Maulamaa wanasema
kuwa: Hadiyth dhaifu ni ile isiyokuwa na sifa zinazokubalika. Na wengine
wakasema kuwa Hadiyth dhaifu ni ile isiyostahiki kuitwa Sahihi wala Hasan
(njema).
Zipo aina nyingi ya Hadiyth dhaifu zikiwemo:
Mursal:
Nazo ni zile zilizonyanyuliwa moja kwa moja kutoka kwa Taabi'iy mpaka kwa Mtume صلى الله عليه
وآله وسلم.
Kwa mfano Tabi'iy aseme:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وآله وسلم amesema…”
Wakati yeye hajawahi kuonana na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.
Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kuzitumia Hadiyth za aina
hii katika makundi manne:
1. Imaam Abu Haniyfah na Imaam Maalik na baadhi ya wanavyuoni
wanasema kuwa Hadiyth hizi zinafaa kutumika.
Munqatwi'i:
Hizi ni zile Hadiyth zilizokatika Isnadi zake, yote sawa
kukatika huko kuwe mwanzo au mwisho wa majina ya wapokezi
Nazo ni zile Hadiyth ambazo muelezaji aeleze kuwa
amehadithiwa na mtu aliyeishi katika zama moja kisha ikathibiti kuwa hawajapata
kuonana. Au ahadithie kama kwamba amehadithiwa na mtu huyo wakati ukweli ni kuwa
hakuhadithiwa na mtu huyo, kwa mfano aseme:
“Amenihadithia fulani.” Au: “Nilimsikia fulani.” Wakati ingekuwa sahihi kama angesema:
“Amesema fulani.” Au: “Kutoka kwa fulani.”
Nazo ni zile Hadiyth nyingi zinazogongana. Hadiyth aina hii
zimedhoofishwa kwa sababu ya kugongana kwake na kutokuwa thaabit.
Nazo ni zile zilizohadithiwa na ‘Dhaifu’ (mtu asiyeaminika)
kisha zikakhitilafiana na Hadiyth zilizohadithiwa na Thiqah (mtu mwenye kuaminika).
Nazo ni zile Hadiyth zilizodhoofishwa na baadhi ya Maulamaa kutokana na udhaifu wa wapokezi wake, wakati
baadhi nyingine ya Maulamaa wakasema kuwa ni sahihi.
Nazo ni zile zilizohadithiwa na mtu anayetuhumiwa kwa uongo
katika Hadiyth au hata katika mazungumzo yake. Au anayetuhumiwa kuwa ni Faasiq
wa maneno au vitendo. Matruuk pia ni yule mwenye kusahau sana au mwenye kukosea sana .
Hadiyth dhaifu inapata nguvu pale tu ikiwa rawi wake
(mwenye kuhadithia) anatuhumiwa kuwa ameanza kusahau sahau. Ni Sharti awe
Thiqah hatuhumiwi kwa Uongo wala kwa Ufaasiq wala kwa kusahau sana . Kisha
Hadiyth alozungumza juu yake ziwe zimepokelewa kwa njia nyingi sana , na hapo inapanda darja na kuwa ‘Hadiyth Hasan.’
Maulamaa wamekhitalifiana katika hukumu za kuzifanyia kazi
Hadiyth za aina hii katika makundi matatu:
Anasema Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj Al Khatwiyb katika kitabu chake ‘Al-Mukhtaswar Al-Wajiyz fiy 'Uluum al-Hadiyth:
“Mimi naunga mkono rai ya mwanzo inayosema kuwa
Hadiyth dhaifu zisifanyiwe kazi kabisa. Zipo Hadiyth za kutosha zilizo sahihi
katika mambo ya fadhail na mawaidha kiasi ambapo haina haja ya kuingiza Hadiyth
zenye shaka zinazoweza kuwa ni maneno ya uongo aliyozuliwa Mtume wa Mwenyezi
Mungu صلى الله عليه وآله وسلم.”
Pia Fadhail na Tabia njema ni katika mambo
muhimu sana katika dini kwa hivyo haina haja kuzitumia
Hadiyth dhaifu kwa ajili yake.”
Na vipi mtu ataweza kuifanyia kazi Hadiyth Mudhtwarib inayogongana na Hadiyth
Swahiyh au
Hadiyth Matruuk iliyodhoofishwa kwa ajili ya tabia ovu za msimulizi kwa ajili
ya uongo na ufasiki n.k.
Na hii ni kwa sababu imepokelewa kwa njia zinazokubalika tena kwa njia ya rawi asiyetuhumiwa kwa uongo au kwa sababu ovu za kumdhoofisha.
Kuzifanyia Kazi Hadiyth Dhaifu:
Maulamaa wamekhitalifiana katika hukumu za kuzifanyia kazi Hadiyth za aina hii katika makundi matatu:
1. Wapo wanaosema kuwa Hadiyth hizi hazifai kuzifanyia kazi kabisa, yote sawa iwe katika kuamrisha mambo ya Fadhila au katika Hukmu. Na hii ni kauli ya Yahya bin Ma'iyn na Abu Bakr bin Al-'Arabiy na pia Al-Bukhaariy na Muslim.
2. Wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi.
3. Na wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi katika mambo ya Fadhila na katika kuwaidh watu tu. Na kwamba zisitumike katika kutoa hukmu au katika ibada, tena ziwe zimekamilisha baadhi ya masharti kama vile asituhumiwe mmojawapo wa wapokezi wake kwa uongo au ufasiki n.k. Na pia udhaifu wa Hadiyth usiwe mkubwa sana , na pia mtu anapoelezea Hadiyth ya aina hii awajulishe watu kuwa ina udhaifu ndani yake.
Anasema Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj Al Khatwiyb katika kitabu chake ‘Al-Mukhtaswar Al-Wajiyz fiy 'Uluum al-Hadiyth:
“Mimi naunga mkono rai ya mwanzo inayosema kuwa Hadiyth dhaifu zisifanyiwe kazi kabisa. Zipo Hadiyth za kutosha zilizo sahihi katika mambo ya fadhail na mawaidha kiasi ambapo haina haja ya kuingiza Hadiyth zenye shaka zinazoweza kuwa ni maneno ya uongo aliyozuliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وآله وسلم.”
Pia Fadhail na Tabia njema ni katika mambo muhimu sana katika dini kwa hivyo haina haja kuzitumia Hadiyth dhaifu kwa ajili yake.”
Rai ya Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj ni bora zaidi kwa sababu mtu atawezaje kuiamini Hadiyth iliyosimuliwa na Mudallis, mtu mwenye kubadilisha majina ya Mashaykh au ya miji akijua kuwa anawadanganya wasikilizaji wake, au muongo ‘Kadhaab’ anayependa kuwadanganya watu katika mambo ya kidunia ambaye hatoshindwa kuwadanganya katika mambo ya dini.
Na vipi mtu ataweza kuifanyia kazi Hadiyth Mudhtwarib inayogongana na Hadiyth Swahiyh au Hadiyth Matruuk iliyodhoofishwa kwa ajili ya tabia ovu za msimulizi kwa ajili ya uongo na ufasiki n.k.
No comments:
Post a Comment