Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limechapisha makala likikiri kwamba Uislamu unaenea kwa kasi kubwa barani Ulaya na kusema: "Hadi kufikia mwishoni mwa karne hii Uislamu utakuwa dini ya kwanza barani humo."
Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limechapisha makala likikiri kwamba Uislamu unaenea kwa kasi kubwa barani Ulaya na kusema: "Hadi kufikia mwishoni mwa karne hii Uislamu utakuwa dini ya kwanza barani humo."
Mwandishi wa makala hiyo ameashiria kitabu cha "Yungiyungi na Mwezi Mwandamo" kilichoandikwa na mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Brussels ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya jamii na kuandika kuwa, kwa mujibu wa yaliyomo katika kitabu hicho, Waislamu wataunda jamii kubwa zaidi ya Brussels mji mkuu wa Ubelgiji hadi kufikia mwaka 2030.
Jina la kitabu hicho pia linaashiria ua la yungiyungi ambalo ni nembo ya mji wa Brussels na mwezi mwandamo ambao ni nembo ya Uislamu, na kusema kuwa ua hilo limo katika hali ya kunyauka na nafasi yake inachukuliwa na mwezi mwandamo.
Mwandishi wa makala hiyo anasema Waislamu ambao kwa sasa ni robo ya jamii ya watu wa mji wa Brussels wameomba kutumia makanisa yaliyogurwa na Wakristo kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Swala.
Vilevile mwaka 2008 majina ya Muhammad, Ayyub, Mahdi, Amin na Hamza yalikuwa miongoni mwa majina yaliyotolewa zaidi kwa watoto wa kiume waliozaliwa nchini Ubelgiji. Asilimia 40 ya wanafunzi wa shule za misingi katika mji huo pia ni Waislamu.
Mwandishi wa makala ya gazeti la Israel la Yedioth Ahronoth ameendelea kuandika kuwa, Ubelgiji haiko pekee katika asuala hilo. Anasema: "Kuhani wa Kiyahudi David Rozan ambaye ni Mkurugenzi wa Mahusiano Kati ya Dini Mbalimbali wa Kamati ya Mayahudi wa Marekani ametahadharisha kuwa Ulaya inakabiliwa na hatari ya kumezwa na Uislamu."
Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha uchunguzi cha Pew cha Marekani, Uislamu unaenea kwa kasi zaidi kuliko dini nyingine barani Ulaya. Idadi ya Waislamu barani Ulaya imeongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka 30 iliyopita na inatabiriwa kuwa thuluthi moja ya watoto wa Ulaya watazaliwa katika familia za Waislamu hadi kufikia mwaka 2025.
Makala ya Yedioth Ahronoth imeendelea kuandika kuwa Uislamu pia unastawi kwa kasi nchini Uingereza na idadi kubwa ya watu wanaoshiriki katika shughuli za kidini ni Waislamu, kwa kadiri kwamba idadi ya Waislamu wanaoshiriki katika Swala za Ijumaa ni kubwa sana kuliko Wakristo wanaokwenda kanisani siku za Jumapili.
Hali hiyo pia inashuhudiwa katika nchi nyingine za Ulaya. Huko Austria ambako katika karne ya 20 asilimia 90 ya jamii ya watu wake walikuwa Wakatoloki, hadi kufikia mwaka 2050 dini ya Uislamu itakuwa ya kwanza kati ya watu wenye umri wa chini ya miaka 15. Huko Ufaransa idadi ya misikiti inayojengwa ni kubwa zaidi kuliko makanisa, na vilevile idadi ya Waislamu wanaokwenda misikitini ni kubwa kuliko Wakristo wanaokwenda makanisani.
Mwishoni, makala hiyo ya Yedioth Ahronoth inasema: "Bernard Luois, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Princeton huko Marekani miaka kadhaa iliyopita aliliambia gazeti la Ujerumani la Die Welt kwamba hadi kufikia mwishoni mwa karne ya sasa Ulaya itakuwa bara la Kiislamu. Wakati huo viongozi wa Ulaya walikasirishwa mno na mtazamo huo lakini sasa na kwa mwenedo huu kuna uwezekano kwamba utabiri wa Luois unaelekea kutimia."
No comments:
Post a Comment