katika jamii ya Makhalifa wa Allah (s.w.) kula kwake, kunywa kwake na mengine yote atakayoyafanya yatatizama lengo kuu, sio kustarehe. 

ISLAMOPHOBIA
Neno - Phobia ni kinyume cha neno Philia. Neno Philia lina maana ya hali ya kupenda kitu fulani kusiko kwa kawaida. Kwa mfano neno Aelurophilia ni hali ya mtu kupenda sana paka. Ndio maana katika matoleo yaliyopita tuliona Paraphilias, maradhi ya kupenda kufanya jambo fulani kinyume na maadili, kama vile kupenda kukodolea macho watu walio kuwa wazi (Voyeurism), au kupenda kuacha wazi sehemu nyeti za mwili (ExhIbitionism) n.k.
Kwa hiyo neno - Phobia lina maana ya kuogopa mno, au kutokupenda kitu au jambo fulani. Kwa mfano watu wenye Claustrophobia ni watu wenye kuwa na hofu wanapokuwa kwenye chumba kilichofungwa au sehemu (uchochoro) mwembamba. Photophobia pia ni tatizo la kisaikolojia la mtu kutokupenda mwanga. Yaani ni hali ambayo mtu akiwepo kwenye hali hiyo ya Pressure (presha) inampanda. Kwa hiyo basi,Islamophobia ni hali ya mtu kuuogopa Uislamu, na hivyo chochote kinachohusiana na Uislamu basi kinampa msisimko hasi, yaani msisimko usiopendeza, na anaingiwa na hofu na tafarani ya moyo.
Kuna wagonjwa wa aina mbili wa Islamophobia. Kundi la kwanza ni wale wanaopewa maelezo ya uongo kuhusu Uislamu na Waislamu. Hawa hupewa picha ya Waislamu kuwa ni watu wakatili, wauwaji, mara nyingi wanaume hunasibishwa na majambia, vilemba (hasa vyekundu) pamoja na madevu. Pia hutajiwa sheria kali za Kiislamu kama ile ya kumkata mwizi mkono, kumtandika bakora mlevi, na mzinifu kupigwa mawe hadi kufa. Kwa hiyo mtu huyu hukua na picha hii ya "ukatili" wa Uislamu. Kwa hiyo akimuona Muislamu basi anapata picha ya chinja chinja.
Kundi la pili ni lile ambalo lina maradhi ya kisaikolojia, hasa yale ya Ukozimeni (Voyeurism), wendauchi (Exhibitionism) n.k. Kwa vile Uislamu ni dini ambayo inapiga vita mambo ambayo wao wanayapenda, basi wanatokea kuuchukia Uislamu, na wanapokuwa katika mazingira ya Kiislamu yasiyo na zinaa, basi wanajisikia kama samaki aliyetolewa kwenye maji akawekwa nchi kavu. Hawa ndio hupambana kiasi wanachoweza kuhakikisha kwamba katika eneo walipo hakuna athari ya Uislamu.
Ndipo kwa mfano, mwalimu anamzuia binti wa Kiislamu kuingia darasani kwa vile amevaa gauni refu linalomstiri, na kwa vile amevaa ushungi unaoziba kifua chake, vitu ambavyo katika jamii ya wendawazi havitakiwi. Uniform nzuri kwake ni ile inayoacha miguu (ikiwezekana mapaja) na hata makwapa wazi. Cha kushangaza, baadhi ya walimu ni wanawake. Ukimuuliza anasema, "hatutaki udini". Yeye kuruhusu mabinti wavae kama dini yake inavyoruhusu, yaani visketi na viblauzi huo sio udini!
Kundi la tatu la wenye maradhi ya Islamophobia ni la mifumo ya kiutawala ya Kitwaghuti. Hawa wamaejaa dunia nzima. Husema kwamba serikali zao hazina dini, lakini utakuta Uislamu unapotangazwa kama unavyotakiwa uwe, wale watangazaji huitwa magaidi, wachochezi, wavunja amani, basi tafarani ndogo tu ya Msikitini itatulizwa na mabomu. Waislamu wa kweli wataitwa Siasa kali n.k. Uislamu wanaotaka wao ni ule wa siasa poa! Yaani wewe ujue lako, uwaache wenzio waendelee na yao, waendelee tu kuchafua mazingira ya jamii kwa ulevi, uzinzi, wizi, ujambazi, uafriti, dhulma n.k. Ukae kimyaa na tasbihi. Hapo utakuwa rafiki yao, na futari watakupikia.
Uislamu usiosafisha jamii na maovu ni mpya. Uislamu niujuao mimi ni ule unaotokana na maneno ya Muumba wa Ulimwengu:
"Hawawi sawa Waislamu wanaokaa tu bila ya dharura (ya kuwakalisha) (kuwa sawa) na wale wanaofanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu..." (4:95).
Tunatakiwa tuufuate Uislamu wetu bila ya kuogopa chuki ya yeyote mwenye Islamophobia, na wakitokea kupata uchungu kwa kuufuata kwetu Uislamu vilivyo, tunaambiwa tuwaeleze:
"Kufeni kwa uchungu wenu..." (3:119)

Imeandikwa na Abu Halima Sachangwa (An Nuur)

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget