Dua
ya kusma Muislamu anapopata maumivu katika mwili wake.
عنعثمان بن أبي العاصأنه شكا إلى رسول الله صلى الله عليه وسلموجعا يجده في جسده , فقال
له رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ضع يدك على الذي يألم من
جسدك وقل : بِسْمِ اللهِ ثلاثا
وقل سبع مرات: أَعُوذُ باللهِ
وَقُدْرَتِهِ مَنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ)) رواهمسلم
Kutoka kwa 'Uthmaan bin Abil-'Aasw kwamba alilalamika kwa Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maumivu aliyopata mwilini mwake,
akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Weka mkono wake
sehemu inayokuuma katika mwili wako na useme: BismiLLaah mara tatu, kisha sema
mara saba: A'uudhu
BiLLaahi wa Qudratihi Min Sharri Maa Ajidu wa Uhaadhiru[Najilinda
kwa Allaah na kwa uwezo Wake kutokana na shari ya ninachokisikia na
ninachokiogopa])) [Muslim]
Ama
kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mara mia na
kumpulizia, hatukupata dalili katika mafunzo yetu, ikiwa ni kwa ajili ya
kuondosha maumivu au hata kwa kutaka tu fadhila zake.
No comments:
Post a Comment