Kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron katika mkutano wa Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa mwezi wa Novemba jijini Perth Australia kuzitaka nchi wanachama ikiwemo Tanzania kuzitambua kikatiba haki za mabaradhuli na ‘ndoa za jinsia moja’ kama sharti la misaada, ilipelekea kupazwa sauti kali na raia wa kawaida, wanafikra, wanasiasa pia viongozi wa dini kukemea na kupinga vikali kauli hiyo ya upotofu na udhalilishaji. Jambo lililopelekea wanasiasa Bara na Visiwani pamoja na Balozi wa Uingereza nchini wote kijanja kutuliza wimbi hilo.
Hapana shaka yoyote jitihada kubwa ya makemeo, kulaani na upinzani wa raia juu ya suala la ubaradhuli lazima ithaminiwe kwa kuwa ni dalili njema ya raia kuhisi uovu na hatari ya thaqafa/mila ya kigeni kusukumwa kwa mabavu katika nchi changa ikiwemo Tanzania kwa kisingizio cha misaada. Hata hivyo, lazima tukiri pia kwamba upinzani na makemeo haya juu ya uovu huu kamwe hayajagusa suala hili kwa upana wake wala katika msingi wake. Ukiachilia mbali wachache wanaoelewa kwa kina mfumo wa kidemokrasia na kuburuza wenzao,tunaamii kwa udhati kabisa kwamba walio wengi katika raia ama hawakuilewa demokrasia kwa udhati wake au wamechanganyikiwa, kiasi cha kutoelewa wanachokipinga wala wanachokiunga mkono.
Kinachodhihirika hapa, kwa upande mmoja watu wanaunga mkono demokrasia na katiba zake zinazotegemea akili finyu ya mwanaadamu, na kwa upande wa pili wanapinga matunda yanayotokana na mfumo huo. Wengi wameshindwa kuelewa kwamba ubaradhuli unaotetewa leo ni natija ya kuipa akili kipaumbele kuamua ‘halali’ na ‘haramu’ na pia ni kutokana na fikra ya uhuru binafsi (personal freedom) inayotokana ndani ya moyo wa mfumo wa kidemokrasia.
Aidha, wameshindwa kuelewa kwamba demokrasia sio tu kuchagua raisi, mbunge, mwakilishi na diwani, bali demokrasia inagusa kila kipengee cha maisha ya mwanaadamu kutokana na aina zake nne za uhuru: uhuru wa kumiliki (uchumi),uhuru wa maoni, uhuru wa itikadi na uhuru binafsi unaomfanya mtu atende alitakalo ukiwemo ubaradhuli, usagaji, zinaa nk. Huku kazi kuu ya serikali katika mfumo wa kidemokrasia ni kulinda na kudhamini aina hizi za uhuru, na kwenda kinyume na aina hizo nne za uhuru ndio husemwa pamevunjwa haki za Binaadamu. Kinachosikitisha na kuhuzunisha zaidi ni hata baadhi ya Waislamu nao kusibiwa na fedheha na aibu ya kuchanganyikiwa huku. Ilhali niUmma usiotarajiwa kamwe kusibiwa na kuanguka kifikra kiasi hiki. Kwa kuwa ni umma bora, umma mtukufu uliotumwa kuukoa ubinaadamu ukiwa na mfumo kamili wa maisha unaofafanua kila kitu ukiwemo uovu na uharamu wa mfumo huu wa kikafiri wa kidemokrasia.
Kwa masikitiko makubwa tulipokuwa tukieleza ubatil na uharamu wa demokrasia kwa hoja na dalili za moja kwa moja (qatwii) baadhi ya masheikh na maustadh hawakujali bali waliandaa madua kuombea vyama vya kidemokrasia vipate wepesi wa kutawala kwa ukafiri huu. Aidha, wengine kama Jumiya ya Maimamu ya Zanzibar wao walitawanya nyaraka kamwe kwamba Wanaharakati wa Hizb ut- Tahrir wasipewe misikiti ‘kuwachanganya’ waumini. Na wengine walisema wanabeba demokrasia kwa mujibu wa Uislamu wao.
Kana kwamba demokrasia ni mfumo wao. Aidha, baadhi ya masheikh na maustadh waliwafanyia hata ‘ihsani’ makafiri kuwasaidia kupinda pinda dalili za kiislamu ili kuifasiri istilahi ya demokrasia iwafikiane na Uislamu. Ilhali makafiri wenyewe hawafichi wameshaweka wazi kwamba: Demokrasia ni mfumo ambao chimbuko lake ni akili ya mwanaadamu na sio Wahyi. Tahamaki leo hii masheikh na maustadhi wale wale wanapaza sauti ‘pamechezwa faul! Kana kwamba walikuwa hawajui kwamba mfumo huu huendeshwa kwa matakwa ya akili pekee.
Aidha, walishindwa kuelewa kwamba tabia ya mfumo wowote hubebwa kama muongozo kwa ulimwengu (universal), kwa hivyo kusema kwamba utaibeba demokrasia kwa mujibu wa mazingira yako, hiyo ni kutoelewa maana ya mfumo. Hata mfumo wetu wa Uislamu tulipofanya fat-hi/ufunguzi maeneo mbalimbali ulimwenguni kama Bara hindi, Fursi, Afrika na kwengineko tuliupeleka Uislamu kama mfumo kwa kufuta mila na desturi zote na kutandika mfumo wetu wa haki kimsingi (radically) pekee. Kwa sababu hayo ndio maumbile ya mfumo.Kauli ya Cameron aliitoa kwa makusudi kwa ujasiri bila ya kujali dini wala mila za wengine, alifanya hivyo kwa kuwa ndio mfumo batil wa kidemokrasia ulivyo. Amma kauli za baadhi ya masheikh, maustadh na taasisi za kidini na nyenginezo kuishukuru serikali juu ya kauli yake dhidi ya ushoga,,amma ni kutoelewa au kuwasaidia watawala kupoza ghadhabu ya umma.
Ni wajibu wanaoishukuru serikali kwanza wakaelewa lengo la jukwaa la Jumuiya ya Madola na nafasi ya Waziri Mkuu wa Uingereza katika Jum iya hiyo. Pia wakumbuke kwamba serikali ya Muungano imeanza kuwa na mawasiliano rasmi na mashoga hata kabla ya kauli ya David Cameron, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo, Vijana na Jinsia wa Tanzania Dr. Incy Nkya alikutana na mabaradhuli hao katika mwaka 2009 (The Weekend African 29-30 Sept. 2009) Aidha, Mtandao wa Kijinsia Tanzania unafanya shughuli zake kihalali, na umefanya kongamano la mabaradhuli eneo la Mabibo- Dares Salaam siku chache hata kabla ya kauli ya Cameroon. (An-nuur Nov 11-17 2011 uk.3).
Kwa upande wa Zanzibar eneo la Chukwani kuna klabu maalum (Coconut Beach) ambayo ni ngome ya mabaradhuli na wasagaji, klabu hiyo inafanya shughuli zake na inatoa matangazo yake jahara ikiwemo kutangaza kuwepo katika klabu hiyo ngoma ya ‘sulsumia’ (ngoma ya mabaradhuli). Serikali yaZanzibar inaelewa kuwepo klabu hiyo yenye leseni kamili. Aidha, Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZACP) ina kitengo maalum cha kushughulikia afya za mabaradhuli (Kituo cha dala dala Hospitali ya Mnazi mmoja), na hapo wameweka mabaradhuli wawili kukaribisha na kuhoji mabaradhuli wenzao. Bila ya kusahau mwanzoni mwa Septemba mwaka huu 2011, taasisi ya UMATI kisiwani Pemba ilipoendesha semina maalum ya mabaradhuli na baadhi ya mabwana zao (mabasha) katika ofisi yao Wete karibu na Hospitali kuu.
Kwa ikhlasi tunawanasihi Waislamu waendele kupambana na uchafu na ufisadi huu wa ushoga na mwengineo, lakini mapambano haya lazima yagonge waziwazi mfumo wa kidemokrasia kwa kuwa ndio chanzo cha kila balaa leo duniani, pia yatoe suluhisho la kudumu la kiislamu. Amma wakiristo hususan walio wakweli katika dini yao ambao tunaamini wapo wengi, nao tunawanasihi waje mara moja katika Uislamu. Kama hawako tayari kusilimu basi waupinge mfumo wa kidemokrasia na wasikubali kutumiwa na mfumo huu dhidi ya
Uislamu na Waislamu. kwa kuwa Wakiristo hupata hali bora zaidi chini ya utawala wa kiislamu kuliko chini ya demokrasia. Mfumo wa demokrasia si tishio tu kwa Uislamu, bali ni tishio kwa ubinaadamu wote na hususan kwa dini. Upande mmoja kijanja unahubiri ‘uhuru wa kuabudu’ na upande wa pili unazitenza nguvu dini na wenye dini kukubali uovu wao.
Qadhia hii ni dalili nyongeza ya kutofaa kwa demokrasia na kutokubalika, na dunia inahitaji mfumo mbadala ambao ni Uislamu, unaoamrisha mema na kukataza maovu kwa mujibu wa maumbile ya mwanaadamu na kuukomboa ubinaadamu.
Imechukuliwa kutoka Islam4Zanzibarالرَّسُولَ النَّبِيَّ الأُمِّيَّ الَّذِي یَجِدُونَھُ مَكْتُوبًا عِنْدَھُمْ فِي
التَّوْرَاةِ وَالإِنجِیلِ یَأْمُرُھُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَیَنْھَاھُمْ عَنْ
الْمُنكَرِ وَیُحِلُّ لَھُمْ الطَّیِّبَاتِ وَیُحَرِّمُ عَلَیْھِمْ الْخَبَائِثَ
وَیَضَعُ عَنْھُمْ إِصْرَھُمْ وَالأَغْلاَلَ الَّتِي كَانَتْ عَلَیْھِمْ
فَالَّذِینَ آمَنُوا بِھِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ
الَّذِي أُنزِلَ مَعَھُ أُوْلَئِكَ ھُمْ الْمُفْلِحُونَ‘Mtume, Nabii asiyesoma wala kuandika, wanayemkuta kaandikwa kwao katika Taurat na Injil, anawaamrisha mema na anawakataza maovu na anawahalalilishia vizuri, na anawaharamishia viovu na anawaondelea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi waliomuamini yeye, na wakamheshimu na wakamnusuru (wakamsaidia), na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye. Hao ndio wenye kufanikiwa. (TMQ 7: 157)
No comments:
Post a Comment