‘Abdun-Naaswir Hikmany
Basi kwa hakika, kila Muislamu ni mwenye kukumbwa na mtihani.
Mitihani yaweza kuja katika sura tofauti. Yawezekana ukazushiwa mambo kutoka kwa walimwengu ambayo hujayafanya. Pia mtihani upo katika mwili, huenda ukakumbwa na maradhi ikawa maji ya kunywa unapenyezewa kwa mirija, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Asitufikishe huko. Halikadhalika, mtihani mwengine ambao wengi wao unawakumba lakini hawauelewi kwamba ndio mkubwa ni
{{Na jueni ya kwamba
Subira ya mtihani wa
{{Hakika leo Nimewalipa (Pepo) kwa sababu ya kusubiri kwao, bila shaka hao ndio wenye kufuzu.}}[Suratul-Mu'minuun: 111]
Kufariki kwa mtu wa karibu pia ni mtihani, nao waweza kumfanya Muislamu kuingia katika shirki kwa kuomboleza hadi kwenda kwa waganga kupiga ramli. Kwa hapa omba uwe miongoni mwa wale ambao wanapofariki vipenzi vyao wanasema:
{{Ambao uwapatapo msiba husema: "Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea (Atatupa jaza Yake)".}} [Suratul-Baqarah: 156]
Kwa hakika hakuna mtihani ambao unatukuta, isipokuwa umeandikwa katika Lawhul-Mahfuudh. Hivyo ni wajibu wetu kusubiri.
No comments:
Post a Comment