Inafahamika vyema kwa kila mmoja wetu Muislamu na asiyekuwa
Muislamu kuwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
asili yake alikuwa Mwarabu. Katika maisha yake aliishi (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam)
katika mazingira ya Kiarabu na vazi lake lilikuwahilo .
Kwa kulichukua kubaki vazi la
kanzu kuwa ni vazi lake baada ya
kupatiwa utume ni dalili tosha kuwa kuvaa vazi hilo ni
kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
na hivyo kuingia katika Sunnah. Kwa muhtasari ni kuwa Sunnah ni kauli, vitendo
na iqrari ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Kwa kuwa alivaa na hakukanya wafuasi wake kuvaa ikaingia hiyo katika Sunnah
zake. Kwani ni wazi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alikuwa haachi jambo ambalo si zuri kuendelea katika wafuasi wake.
Mbali na kusema hayo, Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
kuusahilishia Ummah wake katika mambo mengi na mavazi vile vile alikuwa na
mavazi tofauti kama zinavyotueleza
Hadiyth zake nyingi. Wakati mwengine alikuwa anavaa ‘Imaamah (kilemba), ‘Izaar
(nguo ya chini kama kikoi), kofia, aina nyengine za nguo za kutoka Shaam, Yemen,
na hata Misri na kadhalika. Na katika mavazi alikuwa anapenda sana kuvaa
vazi la rangi nyeupe.
Baadhi ya Hadiyth zinazoelezea
hayo ni:
§ Imepokewa
kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Vaeni katika nguo zenu nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu
zilizo bora kabisa na pia muwakafini nazo maiti zenu” (Abu
Daawuud na at-Tirmidhiy, na akasema ni Hadith
Hasan Swahiuh. Isnadi yake ni Sahihi na ameisahihisha Ibn Hibbaan).
§ Na
amesema Abu Ramthah Rifaa‘ah at-Taymiy (Radhiya Allaahu ‘anhu): Nilimuona
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na nguo mbili za kijani (Abu
Daawuud na at-Tirmidhiy kwa Isnadi iliyo Sahihi. Pia imenukuliwa na
an-Nasaa’iy, na Isnadi yake ni Sahihi).
§ Na
imepokewa kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwamba
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia siku ya kufunguliwa
Makkah akiwa na kilemba cheusi(Muslim).
§ Na
amesema mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha): Mtume wa
Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amevishwa sanda ya nguo tatu
nyeupe zilizotengenezwa Sahuuliyyah (aina ya nguo kutoka kijiji hicho cha Yemen)
kwa pamba, katika hizo hamna kanzu wala kilemba (Ahmad, al-Bukhaariy na Muslim).
§ Na
amesema Mughiyrah bin Shu‘bah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Usiku mmoja
tulikuwa katika safari pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) …Wakati huo
alikuwa amevaa juba la sufi na hivyo hakuweza kutoa mikono yake mpaka alipoitoa
kutoka katika sehemu ya chini ya hilo juba. Aliosha mikono yake na kupangusa
kichwa chake. Kisha nilitaka kumsaidia ili atoe soksi zake, akaniambia: “Ziache
kama zilivyo kwani nilizivaa nikiwa katika hali ya twahara na usafi”. Hivyo
akapangusa juu yake (al-Bukhaariy
na Muslim). Na katika riwaya: Alikuwa
amevaa juba la Shaam lililokuwa na mikono membamba.
§ Amesema
Ummu Salamah (Radhiya Allaahu ‘anha): Ilikuwa
nguo bora kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kanzu (Abu
Daawuud na at-Tirmidhiy, na akasema hii ni Hadyith
Hasan).
§ Na
imepokewa kwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema: “Allaah Hatawaangalia wale watu walioburuza (zikavuka mafundo ya
miguu) nguo zao kama kikoi na kanzu na kilemba kwa kiburi” (Abu
Daawuud na an-Nasaa’y kwa Isnadi Sahihi).
§ Na
imepokewa kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume wa Allaah
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema: “Allaah Hamuangalii mwenye kuburuza (kuvaa nguo yenye kuvuka mafundo
ya miguu [Isbaal]) nguo yake kwa kiburi” (al-Bukhaariy, Muslim na
Maalik).
Kwa mujibu wa Hadiyth hizi
tunapata kuwa vazi bora lake ni kanzu
mbali na kuwa alikuwa akivaa mavazi mengine. Kulingana na Hadiyth wanazuoni
wamekuja na masharti kwa vazi kukubalika Kiislamu. Miongoni mwa masharti hayo
ni:
i. Vazi
lisiwe ni lenye kubana.
ii. Vazi
lisiwe ni la kuonyesha ndani.
iii. Kutoburuza
nguo aina yoyote kwa mwanamme [Isbaal - kuvuka mafundo ya miguu].
iv. Kutosifu
umbile lake (lisimbane).
v. Lisifanane
na vazi la kike.
vi. Lisifanane
na vazi la makafiri.
vii. Lisiwe
vazi la kifakhari, umaarufu, na mitindo [fashion].
No comments:
Post a Comment