Wednesday, February 22, 2012

Kitabu-Ujumbe wa kweli wa Yesu Kristo


wa kweli
wa Yesu Kristo


(ST. DAVID`S COLLEGE, UNIVERSITY OF WALES, U.K.)

Ujumbe wa kweli
wa Yesu Kristo

NA:
DR. BILAL PHILIPS
(ST. DAVID`S COLLEGE, UNIVERSITY OF WALES, U.K.)


Kimefasiriwa na Omari Juma Mangilile
 mangilile@yahoo.com email:   
                          omari_mangilile@hotmail.com
Yaliyomo
      Somo                                                                                       Ukurasa

Ujumbe wa kweli wa Yesu Kristo

NA. DR. BILAL PHILIPS
(.St. David's College, University Of Wales, U.K)

Utangulizi

Y
esu Kristo anawakilisha akiwa ni kiungo cha kuunganisha baina ya dini mbili zenye wafuasi wengi zaidi duniani leo hii; Ukristo na Uislamu. Somo lifuatalo, linalohusu Ujumbe wa Yesu na Haiba yake limeegemea katika kiungo hicho. Inatarajiwa kuwa, kwa kupitia somo hili, wote wawili; Waislamu na Wakristo watafahamu vizuri ukuu wa Yesu na umuhimu wa ujumbe wake.
Hata hivyo, ili tuutambulishe barabara ujumbe wa kweli wa Yesu Kristo, mtazamo usio na upendeleo ulibidi udumishwe katika kipindi cha kufanya uchunguzi wetu. Hisia zetu zisiruhusiwe kuweka kiwingu kwenye uoni wetu na kwa hiyo, kutupofua tusiuone ukweli. Lazima tuyatazame masuala mazima kimantiki na tuutenganishe ukweli uepukane na uongo kwa msaada wa Mungu Mwenye nguvu.
Tukiangalia dini za uongo na imani mbalimbali za upotovu duniani, na moyo wa kuzipenda unaowafanya wafuasi zake waziunge mkono imani hizo, inaonesha ushahidi madhubuti kuwa watu hao hawawezi kuugundua ukweli kwa sababu ya upofu wa misimamo yao juu ya imani zao. Ufuasi wao king`ang`anizi, kwa kawaida hauegemei ufahamu wa kiakili juu ya mafundisho, bali unategemea utamaduni wenye nguvu na vishawishi vya kihisia. Kwa kuwa walilelewa katika familia au jamii maalum, wao wanashikamana madhubuti na imani ya jamii hizo, wakiamini kuwa, wanauunga mkono ukweli.
Njia pekee inayoweza kuufikia ukweli juu ya kitu chochote kile ni kukijongelea kitu hicho kupitia mfumo maalamu na kwa kutumia akili. Kwanza, tuupime ushahidi kisha tunauhukumu kwa akili alizotupa Mungu. Katika ulimwengu wa maada, kimsingi ni akili ndizo zinazowapambanua wanadamu na wanyama, akili ifanyayokazi vizuri katika silika (maumbile) yake. Baada ya kuubainisha ukweli bila kupendelea, hapo ndipo tujibebeshe majukumu ya ukweli huo kihisia. Ndio, kuna nafasi ya kuwa na msimamo wa kihisia, lakini msimamo wa kihisia lazima uje baada ya ufahamu wa kiakili juu ya kadhia husika, kisha ndipo mtu ajiandae kiakili na kiroho kuutetea ukweli huo kwa juhudi.
Ni kwa mtazamo wa kiakili na kiroho, ambapo somo la ujumbe wa Yesu na umuhimu wake kwa wale wote wenye shauku ya kumfuata Mungu litachambuliwa katika kurasa zifuatazo.

 Dr. Bilal Philips
Saudi Arabia, 1989

Sura ya Kwanza: Maandiko Matakatifu

Mada ya 'Ujumbe Wa Kweli Wa Yesu Kristo' ina sehemu kuu mbili:
1. Ujumbe na 2. Haiba ya Yesu Kristo. Kila sehemu katika sehemu mbili hizo haitengani na nyingine. Ili tuufahamu ujumbe wa Yesu, lazima tumjue Yesu alikuwa ni nani, vilevile ni lazima kuufahamisha na kuutambulisha ujumbe wake.
Kuna njia mbili zinazoweza kupitiwa ili kuufikia utambulisho wa Yesu Kristo na yaliyomo katika ujumbe wake. Ya kwanza inaangazia makusanyo ya rekodi za kihistoria za wanahistoria wa kisasa kutoka katika maandiko na masalio ya kipindi hicho na ya pili inaangazia ripoti zilizomo katika Maandiko ya ufunuo.
Kwa ukweli, kuna ushahidi mchache mno unaotufahamisha kuwa Yesu alikuwa ni nani, au unaobainisha ujumbe wake ulikuwa ni nini. Nyaraka rasmi za kihistoria za kipindi hicho kwa hakika hazina rekodi yoyote juu ya Yesu. Msomi wa Biblia, R.T. France, anaandika, "Hakuna andiko lolote la karne ya kwanza linalomtaja Yesu na hakuna kitu chochote au jengo lolote lililobakia na ambalo lina uhusiano naye."[1] Ukweli huu umewafanya baadhi ya wanahistoria wa Kimagharibi kukosea na kudai eti Yesu Kristo wa hakika hajapatapo kuwepo. Kwa hiyo, kimsingi, utafiti lazima uegemee maandiko matakatifu yanayoeleza haiba na kazi za Yesu Kristo. Maandiko matakatifu yatakayoulizwa ni yale yanayotambulikana kirasmi na dini zote mbili Ukristo na Uislamu. Hata hivyo, kuchambua barabara, maelezo yaliyomo katika maandiko ya kidini, ni jambo la msingi kuanzia na kupima usahihi wa maandiko hayo. Je, vitabu vya dini ni vyanzo vya kuaminika kuwa nyaraka za ushahidi, au ni ubunifu wa simulizi za kibinadamu na visaasili, au ni mchanganyiko wa yote mawili? Je, Biblia, Agano la kale na Jipya ni maandiko ya ufunuo wa Mungu? Je, Quran (Kurani) ni sahihi?
Kwa Biblia na Quran ili ziwe maneno matakatifu ya Mungu, lazima ziwe hazina kujipinga zenyewe kusikofafanulika, na kusiwe na shaka juu ya yaliyomo ndani yao wala juu ya watunzi wake. Ikiwa hii ndio kadhia, basi yale yaliyomo katika Agano la kale, Jipya na Quran, ndipo yatakapozingatiwa kuwa ni vyanzo aminika vya maelezo yanayohusiana na ujumbe Yesu Kristo na haiba yake.

Miswada sahihi

Wanazuoni wengi wa madhehebu na vikundi mbalimbali vya Kikristo wamethibitisha kuwa sehemu kubwa ya maandiko ya Biblia ina mashaka makubwa juu ya uhalisia wake.
Katika utangulizi wa Ngano za Mungu mwenye Mwili, Mtunzi ameandika yafuatayo: "Katika karne ya kumi na tisa, Wakristo wa Kimagharibi walifanya marekebisho makubwa mawili ili kuitikia wito wa kupanuka kwa elimu ya wanadamu: imekubalika kuwa mwanadamu ni sehemu ya maumbile na ameibuka kuwa ni miongoni mwa wanamageuzi wa mfumo wa maisha duniani; imekubalika kuwa vitabu vya Biblia vimeandikwa na watu tofauti tofauti katika matukio tofauti tofauti na haviwezi kukubaliwa kuwa ni utunzi wa Mungu wa neno kwa neno."[2]
Katika gazeti la kimataifa la, Newsweek[3], lililobeba makala yenye kichwa 'Oo Bwana, Nani Aliyeandika Dua hii?' kikosi cha wanatiolojia kutoka katika dhehebu kuu la kiporestanti, pamoja na Wasomi muhimu wa Biblia wa Kikatoliki nchini Marekani, baada ya ukaguzi wa kina wa miswada ya mwanzo kabisa ya Agano Jipya, wamehitimisha kuwa maneno pekee ya "Dua ya Bwana"[4]  ambayo yanaweza kunasibishwa barabara na Yesu Kristo ni "baba". Na hilo, ni kwa mujibu wa wasomi hao wa kanisa, maneno yote yaliyokuja baada ya ibara ya kwanza, "Baba yetu", ambayo ni dua muhimu sana ya Kikristo, yaliongezwa karne nyingi na waandishi wa kanisa walionukuu miswada ya mwanzoni ya Injili.[5] Shirika la U.S News & World Report, linanukuu zaidi kuwa, kikundi cha wasomi kilisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno yaliyoandikwa katika Injili kumhusu Yesu huenda ni ya kubuniwa.[6] Miongoni mwa hayo likiwemo neno la Ekaristi ya Yesu[7] katika Karamu ya Mwisho ("Chukua, kula. Huu ni mwili wangu…") na kila neno aliloambiwa kuwa amelitamka toka msalabani.[8]
Dr. J.K. Elliott, wa kitengo cha Thiolojia na Tafiti za Kidini wa Chuo Kikuu cha Leeds, ameandika makala iliyochapishwa katika jarida la The Times, London (10 Septemba, 1987) yenye kichwa "Kutazama mizizi ya Biblia". Ndani ya makala yake, ameeleza kuwa: "Zaidi ya miswada 5,000 inayojumuisha Agano Jipya lote au sehemu yake iliyo katika lugha ya asili. Miswada hii imepangika katika madaraja ya kuanzia karne ya pili hadi kuvumbuliwa kwa uchapaji. Imekisiwa kuwa hakuna hata watu wawili wanaoafikiana kwa kila kitu. Bila shaka, maandishi yote ya mkono yanastahili kuwa na makosa ya bahati mbaya wakati wa kunukuu. Hata hivyo, katika kazi za kitiolojia si jambo la kushangaza kuwa mabadiliko ya kufikirika sana yaliingizwa ili kuondosha au kubadili maelezo ambayo waandishi wanayaona kuwa hayapendezi. Pia kulikuwa na mwelekeo wa wanukuzi wa kuongeza ufafanuzi au fasiri.[9] Mabadiliko ya hadhari yanadhaniwa kuwa yameingizwa katika zama za mwanzo kabla ya kuanzishwa hali ya kanisa ya Agano Jipya.
Mwandishi aliendelea kufafanua kuwa "hakuna hata mswada mmoja wenye matini isiyobadilishwa kutoka katika uasilia wa ukamilifu wake, na kwa hiyo, "hakuna awezae kuchagua mswada wowote miongoni mwa miswada hiyo na kuuamini kwa imani ya pekee eti mswada huo ndio wenye ukiritimba wa kuwa ndio maneno asilia ya watunzi."
Aliendelea kusema zaidi: "Kama mtu ataendelea kupinga na kudai kuwa maandiko asilia yamenusurika pahala fulani kwenye maelfu ya miswada iliyopo,[10] basi mtu huyo atalazimika asome miswada yote hiyo, hatua kwa hatua, ili kukusanya tofauti miongoni mwa miswada hiyo, kisha atathimini, lahaja kwa lahaja, ili ajue ni mswada upi wenye [matini] asilia na upi ndio wa matini ya nafasi ya pili. Matarajio kama hayo yaliwakatisha tamaa[11] wasomi wengi wa Biblia walioaminia yaliyomo katika matini zilizochapwa za zama za mwanzo, wasomi hao walichukua ushahidi wa miswada waliyoiona kuwa ni bora. Hata matoleo ya Agano Jipya kwa Kigiriki yaliyochapwa kisasa, vilevile mafafanuzi ya kisasa yametegemea chapa hizo za zama za mwanzo; kwa kawaida hufuata utaratibu huu wa kujenga matini zao kwa kutumia msingi finyu ambao hauonekani kuwa ni wa asili kikamilifu."

Matoleo ya Biblia ya Kingereza

Katika utangulizi wa toleo la Biblia linalotumika sana, la Revised Standard Version, mtunzi ameandika yafuatayo:
"Biblia ya Revised Standard Version, ni marekebisho yaliyoidhinishwa ya toleo la American Standard Version, lilochapwa 1901, na ambalo nalo pia lilikuwa ni marekebisho ya toleo la King James Version, lilochapwa 1611…
Toleo la King James Version lililazimika kushindana na Biblia ya Geneva Bible (1560) juu ya kutumiwa na watu wengi; lakini hatimaye lilienea, na kwa zaidi ya karne mbili na nusu hakuna tafsiri ya Biblia kwa Kingereza iliyoandikwa na kuidhinishwa. Toleo la King James Version likawa ndilo "toleo lililoidhinishwa" kwa wanaoongea Kingereza… Ndio, Toleo la King James Version lina dosari kubwa mno. Kufikia katikati ya karne ya kumi na tisa, maendeleo ya tafiti za Kibiblia vilevile kugunduliwa kwa miswada mingi ambayo ni ya kale zaidi kuliko ile iliyotegemewa na Toleo la King James Version, yamefanya toleo hilo kuwa ni wazi kuwa lina dosari nyingi na mbaya mno na kusababisha kuitishwa kufanyika marekebisho ya tafsiri ya kingereza. Kazi ikafanywa, kwa idhini ya Kanisa la Uingereza, mwaka 1870. Toleo la Biblia la English Revised Version lilichapwa mwaka 1881 – 1885; na Toleo la American Standard Version, lahaja zake zimejiingiza katika upendeleo wa wanazuoni wa Kimarekani walioshiriki katika kazi hiyo, nalo lilichapishwa mwaka 1901."[12]
Toleo la King James Version la Agano Jipya liliegemea matini za kigiriki zilizovurugwa kimakosa, ikiwemo kujilimbikizia makosa ya karne ya kumi na nne ya kunukuu miswada. Nalo kimsingi, lilikuwa ni matini ya Kigiriki ya Agano Jipya kama lilivyoandikwa na Beza, 1589, ambaye kwa ukaribu zaidi alifuata chapa hiyo ya Erasmus, 1516 – 1535, iliyoegemea juu ya miswada ya zama za kati. Mswada wa kwanza na ulio bora zaidi miongoni mwa miswada minane aliyoishirikisha ulikuwa ni wa karne ya kumi, naye akautumia kidogo mno mswada huo kwa sababu unatofautiana sana na matini za kawaida zilizopokelewa; Beza alipata miswada miwili ya thamani kubwa mno, ikiwa ni ya karne ya tano na ya sita, lakini aliitumia kidogo mno kwa sababu inatofautiana na matini iliyochapwa ya Erasmus."[13]
"… Toleo la American Standard Version lilipewa haki miliki ya kuzuia matini yake isibadilishwe bila idhini. Mnamo 1928 haki hiyo ilipatikana kutoka katika Baraza la Kimataifa la Elimu na Dini, na kwa hiyo likawekwa katika umiliki wa makanisa ya Marekani na Canada yaliyoshiriki katika baraza hilo kwa kupitia bodi zao za elimu na uchapaji. Baraza hilo liliainisha kamati ya wasomi kusimamia matini ya ya Toleo la American Standard Version na kufanya uchunguzi na kujua kama marekebisho zaidi yanahitajika… [Baada ya miaka miwili] uamuzi ulifikiwa; nao ni kuwa; kunahitaji marekebisho kikamilifu katika toleo la 1901, ambalo litabakia kuwa lipo karibu na mapokeo ya Tyndale-King James kama itakavyokuwa… Mnamo 1937 na marekebisho yalipewa idhini kwa kura ya Baraza hilo."[14]
"Wasomi therathini na wawili walitumika kama wanakamati wa kamati iliyotakiwa kufanya marekebisho hayo, nao waliyalinda mabadiliko na kuishauri Bodi ya Ushauri ya wawakilishi hamsini wa madhehebu ili kushirikiana kufanya kazi hiyo…  Toleo la Agano Jipya la Revised Standard Version lilichapwa mwaka 1946."[15] Toleo la Biblia la Revised Standard Version, linajumuisha Agano la Kale na Jipya, nalo lilichapwa mnamo Septemba 30, 1952, na likakubalika sana."[16]
Katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, idadi kubwa ya mistari muhimu kutoka katika Toleo la King Jemes Version ya Agano la Kale na Jipya, ambayo wasomi waliiona kuwa imeongezwa katika karne za baadaye, iliondoshwa kutoka katika matini na kuwekwa katika tanbihi. Kwa mfano, kifungu maarufu sana katika Injili ya Yohana 8:7 kinachohusu mzinzi aliyetakiwa kupigwa mawe. Inasemakana Yesu amesema: "Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe." Tanbihi za Toleo la King Jemes (1952) zinaeleza "Mamlaka za kale mno zinaondosha aya za 7:53 – 8:11"[17] Kwa kuwa mswada namba 1209 wa Vatikani na mswada wa Sinaitic ya tangu karne ya nne haina aya kumi na mbili hizo, wasomi wa Biblia wamefikia uamuzi wa kuwa maneno hayo hayatoki kwa Yesu. Mfano mwingine ni kifungu kinachohusishwa na Yesu na kinachotumika kama ushahidi wa rejeo la Utatu katika Maandiko matakatifu. Katika 1 Yohana 5:7, Inasemakana Yesu amesema: "Kuna watatu wanaoshuhudia huko mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni mmoja"[18] Msomi maarufu sana wa Biblia, Benjamin Wilson, anaandika kuwa; maandiko haya yanayohusu "ushahidi wa mbinguni" hayamo katika mswada wowote wa Kigiriki ulioandikwa kabla ya karne ya kumi na tano! Kwa hiyo, katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, mstari huu umefutwa na kutolewa katika matini tena bila ya kuwekewa tanbihi. Hata hivyo, ili kuwe na idadi ya mistari iliyosawa baina ya Toleo la Biblia la Revised Standard Version, na ile ya Toleo la Biblia la King James Version, warejeaji wameugawa mstari wa sita na kuwa mistari miwili.
Toleo la pili la tafsiri ya Agano Jipya (1971) limefaidika kwa tafiti za matini na isimu tangu lilipotolewa toleo la The Rivised Standard Version, kwanza lilitolewa mwaka 1946. [19] Kwa hiyo, baadhi ya vifungu vilivyofutwa zamani viliandikwa upya, na baadhi ya vifungu vilivyokubaliwa vilifutwa. "Vifungu viwili, vya mwisho mrefu wa Marko (16:9-20) na kifungu cha mwanamke aliyekamatwa kwa uzinzi (Yohana 7:53 – 8:11), vilirejeshwa katika matini, zikitenganishwa kwa nafasi wazi na zikiambatana na nukuu za kauli taarifa… Kukiwa na kuungwa mkono na miswada miwili, vifungu viwili, Luka 22:19b-20 na 24:51b, vilirejeshwa katika matini, na kifungu kimoja, Luka 22:43-44, kiliwekwa katika tanbihi, kama ni ibara katika Luka 12:39."[20]

Utunzi

Kwa mujibu wa wasomi wa Biblia, hata utunzi wa vitabu vya Agano la Kale na Injili zenyewe una mashaka.

Torati

Vitabu vitano vya kwanza katika Biblia (Vitabu vya Musa)[21] kimapokeo vinahusishwa na Mtume Musa,[22] hata hivyo, kuna mistari mingi ndani ya vitabu hivi inayoashiria kuwa Mtume Musa hana uwezekano wa kuandika kila kitu kilichomo katika vitabu hivyo. Kwa mfano, Kumbukumbu la Torati 34:5-8 inasema: "Basi Musa, mtumishi wa BWANA, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la BWANA. Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peroi; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo. Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu zake hazikupunguka. Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku therathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha." Ni wazi kuwa mtu mwingine ameandika mistari hii inayohusu kifo cha Musa.
Baadhi ya wasomi wa Kikristo wamezifafanua hitilafu hizi kwa kupendekeza kuwa Musa ndiye aliyeandika vitabu vyake, lakini mitume ya baadaye pamoja na waandishi waliofunuliwa, wameweka nyongeza iliyotajwa hapo mbele. Kwa hiyo, kwa mujibu wa wasomi hao, matini, kwa ukamilifu wake, inabakia kuwa ni Maandiko ya ufunuo wa Mungu. Hata hivyo, ufafanuzi huu hauwezi kukubalika katika uchunguzi makini, kwa sababu mtindo na fasihi ya wahusika wa mistari iliyotomewa ni sawa sawa na ule wa matini iliyobakia.
Katika karne ya kumi na tisa, wasomi wa Biblia wa Kikristo wameanza kujadili maana ya “kujirudiarudia mara mbili mbili” kulikotokea katika Torati. Hivi ni visa vilivyotokea mara mbili mbili, na kila mara kinakuwa na maelezo tofauti. Miongoni mwa visa hivyo ni visa viwili vya agano la Mungu na Ibrahimu, linalohusu Mungu kubadilisha Jina la Yakobo na kuwa Israeli pia na kisa cha Musa kupata maji kutoka katika mwamba.[23]
Watetezi wanaotetea utunzi wa Musa wamesema kuwa “kujirudiarudia mara mbili mbili” hakukuwa na kupingana, bali ni kuleta faida. Dhamiara zao zilikuwa ni kutufundisha undani, na maana ndogo juu ya Torati. Hata hivyo, madai haya yalifagiwa haraka haraka na wasomi walio na moyo wa uadilifu, walioona kuwa, sio tu baadhi ya vifungu vilikuwa vinapingana kwa uwazi kabisa, lakini pia wakati kule  “kujirudiarudia mara mbili mbili” kulipotenganishwa na kuwa vifungu viwili, kila kifungu kwa uthabiti kilitumia jina la Mungu lilotofauti. Siku zote mtu anaweza kumchukulia Mungu kuwa ni Yahweh au Jehovah, andiko hili liliitwa “J”. Na lingine, siku zote, linamchukulia Mungu kuwa ni Elohim, na liliitwa “E”.[24] Kulikuwa na sifa za kifasihi zilizopatwa kuwa ni moja kwa waraka mmoja au mwingine.
Uchambuzi wa fasihi za kisasa, kwa mujibu wa Profesa Richard Friedman,[25] unaashiria kuwa vile vitabu vitano vya Musa ni mchanganyiko wa Kiebrania wa kuanzia karne ya tisa, nane, saba na sita B.C. (Kabla ya kuzaliwa Kristo). Kwa hiyo, Musa aliyeishi karne ya kumi na tatu B.C., alikuwa yu mbali mno na Kiebrania cha Biblia hata kuliko alivyokuwa mbali Shakespeare na Kingereza cha leo.
Utafiti zaidi juu ya vitabu vitano vya Musa umepelekea kugunduliwa kuwa vitabu hivyo havikuundwa kwa vyanzo viwili vikuu bali ni vine. Imegunduliwa kuwa baadhi ya visa sio tu ni vya kujirudiarudia mara mbili mbili lakini pia ni mara tatu tatu. Sifa za ziada za kuongezea zimetambuliwa katika nyaraka hizi. Chanzo cha tatu kiliitwa “P” (cha kuhani), na cha nne kinaitwa “D” (cha Kumbukumbu la Torati).[26]
Upeo wa kujua ni kiasi gani kilichoongezwa waziwazi katika matini asilia ni vigumu sana kuamua. Kwa hiyo, kivuli kikuu cha mashaka kimegubika utunzi wa vitabu vyote kiujumla.
Katika kiambatisho cha toleo la Rivised Standard Version chenye anuani “Vitabu vya Biblia,” yafuatayo ndiyo yaliyoandikwa kuhusiana na mtunzi wa zaidi ya theruthi moja ya vitabu vilivyobakia katika Agano la Kale:
Kitabu
Mtunzi
Waamuzi
Huenda ni Samweli
Ruthu
Huenda ni Samweli
Samweli wa Kwanza
Hajulikani
Samweli wa Pili
Hajulikani
Wafalme wa Kwanza
Hajulikani
Wafalme wa Pili
Hajulikani
Mambo ya Nyakati wa Kwanza
Hajulikani
Esta
Hajulikani
Ayubu
Hajulikani
Mhubiri
Kuna mashaka
Yona
Hajulikani
Malaki
Hakuna kinachojulikana

Kubuniwa

Zaidi ya nusu ya Wakristo wote duniani ni Wakatoliki. Toleo lao la Biblia lilichapishwa mwaka 1582 kutoka kwa Jerome`s Latin Vulgate, na kutengenezwa tena huko Douay mwaka 1609. Agano Jipya la RCV (Roman Catholic Version) lina vitabu saba zaidi kuliko lile la King Jams Version linalotambuliwa na Ulimwengu wa Wapotestanti. Hivyo vitabu vya ziada vinazingatiwa kuwa ni vya kubuniwa (yaani kuna shaka juu ya mtunzi wake) na vimeondolewa kutoka katika Biblia mwaka 1611 na wasomi wa Biblia wa Kipotestanti.

Injili

Kiarama ilikuwa ndio lugha inayozungumzwa na Wayahudi wa Palestina. Kwa hiyo, inaaminika kuwa Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakizungumza na kufundisha kwa Kiarama.[27] Mapokeo ya mdomo kwa mdomo ya mwanzo kabisa ya matendo na maneno ya Yesu bila shaka yaliduru katika Kiarama. Hata hivyo, Injili nne zimeandikwa kwa kauli tofauti kabisa, Kigiriki, lugha ya ustaarabu wa ulimwengu wa eneo la bahari ya kimediterania, ilihudumia makanisa mengi, na kuyafanya yawe ya Kigiriki (Yanatumia Kigiriki) badala ya Kipalestina (Kiarama). Alama za Kiarama bado zipo katika Injili za Kigiriki. Kwa mfano, katika Marko 5:41, “Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.” na Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?[28]
Ingawa, Injili ya Marko katika Agano Jipya, Wasomi wa Kanisa wanaizingatia kuwa ndio Injili ya kale zaidi, haijaandikwa na mwanafunzi wa Yesu. Wasomi wa Biblia kwa kutegemea ushahidi uliopo katika Injili hiyo, wanahitimisha kuwa Marko mwenyewe hakuwa mwanafunzi wa Yesu. Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa wasomi hao, hawana yakini juu ya huyo Marko alikuwa ni nani hasa. Mtunzi wa kale wa Kikristo, Eusebius (325 C.E.) ameripoti kuwa Mtunzi wa kale mwingine, Papias (130 C.E.), alikuwa wa mwanzo kuihusisha Injili ya Marko kwa John Mark, mfuasi wa Paulo.[29] Wengine wanaonelea kuwa huyo mwandishi wa Marko huenda alikuwa mwanafunzi wa Peter, pia wengine wanang`ang`ania kuwa huenda alikuwa ni mtu mwingine kabisa.
Hali hiyo hiyo kwa Injili nyinginezo, ingawa Mathayo, Luka na Yohana ni majina ya wanafunzi wa Yesu, watunzi wa Injili zinazobeba majina yao hawakuwa hao wanafunzi mashuhuri wa Yesu, ispokuwa ni watu wengine waliotumia majina ya wanafunzi wa Yesu ili kuyafanya maelezo yao yasadikike. Kwa hakika, Injili zote kiasili zinaduru katika mzingo wa kutotajwa jina la mtunzi. Majina ya watunzi yamepewa vitabu hivyo na watu wasiojulikana wa kanisa la mwanzo.[30]

Kitabu
Mtunzi
Mathayo
Hajulikani[31]
Injili ya Marko
Hajulikani[32]
Injili ya Luka
Hajulikani[33]
Injili ya Yohana
Hajulikani[34]
Matendo ya Mitume
Mtunzi wa Luka[35]
I, II, II, Yohana
Mtunzi wa Yohana[36]
J.B. Phillips, kasisi wa kulipwa[37] wa Kanisa kuu la Chichester, Kanisa la Kianglikana la Uingereza, ameandika utangulizi ufuatao katika tafsiri yake ya Injili kwa mujibu wa Mtakatifu Mathayo: “Mapokeo ya mwanzo yanaipachika Injili hii kwa mwanafunzi wa Yesu aitwaye Mathayo, lakini wasomi wa kisasa karibu wote wanapinga mtazamo huo. Mtunzi tunayeweza kumwita Mathayo bila shaka, kwa uwazi kabisa ameshaandikwa katika fumbo lisiloelezeka “Q”,[38] kitu ambacho kinaweza kuwa ni mkusanyo wa mapokeo ya simulizi za mdomo kwa mdomo. Alitumia Injili ya Marko kwa uhuru, ingawa alipanga upya mpangilio wa matukio vilevile katika mifano kadhaa alitumia maneno tofauti tofauti kwa kile ambacho kwa uwazi kabisa ni kisa kile kile.”[39] Injili ya nne (Yohana) ilipingwa ikichukuliwa kuwa ni uasi katka kanisa la kwanza, na Injili hiyo haijui habari zozote zinazohusiana na Yohana, mwana wa Zebedayo.[40] Katika uamuzi wa wasomi wengi, Injili hiyo iliundwa na “shule” ya wanafunzi wa Yesu, huenda ni huko Syria katika muongo wa mwisho wa karne ya kwanza.[41]

Kupingana

Ushahidi wa kuonyesha kutokuwa na uhakika wa mambo mengi yaliyomo katika Biblia, pia unaweza kupatikana katika kupingana kwingi kwa maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya. Ifuatayo ni mifano michache tu:

Agano la Kale

1.           Watunzi wa Samweli na Mambo ya Nyakati wanasimulia kisa kimoja kuhusu Mtume Daudi kufanya sensa ya Wayahudi. Hata hivyo, katika 2 Samweli, inaeleza kuwa Mtume Daudi alitenda hilo kwa maelekezo ya Mungu, huku 1 Mambo ya Nyakati, Daudi alitenda hilo kwa maelekezo ya Shetani.
2 SAMWELI 24:1
       Kuhesabu
Tena hasira za BWANA ikawaka juu a Israeli, akamtia Daudi nia juu yao, akisema, ukawahesabu Israeli na Yuda.
1 NYAKATI 21:1
       Kuhesabu
Tena Shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.
2.           Katika kuelezea urefu wa baa la tauni lililotabiriwa na Gad,[42] mtunzi wa 2 Samweli, analiorodhesha tukio hilo kuwa lilikuwa la miaka saba, huku mtunzi wa 1 Nyakati analiorodhesha kuwa lilikuwa la miaka mitatu.
2 SAMWELI 24:13
Baa la tauni
Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza,  akamwambia, Basi miaka saba ya njaa ikujie katika nchi yako? au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya sahauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.
1 NYAKATI 21:11-12
Baa la tauni
Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, BWANA asema hivi, Kubali upendavyo; miaka mitatu ya njaa au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa BWANA, yaani tauni katika nchi, na malaika wa BWANA akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli.
3.     Katika 2 Nyakati, Jehoiachin alielezwa kuwa alikuwa na miaka minane wakati alipoanza kutawala, huku katika 2 Wafalme anaelezwa kuwa alikuwa na miaka kumi na nane.
2 NYAKATI 36:9
Umri
Yekonia alikuwa na umri wa miaka minane (Biblia za kisasa zinaandika kumi na minane) alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi; akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
2 WAFALME 24:8
Umri
Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala miezi mitatu katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathan wa Yerusalemu.
4.     Mtunzi wa 2 Samweli alieleza idadi ya Wasyria waliokufa katika kipindi cha vita na Mtume Daudi kuwa walikuwa watu mia saba, huku mtunzi wa 1 Nyakati ametoa idadi yao ya kuwa ni watu elfu saba.
2 SAMWELI 10:18
Waliouawa
Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.
1 NYAKATI 19:18
Waliouawa
Washami Wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari saba elfu, na askari waendao kwa miguu arobaini elfu, naye akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.
Ingawa wengine wanaweza kusema kuwa kuongezeka au kuondoka kwa ‘1’ au zero si kitu cha muhimu sana, kwa kuwa ni kasoro za kunukuu tu, kwa hapa hilo silo tunalojadili kwa sababu Wayahudi walikuwa wanaandika kwa maneno idadi ya namba zao na hawakutunia namba.
Hitilafu kama hizo haziwezi kukubalika kuwa ni sehemu ya andiko takatifu lililofunuliwa. Zaidi ya hayo, yanathibitisha uwezekano wa kukosea kwa utunzi wa wanadamu na zaidi zinathibitisha kuwa maandiko ya Agano la Kale hayakulindwa na Mungu.

Agano Jipya

Katika Agano Jipya kunapatikana idadi kubwa ya kupingana kule kule kulikokuwepo katika Agano la kale. Ifuatayo ni mifano michache tu:
1.     Injili inatoa maelezo tofauti tofauti kuhusu ni nani aliyebeba msalaba unaodhaniwa kuwa ndio aliosulibiwa nao Yesu. Katika Mathayo, Marko, na Luka, mtu huyo alikuwa ni Saimoni Mkananayo, na katika Yohana, alikuwa ni Yesu.
LUKA 23:26[43]
Msalaba
Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shamba, wakamtwika msalaba, akauchuka nyuma  yake Yesu.
YOHANA, 19:16
Msalaba
Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulubiwe; nao wakampokea Yesu. Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahala paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.
2.     Baada ya “kusulubiwa” kwa Yesu, Injili inasema tofauti tofauti kuhusu ni nani aliyetembelea kaburi lake, wakati tukio hilo lilipotokea kabla ya kuchomoza jua, huku Injili ya Marko ikieleza kuwa hilo lilikuwa baada ya kuchomoza kwa jua. Katika Injili tatu nyingine:     (Marko, Luka, na Yohana) zinzeleza kuwa huyo mwanamke alilikuta jiwe la mlango wa kaburi limebiringikia mbali, lakini katika (Mathayo) hilo kaburi lilikuwa limefungwa hadi pale malaika aliposhuka mbele yao na kulibiringisha jiwe hilo na  kuliweka mbali.
MARKO 16:1-2
Kutembelea
Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza,
YOHANA 20:1- 4[44]
Kutembelea
Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kuangalia giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. 
MATHAYO 28:1-2
Kutembelea
Hata sabato ilipokwisha, ikapambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akiliviringisha lile jiwe akalikalia.
3.     Agano Jipya linatoa maelezo tofauti tofauti kuhusu majaaliwa ya Yuda Iskariote na pesa alizozipokea kwa kumsaliti Yesu. Katika Mathayo, Yuda alijiua mwenyewe, huku katika Matendo, alianguka kondeni na kufia huko.
MATHAYO 26:3-6
Majaaliwa ya Yuda
Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelethini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe. Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.
MATENDO YA MITUME 1:18
Majaaliwa ya Yuda
(Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka, matumbo yake yote yakatoka.
4.     Kinapolinganishwa kizazi cha Yesu kwa upande wa Daudi katika Mathayo 1:6-16, na Luka 3:23-31, kuna tofauti kubwa mno. Mosi, katika Mathayo, kuna wazazi 26 walio kati ya Yesu na Daudi huku katika Luka kuna wazazi 41. Pili, majina katika orodha zote mbili yanatofautiana kimsingi baada ya Daudi, ni majina mawili tu yanayofanana: nayo ni Yusufu na Zorobabel. Ajabu sana, orodha zote mbili zinaanza na Yusufu, eti ndiye baba yake Yesu, lakini katika Mathayo, mtunzi anarekodi kuwa babu wa kuumeni wa Yesu ni Yakobo, huku katika Luka anamtaja kuwa ni Heli. Kama mtu atakubali pendekezo la kuwa moja ya orodha hizo ndio inataja kizazi cha Maria, hilo haliwezi kuhesabiwa kuwa na tofauti yoyote baada ya kuwa mzee wao wa pamoja ni Daudi. Orodha zote mbili zinakutana tena kwa Abrahamu na baina ya Daudi na Abrahamu majina mengi ni sawasawa. Hata hivyo, katika orodha ya Mathayo, jina la mwana wa Hezron ni Ram, baba wa Ammin’adab, huku katika orodha ya Luka, jina la mwana wa Hezron ni Ami, ambaye mwanawe anaitwa Admin, baba wa Ammin’adab.[45] Kwa hiyo, kati ya Daudi na Abrahamu kuna mababa kumi na wawili katika orodha ya Mathayo, na mababa kumi na tatu katika orodha ya Luka. Hitilafu hizi na nyingine nyingi zilizo kama hizo katika Injili kwa uwazi kabisa ni makosa yanayotia kivuli cha shaka kuhusu uhakika wake wa kuwa ni maandiko matakatifu yaliyofunuliwa. Kwa hiyo, wasomi wengi wa Kikristo, leo hii, wanavitazama vitabu vya Agano la Kale na Jipya kuwa ni maelezo ya wanadamu wanayoyaamini kuwa yalifunuliwa na Mungu. Hata hivyo, hata madai ya kudai kuwa maandiko hayo yalifunuliwa na Mungu ni ya kuulizwa kwa kuwa yanaashiria kuwa Mungu amewafunulia watunzi waandike makosa na kupingana ndani ya Kitabu chake Kitakatifu.
Kuthibitisha uhalisia wa maagano yote mawili Jipya na la Kale ni jambo la kuhojiwa, hivyo inawezekana kusema kwa uhakika kabisa kuwa Biblia haiwezi kutumiwa na kuwa ndicho chanzo rejeo cha uhakika katika kuthibitisha suala la Yesu alikuwa nani, wala kuthibitisha yaliyomo katika ujumbe wake.

Quran

Kwa upande mwingine, Quran – inayoaminiwa na Waislamu kuwa ni neno la Mungu lililofunuliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) iliandikwa na kuhifadhiwa kwa moyo, kuanzia mwanzo hadi mwisho wake, ndani ya kipindi cha maisha ya Mtume Muhammad mwenyewe.
Ndani ya mwaka mmoja baada ya kifo chake, matini ya kwanza iliyosawa sawa iliandikwa na kukamilishwa.[46] Na ndani ya miaka kumi na nne baada ya kifo chake, nakala zilizoidhinishwa (Nakala za Athumani) zilitengenezwa kutokana na mswada huo wa kiwango cha sawa sawa[47] zilipelekwa katika makao makuu ya majimbo ya Kiislamu, na zile nakala zisizoidhinishwa ziliharibiwa.[48]
Tangu kufa kwa Mtume mwaka 632 CE, idadi kubwa ya watu - inayoongezeka - katika kila mfululizo wa vizazi wameshahifadhi kwa moyo matini yote ya Quran kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Leo hii wapo makumi elfu ya watu duniani wanasoma Quran yote, kwa moyo, katika mwezi wa Ramadhani kila mwaka, na katika matukio mengine.
Mmojawapo wa wataalamu wa mambo ya mashariki, Kenneth Cragg, amesema yafuatayo kuhusu kuhifadhiwa kwa moyo na kulindwa kwa maandiko ya Quran, “Tukio la kusomwa Quran linamaanisha kuwa Mandiko hayo yamepitia karne nyingi kwa mfuatano wa moyo wa kuipenda usiovunjika. Kwa hiyo, haiwezi, kushughulikiwa kama ni kitu cha kale, wala kuwa ni waraka wa kihistoria wa yaliopita.”[49] Mtaalamu mwingine wa mambo ya mashariki, William Graham, ameandika “Kwa mamilioni ya Waislamu wasio na Idadi, kwa zaidi ya karne kumi na nne za historia ya Uislamu, ‘Andiko’ al-kitabu kimekuwa ndicho kitabu kilichofunzwa, kisomeshwa na kusambazwa kwa njia ya kukikariri kwa sauti na kukihifadhi. Quran iliyoandikwa inaweza ‘kurekebisha’ kwa uwazi utunzi wa maandiko ya Neno la Mungu kwa njia isiyopata kujulikana katika historia, lakini utunzi wa kitabu cha Quran unatambulika kwa ukamilifu na utimilifu wake inaposomwa kwa usahihi.”[50] Ndio mtaalamu mwingine, John Burton, anaeleza: “Mfumo wa kusambaza Quran kutoka kizazi kimoja hadi kinachofuata kwa kuwataka watoto wahifadhi kwa njia ya mapokeo ya mdomo kutoka kwa wazee wao, kwa kiasi fulani tangu mwanzo wake, umepunguza makali ya hatari ya kutegemea moja kwa moja rekodi za maandishi…”[51] Mwishoni mwa kazi kubwa ya kuikusanya Quran, Burton ameeleza kuwa maandiko ya Quran yanayopatikana leo hii ni “maandiko yaliyotufikia katika mfumo uliopangwa na kuthibitishwa na Mtume… Kile tulicho nacho mikononi mwetu leo hii ni msahafu [52] wa Muhammad.”[53]

Uhakiki wa Maandiko

Msingi huo huo wa uchambuzi uliotumiwa katika miswada ya Biblia na wasomi wa Biblia na ambao umeweka wazi dosari na mabadiliko ya Biblia, umetumika kwa miswada ya Quran iliyokusanywa pamoja kutoka sehemu zote za dunia. Mswada wa kale wa Quran unapatikana katika Maktaba ya Congress Washington, Makumbusho ya Chester Beatty Dublin, Ireland, Makumbusho ya London, vile vile Makumbusho ya Tashkent, Uturuki na nchini Misri, vipindi vyote vya historia ya Uislamu, vimelinganishwa tangu mwanzo wake. Matokeo ya uchunguzi wote huo yanathibitisha kuwa hakuna badiliko lolote katika matini kutoka katika maandiko asilia. Kwa mfano, “Institute fur Koranforschung” ketengo hiki cha Chuo Kikuu cha Munich, Ujerumani, kimekusanya na kukusanya zaidi nakala kamili au zisizokamilika za Quran. Baada ya miaka hamsini ya utafiti, waliripoti kuwa, kuhusiana na tofauti baina ya nakala mbalimbali, hakuna, mbadala mwingine, ispokuwa yale makosa ya kawaida ya wanukuzi, ambayo yanaweza kurekebishwa kiwepesi. Kitengo hicho kiliharibiwa na mabomu ya Marekani wakati wa vita vya pili vya dunia.[54]

Kupingana katika Quran

Quran inabakia na uhalisia wa lugha yake; Kiarabu, na Quran inawapa changamoto wale wanaoisoma katika Sura ya An-Nisaa, 4:82, wagundue makosa ndani ya Quran, kama hawaiamini kama ni kweli inatoka kwa Mungu.
"أَفَلاَ يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللّهِ لَوَجَدُواْ فِيهِ اخْتِلاَفًا كَثِيراً"
"Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi." An-Nisaa, 4:82
Mifano michache ya “kupingana kwa wazi” imetajwa sana na wale wanaojaribu kuishusha Quran na kuiweka katika kiwango cha Biblia, mifano hiyo imefafanuliwa kiwepesi kabisa. Kwa mfano, “muumini wa kwanza” katika aya mbili zifuatazo:
Sura Al-An’aam 6:14
Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anayelisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.
Sura Al-Aaraf 7:143
…Basi alipojionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipozindukana alisema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini.
Aya ya kwanza inamtaja Mtume Muhammad (SAW), aliyeambiwa awafahamishe wapagani wa zama zake kuwa yeye kamwe hatokubali masanamu yao na atakuwa wa kwanza kumtii Allah. Katika aya ya pili, Mtume Musa (AS) anajieleza mwenyewe kuwa yeye ni wa kwanza miongoni mwa watu wa zama zake kumtii Allah baada ya kutambua kuwa haiwezekani kumuona Allah. Kila mtume alikuwa wa kwanza katika zama zake kumtii Allah.
Sawasawa na, “siku moja mbele ya Mungu” iliyotajwa katika aya mbili zifuatazo:
 Sura Al-Sajdah 32:5
Anapitisha mambo yote yalio baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohisabu nyinyi.
Sura Al-Mi’raaj 70:4
Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!
Aya mbili hizo zinaashiria matukio mawili tofauti kabisa. Aya ya kwanza inaashiria uwezo wa kuituma na kuirejesha ripoti katika siku inayofanana na miaka elfu ya maisha ya kibinadamu.[55] Na ya pili inaashiria kupaa kwa malaika kutoka dunia hadi mbingu za juu, jambo ambalo linawachukua hao malaika siku moja tu iliyo sawa na miaka hamsini elfu 50,000 ya kibinadamu.[56] Mungu hasimamiwi na wakati. Yeye ameuumba wakati na kuufanya uwe unahusiana na viumbe wanaoendeshwa na huo wakati. Kwa hiyo, kwa mujibu wa mahesabu ya wanasayansi wa kisasa, mwaka mmoja wa Mars ni sawa na siku 687 za Dunia, wakati mwaka mmoja wa Uranusi ni sawa na miaka 84 ya Dunia.[57]
Matini ya Quran ina uthabiti unaotambulika kwa mada zake na uwasilishaje wake. Katika utangulizi wa moja ya tafsiri bora ya Quran ya mtaalamu wa mambo ya kimashariki, mfasiri, Arthur John Arberry, anaandika: “Kuna hazina ya habari ya viini vilivyoshikamana vinavyotembea katika Quran yote; kila Sura[58] inachanganua au inadokeza[59] moja au mengi miongoni mwa hazina hizo. Kwa kutumia lugha ya kimziki, kila Sura ni utungo wa furaha uliotungwa kwa dhamira kuu yenye kujirudiarudia[60] kwa Sura yote au vipande vipande, mlinganisho unaongezwa nguvu na midundo mbali mbali ya kistadi sana inayotiririka kwa mtiririko wa hotuba.”[61]
Marejeo ya kisayansi ndani ya maandiko ya Quran yamethibitisha kuwa ni ya uhakika na yenye ubora usioelezeka. Katika muhadhara uliotolewa katika French Academy of Medicine, mwaka 1976, wenye kichwa “Data za Fiziolojia na Embriolojia katika Quran”, Dr. Maurice Bucaille amesema, “Hukuna kazi za binadamu zinazokusanya maelezo ya kiwango cha kina zaidi kisayansi katika wakati wa Quran na kuipita Quran. Mawazo ya kisayansi yakilinganishwa na yale yaliyomo katika Quran yanatoa elimu ya kisasa.”[62]
Akiongelea kuhusu utunzi wa Quran, Profesa Reynold A. Nicholson amesema, “Tuna [ndani ya Kuruna] vitu vya kipekee na mamlaka isiyokanushika kwa mfululizo wa asili na maendeleo ya mwanzo ya Uislamu, vitu kama hivyo, havipo katika Ubudha wala Ukristo wala dini yoyote ya kale.”[63]
Kwa hiyo, ni Quran pekee inayowakilisha kama njia madhubuti ya kutoa uamuzi juu ya Yesu alikuwa ni nani na ujumbe wake ulikuwa ni nini. Zaidi ya hayo, vilevile Quran inaweza kutumika kuamua ni kwa kiwango gani baadhi ya maneno ya ufunuo wa Mungu yanaendelea kuwepo ndani ya Biblia.
Katika Quran, Mungu anawaamuru walioamini wayakubali, - na hiyo ikiwa ni sehemu ya imani yao - maneno matakatifu yaliyofunuliwa kwa Mtume Musa, yanayojulikana kama Torati, na Mtume Daudi katika Zaburi asilia; na Yesu katika Injili asilia. Waislamu wote wanapaswa kuamini vitabu vyote vilivyofunuliwa. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa katika Quran, vitabu vyote vilivyofunuliwa kabla ya Quran havipo kama vilivyokuwa. Watu wamebadilisha sehemu za vitabu hivyo ili ziafikiane na matamanio yao.
"فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـذَا مِنْ عِندِ اللّهِ لِيَشْتَرُواْ بِهِ ثَمَناً قَلِيلاً فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُمْ مِّمَّا يَكْسِبُونَ"
"Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyoandika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma." Al-Baqarah 2:79
Zaidi ya hayo, katika Agano la Kale, Mungu ananukuliwa katika Yeremia 8:8 akisema, “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na Torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.[64]

Sura ya Pili: Yesu Mwanadamu

Kama ilivyoonyeshwa katika sura iliyopita, maandiko ya Biblia, maagano yote mawili; Jipya na la Kale, ni chanzo kisichotegemewa, na kwa hiyo, hakiwezi kutumiwa kama njia ya uhakika wa kuujua ukweli kuhusu mtu aliyeitwa Yesu Kristo au kuhusu kazi na ujumbe wake. Hata hivyo, ukaguzi wa makini wa maandiko haya katika mwangaza wa aya za Quran utafunua baadhi ya ukweli unaomuhusu Yesu aliyeishi katika Biblia.

Mtume

Kwa kupitia Quran, kimsingi Yesu ametambulishwa kuwa ni Mtume wa Mungu. Katika Sura As-Saff 61:6, Mungu anamnukulu Yesu kama ifuatavyo:
"وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ ..."
"Na Isa bin Mariamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati…" As-Saff 61:6
Kuna aya nyingi katika Agano Jipya zinazounga mkono utume/unabii wa Yesu. Zifuatazo ni aya chache tu miongoni mwa aya hizo: katika Mathayo 21:11, watu wa zama za Yesu wamerekodiwa wakimchukulia Yesu kuwa ni mtume: “Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.” Katika Marko, 6:4, imeelezwa kuwa Yesu amejitaja yeye mwenyewe kuwa ni mtume: “Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, ispokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani kwake.” Katika aya zifuatazo, Yesu anachukuliwa kuwa ametumwa akiwa ni mjumbe. Katika Mathayo 10:40, imedaiwa Yesu amesema kuwa: “Awapokee ninyi, anipokee mimi, naye anipokeaye mimi, ampokea aliyenituma.” Katika Yohana 17:3, pia, Yesu alinukuliwa akisema: “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”[65]

Mtu

Aya za ufunuo wa Quran sio tu zinathibitisha utume wa Yesu, lakini pia zinakana kiwazi wazi uungu wa Yesu. Katika Sura ya Al-Maaidah, 5:75, Mungu anaashiria kuwa Yesu alikula chakula, tendo ambalo ni la kibinadamu, na kwa uwazi kabisa halimfai Mungu.
"مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلاَّ رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ كَانَا يَأْكُلاَنِ الطَّعَامَ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّى يُؤْفَكُونَ"
"Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwishapita Mitume kabla yake. Na mama yake nimwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyowabainishia Aya, kasha angalia vipi wanavyogeuzwa." Al-Maaidah, 5:75
Kuna vifungu vingi katika Agano Jipya vinavyokana uungu wa Yesu. Kwa nfano, katika Mathayo 19:17, Yesu alimjibu yule aliyemtambulisha yeye kama ni “Mwalimu mwema” kwa kusema “Akawaambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja…” Kama Yesu amekataa kuitwa “mwema”,[66] na ameeleza kuwa ni mungu pekee ndiye aliyemwema wa kweli, naye kwa uwazi kabisa ameashiria kuwa yeye si Mungu. Katika Yohana 14:28, yesu alikuwa anasema: “Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahia kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.” Kwa kusema “Baba” ni mkuu kuliko yeye, Yesu amejitenganisha na Mungu. Pia katika Yohana 20:17, Yesu alimwambia Mariam Magdalene awaambie wafuasi zake: "Yesu akawaambia, Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.” Yesu amemwashiria Mungu kuwa ni “Baba yangu na Baba yenu” amesisitiza zaidi, tofauti yake na Mungu. Zaidi ya hayo, Yesu amemwashiria Mungu kuwa ni “Mungu wake”, hakutoa nafasi kwa yoyote kudai kiujanja ujanja kuwa Yeye Yesu ndiye Mungu.
Ingawa katika baadhi ya maandiko ya Paulo, yaliyochukuliwa na kanisa kuwa ni matakatifu, Yesu anaonyeshwa kuwa ni “mtu” ametofautiana na kutengana na Mungu. Katika 1 Timotheo 2:5, Paulo anaandika “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu.”
Pia kuna aya katika Quran zinazothibitisha utu wa Mtume Muhammad (SAW), ili kuwakinga wafuasi wake wasimapandishe na kuwa na hali za uungu au nusu Mungu, kama ilivyofanywa kwa Nabii Yesu. Kwa mfano, katika Sura ya Al-Kahfi 18:110, Allah anamwelekeza Mtume Muhammad (SAW) awafahamishe wote wanaosikia ujumbe wake:
"قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَى إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ..."
"Sema: Mimi ni mwanadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja…" Al-Kahfi 18:110
Katika sura Al-A'raaf 7:187, pia, Allah anamuelekeza Mtume Muhammad (SAW) akiri kuwa Siku ya Hukumu inajulikana na Mungu tu.
"يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي لاَ يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلاَّ هُوَ..."
"Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye…" Al-A'raaf 7:187

Katika Injili, kwa mujibu wa Marko 13:31-32, vilevile, Yesu anaripotiwa kukana kuwa hana elimu ya kujua lini itakuja saa ya mwisho ya dunia hii, anasema: “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Moja ya sifa za Mungu ni mjuzi, mjuzi wa kila kitu. Kwa hiyo, kukataa kwa Yesu kuwa hajui siku ya hukumu pia ni kukataa uungu, kwa kuwa yule asiyejua muda wa saa ya mwisho hawezi kuwa Mungu.[67]

Dhana sahihi

Quran inathibitisha maelezo ya Biblia kuhusu Yesu kuwa amezaliwa na bikira. Hata hivyo, katika vifungu vya Quran kuhusu kuzaliwa kwa Yesu inasema, Mariamu alikuwa ni mwanamwali asiyeolewa na ambaye maisha yake yalitolewa na mama yake yawe ya kumwabudu Mungu. Alipokuwa anaabudu katika eneo la kidini la kujitengea na watu, malaika alimjia na kumweleza juu ya kushika mimba kwake kuliko karibia mno.
"إِذْ قَالَتِ الْمَلآئِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ"
"Na pale Malaika waliposema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa waliokaribishwa (kwa Mwenyezi Mungu)." Aal-‘Imran 3:45
"قََالَتْ رَبِّ أَنَّى يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ قَالَ كَذَلِكِ اللّهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاء إِذَا قَضَى أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ."
"Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho. Anapohukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa.  Aal-‘Imran 3:47
Hata hivyo, Quran inafafanua kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kibikira hakujambadilisha hali ya ubinadamu. Kuumbwa kwake ni sawa na kuumbwa kwa Adamu, ambaye hakuwa na baba wala mama.
"إِنَّ مَثَلَ عِيسَى عِندَ اللّهِ كَمَثَلِ آدَمَ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثِمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ."
"Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. Aal-‘Imran 3:59

Miujiza

Vifungu vya Quran kuhusu mahubiri ya Yesu vinathibitisha miujiza yake mingi[68] iliyotajwa katika Biblia. Kwa mfano, Quran inaeleza kuwa Yesu alikuwa ni mjumbe wa Mungu tangu kuzaliwa kwake, na mwujiza wake wa kwanza ulikuwa ni kuzungumza akiwa ni mtoto mchanga. Mariamu baada ya kumzaa Yesu, watu walimtuhumu kwa uasherati. Badala ya kujibu tuhuma zao, alimwashiria mwanawe aliyemzaa karibuni:
"فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا."
"Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliyebado mdogo yumo katika malezi? (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii." Maryam 19:29-30
Miongoni mwa miujiza yake ni kufufua wafu, kuponya wakoma, na kufanya vipofu waone, Quran inarekodi miujiza mingine isiyotajwa katika Biblia. Nabii Yesu aliwaunda ndege kwa udongo mfinyanzi, kisha akawapulizia na wale ndege wakaruka, wakiwa hai. Lakini nukta inayosisitizwa na Quran ni kuwa wakati wowote ule Yesu alipotekeleza miujiza, aliwaeleza watu kuwa hilo limetokea kwa idhini ya Mungu. Aliwawekea wazi wafuasi zake kuwa, yeye hakufanya mwujiza kwa uwezo wake mwenyewe, kwa njia ile ile walioitumia Mitume iliyopita kabla yake kwa uwazi kabisa kwa waliowazunguka.
Kwa bahati mbaya, wale wanaodai uungu wa Yesu, siku zote, wanang`ang`ania miujiza kama ndio ushahidi. Hata hivyo, mitume wengine wamenukuliwa kuwa wamefanya miujiza kama hiyo katika Agano la Kale.
Yesu aliwalisha watu 5,000 kwa vipande vitano vya mkate na samaki wawili.
Elisha aliwalisha watu 100 ---  (2 Wafalme 4:44)
Yesu aliwaponya wakoma.
Elisha alimtibu mkoma Naaman (2 Wafalme 5:14).
Yesu alimfanya kipofu aone.
Elisha alimfanya kipofu aone (2 Wafalme 6:17 na 20).
Yesu alifufua wafu.
Elijah alifanya hayo hayo (1 Wafalme 17:22) Pia na Elisha ameyafanya (2 Wafalme 4:34). Vilevile hata mifupa ya Elisha inawafufua wafu (2 Wafalme 13:21).
Yesu alitembea katika maji.
Musa na watu wake walivuka bahari maiti (Kutoka 14:22).
 Pia kuna andiko katika Agano Jipya linalothibitisha kuwa Yesu hakutenda kwa uwezo wake. Yesu ananukuliwa katika Yohana 5:30, akisema: “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.”. Katika Matendo 2:22, Paulo anandika: “Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua.”

“Ushahidi” wa Uungu wa Yesu

Kuna baadhi ya mistari iliyotafsiriwa na makanisa ya Kikatoliki pamoja na Kiprotestanti kuwa ndio ushahidi wa uungu wa Yesu Kristo. Hata hivyo, kwa uchunguzi wa kina kuhusu mistari hiyo, imekuwa ni dhahiri kuwa, ama maneno yake ni tata, yanayoacha tafsiri nyingi tofauti tofauti, au imeongezwa na haikuwepo katika miswada ya mwanzo ya mapokeo ya Biblia. Ifuatayo ni baadhi ya mistari hiyo iliyotajwa sana:

1. Mwanzo na Mwisho

Katika kitabu cha Ufunuo 1:8, inadokezwa kuwa Yesu amesema yafuatayo kujihusu yeye mwenyewe: “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi”. Hizi ni sifa za Mungu. Kwa hiyo, hapa Yesu, kwa mujibu wa Wakristo wa mwanzo, anadai uungu. Hata hivyo, hayo maneno yalitajwa hapo juu ni kwa mujibu wa toleo la King James Version. Ama katika toleo la Revised Standard Version, wasomi wa Biblia wanarekebisha makosa ya kitafsiri na wameandika: “Mimi ni wa mwanzo na wa Mwishom” asema Bwana Mungu,..”.  Pia, marekebisho yalifanywa katika toleo la New American Bible iliyotayarishwa na Wakatoliki. Tafsri ya aya hiyo imerekebishwa ili iwekwe katika muktadha wake ulio sahihi kama ifuatavyo: “Bwana Mungu anasema: “Mimi ni wa mwanzo na wa Mwishom…” Ikiwa na marekebisho haya, inadhihirika kuwa, mstari huu ulikuwa ni maelezo ya Mungu na sio maelezo ya Mtume Yesu. 

2. Maisha ya kabla ya Kristo

Mstari mwingine unaotumiwa sana ili kuunga mkono uungu wa Yesu ni Yohana 8:58: “Yesu akawaambia, amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Mstari huu umechukuliwa na kuashiria kuwa Yesu alikuwepo kabla ya kudhihiri kwake duniani. Uamuzi uliofikiwa kutokana na mstari huo ni kuwa Yesu lazima awe Mungu, kwa kuwa kuwepo kwake kumetangulia tarehe ya kuzaliwa kwake duniani. Hata hivyo, dhana ya kuwepo kabla ya kudhihiri kwa mitume, na kwa watu wengine, ipo katila vitabu vyote viwili, Agano la Kale, vilevile katika Quran. Yeremia anajielezea mwenyewe katika Kitabu Cha Yeremia 1:4-5 kama ifuatavyo:
“Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”
Nabii Suleimani anaripotiwa katika Mithali 8:23-27, ya kuwa amesema, “Nalitukuka tokea milele, tangu awali, kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa, Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji. Kabla milima haijawekwa imara, Kabla ya vilima nalizaliwa. Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde, Wala chanzo cha mavumbi ya dunia; Alipozithibitisha mbingu nalikuwako…"
Kwa mujibu wa Ayubu 38:4 na 21, Mungu amemtambulisha Nabii Ayubu kama ifuatavyo: “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa unafahamu.”
Katika Quran, Sura ya  Al-A’aaraf, 7:172, Mungu anaeleza kuwa mwanadamu alikuwepo kiroho kabla ya kuumbwa ulimwengu wa kimwili.
"وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنفُسِهِمْ أَلَسْتَ بِرَبِّكُمْ قَالُواْ بَلَى شَهِدْنَا أَن تَقُولُواْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ."
"Na pale Mola wako Mlezi alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwa kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo." Al-A’aaraf, 7:172
Kwa hiyo, maelezo ya Mtume Yesu, “Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko”. Hayawezi kutumiwa kuwa ni ushahidi wa uungu wake. Katika muktadha wa Yohana 8:54, Yesu amedaiwa kuwa ametamka kuhusu ujuzi wa Mungu kwa Mitume yake, ambayo inatangulia tarehe ya kuumbwa kwao katika ulimwengu huu.

3. Mwana wa Mungu

Ushahidi mwingine uliotumiwa kwa ajili ya uungu wa Yesu ni kule  kutumiwa sifa ya “Mwana wa Mungu” kwa Yesu. Hata hivyo, kuna sehemu nyingi katika Agano la Kale ilipotumiwa sifa hiyo kwa watu wengine.
Mungu alimwita Israeli (Nabii Yakubu) “Mwanawe” pale alipomuelekeza Mtume Musa aende kwa Firauni katika Kutoka 4:22-23, “Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia…”[69]
Katika 2 Samweli 7:13-14, Mungu anamwita Nabii Suleimani Mwanawe, "Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu…"
Mungu alimuahidi Nabii Daudi kumfanya mwanawe katika Zaburi 89:26-27: “Yeye ataniita, Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.”[70]
Malaika wanachukuliwa kuwa ni “wana wa Mungu” katika kitabu cha Ayubu 1:6, “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.[71]
Katika Agano Jipya, kuna marejeo mengi ya “mwana wa Mungu” ya watu wengine wasio Yesu. Kwa mfano, pale mtunzi wa Injili kwa mujibu wa Luka amewaorodhesha wahenga wake hadi kwa Adamu, ameandika: Luka 3:38 “Wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu”.[72]
Baadhi ya watu wanadai kuwa kile cha kipekee kilichopo kwa Yesu ni kuwa yeye ndiye mwana wa pekee wa kuzaliwa[73] Mwana wa Mungu, huku hao wengine ni “wana wa Mungu tu.” Hata hivyo, Mungu ananukuliwa akimwambia Mtume Daudi, katika Zaburi 2:7, “Nitaihubiri amri, BWANA aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.”
Pia inapaswa ijulikane kuwa hakuna hata sehemu moja katika Injili ambapo Yesu alijiita yeye mwenyewe kuwa yeye hasa ndiye “mwana wa Mungu”.[74] Badala yake, amenukuliwa kuwa amekariri kujiita “Mwana wa Adamu” (mfano Luka 9:22) kwa mara zisizohesabika. Na katika Luka 4:41, kwa hakika amekataa kuitwa “Mwana wa Mungu”: “Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.”
Kwa kuwa Wayahudi wanaamini kuwa Mungu ni Mmoja, na hana mke wala mtoto kwa maana halisi yoyote ile, ni wazi kuwa ibara “mwana wa Mungu” kwa Wayahudi ina maana ya “Mtumishi wa Mungu tu” yaani mtu aliye karibu na Mungu, kwa sababu ya huduma yake ya kiimani, akiwa kama mtoto kwa baba yake. Wakristo waliokuja kutoka katika historia za kuwa walikuwa ni Wagiriki au Warumi, baadaye waliitumia vibaya istilahi hiyo. Kwani katika urithi wao, “mwana wa Mungu” inamaanisha mungu ana mwili au mtu aliyezaliwa kwa muungano wa kimwili kati ya mungu mwanamume na mwanamke.[75] Wakati Kanisa lilipoacha msingi wa Kiyahudi, lilitwaa dhana ya kipagani ya “mwana wa Mungu”, ambayo kwa ukamilifu, ilikuwa ni tofauti na matumizi ya Kiyahudi.[76]
Kwa hiyo, matumizi ya istilahi “mwana wa Mungu” inafaa ifahamike kuwa ni alama ya ufahamu ya kisemintiki yenye maana “mtumishi wa Mungu”, na sio katika ufahamu wa kipagani wa uhalisi wa kuwa kinda la Mungu. Katika Injili nne, Yesu anarekodiwa akisema: “Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.” Mathayo 5:9.[77]
Vivo hivyo, matumizi ya Yesu ya istilahi abba, “baba mpendwa” lazima ifahamike hivyo hivyo. Kuna ubishani miongoni mwa wasomi wa Agano Jipya juu ya nini maana ya abba kwa uhakika kabisa katika zama za Yesu na Wayahudi wa makundi mengine wa muongo huo huo walilitumia kwa upana gani.
Hivi karibuni kwa ukali kabisa, James Barr amedai kuwa hilo halikuonyesha wazi wazi ufahamu wa kuwa hilo lilikuwa linamuhusu yeye ila hilo kiwepesi kabisa linaashiria “baba” tu.[78] Ili kufikiria kuwa Mungu ni “Baba yetu wa mbinguni” haina maana mpya, kwa kuwa katika sala ya bwana amenukuliwa kuwa amewafundisha wanafunzi wake kumtambulisha Mungu katika njia hii hii.

4. Pamoja na Mungu

Wale wanaodai kuwa Yesu alikuwa Mungu, wanashikilia kuwa yeye hakuwa Mungu aliyetengeka, bali ni mmoja na ni Mungu yule yule mwenye mwili. Wao wanaunga mkono imani hii kutokana na mstari wa 30 wa Injili kwa mujibu wa Yohana, sura 10, ambayo ndani yake Yesu anaripotiwa kuwa amesema, “Mimi na Baba ni kitu kimoja.” Nje ya muktadha, mstari huu unaashiria uungu wa Yesu. Hata hivyo, pale Wayahudi walipomtuhumu kwa kudai uungu, kwa kutegemea sentesi hiyo, Yohana 10:34 “Yesu akawajibu, Je, haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu;"[79] Amewabainishia, kwa mfano wa maandiko unaojulikana sana kwao, kuwa yeye alikuwa anatumia lugha ya kistiari ya manabii ambayo haipaswi kufasiriwa kwa kujipachika uungu yeye mwenyewe au kwa mtu mwingine yoyote.
Ushahidi zaidi unachukuliwa kutoka katika mstari wa kumi na wa kumi na moja wa Injili kwa mujibu wa Yohana, sura ya 14, pale watu walipomtaka Yesu awaonyeshe Baba, naye inaaminiwa alisema: "Husadiki ya kwambi mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwambi mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.”
Ibara hizi zingeashiria uungu wa Yesu, kama sehemu iliyobakia ya Injili hiyo hiyo inapuuzwa. Hata hivyo, aya tisa baadaye, katika Yohana 14:20, pia Yesu anarekodiwa akiwaambia wanafunzi wake, "Siku ile mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.” Kwa hiyo, kama maelezo ya Yesu "Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; yanamaanisha kuwa yeye ni Mungu, basi vivyo hivyo iwe kwa wanafunzi wa Yesu. Hii sentensi ya kiishara inamaanisha umoja wa lengo na sio umoja wa asili. Tafsiri ya kiishara inasisitizwa zaidi katika Yohana 17:20-21, pale Yesu aliposema, "Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.”[80]

5. Amekubali kusujudiwa

Inadaiwa kuwa Yesu tangu aliporipotiwa kuwa amekubali kusujudiwa na baadhi ya wafuasi zake, lazima atakuwa ni Mungu. Hata hivyo, uchunguzi makini kuhusu andiko hilo unaashiria mambo mawili; tafsiri wasiwasi, na tafsiri potofu. Istilahi “kusujudu” inaweza kupatikana katika King Jemes Version na The Revised Standard Version yakielezea watu watatu wenye busara waliokuja kutokea mashariki. Wameripotiwa katika Mathayo 2:2, wakisema, "Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.”[81] Hata hivyo, katika Biblia ya The New American Bible (Catholic Press, 1970), hilo andiko linasomeka: "Yu wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa sasa? Tumeona nyota yake ikichomoza na tumekuja kutoa heshima kwake.”
Katika The Revised Standard Version, Yohana 9:37-38, "Yesu akawaambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia. [82] Hata hivyo, katika The American Biblke, wafasiri wasomi wameongeza tanbibihi inayosomeka: 9:38. Mstari huu, imefutwa kwa umuhimu wa MSS [miswada], unaweza kuwa ni nyongeza kwa liturujia ya ubatizo.
Mistari hii haipatikani katika miswada muhimu ya kale yenye Injili hii. Huenda ni nyongeza ya baadaye iliyowekwa na waandishi wa kanisa ili yatumike katika huduma ya ubatizo. Zaidi, kama alivyofafanua, mwenye mamlaka makuu na adhima katika Biblia na lugha zake za asili, George M. Lamsa, “Neno la Kiarama sagad, sujudu, pia lina maana ya kuinama au kupiga goti kwa watu wa mashariki wakati wa kusalimiana kwa kawaida ya kuinamisha kichwa au kuinama chini.[83] “Alimsujudia”  haiashirii kuwa yeye alimwabudu Yesu kama vile mtu alivyomwabudu Mungu. Tendo kama hilo lilitakiwa lichukuliwe ni la kukufuru na la uvunjaji wa Amri ya kwanza mbele ya macho ya Wayahudi, na huyo mtu angepigwa mawe. Lakini yeye alipiga magoti mbele yake kwa kutoa heshima na shukurani.”[84]
Kitabu cha mwisho, Quran, kinaeleza tukio la kuabudiwa au kutoabudiwa kwa Yesu, kwa kunukuu mazungumzo yatakayotokea baina ya Yesu na Mungu siku ya Kiama. Allah anaeleza katika Sura Al-Maa`idah, 5:116-117
"وَإِذْ قَالَ اللّهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـهَيْنِ مِن دُونِ اللّهِ...،  مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلاَّ مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُواْ اللّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ..."
"Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu?...,  (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu…, Sikuwaambia lolote ila uliyoniamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi…" Al-Maa`idah, 5:116-117

6. "Hapo mwanzo kulikuwa na Neno"

Huenda ‘ushahidi’ wa uungu wa Yesu ulionukuliwa sana ni Yohana 1:1 na 14, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, na Neno alikuwa Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” Hata hivyo, maelezo haya hayakutolewa na Yesu Kristo, wala hayakuhusishwa naye na mtunzi wa Injili kwa mujibu wa Yohana. Hivyo, mistari hii haiundi ushahidi wa uungu wa Yesu, hasa hasa kuzingatia shaka inayoshikiliwa na wasomi wa Kikristo juu ya Injili ya Nne. Wasomi wa Biblia waliotunga Injili tano: “Picha mbili zilizochorwa na Yohana na muhtasari wa injili (yaani Injili ya Mathayo, Marko na Luka) zote mbili haziwezi kuwa ubainifu wa kihistoria.[85] Neno lilohusishwa na Yesu katika Injili ya Nne limeundwa na wainjilisti kwa sehemu kubwa, na linaakisi mwendelezo wa lugha ya jamii ya Wakristo wa Kiyohana.[86] Neno la Kigiriki lilotumiwa na mtunzi wa Injili ya Nne asiyejulikana kwa “neno” ni logos.[87] Kwa kufanya hivyo, huyo mtunzi anamtambulisha Yesu kwa logos la wanafalsa wapagani wa Kigiriki, neno ambalo lilikuwa na lengo takatifu na thabiti lililojitokeza ulimwenguni, huyo mtunzi akalipangilia neno hilo na kulipa mfumo na maana.[88]
Wazo la logos katika fikra za Kigiriki huenda linarejea nyuma, kwa uchache hadi kwa mwanafalsafa wa karne ya sita BC, Heracleitus, aliyependekeza kuwa, kulikuwa na logos ulimwenguni anayetenda kwa mwanadamu kulingana na nguvu ya hoja. Baadaye, Stoics[89] analitambulisha logos kuwa ni tendo, mantiki, na kanuni ya kiroho inayosambaa katika ukweli wote.[90] Mwanafalsafa wa Kiyahudi anayeongea Kigiriki, Judaeus Philo wa Alexandria (15 BC -45 CE), amefundisha kuwa logos alikuwa ni mpatanishi baina ya Mungu na ulimwengu, kwa kuwa na sifa mbili za uwakala wa Mungu na ulimwengu,  na kuwa na sifa mbili za uwakala wa viumbe na wakala wa ambaye kupitia kwake akili ya mwanadamu inaweza kumfahamu Mungu.[91] Maandiko ya Philo yalihifadhiwa na kutunzwa na kanisa, na kueneza ufunuo kwa mafundisho ya kistaarabu ya tiolojia ya kifalsafa ya Kikristo. Aliacha mafundisho ya fikra za Kipilato wakichukulia logos (Neno) na kuliita “mtoto wa kwanza wa kuzaliwa na Mungu.”[92]
Utambulisho wa Yesu kwa logos, uliendelezwa katika kanisa la kwanza ikiwa ni tokeo la majaribio yaliyofanywa na wanatiolojia wa kwanza wa Kikristo pamoja na watetezi kuielezea imani ya Kikristo kwa istilahi ambayo ingekuwa wazi kwa ulimwengu wa Wayunani. Zaidi ya hayo, ilikuwa ni kuwavutia wasikilizaji wao na mtazamo wao kuwa Ukristo ulikuwa unashinda, au mrithi wa wale wote waliokuwa wanafalsafa bora wa kipagani. Kwa hiyo, katika kazi zao za utetezi na ubishani, Mapadri wa Kikristo wa kwanza wameeleza kuwa Yesu alikuwa ni logos aliyekuwepo hapo kabla.[93]
Neno la Kigiriki lililotumika kwa maana ya ‘Mungu’ katika hiyo ibara ni “na Neno lilikuwa kwa Mungu,” lipo katika mtindo wa “definite form- yaani mtindo uliowazi, au unaofahamika” batheos, Linalomaanisha “Huyo Mungu, au Mungu maalum”. Hata hivyo, katika ibara ya pili “na Neno alikuwa Mungu”, neno la Kigiriki lililotumika kwa maana ya ‘Mungu’ katika ibara lipo katika mtindo wa “indefinite form- yaani mtindo usiowazi, au usiofahamika” tontheos, Linalomaanisha ‘mungu yoyote, yaani mungu asiyejulikana, au mungu yoyote asiye maalumu’.[94] Kwa hiyo, Yohana 1:1, kwa uwazi zaidi ilipaswa itafsiriwe, “Hapo Mwanzo kulikuwa na Neno, na hilo Neno lilikuwa kwa Mungu, na hilo Neno lilikuwa mungu mwingine.” Kwa hiyo, kama hilo neno lilikuwa mungu mwingine kwa ufahamu wa kifasihi, itamaanisha kuwa kulikuwa na miungu miwili na sio mmoja. Hata hivyo, katika lugha ya Kibiblia, neno ‘mungu – asiyefahamika’ linatumika kwa maana ya istiari ili kuashiria nguvu. Kwa mfano, Paulo alimtaja shetani kuwa ni ‘mungu – asiyefahamika’ katika 2 Wakorintho 4:4, "ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu." Pia, Musa alitajwa kama ni ‘mungu – asiyefahamika’ katika Kutoka 7:1, "BWANA akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruna atakuwa nabii wako.[95]

Mawazo ya kale

Kulikuwa na mgogoro mkubwa kati ya tafsiri ya Pauline na ya Jerusalem kuhusu Yesu na ujumbe wake. Mgogoro huo, baada ya kutokea pole pole kwa miaka mingi, hatimaye ulipelekea mpasuko kabisa, katika mpasuko huo, ulipelekea kuundwa Kanisa la Wakristo wa Pauline, kwa athari hiyo, dini mpya iliyojitenga kutoka Uyahudi. Kwa upande mwingine, Wanazareti wa Jerusalem hawakukata uhusiano wao na Uyahudi, bali walijizingatia kuwa wao ndio kiini cha kuutekeleza Uyahudi, watiifu wa Torati, pia walimwamini Yesu, umbo la Masihi mwanadamu.[96]
Wakati uasi wa Kiyahudi ulipopondwa pondwa na Warumi na mahekalu yao kuharibiwa mwaka 70 CE, Wakristo wa Kiyahudi walitawanyika, nguvu yao na mvuto wao wa kuwa wao ndio Kanisa Mama na kituo cha vuguvugu la Yesu zilifikia kikomo.[97] Vuguvugu la Wakristo wa Kipauline, vuguvugu ambalo mpaka mwaka 66 CE. Lilikuwa linapigania liendelee kuishi, dhidi ya kutokubaliwa huko Jerusalem, sasa lilianza kusonga mbele.
Kanisa la Jerusalem, chini ya uongozi wa James, kiasili lilijulikana kuwa ni la Wanazareti, baadaye likajulikana kwa jina la kupanga na la kuaibisha la Ebionites (Kwa kiyahudi evyonium, “watu maskini”), jina ambalo baadhi ya Wanazareti walilitwaa kwa ufahari wakilichukulia kuwa ni kikumbusho cha maneno ya Yesu yasemayo, “Wabarikiwe maskini.” Baada ya Kanisa la Graeco-Roman kushika hatamu, Wanazareti wakawa wanadharauliwa na kuonwa kuwa ni waasi, kwa sababu ya kukataa kwao mafundisho ya Paulo.[98]
Kwa mujibu wa historia ya kanisa la wahenga, Irenaeus (c. 185 CE,) hao watu maskini walimwamini Mungu mmoja, Muumba, aliyefundisha kuwa Yesu alikuwa ni masihi, kwa mujibu wa Mathayo, walitumia Injili tu, na kumpinga Paulo kwa kumwona kuwa ni muasi aliyeasi Sheria ya Kiyahudi.[99]
Hao watu maskini walijulikana kuwa waliishi mpaka katika karne ya nne. Baadhi yao walihama Palestina na wakaishi huko Transjordan na Syria na baadaye sehemu hiyo ikajulikana kuwa ni Asia ndogo, Misri na Roma [100].
Kwa mfumo wa kifalme,[101] vuguvugu la Wakristo wa Mataifa lilioendelezwa kipindi cha karne ya pili na ya tatu liliendelea kuwakilisha mtazamo wa kuamini Mungu mmoja uliokithiri na ule wa Waibionia ‘watu maskini’. Mtazamo huo ulishikilia kuwa Kristo alikuwa ni mtu, mimba yake ni ya kimuujiza, lakini alikuwa ni “mwana wa Mungu” wa pekee kwa kuwa amejazwa busara takatifu na nguvu. Mtazamo huu ulifundishwa huko Roma takriban mwishoni mwa karne ya pili na Theodotus, aliyetengwa na Papa Victor, na ulifundishwa sehemu Fulani hapo baadaye na Artemon, aliyetengwa na Papa Zephyrinus. Takriban mwaka 260 CE mtazamo huo ulifundishwa tena na Paulo wa Samosata,[102] Askofu mkuu wa Antokia huko Syria, ambaye alihubiri kiwazi wazi kuwa Yesu alikuwa ni mtu na kupitia kwake Mungu ameongea maneno yake (Logos), naye kwa nguvu kabisa amethibitisha upweke wa Mungu.
Kati ya mwaka 263 na 268 kwa uchache vikao vitatu vya baraza la kanisa viliitishwa huko Antokia ili kujadili usahihi wa Paulo. Kikao cha tatu kililaani mafundisho yake na kumvua madaraka. Hata hivyo, Paulo alifaidika na ulinzi wa Zenobia, malkia wa Palmyra, ambaye kwake yeye, Antokia ilikuwa ndio mada, na haikuwa ila mpaka mwaka 272 pale mfalme Aurelian alipomshinda Zenobia kwa kiwango ambacho madaraka halisi yakanyakuliwa.[103]
Mwishoni mwa karne ya tatu na mwanzoni mwa karne ya nne, Arius (b.c 250, Libya – 336 CE), kasisi wa Alexandria, Misri, pia amefundisha maumbile yenye mipaka ya Kristo upweke kabisa wa Mungu, jambo lililowavutia idadi kubwa ya wafuasi, mpaka alipotangazwa kuwa ni mzandiki na baraza la Nicaea mnamo Mei mwaka 325 CE. Wakati wa baraza hilo, alipinga kutia saini mfumo wa imani unaoeleza kuwa Kristo alikuwa na tabia ile ile kama Mungu. Hata hivyo, akiwa ameshawishiwa na wenzake wa Asia ndogo na kutoka Constantia, binti wa mfalme Constantine, alifanikiwa kushawishi kurejea kwa Arius kutoka uhamishoni na kurudi kanisani.[104] Vuguvugu alilodhaniwa kuwa amelianzisha, lakini kwa hakika lilikuwa ni kupanua imani ya Wakristo wa kiyahudi Wanazareti wa Jerusalem, Vuguvugu hilo lilijulikana kama Arianism na kuunda tisho kubwa ndani ya imani ya itikadi ya Wakristo wa Kipauline juu ya uungu wa Yesu.
Kutoka mwaka 337 hadi 350 CE, mfalme wa Magharibi, Constans, alionyesha huruma kwa Wakristo waoksodoksi, na Constantius wa pili, aliyekuwa mfalme wa Mashariki, aliwahurumia Waarians. Ushawaishi wa Arian ulikuwa mkubwa mno kiasi ambacho katika baraza la kanisa lililofanyika Antokia (341 CE), uthibitisho wa imani ulikuwa ndio jambo lililoondoa kifungu cha kuwa Yesu alikuwa na maumbile yale yale ya uungu kama Mungu”. Mwaka 350 CE Constantius wa pili akawa mtawala wa pekee wa himaya yote, na chini ya uongozi wake sehemu ya Nicene (Wakristo Waoksodoksi) waliangamizwa kwa kiasi kikubwa. Baada ya kifo cha Constantius wa pili mwaka 361 CE, Wakristo Waoksodoksi walio na wingi mkubwa huko Magharibi waliimarisha nafasi yao. Hata hivyo, utetezi wa kuwa na Mungu mpweke kabisa, na kukandamizwa kwa Wakristo Waoksodoksi, imani ya utatu iliendelea huko Mashariki chini ya mfalme Arian Valens (364-383 CE). Haikuwa ila mpaka pale Mfalme Theodosius wa kwanza (379-395 CE) alipotwaa ulinzi wa imani ya Arius, hata hivyo, imani hiyo iliendelea miongoni mwa makabila ya Kijerumani hadi mwishoni mwa karne ya saba.[105]

Mawazo ya kisasa

Leo hii, kuna wasomi wengi katika Ukristo wanaoshikilia kuwa Yesu Kristo hakuwa Mungu. Mwaka 1977, kikundi cha wasomi saba wa Biblia, akiwemo mwanatiolojia kiongozi wa Kianglikana na wasomi wengine wa Agano Jipya, walichapisha kitabu kiitwacho The Myth of God Icarnate, (Kisa cha kubuni cha Mungu mwenye mwili) kilichosababisha fujo kubwa kwa makutano makuu ya Kanisa la Uingereza. Katika utangulizi, mwandishi, John Hick, ameandika yafuatayo: “Waandishi wa kitabu hiki wamekinaishwa kuwa mwendelezo mkubwa wa kitiolojia uitishwe katika muda huu wa karne ya ishirini.
Dai linaibuka kutokana na kukuwa kwa maarifa ya asili ya Ukristo, na kuhusisha kutambua kuwa Yesu alikuwa ni (kama alivyowasilishwa katika matendo 2:21) ‘mtu aliyethibitishwa na Mungu’ kwa kazi maalum kwa lengo la kiungu, na kuwa dhana ya baadaye juu kumhusu yeye kama ni Mungu mwenye mwili, Nafsi ya Pili ya Utatu Mtakatifu inayoishi katika maisha ya kibinadamu, ni ngano ya kubuni au njia ya kishairi ya kuelezea umuhimu wake kwetu.”[106] Kuna makubaliano makubwa miongoni mwa wasomi wa Agano Jipya kuwa, kihistoria Yesu hajadai uungu ambao fikra ya Kikristo ilimfanyia; yeye hajajielewa kuwa yeye ni Mungu, wala Mungu Mwana, mwenye mwili [katika mwili].[107] Askofu mkuu wa hivi mwishoni Michael Ramsy, ambaye alikuwa ni msomi wa Agano Jipya, ameandika kuwa “Yesu hajadai uungu.”[108] Mwenzake wa zama moja, msomi wa Agano Jipya C.F.D. Moule. Amesema kuwa, “Kwa hali yeyote ile ya Elimu ya Ukristo ya hali ya juu inayotegemea usahihi wa madai ya Yesu mwenyewe, hasa hasa katika Injili ya Nne, kwa hakika atakuwa hatarini.”[109]
Katika utafiti mkubwa juu ya asili ya imani ya kuwa na mwili, James Dunn, anayethibitisha Elimu ya Ukristo wa Kioksodoksi, anahitimisha kuwa “hakuna ushahidi wa hakika katika mapokeo ya mwanzo ya Yesu kwa kile ambacho kwa uadilifu, kitaitwa ufahamu wa uungu.”[110] Tena, Brian Hebblethwaite, mtetezi kwa nguvu wa Elimu ya Ukristo ya mapokeo ya Nicene-Calcedonian, anakiri kuwa “haiwezekani tena kutetea uungu wa Yesu kwa kurejea katika madai ya Yesu.”[111] Hebblethwaite na Dunn, na wasomi wengine kama wao wanaoendelea kuamini uungu wa Yesu, wanadai kuwa licha ya kuwa Yesu hakujijua kuwa Yeye alikuwa Mungu mwenye mwili. Haya yalijulikana baada ya kufufuka kwake tu.
Wengine wengi miongoni mwa Maaskofu wakuu mashuhuri wa Kanisa la Uingereza, wanoshuku uungu wa Yesu, ni Kasisi asemaye wazi wazi Profesa David Jenkins, Askofu mkuu wa Durham Uingereza, ambaye anaeleza kwa uwazi kuwa Yesu hakuwa Mungu.[112]
Makala ifuatayo, ilitokoea katika The Daily News miaka iliyopita, kwa uwazi kabisa inaonyesha kiasi gani cha shaka miongoni mwa wakuu wa kidini kuhusu uungu wa Yesu.
Uchunguzi wa kushtusha wa Maaskofu wa Kianglikana

LONDON: Zaidi ya nusu ya Maaskofu Waingereza wa Kianglikana wanasema kuwa: “Wakristo hawalazimiki  kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mungu, kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa leo.
Kura za maoni za Maaskofu Waingereza 31, miongoni mwa Maaskofu 39, zinaonesha kuwa, wengi wao wanaona kuwa, Miujiza ya Kristo, kuzaliwa na bikira na kufufuka huenda hayo hayajatokea kama ilivyoelezwa katika Biblia. Ni Maaskofu 11 tu, ndio waliosisitiza kuwa "Wakristo lazima wamchukulie Yesu Kristo kuwa ni Mungu mtu, huku 19 wakisema kuwa inatosha kumchukulia Yesu kama ni "Mwakilishi mkuu wa Mungu". Na mmoja alijizuia kutoa maoni yake.
Hiyo kura ya maoni iliendeshwa na London Weekend Television's weekly religion show, Credo.
"DAILY NEWS" 25/6/84

 


Sura ya Tatu: Ujumbe

Suala la pili ni, ‘Ujumbe wa Yesu’, huenda ni nukta muhimu zaidi kuizingatia. Kwa kuwa, kama Yesu hakuwa Mungu mwenye mwili, ila ni nabii wa Mungu, ujumbe aliouleta kutoka kwa Mungu ni kiini cha kazi yake.

Utiifu

Msingi wa ujumbe wa Yesu ulikuwa ni utiifu wa kutii matakwa ya Mungu, kwa kuwa huo ndio msingi wa dini uliofanywa sheria na Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu tangu mwanzo. Mungu anasema katika Sura ya Al-Imraan, sura ya tatu ya Quran, aya 19:
"إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللّهِ الإِسْلاَمُ ..."
"Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu…"
Kwa kiarabu kutii matakwa ya Mungu kunaelezwa na neno ‘Uislamu’. Katika Injili kwa mujibu wa Mathayo 7:21, Yesu ananukuliwa akisema: “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye  mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Katika maelezo haya, Yesu anaweka mkazo juu ya “matakwa ya Baba”, utiifu wa matakwa ya mwanadamu kwa matakwa ya Mungu. Katika Yohana 5:30, imesimuliwa kuwa Yesu vilevile amesema: “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.”

Taurati (Torati)

“Matakwa ya Mungu” yamejumuishwa katika sheria za ufunuo mtakatifu ziliofundishwa na manabii kwa wafuasi wao. Kwa hiyo, utiifu kwa sheria ya Mungu ni msingi wa kuabudu. Quran inathibitisha haja ya utiifu kwa sheria ya ufunuo mtakatifu katika sura ya Al-Maaidah, aya 44.
"إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُواْ...، وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ"
"Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walionyenyekea Kiislamu…, Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri." Al-Maaidah, aya 44.
Pia, Yesu ameripoti katika Injili kwa mujibu wa Mathayo 19:16-17, kuwa alifanya utiifu kwa sheria ya ufunuo mtakatifu ambayo ndio ufunguo wa Peponi: “Na tazama, mtu mmoja akamwendea akawaambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?Akamwambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.”.[113] Pia katika Mathayo 5:19, Yesu Kristo ameripotiwa kuwa amesisitiza utiifu mkali wa kuzitii amri kwa kusema, “Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbingubi.”
Sheria ya Mungu inawakilisha mwongozo kwa wanadamu katika pande zote za maisha. Inafafanua zuri na baya kwa wanadamu na kuwapa wanadamu mfumo kamili unaosimamia mambo yao yote. Muumba pekee ndiye ajuaye vizuri kipi kina manufaa kwa viumbe wake na kipi hakina. Kwa hiyo, sheria ya Mungu inaamuru na kukataza matendo na vitu mbali mbali ili kuikinga roho ya mwanadamu, mwili wa mwanadamu, na jamii ya wanadamu isidhurike. Ili wanadamu watimize uwezo wa kuishi kwa wema, wanahitaji kumwabudu Mungu kwa kutii amri Zake.[114]
Hii ndio iliyokuwa dini iliyoletwa katika ujumbe wa Yesu; kutii matakwa ya Mungu mmoja wa kweli kwa kutii amri zake. Yesu aliwasisitizia wafuasi zake kuwa kazi yake haikuwa kutangua Sheria (Taurati) iliyopokelewa na Nabii Musa. Akiwa kama Mitume iliyokuja baada ya Musa iliyoimarisha sheria, Yesu alifanya hivyo hivyo. Sura ya al-Maaidah, aya ya 46 ya Quran inaashiria kuwa Yesu ameimarisha Sheria ya Taurati katika ujumbe wake.
"وَقَفَّيْنَا عَلَى آثَارِهِم بِعَيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَآتَيْنَاهُ الإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ..."
"Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati…" Al-Maaidah, aya 44.
Katika Mathayo 5:17-18, Yesu ameeleza: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Hata hivyo, Paulo, aliyedai kuwa ni mwanafunzi wa Yesu, kimsingi ametangua sheria. Katika waraka wake kwa Warumi, sura 7:6, ameeleza, Bali sasa tumefunguliwa katika Torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani ya andiko.”

Upwekesahaji

Yesu amekuja akiwa ni Nabii, akiwaita watu wamwabudu Mungu peke yake. Kama walivyofanya manabii wa kabla yake. Mungu anasema katika sura An-Nahli 16:36 ya Quran:
"وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولاً أَنِ اعْبُدُواْ اللّهَ وَاجْتَنِبُواْ الطَّاغُوتَ..."
"Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani…" An-Nahli 16:36[115]
Katika Luka 4:8, Shetani anamtaka Yesu amwabudu yeye, kwa kumuahidi mamlaka na utukufu wa ufalme wa dunia nzima, “Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” Kwa hiyo kiini cha ujumbe wa Yesu kilikuwa ni kuwa Mungu pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa na kuwa kumwabudu yeyote au chochote kandoni au pamoja na Mungu ni kosa. Yesu sio tu, amewaita watu katika ujumbe wake lakini pia uliutekeleza na kuuonesha kwao kwa kusujudu katika sala na kumwabudu Mungu mwenyewe. Katika Marko 14:32, inaeleza: “Kisha wakaja mpaka bustani iitwayo Gethsemane; akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa muda niombapo.” Na katika Luka 5:16, “Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.”
Yesu aliwaita wamwabudu Mungu mmoja wa kweli ambaye ni wa kipekee katika sifa zake. Mungu hana sifa za viumbe zake, na hakuna kiumbe yeyote anayeshirikiana naye kwa sifa yoyote ile. Katika Mathayo 19:16-17, pale mtu mmoja alipomwita Nabii Yesu ‘mwema’, akisema “Na tazama, mtu mmoja akamwendea akawaambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akawaambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja…" Yesu alikana sifa ya ‘uungu wenye mipaka’ au ‘wema kamilifu’ kwa nafsi yake, na kuthibitisha kuwa sifa hii inamilikiwa na Allah peke yake.
Idadi kubwa mno ya Wakristo duniani leo hii wanamwabudu Yesu, wakidai kuwa yeye ni Mungu. Wanafalsafa miongoni mwao wanadai kuwa wao hawamwabudu Yesu mtu, ila Mungu aliyejidhihirisha kwa Yesu mtu. Hii vilevile ndio akili ya wapagani wanaosujudia masanamu. Mwanafalsafa wa kipagani alipoulizwa kwa nini anaabudu sanamu lililotengenezwa na mikono ya mwanadamu, alijibu kuwa kwa hakika yeye haabudu sanamu. Zaidi, anaweza kudai kuwa sanamu ni nukta ya kuunganisha kwa kuwepo kwa Mungu, na kwa hiyo ni kudai kuwa anamwabudu Mungu anayejidhihirisha kwa sanamu, na wala sio umbo la sanamu lenyewe. Kuna tofauti ndogo au hakuna tofauti kati ya ufafanuzi na jibu lililotolewa na Wakristo kwa kumwabudu Yesu. Asili ya kupotoka huku ipo katika imani ya uongo ya kuwa Mungu yupo katika Viumbe vyake. Imani kama hiyo inahalalisha kuabudu viumbe wa Mungu.
Ujumbe wa Yesu, unaowataka wanadamu wamwabudu Mungu mmoja peke yake, uliharibiwa baada ya kuondoka kwake. Baadaye, wafuasi wakianzia na Paulo, waliubadilisha ujumbe mtakatifu na mwepesi na kuwa falsafa ya utatu yenye utata inayohalalisha kumwabudu Yesu, kisha kumwabudu Mama yake Yesu, Mariamu,[116] na kuabudu malaika[117] na watakatifu wengine. Wakatoliki wana orodha ndefu ya wale wanaowaendea wakati wa shida. Kama kitu kimepotea, Mtakatifu Anthony wa Thebes anaombwa ili asaidie kipatikane.[118] Mtakatifu Jude Thaddaeus ni mlinzi mtakatifu wa yasiyowezekana na anaabudiwa kwa maombezi ya magonjwa yasioponyeka, kinyume na ndoa au kitu kama hicho.[119] Mlinzi mtakatifu wa wasafiri alikuwa ni Mtakatifu Christopher, ambaye aliabudiwa na wasafiri ili awape ulinzi hadi mwaka 1969, pale alipofutwa rasmi na kuwa nje ya orodha ya watakatifu kwa mujibu wa amri ya kipapa, baada ya kuthibitishwa kwamba alikuwa ni[120] wa uongo. Ingawa alifutwa rasmi na kuwa nje ya orodha ya watakatifu, kuna Wakatoliki wengi duniani leo hii wanaomwabudu Mtakatifu Christopher.
Kuwaabudu ‘watakatifu’ kunapingana na kufisidi kumwabudu Mungu Mmoja; na ni kazi bure, kwa sababu si aliye hai wala mfu awezaye kujibu maombi ya wanadamu. Kumwabudu Mungu hakutakiwi kuwe na kumshirikisha na viumbe vyake kwa njia, umbo au mfumo wowote ule, kwa mazingatio haya, Allah amesema yafuatayo katika Sura Al-Aaraaf 7:194:
"إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللّهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ..."
"Hakika hao mnaowaomba kinyume na Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi..." Al-Aaraaf 7:194
Huu ndio uliokuwa ujumbe wa Yesu Kristo na mitume yote wa kabla yake. Vilevile ulikuwa ndio ujumbe wa mtume wa mwisho, Muhammad - Rehema na amani ziwe juu yao wote. Kwa hiyo, kama Mwislamu au mtu anayejiita Mwislamu atamwabudu mtakatifu, atakuwa ashatoka nje ya mipaka ya Uislamu. Uislamu si imani tu, ambapo mtu anatakiwa aeleze kuwa yeye anaamini kuwa hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Allah, na Muhammad alikuwa ni mtume wa mwisho, ili kuingia peponi. Hili tangazo la imani linamruhusu mtu anayelitangaza kuingia mlango wa Uislamu, lakini kuna matendo yanayoweza kupingana na tangazo hilo na kumwondosha mtendaji kutoka katika Uislamu punde tu anapolitenda. Tendo hatari mno miongoni mwa hayo ni kuabudu kitu kingine zaidi ya Mungu.

Mwislamu sio “Mmuhammadi”

Kwa kuwa dini ya Yesu, na hivyo hivyo kwa mitume yote ya mwanzo, ilikuwa ni dini ya kumtii Mungu,  ijulikanayo kwa Kiarabu kama Uislamu, wafuasi wake wa kweli wanapaswa waitwe watiifu wa Mungu, wakijulikana kwa Kiarabu kama Waislamu. Katika Uislamu, sala-dua inazingatiwa kuwa ni tendo la kuabudu. Mtume Muhammad (SAW) ameripotiwa akisema, “Dua ni ibada”.[121]  Kwa hiyo, Waislamu hawakubali kuitwa Wamuhammadi, kama ilivyo kwa wafuasi wa Kristo wanavyoitwa Wakristo na wafuasi wa Budha wanaitwa Mabudha. Wakristo wanamwabudu Kristo na Mabudha wanamwabudu Budha. Neno Wamuhammadi linaashiria kuwa Waislamu wanamwabudu Muhammadi, kitu sicho kabisa. Katika Quran, Mungu amelichagua jina Mwislamu kwa kila anayemfuta mtume kikweli kweli. Jina Mwislamu kwa Kiarabu linamaanisha “anayetii matakwa ya Mungu.”
"... هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَذَا..."  
"Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia." Al-Hajj 22:78.
Kwa hiyo, kiini cha ujumbe wa Yesu kilikuwa hivi, mtu anatakiwa amwabudu Mungu peke yake. Hapaswi kuabudiwa kwa kupitia viumbe wake kwa njia yoyote ile.
Hivyo, picha yake isichapishwe, isichongwe wala kuchorwa. Yeye yupo nje ya ufahamu wa binadamu.

Masanamu

Yesu hakufumbia macho matendo ya wapagani ya kujiundia masanamu ya Mungu. Yeye alisisitiza katazo lililotajwa katika Torati, Kutoka 20 mstari wa 4: “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia." Hivyo, matumizi ya masanamu ya kidini, alama za kuombwa,[122] yalipingwa vikali na kizazi cha kwanza cha wasomi Wakristo. Hata hivyo, katika kipindi cha, tamaduni za Kigiriki na Kirumi za kuunda sanamu na picha za Mungu kwa mfumo wa mwanadamu, hatimaye ulishinda. Katazo ni la kuzuia hatima ya kuzorota kumwabudu Mungu na kuwaabudu viumbe vyake. Mwanadamu akiweka picha ya Mungu akilini mwake, huyo mtu, kwa hakika, anajaribu kumfanya Mungu awe kama viumbe wake, kwa sababu akili ya mwanadamu inaweza kuvuta taswira vitu ilivyoviona, na Mungu haonekani katika maisha haya.
Wakristo wakiwa na utamaduni wa kuabudu kwa kupitia masanamu mara nyingi wanauliza vipi Mungu aweze kuabudiwa bila ya kumuona. Mungu anapaswa kuabudiwa kwa kuegemea elimu ya kujua sifa zake alizozifunua katika vitabu sahihi. Kwa mfano, Allah anajieleza yeye mwenyewe katika Quran kuwa yeye ni Mwenye rehema, kwa hiyo, Wanaomwabudu wanatakiwa waonyeshe rehema nyingi za Mungu na kumshukuru Mungu kwa rehema hizo. Pia wanapaswa kutafakari juu ya tabia ya rehema zake kwao na kuonyesha rehema kwa watu wengine. Hivyo hivyo, Mungu anajitambulisha kuwa yeye ni Msamehevu, kwa hiyo wanaomwabudu wanatakiwa wamgeukie na kutubu na wasikate tamaa wanapofanya madhambi. Pia wanatakiwa waheshimu msamaha wa Mungu kwa kuwa wasamehevu kwa watu wengine.

Utabiri

Sehemu mojawapo ya ujumbe wa Nabii Yesu ilikuwa ni kuwafahamisha wafuasi wake juu ya nabii atakayekuja baada yake. Kama vile Yohana Mbatizaji alipobashiri ujio wa Yesu Kristo, naye Yesu alitabiri kuja kwa nabii wa mwisho wa Mungu, Muhammad. Katika Quran, Sura ya As-Swaff 61:6, Mungu ananukuu utabiri wa Yesu juu ya Muhammad (SAW).
"وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ..."
"Na Isa bin Mariamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad…" As-Swaff 61:6[123]
Pia kuna baadhi ya marejeo katika Injili yanayoonekana kuwa yanaonyesha kuja kwa Mtume Muhammad – Rehema na amani ziwe kwa mitume wote. Katika Injili, kwa mujibu wa Yohana 14:16, Yesu ananukuliwa akisema, “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.”.[124]
Walei wa Kikristo kikawaida wanamfasiri "Msaidizi" aliyetajwa katika Yohana 14:16 kuwa ni Roho Mtakatifu.[125] Hata hivyo, ibara "Msaidizi mwingine" inadokeza kuwa huyo atakuwa ni mtu mwingine aliye kama Yesu na sio Roho Mtakatifu, [126] hasa hasa ukizingatia Yohana 16:7, pale Yesu anaporipotiwa kuwa amesema, “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.” Neno "Msaidizi" haliwezi kumwonyesha Roho Mtakatifu kwa hapa, kwa sababu – kwa mujibu wa Injili - Roho Mtakatifu tayari ameshakuwepo duniani kabla ya Kuzaliwa Yesu,[127] pia wakati wa unabii wake.[128] Mstari huu unaashiria kuwa "Msaidizi" bado hajaja.
Tangazo la Yesu ni kuwa mtume "Msaidizi" atakuwa nanyi milele" lingepaswa kutafsiriwa na kumaanisha kuwa kutakuwa hakuna haja ya mitume ya ziada ili kumfanya afanikiwe huyo Msaidizi. Naye atakuwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, na ujumbe wake utalindwa mpaka mwisho wa Dunia.[129]
Utabiri wa Yesu kwa ujio wa Muhammad – Mungu awarehemu wote wawili – unauthibitisha utabiri wa Muhammad (SAW) katika Torati. Katika Kumbukumbu la Torati 18:18 na 19, imeandikwa kuwa Bwana alimwambia Musa, “Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao[130] mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake,[131] naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu,[132] nitalitaka kwake.” Katika Isaya 42:1, Isaya anatabiri juu ya mteule "Mtumishi wa Bwana" ambaye kazi yake ya utume itakuwa kwa watu wote, kinyume na manabii wa Kiisraeli ambao kazi zao zilifungika kwa waisraeli tu. “Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu… Hatazimia, wala hatakata tama, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake… Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari… Huyu mtumishi wa kipekee wa Bwana ni yule aliyetambulishwa kuwa ni Kedar,[133] yaani Warabu.

Sura ya Nne: Njia

Kipengele kingine cha ujumbe wa Nabii Yesu kilikuwa ni mwaliko wake wa kuwaalika watu wafuate njia yake. Mitume ilileta sheria au kuendeleza zile zilizoletwa na mitume iliyopita, na kuwaalika watu wamwabudu Mungu kwa kutii sheria takatifu zilizofunuliwa. Wao, pia wanafafanua kimatendo kwa wafuasi wao vipi mtu ataishi kisheria. Hivyo, hao mitume, vilevile wanawaalika wale wote wanaowamini wao wafuate njia zao zikiwa ndio njia sahihi za kumkaribia Mungu. Msingi huu umewekwa katika Injili kwa mujibu wa Yohana 14:6: “Yesu akawaambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Ingawa wale wanaomwabudu Yesu kwa kawaida wananukuu mstari huu ukiwa ni sehemu ya ushahidi ya uungu wake, lakini Yesu hajawaita watu wamwabudu yeye badala ya Mungu, au kama Mungu. Kama maneno haya kwa ukweli kabisa yametamkwa na Yesu, yanamaanisha kuwa mtu haruhusiwi kumwabudu Mungu ispokuwa kwa kutumia njia iliyofafanuliwa na manabii wa Mungu. Yesu ametia mkazo kwa wanafunzi wake kuwa wanatakiwa wamwabudu Mungu kwa njia ile aliyowafundisha. Katika Quran, Sura Al-Imran 3:31, Mungu anamwelekeza Mtume Muhammad (SAW) awafundishe wanadamu wamfuate kama kweli wanampenda Mungu:
"قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ"
"Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu." Al-Imran 3:31
Njia ya manabii ni njia ya pekee kuelekea kwa Mungu, kwa sababu Mungu Mwenyewe ameifanya iwe sheria, na lengo la mitume lilikuwa ni kufikisha mafundisho ya Allah kwa wanadamu. Bila ya manabii, watu wasingejua namna ya kumwabudu Allah. Hivyo, mitume yote iliwafahamisha wafuasi zao namna ya kumwabudu Mungu. Kinyume chake, kuongeza chochote katika dini iliyoletwa na mitume ni makosa.
Badiliko lolote litakalofanywa katika dini baada ya kipindi cha mitume litamaanisha kupotoka kulikofunuliwa na Shetani. Kwa mazingatio haya, Mtume Muhammad (SAW) ameripotiwa akisema: "Atakayezusha kitu katika dini yetu, kitu ambacho sio katika dini yetu, basi kitu hicho kinarudishwa." Imepokewa na Bukharin na Muslim."[134] Zaidi, mtu yeyote anayemwabudu Allah kinyume na mafundisho ya Yesu, atakuwa anaabudu bure.

Njia ya Yesu

Kwanza na kabla ya yote, lazima itambulike kuwa Yesu Kristo, mwana wa Mariamu, alikuwa ni wa mwisho katika orodha ya manabii wa Kiisraeli. Aliishi kwa mujibu wa Torati, na sheria ya Musa, na aliwafundisha wafuasi zake wafanye hivyo hivyo. Katika Mathayo 5:17-18, Yesu ameeleza: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kuitimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Kwa bahati mbaya, kiasi cha miaka mitano baada ya kuisha kwa uchungaji wa Yesu, Rabbi kijana kwa jina la Sauli wa Tarsus, aliyedai kuwa amemuona Yesu katika maono, alianza kubadilisha njia ya Yesu. Paulo (jina lake kwa Kirumi) alikuwa na heshima kubwa kwa falsafa ya Kirumi na alizungumza kwa ufahari kwa kuwa na uraia wa Roman. Imani yake ilikuwa ni kuwa wasio-Wayahudi walioingia Ukristo wasibebeshwe mzigo wa Torati kwa hali yoyote ile. Mtunzi wa Matendo 13:39 anamnukuu Paulo akisema, “Na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.” Kimsingi ilikuwa ni kwa kupitia juhudi za Paulo ndipo kanisa lilipoanza kufuata mkondo wa tabia za wasio-Wayahudi. Paulo[135] ameandika barua (nyaraka), nyingi za Agano Jipya zinazokubaliwa na kanisa zikiwa ni kama mafundisho rasmi ya kiitikadi na Kitabu kilichofunuliwa. Nyaraka hizo hazikuilinda Injili ya Yesu wala hata kuiwakilisha;[136] badala yake amegeuza mafundisho ya Kristo kuwa ya falsafa ya Kihelleniki (Graeco-Roman).
Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya mafundisho aliyoyafuata nabii Yesu na kuyafundisha, lakini baadaye yaliachwa na Kanisa. Hata hivyo, mengi miongoni mwa mafundisho hayo yalifufuliwa katika ujumbe wa mwisho wa Uislamu ulioletwa na Mtume Muhammad (SAW) na yakaendea kubakia kuwa ni sehemu ya msingi katika matendo ya dini ya Kiislamu hadi leo hii.

Kutahiri

Yesu alitahiriwa. Kwa mujibu wa Agano la Kale, mapokeo haya yalianzia na Mtume Ibrahimu, ambaye yeye mwenyewe hakuwa Myahudi wala Mkristo. Katika Mwanzo 17:10-13, imeandikwa, “Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na nyinyi. Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako. Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa na fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.
Katika Injili kwa mujibu wa Luka 2:21: “Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.” Kwa hiyo, kutahiriwa ilikuwa ni sehemu ya njia ya Yesu. Hata hivyo, leo hii Wakristo wengi hawajatahiriwa, kwa sababu ya mantiki iliyoletwa na Paulo. Yeye alidai kuwa kutahiriwa kulikuwa ni kutahiriwa kwa moyo. Katika waraka wake kwa Warumi 2:29, ameandika: Bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani; na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko;..." Na katika waraka wake kwa Wagalatia 5:2, ameandika “Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.”[137] Hii ni tafsiri isiyo ya kweli ya Paulo. Kwa upande mwingine, Yesu hakutahiriwa moyoni wala hajasema lolote juu ya kutahiriwa moyoni; yeye aliliendeleza "agano la milele" na alitahiriwa katika nyama. Kwa hiyo, sehemu muhimu ya kufuata njia ya Yesu ni kutahiriwa. Mtume Muhammad (SAW) amenukuliwa akisema: "Mambo matano ni katika maumbile,[138]  kutahiri, kunyoa nywele za sehemu za siri, kunyoa nywele za kwapani, kukata kucha, na kupunguza masharubu." Imepokewa na Bukharin na Muslim." [139]

Nguruwe

Yesu hajakula nguruwe. Alifuata sheria za Musa na hakula nguruwe. Katika Walawi 11:7-8, “Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi, kwenu, msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.”[140]
Yesu alishughulika na nguruwe pale tu, alipowaruhusu pepo wabaya waliomwingia mtu wawaingie nguruwe. Na walipoliingia kundi la nguruwe, hao nguruwe walikimbilia kwenye maji na kuzama. Hata hivyo, watu wengi wanaojiita Wakristo leo hii sio tu wanakula nguruwe, lakini pia wanampenda sana kiasi cha kumfanya nguruwe kuwa mada ya wimbo wa chekechea [mfano wimbo: Huyu Nguruwe Mdogo alienda sokoni…] na hadithi za watoto [mfano: Nguruwe Wadogo Watatu]. Nguruwe na Nyama ya nguruwe ni wahusika mashuhuri wa katuni, na hivi karibuni hadithi ya sinema ndefu imetayarishwa kuhusu nguruwe aitwaye "Babe". Kwa hiyo, inawezekana kusema kuwa wale wanaojiita ni wafuasi wa Kristo kwa hakika hawafuati njia ya Kristo.
Katika sheria ya Kiislamu, kuharamishwa kwa nguruwe na mazao yake kumetekelezwa kwa nguvu tangu wakati wa Mtume Muhammad (SAW) hadi leo hii. Katika Quran, Sura ya Al-Baqarah 2:173, Mungu anasema:
"إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللّهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلاَ عَادٍ فَلا إِثْمَ عَلَيْهِ إِنَّ اللّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ"
"Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliyefikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Al-Baqarah 2:173 [141]

Damu

Pia, Yesu hakula kitu chochote cha damu, wala hajakula damu. Mungu amenukuliwa akimfundisha Mtume Musa katika Torati, Kumbukumbu la Torati 12:16, “Lakini msiile damu; imwageni juu ya nchi kama maji.”. Na katika Lawi 19:26, “Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.” Katazo hili limelindwa hadi leo hii katika ufunuo wa mwisho katika Sura Al-Anaam 6:145
"قُل لاَّ أَجِدُ فِي مَا أُوْحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلاَّ أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ..."
"Sema: Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharimishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu;…" Al-Anaam 6:145
Hivyo, ibada maalum ya kuchinja ilifanywa iwe sheria na Mungu kwa mataifa yote yaliyopelekewa mitume, ili kuhakikisha kuwa damu nyingi inaondoshwa kwa ufanisi kutoka kwa mnyama aliyechinjwa na kumkumbusha mwanadamu fadhila za Mungu. Quran inataja mafundisho haya katika sura ya Al-Hajji 22:34 kama ifuatavyo:
"وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَى مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ..."
"Na kila umma tumewafanyia mahala pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyoruzukiwa katika wanyama wa mifugo…" Al-Hajji 22:34
Yesu na wafuasi wake wa kwanza waliuona mfumo mkamilifu wa kuchinja kwa kutaja jina la Mungu na kukata mishipa ya shingo ya mnyama akiwa hai ili kuuruhusu moyo usukume nje damu. Hata hivyo, Wakristo wa leo hii hawaambatanishi sana umuhimu wa mfumo wa kuchinja kikamilifu, kama ulivyofanywa sheria na Mungu.

Kilevi (pombe)

Yesu aliitoa nafsi yake kwa ajili ya Mungu na kwa hiyo alijizui na vinjwaji vya kulevya kwa mujibu wa mafundisho yaliyorekodiwa katika Hesabu 6:1-4 “Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu mume au mke atakapoweka nadhiri kubwa, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa BWANA; atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yoyote ya zabibu, wala asile zabibu mbichi wala zilizokauka. Siku zote za kujitenga kwake asile kitu cho chote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda." ”.[142]
Katika Quran, Sura Al-Maaidah 5:90, Allah anaharamisha kileo bila kubadilika.
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالأَنصَابُ وَالأَزْلاَمُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ"
"Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa." Al-Maaidah 5:90
Na ule muujiza wa 'kugeuza maji yawe pombe',[143] unaopatika katika Injili ya Yohana tu, na ambao mtiririko wake unapingana na Injili nyingine. Kama ilivyotajwa mwanzoni, Injili ya Yohana ilipingwa ikiwa kama uasi katika kanisa la kwanza,[144] huku Injili tatu zilizobakia zimetajwa kama ni muhtasari wa Injili kwa sababu maandiko yaliyomo ni sawa na matendo ya maisha ya Yesu.[145] Hivyo, wasomi wa Agano Jipya wameonyesha shaka juu ya uhalisia wa utunzi wa tukio hili.

Udhu kabla ya Kusali

Kabla ya kusali kikawaida, Yesu aliosha viungo vyake kwa mujibu wa mafundisho ya Torati. Musa na Haruna wamenukuliwa wakifanya hayo hayo katika Kutoka 40:30-31, “Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea. Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yak.”
Katika Quran, Sura Al-Maaidah, 5:6, udhu kwa ajili ya sala umefanywa kuwa ni sheria na lazima kama ifuatavyo:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلاةِ فاغْسِلُواْ وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُواْ بِرُؤُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَينِ..."
"Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni…" Al-Maaidah, 5:6

Kusujudi katika Sala

Yesu ameelezwa katika Injili kuwa amesujudi alipokuwa akisali. Katika Mathayo 26:39, mtunzi anaeleza tukio lililotokea pale Yesu alipoenda na wanafunzi wake hadi Gethsemane: “Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akasema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utavyo wewe.”
Wakristo wa leo hii wanapiga magoti, wanakutanisha viganja vyao, katika mkao ambao hauwezi kuwa ndio sheria ya Yesu. Mfumo wa kusujudu katika sala uliofuatwa na Yesu haukuwa wa kujifanyia mwenyewe. Ulikuwa ndio mtindo wa sala wa manabii wa kabla yake. Katika Agano la Kale, Mwanzo 17:3, Nabii Ibrahimu anarekodiwa kuwa alianguka juu ya uso wake katika sala; katika Hesabu 16:22 na 20:6, wote wawili Musa na haruna wamerekodiwa kuwa wameanguka juu ya nyuso zao katika kuabudu; katika Yoshua 5:14 na 7:6, Yoshua alianguka juu ya uso wake ardhini na aliabudu; katika 1 Wafalme 18:42, Eliya alisujudu ardhini na kuweka uso wake kati ya magoti yake. Hii ilikuwa njia ya mitume ambayo kupitia kwao Mungu amechagua kufikisha neno Lake duniani; na kwa njia hii tu, wale wote wanaodai kumfuata Yesu watapata uwokovu aliouhubiri katika Injili.
Sura ya Al-Insaan 76:25-6, ni mfano mmoja tu katika mifano mingi ya Quran juu ya mafundisho ya Mungu kwa waumini wasujudu wanapomuabudu.
"وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا، وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا"
"Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni; Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu." Al-Insaan 76:25-6

Hijabu

Wanawake waliomzunguka Yesu walivaa hijabu kulingana na matendo ya wanawake waliokuwa karibu na mitume ya mwanzo. Nguo zao zilikuwa ni pana na za kufunika mwili wao wote, na walivaa ushungi unaofunika nywele zao. Katika Mwanzo 24:64-5: “Rebeka akainua macho, naye alipomwona Isaka, alishuku juu ya ngamia. Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwa shela yake akajifumika.” Paulo ameandika katika waraka wake kwa 1 Wakorinto 11:5-6, Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.” Kuna wanaoweza kupinga na kudai kuwa hilo lilikuwa ni mila ya wakati huo kujifunika mwili mzima. Hata hivyo, hiyo sio hoja. Katika sehemu zote Roma na Ugiriki, ambao utamaduni wao ndio ulikuwa ukiongoza eneo hilo, vazi la wengi lilikuwa ni fupi hasa na kuonyesha mikono, miguu, na kifua. Ni wanawake wa Kipalestna wanaofuata dini tu, wakifuata mapokeo ya Kiyahudi, ndio waliojifunika kwa kujistiri.
Kwa mujibu wa Rabbi Dr. Menachem M. Brayer (Profesa wa Biblical Literature wa Chuo Kikuu cha Yeshiva), Ilikuwa ni mila kuwa wanawake wa Kiyahudi kutoka nje kwenye watu wengi wakiwa wamefunika vichwa, na wakati mwingine wanafunika uso mzima, na kuacha jicho moja tu.[146] Ameendelea kueleza zaidi kuwa "katika kipindi cha Tannaitic, mwanamke wa Kiyahudi atakayeshindwa kufunika kichwa chake alichukuliwa kuwa anafedhehesha utu wake. Na kichwa chake kinapokuwa kimefunuka anapaswa apigwe faini ya zumzim mia kwa kosa hilo.[147]
Mwanatiolojia mashuhuri wa Kikristo wa mwanzo, Mtakatifu Tertullian (d. 220 CE), katika pendekezo lake maarufu, 'Juu ya Hijabu ya Mabikira'  ameandika, "Wasichana, vaeni hijabu zenu nje huko mitaani, pia mzivae kanisani; mzivae mnapokuwa na wageni, kisha zivaeni mkiwa na kaka zenu…" Miongoni mwa sheria za kanisa la Katoliki hadi leo hii, kuna sheria inayowataka wanawake wafunike vichwa vyao wakiwa kanisani.[148] Madhehebu ya Kikristo, kama vile Waamish na Wamenonites, wanawake wao waneendelea kuvaa hijabu hadi leo.
Katika Quran, Sura An-Nuur 24:31, waumini wanawake wanaagizwa wafunike mapambo yao na wavae hijabu kichwani na vifuani mwao.
"وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ..."
"Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, …" An-Nuur 24:31
Katika Sura ya Al-Ahzaabu 33:59, lengo la kuvaa hijabu limetolewa. Allah anaeleza kuwa hijabu inawafanya waumini wanawake wajulikane katika jamii na kupata kinga dhidi ya uwezekano wa kudhuriwa na jamii.

Salamu

Yesu aliwasalimia wafuasi zake kwa kusema, "Amani iwe kwenu". Katika Sura 20:19, mtunzi asiyejulikana wa Injili ya Yohana ameandika yafuatayo kuhusu Yesu baada ya dai la kusulubiwa: “Akaja Yesu, akasimama katikati akawaambia, Amani iwe kwenu.” Salamu hii ilikuwa ni kama zile za manabii, kama ilivyotajwa katika vitabu vya Agano la Kale. Kwa mfano, katika 1 Samweli 25:6, Nabii Daudi amewaaagiza wajumbe aliowapeleka kwa Nabal: “Na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishiye salama, Amani iwe kwenu”. Quran inawaagiza wale wote wanaoingia katika majumba watoe salamu ya amani;[149] na wale watakaoingia Peponi watasalimiwa hivyo hivyo na malaika.[150] Katika Sura Al-Anaam 6:54, Mungu anawaagiza waumini wasalimiane wao kwa wao kwa amani:
"وَإِذَا جَاءكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلاَمٌ عَلَيْكُمْ..."
"Na wanapokujia wanaoziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! Amani iwe juu yenu!..." Al-Anaam 6:54

Zaka

Yesu aliimarisha taasisi ya zaka za lazima, ijulikanayo kama "moja ya kumi", iliyokuwa inachukuliwa kutoka katika mavuno ya kila mwaka na kurejeshwa kwa Mungu kwa sherehe. Katika Kumbukumbu la Torati 14:22: “Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.”
Katika Sura ya sita, Al-Anaam, aya ya 141, Mungu anawakumbusha waumini walipe zaka wakati wa mavuno:
"وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُواْ حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ وَلاَ تُسْرِفُواْ إِنَّهُ لاَ يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ"
"Na Yeye ndiye aliyeziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisizotambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbalimbali, na mizaituni na mikomamanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni matunda yake inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo." Al-Anaam 6:141[151]
Mfumo wa zaka (kwa Kiarabu, zakaah) umepangwa vizuri, kwa viwango tofauti tofauti kwa pesa na vito vya thamani na vile vya mazao ya kilimo na mifugo. Pia, wote wanaofaa kuipokea wametambulishwa kwa uwazi katika Quran, Sura ya At-Tawbah 9:60. kimsingi inagawanywa miongoni mwa makundi mbalimbali ya maskini na haitumiki katika kuwapa maisha ya anasa viongozi wa kidini.

Kfunga

Kwa mujibu wa Injili, Yesu alifunga kwa siku arobaini. Mathayo 4:2 “Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.”.[152] Hili lilikuwa linalingana na matendo ya manabii wa mwanzo. Pia Musa amerekodiwa katika Kutoka 34:28, kuwa alifunga: “Naye alikuwa huko pamoja na BWANA siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.”
Katika Quran, Sura Al-Baqarah 2:183, waumini wameagizwa watekeleze funga.
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ"
"Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyoandikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu." Al-Baqarah 2:183
Lengo la kufunga limefafanuliwa kwa uwazi nalo ni kendeleza uchamungu. Ni Mungu pekee ajuaye ni nani afungaye kweli na nani hafungi. Hivyo, mfungaji anajizuia na kula, kunywa kwa kutegemea Mungu yu macho. Funga inanyanyua mwamko unaopelekea kupenda sana mema.
Waumini wanapaswa wafunge kuanzia alfajiri hadi kuzama kwa jua katika mwezi mzima wa Ramadhani (mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislmamu ya miezi miandamo). Mtume Muhammad (SAW) pia amesema, "Hakika ya  funga bora ni funga ya Daudi, alikuwa akifunga siku moja na kufungulia inayofuata." [153]

Riba

Kwa kukamata sheria, Nabii Yesu pia alipinga kutoa au kupokea riba kwa sababu maandiko ya Torati yanakataza vikali riba. Imenukuliwa katika kumbukumbu la torati 23:19 kuwa, “Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula,[154] riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba;"[155] Pia riba imekatazwa vikali katika sura Al-Baqarah 2:278 ya Quran:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اتَّقُواْ اللّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ"
"Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini." Al-Baqarah 2:278
Ili kukamilisha takwa hili la Mwenyezi Mungu, Waislamu wamendeleza mfumo mbadala wa Benki, kwa kawaida unajulikana kama 'Benki ya Kiislamu', isiyo na riba.

Mitala (wake wengi)

Hakuna rekodi zinazoonyesha kuwa Nabii Yesu anapinga mitala. Na kama alifanya hivyo, ingeonyesha kuwa analaani matendo ya manabii waliotangulia kabla yake. Kuna mifano mingi ya ndoa za mitala miongoni mwa manabii iliyorekodiwa katika Torati. Nabii Ibrahimu alikuwa na wake wawili, kwa mujibu wa Mwanzo 16:3: “Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.” Pia Nabii Daudi, kwa mujibu wa kitabu cha kwanza cha Samweli 27:3, “Daudi akakaa huko Gathi pamoja na Akishi, yeye na watu wake, kila mtu na watu wa nyumbani mwake; Daudi naye alikuwa na wakeze wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, aliyekuwa mkewe Nabali.” Katika 1 Wafalme 11:3, Suleimani inasemwa kuwa alikuwa na  “…wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.” Mototo wa Suleimani, Rehobo'am, pia alikuwa na idadi kubwa ya wake, kwa mujibu wa 2 Nyakati 11:21, “Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu kuliko wakeze wote na masuria yake; (maana alioa wake kumi na wanane, na masuria sitini, akazaa wana ishirini na wanane na binti sitini).” Kwa hakika, Torati inafafanua sheria ya kugawa mirathi katika hali za mitala. Katika Kumbukumbu la Torati 21:15-16, sheria inasema: “Ikiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa; ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu;” Kikwazo pekee cha mitala kilikuwa ni kukataza kuoa dada ya mkeo awe mke mwenza katika walawi 18:18, “Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai.” Kitabu cha Talmudi kinashauri kuoa mwisho wake wanne kama ilivyokuwa ikitendwa na Nabii Yakobo.[156]
Kwa mujibu wa Padri Eugene Hillman, "Katika Agano Jipya hakuna sehemu yoyote yenye amri iliyowazi ya kuwa ndoa iwe ya mke mmoja au amri yoyote iliyowazi inayokataza mitala."[157] Akaendelea kutilia mkazo ukweli kuwa, kanisa huko Roma lilikataza mitala ili kuafikiana na utamaduni wa Graeco-Roman unaoweka sheria ya mke mmoja tu huku ikisamehe vimada na ukahaba.[158]
Uislamu umeweka mipaka ya mitala kuwa mwisho kuoa wake wanne kwa wakati mmoja na Uislamu umetangaza kuwatendea wake kwa uadilifu kuwa ndio sharti la msingi la mitala. Katika Sura An-Nisaa 4:3, Mungu anaeleza:
"...فَانكِحُواْ مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاء مَثْنَى وَثُلاَثَ وَرُبَاعَ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلاَّ تَعْدِلُواْ فَوَاحِدَةً..."
"…Oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu…" An-Nisaa 4:3

Hitimisho

Kuna Mungu mmoja tu aliyeumba jamii moja ya wanadamu, na akawafikishia ujumbe mmoja: nao ni kutii matakwa ya Mungu – kunakuojulikana kwa Kiarabu kama Uislamu. Ujumbe huo ulipelekwa kwa watu wa kwanza duniani, na kuthibitishwa na manabii wote wa Mungu waliokuja baada yao, zama zote zilizopita. Kiini cha ujumbe wa Uislamu ni kuwa binadamu lazima wamwabudu Mungu mmoja tu kwa kutii Amri zake, na kuacha kuabudu viumbe wa Mungu vikiwa kama njia, umbo au mfumo wowote ule.
Yesu Kristo, amezaliwa na Bikira Maria, amefanya miujiza na kuwaita Waisraeli katika ujumbe ule ule wa kutii (Uislamu), kama walivyofanya manabii wote waliomtangulia. Yesu hakuwa Mungu, wala hakuwa 'Mwana wa Mungu', lakini alikuwa ni Masihi, Mtume wa Mungu mwenye heshima kubwa. Yesu hajawaita watu wamwabudu yeye; kinyume chake, aliwaita wamwabudu Mungu, na yeye mwenyewe pia alimwabudu Mungu. Aliithibitisha sheria za Torati alizozifundisha Nabii Musa; aliishi nazo na kuwaagiza wanafunzi wake wazifuate kwa maelezo mazuri sana. Kabla ya kuondoka kwake, aliwafahamisha wafuasi wake juu ya Nabii wa mwisho, Muhammad wa Arabuni (SAW), atakayekuja baada yake, na kuwaagiza watii mafundisho yake.
Katika vizazi vya baada ya kuondoka kwa Yesu kutoka katika dunia hii, mafundisho yake yaliharibiwa naye akakuzwa na kufikishwa kuwa Mungu. Karne sita baadaye, baada ya kuja kwa Mtume Muhammad (SAW), hatimaye ukweli juu ya Yesu Kristo ukaelezwa upya na kuhifadhiwa milele katika kitabu cha ufunuo wa Mungu cha mwisho, Quran. Zaidi, sheria za Musa, alizozifuata Yesu, zilifunuliwa upya katika mfumo safi na nadhifu, na kutekelezwa katika njia ya maisha iliyowekwa iwe sheria na Mungu ijulikanayo kama Uislamu.
Hivyo, ukweli wa manabii, ujumbe wao wa aina moja, na njia ya maisha waliyoifuata, vinapatikana vikiwa vimehifadhiwa katika dini ya Kiislamu, dini ya pekee iliyoletwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Na zaidi, leo hii ni Waislamu pekee wanaomfuata kikweli kweli Yesu na mafundisho yake ya kweli. Njia yao ya maisha inaendana sana na njia ya maisha ya Yesu kuliko "Mkristo" yeyote wa siku hizi. Mapenzi na heshima kwa Yesu Kristo ni kipengele cha imani katika Uislamu. Allah amesisitiza umuhimu wa kumwamini Yesu katika sehemu nyingi katika Quran. Kwa mfano, katika Sura An-Nisaai 4:159, Amesema:
"وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلاَّ لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا"
"Na hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao." An-Nisaai 4:159

Kurudi kwa Yesu

Ingawa kuna matarajio ya kurudi kwa Yesu, wanayoyasubiri Wakristo, pia hiyo ni sehemu ya imani ya Kiislamu. Hata hivyo, hatorudi kuhukumu dunia kama wanavyoamini Wakristo wa kisasa, kwa sababu hukumu inamilikiwa na Mungu peke yake. Quran inafundisha kuwa Yesu hakuuliwa na Wayahudi, lakini badala yake alinyanyuliwa na Mungu akiwa hai kwenda mbinguni. An-Nisaai 4:157-158:
"وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـكِن شُبِّهَ لَهُمْ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُواْ فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلاَّ اتِّبَاعَ الظَّنِّ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا،  بَل رَّفَعَهُ اللّهُ إِلَيْهِ وَكَانَ اللّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا "
"Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu – nao hawakumuuwa wala hawakumsulubu, bali walifananishiwa tu. Na hakika waliokhitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima." An-Nisaai 4:157-158
Miongoni mwa vitu vilivyoripotiwa kuwa Mtume Muhammad (SAW) amevisema kuhusiana na kurudi kwa Nabii Yesu ni vifuatavyo, "Hakutakuwa na Nabii katika yangu na Isa (Yesu), naye atarejea. Na atakaporeja mtamjua. Atakuwa mtu mwenye umbo zuri na ngozi nyekundu na atashuka akiwa amevaa vipande viwili vya shuka. Nywele zake zitaonekana zimelowa, ingawa hazijaguswa na maji. Atapambana na watu ili kuuimarisha Uislamu, atavunja msalaba, ataua nguruwe na kubatilisha kodi ya jizya.[159] Katika wakati wake, Allah ataziangamiza dini zote ispokuwa Uislamu, pia, Masihi Dajjali atauliwa. Isa atakaa duniani kwa miaka arobaini, na atakapokufa, Waislamu watamsalia sala ya maiti." [160]
Kurejea kwa Yesu kutakuwa ni moja ya alama za kufika Siku ya Kiama.

Bibliografia

Arberry, Arthur J., The Koran Interpreted, London: George Allen & Unwin, 1980.
Barr, James, "Abba Isn't 'Daddy'," in Journal of Theological Studies, vol. 39, 1988.
-----------, "Abba, Father", in Theology, vol. 91, no. 741, 1988.
Brayer, Menachem M., The Jewish Woman in Rabbinic Literature: A Psychosocial Perspective, Hoboken, N.J: Ktav Publishing House, 1986.
Burton, John, An Introduction to the Hadith, UK: Edingurgh University Press, 1994.
-----------, The Collection of the Qur'an, Cambridge: Cambridge University Press, 1997.
Cragg, Kenneth, The Mind of the Qur'an, London, George Allen & Unwin, 1973.
Deedat, Ahmed, Christ in Islam, Durban, South Africa: The Islamic Propagation Centre, n.d.
Dunn, James, Christology in the Making, London: SCM Press, and Philadelphia: Westminister Press, 1980.
Eriedman, Richard, Who Wrote the Bible?, U.S.A.: Summit Books, 1987.
Funk, Robert W., Roy W. Hoover and The Jesus Seminar, The Five Gospels, New York: Polebridge Press, Macmillan Publishing Co., 1993.
Graham, William, Beyond the Written Word, Uk:  Cambridge University Press, 1993.
Hamidullah, Mohammed, Muhammad Rasullullah, Lahore, Pakistan: Idara-e-islamiat, n.d.
Hasan, Ahmad, Sunna Abu Dawud, (English Trans.), Lahore: Sh. Muhammad Ashraf Publishers, 1st ed., 1987.
Hastings, J., Dictionary of the Bible, New York: Chas. Scribner's Sons, revised ed., 1963.
Hebblethwai, Brian, The Incarnation, England: Cambridge University Press, 1987.
Hick John, ed., The Myth of God Incarnate, London: SCM Press Ltd, 1977.
----------, The Metaphor of God Incarnate, London: SCM Press Ltd, 1993.
Hillman, Eugene, Polygamy Reconsidered: Africans Plural Marriage and the Christian Churches, New York: Orbis Books, 1975.
Hornyby, A.S., The Oxford Advanced Learner's Dictionary, EnglandOxford University Press, 4th ed., 1989.
Khan, Muhammad Muhsin, Sahih Al-Bukhari, (Arabic-English), Lahore: Kazi Publications, 6th ed., 1986.
Gibb, H.A.R. and J.H. Kramers, shorter Encyclopaedia of Islam, Ithaca, New York: Cornell University Press, 1953.
Maccoby, Hyam, The Myth-maker: Paul and the Invention of Christianity, New York: Harper & Row, 1987.
Mayfield, Joseph H., Beacon Bible Commentary, Kansas City: Beacon Hill Press, 1965.
Moule, C.F.D., The Origin of Christology, U.K.: Cambridge University Press, 1977.
Mufassir, Sulayman Shahid, Biblical Studies from a Muslim Pespective, Washington: The Islamic Center, 1973.
----------, Jesus, A Prophet of Islam, Indianapolis: American Trust Publications, 1980.
Nicholson, Reynold A., Literary History of the Arabs, Cambridge: Cambridge University Press.
Philips, Abu Ameenah Bilal, The Purpose of Creation, Sharjah, U.A.E.: Dar Al Fatah, 1995.
Ramsey, Michael, Jesus and the Living Past, UK: Oxford University Press, 1980.
Ruether, Rosemary R., ed., Religion and Sexism: Images of Woman in the Jewish and Christian Traditions, New York: Simon and Schuster, 1974.
Spray, Lisa, Jesus, Tucson, AZ: Renaissance Productions, 1987.
Siddiq, Abdul Hamid, Sahih Muslim, (English Trans.) Lahore: Sh. Muhammad Ashraf Publishers, 1987.
The New Encyclopaedia Britannica, Chicago: Encyclopaedia Britannica, Inc., 15th Edition, 1991.
The World Book Encyclopaedia, Chicago: World Book, Inc., 1987.
p.31 and unauthorized copies were destroyed.
p.34 to the level of the Bible are easily explained. For ex-
p.38 authority for tracing the origin and early develop-
p.46 The Biblical story of Jesus turning water into wine (John 2:1-10) is con-
p.50 "When your Lord gathered all of aadam's descendants [before creation] and made them bear witness for themselves, saying: 'Am I not your
Lord?' They all replied: Yes indeed, we bear wit-
p.53 of these speeches is that they accurately reflect the original belief and termi-
p. 74 "surely, I have sent to every nation a messe-
p.77 was officially struck off the list of saints by papal de-
p.80 portraying God in human from eventually won out.
p.91 nor did he eat blood. God is recorded as having in-
p.92 eaten by one who wishes to eat, except for ani-
Consequently, particular rites of slaughter were pre-
p.95 little farther be fell on his face and prayed, 'My Father, if it be possible, let this cup pass from me; never-
p.98 Clara M Henning, "Canon Law and the Battle of the Sexes," in Relig-
p.99 sent me, even so I send you.' "This greeting was ac-
p.103 interest remains due to you, if you really are be-
However, in the verse following this one, the Jews made lending on in-
p.105 cus 18:18, "And you shall not take a woman as a ri-
p.109 "And their (the jews) saying: 'We killed the Mes-

Mwisho.

   في الغلاف الخارجي:
Yesu Kristo anawakilisha akiwa ni kiungo cha kuunganisha baina ya dini mbili zenye wafuasi wengi zaidi duniani leo hii; Ukristo na Uislamu. Somo lifuatalo, linalohusu Ujumbe wa Yesu na Haiba yake limeegemea katika kiungo hicho. Inatarajiwa kuwa, kwa kupitia somo hili, wote wawili; Waislamu na Wakristo watafahamu vizuri ukuu wa Yesu na umuhimu wa ujumbe wake.
Miongoni mwa vitu vilivyoripotiwa kuwa Mtume Muhammad (SAW) amevisema kuhusiana na kurudi kwa Nabii Yesu ni vifuatavyo, "Hakutakuwa na Nabii katika yangu na Isa (Yesu), naye atarejea. Na atakaporeja mtamjua. Atakuwa mtu mwenye umbo zuri na ngozi nyekundu na atashuka akiwa amevaa vipande viwili vya shuka. Nywele zake zitaonekana zimelowa, ingawa hazijaguswa na maji. Atapambana na watu ili kuuimarisha Uislamu, atavunja msalaba, ataua nguruwe na kubatilisha kodi ya jizya. Katika wakati wake, Allah ataziangamiza dini zote ispokuwa Uislamu, pia, Masihi Dajjali atauliwa. Isa atakaa duniani kwa miaka arobaini, na atakapokufa, Waislamu watamsalia sala ya maiti." 
Kurejea kwa Yesu kutakuwa ni moja ya alama za kufika Siku ya Kiama.




HAKIUZWI
KINATOLEWA BURE



[1]  Time, December 18, 1995, p.46.
[2] The Myth of Gold Incarnation, p. ix.
[3] October 31, 1988, p. 44.
[4]  Luka 11:2 na Mathayo 6:9-10.
[5] Hilo neno Gospel limetokana na neno la Anglo-Saxon god-spell, lenye maana ya "hadithi nzuri", tafsiri ya neno la Kilatini evangelium na Kigiriki euangelion, lenye maana ya "habari njema" au "simulizi nzuri." (The New Encyclopaedia Britannica, vol. 5, p. 379).
[6] Kubuniwa: si halisi; si ya kweli au yamevumbuliwa. (Oxford Advanced Learner's Dictionary, p. 4 5).
[7] Ekaristi ni mkate na divai vinavyoliwa katika sherehe za Kikristo vinatokana na chakula cha karamu ya usiku ya mwisho ya Kristo. (Oxford Advanced Learner's Dictionary, p. 410). 
[8] Julai mosi, 1991, p. 57.
[9] Gloss ni maelezo ya yaliyoongezwa katika matini. (Oxford Advanced Learner's Dictionary, p. 45).
[10] Iliyopo: iliyonusurika na kupatikana hadi leo.
[11] Kukatisha tamaa; kuogopesha.
[12] The Holy Bible: Rivised Standard Version, p. iii
[13] Ibid, p. v.
[14] The Holy Bible: Rivised Standard Version, p. iii-iv.
[15] Ibid, p. iv.
[16]Ibid, p. vi.
[17] The Holy Bible: Rivised Standard Version, p. 96.
[18] The Holy Bible: (King Jems Version)
[19] The Holy Bible: Rivised Standard Version, p.
[20] Ibid, p. vii.
[21] Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati.
[22] Wayahudi wa Kiothodoksi wanadai kuwa Torati, yaani jina la Kiyahudi la vitabu vitano vya kwanza, eti iliumbwa kwa vizazi 974 kabla ya kuumbwa kwa dunia. Kwa mujibu wa Wayahudi hao, Mungu aliitamka Torati wakati wa siku 40 pale Musa alipokuwa Mlima Sinia, ikiwa katika mfumo wa mwisho usio na kughairi na ni dhambi kudai kuwa Musa ameandika mwenyewe hata herufi moja ya kitabu hicho.
[23] Nani aliyeiandika Biblia, pp. 54-70.
[24] Mwishoni mwa karne ya kumi na tisa msomi wa Kijerumani, Julius Wellhausen, alikuwa wa kwanza kutambulisha vyanzo mbadala vya vile vitabu vitano.
[25] Richard Elliot Friedman ni profesa wa chuo Kikuu cha California huko San Diego. Amepata Udaktari wa Biblia ya Kiyahudi huko Chuo Kikuu cha Harvard, naye ni mtunzi wa kazi yenye mabishano ya, Nani Aliyeandika Biblia.
[26] Kamusi ya The Interpreter`s Dictionary ya Biblia, toleo 1, p. 756, na  toleo 3, p. 617. Pia tazama The New Encyclopaesia Britannica, toleo 14, pp. 773-4.
[27] Kiarama ni lugha ya Kisemiti iliyochukua nafasi ya lugha ya Akkadian kidogo kidogo na kuwa lugha ya kwanza ya watu wa Mashariki ya Karibu katika karne ya saba na sita BC. Baadaye kikawa lugha rasmi  ya Himaya ya Persian. Kiarama kimechukua nafasi ya Kiebrania na kuwa lugha ya Wayahudi; sehemu ya Vitabu vya Agano la Kale ya Danieli na Ezra zimeandikwa kwa Kiarama, kama zilivyoandikwa Talmudi (kitabu cha Wayahudi) za Jerusalem na Babyloni. Hicho ni kipindi cha athari kubwa zilizopanuka kuanzia mwaka 300 BC hadi 650 CE, baada ya hapo kidogo kidogo Kiarabu kilichukua nafasi yake. (The New Encyclopedia Britannica, toleo 1, pp. 516)
[28]Encyclopedia Americana, vol. 3, p. 654.
[29] The five Gospels (Injili tano), p. 20, na The New Encyclopaesia Britannica, toleo 14, pp. 824. ili kupata marejeo mbali mbali ya Marko katika Agano Jipya, tazama yafuatayo: Matendo 12:12; 13:5; 15:36-41; Wakorintho 4:10; 2 Timotheo 4:11; Philemon 24; na 1 Peter 5:13.
[30] The five Gospels (Injili tano), p. 20.
[31] Ingawa kumetajwa Mathayo miongoni mwa orodha mbalimbali za wanafunzi wa Yesu… mwandishi wa Mathayo huenda hajatajwa.” . (The New Encyclopedia Britannica, toleo 1, pp. 826)
[32]- “Ingawa mtunzi wa Marko huenda hajulikani…” . (The New Encyclopedia Britannica, toleo 1, pp. 824)
[33] The Murtorian Canon inamuelekeza Luka. Tabibu, mfuasi wa Paulo; Irenaeus anamueleza Luka kuwa ni mfuasi wa Injili ya Paulo. Eusebius alikuwa na Luka akiwa kama mganga  wa Antiochene aliyekuwa na Paulo ili kuipa hiyo Injili sifa ya utunzi wa wanafunzi wa Yesu.” . (The New Encyclopedia Britannica, toleo 1, p.827)
[34] Kutoka katika ushahidi wa ndani, Injili hiyo iliandikwa na mwanafunzi mpendwa wa Yesu asiyejulikana jina lake.” . (The New Encyclopedia Britannica, toleo 1, p. 828.
[35] The New Encyclopedia Britannica, toleo 1, p. 830.
[36] Ibid., vol. 14, p. 844.
[37] Kasisi anayepokea malipo kutokana na mapato ya kanisa, hasa hasa kanisa kuu. (Oxford Advanced Learner’s Dictionary, p. 973.)
[38]Kuna kiasi cha mistari mia mbili inayopatikana katika Injili mbili za Mathayo na Luka (mfano Mathayo 3:7-10 na Luka 3:7-9; Mathayo 18:10-14 na Luka 15:3-7, bila ya kulingana katika Marko wala Yohana. Kama njia ya kufafanua maafikiano hayo yanayogonga, Msomi wa Kijerumani ameweka nadharia tete ya kuwa kulikuwa na nyaraka za chanzo, alichokirejea ambacho ni kama Quelle (Neno la Kijerumani kwa maana “chanzo”). Kifupisho “Q” baadaye kilijengewa kuwa ndio jina lake. Kuwepo kwa Q mara moja kulipewa changamoto na baadhi ya wasomi katika uwanja wa kuwa isemwayo ni Injili kwa hakika haikuwa Injili. Changamoto hiyo inadai kuwa hakukuwa na kufanana kwa ukale kwa Injili ikiwemo na maneno na mafumbo na ukosefu wa historia ya Yesu, hasa hasa historia ya majaribu yake na kifo chake. Kugundulika kwa Injili ya Thomas imebadilisha yote hayo. (Injili Tano, p. 12) Injili ya Thomas ina misemo na mafumbo mia moja na kumi na nne alioandikiwa Yesu; haina mfumo simulizi; hakuna maneno ya Yesu mpunga pepo, tabibu, majaribu, kifo, wala kufufuka; hakuna habari za kuzaliwa wala utoto; na hakuna kifungu kilichosimuliwa cha uchungaji wake kwa hadhira ya watu huko Galilaya na Judea. Tafsiri ya Coptic ya maandiko haya (imeandikwa kiasi cha miaka 350 C.E.), iliyopatikana mwaka 1945 huko Nag Hammadi nchini Misri, imewawezesha wasomi kutambua vipande vitatu vya Kigiriki (vyenye tarehe ya takriban miaka 200 C.E.) imegunduliwa mapema zaidi, ikiwa ni kipande cha nakala tatu tofauti tofauti za Injili hiyo hiyo. Injili ya Thomas inafanana mara arobaini na saba na Marko, kufanana na Q mara arobaini, na Mathayo mara kumi na saba, na Luka mara nne, na Yohana mara tano. Kiasi cha misemo sitini na tano au sehemu ya misemo ni ya kipekee kwa Thomas. (The Five Gospel, p.15).     
[39] Injili katika Kingereza cha kisasa.
[40] Tangu mwishoni mwa karne ya kumi na nane, Injili tatu za kwanza ziliitwa Muhtasari wa Injili, kwa sababu, maandiko yakiwekwa, pamoja, na kuonyesha matendo sawasawa ya maisha na kifo cha Yesu Kristo. (The New Encyclopedia Britannica, toleo 5, p. 379.
[41] -The Five Gospel, p. 20.  
[42] - “Naye BWANA akanena na Gadi, mwonaji wake Daudi, akisema.” 1 nyakati 21:9. Kwa mujibu wa maandiko haya, Gad lilikuwa jina la mpiga ramli wa Mtume Daudi.
[43] Pia tazama, Mathayo 27:32 na Marko 15:21.
[44] Pia tazama, Luka 24:1-2.
[45] Pia katika orodha ya Mathayo, mwana wa Nahshon anaitwa Salmon, huku katika orodha ya Luka, jina la mwana wa Nahshon ni Sala.
[46] Shorter Encyclopedia of Islam, p. 278.
[47] Kitabu kilichoandikwa kwa mkono cha maandiko ya kale
[48] - Shorter Encyclopedia of Islam, p. 279. Pia tazama The New Encyclopedia Britannica, vol. 22, p. 8.
[49] The Mind of the Qur’an, p. 26.
[50] Beyond the Written Word, p. 80.
[51] An Introducton to the Hadith, p. 27.
[52] Neno la Kiarabu linalotumiwa kujulisha maandiko ya Quran.
[53] The collection of Qur`an, p. 239-40.
[54] Muhammad Rasullullah, p. 179.
[55]  Tafsiri ya Qurtubee, vol. 8, pp 5169-70.
[56] Fat-hul-Qadeer, vol. 4, p.349.
[57] The New Encyclopedia Britannica, toleo 27, pp.551 na 571.
[58]  Qur’aanic chapter.
[59] Inaashiria kwa mbali au kwa ufupisho
[60] Kurudia picha Fulani.
[61] The Koran Interpreted, p. 28.
[62] The Qur’an and Modern Science, p.6.
[63] Literary History of the Arabs, p. 143.
[64] Revised Standard Version.
[65] Pia tazama, Yohana 4:34, 5:30, 7:16 na 28, 11:42, 13:16, 14:24.
[66] Hapa Yesu anakataa kuitwa “mwema mkamilifu”, kwa kuwa ukamilifu ni wa Mungu tu. Yesu alikuwa ‘mwema’, lakini pia na kuwa “mwana wa binadamu” (Mathayo 19:29) – kama alivyokuwa akijiita yeye mwenyewe – alikuwa anakosea.
[67] Ilitakiwa iandikwe kuwa, licha ya maonyo ya Quran na maneno mengine ya Mtume Muhammad (SAW) mwenyewe, baadhi ya Waislamu wamemnyanyua Mtume hadi kumfikisha hali ya unusu mungu kwa kumuomba.
[68] Maelezo ya Biblia kuhusu Yesu aliyegeuza maji kuwa mvinyo (Yohana 2:1-10) ni jambo la kuvutia kabisa hayapo katika Quran.
[69] Pia tazama, Hosea 1:10, ya King James Version.
[70] Katika Revised Standard Version, inasema: “Na mimi nitamfanya mzaliwa wangu wa kwanza, mkuu wa wafalme duniani.” Pia tazama Yeremia 31:9, “Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyooka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.”
[71] Pia tazama, Job 2:1 na 38:4-7. marejeo mengine ya wana wa Mungu pia unaweza kupatikana katika Mwanzo 6:2, Kumbukumbu la Torati 14:1 na Hosea 1:10.
[72] Luka 3:38.
[73] Neno “wa kuzaa” katika Kingereza cha Kale linamaanisha ‘kuzaliwa na baba’ na lilikuwa linatumiwa kutofautisha kati ya Yesu, aliyechukuliwa kuwa ni mwana halisi wa Mungu, na mfumo wa kistiari wa kutumia neno ‘mwana’ kwa “wana wa Mungu walioumbwa”.
[74] Katika kitabu cha Matendo cha Agano Jipya, kuna mihtasari ya hotuba za wanafunzi wa kwanza wa Yesu, maneno ya tarehe zinazoanzia mwaka 33 CE., takriban miaka arobaini kabla ya kuandikwa zile Injili nne. Katika moja ya hotuba hizi, Yesu anaaonyeshwa kwa bayana kuwa ni andra apo tou theou: “yaani, mtu kutoka kwa Mungu.” Matendo 2:22. Hakuna hata nara moja kuungama huku kwa mwanzo kwa imani ukitumia maelezo wios tou theous: “Mwana wa Mungu”, lakini wao wanaongea mara kadhaa kuwa Yesu ni mtumishi wa Mungu na ni mtume Matendo 3:13, 22, 23, 26. Maana ya hotuba hizi ni kuwa hotuba hizo kibarabara zinaakisi imani asilia na istilahi za wanafunzi wa Yesu, kabla ya kubadilishwa kwa imani na istilahi chini ya ushawishi wa Dini ya Warumi na Falsafa za Kigiriki. Wao wanaakisi mapokeo ambayo ni ya zamani kuliko yale yanayotumiwa na Injili Nne, ambapo Yesu havikwi uungu wala umwana wa Mungu. (Bible Studies From a Muslim Perspective, p. 12). 
[75] Tazama Matendo14:11-13. Katika mji wa Lystra (Uturuki), Paulo na Barnabas walihubiri, na wapagani walidai kuwa Paulo na Barnaba walikuwa ni miungu wenye miili. Walimwita Barnaba mungu wa Kirumi Zeus, na Paulo mungu wa Kirumi Hermes.
[76] Bible study from a Muslim Perspective, p. 15.
[77] Mathayo 5:9.
[78] Journal of Theological Studies, vol. 39 na Thewology, vol. 91, no. 741.
[79] Yesu ananukuu Zaburi 82:6 “Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.”
[80] Pia tazama Yohana 17:11.
[81] Pia tazama, Mathayo 2:8.
[82] Pia tazama Mathayo 28:9, "Na tazama, Yesu akakutana nao, akasema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia."
[83] Tazama, kwa mfano, 1 Samweli 25:23, "Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi."
[84] Gospel Light, (1936 ed.) p. 353, quoted in Jesus, p.21.
[85] Injili ya Yohana kimsingi inatofautiana na Injili nyingine tatu (Injili za muhtasari) kiasi cha kutilia shaka uhakika wake. Kwa mfano:
Injili za Ufupisho
Injili ya Yohana              
Mahubiri ya Yesu kwa umma yalikuwa ni mwaka mmoja
Mahubiri ya Yesu kwa umma yalikuwa ni miaka mitatu
Yesu aliongea kwa ufupi kiasi cha mstari mmoja hivi, na kwa mafumbo
Yesu aliongea kwa urefu na kwa mijadala ya kifalsafa.
Yesu amesema kidogo mno kujihusu yeye mwenyewe
Yesu aliakisi kwa upana zaidi juu ya kazi yake na haiba yake.
Kumtoa mbadilisha pesa nje ya hekalu ndio tukio lake la mwisho katika kazi yake duniani
Kumtoa mbadilisha pesa nje ya hekalu ndio tukio lake la kwanza katika kazi yake
Yesu alitetea maskini na wakandamizwaji
Yesu alikuwa na jukumu dogo au hakuwa na jukumu lolote kwa maskini na wakandamizwaji
Yesu ni mtoa pepo
Yesu hajatoa pepo
Yesu alisulubiwa mnamo 15 Nisan
Yesu alisulubiwa mnamo 15 Nisan, siku ya Pasaka ya muhanga wa Wayahudi.

[86] The Five Gospels, p. 10.
[87] Wingi wake ni logoi nalo pia linamaanisha “hoja” au “mpango”.
[88] Dhana inayotambulishwa na neno logos pia linapatikana kwa wanafalsafa wahindu, Wamisri, na Wairani na mifumo ya kitiolojia. (The New Encyclopaedia Britannica, vol. 7, p. 440)
[89] Stoics walikuwa ni wanafalsafa waliofuata mafundisho ya mtambuzi Zeno wa Citicum (karne ya 4-3 BC).
[90] Wao wanaliita logos majaaliwa ya Mungu, maumbile, mungu, na roho wa ulimwenguni.
[91] Kwa mujibu wa Philo na wanafalsafa wa The Middle Platonists, waliofasiri kwa istilahi za kidini mafundisho ya karne ya nne BC ya mwalimu wa falsafa wa Kigiriki Plato, logos alizaliwa duniani kama ni msingi na wakati huo huo akili ya kiungu ya hali ya juu. (The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 7, p. 44o)
[92] The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 9, p. 386.
[93] Ibid, vol. 7, p. 440.
[94] Kristo katika Uislamu, pp. 40 – 1.
[95] Hili ni kwa mujibu wa King James Version na the Authorized Version. Katika Revised Standard Version, tafsiri ya mstari huu ni rejesho, “Na Bwana alimwambia Musa, ‘Tazama, Ninakufanya uwe Mungu kwa Farao; na Aroni nduguyo atakuwa mtume wako.
[96] - The Myth-maker, p. 172.
[97]Miaka sabini baadaye Kanisa la Kikristo lilijengwa upya huko Jerusalem, baada ya huo mji kuharibiwa na Warumi kwa mara ya pili na kujengwa upya ukiwa ni mji wa Mataifa usio wa Wayahudi ukiitwa Aelia Caitolina. Hili kanisa Jipya la Kikristo halikuendeleza ‘Kanisa la Jerusalem’ lile la kwanza lililongozwa na James. Wafuasi wake walikuwa ni watu wa Mataifa, kama anavyothibitisha Eusebius, na imani yake ilikuwa ni ile ya Ukristo wa Kipauline. (Eusebius, Ecclesiastical History, III. V. 2-3, iliyonukuliwa katika The Myth-maker, p. 174)
[98] The Myth-maker, p. 175.
[99] The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 4, p. 344.
[100] Ibid., vol 4, p. 344.
[101] Pia ilijulikana kwa jina la Dynamic au Adoptionst Monarchianism.
[102] The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 8, p. 244.
[103] The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 9, p. 208.
[104] Ibid., vol. 1, pp. 556-7.
[105] The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 1, p. 549-50.
[106] The Myth of God Incarnate, p. ix.
[107] The Metaphor of God Incarnate, pp. 27-8.
[108] Jesus and the Living Past, p. 39.
[109] The Origin of Christology, p. 136.
[110] Christology in the Making, p. 60.
[111] The Incarnation, p. 74.
[112] The Economist, April 1, 1989, vol. 311, no. 7596, p. 19.
[113] King James Version and The Authorised Version.
[114] The Purpose of Creation, pp. 42-3.
[115] Kifasihi “sisi”, inajulikana kama “sisi ya kujitukuza” au “utukufu wetu”, ikimkusudia Allah.
[116] Akiitwa Mtakatifu Maria, amekuwa ni kitu cha heshima katika Kanisa la Wakristo tangu zama za wanafunzi wa Yesu. Alipewa jina la theotokos, likimaanisha “mzaa-Mungu” au “mama wa Mungu” katika karne ya tatu au nne. Ibada ya wengi ya kumwabudu Maria – katika mfumo wa sikukuu, huduma za ibada, na rozari – zimecheza duru muhimu mno katika maisha ya Waroman Katoliki na Waoksodoksi. (The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 7, pp. 897-8 na vol. 16, pp. 278-9).
[117] Malaika, Michael, Gabriel na Raphael walifanywa watakatifu na sherehe za kidini zijulikanazo kama Michaelmas (inaitwa “sikukuu ya Mtakatifu Michael na Watakatifu wote” na Waanglikana) aliwekwa kwa ajili yao tarehe 29 Septemba na makanisa ya Kimagharibi, na tarehe 8 Novemba na Kanisa la Kioksodoksi la Mashariki. Ibada ya mtakatifu Michael ilianza katika kanisa la Mashariki katika karne ya nne CE. Kwa sababu ya nafasi ya kimapokeo ya mtakatifu Michael akiwa kama kiongozi wa majeshi ya mbinguni, hatimaye heshima ya malaika wote iliingizwa katika ibada yake. (The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 8, p. 95.). Akawa mlinzi mtakatifu wa majeshi.  
[118] The world Book Encyclopedia, vol. 1, p. 509.
[119] The world Book Encyclopedia, vol. 11, p. 146.
[120] Ibid., vol. 3, p. 417.
[121] -Sunan Abu Dawud, vol. p. 387, no. 1474.
[122] Mapambano ya uasi yalikuwa juu ya kutumia sanamu za kidini (alama) katika himaya ya Byzantine kipindi cha karne ya nane na tisa. Waasi (wote waliopinga masanamu) wa suala la alama za kuabudiwa kwa sababu kadhaa, ikiwemo katazo la Agano la Kale dhidi ya masanamu katika Amri Kumi (Kutoka 20:4) na uwezekano wa kuabudu sanamu. Watetezi wa alama za ibada wameng`ang`ania tabia ya kuwa masanamu ni alama na ni kwa heshima kitu kilichoundwa.
Katika kanisa la kwanza, utengezaji na kuheshimiwa kwa picha ya Kristo na watakatifu ulipingwa kwa mfululizo. Matumizi ya alama hizo, licha ya, kasi ya umashuhuri iliyoipata, hasa hasa katika majimbo ya mashariki ya himaya ya Warumi. Katika kipindi cha mwishoni mwa karne ya sita CE na katika karne ya saba, alama za ibada zikawa ibada rasmi ya kutia moyo, mara nyingi inaashiria imani ya kishirikina katika harakati zao. Upinzani wa matendo hayo ukawa mkali mno huko Asia Ndogo. Mwaka 726, mtawala wa byzantine Leo III alikuwa upande wa watu wengi kupinga alama za ibada na kufikia 730 matumizi yake yakakatazwa rasmi. Hilo lilipelekea kuteswa kwa waabudu alama za ibada mateso yaliyofikia ubaya katika kipindi cha mafanikio ya utawala wa Leo, Constantine V (741-775 CE).
Mwaka 787, hata hivyo, mtawala Irene aliitisha baraza la saba la dunia la Nicaea, katika baraza hilo kuvunja masanamu ya kidini kulilaaniwa na matumizi ya masanamu yaliyanzishwa upya. Waabudu sanamu walipata nguvu upya mnamo mwaka 814 baada ya kujiunga kwa Leo V, na matumizi ya alama za ibada yalikatazwa tena katika baraza la mwaka (815 CE). Kipindi cha pili cha waabudu sanamu kiliisha kwa kifo cha mfalme Theophilus mwaka 842. Mwaka 843, hatimaye, mjane wake aliwarejesha upya heshima ya alama za ibada, tukio linaloendelea kusherehekewa mpaka leo katika Kanisa la Kioksodoksi la Mashariki likiwa kama Sikukuu ya Kioksodoksi. (The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 6, p.237)
[123] "Ahmad" kama "Muhammad" limetokana na mzizi wa Kiarabu hamd yaani "shukurani, sifa njema". Mtume Muhammad (SAW) pia alikuwa akijulikana kwa jina la Ahmad.
[124] Neno la Kigiriki paraclete limetafsiriwa kama "Mfariji" katika King James Version, na "Wakili" na "Msaidizi" katika tafsiri nyingine. Parakletos inamaanisha mtu anayewaombea wengine, mtu anayewashauri au kuwanasihi wengine kwa kutilia umuhimu sana mambo ya wengine. (Beacon Bible Commentary, vol. 7, p. 168).  
[125] Tazama Yohana 14:26, "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote…" Hata hivyo, katika 1 Yohana 4:1, neno "Roho" limetumika kuonyesha nabii, "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani"
[126] Kwa Kingereza, "onother" linaweza kumaanisha "mwingine zaidi ya yule wa kwanza" au "mwingine wa aina tofauti." Andiko la Kigiriki la Agano Jipya neno linalotumika ni allon, ambalo ni la kiume kwa hali ya kutendwa ya mzizi allos: "mwingine wa aina hiyo hiyo". Neno la Kigiriki kwa "mwingine wa aina tofauti". Ni heteros, lakini Agano Jipya halikulitumia neno hili katika Yohana 14:16. (Yesu, a Prophet of Islam, pp. 15-6).
[127] - Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu akiwa tumboni mwa mama yake (Luka 1:15); Elizabeth alijazwa Roho Mtakatifu (Luka 1:67).
[128] Roho Mtakatifu alikuwa kwa Simeon (Luka 2:26) naye alitua kwa Yesu katika umbo la njiwa (Luka 3:22).
[129] - Jesus, A Prophet of Islam, p. 13.
[130] Ndugu wa Wayahudi – ambao ni kizazi cha mtoto wa Ibrahimu Isaka – ni Warabu, kizazi cha ndugu wa Isaka , Ismaili.
[131] Quran kifasihi inamaanisha "msomaji-mkaririji". Mtume Muhammad (SAW) alifundisha kuwa Quran ni maneno ya Mungu. Ufafanuzi na mafundisho yake mwenyewe yanajulikana kama ni hadithi.
[132] Sura zote 114 za Quran zinaanza na dua: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu." Ispokuwa sura moja tu, sura ya 9.
[133] Kizazi cha Ismaili kilijulikana kwa jina la Warabu, neno ambalo kwa Kiebrania, linamaanisha wale wanaoishi katika 'arabah au jangwani (Dictionary of the Bible, p. 47). Aliyetajwa sana miongoni mwa wana kumi na mbili wa Ismaili ni Qaydar (Kedar kwa Kiebrania). Katika baadhi ya mistari ya Biblia Qaydar ni kisawe cha Warabu kiujumla (Yeremia 2:10; Ezekieli 27:21; Isaya 60:7; Wimbo wa Selemani 1:5).
[134] Sahihi Al-Bukhari, vol. 3, p. 535, no. 861, na Sahihi Muslim, vol. 3, p. 931, no. 4266.
[135] Alikatwa kichwa huko Roma miaka 34 baada ya kuisha kwa kazi ya uchungaji wa Yesu.
[136] Biblical Studies From a Muslim Perspective, p. 18.
[137] Pia tazama Wagalatia 6:15.
[138] Neno la Kiarabu lililotumika ni fitrah, linalomaanisha 'maumbile'.
[139] Sahih Al-Bukhari, vol. 7, p. 515, no. 777 na sahihi Muslim, vol. 1, p. 159, no. 495.
[140] Pia tazama, Kumbukumbu la Taroti 14:8.
[141] Pia tazama Sura Al-Maaidah, 5:3.
[142] Huyo ni mtu aliyetengana au mtu aliyejitenga, tunza, weka wakfu.
[143] Yohana 2:1-11.
[144] The Five gospels, p. 20.
[145] The New Fncyclopaedia Britannica, vol. 5, p. 379.

[146] The Jewish Woman in Rabbinic Literature, p.230.
[147] Ibid., p. 139.
[148] Clara M. Henning, "Canon Law and the Battle of thae Sexes," in Religion and Sexism, p.272.
[149] Sura An-Nuur 24:27.
[150] Sura Al-Araaf, 7:46.
[151] Moja ya kumi ikiwa shamba limenyeshewa na mvua na moja ya ishirini kama limemwagiliwa.
[152] Pia tazama Mathayo 6:16 na 17:21.
[153] Sahih Al-Bukhari, vol. 3, pp. 113-4, no. 200 n1 Sahih Muslim, vol. 2, p. 565, no. 2595.
[154]  Chakula au utoaji.
[155] Hata hivyo, katika mstari uliofuatia huu, Wayahudi wamefanya kumkopesha kwa riba mtu asiye Myahudi kuwa ni ruhusa:  "Mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; …" (Kumbukumbu la Torati 23:20).
[156] Women in Judaism, p. 148.
[157] Polygamy Reconsidered, p. 140.
[158] Ibid., p. 17.
[159] Kodi ichukuliwayo kutoka kwa Wakristo na Wayahudi wanaoishi chini  ya utawala wa Kiislamu badala ya zaka (sadaka ya wajibu) na kuhudumia jeshi.
[160] Sunan Abu Dawud, vol. 3, p. 1203, no. 4310 na imesahihishwa katika Saheeh Sunan Abee Dawood, vol. 3, p. 815-6, no. 3635.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget