Dalili katika Qur-aan tunaona kwamba
hata mitume walikuwa wakifuga ndevu. Hii ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) kuhusu Haaruun ('alayhis-salaam alipomwambia Musa
('alayhis-salaam) alipomshika ndevu zake baada ya kuwaona wana wa Israaiyl wamepotoka:
((Akasema:
Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika
naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli
yangu)) [Twaaha
20:94]
Hapa tunakupa
dalili zilizothibitika katika Sunnah:
1. Mtawala
wa Yemen, aliyechaguliwa na Mfalme wa Kiajemi Kisraa, alituma majumbe wawili
kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumpelekea
mwaliko. Wakati hao walipotokezea mbele ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam), aliwaona hao wamenyoa ndevu na kufuga masharubu
(ndevu za mdomo). Kwa hayo yeye alichukizwa kuwatazama hao (kwa sababu ya
kuonekana visivyo sawa) na aliwaambia : "Ole wenu ! Je ni nani
aliyewaambia kufanya hivyo ?" Wao walimjibu: "Bwana wetu!
(wakimaanisha Kisraa)."
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia: "Lakini Mola wangu, aliye Mkuu
na Aliyetukuzwa, ameniamrisha mimi kuibakiza ndevu yangu peke yake na kunyoa masharubu yangu." [Imerekodiwa na Ibn Jarra-abar, na al-Albaaniy kuwa ni Hasan (nzuri) ]
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia: "Lakini Mola wangu, aliye Mkuu
na Aliyetukuzwa, ameniamrisha mimi kuibakiza ndevu yangu peke yake na kunyoa masharubu yangu." [Imerekodiwa na Ibn Jarra-abar, na al-Albaaniy kuwa ni Hasan (nzuri) ]
2. Mtume
Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewaamrisha wanaume
wafuge ndevu peke yake. Hadiyth zifuatazo pia zina maana hizi hizi : "Nyoeni masharubu na muziache ndevu".[Al-Bukhaariy
na Muslim]
3. Mtume
Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:"Nyoeni masharubu yenu na muoteshe ndevu zenu. Muonekane
tofauti na Wamajusi (wafuasi wa dini ya waabudu moto iliyokuwapo huko Uajemi
[Iran]). [Muslim]
4. Mtume
Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nyoeni masharubu yenu na kuziacha ndevu zenu peke yake. Muwe
tofauti na Ahlul Kitaab (Mayahudi na Manaswara)." [Muslim]
5. Mtume Muhammad
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muwe
tofauti na Mushrikiyn, mnyoe masharubu yenu na kufuga ndevu" [Al-Bukhaariy na Muslim]
Kwa kifupi hizi ni
dalili chache kuonyesha Uwajibu wa jambo hilo, na vilevile ni maarufu kuwa
Maimam Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi'iy, Ahmad bin Hanbal na wengineo
wamesema ni HARAAM kunyoa ndevu.
Na kwa kufahamu
kuwa jambo hilo ni baya na ni ukiukwaji wa sheria ambayo imetoka kwa Muumba na
kuthibitishwa kimaelekezo na kivitendo kwetu na Mjumbe Wake (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) ndio Maimaam hao wakatoa maamuzi yao katika suala
hilo.
Amiyr Muadilifu
'Umar ibn 'Abdul-'Aziyz inasemekana katika vyanzo vya kihistoria kuwa alikuwa
hakubali katika utawala wake ushahidi wa mtu mwenye kunyoa ndevu! Vilevile
tunaona kwenye madhehebu mbalimbali za Kiislam, haruhusiwi mtu kuswalisha ikiwa
haweki ndevu kutokana na jinsi walivyofahamu uzito wa jambo hilo na Uwajibu
wake.
Na ndevu ni
mashavuni na kidevuni, unapaswa kufuga ndevu zote na si kidevuni pekee ambazo
zaitwa mzuzu na ukanyoa za mashavuni; utakuwa unafanya makosa; zote hizo ni
ndevu, ama zilizoko juu ya mdomo wa juu ambazo ni masharubu, hizo zatakiwa
kupunguzwa na zisiwe refu.
No comments:
Post a Comment